Items by SIMON KITURURU

SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • ILI UBENJUE KISIASA labda kihitajikacho ni kidude KIBENJUKACHO hata bila SIASA!:-(

    Posted: February 8, 2012, 6:57 am by SIMON KITURURU
    Na ili uwe MSOMI hata KISIASA,....... labda yahitajika kihitajikacho hasa KUSOMWA hata na wasio WANASIASA ,........ na labda ndio maana siku HIZI unajua WASOMI WENGI na USOMI wao MADUDU na hata chamuhimu kwako KIKISIMI  KISIASA hawajui labda waongeacho ni siasa na WANANCHI watakacho ni kutibu ni KLOROKWINI na tatizo ni MALARIA na wala sio SIASA!:-(

    Swali:
    • AU?

    Na kihitajiwacho KUBENJULIWA ,...
    ... unajua KIPO aisseee!:-(

    Swali:
    • Unabisha?
    Na KIBENJULIWACHO kipo aisee,....... hata kama ni KIMAWAZO tu aisee MHESHIMIWA na kiuheshimiwa siku hizi ni mpaka MHESHIMIWA awe ni yule JAMII inamtambua kama yeye ni MHESHIMIWA hata KIDINI na wala  huyo BINGWA kwa kuwa ni SHEKHE au ASKOFU basi hana jina katika heshima za JAMII zimtambuazo kama MWANASIASA kisa yeye ni ukiondoa DINI ana GOVI lenye UTOKO!:-(
    Swali:
    • SI labda CHA KIKWELI hata kile KISICHO BENJULIWA bado kipo na ni kweli ni CHA KIKWELI ingawa VYA UKWELI kwa WENGINE ni vile viishivyo MAWAZONI tu na havipigiki punyeto mMMmmmmkikweli kisa vyaishi tu kwa ambao vyakikweli vuko sebuleni huyo hata ki- MAWAZONI yake yako CHOONI hasa kutokana na WAHESHIMIWA yao YAKIHESHIMIWA ni NINI?



    Ndio,....... labda KIWAZWACHO,....... kwa baadhi wawezao hata kuwa ni wengi KULIKO AMBAO NI WACHACHE  TU  -tu hata kwenye wingi wa mavuzi pale ambako UNAAMINI  kihitajikacho ni KIKISIMI,...


    .... kiwazwacho ni MUHIMU ZAIDI hata kama sio kama umfikiavyo MUNGU wa WACHAWI afanikishaye kwa WACHAWI wanafanikiwa kuliko wewe katika yako ufikiriayo ni yapendwayo hata na PADRI poa hata kama ni yule mwenye nyege za waumini wake kisiri na kashawapa watoto wa watu MIMBA ambaye kisifa kakaa kisifa za KIMUNGUMUNGU wa asiye wa IBURAHIMU,...

    .... na si kama kile angalau hata kwa kuwa ni cha kikweli mpaka chaweza kutiwa kidole au kushikiliwa kama bamia,...
    ...KWA KUWA umuhimu LABDA kitafsiri ni tofauti kwa baadhi  ya  WATU,...

    ....ili UBENJUE labda unabenjua tu kwa MAWAZO na wala hata sio kwa kushikilia tonge KIKUFINYANGA kwa kuwa kuna watu kimawazo tu hilo ni TENDO na ndio maana labda twajua TANZANIA ni nchi TAJIRI hata KIMAWAZO TU ingawa wajanja ambao fulu ufunguo IKULU na maeneo ambako POCHI lako ndio HULOANISHA kiharage kisiasa za BONGO wasio na pesa wanazidi kutoonekana.:-(

    Swali:
    • Hivi ushawahi kustukia katika ufikiriayo ni ya BAADHI labda kwa mwingine WENGI hicho hicho ni  kingi na cha WENGI?

    Ndio,...... ili UBENJUE ,...... labda BENJUA kivyako kwakuwa cha siri ufikiriayo ni yako MOJA ,...... labda ni siri kweli yako moja ila kihitajikacho ili ujisikie VIZURI ki vile ambavyo unajisikia ukijamba huru wakati uko choooni,...... ni labda hata ambayo hutaki KUYABENJUA angalau ujisikie huru kuyaongelea kwa nini hutaki KUYABENJUA hadharani.


    Ni wazo tu hili na kutolielewa RUKSA!:-(

    Hebu tubadilishiwe kimuanzisho mpya kwa bezi gitaa katika kukumbushwa kiFANKYbezigitaaa aisee -THE name is BOOTSY baby



    Hebu Bootsy Collins ajaribu kulainisha kwa katika kigitaa ...Bass Solo




    Bootsy Collins aongezee SPESI BEZI na kama unaelewa FANKI MUZIKI na pia jinsi ya kupiga bezi gitaa utaelewa ni kwaniii...




    Snoop Dogg ajaribu kulainisha zaidi tena umwagia maji kwa ya NGULI huyuhuyu Bootsy Collins katika mpanuo-Undercover BROTHER
    Snoop Dogg, George Clinton na Bootsy Collins warudi kiaina ....





    Au tu hebu SNOOP dogg DOGGY azime akiwa tena na The Dogg Pound &  The Dramatics katika kidude- Doggy Dogg World




    Au tu Black STREET , Dr DRe na QUEEN Pen waweke nukta tena kwa- No Diggity

  • Kwa kuwa labda PROFESA wa KUKUPENDA KIMAPENZI kwako UNGEPENDELEA asiwe MALAYA!

    Posted: February 8, 2012, 3:14 am by SIMON KITURURU

    Ndio,........ yasemekana AKUPENDAYE ,....... moja ya sifa zake kwa wengi ni UCHOYO,....... hasa kama anyimwaye sio WEYE !
    Swali:
    • Si unajua lakini UCHOYO ni sifa mbaya KIAINA?
    • Na ugawaji si KIAINA kunawadaio ni ushahidi wa ROHO nzuri ya MTU apendaye WATU ingawa bado kuna watafsirio wagawaji kuwa ni MALAYA kutokana tu na wagawacho kitu?

    Ndio,...
    ....TAFSIRI balaa,...
    ... kwa kuwa zaweza kugeuza MGAWAJI kwa ROHO NZURI TU  kutafsirika kama MALAYA,...
    ... na MCHOYO kuwa ni MTU mwenye tabia MWANANA kwako hasa kama kiaina  AGAWACHO ni kipenzi chako na uchoyo wake kwa wengine kuhusiana na hicho KIDUDE  ndio kichocheo cha upendacho kukitafsiri kama TABIA NZURI!:-(
    Swali:
    • AU?
    • Hufikiri labda Profesa wa KUGAWA penzi - PHD yake huhitaji awe MALAYA kiaina kistaili za kugawa?

    Ndio,....... KIMPENZI,........labda wala UJUZI SANA hauhitajiki kwa kuwa USHAPENDA na ukitekenywa hata kidogo kama akudongolosaye unampenda unaweza ukastukia UNACHEKELEA kwa sana TU hata kama ni kwa KUJICHEKELESHA kwa kuwa wala haichekeshi sana.

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(


    The Mighty Sparrow aanzishe tena UPYA kwa- Good Morning Mr Walker




    Lloyd D Stiff ajaribu kubadili kwa - Bum bum fatty




    Lord Kitchener aingilie kati tena kwa - Drink Ah Rum


    Mighty Sparrow arudi kidogo na kuongelea kidude katika- Saltfish



    Halafu sijui kwanini Lord Kitchner azime tena kwa-Sugar BUM BUM






  • Tyson Gay

    Posted: February 8, 2012, 2:59 am by SIMON KITURURU
    Tyson Gay
  • Hata kama SURUALI ni ileile,...

    Posted: February 7, 2012, 9:58 pm by SIMON KITURURU
    ... MFUKO wa MBELE,....... ni tofauti na MFUKO wa NYUMA.
    Swali:
    • Kwani hata mtu abishe bado ukweli uko palepale MBELE ni tofauti na NYUMA?

    Ingawa labda,....... ukigeuka,........ kulikowahi kuwa nyuma,........ ndiko MBELE kisafari hata kama safari yenyewe ni ya KURUDI nyuma.
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


    Hebu tukatizie GHANA tena ili Nana Boroo na Mugeez warudie- Bebia Soso




    Hapahapa GHANA ngojea tu tena Nana Boroo arudie- Ahayede


    Au tu hebu WINSTON SOSO azime kwa-I don't MIND


  • Jinsi ya KUPOPOA tunda!

    Posted: February 6, 2012, 8:45 am by SIMON KITURURU
    TUNDA  tamu,....... ila TUNDA labda ni TAMU kwa MPOPOAJI,....... kutokana na lilivyopopolewa TUNDA na MPOPOAJI!:-(
    Swali.
    • AU?


    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
    Jumatatu NJEMA aisee!

    Hebu tubugi dauni kwa kurudi tena HAITI ili Brother C atekenye-Tourbillon


    Hapahapa HAITI hebu Brother's Posse wadinye-Stayle




    Au tu T-MICKY aje laivu tena....

  • NYANI kwa kutumia KIOO au tu KAMERA ya SIMU siku hizi -LABDA huona KUNDULE aisee!:-(

    Posted: February 4, 2012, 8:21 am by SIMON KITURURU
    Ndio,........ labda msemo wa NYANI haoni KUNDULE,....... sio kweli kwa asilimia MIA!
    Swali:
    • Kwani unafikiri ni kweli kila udhanialo NANILII halistukii KISA anaonyeshadalili za kutolijali kama WEWE ULIJALIVYO maana yake ni kweli huyo NANILII wako HALISTUKII  hilo li kitu?


    Ndio,...
    .... nyani wa sikuhizi  hata kwa VIDEo na KAMERA za kwenye simu zao,...
    .... labda vizuri tu huona yao makundungu,........ ila wanakomalia kujibaraguza kuwa hawastukii kwa kuwa hata KIFISADI inalipa bado!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


    Hebu KWANZA UNIT waturudishe Dar-es Salaam kwa -MSAFIRI



    Halafu sijui kwanini hebu turudi SENEGAL ili Daara-J warudie- Allah
  • Somo MOJA kutoka ZIMBABWE!

    Posted: February 4, 2012, 7:53 am by SIMON KITURURU
    Kila MTU anaweza kuwa MILIONEA,....... ingawa pamoja na UMILIONEA WAKE,......... MKATE na VITUMBUA bado vikawa GHALI na havinunuliki!:-(
    Swali:
    • Ushawahi kusikiliza MABABU hapa TANZANIA wakakuambia jinsi gani SHILINGI tano ya TANZANIA ilikuwa inatosha  kimshahara ?

    Ndio,........ labda UCHUMI ni kichaa,........ kwa kuwa waweza kukujaza MANOTI na kuondoa makali ya UTHAMANI wa  hayo ma- NGAWIRA PESA!


    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
    Jumamosi NJEMA MDAU!

    Hebu Kenyan Boys Choir waingilie kati kwa kudinya- Jambo Bwana






    Halafu tena Mighty Sparrow ajaribu kuzima kwa -Jean & Dinah-The Lizard-Melda-Drunk & Disorderly (Medley)



    Halafu The Roots ndio wazime kwa-Next Movement na Pussy Galore


  • Unafikiri WATANZANIA bado ni WABONGO miaka yote hii baada ya UHURU na BONGO zenyewe hazijafanya tuwazidi angalau KENYA angalau KIUCHUMI?

    Posted: February 3, 2012, 8:55 am by SIMON KITURURU
    BONGOOOOO!
    Na ukisikia tu jina hilo maarufu kwa WATANZANIA,....... wawezafikiri ni kweli UBONGO ni misingi katika kila wafanyalo WABONGO ni kistaili ya kutumia sana UBONGO

    Swali la KICHOKOZI:
    • Na kama tunatumia BONGO sana sie WABONGO,....
    ......mbona BONGO zenyewe hata katika kuchagua VIONGOZI wetu kuna watakaodai na kutoa ushahidi labda BONGO hazifanyi kazi?
    Ni wazo tu hili!

    Hebu tena Jaziel Brothers warudie-Ngeke Ndiphinde


    Au tu hebu Oliver Mtukudzi na Thomas Mapfumo warudie-Muchatuta






  • R.I.P Don Cornelius !:-(

    Posted: February 2, 2012, 3:06 am by SIMON KITURURU
    I loved SOUL TRAIN!Pumzika Donald Cortez "Don" Cornelius!
    
    (September 27, 1936 – February 1, 2012)



    


    Hebu aongee kidogo kikumbukumbu....



    Aendelee....



    Aendelee....


    Sijui yaliyokukuta lakini R.I.P DON....... hebu nikumbuke tena pia hiii.....


    Au tu James Brown aturudishe kwenye SOUL TRAIN...kwenye shoo yako

  • Kwenu Blog mpya ya Rural and Urban

    Posted: February 1, 2012, 11:10 am by SIMON KITURURU
    Kutembelea Libeneke hili JIPYA bofya hapa: [www.mrs-ca.blogspot.com]




    Heshima zenu Wadau wote!
    Nilikuwa napenda Kuwatambulisha Kwenu Blog mpya ya Rural and Urban ambayo itakuwa ikizungumzia maisha hayo zaidi ya mjini na Vijijini. Karibuni sana ukiona Link hii mpatie na mwengine. Natanguliza Shukrani zangu asanteni.

    -ESTER ULAYA.

    Baada ya tamutamu hebu Bassekou Kouyate na Ngoni Ba waendelee....



    Hebu tu tena na  Chuck Brown arudie tu na  -BUSTIN' LOOSE



  • HALAFU,....

    Posted: February 1, 2012, 10:40 am by SIMON KITURURU
    ....HALAFU hata KISENTENSI,.......ukianza na  HALAFU ili kunasa yasiyo na HALAFU,....... kuna wawezao kuona kuna zaidi  ya HALAFU katika uyaongeleayo yasiyo na HALAFU.:-(
    Swali:

    • AU?


    Ndio,...
    ...HALAFU,...
    .... si inawezekana yenye HALAFU hata uyasemayo au tu kuongeayo ni yale tu UYANUKUUYO kutoka kwa MTU mwingine bila kufikiria katika uhakika wake kuwa hata katika ya  Rais OBAMA hajikojolei kitandani kama BIBIE au BABUYE na ushahidi huna kama yale ya kuwa mafuta ya CHIPSI MAYAI ni yatokayo kwenye transfoma za UMEME mtaa wa jirani yana HALAFU ?

    HALAFU,........ udhaniacho nimeandika,........ labda kimaana kuna HALAFU Mkuu!:-(Ni wazo tu HILI Mheshimiwa!

    Hebu turudi HAITI ili Rasin Kita wakite....kijina la wimbo tubakie na ....-DI MOVE


  • Kimishemishe LABDA ni kweli ni KIMISHEMISHE tu- na labda KIMISHEMISHE ndio MPAKA ni siri TUKUFU mpaka za tuna MARAIS AFRIKA na hata.... mpaka MAREKANI ambao LABDA NAHISI najua unajua wamekaa KIMISHEMISHE tu!:-(

    Posted: February 1, 2012, 5:48 am by SIMON KITURURU
    Na KIMISHEMISHE,....
    .... yasemekana KUNA wapatao,.......hata kama YASEMEKANA kuna KATIKA  wapatao ambao WAPATACHO WATHAMINISHO ni mpaka  demu/KIJEBA  na wala sio OFISI tu, dengelua ,kashata, chipsi mayai,tako, sehemu za mbele za mwanamume rijali ,Ubunge  kisa wametoa mbele na nyuma, OFISI kwenye shirika fulani ILIPAYO SANA TU,  au hata tu BAMIA tu kwa MLENDA kisa CHUNGA hakuna.:-(
    Swali:
    • Si unajua ingawa MISHEMISHE kitafsiri FULANI  mtaani ni MISHENI TAUNI -lakini labda MISHEMISHE ni zaidi -na ndio maana siku hizi wajanja wana mpaka  na MAKANISA KIUJASIRIAMALI  ingawa YESU sio rafiki yao?
    • Si ikibidi KIMISHEMISHE - ndio maana WALIOBANANA kwenye DALADALA kule kwa kajamba nani kuna wastukiao KUNA wenye nafasi mbele kwa DEREVA bila sababu maalumu ?


    Ndio,........Labda BINADAMU WOTE si sawa,..... kwa kuwa,....:

    • Kwanini WENGINE  wafananao na SISI bado wako kama sio kama SISI na wao kidogo tu KWA SABABU HIZOHIZO hata UBUNGE majirani zako watawapigia kura wao ingawa wanajua wewe  kama MIMI labda ndio kitabia ni WATOTO MZURI  KIBANANGENGE kijijini hapo?
    • Unabisha?


    Ndio,....... kimishemishe wewe kama ni angalau ni mjukuu wa NYERERE  hata kwa kujisingizia pale karagwe iitwayo TANZANIA,....... labda wewe tayari sio MWENZETU kwa kuwa KIMISHEMISHE wewe hata kama hutaki waweza kuishi bila kazi na usife njaa na fulu kuongeleshwa na kama unapenda sehemu za siri za watu labda utagawiwa na hata wasio kupenda kisa jina,...
    ....eti kwa kuwa KUNA wathaminio wajuacho hata ufanye nini ,...WEWE  uko konekted hata bila kuhonga kama tu watoto wasio wa MORINGE SOKOINE Ze BONGO!:-(

    Swali:
    • Hivi unauhakika  KUNA MTANZANIA  sasa hivi hajawahi kuhonga angalau hata chumvi ili agawiwe MAPERA?

    Samahani,......mie nakiri nshawahi kuhonga kupatiwa mpaka kipenyo kidogo tu kiitwacho UKE,....... nimejirekebisha  LAKINI!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
    JUMATANO NJEMA MHESHIMIWA!


    Hebu turudi tu nyuma ya jukwaa na wanamuziki wa TANZANIA halafu Nguli John Kitime aongee...


    Halafu sijui kwanini hebu DEKULA arudishe za enzi ndude katika-Mayanga





    Dekula Kahanga azime tena kwa-Bamakonde
    
    Nipo bado  Bandugu bapendwa!:-(


  • Kuhusu UGONJWA wa MAHITAJI hata kama MAHITAJI yenyewe ni PIPI kwa mwenye hitaji hasaaa la WALI!

    Posted: January 31, 2012, 10:14 pm by SIMON KITURURU
    PIPI huweza kugeuzwa kuwa HITAJI,....... hata kwa ambaye hitaji lake la  kweli kwa kihitajikacho ni NGUNA na MLENDA.Swali:
    • Unauhakika UNAHITAJI ufikiriacho kwako ni HITAJI?
    • Si unakumbuka kuna mahitaji watu hujifunza tu kuyachukulia kuwa HITAJI yasemekana?
    • Na UKIHITAJI UGALI na ukapata UGALI - si uleule UGALI yasemekana unakuwa MTAMU zaidi kitofauti?

    Na katika GONJWA la HITAJI,........kuna WAHESHIMIWA hubaka kuku,...... kisa wamegeuza kitu HITAJI,....... na kihitaji fulani MTU akiamini ndilo HITAJI,........labda ndio maana WATU huwa na mahitaji tofauti hata kama wako kwenye CHAMOTO KILEKILE,...
    ..... na labda ndio maana katika ``CHAMOTO UNAKIONA KILEKILE kwenye MAISHA´´  yasemekana  kuna wamkimbiliao YESU, MOHAMEDI, au hata MGANGA WA KIENYEJI hata kwenye hoja ambazo wangeweza kujitetea wenyewe bila NUKUU za MWALIMU NYERERE alisemanini kuhusu HILO kama tu jinsi ambavyo kuna wachaguao KUFA MOYO na kusubiria tu litokealo na LIWE!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na USIKONDE!







