Mviringo wa blogu za Kenya

English version of this page



Nini

Mviringo wa blogu za Kenya (KBW) ulianza 5 Julai 2004 na madhumuni yake ni kuleta pamoja blogu zilizo andikwa na wakenya au zile zinazozungumzia kenya.

Nani aweza kujiunga

Mkenya yeyote, mkaazi au rafiki wa kenya mwenye miaka 14 au zaidi na mwenye blogu au sharaja kwenye mtandao.

Kwanini ujiunge

Kujiunga na mviringo wa mtandao ni njia mojawapo ya kuongeza usomaji wa blogu na si usomaji shaghala bali usomaji wa watu wenye nia, watu wengi hufurahia miviringo hii kwani huwa inaleta pamoja tovuti zinazofanana na hivi kujenga mitandao sebayana kwenye intaneti.

KBW imegeuka kuwa jumuiya chipukizi sana kwenye mtandao. Mviringo huu kando na kuunganisha wanablogu wa kenya umekuwa kama kikao cha kubadili mawazo, kuelimishana na kujadiliana.

How?

Jiunge keo. Jiandikishe hapa.