Nini
kenyaUnlimited ilianzishwa Machi 2005 na ni jumuiya ya mtandao ya wakenya inayosimamiwa na wakenya ambayo pia inawahusisha marafiki wa kenya.
Sababu
Kulingana na ongezeko ya blogu kwenye mviringo wa blogu za Kenya (KBW) kenyaUnlimited imejitokeza kama ukumbi wa mawazo, maoni, akili na sauti tofauti za kenya ambazo ziko kwenye intaneti - japo kwa sasa tuko kwenye mtandao tu siku zijazo tunanuia kufanya tovuti hii kama kianzilishi cha miradi kadha wa kadha ya kikweli.
Nani
Kama tovuti ya kijumuiya kitambulisho cha kenyaUnlimited kina mizizi yake kwenye wanachama wake. Kwa sababu za uzoezi utunzi na umiliki wa tovuti hii ni wakujitolea kwa sasa. Na uko katika miliki ya wanablogu wanne ambao historia zao ziko kwenye nguzo ilioko mkono wa kuume wa tovuti hii.
Kuhusu hii tovuti
kenyaUnlimited awamu ya 1.0 imetengenezwa na msimbo wake kuandikwa na Mentalacrobatics, Mama Junkyard na Mshairi wakitumia Notepad na Edit Plus. Tafsiri za kizungu kwa kiswahili zimefanya na Maitha. Mpangilio wake umeshikiliwa na CSS ambao uko sahihi. Tovuti hii pia ina halali za XHTML 1.0 isipokuwa kurasa mbili ambazo zinakiuka XHTML 1.0 kulingana na hali.
kenyaUnlimited iko kwenye seva za StudentWebhosting ambazo zina mfumo unendeshaji wa Linux na zinatumia Linux, Apache [Version:1.3.33 (Unix) ], Perl [Version:5.8.1], PHP [Version:4.3.9] and MySQL [Version:4.0.22-standard]. Blogu yake inatumia Wordpress [Version:1.5].
Ilani
kenyaUnlimited ndiko nyumbani kwa Mviringo wa blogu za kenya, japo tunajaribu kumudu uanachama wa blogu kwenye mviringo huu - kila blogu unayoitembelea iko kwenye seva tofauti na inamilikiwa na mtu au watu binafsi ambao hawana uhusiano na kenyaUnlimited. Hatuna umiliki usimamizi wala wajibu wa yaliomo kwenye blogu hizo - pamoja na taswira zake na vyote viliyomo na vilivyo na hatimiliki. Kwa sababu hii ukitumia mviringo huu unaelewa na kukubali kuwa unaweza kupatana na mambo ya uzushi ama ya kukera. Kama unaona kuwa yaliyomo kwenye blogu haya furahishi au ni ya kuudhi au yasio kuridhisha basi wasiliana na mwenye blogu hio.
Hakimiliki
Kila kitu kwenye tovuti hii, (maandiko, fasihi taswira, faili sikizi, video, sanaa na kazi nyingine zote) isipokuwa pale kulipotajwa. Zimehifadhiwa haki zake chini ya Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 2.0 License. Kwa bahati mbaya hakuna toleo la kiswahili la hakimiliki yetu - japo unaweza kusoma toleo la kizungu au msimbo wote halali kwa kiingereza.
Toleo la Kizungu
Msimbo wote halali kwa kiingereza