    Hebu KANDA BONGOMAN arudi tena na kuanzisha upya kwa-JT




    Halafu sijui kwanini ngojea KANDA BONGOMAN arudie-Wallow



    Burning Spear aingilie ghafla nakukumbushia - Identity


    Ili tu eti BURNING SPEAR apunguze spidi ya muwasho tena kwa-SHE IS MINE


    Au tu Burning Spear alainishe mzimo wakati anazima kwa-Reggae Physician
  • HISIA ni HALIHALISI ingawa sio lazima HISIA ni UKWELI kiuhalihalisi wa KITU!

    Posted: January 31, 2012, 10:04 pm by SIMON KITURURU
    Na LABDA ukihisi ,....... wewe labda UMEHISI TU na  hiyo kwako ni HALIHALISI,........ ingawa labda pia kuna umuhimu wa KUKUMBUKA,........ HISIA sio lazima ni UKWELI.

    Ni wazo tu hili BINGWA!

    Hebu tena SAM MANGWANA aingilie kati na kurudia mdinyo-AFRICA




    Halafu Kanda BONGOMAN azime la njugu live kwakuanza na -Isambe

  • Eti kuna watakao BABA kwenye MUME kama wageuzao MKE kuwa kama MAMA YAO!

    Posted: January 29, 2012, 9:08 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,....... inawezekana kuna wake za watu ambao MME kageuka BABA na wala sio MPENZI wala rafiki,......... kama tu isemekanavyo kuna MIDUME kwa MKE  inadeka kama MKE ni MAMA na sio limpenzi!:-(

    Swali:
    • Unabisha?

    Ndio,....
    .....UNACHOTAFUTA,.....
    ...... saaa nyingine unaweza kuwa unacho ila umekigeuza na wakummtongoza umemgeuza DADA au KAKA  ambayo ni hatua ya mbali zaidi ya ile BINAMU nyama ya HAMU!:-(
    Swali:
    • Unabisha?



    Ndio,...
    ......UNACHOTAFUTA,....
    .... saaa nyingine unaweza kuwa unakitafutia kwenye FIRIGISI wakati kiko kwenye MCHICHA  ambao UNAO.:-(
    Swali:
    • Unabisha?
    • Unauhakika kwako BABA ni BABA, Mama ni MAMA na RAFIKI sio PADRE kama HAUSIGELI /Hausiboi alivyo kisiri ni MPENZI?

    Ndio,....... kuna wageuzao ,......... ambacho KIPO hata kifudifudi MBELE ZAO!:-(
    Ni hilo tu na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

    Hebu Bassekou Kouyate arudishe mdinyo - Segu Blue




    Halafu ghafla The Commodores warudishe tena kile kitu fanki kile - Brick House
    Halafu The Temptations watubakize kwenye fanki na kuzima tena kwa -Shakey Ground


  • Huwa NAJARIBU!:-(

    Posted: January 29, 2012, 12:56 pm by SIMON KITURURU
    Hebu Kaka Joseph Hill anisaidie katika-I  TRIED




    Au ngoja tu Jean-Claude Naimro alainishe kwa - En Balaté
  • Kuhusu yule KISURA ambaye kwako LABDA ni KISURA tu mpaka ukiunganisha umfikiriavyo akiwa UCHI!

    Posted: January 29, 2012, 7:08 am by SIMON KITURURU
    Ndio,....... labda NGUO ukatizia denge katika kuficha kitu,...... na umtamaniye labda ni nguo tu ambazo zaongezea matamanio kwa kuwa ukimfumania chooni wakati anakunya labda hapendezi kama akuvutiavyo UKIMTAZAMA wakati ANALIA kisa unamemfumania USO UKO UCHI ingawa hata umjuavyo huwa hafuniki USO hadharani!:-(

    Swali:
    • Si unajua ni RUKSA kunibishia?
    • Na si wajua kuwa UCHI si lazima uvue NGUO?


    Ndio,...... labda kuna ambao unapenda mpaka mawazo yao,.......... LABDA kwasababu tu hata KIMAWAZO ,........mawazo yao yanakufikia wakati yameshavalishwa CHUPI,...... na yangekufikia  HAYO MAWAZO wakati yako UCHI kama walivyo UCHI,......... labda ungetafuta MWAVULI kujikinga ili usinyeshewe MAVI hata KIMAWAZO!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
    JUMAPILI NJEMA MKUU!



    Hebu Chaka Demus na Pliers waanzishe zaidi kwa-Gal wine




    Chaka Demus , Pliers na Jack Radics waingizie pia kamanyola bila jasho ile -Twist and SHout




    Halafu ghafla BUJU BANTON aingilie kati kwa-HUSH baby HUSH




    SHABBA RANKS ajaribu kuzima kwa tusi-Wicked in a bed




    Ila INNER CIRCLE ndio wazime tena kwa- SWEAT
  • Kabla HUJAONDOKA,....

    Posted: January 28, 2012, 3:57 pm by SIMON KITURURU
    ..... LABDA kuna MAHALI unaelekea TAYARI,......... hata kama unafikiria umekaa tu KITAKO kwenye eneo ulokalia HATA KAMA ni lile  uliitalo KIGODA.
    Swali:
    • Unabisha?

    Ndio,......... na KIMAWAZO,.........labda hata sasa hivi HAUKO ulipo hapohapo udhaniapo ndipo ULIPO!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


    Hebu tupate TUKUNYEMA kutoka kwa EDDY GRANT katika -WAR PARTY




    EDDY GRANT arudishe ile tukunyema-Walking On Sunshine





    EDDY GRANT arudie na tukunyema-HELLO AFRICA


    Adinye kiduchu tena -Gimme HOPE Joanna
    EDDY GRANT atungunyue kiduchu pana zaidi ile tukunyema-Killer on the RAMPAGE


    Halafu azime kwa-Living on the FRONTLINE

  • ....labda MTU hawezi kusema kaona aibu ya kuchungulia kabla ya KUCHUNGULIA!

    Posted: January 28, 2012, 12:32 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,......... na labda AIBU za MTU ,........ ni MATUNDA na FUNUNU za VIJULIKANAVYO vidude kwa MTU,....... na aoneacho aibu mtu ,...
    .... kwenye hicho LABDA kuna kitu ANAJUA kimfanyacho aone aibu.


    Swali:
    • AU?

    Ndio,........ labda UKIONEACHO aibu,....... umekiona hicho hata kwa kukichungulia!
    Swali la kizushi:
    • Unafikiri VIPOFU hawana aibu?
    • Na unafikiri VIPOFU hawaoni hata kwa jicho la ndani?
    Ndio,......na KIPOFU huchungulia pia ,.........kama ukiangalia kiundani!
    Ni wazo tu hili MKUU!
    Jumamosi Njema MKUU!

     Hebu Nit Doff aingilie kati kwa - Sunugal



    Halafu Kool & The Gang waingilie kati na kurudisha -Fresh



    Halafu Kool & The Gang wazime kwa -Hi De Hi Hi De Ho

  • Kwa kuwa ETI kunawadhaniao hakuna JINSI ya kuutafutia UTAMU jina JIPYA!

    Posted: January 27, 2012, 9:04 pm by SIMON KITURURU
    LAKINI,...
    ..... tokea enzi za kale LABDA,....
    ..... utamu ni uleule ila ni MAJINA tu unapewa MAPYA!

    Swali
    • Si wajua CHACHU , chungu, tofauti ya utamu wa uke na kachumbari, tamu kama WAZO LA  ngono .... au tu tamutamu kama sukari -ilikuwepo tu tokea enzi na LABDA ni majina TU inapachikwa tu ili JUMA na ROZA waelewane wanaongelea PILIPILI au BAMIA kiutamu katika hoja za KITUMBUA?

    Ndio,...
    .....ni wazo tu hili NGULI!
    Ijumaa na WIKIENDI NJEMA Bingwa!


    Hebu La Chepuya waingilie kati kwa - Checo Acosta


    UB40 wajaribu kupunguza spidi kwa kulalamikia ya PANYA FULANI katika -Rat in mi Kitchen




    Halafu BUSTA a busti kwa kuzima katika -HATARI

  • Wakati bado TUNAPENDA yale MAJIBU tuyapendayo!

    Posted: January 26, 2012, 10:27 pm by SIMON KITURURU
    Ndio unaweza kubisha,....... LAKINI,...
    ... labda ni kweli WATU WENGI hata UWAJUAYO hawapendi MAJIBU TU,...
    ... ila KIPENZI  ``KIJIBU ´´ kwao ni MAJIBU wasiyoyajua,...... na  ila MAJIBU ni  yale AMBAYO  yanaegemea kwa wayaaminiyo ndiyo MAJIBU  HAAAASAAAA kistaili ya WAAMINIVYO,....... kitu kifanyacho  katika ukweli wa ni nani kiudaku ni CHANGUDOA  waaminio hata KIHISIA TU  kabla  ,....
    .....kuwa ni CHANGUDOA,...
    .....watafurahia au hata kukubaliana nawe KIRAHISI ni CHANGUDOA hata kama hakuna USHAHIDI yule umsemaye ni kweli ni  CHANGUDOA  ambaye tayari wanahisi ni CHANGUDOA.
    Swali:
    • SI ni kweli hata kama majibu ni ya kihisia tu na hatuna uhakika kiushahidi au KISAYANSI- majibu yakaayo KIKRISTO yanaweza furahisha kama sio kukubalika na WAKRISTO kama tu yale MAJIBU ya KIISLAMU yawezavyo kukubalika na WAISLAMU kama sio kuwafurahisha  hata kama hayana UTHIBITISHO?

    Ndio,...
    ...labda TUNAPENDA majibu tuyapendayo,...
    .. na kwa MLEVI majibu yafagiliayo ULEVI hunoga zaidi kuliko yale yaonao WALEVI kuwa mambo zao DUKINAA tu!:-(
    Swali kiaina:
    • Hivi enyi wachawi WA  TANZANIA mbona Hamsifiwi wakati fani yenu  ya KICHAWI ni imara tu tokea enzi za mababu  TANZANIA na wengi wenu HAMJITOKEZI kunenepea fani yenu ilivyo nene TANZANIA mpaka muwe mnaumiza tu?
    • Halo MCHAWI hivi kweni MAZERUZERU mnawafanyia nini kikweli?
    Ndio,...
    ... jibu la nililouliza hapo juu naweza KUOGOPA JIBU,...
    ... ila NIMEULIZA!:-(

    Ndio,...... ni wazo tu hili MHESHIMIWA Kibanangenge!PAMOJA SANA BANDUGU BAPENDWA!

    Hebu tubadili kidude kwa msaada wa Bi KIDUDE kwa kuanzisha upya kwa -KIJITI



    Bi KIDUDE azime tena kwa-AHMADA
  • Stori za MTOTO Mzuri avutiaye KWA MBALI kwenye BAA kabla HUJAONGEANAYE!

    Posted: January 26, 2012, 9:54 pm by SIMON KITURURU
    Kuna MTOTO MZURI kwenye baa ambaye anavutia kabla hujaongea naye hata KITAFSIDA!Ila kuna MAMBO labda ongea na mtu NA utasahau mwanzo mapaja, KIFUA CHAKE KAMA SIMBA au sura yake ilikuwa ndiyo SUMAKU kimvuto ili uongee naye hata kuomba ambayo kimajina ni mazuri hasa bila kuya ita- KITAFSIDA!
    Swali:
    • Kwani hujastukia kwa mbali MVUTO unaweza kuuawa  na kusikiliza AVUTIAYE anaongea NINI baada ya kumsogelea?
    • Na si ushastukia saa nyingine  ni MIAKILI au TABIA zijitokezazo kwenye UONGEAYENAYE na wala SIO kwenye ndoto za utakaye kuongea naye - ndizo huua MVUTO wa MTOTO MZURI yule kwa nje anakalio kama malaika au MHESHIMIWA ambaye akifunga mdomo unakuwa unauhakika anamiakili na masuluhisho kuliko BULICHEKA na suluhisho la kujenga NYUMBA juu ya MTI?


    Ndio,...... fantansi zako hata za Rais KIKWETE  wa jamuhuri wa muungano wa TANZANIA labda zinamvuto zaidi kabla HUJAMSIKILIZA ,....
    .....na ukimsikiliza ASKOFU TUTU kama tu BABU wa LOLIONDO na SHEKHE YAHYA waweza kuhitimisha labda SURA ni NZURI kuliko waongeleayo!
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!Siku NJEMA!

    Hebu OffSide Trick na Baby J warudishe tena kidude- Kidudu Mtu



    OFFSIDE TRICK waongezee kipele-FATAKI



    OFFSIDE TRICK waongezee SHUGHULI kwa-Samaki





    Halafu hebu OFFSIDE TRICK na Mzee Yusuph wazime tena kwa jipu lawalawa-BATA



  • Katika TASNIA ya KIFICHO ile ya MHESHIMIWA kuonea aibu anachowaza HADHARANI!

    Posted: January 26, 2012, 9:48 pm by SIMON KITURURU
    Kuna tasnia ya AIBU,...
    ....NA LABDA ILE AIBU ya kuonea aibu hata UNACHOWAZA,....
    .....kisijulikane  unakiwaza HADHARANI bila sababu MAALUMU!:-(
    Swali:
    • AU?

    Ndio,.......na LABDA KUNA KITU katika  yasemekanayo HATA katika  kila KITU,....... kama katika ya kila KITU,........ inahitajika kukisema katika HADHARA  fulani hata kama HADHARA yako ni BAFUNI wakati unaoga na UKO PEKE YAKO kisa unakionea aibu ingawa wakati huo hicho ndicho KILA KITU!:-(

    Swali:
    • AU?
    • Kwani haujui kikusumbuacho rohoni moja ya dawa ni kukitamka?
    Na kama unajiheshimu na utakacho ni kutosikika katika ambacho wakati huo kiumuhimu ndicho kila kitu kwako,...
    ....labda BAFUNI  ukiwa peke yako ni MUHADHARA,...
    .... na peke yako kwenye kelele za maji SEMA KWA SAUTI utoe DUNGUDUNGUDUNGUNYIKO ROHONI  kwa kuwa hapo bafuni ni HADHARA yako ya kuongelea ambacho bado huna nguvu yakuongelea hadharani katika hata swala la kwanini chupi yako na sio MAWAZO YAKO ,.......ghafla NDIO  inachafuka zaidi NANIHII kuliko zamani INGAWA bado wataka hiyo iwe siri yako kwa watu walio HADHARANI kwenye wambea, WAZAZI uwaheshimuo mpaka kwa mpenzi wako kibogoyo bado wadhani ni busara iwe SIRI kwa siri ili utunze woga wako uliouzoea wakutotaka kuchafua NANIHII!:-(

    Swali:
    • Unabisha?
    • Na si unajua kuchafua hata hali ya hewa kimawazo au kiushuzi  maranyingi ni tatizo kubwa kisaikolojia kwa alipaye uzito chafuo hasa kwa kuwa kwa wengine labda wala sio CHAFUO?

    Ndio,...
    .... LABDA kuna tasnia za watu zilengazo ya KUONEA AIBU WATU ambayo usipoona aibu utatia AIBU kisa maswala tu ambayo JAMII imejijengea mpaka YAFANYA WANAJAMII BAADHI WALIO WENGI wanawazo MPAKA  la kuficha ndani ya CHUPI YA MAWAZO yale MAWAZO yahitajikayo kuwa UCHI HADHARANI katika jamii,....

    .... kwa kuwa ETI labda TU labda visivyosemwa HADHARANI ili MHUSIKA ATUNZE ADHANIAVYO NI HESHIMA hadharani,.........na labda ndio MAANA kuna watu wanaendelea KUFA BILA SABABU SASA HIVI PIA kisa WAVIJUAVYO WANAAIBU navyo  HADHARANI na wanajiheshimu navyo ambavyo visingewaua ila wanavionea AIBU ,...
    ....ila VYAWAUA  kwa kuwa WAHESHIMIWA  wale WAATHIRIKA wawaheshimuo ,...
    .....kwa matendo yao yametabiri YASIYOHESHIMIKA ni NINI- na yawafanya WAATHIRIKA wajisikie AIBU mpaka KUFA kwa yatibikayo kisa WANATAKA waheshimike KATIKA JAMII YA wawaheshimuo!:-(

    Ni wazo tu hili NGULI!Siku Njema Mkuu!
    Hebu Al Green abadili tena kwa KURUDISHA old schooL soul ile-Tired Of Being Alone




    Al Green aongezee ndude-Love and Happiness




    Halafu Aretha Franklin aongezee dozi kwa -Chains of FOOLS


    Aretha Franklin alainishe kwa makali-Respect


    Ila tu hebu SHAGGY , RIHANNA na Mr BEAN wajaribukuzima kwa -Bombastic



    Au tu SHAGGY mwenyewe ndiye azime kwa-Boombastic




  • Etta James!

    Posted: January 24, 2012, 7:12 pm by SIMON KITURURU
    Nimechelewa kidogo kukuaga rasmi!R.I.P Miss James! !
    Jamesetta Hawkins a.ka Etta James (January 25 1938-January 20 2012)



    Bado nasikiliza kazi zako MISS kama hii-AT LAST
  • Eti kisa ni kwamba KACHUMBARI huwa haisifiwi kuwa ni CHAKULA!

    Posted: January 24, 2012, 4:19 am by SIMON KITURURU
    KACHUMBARI ni CHAKULA,....... ingawa bado kuna wadaio  kama KILIWACHO  sio UGALI kwa kuwa ni WALI basi kiliwacho sio CHAKULA na alaye anapasha tu moto kabla hakijaletwa cha kikweli CHAKULA..


    LAKINI  ukikaa mkao wa kuchukulia KACHUMBARI kama CHAKULA,...
    .... kachumbari hushibisha  tu pekee hata bila chipsi dume au chipsi mayayi ambayo  kwa wengine ni kifungua kinywa tu  au  kionjo tu cha barabarani kabla hujaenda nyumbani  kwenye FULU KUBUGIA NANIHII kwa watazamavyo baadhi CHAKULA.
    Swali:
    • Si umestukia SHUKA ni nguo yakutosha  hata bila chupi kama ukiliangalia kimtazamo wa KILUBEGA Kimasai?
    • Kwani kwako chenye sifa fulanifulani hakiathiri ukipavyo sifa FULANIFULANI? 
    • Unafikiri KACHUMBARI PEKEE haishibishi?

     Ndio LABDA,.......ukigeuza mtazamo  ,.........KACHUMBARI ni chakula tosha TU hata kama hiyo sio SIFA YAKE ,........ na hata kama kachumbari yenyewe tuongeleayo hapa NI baiskeli  katika ya wafikiriao usafiri lazima iwe ni wa GARI na yabaiskeli hayaitwi SAFARI!


    Ni wazo tu hili kinanihii MHESHIMIWA!Jumanne NJEMA sana MKUU!

    Hebu UB 40 waingilie kati kwa - Please Don't Make Me Cry



    UB40 waongezee dozi kwa -The Way You Do The Things You Do



    Halafu hawahawa UB 40 wazime kwa -Here I am Baby





    Juzijuzi niliwadaka UB40 wakiwa live kama katika baadhi ya picha za juzijuzi zifuatazo...







  • Jinsi ya kuanza KUKALISHA Mawazo sio KIBIBLIA!

    Posted: January 23, 2012, 10:19 am by SIMON KITURURU

    Kuna MKAO fulani MAWAZO yako yamekaa,...... hata kama hayajakaa KIPAGANI au KIKURUANI!

    Swali:
    • AU?
    • Si yasemekana kunawasahauo kuwa mawazo yao labda yameegemea MRENGO fulani?

