Neno blogu limetolewa kwenye neno la kizungu “weblog” ambalo lina maanisha tovuti ambayo huwa inaandikwa mara kwa mara. Maandiko huwa yamepangwa kulingana na tarehe na yale mapya hupewa kipao mbele zaidi.
Mfano wa blogu zilizoko kwenye mtandao
Lakini orodha hii si kamili kuna blogu nyingine za aina tofauti na mara kwa mara blogu nyingi huwa zimechanganya aina.
Blogu nyingu huchanganya kazi za fasihi na taswira lakini kuna nyingine zilizo na maalum tofauti:
Kuwa mwanablogu si vigumu kama unavyo fikiria, na si lazima uwe na ujuzu mwingi wa kompyuta. Kuna tovuti nyingi ambazo zinatoa huduma kamili za blogu, zinazojulikana sana ni Blogger, Live Journal na Xanga. Kama unaweza kufungua anwani ya hotmail basi hutashindwa kutengeneza blogu hizi.
Abudi nyingine ni kutumia programu kama Movable Type, Bblog, WordPress na b2evolution lakini abudi hii itakubidi uwe na ujuzi wa ndani kidogo wa maswala ya kopyuta kando na kuwa na nafasi yako kwenye intaneti. Lakini tovuti za programu hizi zinatoa miongozo na zina kumbi za usaidizi kama utahitaji usaidizi zaidi.
Kuamua jinsi ya kuanzisha blogu huwa ni chaguo la mtu na huwa ni vizuri mtu kufanya utafita ili aweze kuchagua blogu itakayomfaa.
Kuna habari nyingi sana kwenye intaneti kuhusu historia za blogu na jinsi ya kuanza, ukurasa wetu wa viunganishi ni mahala pazuri pa kuanzia.