    Ndio,....... labda kukalisha MAWAZO ni jambo MTU ajifunzalo tu,......... na kuna uwezekano MAWAZO ya mtu hata yale yasiyokaa KIKURUANI au KISABATO bado yamekaa tu MKAO fulani ambao LABDA   ni wa KIVYAKOVYAKO!


    Ndio,... ... ni WAZO tu hili MHESHIMIWA!Jumatatu NJEMA Mwayego!

    Hebu Mighty SHADOW arudishe makalipso katika -Universal Language



    Mighty Shadow aongezee-I wish






    The Mighty Shadow atekenye pia - Doh Mix Meh Up


    Halafu ghafla Mrisho Mpoto na Maunda waturudishe Tanzania kwa pini - Samahani Wanangu


  • NI rahisi KUJENGEA MIPAKA uyajuayo kama tu UWAJUAO ingawa labda uhitajiyo ni yale USIYOJUA na wale USIOWAJUA!

    Posted: January 22, 2012, 12:35 pm by SIMON KITURURU




    Na siye TUSIOFITI kwenye UYAJUAYO na UWAJUAO,....... labda  usipoangalia  waweza kufikiri kwenye MAISHA yako UNATURUKA.
    Ila tusiofiti na YASIYOFITI kwenye ULIMWENGUWAKO,...... yapo tu AISEE na labda tuna na YANAKUGUSA hata kiusivyotegemea,.....
    ....ingawa hutustukiii hata katika tukojoayo pembeni ya BARABARA hadharani.:-(

    Swali:
    • SI unakumbuka YAKO na YA DUNIA YAKO labda bado nni nukta tu hata katika INSHA ya ULIMWENGU wako?


    Ndio,...
    ... YAKO  hata tukiyajumlisha na YANGU YOTE,...
    .... labda kihesabu bado sio YOTE!
    Na ni wazo tu hili MKUU!
    Hebu turudi ANGOLA ili David Zé aanzishe upya kipengele kwa - Mwangolé(O guerrilheiro)






    David Zé aongezee dozi kwa -Undenge Uami

    '
    Tuhame kidogo kwa msaada wa Stephen Marley katika kitekenyeo - Made In Africa




    Halafu hebu Damian Marley na Nas wazime kwa kuchezea wimbo wa DAVID Zé katika -Friends

  • UPOLE!

    Posted: January 22, 2012, 11:12 am by SIMON KITURURU
    UPOLE  labda ni ni SANAA tu ya kuficha HASIRA au tu HAMAKI!
    Swali:
    • AU?
    Ndio,...
    ...LABDA upole wa MTU ni tafsiri yako tu!


    Ni wazo tu hili BINGWA!Jumapili njema MHESHIMIWA!
    Hebu KASSAV waingilie kati tena kwa -Ave'w Doudou


    Halafu Ambelique azime kwa - New Sheriff In Town


  • Kijiwe kiko PUMZIKONI,...

    Posted: November 28, 2011, 10:04 am by SIMON KITURURU
    ...tutaonana hapa MWAKANI,........ kama MUNGU akipenda!

















  • TANZIA

    Posted: November 27, 2011, 11:57 am by SIMON KITURURU



    FAMILIA YA MWAKIPUNDA WA NGAMANGA IPINDA KYELA MKOANI MBEYA WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MPENDWA WAO ANNEL MWAKIPUNDA MWAISUMO KILICHOTOKEA TAREHE 26/11/2011 DAR ES SALAAM. MAZIKO YATAFANYIKA MOROGORO TAREHE 28/11/2011.

    HABARI ZIWAFIKIE FAMILIA YA MWAKIPUNDA,FAMILIA YA MWAISUMO,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI POPOTE WALIPO.

    BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE NA MILELE

    AMEN
  • Haya tena:Jesus was a Buddhist Monk( BBC Documentary )

    Posted: November 26, 2011, 8:15 pm by SIMON KITURURU

  • VIVA KAMANDA LOWASSA

    Posted: November 26, 2011, 4:17 pm by SIMON KITURURU



     LOWASSA KUANZA KUANIKA UKWELI KUHUSU RICHMOND KWA KWELI NAONA ANAFANYA KILE NILICHOWAHI KUTABIRI KWENYE MAKALA YANGU YA "LOWASSA SEMA NENO MOJA TU"
    ...NIMEAMUA KUMTUNGIA SHAIRI HILO HAPO CHINI...





    Kalamu yangu nashika, shairi nakutungiaKamanda umeongea, kiwingu umeondoaHukutaka kusinzia,makosa kuyarudiaJibu umetupatia, viva kamanda Lowassa


    Mwananchi nimesoma, la jana nilinunuaMachoya yakatuama, dukuduku umetoaUliyosema Dodoma, Kwakweli yanavutiaJibu umetupatia, viva kamanda Lowassa


    Richmond kupasua, mapema uligunduaKikwete ukamwambia, mkataba kuondoaRais akakataa, nini alitegemea?Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa


    Nape akashikilia, lile asilolijuaMikoani kaambaa, uzushi kang’ang’aniaJinalo kulichafua, wewe ukavumiliaJibu umetupatia, viva kamanda Lowassa


    Mapema nilitabiri, falsafa nikapingaMagamba sikukariri, kuvuana sikuungaUkweli niliukiri, mantiki iso kungaJibu umetupatia, viva kamanda Lowassa


    Beti sita nakomea, kalamu naweka chiniMengi nimeongelea, soma tena kwa makiniYatazidi kutokea,kusini kaskaziniJibu umetupatia, viva kamanda Lowassa.

    Shairi limetungwa na Nova Kambota Mwanaharakati,+255717 709618novakambota@gmail.comwww.novakambota.comTanzania, East AfricaJumamosi, November 26, 2011
    Nimetumiwa hii nanihii na:Nova Kambota
  • Kama NCHI iumwayo inahitaji TIBA ya haraka , labda DEMOKRASIA sio DAWA .

    Posted: November 26, 2011, 3:22 pm by SIMON KITURURU
    Mifumo ya KIDEMOKRASIA inakamchezo ka KUCHELEWESHA mgonjwa kupewa DAWA hata ijulikanayo kuwa inatibu GONJWA,...
    ... kisa DEMOKRASIA inafanya WATU hata WASIOJUA KINACHOENDELEA kuruhusiwa KULUMBANA hata kuhusu dawa wasizozijua  wakati mgonjwa anaendelea kuugua ,......kisa KIDEMOKRASIA kila KIMBULUKUTU inabidi KISIKILIZWE ili iaminike hata dawa sahihi aijuaye ni MTU MMOJA imeamuliwa na WENGI.

    Swali:
    • SI unakumbuka WENGI WAPE lakini kama wengi watakacho kupewa kinavimavimavi bado MMOJA ajuaye hao wengi wanakosea bado ndio MWENYE dawa sahihi hasa kama vimavimavi sio sahihi hata kwa hao wengi waliochagua bila KUJUA wanachagua nini?


    NI wazo tu hili MKUU!Hebu tupumzike kiwazo zaidi kwa kudeku...


    China's Capitalist Revolution - BBC (6.2009)

    http://www.bbc.co.uk/programmes/b00lfcz6
    Producer: Robert Coldstream
    Executive Producer: Nick Fraser.
    Aired: June 20, 2009, July 25, 2009
  • Twanga Pepeta wavamia jiji la London

    Posted: November 26, 2011, 12:15 pm by SIMON KITURURU
    [www.youtube.com]
    Bendi ya Twanga Pepeta imewasili leo mjini london tayari kwa makamuzi katika
    ukumbi wa Silver Spoon London kwa ajili ya Kuadhimisha miaka 50 ya
    uhuru wa wa Tanganyika. Usikose show hii ya Ukweli
    Asanteni,
    Urban Pulse Creative



    Nimetumiwa na:Frank Eyembe wa Urban Pulse
  • Leo katika Mtonesho: CHINA ndani ya Bongo / AFRIKA/The Chinese Are Coming

    Posted: November 26, 2011, 10:05 am by SIMON KITURURU
    China's Investments in Africa








    BBC Documentary - The Chinese Are Coming



    Hebu tudeku mahali pengine ambako sio AFRIKA kwa kina WAZUNGU OBAMA  katika kidude:The CHINESE are not COMING, They are ALREADY here




    Ni MTONESHO tu huu MKUU!
  • Ya DUNIA: Mwanamke ampika MUMEWAKE!

    Posted: November 25, 2011, 10:55 pm by SIMON KITURURU
    Haya DEKU mwenyewe stori,...
  • Kikuchekeshacho chakuchekesha kwa kuwa kuna kitu katika hicho unajua Mshikaji!

    Posted: November 25, 2011, 1:20 pm by SIMON KITURURU
    Na vichekesho kwa kawaida havina maana ,....... kama havibebi  unalojua Mshikaji!
    Swali:
    • Mshikaji  si unakumbuka lakini  kuwa huhitaji  kujua kikulizacho  ili ulie?

    Ni hilo tu MSHIKAJI!Na Ijumaa na WIKIENDI njema MSHIKAJI!

    Hebu BARON aturudishe Trinidad & Tobago katika-Somebody




    Eddy Grant aturudishe Guyana tena kwa SUGAR BUM BUM


    Halafu azime tena kwa -Hello AFRIKA


  • Watanzania wawili kucheza ligi daraja la pili Sweden

    Posted: November 25, 2011, 12:13 pm by SIMON KITURURU

    William John

    Joseph Kaniki (Golota)



    Wachezaji wawili wa kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) na William John wamefanikiwa kujiunga na timu ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio( Trials). Majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya thelathini ambapo wachezaji watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF)
    Habari hii imeletwa kwenu na:http://www.africa4life.com/

    Nimetumiwa na:Nancy Mtunga
  • Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone Awarusha Wakaazi wa DMV

    Posted: November 25, 2011, 10:57 am by SIMON KITURURU
    Mwana muziki wa kizazi kimpya ndani ya Washington DC, AJ Ubao wa kwanza (kushoto) pamoja mzee wa kuwachanganya Dmk global Dickson Mkama. wa kwanza( kulia) wakiwanyumba ya jukwa na mwana muzingi aliekuwa anasubiriwa kwa hamu siku ya jana Jumatano Nov23, 2011 katika sherehe za Thanksgiving Muimba Jose Chameleone katikatia, akisubiriwa kwa hamu na wapenzi wakeNyuma ya jukwa mwana dada Luren akipata flash ya pikee kabla ya unyesho kuanzaaMuimbaji Ana Lov akipata flash ya pamoja na rafiki yake kwenye onesho hilo la  Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone.Cheif wa swahilivilla Abou Shatry akipata picha ya pamoja na kundi zima la muimbaji kutoka Uganda  Jose Chameleone.Aj Ubao alikuwa ni mumbaji wa pili kuimba katika onyesho hilo waliosherikiana na mwanamuziki wa kutoka Uganda Jose Chameleone, wakiwa nyuma ya jukwa  akipata flash ya pamoja na mdhamin wake wapendoWapenzi wa tazamaji wakisubiri kwa hamu onyesho hilo kuazarasmi ndani ya ukumbi wa Rendezvous mitaa ya Parklawn Dr, Rockville Maryland U.SMwana muziki wa kizazi kimpya kwa muziki wa R&B ndani ya Washington DC, AJ Ubao akiwarusha vibaya sana wapenzi wa muziki wa nyumbani wanaoishi hapa DMV Jana jumatano Nov 23, 2011 Nchini Marekani.  Wapenzi wa muziki wakinyumbani wakiwa wanamshangaa Msanii wa hapa Washington DC, AJ UbaoMwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone akifanya vituz vyake ndani ya Rendezvous Hall mitaa ya Parklawn Dr, Rockville Maryland U.SMamia ya watu jana walifurika kuja kumuangali Msanii kutoka Nchini Uganda  kwa jina maarufu la Jose Chameleone, ana nyimba zake, ikiwemo mama roda, Jamalila analia, na nyingi nyenginezo.Mamia ya warembo waliohudhuria kwenye Show hiyo ya Mwanamuziki wa Uganda Jose ChameleoneWarembo mikono juu wakiwa wamevudiwa na uwimbaji wa mwanamuziki huyo ndani ya ukumbi uliofurika warembo wa Kiafrica.Juu na chini full warembo wakipata hisia za muziki wa muimbaji maarefu kutoka nchini Uganda Jose Chameleone.   Sauti ya muimbaji Jose Chameleone inayofurahisha warembo wamuziki wa kinyumbaniKama kawaida yake akiwa na kundizima ndani ya Washington DC Jana Jumatano Nov 23,2011Wakati mwengine warembo hupandwa na jazbaba wale wanaposhindwa kujizuwia na kuomba mic ili kuchombeza wimbo uliokuwa unaimbwa hewani wa kipepo   Mambo ya jana hayo cheza ni kucheze ndani ya Rendezvous HallMapozi na wewe: mrembo akipata picha kutoka kwa mpiga picha wetuHivyo ndiovyo ilivyoo hakuna fitinaCheza nikucheze juu na chini warembo wa Kiganda ndani ya Nyumba Mrembo aleehudhuria ndani ya unyesho hilo kabambe la Muimbaji Kutoka Nchini Uganda  Jose ChameleoneKwakweli ilikuwa sho ya aina yake wapenzi wengi ambao ni Waganda aliofurika na kumuunga mkono jamaa yaoMwana mitindo wa Uganda jina lake hatujaweza kulipata vyema lakini ni Mwanamitindo wa Uganda!Cheza ni kuche hiyo huku warembo wakipata flashi ya pamoja kwenye show hiyo ya Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone Alivyo warusha Wakaazi wa DMV Jana Nov 23, 2011 kwenye siku kuu ya Thanksgiving Nchini Marekani. Picha zote na [swahilivilla.blogspot.com]

    Nimetumiwa hii na:Juma Issa
  • Twanga Pepeta Wakamata Pipa

    Posted: November 25, 2011, 10:13 am by SIMON KITURURU
    Bendi ya Twanga Pepeta wakijiandaa kuingia kwenye PipaChalz baba akiwa tayari kuingia kwenye PipaFull Mzukakikosi cha Twanga kikijiaandaa kuingia Katika Uwanja wa Julius NyerereKutoka Kulia Amigolous akiwapa Mikoba Jojoo, Jumanne, Baby Tall na Luizakutoka kushoto Shalapova, Charles Baba na ShakashiaMaria Soloma akiwaaga mashabiki wake NyumbaniVictor Mkambi mpiga kinanda wa Twanga akiwa na Maria Soloma ambae ni dancer wa twanga


    Salam,

    Twanga Pepeta ''KISIMA CHA BURUDANI''  wameondoka leo asubuhi kutoka uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea  kuvinjari katika Jiji la London ili kusugua kisigino na wapenzi wao walioko nchini Uingereza na nchi jirani ikiwa ni katika kusherehekea maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.  Kundi hilo lililokamilika katika safu zake za waimbaji, wapiga vyombo na wacheza show linatarajiwa kuwasha moto wa burudani yao siku ya Jumamosi, tarehe 26 Novemba 2011 katika Ukumbi wa Club 2000 Savoir Banqueting Suite, Popin Building Southway, Wembley HA9 0HB kuanzia saa Tatu Kamili Usiku mpaka alfajiri (9pm  til late).Mheshimiwa Balozi Peter Kalaghe atakuwa mgeni rasmi. CD za album mpya na za zamani zitauzwa na vinywaji pamoja na vyakula vya kitanzania vitakuwepo vya kumwaga. Viingilio vitakuwa £20 (singles)  na £35 (couples) kabla ya saa sita (mid night) na £25 (singles) na £40 (couples) baada ya saa sita usiku.
    Njoo tujumuike, njoo usugue kisigino, njoo usherehekee uhuru wa nchi yako, njoo ule na kunywa kitanzania. Burudani ni watu na watu ni pamoja na wewe. Tanzania itajengwa na watu wenye moyo kama wewe. Karibuni sana.
    Shughuli hii imeandaliwa na Urban Pulse Creative wakishirikiana na Miss Jestina Blog, chini ya maelekezo thabiti ya Ubalozi wa Tanzania, London. Tumethubutu, Tumeweza na Tunaendelea Mbele

    Nimetumiwa na :Frank Eyembe
  • Katika KUMBUKUMBU:George Washington Carver

    Posted: November 24, 2011, 7:00 pm by SIMON KITURURU
    George Washington Carver
    SIO SIRI
    .....jamaa NAHISI ni mmoja ya MTUZ,........ambaye naamini WATU weusi wanahitaji KUJIVUNIA!




    Hebu tekenya.........An Introduction to Dr George Washington Carver



    Endeleza kipengele....



    Mdake kwenye HABARI...



    Habari zake zaidi jaribu kubinyabinya HAPA
    .... au hata  HAPA
  • ASANTE KOTOKO in DAR

    Posted: November 24, 2011, 5:48 pm by SIMON KITURURU


    TIMU ya soka ya KUMASI  Asante kotoko ya Ghana inatarajiwa kuwasili nchini Desemba 9 tayari kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya kombaini ya timu za Yanga na Simba siku ya Desemba 11 kwenye uwanja wa Taifa.Mchezo huo ni sehemu ya kukamilisha maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Future Century Limited, Helen Masanja.Masanja alisema kuwa timu hiyo itafikia Zanzibar na baadaye kuja jijini Dar es Salaam kwenye hotel ya Lamada tayari kwa mchezo huo ambao umedhaminiwa na PPF, Kenya Airways, Vanedrick Tanzania Limited, Lamada Hotel na Vanne Fashion Tabata. Alisema kuwa wanatarajia kuwa na burudani ya aina yake kwani tayari kombaini ya timu ya Yanga na Simba itaundwa na wachezaji nyota wanaocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.Aliongeza kuwa   makocha wawili, mkongwe, Abdallah “King  Mputa” Kibaden na Fred “ Minziro” Felix ndiyo watakuwa wakuu wa benchi la ufundi la timu hiyo ambayo itaundwa na wachezaji 20 watakaotangazwa hapo baadaye. Wengine katika benchi la ufundi na meneja, Boniface Pawasa na daktari wa timu, Juma Sufiani.Alifafanua kuwa uteuzi wa timu hiyo hautajali uraia wa wachezaji hivyo kama wachezaji kutoka nchi za nje ambao wanachezea timu hizo watateuliwa, basi watacheza mchezo huo.Masanja alisema kuwa Yanga na Simba zimekubaliana na kuweka historia kwa mara ya kwanza tangu timu hizo zitengane mwaka 1935. Alisema kuwa historia inaonyesha kuwa timu hizo zilikuwa pamoja kuanzia mwa 1922.Mwenyekiti wa Yanga Lyod Nchunga alisema kuwa mechi hiyo itaondoa tofauti iliyopo baina ya mashabiki wa Simba na wale wa Yanga hasa zinapotokea timu hizo zinacheza mechi za kimataifa ambapo imekuwa ni kawaida mashabiki wa timu hizo kushangilia timu pinzania.Wakati Nchunga akisema hayo, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kuwa muungano huo utaleta tija kwa timu hizo ambapo mashabiki wa Simba na Yanga siku hiyo watakuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuishangilia timu yao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.Alisema kuwa huu ndiyo mwanzo wa kuanza kushirikiana katika mechi za kimataifa na kuwataka mashabiki kufika kwa wingi na kutoa sapoti kubwa kwao.


    Nimetumiwa taarifa na:Shaffi Dauda
  • Kwani MTANDAONI unastukiaje ANONYMOUS ni MWANAMKE au MWANAUME kimaandishi yake TU?

    Posted: November 24, 2011, 12:45 pm by SIMON KITURURU
    Najiuliza tu  baada ya kukutana  na baadhi ya WADAU WAWILI JANA  ambao mtandaoni nilikuwa nadhani ni WANAUME  ,....
    .... na kumbe ni vigoli bomba tu!(Msinitusi  kama mwanisomalakini leo)
    Na katika kuongeanao  tukatofautiana  kidogo kuhusu EMU THREE ,...
    ....wa DIARY YANGU
    ... wao wanadai ni demu na mimi tokea enzi hana BLOGU yake na nakutana na comment zake kwa DINAHICIOUS wa MAHABA  HUKU,...
    ... kuwa huyu NGULI ambaye nakiri simjui jina lake halisi ni DUME.

    Kwa M3:

    Ambiere M3 EEEH!,.....jana  kuna katopiki  ambako  kamefanya nipende zaidi staili yako kwani mpaka leo niwafahamuo kila mtu  anauhakika kivyake TOFAUTI kuwa wewe ni JINSIA GANI.
    Ila mie niko pale pale kuwa weye ni (kwa kipare)MGHOTHI aithee!
    Tukiachana na hilo:
    • Wewe unastukiaje JINSIA ya mwandishi asiye jitambulisha mtandaoni?
    • Na kwani ni lazima  kujua MWANDISHI KIJINSIA ni yule akojoaye kirahisi  kasimama  au ni yule achuchumaye  kiusataarabu ili kukojoa kirahisi  ili kulenga shimo  la choo cha shimo wakati MADA iongelewayo  labda haina uhusiano na jinsi ya kukaa kistaarabu  kwa aliyevaa sketi fupi kwa kuwa ni ile ya  hivi DAR -ES- SALAAM ile posta mpya itaitwa POSTA mpya mpaka LINI wakati labda wala sio MPYA tena siku hizi?


    Ni MTONESHO tu huu MHESHIMIWA na usikonde!
    Hebu Kleptomaniacs watunishe- Tuendelee



    Mashifta warudishe - System ya Majambazi




    Mashifta waongezee-Pesa ,Pombe, SIASA  na Wanawake

    Halafu LONGOMBAS wazime kwa kukumbusha-Vuta pumzi

  • Labda wenzetu WAZURI na wale wenye MIAKILI SANA watuachie kwanza siye wengine NDIO tuwastukie kwanza kuwa wao ni WAZURI au ndio WENYE MIAKILI sana!

    Posted: November 24, 2011, 11:17 am by SIMON KITURURU
    YATUMIAYO AKILI SANA ,...........labda ni YA KAWAIDA kwa  MWENYE akili,.......a.k.a  yatumiayo akili sana KWAKE ni kawaida !
    Na kwa isemekanaye ni  MZURI SANA,... ... labda yatakiwa UZURI wake uwe kwake ni KAWAIDA  kwa kuwa umemng'ang'ania  na kwake huo sio kitu cha kutia akili,...
    ....a.k.a UZURI  kaumbwanao kwa hiyo huo  kwake ni KAWAIDA.
     Swali:
    • AU?

    NDIO,...
    ... labda kustukia yatumiayo sana AKILI,...
    ... labda hiyo ni shughuli ya WENGINE ambao hustukia nani ni mwenye AKILI,...
    ... kama labda kama MTU  ni MZURI  labda hiyo  ni shughuli ya wengine  wastukio kwanza !

    LAKINI:
    • Si labda mtu akisubiria WENGINE   , wengine wanaweza wasistukie anamiakili  na pia haki yanani  labda ni kweli  yeye ni mzuri kweli  hata bila nguo kitu ambacho JAMII  kwa jamii IJIFUNDISHAYO  miakili na UZURI wake unaweza USITAMBULIWE?:-(

    Ndio,..... kuna WENYE akili wajijuao wanamiakili WASIOTAMBULIKA na JAMII kwa kuwa jamii  inakipimo tofauti cha nini AKILI SANA na usipopasi  mtihani wa jamii  basi weye hutambuliki,...
    ... kama tu ijulikanavyo kuwa JAMII ikijifunza kupenda wenye tako lililopigwa pasi  WAZURI  wenye tako kubwa huondoka kwenye kipimo cha wazuri katika jamii kisa tako kubwa na matege kwa mbaaaaali!:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

    Hebu DIDO aingilie kati na kulainisha kwa-THANK YOU




    Ghafla Youssou Ndour aingilie kati kwa-Medina


    Halafu Youssou N'dour azime kwa -Africa, Dream Again

  • Kuna wadhaniao UJINGA KISIRI CHOBISI unanafuu kuliko UJINGA HADHARANI kwenye UMMA!

    Posted: November 24, 2011, 10:00 am by SIMON KITURURU
    Lakini,........ labda MJINGA,....... ni MJINGA tu kama kitafsiri za wadaio kuna BINADAMU mwenye pumba za KIJINGA,...... hata kama ujinga wake MHESHIMIWA kafanya SIRI.

    Swali:
    • Kwani KUHUSU YA SIRI-unafikiri HATA kwa kuficha HATA nyege KISIRI inamaana mwenye nyege hana NYEGE kisa anazificha na hiyo nni SIRI?

    Na ndio ,........ hata kwa KISIRI,.......... labda kifanyacho MTU hufanya hicho ni SIRI,....... ni kwa kuwa UKWELI NI KWAMBA jambo lifanywalo siri hilo SIO SIRI na  lipo PALEPALE na ndio maana mwangalifu katika kumdeku mficha SIRI ,...
    ...yasemekana  jinsi MTU afichavyo siri ndio KIFICHUA SIRI.:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

    Hebu MCHUNGAJI Solomon MUKUBWA abadili wazo na kurudisha hali ya hewa laini kwa watu baadhi kwa kudinya pini la kikristo lile-Mfalme Wa Amani


    Halafu Zain Bhikha aingilie kati  mchezo kwa - Give Thanks to Allah

  • ...ndio HERUFI hujenga NENO na MANENO hujenga SENTENSI....

    Posted: November 23, 2011, 6:43 pm by SIMON KITURURU
     ...... ila  maswala ya  UJUMBE,............ hata sentensi iwe ni ipi LABDA hilo ni swala JINGINE!:-(
     Swali:
    • Na  si  unakumbuka maswala ya UJUMBE umuhimu wake labda UNATEGEMEA apataye UJUMBE anastukia au tu anahitaji UJUMBE GANI?


    Ndio,.........na SENTENSI zozote zile  labda zina UJUMBE,........ kama tu KWAKO  katika hizo unastukia UJUMBE,.........ingawa bado  swala la UMUHIMU wa UJUMBE HUO kwako,....... hilo nalo ni SWALA JINGINE.:-(
     NI wazo tu hili MHESHIMIWA!

    Hebu Zap Mama, Talib Kweli, Common wabadili kwa  - Yelling Away




    Au tu Talib Kweli azime kwa-Move Somethin'

  • Swala la kuwa na ``UHAKIKA NA KITU´´ labda ni jambo la kufanyia kazi KILA SIKU....

    Posted: November 23, 2011, 4:14 pm by SIMON KITURURU
     ....kwa kuwa  SWALA la UHAKIKA,...
    .... laweza kuwa lahitaji IMANI..........na  kwa bahati mbaya labda IMANI,....... moja ya misingi yake ni KUTOKUWA na UHAKIKA baadhi ya nyakati.:-(
    Swali:
    • Si unajua ulichonauhakika nacho LEO sio LAZIMA kila siku zijazo/KILA WAKATI  utakuwa na UHAKIKA nacho kwa KIPIMO HIKIHIKI cha LEO?

    Na  USICHO na UHAKIKA wala IMANI nacho LEO,...... labda ni swala la kukipa MUDA tu HICHO.

    Ni wazo tu HILI MHESHIMIWA!:-(


    Hebu Asa arudie - Jailer


    Halafu Seu Jorge aturudishe kidogo brazil kwa - Pretinha ao Vivo


    Halafu CEU hapahapa Brazil azime kwa- Malemolencia

  • Wakati kuna SARESARE MAUA -Weye UNAOGOPA nini na WENZAKO wanaogopa NINI?

    Posted: November 23, 2011, 3:17 pm by SIMON KITURURU
     Na labda  huhitaji hata HISTORIA kujua,....... labda wengine  hawaogopi hata KUFIA wanachokiamini ,...... kiwe ni  SIASA au hata DINI.
    Na wajua wengine HAWAOGOPI   MTU  wasiyemjua au hata kufia  NCHI  ambayo  kwa walivyo nyong'onyea labda ni nchi isiyo wajua angalau hata  KWA kuwaunga mkono angalau nao  wafaidike angalau na yake MADINI.

    Swali tena:
    • Je wewe UNAOGOPA nini?

    Na ni  ndio ,........kuna ambao waogopacho sana ni  VIBOKO,mitihanin, mende  au tu kuparuriwa na KUKU.

    Na ndio,...
    .... kuna waogopao vifo  ingawa wanapoteza muda kwa kuogopa visivyoua kama  vile vya majungu  rasharasha aka ``JE WATU WENGINE  WANAWAWAZAJE TU ´´ kitu ambacho  HAKIUI MTU  labda.:-(

    Je waogopa NINI?Ni wazo tu hili NGULI!



    Hebu Nneka Egbuna aanzishe tena kwa-Beautiful



    Nneka aongezee- Lost Souls


    Halafu Nneka ,Ziggy Marley na Eeday wazime kwa-Express Yourself

  • LABDA hakuna MTOTO awazaye akikuwa atakuwa mfanyakazi wa MOCHWARI kuosha MAITI!

    Posted: November 23, 2011, 2:13 pm by SIMON KITURURU
    Swali:
    • Au unafikiri kuna MTOTO atamaniye akikuwa ofisini kwake kuwe kunalazwa WAHESHIMIWA MAREHEMU?

    Ndio kuna ya UTOTO,....... na ya UTOTO ya mpenda UDEREVA ,......... mara nyingi sio  yale ya UKUBWANI ambayo huweza geuza MTOTO aliyependa kuendesha apende KUENDESHWA!:-(Swali:
    • SI umestukia UKUBWA nuksi  hasa pale  kama MTU ni mwenzangu na mimi asiye na MIURITHI ya KITAJIRI astukiapo inabidi afanyie kazi MSHAHARA na ofisi labda ni popote?
    • Na kazi si  ni KAZI tu  ingawa bado ukweli uko palepale  kuwa kazi nyingine MUHIMU   ni zile za kupima wingi wa minyoo kwenye kinyesi cha Mheshimiwa MAABARA ili kuhakikisha kama kweli MHESHIMIWA ana MINYOO?

    NDIO,....... na MAITI wanahitaji WATAALAMU husika ambao ni muhimu tu,....... ndio maana MOCHWARI ni ofisi tu za kawaida za WATU  tena labda wale waliokuwa wanaogopa stori za vifo UTOTONI.:-(

    NI WAZO TU HILI MKUU!



    Hebu AKON aanzishe upya kwa-Mama Africa



    Halafu Céu azime  kwa - Roda

  • Amigolous na Saleh Kupaza walonga.

    Posted: November 23, 2011, 1:38 pm by SIMON KITURURU
    Salam,
    [www.youtube.com]
    Wanamuziki Amigous na Saleh Kupaza kutoka  bendi ya Dansi Twanga Pepeta "KISIMA CHA BURUDANI" wakiongelea kuhusu maandalizi ya ziara yao Nchini Uingereza Katika Kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania yatakayofanyika tarehe 26 Novemba 2011 katika ukumbi Club Club 2000 Banqueting Suite(Former Silver Spoon) Popin Building Southway. Wembley HA9 0HB kuanzia saa 9pm- 4am. Kiingilio ni £20.00 kwa single na couple £35.00 kabla ya saa sita Usiku
    Asanteni
    URBAN PULSE CREATIVE wakishirikiana na MISS JESTINA BLOG




    Nimetumiwa hii na:Frank Eyembe
  • Afrika KUSINI na vyombo vya HABARI!

    Posted: November 23, 2011, 1:24 pm by SIMON KITURURU
    Ya: ``STATE SECRETS´´ law.......na dalili za WANAHABARI kufungwa midomo.....
  • Na ni mstari mwembamba kati ya KUFAULU na KUFELI!

    Posted: November 22, 2011, 5:36 pm by SIMON KITURURU
    Na  kama UMEFAULU,...
    .....labda  kumbuka kufeli kupo tu  ,...
    .... na kuna uwezekano  ALIYEFAULU  hajisikii kafeli kwa kuwa kaegemeza mitazamo yake mbali na YALE  aliyofeli.

    Na kama  MTU anajisikia KAFELI,....... akumbuke tu  KUFAULU kupo tu,....... .... na kiendeleacho  ni labda kabobea katika kuangalia zaidi ayatambuayo kama KUFELI.

    Swali:

    • Si  katika  MTU alilofaulu  akijichunguza bado MAISHANI anaweza kustukia nini alichofeli na ndio maana hata mtu ajulikanaye kwa kufaulu KISIASA kama NELSON MANDELA  bado anakiri wakati anafanikiwa KISIASA , kifamilia ALIKUWA anafeli  kitu kilichofanya ndoa zake mbili kufa na watoto kulelewa bila BABA?


    • Na si unakumbuka hata MOTHER TERESA yasemekana alikuwa anaona wale WALIOONEKANA na JAMII kuwa ndio waliofeli kimaisha  na kuwa masiki kupindukia ndio ambao KIIMANI  walionyesha kufaulu zaidi kuwa karibu na MUNGU?
    • Na si nasikia hata katika LIFAULIWALO/Lifaulwuo moja ya siri ya wafauluo HILO  ni kufeli katika hilo  bila kukata tamaa nakulifanyia kazi  hata kama ni  kimazoezi mara kwa mara  kitu kisahauliwacho na washabikiao  KUFAULU tu ?

    Ndio,...... labda tukumbuke  hakuna AFELIYE au KUFAULU  kila kitu,....... na  ni tabia tu zawatu  kuruka baadhi ya mambo kufanyacho  hapa DUNIANI kuna wenye lebo za kuwa wao WAMEFAULU,...
    .... autu ni wale WALIOFELI:-(


    Ni wazo tu hili MKUU!

    Hebu BONEY M warudie-MALAIKA



    Au tu Anjelique KIDJO naye arudie-MALAIKA

    Halafu tu tena BONEY M wazime kwa-JAMBO BWANA/Hakuna MATATA

  • Anayenipa motisha fulani leo ni: HELEN OYEYEMI!

    Posted: November 22, 2011, 5:15 pm by SIMON KITURURU
    Kama unahusudu kusoma au unahamu yakuandika,...
    ... cheki kazi za huyu mdada Helen Oyeyemi.......ambazo kiaina zimenianzishia wiki kisababu mbalimbali:
    Msikie kidogo akiongea....







    Habari zake zaidi HUKU


    Kwa kifupi:






    Helen Oyeyemi was born in Nigeria in 1984 and has lived in London since the age of four.

    She completed her book The Icarus Girl just before her 19th birthday while studying for her A-level exams. She is now a student of social and political sciences at Cambridge University.










    AU:

    Helen Olajumoke Oyeyemi (born 10 December 1984) is a British novelist. She was born in Nigeria and raised in London.

    She wrote her first novel, The Icarus Girl, while still at school studying for her A levels at Cardinal Vaughan Memorial School.

    Oyeyemi studied Social and Political Sciences at Corpus Christi College, Cambridge, graduating in 2006. Whilst at Cambridge, two of her plays, Juniper's Whitening and Victimese, were performed by fellow students to critical acclaim and subsequently published by Methuen.

    In 2007 Bloomsbury published her second novel, The Opposite House which is inspired by Cuban mythology.

    Oyeyemi is a lifelong Catholic who has done voluntary work for CAFOD in Kenya[1].

    In 2009 Oyeyemi was recognised as one of the women on Venus Zine’s “25 under 25” list. [2]

    Her third novel, White is for Witching, described as having "roots in Henry James and Edgar Allan Poe" was published by Picador in May 2009. It was a 2009 Shirley Jackson Award finalist and won a 2010 Somerset Maugham Award.

    Her fourth novel, Mr Fox, was published by Picador in June 2011.
  • YA PAKISTANI:Kutuma meseji ZA SIMU zenye matusi mwiko kuanzia hivi karibuni !

    Posted: November 22, 2011, 12:55 pm by SIMON KITURURU
    PAKISTANI yataka kampuni za simu kuzuia meseji zenye maneno ya matusi.
    ... na maneno kama ,Jesus Christ, Satan, TAXI, Idiot, yakiwa ni miongoni mwa ambayo itakuwa mwiko kumtumia meseji rafikiyo  ukitumia sentensi yenye maneno hayo..... DEKU ndude,...





  • ASHA BARAKA na AMOSI wazungumzia kuhusu 50th Independence Tour

    Posted: November 22, 2011, 11:01 am by SIMON KITURURU
    Salam,

    [www.youtube.com]


    Mkurugenzi wa African Stars ASHA BARAKA pamoja ofisa wa Ubalozi nchini Uingereza AMOSI MSANJILA wanazungumzia kuhusu maandalizi na matayarisho kwa ajili ya ziara ya Twanga Pepeta "KISIMA CHA BURUNDANI'' nchini Uingereza katika Kuazimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Show hii itafanyika jumamosi Tarehe 26 November 2011 katika Ukumbi wa Club 2000(Silver Spoon)Savoir Banqueting Suite, Popin Building Southway, Wembley HA9 0HB.
    Asante,
    Urban Pulse Creative


  • Ngumi kupigwa Desemba 18,MZALENDO PUB

    Posted: November 21, 2011, 12:23 am by SIMON KITURURU



    Na MWANDISHI WETU

    WASANII mbali mbali hapa nchini wanatarajiwa kutoa burudani katika pambano la mchezo wa ngumi lisilo na ubingwa litakalowakutanisha bondia, Mada Maugo na mpinzani wake Suleimani Saidi 'Toll' Desemba 18 mwaka huu katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama JIjini Dar es Salaam.

    Akizungumza na kona hii ya burudani Raisi wa shirikisho la ngumi za kulipwa hapa nchini (PST) Emanuel Mlundwa alisema, maandalizi kwa ajili ya pambano hilo yamekamilika.


    Aliwataja wasanii watakaotoa burudani siku hiyo kuwa ni Kundi la mapacha watatu Khalid Chokoraa (Halidi Chuma)pamoja na msanii wa mziki wa bongo fleva Mwana FA (Hamisi Mwinjuma).

    Alisema licha ya kuwepo kwa burudani hizo vile vile atakuwepo kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila Super D kwa ajili ya kutoa mafunzo kupitia Dvd pamoja na kuzisambaza.

    Aliwataka mashabiki wao wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani hiyo, licha ya kuwa mchezo huo haupewi kipaombele watahakikisha wanasonga mbele katika kuazimisha miaka 50 ya uhuru.

    aidha katika mapambano ya ngumi ya utangulizi mabondia Yohana Miyayusho na Shadrack Juma, Doto Kipacha atazidunda na Saidi Muhidini na kwa upande wa mchezo wa Kick Boxing ambao utatuwakilisha kimataifa Tanzania Muaythai Academy of Combat watawaletea mpambano kwa mara ya kwanza nchini kati ya bondia Emanuel Shija kutoka Tanzania na Munyeshyaka Vincent kutoka Rwanda Mpambano huo utakuwa wa kimataifa kutokana na ushiriki wake wa nchi hizo mbili nchini zitakuwa zikipeperusha bendera zao.
    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania


    Nimetumiwa hii na:Super D
  • Mahojiano Maalum na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda Part 3

    Posted: November 21, 2011, 9:23 am by SIMON KITURURU
    Salam,
    [www.youtube.com]
    Urban Pulse Creative inakuletea sehemu ya tatu katika Mahojiano maalum kutoka kwa Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
    .
    Asanteni,

    Urban Pulse Creative






    Nimetumiwa hii na :Frank Eyembe wa Urban PULSE
  • Ngumi kupigwa Desemba 9 DDC Keko Dar es Salaam

    Posted: November 21, 2011, 9:19 am by SIMON KITURURU
    Ramadhan Nassib kulia



    BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Ramadhan Nassib, anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na mpinzani wake Antony Kariuki wa Kenya, katika pambano la maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru litakalopigwa kwenye Ukumbi wa DDC Keko Dar es Salaam, Desemba 9 mwaka huu.

    Akizungumza  Mratibu wa pambano hilo, Pius Aghaton, alisema kuwa pambano hilo linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na rekodi zilizopo kwa mabondia wote.

    Alisema kuwa pambano hilo litakuwa la uzito wa Fly ambalo litapigwa katika raundi 10.

    “Tumeandaa pambano la aina yake kwa ajili ya kusherekea miaka 50 ya Uhuru na pia kuweza kuwajengea mabondia wetu uwezo wa kucheza mapambano ya kimataifa” alisema.

    Mratibu huyo alisema kuwa katika pambano hilo, kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo bondia Juma Fundi atazichapa na Juma Seleman katika pambano la uzito wa Fly la raundi sita, Fred Sayuni atazipiga na Bakari Dunda katika pambano la uzito wa Feather la rfaundi sita.

    Pambano jingine litawakutanisha mabondia Rashid Ally pamoja na Daud Mhunzi katika pambano la uzito wa Feather la raundi sita na Faraji Sayuni atazichapa na Alpha George katika pambano la uzito wa Fly la raundi nne.

    Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

    Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

    '' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

    DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

    Super D Boxing Coach
    Photojournalist at Majira, Business Times
    Email.superdboxingcoach@gmail.com
    www.burudan.blogspot.com
    Mob;+255787 406930
    +255774406938
    Po.Box. 15493
    Dar es Salaam Tanzania
    --
    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania


    Nimetumiwa hii na:SUPER D
  • LABDA hakuna PENZI liishilo bila UCHIZI wa wapendanao WAPENZI!

    Posted: November 20, 2011, 11:19 am by SIMON KITURURU
    Ndio,....... labda  kama hakuna UCHIZI kwenye PENZI LAKO,.........labda kumbuka kwa wengi  ukitumia akili  penzi tamu  sana  kwa kutumia akili  hushushwa dozi KIUTAMU  na kuna washushwao dozi  WAPENZI mpaka  penzi lao hata likichunguliwa halitawezwa kutofautishwa na PENDO LA DADA na KAKA hata ingawa pendo la DADA na KAKA ni chanya  tu hata katika maisha ya wasio DADA na KAKA kibinamu .

    SWALI:
    • Au?

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!JUMAPILI NJEMA  Mkuu!
    Hebu WILLIE BOBO asigine kidude kwa-GUAJIRA



    Au tu azimaye awe ni Oliver N'goma apenyezaye  tena ya- Lili

  • Wakati MHESHIMIWA labda sasa hivi ana hamu kweli ya KUMA leo!

    Posted: November 20, 2011, 10:50 am by SIMON KITURURU
    Na yasemekana,........TATIZO la kuma ni kuwa hicho kidude huja na MWENYE kuma.!
    Na nasikia,...... kuma na mwenye kuma ,........ maringo yao kwa watu wakawaida ambao ni wahitajio tu chakula kama kitu muhimu zaidi kimtazamo,...... yasemekana kuma na MWENYE kuma ni vitu viwili tofauti sana kama unaujasiri wa KUTOFAUTISHA. vitu:-(

    Swali:
    • AU?
    • Na si unakumbuka yasemekana MBOO haifanani na mwenye MBOO?

    Ndio,...... ni wazo tu hili MHESHIMIWA ,....... hata kama kwako wazo hili labda halijavaa chupi!:-(

    Hebu SEAL aanzishe upya kisiri kwa-SECRET



    SEAL aendelee kurudisha ustaarabu kwa - Fly Like An Eagle


    Au tu SEAL asitishe dozi kwa- Kiss from a Rose

  • Safari ni NDEFU,...

    Posted: November 19, 2011, 1:47 pm by SIMON KITURURU
    ... lakini,......UKISAFIRI  kuelekea ufikiriako ni utakako KWENDA,........ waweza kuja kustukia utakalo  kwa unakotaka kwenda  lipo palepale  TAYARI ulipo.:-(

    Ni wazo tu hili MKUU!Jumamosi njema MKUU!


    Hebu turudi MALI ili Oumou Sangaré aingilie tena kati kwa - Seya



    Halafu huyuhuyu Oumou Sangaré azime kwa -Ahn diyah
  • Hamu ya KUGUSAGUSA kidogo kidude HUWEZA KUWA ndiyo ianzishayo yajulikanayo kuwa ni ya MAKUBWA ya KUSHIKASHIKA NDUDE!

    Posted: November 19, 2011, 1:33 pm by SIMON KITURURU
    NDIO,....... LAKINI na DOGO lichukuliwalo kuwa ni LA PILI,...... labda ndilo lilianzia kwenye lile dogodogo lile LA MOJA  kikutambulika tu,....... kwa kuwa kiukweli labda dogo tokea mwanzo ni KUBWA!:-(

    Swali:
    • Kwani unafikiri MAKUBWA hutokea ghafla tu  kwa kawaida?
    • Na katika DOGO si labda ni MTAZAMO wa MTU tu hasa kwa kuwa labda DOGO KWANGU ni KUBWA KWAKO?

    Ndio,..
    .... labda mpenda MAKUBWA agusagusaye DOGO ambalo laweza zaa MAKUBWA,...
    .......huyo  kiaina hata kama atadai sio tafakari  zake dogo HILO  halikuwa lamkumbusha MAKUBWA....
    ..........yawezekana hata kuvutiwa kwake na dogo hilo  hata bila yeye kujua  ni kwa sababu DOGO hilo hata kama sio kiudogo wa kugusagusa  kiaina kuna kimstuacho  kuwa hapo  kuna lake apendalo kubwa  hata kama sio lile la KUSHIKASHIKA!:-(
    Swali:
    • Unafikiri ukiangalia DOGO  hustukii kubwa kama dogo hilo UNAHISI   laelekea kuwa KUBWA?

    Ndio,...... na UWEPO wa  hamu ya kugusagusa KIKUBWA kwa mwenye DOGO,....... inawezekana ni kwa kuwa tu  kuna MAKUBWA  na pia kuna kishikikacho KIDOGO!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na si lazima ulielewe!:-(





    Hebu Africando waanzishe upya ili tubadili mawazo kwa - Aicha


    Africando waongezee dozi kwa - Sabador La Bamba



    Africando wadinye - Gombo



    Halafu hapahapa Senegali  Wasenegali hawa wa Africando wajaribu kuzima kwa - Yay Boy

    Halafu tu BALOJI na Konono N°1 ghafla waturudishe KONGO na ndio wazime tena kwa-KARIBU YA BINTOU
  • AFRIKA BAMBAATAA recklessly!

    Posted: November 19, 2011, 11:12 am by SIMON KITURURU
    Hebu UB 40 na Afrika Bambaataa warudie tu kutonesha- Reckless




    Na mie CHICHEMI sasa hivi ila  kama tamu muhimu,......labda  fanya iwe TAMUKUNOGA leo hata kama si ki-RECKLESS...!:-(

    Tuko Pamoja na siku njema mkuu!
  • Hebu USENGE utetewe kiduchu tena UGANDA!

    Posted: November 19, 2011, 5:55 am by SIMON KITURURU

    ... hebu tudake hii ndude,........Uganda gay rights.....
    ...wakati FRANK MUGISHA kutoka UGANDA akinyambulisha haki hizi ambazo yasemekana kuna wengi wazibaniazo mapaja....




    Swali:
    • Si nasikia kama tumizi la kinyeo ni la MTU mwingine kinyeo cha mwingine hata bila PENZI labda hilo swala sio dili lako utumbuaye kwa mbele?

    Ni nanilii  tu hii alwatani KIHESHIMATU kabisaa!
  • LEO baada ya Rais wa zamani wa PHILIPPINES yule GLORIA ARROYO kudakwa kwa wizi wa kura za mwaka 2007

    Posted: November 18, 2011, 9:13 pm by SIMON KITURURU


    Kama Mtanzania:
    • Unahisi ipo siku  mambo kama haya  ya kujaribu  kumuwajibisha kiongozi  baada ya  kuondoka madarakani yatakuja tokea BONGO?


    Ndio,....... Rais Gloria Arroyo leo kadakwa tena akiwa anaumwa hospitalini  kisa  maswala ya wizi wa kura ya mwaka 2007 akiwa Rais.

    Na kikubwa   kisa cha kudakwa kwake  wala hakuhusiani na kura zake mwenyewe kama Rais ,........ bali kwakuhusishwa na kuhusika kwake  katika kufanikisha mpambe wake anashinda kiti cha useneta kwa kufanikisha wizi wa kura za mpambe wake huyo.


    HABARI zaidi HAPA
    Swali tena kimarudio:
    • Unafikiri  ipo siku KATIBA YA BONGO itaruhusu  kuwajibishwa kwa watawala washirikio  kuhaini  nchi  baada ya wao kuondoka katika hatamu?

    Nawaza tu kwa SAUTI!

    Hebu tujaribu kubadili wazo kwa uchokozi kutoka kwa mtoto mzuri JOSEY PRISCILLE





    Haya basi NIMEACHA MKUU!
  • KOZI YA MAKOCHA WA NGUMI MKOA WA PWANI YAOTA MBAWA

    Posted: November 18, 2011, 8:54 pm by SIMON KITURURU



    Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa Kibaha Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuhuzuria kozi ya makocha iliyotarajia kuanza jumamosi ya kesho ata hivyo kozi hiyo iliota mbawa baada ya mkufuzi alieteuliwa na chama cha ngumi cha dunia (AIBA) kupata dharura kozi hiyo iliyoandaliwa na kamati ya Olimpic (TOC) iliota mbawa na kufanya makocha hao kutojua hatma yao baada ya kufika Pwani bila kupewa stahiki zao walizoahidiwa katika barua ikiwemo usafiri wa kwenda na kurudi pamoja na chakula ambavyo hawajapatiwa na kujitafutia usafiri kwa njia yao wenyewe kurudi mikoani kwao.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
    Makamu wa Rais wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini (BFT), Michael Changalawe (kulia) akizungumza na makocha wa ngumi nchini wakati walipowasili, Kibaha Mkoa wa Pwani Juzi kwa ajili ya kozi ya mchezo huo na kuambiwa kozi hiyo iliyoandaliwa na kamati ya Olimpic (TOC)  imehairishwa kutokana na mkufuzi wake aliyeteulia kupata dharura . Hata hivyo, makocha hao kutoka mikoa mbalimbali ya nchi walinyimwa stahiki zao hususani maladhi na posho za nauli za kuwarudisha mikoani walikotoka na kupatiwa kwa makocha wachache tu kinyume na barua walizopewa makocha ya kuwa watalipiwa gharama zote za kwenda na kuwarudisha mikoani kwao.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania

    Nimetumiwa taarifa na:SUPER D
  • Dawa CHUNGU saa nyingine NDIYO mgonjwa AHITAJIYO!:-(

    Posted: November 18, 2011, 12:02 pm by SIMON KITURURU
    NDIO,....... saa nyingine kwa mpenda UTAMU,...... huweza kuchanganya kila TAMU na UZURI wa kitu ,......kitu kifanyacho kwa kupenda kwake UTAMU kuathiriwa kutostukia kuwa TIBABU la RIDHISHO kwake ni ndude CHUNGU.



    Swali:
    • AU?

    ILA yasemekana kwa bahati mbaya TAMUTAMU KUNOGA inamchezo saa nyingine kwa BAADHI YA WATU kiladha zao  kunasia,...
    .... kwa MALAYA wa kulipia MTAANI zaidi ya kwa MAMA WA NYUMBANI,........kwa totoz  la kilokole ambalo ni MALAYA  CHUMBANI kama liliopolewa disko vile ZAIDI  ya BONGE la totoz la  kilokole  ambalo chumbani liko kama KANISANI ambalo linaheshima za kilokole zote  kwenye mpaka ya UNYUMBA HALALI usio DHAMBI chumbani,.......kitu ambacho labda ni swala la kuchunguza ni kwanini kwa mtu saa nyingine anasahau maji ni matamu SANA kiladha  na kuongelea juisi kama ndizo TAMU  kwa kuwa hazina maji mengi KILADHA.
    Swali:

    • Si unakumbuka kuna watu hawana LADHA mdomoni?
    • Na si unakumbuka PILIPILI sio kionjo kitamu kwa kila mtu MDOMONI?

    Ndio,.......KIDAWA,....... MCHUNGU  saa nyingi  HUYO ndiye DAWA,...... na kihitajiwacho kisichopendwa ladha  mara nyingi labda NI DAWA na NDICHO MUHIMU ZAIDI   hata kama  kwa kuwa kitibiwacho  hakiitwi UGONJWA  basi na TIBABU  hata lile  lisilo na mahaba  nalo haliitwi DAWA .



    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(



    Hebu kwenye GITAA LA BEZI  aingilie kati VICTOR WOOTEN nimuheshimuye kwenye chombo  ili aanzishe vita mpya kwa -U can't hold no groove if U aint got no pocket



    Turudi KAMERUNI ili mpiga bass nizimiaye kazi zake Richard Bona aanzishe upya kwa - Djombwe


    Halafu Richard Bona azime tu dozi tena kwa- Ekwa Mwato
  • Twanga Pepeta 50th Tanzania independence Tour

    Posted: November 18, 2011, 11:08 am by SIMON KITURURU
    Salam,
    African stars Entertainment Tanzania wanakuletea Bendi nzima ya Twanga Peteta ili iweze kufanya Makamuzi Live ndani ya Nchi ya Uingereza. Terehe 26.11.2011.

    [www.youtube.com]




    Asante sana!

    Nimetumiwa TANGAZO na:FRANK Eyembe wa Urban PULSE
  • Swala la ``KUFAIDI´´ ambalo huwezazalisha mpaka ``LABDA anafaidi zaidi alalaye na RAIS!´´

    Posted: November 18, 2011, 10:47 am by SIMON KITURURU
    Swala la KUFAIDI,...... laweza hitimishwa kwa kudhaniwa ``WENGINE wanafaidi zaidi ´´´......na nakama kwa wengine  wana`` URAIS ``  kama kipimo cha juu cha KUFAIDI hufanya  hata yahusianishwayo na URAIS kuwa  ni kigezo kizima cha nini  ni KIPIMO cha juu cha KUFAIDI,...
    ... na kufanya  mpaka twaweza kusahau   labda kuna mengine ni hausi boi wa  MWENYEKITI WA KIJIJI  ndiye ajinomayo KIKUFAIDI na na  sio RAIS.:-(
    Swali:
    • Unabisha?

    Na kwa kuwa labda inahitaji kwanza MTU awe na tafsiri yake BINAFSI  yakuwa KUFAIDI ni nini,...
    ... labda ikitafsiriwa vizuri WATU huweza kuhitimisha KIDUDE ni KIDUDE tu hata kama kimemnasia BINADAMU MWINGINE  asiyelengwa na FANTASI za mtu  zilizojengwa na tafsiri zake za nini ni KUFAIDI.:-(
    Swali:
    • AU?

    Ndio,......katika swala zima  la  KUFAIDI,...... labda faidi tu ulichonacho KINGUNGE  ,........ kwa kuwa labda ni FANTASI tu  ambazo   zafanya MENGINE na YAWENGINE  kwako kitafsiri ni KUFAIDI,....... na waweza kujikuta unapoteza muda kwa kutamani nyama ya kuku wa kizungu  USIYONAYO  kikufaidi ambayo ukiipata matokeo yake ni  kustukia unanogewa zaidi na nyama ya kuku wa kienyeji ambayo ulikuwa nayo tokea zamani  na hukuifaidi  kwa kuwa ulikuwa huipi chansi kinafasi  ili UIFAIDI kwa kuwaza usiyo nayo ile ya paja la kuku wa KIZUNGU.
    Swali:
    • AU?
    • Si wajua ukichunguza labda kila MTU kuna afaidicho kuliko wengine ?
    Ndio,...
    ... labda KUFAIDI,...
    .... ni tendo la kustukia ni kitu gani MAISHANI mwako weye hicho UNAKIFAIDI zaidi ya WENGINE!:-(
    Ni wazo tu hili KAMANDA na usikonde!Ijumaa na WIKIENDI NJEMA MHESHIMIWA!



    Hebu turudi KONGO ili Staff Benda Bilili waanzishe upya kwa - Je t'aime



    Hapahapa KONGO hebu KONONO No. 1 Waingilie shughuli kwa....




    Konono No 1 waendelee---

    Au tu KONONO No.1, Herbie Hancock ,India Arie na wengine wazime tu kwa-IMAGINE

  • Kuna ambao kwao KILADHA ni idadi ya SHILINGI hasa kwa kuwa LADHA hunogeshwa na GHARAMA!

    Posted: November 18, 2011, 10:08 am by SIMON KITURURU
    Kuna wanogewao na kitu ,...... kisa hicho kidude ni GHALI!Swali:
    • AU?

    Na pamoja na kuwa kuna wadaio kuna wengi DUNIANI ambao kwao GHALI SANA NDUDE ni ile igawiwayo BURE,...
    ...bado ni kweli pia kuna wanogewao na NDUDE na kuapia ni tamu kisa hicho ni kitu GHALI.
    Swali:
    • Si yasemekana kuna wavutiwao na GHARAMA kitu kifanyacho kwao kitu cha thamani wakikipata BURE huwa hawakithamini kisa TAMU ZAO zimebobea katika kuunganisha GHARAMA ya KITU KISHILINGI DUKANI na TAFSIRI kuwa kama ni BEI KUBWA basi hicho BABU KUBWA kitu kifanyacho wanaruka kustukia thamani ya kweli ya KITU?


    Ndio,...
    ....labda kuna TAMU,...
    ... na kwa watu wengine hiyo ni TAMU tu kwa kuwa ni GHALI!:-(

    NI wazo tu hili KINGUNGE!

    Hebu tupate zilipendwa ya KIBRAZIL kwa msaada wa Gilberto Gil aturushaye studio mwaka 1979 kudinya - Back in Bahia / Aquele abraço


    Sijui kwanini hebu Gilberto Gil arudie tena-Aquele abraço


    Gilberto Gil hapahapa BRAZIL apenyeze - Kaya n Gan Daya


    Halafu ajaribu kuzima tu kwa -Waiting in vain


    Halafu ghafla Bob Marley aingilie na kurudia-Waiting in vain



    Halafu huyuhuyu WACHAGA wadaio ni MCHAGA BOBU MALIYA  azime kwa-BAD CARD


  • Kwa kujitahidi SANA kuna wafikiao KUCHUNGULIA mpaka ambavyo WANGEANGALIA tu kwa kuwa DUKA la MZUNGU li WAZI!

    Posted: November 17, 2011, 10:54 pm by SIMON KITURURU
    Yasemekana,...
    ....UKIJITAHIDI SANA,...
    .... mara lukuki yawezafikia kuwa JUHUDI  SANA ziko katika KUJITAHIDI SANA  kuliko hata  katika ni nini kwa KUJITAHIDI UNAFANYA.:-(
    Na yasemekana,..... tuko wengi tu  ambao  kwa KUJITAHIDI SANA mpaka tunapofuka na kufikia  KUCHUNGULIA mpaka zile IHANA,...
    ...ambazo labda  tungeziangalia tu  na  KUSHUHUDIA mpaka ya firigisi na kitumbua makunyanzi  na kiponzacho ni JUHUDI!
    Swali:
    • Unafikiri  wakati unajuhudi na HIKI hilo sio kikwazo  kwako kifanyacho huoni KILE?

    Ndio ,...
    .... LABDA,...
    ..... au tu ni LABDA saa nyingine LABDA,...
    ...... kifanyacho MTU au tu hata WEWE  hustukii mengine,........ni JITIHADA ZAKO  na JUHUDI  zako  kwenye VITU  ambavyo labda sio hicho KITU kiwezacho kuwa ni muhimu KABISAAA kwako !:-(
    SWali:
    • Unabisha?


    Ndio,...... ukijitahidi,..........LABDA saa nyingine labda UNAJITAHIDI SANA mpaka  hata katika YAFANYIKAYO KIVIVU weye wayafanyia JUHUDI  mpaka yanaanza kuonekana ni MAGUMU  hata kwa wasio WAVIVU wa kufanya.:-(


    Ni wazo tu hili NGULI!:-(






    Hebu Inner Circle  wabadili kwa - Games People Play


    Inner Circle wachokoze  zaidi mpaka wale WAKRISTO wa siku mojamoja kalika WIKI hata kama hiyo ni JUMAPILI na sio JUMAMOSi katika mtuno- One Day Christian


    Halafu  tu INNER CIRCLE wazime kwa -BAD BOYZ
  • MATANGAZO mengine BWANA!

    Posted: November 17, 2011, 3:57 pm by SIMON KITURURU
    Haya MAMBO ya UHURU hayo!!....
    ...kama yafanyiwavyo kazi na kampuni ya UNITED COLORS of BENETTON ........katika kampeni yao waiitayo``UNHATE´´




    Tunakoelekea usishangae kukutana na matangazo ya kampuni za KIBONGO ya aina hii BONGO lakini!AU?

  • TWANGA PEPETA independence tour

    Posted: November 16, 2011, 7:56 pm by SIMON KITURURU


    Nimetumiwa na :Urban Pulse
  • Bado kiwezeshacho``KUPENDA´´ chaweza kugeuka TATIZO,...

    Posted: November 16, 2011, 3:42 pm by SIMON KITURURU
    ....  kwa kuwa CHOCHOTE kile chaweza KUPENDEKA ukikaa vizuri,...... na KUPENDA kwa MTU,........kwa wengine labda tayari ni TATIZO.:-(
    Swali :
    • AU?

    NDIO,...
    .... ``NAPENDA´´,...
    .... hata kama ni ile ``NAKUPENDA´´,...
    .... kuna watakaodai hubobea maudhaifu ya watu husika WAPENDAO ambayo si lazima kwa mtazamo wa asiyehusika kuonekana kama ni CHANYA au hata TATUZI hata kwa PENZI,....
    ... na labda ndio maana MAPENZI yamejaa WAPENDAO MTU wasio pendwa na huyo WAMPENDAYE.:-(


    Ni wazo tu hili MKUU!
    Hebu turudi NIGERIA kwenye ile zilipendwa Easy Motion Tourist kama ilivyodungwa na Fatai Rolling Dollar / Harbors Band




    Au tu Fatai Rolling Dollar aongezee - Allah Na Tu Ba

  • KWA WALE WAPENZI WA SWAHILIVILLA FACEBOOK PAGE

    Posted: November 16, 2011, 3:01 pm by SIMON KITURURU



    KWA WALE WAPENZI WA SWAHILIVILLA FACEBOOK PAGE 
    TUMEVUMBUA MTINDO WA KILA SIKU KATIKA [swahilivilla.blogspot.com] KUWEKA (WAPENZI WETU WA FACEBOOK PAGE KWA KILA SIKU ) 
    NITUMIE PICHA ZENU NDANI YA INBOX YANGU AU HATA KATIKA PROFILE YANGU. PICHA ZIAMBATANE NA MAELEZO PAMOJA NA SALAMU KWA WAPENZI UWAPENDAO. KUFANYA HIVYO KUTATOA CHANGAMOTO YA UKUWAJI WA JAMII YETU KATIKA MAZINGIRA UA UPENDO KWA JAMII YETU HII TUIPENDAYO SHKRAN! TUPENDANE
    ANGALIA MFANO HAI NEANI YA: http://swahilivilla.blogspot.com
    JIUNGEA NA FACEBOOK PAGE HAPA [www.facebook.com]
  • MASHINDANO YA NGUMI YA KAMANDA KOVA YANAENDELEA

    Posted: November 16, 2011, 2:55 pm by SIMON KITURURU





     Bondia Mussa Mohamedi (kulia) kushoto akioneshana ufundi wa kutupa makonde na John Christian wakati wa mashindano ya Kova Cup Dar es salaam jana Mussa alishinda kwa point.

    (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)




    Bondia Sunday Elius akipambana na Abdallah Kasimu wakati wa mashindano ya Kova Cup Dar es salaam jana Kasimu alishinda kwa point.
    (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)





    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.com www.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
  • Hebu tumsikilize TAJIRI kuliko wote DUNIANI kingawira PESA!

    Posted: November 15, 2011, 10:15 am by SIMON KITURURU

    OOOOKEI,........ ngojea Carlos Slim ambaye ndiye mwenye pesa kuliko wote DUNINANIN,......aongee,...
  • MALIKA NDLOVU na The BADILISHA Poetry X-Change

    Posted: November 15, 2011, 3:26 am by SIMON KITURURU


    Turning & Returning



    Showreel



    BADILISHAAn African Poetry Exchange



  • Nigeria's YouTube poet /Mshairi wa Kinaijeri CHIEDU IFEOZO ananilie USHAIRI katika YOUTUBE.

    Posted: November 14, 2011, 7:23 pm by SIMON KITURURU
    Chiedu Ifeozo,..... yuko ONLINE.








    WASHAIRI wa BONGO mpo?
    Ni changamoto KIAINA tu hii NGULI na wala usikonde!


    Au tu tupate Ushairi kutoka kwa Wayne Visser uitwao- I am an African

  • MABONDIA WAPIMA AFYA ZAO

    Posted: November 14, 2011, 6:04 pm by SIMON KITURURU




    Daktari wa Mchezo wa ngumi, Josefu Magesa akiwapima mabondia watakaoshiriki mashindano ya kova Cup yaliyoanza Dar es salaam leo katika ukumbi wa PR hotel zamani IMASCO CENTER mashindano hayo ya siku mbili yanamalizika jumanne ya 15/11/2011.

    (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com) --
    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.com Mob;+255787 406930         +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania






    Nimetumiwa taarifa na:Super D Boxing Coach
  • ....labda TATIZO ni RAIS NYERERE kufanikiwa zaidi kama MTU binafsi NYERERE katika mfumo uathirio zaidi ya mtu binafsi HATA asiye mchumba wa NYERERE!:-(

    Posted: November 14, 2011, 12:15 pm by SIMON KITURURU
    Yasemekana,....... kama mafanikio ya Mheshimiwa NDUGU ZITTO KABWE yatakuwa ni yale ya mtu BINAFSI kama yalivyokuwa ya GADDAFI,...
    .... yahitajio MFUMO MZIMA au tu yale yafanikishwayo  kwa  msaada wa ki(kwa KI-ung'eng'e )``INSTITUTIONS´´ ili wengi waendelee kufanikiwa hata aliyefanikisha ambaye ni Rais MWINYI kwa kuwa bado sio ZITTO KABWE  akiondoka ,...
    ....yahitajiyo MFUMO MZIMA au tu hata ``INSTITUTIONS BOMBA´´ ili yaendelee ,...
    ....aliyefanikiwa binafsi kama Rais DOKTA BABA WA TAIFA Mwalimu NYERERE aking'atuka hayo hufa kwa kuwa misingi ya yakuyaendeleza kimfumo au hata ki vyombo vya UMMA  kiidara  ambavyo vyaweza kuendelea na mchezo uleule,......hushindwa kucheza mchezo uleule VILEVILE  kisa mtu binafsi hata KIMKAPA hayuko tena katika HATAMU.
    Swali:
    • Kwani unafikiri baada ya NYERERE - ile ndude CCM bado ni ileile KIVILEVILE?
    • Na si yasemekana kama kuna MISINGI MIZURI ya mfumo katika idara za KIKWETE yeyote asiye kikwete  , KIKWETE  akiondoka anaweza kujikuta kirahisi tu ana KIKWETESESHA?
    • Si unakumbuka labda mtu mmoja ni chachu tu na huhitajika KIJIJI KIZIMA ili kutunza kijiji KIZIMA?

    Ndio,....... yasemekana SABABU MOJAWAPO  ifanyayo ya GEORGE BUSH yafanane na ya BARRACK HUSSEIN OBAMA ni mfumo na idara zichezazo vilevile MCHEZO ULEULE na ndio maana VITA za GEORGE BUSH huchezeka vilevile hata kama ashikiliaye kiuno ni OBAMA.:-(

    Ni wazo tu hili lililopinda KIDOOOOOGO MHESHIMIWA !:-(



    Hebu tu tena Baaba Maal na wenzake wabadili WAZO kwa kurudia tena- Three Little Birds



    Au tu tena Herbie Hancock na Céu waingilie tena kati na kuzima kwa - Tempo de Amor


  • UKWELI labda ni KWAMBA,...

    Posted: November 14, 2011, 11:15 am by SIMON KITURURU
    .... hakuna  atakaye kuweka HURU,....... na  kama unataka kuwa HURU kiuhuru ,........ hiyo ni shughuli yako MWENYEWE kujiweka HURU.:-(

    Swali:
    • Si starehe JIPE MWENYEWE?
    • Kwani  unafikiri kuna  kitu  kusaidiwa kuwa HURU?

    Ndio,...
    .... uhuru labda ni JAMBO la kujitakia MWENYEWE,...
    ... kama tu ilivyo kuwa labda UHURU  ni jambo tu pia la mpaka KUJITAFSIRIA mwenyewe.:-(
    Swali:
    • Kwani kwako kuwa HURU maana yake ni NINI?
    • Unafikiri TANZANIA ni NCHI huru?
    • Watanzania je?
    • Wewe je?


    Ndio,...... labda ni swala la MTU aliye huru,...... kuwa HURU  hata katika swala la KUFICHA hayuko huru  ujue alikuwa anafanyanini MSALANI!:-(

    Ni wazo tu hili MKUU!Jumatatu njema!
    Hebu Toni Braxton alainishe kwa-Spanish Guitar


    Au tu TONI BRAXTON alainishe zaidi kwa-Unbreak MY heart

  • YA DUNIA: Human echolocation lets blind man 'see' /Kuona kwa KIPOFU kwa KUSIKIA.

    Posted: November 14, 2011, 10:51 am by SIMON KITURURU
    Swali:
    • Kama unaona-JE wakumbuka wasioona wanadinyaje wasiyoyaona ?

    Cheki moja ya mbinu ya wasioona KUONA,...... katika -Human echolocation lets blind man 'see'


  • UMUHIMU wa KITU kwa MTU asiye WEWE uwezavyo kuwa ni CHIPSI MAYAI!

    Posted: November 14, 2011, 9:58 am by SIMON KITURURU
    Cha MUHIMU  kwa  MTU asiye WEWE,....... labda   ni kile ambacho  kwa apaye umuhimu NYAMA,...... hicho ni MCHICHA.:-(

    Swali:
    • Na si  unakumbuka KIPEWACHO UMUHIMU  na MTU , na kitu MUHIMU  kwa kustahili UMUHIMU vyaweza kuwa kwa kawaida ni vitu viwili TOFAUTI?
    • SI unakumbuka labda umuhimu wa KITU hata kwako ni PIPI kwa kuwa unahitaji sukari mwilini na wala sio MCHICHA  usifiwao kwa kutohusishwa na MHESHIMIWA anukaye mdomo kuoza MENO?

    Ndio,..... labda bado ni KWELI,....... la MUHIMU  kwako ni MUHIMU kwako tu,....... hasa kwa sababu tu  UMELIPA umuhimu!:-(
    Ni wazo tu hili MKUU!
    Hebu Rick James arudie-COLD BLOODED


    Au tu Ol' Dirty Bastard arudie tu - Cold Blooded



    Halafu tena Ol' Dirty Bastard azime kwa -Baby, I got your money

  • Leo baada ya kutoka KANISANI: Helloo dhambi -MAMBOZ vipi aisee!

    Posted: November 13, 2011, 8:56 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,....... labda DHAMBI MPYA  ya ufikiriaye hana DHAMBI kanisani kwa kaupole kake ,.....UCHUNGAJI WAKE ulivyo KIASKOFU... ...uimbaji KWAYA WAKE,........au tu hata kwa akuangaliavyo kwa MAHABA katika jina la BWANA kiuchumba,.......na wala hata sio kwa jazba yake ya kunena kwa lugha ,...
    .... labda ni kweli DHAMBI MPYA za walio KANISANI huanziaga hukohuko KANISANI lakini!:-(
    Swali:
    • Si MAHALI popote na WAKATI wowote ni wa CHAI hata katika ya CHAI?

    SAMAHANI NILITAKA KUSEMA:
    • SI labda mahali POPOTE na WAKATI WOWOTE MPEKECHO -dhambi KIMPENYEZO inaweza kupenyeza na kugusagusa eneo au tu kutekenya hata kidude hata kwa watiwao majaribuni na PAJA bila kuona PAJA?

    Ndio,...... labda ni kwa MAPENZI YA MUNGU TU,...... kuna atakaye piga kambi au kuchezea midoli MBINGUNI!:-(
    Ni wazo tu hili KAMANDA na samahani kama kimkwazo nimefanikisha!:-(






    Hebu R.E.M waachie- Losing My Religion



    Au tu R.E.M wapunguze kwa kitu kwa-Everybody HURTS

  • TISHA TISHA ina MIPAKA na LABDA ndio maana HATA utishie UKIMWI ,ngono hatuachi NG'OOO!:-(

    Posted: November 10, 2011, 3:15 pm by SIMON KITURURU
     Funzo kutoka kwenye TAHADHARI  za hatari  za UVUTAJI SIGARA ziwekwazo kwenye PAKETI  za SIGARA , sigara yenyewe au hata kwenye MATANGAZO ya SIGARA zaonyesha kuwa ,...
    ......WATAKAO KUVUTA SIGARA asilimia za kutosha TU,...... watavuta tu SIGARA hata kama wanajua na WAMETAHADHARIWA kuwa uvutaji wao SIGARA utawapatia SARATANI ya MAPAFU.:-(
    Swali:
    • Kwani unafikiri WAVUTA BANGI wangapi huacha kuvuta bangi kwa tahadhari wapewazo kuwa BANGI huleta KICHAA?
    • SI walevi wanajua POMBE si CHAI?
    • Na kwani unafikiri swala la NGONO PUMBAVU  kuwa chanzo cha uenezaji UKIMWI latisha wahusudu NGONO asilimia ngapi ambao wanafanya kazi katika N.G.O . za ``TISHATISHA UKIMWI UNAUA´´ ambao kazi yao  ni kinyume na NGONO pumbavu waendekezazo wakati wako katika ZIARA za kikazi ya KUELIMISHA watu watishike na UKIMWI?

    Ndio,....... na labda  TISHATISHA inamipaka yake KIMAFANIKIO,...... kwa kuwa kwanza WATU TWATISHIKA kwa vitu tofauti kitu kifanyacho  hata UCHOCHORO ukutishao  ule wenye GIZA kwa mwingine ndio mahali pazuri pakujibanza BILA WASIWASI kiofisi ya kazi maalumu kwake ya UPORAJI waogopao HUO uchochoro.:-(
    Swali:
    • AU?


    Ndio,...... TISHATISHA  ina MIPAKA katika KUTISHIA kitu mtu,...... kwa kuwa labda pia kwa baadhi kilengwacho kutumika kama TISHIO ilikusitishwa ,...... hichohicho ndicho kifanyacho MAISHA ya MLENGWA kuleta MAANA.:-(

    Swali zaidi:
    • Na si  wakati  mmoja anatishia mtu atakufa labda  kuna ambaye  ALENGWAYE NA KUTISHIWA KIFO ambaye kufa ndio kitu kiletacho maana KWAKE na ni poa kwa kuwa NAAMINI  ndio staili ya kwenda mbinguni kiaina?


    Ndio,....... ukikosea WAKULENGA  na ulengacho kama TISHIO ,.......... KITISHO CHAKO chaweza kuwa ni KICHEKESHO kwa kuwa UTISHACHO NACHO  kwake hukitambua kama Ze COMEDY.:-(

     NI wazo tu hili MHESHIMIWA!

    Hebu DJ JESUS aanzishe kwa-Homem Casado



    Tuga Agressiva na Titica waongezee dozi ya pambio kwa - MOTO



    Halafu Gata Agressiva wazime kwa - Fula Mupepi

  • Ya KINYAA CHA MTU kisa katika STORI na PICHANI bata kaharisha!

    Posted: November 10, 2011, 2:30 pm by SIMON KITURURU
     KINYESI kwenye  PICHA itiayo KINYAA mtu ,...... kama tu kwenye STORI za WATU zitiazo KINYAA mtu ,........huwa HAKINUKI ingawa kwa kuwa kuna wenye KINYAA,......... hata stori za USHUZI  TU  kuna wakunjao  USO  utafikiri wamenusa harufu MBAYA,.......eti WANAKINYAA.:-(

    Swali:
    • SI  umestukia harufu nyingi ni za KUFIKIRIKA kutokana na MAZOEA tu  yafanyayo  watu  hata KISAIKOLOJIA  WANUSE na  kufananisha na wajuavyo VYATIA KINYAA kitu kifanyacho wafanikiwe kusikia KINYAA?
    • Na  si umestukia YA PICHANI bado  KIAINA labda  yako  kwenye hiyo PICHA  TU kama  ya SIMULIZI yawezavyo kuwa kwenye SIMULIZI TU  na kihalihalisi kwako hayapo na hutakutananayo?


    Ndio,.......KIAINA,...... ya SIMULIZI kama tu  yalivyo kwenye  TV/LUNINGA,....... ayapayo MAISHA na kuyafanya yawe HALIHALISI / YA KWELI hata kwa KIKUHUZUNISHA kama sio KIKUTIA KINYAA,...
    .... labda ni WEWE mwenyewe kwa jinsi uyaoanishavyo na HALI HALISI itiayo KINYAA.:-(
    Swali:
    • Si ili  hata utishike na SINEMA ya KUTISHA labda yahitaji uoanishaji  wako  wa UONACHO na KUSIKIA na ujuacho KINATISHA kwenye UBONGO WAKO?


    Na ndio,...
    .....LABDA  kinyesi  kisipooanishwa na mavi na MKULIMA ,.......kwa MKULIMA hicho hugeuka MBOLEA NZURI tu  na wala isiyotia kinyaa na itafutwayo kwa juhudi KABISAAA  BILA KINYAA kwa ajili ya bustani ya NYANYA  za KACHUMBARI uipendayo!:-(

    Ni wazo tu hili MKUU!




    Meiway hebu aanzishe upya kwa - Les Genies Vous Parlent

    Halafu hebu tu Vusi Mahlasela arudie-When You Come Back/Ndakupenda Sana

  • Katika TAFAKURI za wafikiriao KUISHI MIAKA MINGI ni KUFAIDI MENGI kiaina!

    Posted: November 10, 2011, 2:13 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,...... kuna WAHURUMIWAO pia na KUHUZUNIKIWA kwa kuwa,...... hawakula CHUMVI nyingi  kabla ya  kuanza kivyao kwa  staili ile ya  KUDEDI.:-(
    Swali :
    • Si  kuishi MIAKA MINGI kwa WENGINE  maana yake ni``JAMAA LILIFAIDI LILE ?´´
    • Katika HAMU YA KUISHI miaka MINGI umewahi CHUNGUZA matatizo  ya WALA CHUMVI NYINGI?
    • Lakini  si KUISHI  miaka MINGI  maana yake  pia ni KUZEEKA sana kitu ambacho kuna WASIOPENDA?
    • Si kwa kula chumvi nyingi kuna warudiao NEPI tena?

    Na labda,...
    .... kuna WASAHAUO kuwa KUISHI  KUREFU labda  wala sio TIJA  na FARAJA kwa  AISHIYE MAISHA MAREFU  hasa kama AFYA na HALIHALISI ya KIMAISHA ndio HIVYO TENA  kitu kifanyacho labda KUISHI KUREFU kukawa maana yake ni KUTESEKA  kwa muda MREFU kiaina.:-(
    Swali KIAINA:
    • Unakumbuka kufaidi VIWEZEKANAVYO sasa hivi hasa UKIZINGATIA miaka izidivyo labda VIWEZEKANAVYO  SASA uviwezavyo kuvipindia mgongo yawezekana ikawa ni tatizo  kuwezananavyo baadaye kisa UMRI wafanya mgongo unauma?

    Ndio,....... kuishi kwingi  ni KUONA mengi,........ kitu ambacho  pia LABDA ni kuongezea muda wa KUJUTIA URUKAVYO kufanya sasa hivi UVIWEZAVYO SASA HIVI  ambavyo havitawezekana siku UKILA CHUMVI NYINGI.:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!





    Hebu Baaba Maal abadili wazo na aanzishe upya kwa - Miyaabele




    Baaba Maal azime - Three Little Birds


  • Jumuiya ya Afrika yang'ara ndani World Trade Market Uingereza

    Posted: November 10, 2011, 1:30 pm by SIMON KITURURU
    Salam,


    Leo ilikuwa ni siku ya jumuiya ya Afrika mashariki ambayo hufanyika kila mwaka katika maonyesha ya WTM hapa nchini Uingereza. Kwa kawaida sherehe hizi hufanyika katika banda la nchi ambayo ni mwenyekiti wa Afrika Mashariki, kwa hiyo mwaka huu tafrija hii ilifanywa kwenye banda la ndugu zetu wa Kiburundi. 
    Asanteni,
    URBAN PULSE CREATIVE
    Asamoah Gyan alipotembelea Banda la Tanzania


    Asamoah na wapenzi wake kutoka Tanzania

    Bw Meena. Bw Issa. Mh A. Jihad Naibu Balozi Chabaka, Jonathan

    Frank, Bw Issa na Bi Jestina

    Mwenyekiti wa bodi ya utalii ya Uganda akiwa na Bw William Byeruhanga

    Mh Jihad akiwa na wafanyakazi wa Bodi ya utalii  ya Zanzibar
    Waheshimiwa Ephraim Kamuntu, Najib Balala na Victorie Ndikumana

    Waziri Maige na  Naibu Balozi Chabaka wakipokea zawadi ya mpira

    Waziri wa Utalii na Mali asili Mh Ezakiel Mahige



    Nimetumiwa na:Frank Eyembe wa Urban PULSE Creative
  • Tangazo:TEENSPOT MAGAZINE !! ON SALE .. WE DO IT FOR THE YOUTH

    Posted: November 10, 2011, 1:27 pm by SIMON KITURURU
  • DR. REGINA KAPINGA AIPEPERUSHA VEMA BENDERA YA TANZANIA NDANI YA BILL AND MELINDA GATE FOUNDATION.

    Posted: November 9, 2011, 5:25 pm by SIMON KITURURU
    DR. Regina Kapinga
    Mama Regina (Program Officer of Bill & Melinda Gate Foundation) ni Mtanzania wa kwanza kuchaguliwa kuwa Staff wa Bill and Melinda Gate Foundation.
    Kutokana na Elimu na uzoefu aliokuwa nao katika kufanya kazi kwenye Taasisi za kimataifa, Taasisi ya kimataifa inayomilikiwa na Tajiri mkubwa Duniani Bill Gate ambaye ni mmiliki wa kampuni kubwa ya technolojia ya Microsoft ikaona imtumie katika kuweza kusimamia shughuli zote zinazohusu misaada mbali mbali katika mabara maskini Duniani, yaani Afrika na Asia.
    Watanzania tunakutakia afya njema ili uweze kuitangaza zaidi Nchi yetu, tunaamini kupitia wewe Taifa letu litafaidika na misaada mbali mbali kutoka kwenye Foundation hiyo.
    Nimetumiwa na:Henry KAPINGA wa KAPINGAZ Blog.
  • PSPF YAPEWA TUZO KWA KUTOA MIKOPO YA NYUMBA KWA WASTAAFU

    Posted: November 9, 2011, 5:04 pm by SIMON KITURURU




    Wafanyakazi wa PSPF wakifurahia tuzo waliyoipata baada ya kukabidhiwa na wazirei wa kazi na Ajira Bi. Gaudensia Kabaka wakati wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii iliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam jana tuzo hiyo ni kwa kutambua juhudi za mfuko huo katika kutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama wake wanaokaribia kustaafu.

    (Picha na Mpigapicha wetu)



    Waziri wa Kazi na Ajira Bi. Gaudensia Kabaka akimkabidhi kaimu Mkurugenzi wa PSPF .Bw.Adam Mayingu tuzo ya kutambua juhudi za PSPF katika kutoa mkopo wa nyumba kwa wanachama wake wanaokaribia kustaafu wakati wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii iliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam jana

    (Picha na Mpigapicha wetu)





    Waziri wa Kazi na Ajira Bi.. Gaudensia Kabaka akijaza fomu ya uhakiki  wa wastaafu wakati alipotembelea banda la PSPF katika maonesho ya Wiki ya hifadhi ya Jamii Mnazi Mmoja Dar es salaam jana Kabaka ni mmoja wapo wa wastaafu wa PSPF kushoto ni Ofisa wa Fedha Mwandamizi Bw. Victor Luvena

    (Picha na Mpigapicha wetu)







    --

    Rajabu Mhamila 'Super D'Photojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania

    Nimetumiwa na :SUPER D
  • KOCHA WA MCHEZO WA NGUMI SUPER D KUHUDHURIA KOZI YA KIMATAIFA YA NGAZI YA JUU YA MCHEZO HUO

    Posted: November 9, 2011, 4:27 pm by SIMON KITURURU

    Rajabu Mhamila 'Super D'




    Na Mwandishi wetu

    KOCHA wa timu ya ngumi ya Ashanti ya Ilala na Mkoa wa Kimchezo Ilala, Rajabu Mhamila 'Super D', ameteuliwa kuhudhuria mafunzo ya ngumi yaliyoandaliwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).

    Miongoni mwa makocha wa ngumi watakaoshiriki mafunzo hayo, ni mpiga picha wa Magazeti ya Business Time inayochapicha Magazeti ya Majira, Sports Starehe na jarida la Maisha, Mhamila ambaye maarufu kwa jina la Super D.

    Super D mbali na kuwa kocha wa ngumi na mpiga picha, pia ni bondia wa zamani wa ngumi za ridhaa na kulipwa.

    Akizungumza Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, alisema kozi hiyo itawahusisha makocha wa mchezo wa ngumi nchini kuanzia Novemba 12, mwaka huu hadi 20, ambapo itafanyika wilayani Kibaha, Pwani.

    Mashaga alisema Mkufunzi wa kozi hiyo atatoka nchini Algeria, ameteuliwa na Chama cha Ngumi Ridhaa cha Dunia (AIBA), ambapo makocha  30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara, wameteuliwa kushiriki.

    Mashaga alisema makocha hao wamechaguliwa kwa kuzingatia mchango wao katika ushiriki wa matukio mbalimbali ya BFT, hasa mashindano kwa kuleta timu au mikoa yao kushiriki mashindano mbalimbali yaliyoandaliwa na BFT.

    "Baadhi ya makocha hao, walipata  mafunzo ya awali yaliyoandaliwa na BFT, watakaofuzu mafunzo haya, watatambuliwa na kuingizwa katika kumbukumbu za AIBA," alisema Mashaga.

    Alisema makocha hao wataweza kufundisha mchezo huo popote duniani na kuruhusiwa kushiriki mashindano yote ya kimataifa kama makocha katika mashindano  yatakayoandaliwa kwa kufuata sheria za AIBA.

    Alisema kwa uzoefu wao BFT, wanategemea mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo, kutakuwa na ushindani wa uhakika kutoka kwa makocha hao.

    Mashaga alisema kwa msingi huo, wanatarajia kupata ushiriki wenye tija katika mashindano kufuzu kushiriki katika mashindano ya Olimpiki 2012, London Uingereza.

    Nae Super D aliongezea kwa kusema kozi hiyo imekuja wakati muafaka kwa kuwa dhamira yake ni kukuza na kuendeleza mchezo wa ngumi kimataifa Super D ambaye sasa ni muandaaji wa mafunzo ya ngumi kwa njia ya DVD ambazo huwa anaweka matukio mbalimbali ya mapambano ya ngumi za Dunia wakiwemo Floyd Mayweather, Manny Pacquiao,Mohamedi Ali, David Haye, Mike Tyson na wengine wengi . DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi Ilala na klabu ya Ashanti nayo ya ILala.


    Ciao...
    --
    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania


    Nimetumiwa habari na:Super D
  • R.I.P HEAVY D!

    Posted: November 9, 2011, 8:44 am by SIMON KITURURU
    Dwight Arrington Myers aka HEAVY D(May 24, 1967 – November 8, 2011)





    R.I.P Dwight Arrington Myers!Kazi zako bado nazisikiliza!


    Hebu tujikumbubshe moja ya kazi zake-Nuttin' But Love

  • Je tukubali moja ya sifa ya UTANZANIA ni kuwa WOGA na sio tu wa SERIKALI na VYOMBO vyake?

    Posted: November 8, 2011, 9:32 pm by SIMON KITURURU
    Moja ya kisababishacho  asilimia kubwa ya watu kuwa ma-ANONYMOUS kwenye hata michango ya maendeleo mitandaoni ni WOGA wa kuhusishwa na wawazacho.

    Watu huogopa VISASI hata bila kujua kama kuna ukweli kutakuwa na kisasi kama uwazacho kinatofautiana na WATAWALA wawazavyo kitu kilichozaliwa enzi za Rais Nyerere ambapo ilijengeka kuwa ukipingana naye hukuweka nje ya mtandao usisikike . Ingawa kuna waliofika kutumia maneno kama ``Uta KOLIMBWA wewe) ikimaanisha mpaka uhai wako huweza kuwa hatarini kama ikijulikana hukubaliani na UTAWALA.

    Watu  huogopa kuonekana WAJINGA kwa kusema kitu hadharani   labda kutokana na tokea watoto tunaimbiwa madhara yakuwa wajinga na labda na mpaka viboko kuchapwa kosa likiwa ni ujinga. Madhara yake hata wajuao vizuri yenye hekima na busara wako KIMYA kwa kutojiamini na WAJUAVYO ili wajije hakikishia umma kuwa WAJINGA.

    Na moja ya sababu karibu MAJUKWAA yote ni wachache  huchukua muda kuchangia hoja pamoja na kwamba labda mtandao ni ghali na muda hautoshi,... sbabu kubwa bado mimi naamini ni WOGA. Woga wa kujiharibia  kitu  ingawa nasikia kujiharibia kazi aka MLO ni kitu kiongozacho.

    Na yasemekana hata kwa kisingizio cha Utamaduni/Mila na desturi . Watanzania ni waoga hata kuonyesha wamempenda mtu hadharani ingawa UKIMWI na magonjwa ya zinaa bwelele yanaonyesha PENZI kivitendo linagidwa kimadhubuti

    Kuna ule uoga wa hata kumsema/kumtukana mtu hadharani ingawa  vifanywavyo kwa siri vina ushahidi HADHARANI hata  kwa kupitia mapenzi yetu ya UDAKU yafanyayo vyombo vya udaku kushamiri. Kupigana majungu ambayo ni moja ya dalili za WOGA, .....nk

    Tukiachana na hilo:
    • SI nasikia ni MPIRA wa miguu tu ambao WATANZANIA  wengi sio waoga kuambatanisha MAJINA yao na Wafikiriacho kuhusu YANGA na SIMBA?

    • Si nasikia kisiasa bado ni swala liogopwalo na wengi bado hata kujulikana vizuri wanawaza nini kwa kuhofia isijeharibu ulaji?

    • Na ni kiadoado tu  maswala ya JAMII mengine huamsha MIJADALA  na hasa  yakiongozwa na swala la kijamii la MALAVEDAVE ingawa staili ipendwayo katika mijadala hii pia ni ile ya mtu kutotaka kujulikana ni nani?


    Naendelea kuwaza!:-(


    Hebu Pepe Kalle arudie- Simplicite




    Au tu Tshala Muana azime kwa- Benga Nga Na Respect

  • Action! Developing the Commonwealth's cinematic culture -HORACE OVE na ZINA SARO WIWA

    Posted: November 8, 2011, 8:53 pm by SIMON KITURURU
    Kwa apendaye sinema zitengenezwazo na Watu weusi,...
    .... deku,...



    Katika nanihii:

    Ndio ,.... ZINA SARO WIWA ni binti ya Ken SARO WIWA yule jamaa mwanaharakati aliyeuawa na Jenerali Sani ABACHA kwa kuwa mwiba katika swala la uharibifu wa mazingira ufanywao na SHELL.

    Horace Ové pamoja na mengine,...
    .... yeye ndiye (kwa ung'eng'e) Guinness World Record HOLDER for the first Black British film-maker to direct a feature-length film, Pressure (1976)



    Kipengele katika kazi za Zina Saro WIWA,......kazi iitwayo..
    This Is My Africa.


    Ni mtonesho tu huu KAMANDA! Siku NJEMA!
  • R.I.P Joe Frazier

    Posted: November 8, 2011, 5:53 pm by SIMON KITURURU
    Joseph William "Joe" Frazier (January 12, 1944 – November 7, 2011)






    R.I.P Smokin' Joe!
    Bado mie nacheki kazi zako za  enzi za ...





    Habari zaidi cheki HUKU
    ...au ..

    Joseph William "Joe" Frazier
  • Sherehe za siku ya Kuzaliwa Mwanzilishi wa Dini Ya Sikh Guru Nanak

    Posted: November 8, 2011, 5:07 pm by SIMON KITURURU
    Salam,Maelfu ya wafuasi wa dini ya Sikh walijitokeza siku ya Jumapili tarehe 6 Novemba 2011 katika mjini wa Southall, Middlesex UK ili kusherekea siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa dini yao Guru Nanak aliezaliwa mwaka 1469 nchini Pakistani.Wakati akiwa na umri wa miaka 30 alipotea kwa hali ya miujiza kwa mda wa siku tatu. Alipo rejea alianza kuhubiri, kufundisha na kuandika dini ya Sikh wakati maisha yake yote. Pia Guru Nanak alisafiri dunia nzima kuitangaza na kujadili dini hii kwa waumini wengine kama waislamu pamoja na HindusKwa Miaka zaidi 550 wafuasi wa dini hii wamekua na desturi hii ya kusherekea siku moja kabla ya kuzaliwa kwake Guru Nanak kwa kuandaa maandamano haya makubwa ya Sherehe hii ambayo hufanyika India pamoja na baadhi ya sehemu za nchi ya Uingereza. Kwa kawaida sherehe hizi huongozwa na wafuasi wakuu watano wanaojulikana kama ''Panj Piare'' wakiambatana waimbaji, wanamuziki na timu ya wacheza upanga (Martial Arts) kuelekea hekaluni kwao ''Gurdwara'' Sri Guru Singh Sabha,  hapa Southall hekalu lao ndio kubwa kuliko yote katika bara la ulayaSherehe hizi huanza mapema asubuhi kwa kuimba, kuomba kwa pamoja. Baadae chakula cha kitamaduni kinachojulikana kama ''Langar'' hutolewa bure kwa kila mtu.Maandamano ya Southall yanaitwa Nagar Kirtan,Asanteni,URBAN PULSE CREATIVE

    chakula kilikuwa bure kwa kila mtu.halaiki ya kubwa ya waumini wa dini ya Sikh wakisherekea .Hata watoto nao walikuja kusaidia kutayarisha chakula.Southall Palikuwa hapatoshi.wadau wakiwa kazini kutayarisha chakula.wakati wa kupata mapocho pocho.Frank akiwa katikati ya mitaa ya Southall kushuhudia sherehe hii .Maandamano yakiendelea.Waumini wa dini ya Sikh wakiazimisha siku hii .Frank akipata chai ya tangawizi na iliki kutoka India.Muasisi wa Dini ya Sikh Guru Nanak.

    Nimetumiwa na :Frank Eyembe
  • Tuff rec yafanya wimbo wa miaka 50 na wasanii wa Morogoro

    Posted: November 7, 2011, 8:27 pm by SIMON KITURURU


    Studio ya Tuff Records iliyopo mjini Morogoro,Katika kushehelekea Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.katika sherehe hizo Tuff Records yawakusanya wasanii wa kizazi kipya ambao ni wapya katika tasnia ya muziki,ikiwa kama kuonesha umoja wao katika taifa.Wimbo huu ni kwajili ya watu wote wenye upendo na inchi hii. Ni kwa ushilikiano na blog ya CHUMA (BFL) http://bongoflavalink.blogspot.com
    WASANII WALIO SHILIKI KATIKA NYIMBO NI:

    NellyTuff Rec Ft Nelly Crizy, Man Fair, Nasreal, Malale,GS, Big Poppa, Raz Q, Roberly &Young Steve

    Mtayalishaji wa muziki
    GQ- 0657659969

    WIMBO:
    TUNAWEZA(MIAKA 50)

    STUDIO:
    TUFF RECORDS
    kwa mawasiliano: +225 712 222244

    Tuff Rec Ft Nelly Crizy, Man Fair, Nasreal, Malale, GS, BIG Poppa, Raz Q, Roberly & Young Steve - Miaka 50 Ya Uhuru (Prod By GQ).mp3
    9320K   Play   Download  


    Nimetumiwa na:Salim Chuma
  • Unamkumbuka CARLOS the JACKAL?

    Posted: November 7, 2011, 6:14 pm by SIMON KITURURU
    Carlos the Jackal


    Kuna kipindi ilikuwa ukiongelea maswala ya ugaidi au hata ya ``Terrorism´´ jina lake lilikuwa maarufu kuliko Bin Laden maeneo fulanifulani .

    Naona anakesi mpya tena huko UFARANSA huyu jamaa iliyoanza leo.

    Jikumbushe kama umemsahau  huyu Ilich Ramírez Sánchez aka Carlos the Jackal.




    Katika kujikumbusha zaidi kiaina kisimulizi za Wamagharibi kuhusu Carlos,...





  • CHAMA CHA NGUMI DUNIA (AIBA) KUWAPIGA MSASA MAKOCHA WA TANZANIA

    Posted: November 7, 2011, 6:00 pm by SIMON KITURURU
                        BOXING FEDERATION OF TANZANIA (BFT)
                                                                                      SLP 15558                                                                                   DAR ES SALAAM                                                                                       6/11/2011                                                               Email; bft.tanzania2009@gmail.comTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI;         YAH;KUFANYIKA KWA MAFUNZO YA KIMATAIFA KWA                  WALIMU WA MCHEZO WA NGUMI ZA RIDHAA                  TANZANIA 12-20 Nov 2011 KIBAHA PWANI.Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) wameandaa mafunzo kwa walimu wa mchezo wa ngumi Tanzania.Kozi hiyo itafanyika kuanzia tarehe 12-20 Nov 2011 Kibaha, Pwani katika shule ya Filbert Bayi.Mkufunzi katika kozi hiyo ni kutoka Algeria,aliyeteuliwa na Chama cha ngumi cha Dunia (AIBA)Jumla ya washiriki ni 30 wamechaguliwa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara kuja kuhudhuria mafunzo hayo, kwa kuzingatia mchango wao katika ushiriki wa matukio mbali mbali ya BFT hasa mashindano kwa kuleta timu au mikoa yao kama makocha na kujihusisha kikamilifu katika shughuri mbalimbali zinazohusu kuendeleza mchezo wa ngumi TanzaniaZaidi makocha hao tayari walishapata mafunzo ya awali yaliyoandaliwa na BFT.Baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo washiriki watakaofuzu watatambuliwa na kuingizwa katika data base za Chama cha ngumi cha Dunia [AIBA]Pia wataweza kufundisha mchezo wa ngumi popote Duniani na kuruhusiwa kushiriki mashindano yote ya kimataifa kama makocha kwa mashindano yote yatakayo andaliwa kwa kufata sheria za AIBA.Kwa uzoefu sisi kama BFT tunategemea mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo,tunategemea kupata ushindani wa uhakika kutoka katika mikoa iliyopata nafasi ya ushiriki,na tunategemea kupata timu ya Taifa ya ngumi yenye sura ya kitaifa tofauti na awali ambapo wachezaji wengi walitokea DAR ES SALAAM na hasa katika vyombo vya ULINZI NA USALAMA.Kwa msingi huo sasa tutategemea kupata ushiriki wenye tija katika mashindano mbalimbali ya kimataifa hasa kufuzu katika ushiriki wa timu yetu ya Tanzania katika mashindano ya Olimpiki 2012 London Uingereza.Na mashindano mengine ya kimatafa.Makore Mashaga.KATIBU MKUU BFT. Mob; 0713588818. Email;mashagam@yahoo.com                                                                              






    --
    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
  • THREE DAYS REMAINING CAST YOUR VOTE NOW FOR SWAHILI FASHION WEEK 2001 AWARDS / ZIMESALIA SIKU TATU PIGA KURA YAKO SASA KATIKA TUZO ZA SWAHILI FASHION WEEK AWARDS 2011

    Posted: November 7, 2011, 5:35 pm by SIMON KITURURU


    THREE  DAYS REMAINING CAST YOUR VOTE NOW FOR SWAHILI FASHION WEEK 2001 AWARDS / ZIMESALIA SIKU TATU  PIGA KURA YAKO SASA KATIKA TUZO ZA SWAHILI FASHION WEEK AWARDS 2011
    FEW DAYS HAVE REMAINED FOR THE VOTING LINES OF SWAHILI FASHION WEEK AWARDS 2011 TO BE CLOSED, VOTE FOR YOUR FAVORITE TIME RUNS OUT SO QUICKLY. DON'T EVER TRY MISS THIS FASHION EVENT AS IT IS BEING THE BIGGEST FASHION EVENT OVER EAST AND CENTRAL AFRICA
    ZIKIWA ZIMESALIA SIKU CHACHE HADI KUFUNGWA KWA NJIA ZA KUPIGA KURA KWA AJILI YA TUZO ZA SWAHILI FASHION WEEK 2011 WEWE KAMA MUWEZASHAJI WA TUZO HIZI MPIGIE KURA YULE UMPENDAYE NA UNAYEONA ANAFAA KUSHINDA. USIJARIBU KUTOKUWA MMOJA WA WASIOPIGA KURA JIVUNIE MAVAZI YA KIAFRIKA KWANI HILI NI ONESHO KUBWA LA MAVAZI AFRIKA MASHARIKI NA KATI
    PIGA KURA YAKO SASA HAPA:  www.swahilifashionweekawards.blogspot.com

    Nimetumiwa habari hii na:Esi Mgimba
  • PSPF YAKABIZI MSAADA KWA KIKUNDI CHA WALEMAVU CHANG'OMBE

    Posted: November 7, 2011, 5:30 pm by SIMON KITURURU


    Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma PSPF, Bi.Fatma Elhady  (kushoto) akimkabidhi msaada wa hundi ya shilingi milioni 1.5 Bi.Dominion Apiyo wa Kikundi cha Walemavu cha Little cha Chang'ombe wilayani Temeke,Dar es Salaam jana(.Picha na mpigapicha wetu)

    --

    Rajabu Mhamila 'Super D'Photojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania


    Nimetumiwa habari na : Rajabu Mhamila.
  • Boko Haram

    Posted: November 7, 2011, 10:10 am by SIMON KITURURU
    Najaribu sana kuwaelewa hawa jamaa wa NIGERIA wa Jama'atu Ahlis Sunna Lidda'awati wal-Jihad
    ...ingawa mpaka sasa  ni kwa bila mafaninkio.

    Cheki moja ya kazi zao...



    Naendelea kuwaza!
  • SIKU ALIYOFARIKI BIBI TITI MOHAMED, MMOJA WA WANAWAKE WALIOKUWA WANAHARAKATI WA UKOMBOZI WA TAIFA LETU

    Posted: November 7, 2011, 9:27 am by SIMON KITURURU
    Bibi Titi Mohamed enzi za uhai wake.


    Hapa akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Bibi Titi Mohammed (1926 - 5 Novemba, 2000) alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania. Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika.Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere.
    Juu ya kutolewa kwake, Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wa kisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlani.Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi ameonekana kwenye makaratasi ya chama tawala kama "Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".Mnamo tar. 5 Novemba, 2000 Mohammed amekufa kwenye hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.Moja kati ya mabarabara makubwa ya mjini Dar es Salaam yamepewa jina la Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.

    Nimetumiwa na:Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog.
  • ALFEO SILUNGWE AKIITANGAZA TANZANIA KATIKA MOJA YA PRESENTATION ZAKE INDIA.

    Posted: November 7, 2011, 9:17 am by SIMON KITURURU

    Alfeo Silungwe Mtanzania anaye piga Nondo ya Masters of Statistic ndani ya Nchi ya India akiwa anafanya presentation katika moja ya kozi anayo isomea chuoni hapo.

    Nimetumiwa na:Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog
  • Mahojiano Maalum Kutoka Kwa Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda

    Posted: November 7, 2011, 9:06 am by SIMON KITURURU
    [www.youtube.com]

    Salam,

    Wakati  tunapokuwa tunajiandaa kuelekea katika sherehe za miaka 50 ya uhuru Urban Pulse Creative watakua wanakuletea mtiririko wa Mahojiano maalum kutoka kwa Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili kutuelimisha na kutupatia changamoto mbalimbali zinazozikabili taifa letu. Hii ni sehemu ya kwanza ya Mahojiano hayo.
    Asanteni Sana,
    URBAN PULSE CREATIVE

    Nimetumiwa na:Frank Eyembe
  • Jinsi jina la SEHEMU ZA SIRI za BINTI FULANI lilivyogeuka kuwa TUSI!

    Posted: November 7, 2011, 3:02 am by SIMON KITURURU
    Tupo wengi  tupendao sehemu za siri za mabinti fulani,...... lakini  SEHEMU ZA SIRI  za wanawake tuwapendao bado KIJINA ni TUSI.
    Swali:
    • Na si nasikia mapaka kwa baadhi ya WANAWAKE hutumia jina la sehemu  maridhawa ya sili ile ya chini ya kitovu  yenye kusaidia mapaka kukojolesha binti kama TUSI?:-(

    Na  sehemu za siri  za kike  zile nizipendazo kama wengine tu  wapendao  kunanilii  kama mimi mara kwa mara  halihalisi ikiruhusu,...
    .... hizo zinamajina mengi ingawa kwa bahati mbaya ili utukane KWA MAFANIKIO ,.......sio kila jina la KIPENGELE HIKI  ni TUSI.:-(

    Swali :
    • Si unakumbuka ili kitu kizuri kama UKE  ilikigeuke TUSI labda yahitaji  atukanwaye kutafsiri mpaka  jina la ANDAZI  kuwa sio ANDAZI kihivyo?

    NDIO,....... labda tusi ni TAFSIRI,....... ndio maana maka  kitafsiri za watu kipengele TAMUKUNOGA  ni tusi pia.:-(
    Ni wazo tu hili KAMANDA!Jumatatu njema MKUU!






    Hebu Mighty Sparrow aanzishe kwa - Wood in De Fire



    Mighty Sparrow aongelee yaonglewa kuwa - Sparrow Dead

    Mighty Sparrow adai - No, Doctor, No



    Mighty Shadow a- Roll de Bumbalum



    Shadow aachie-Obeah




    Mighty Shadow amwage -Tabanka

    Baron aingilie kati kwa-Come By Me



    Baron adai-Sweetness is My Weakness


    Au tu turudi tu TANZANIA ili Dr Remmy azime kwa-Nalilia MTOTO

  • Katika kufupisha`` SHENZI´´

    Posted: November 6, 2011, 8:17 pm by SIMON KITURURU
    ``KIREFU´´ kuna wasiosikiliza,...... na pia hata WASIOSOMA ya MUHIMU kwa kuwa tu eti yako ``KIREFU´´.:-(
    Swali:
    • Si kama REFU lahitaji UREFU basi labda acha tu liwe REFU?

    Na  kwa kuwa kuna WAFUPISHAO ``kifupi´´,...... isije tu kuwa  ``KIFUPI´´ maana yake nayo  KIMAANA imefupishwa na kuwa fupi!
    Swali:
    • SI kifupi  bado huhitaji kuwa bado ni kitu kizima?


    Ndio kuna vipufishwavyo  ,....... na labda ni vifupi kwakuwa sio vitu vizima kiujazo!:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(


    Hebu tu BILAL aanzishe tena kwa-SOUL SISTA



    Bilal aongezee - Fast Lane


    Halafu tu BILAL azime kwa - Sorrow Tears and Blood
  • KWA KUWA si kila avutaye SIGARA hufa na SARATANI ya MAPAFU,.....

    Posted: November 6, 2011, 5:56 pm by SIMON KITURURU
    ..... Lakiiiiniiiii!
    Na sio kila MALAYA hupata magonjwa yaambukizwayo kwa UASHERATI,........... Lakiiiiniiiiii!

    Na sio kila KICHAA alaye majalalani huugua kipindupindu,....
    ..... LAKINIIIII!




    Swali:
    • SI nanihii isababishayo NANIHII si kila ANANILIYE hufanikiwa kuwa na NANIHII na ndioa maaana sio kila mfanyakazi bora ana MSHAHARA MZURI na sio kiala ananiliwaye hupata MIMBA?


    NI nanilii tu hiii BINGWA na wala usikonde.
    Hebu AL GREEN abadili NANILII kwa ndude- Love and Happiness


    Al Green kwa kuwa ni JUMAPILI kikristo adinye pia - Too close to heaven



    Hebu Extra Large waingilie kati na kuturudisha ZIMBABWE kwa - Muti Wemusango


    Xtra Large waongezee ya - House Girl

    Wadodose ile ndude -MUROORA


    Au tu hapahapa ZIMBABWE Xtra Large wazime kwa -Kushamura Newe




  • Sayansi ya KUCHAPA m-TOTOZ!

    Posted: November 6, 2011, 5:26 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,....... naamini VIBOKO Wabongo wengi wamekula katika makuzi yao..
    ...hebu tudeku .....Science behind physically disciplining children.

    Fundamentalism & Corporal Punishment





    Breaking the Will of the Child




    Social Science & Corporal Punishment- Introduction




    Cultural Attitudes Toward Children



    Scientific Evidence



    Denial-"I was spanked & I'm Okay."


    Spanking: Spare the Rod or Spare the Child



    Discipline Without Hitting



    Training Parents


    Spanking kids in Zambia





    Swali:
    • Ushawahi kulichapa totot lako?
    • Kwani ni MIKUBWA mingapi ushawahi kufikiri inafaa kutandikwa?
    • Ushawahikulichapa kubwa zima na kama hujawahi ni kwanini?
    • Unafikiri ZE MZUNGUZ na Ze WABONGOZ ki kifimbocheza hufundikishwa tofauti kitu kifanyacho ze MBONGOZ kuchapwa na Ze MZUNGU kuchapwa ni vitu tofauti?

    Ndio,...... kuna mikubwa MIZIMA  ichapanayo PIA,....... na eti kisa katika matumizi hayo ya mikanda au fimbo  ni KITENDO ndani TU tendo la penzi.:-)








    NI mtonesho tu huu MKUU!
  • Katika HAMU ya VIJISENTI!

    Posted: November 4, 2011, 5:02 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,...... yasemekana hakuna BINADAMU aliyezaliwa FISADI,...... na yoyote yule anaweza kuwa FISADI  kitu kiwekwacho uzito na ukweli kuwa karibu MAFISADI wote uwajuao wenye VIJISENTI vya WIZI au hata tu ambao wanalia ofisini  huku bado hawajastukia kuwa waliavyo ofisini ni WIZI;...

    ... bado ukweli uko palepale kuwa WAINGIAO OFISINI ambazo zina FWEDHA,......huwa yasemekana hujistukia HUMOHUMO  ofisini  kuwa wanapenda VIJISENTI na kama KIUHASIBU wamestukia hawatastukiwa WAKIDOKOA  ,...

    ....hujichukulia vyao MAPEMA huku wengine wakiahidi WATAENDA KUTUBU  makanisani  au tu kwa MIUNGU YAO baadaye!:-(
    Swali:
    • Unauhakika hutaki VIJISENTI?
    • Unauhakika VIJISENTI vikigalagala mbele zako  hutadokoa kama hatutajua?
    • Lakini si unakumbuka pia  hata yaliyowazi kama TITI  na MWANA  kuwa sio kila mtoto azaliwaye hupenda TITI la MAMA na ili ale kikunyonyeshwa ni bonge la shughuli kwa MAMA mnyonyeshaji?



    Ndio,..... labda kumbuka tu tena kuwa,......karibu  asilimia  mia ya mafisadi hawakuzaliwa MAFISADI,...... na hustukia tu kuwa wamegeuka MAFISADI baada ya kuanza kuitwa MAFISADI,........LAAAKIIIINIIII!!:-(


    NDIO ni  wazo tu hili NGULI!Ijumaa na WIKIENDI NJEMA Mheshimiwa!
    Hebu COSTULETA aanzishe upya  kwa - Do Milindro






    COSTULETA apenyeze kachumbari zaidi tena na - LADJUM



    Costuleta apandishe mita za dozi  zaidi kiujazo kwa - Tchiriri





    Au tu tusiende mbali Dj Anjo Negro aingilie kati na kuzima kwa miondoko hiihii ya KUDURO kwa ndude pana kikishimo ile -Chuco Chuco

  • Katika CHANGAMOTO zaidi : Hawa washindi wa NOBEL akina BERTRAND RUSSELL na EINSTEIN kuhusu Sir GOD/MUNGU

    Posted: November 4, 2011, 4:30 pm by SIMON KITURURU
    Bertrand aanzishe


    Einstein amalizie...




  • Leo katika CHANGAMOTO:Stephen Fry

    Posted: November 4, 2011, 3:44 pm by SIMON KITURURU
    Getting out of the I-Mode





    Philosophy, Logic And Reason /Importance of unbelief






    Au cheki pia kuhusu SELF- PITY
  • Leo katika UCHOKOZI: Hebu KARY BANKS MULLIS ( Nobel Prize winning American biochemist)adai hakuna ushahidi H.I.V inasababisha A.I.D.S.

    Posted: November 4, 2011, 2:59 pm by SIMON KITURURU
    Kuhusu jamaa huyu NGULi kisayansi,...
    .. mgugo tuu au kiaina bofya hata HAPA


    Hebu tumsikilize yeye na wengine...

  • Na kwa kuwa LEO yaaminika ni JUMATATU kwa wengi!

    Posted: October 24, 2011, 4:39 am by SIMON KITURURU
    Kumbuka tu kuwa,....... KALENDA ifanyayo jana ni JUMAPILI na juzi ilikuwa ni JUMAMOSI,......... ni kitu kilichotungwa tu na WATU kama WEWE,......... kitu kifanyacho labda bado kama tu enzi za mababu zilizokuwa hazifuati KALENDA hizi,......JUMATATU HII kwako ni JUMATANO ya mwaka jana kwa mwingine.

    Swali la kizushi:
    • Unakumbuka KIISLAMU leo ni MWAKA gani?

    Ni angalizo tu hili MHESHIMIWA na usikonde!:-(

    Hebu BILAL aanzishe upya kwa-FREE


    Nottz aingilie kati kwa - Shine So Brite


    Shafiq arudi na Bilal katika pini- Cheeba

    Nottz na Bilal warudi tena kwa- Right Here


    Au tu tena Amerie azime kwa - 1 Thing

  • WAMAREKANI bwana kwa kukasifia kanchi kao bwana- ETI kanchi kao ni ``THE GREATEST PLACE on EARTH!´´

    Posted: October 23, 2011, 6:35 pm by SIMON KITURURU
    Haki ya nani ukisikiliza WANASIASA wa MAREKANI wakisifia MAREKANI,...... unaweza kudhani MAREKANI ni nusu MBINGUNI kwa jinsi wanavyopasifia na pia kusifia WAMAREKANI kama wao ni watu bomba sana na SPESHO hapa DUNIANI ,...
    ....mpaka unaweza kuelewa fununu ZA KITU  hata bila ya  kuhoji WAENDEKEZAO UMAREKANI hata bila kufika MAREKANI kwanini labda kuna  uwezekano WAPO waaminio  WAMAREKANI wakienda haja zitengenezwazo na malighafi CHAKULA,...... labda watoacho kihaja kubwa ni  karibu na keki au angalau kwa wapenda ubwabwa wanaweza hisi tokeo lao la ya msalani AREKANI AKIENDA KUJISITIRI ni PILAU.
    Lakini: 
    • Umestukia ukiongea na MSWISI ,.....au MFINI hata tukiruka nchi nyingine unaweza kukuta na wao wanaamini nchini kwao ndio BOMBA zaidi na wanafundishana hivyo hata katika porojo za hapa na pale na kama kunakasoro wanaamini ni kwa sababu WAGENI nchini kwao ndio wanawaharibia NCHI?
    • Na si unastukia sie kwetu hata kitu kirahisi kujivunia kama Mlima KILIMANJARO tunashindwa kuutetea kuwa uko Tanzania na  nasikia kuna Watanzania kibao kama hailazimiki wanakwepa kujitambulisha kuwa ni Watanzania huko ughaibuni kisa hata waowenyewe wanashindwa kujivunia TANZANIA?



    Ndio ,..... na labda ni JANJA moja wapo,........ kujisifia wenyewe hata ki-PROPAGANDA kama wafanyavyo WAMAREKANI,...
    ...lakini:
    • Ukijivunia TANZANIA ya leo si kunawatakaoamini tu kirahisi UNADANGANYA?
    Ndio,....... wenzetu hata KIPOROJO za uongo kikuombea KURA ,........wanajivunia sana KWAO na kudai kuwa kwao ni ``THE GREATEST´´!

    Ni wazo tu hili kiangalizo MHESHIMIWA!:-(



    Hebu Kassav waingilie kati na kubadili mchezo kwa ndude kimchanganyiko yenye -OH, MADIANA


    Kassav bado kipaza sauti kikishikiliwa na Jacob Desvarieux wapandishe dozi kwa - Mwen Malad Aw

    Hebu ndani ya KASSAV huyu Jean-Claude Naimro ashike kipaza sauti tena katika- Ave'w Doudou


    Ndani ya KASSAV mdada Jocelyne Béroard zamu yake ashike kipaza sauti na kurudisha-SIWO



    Au tu kundi zima la KASSAV wazime tu manyanga   kwa-Tim Tim Bwa Sek
  • UNAKUMBUKA Mapinduzi ya TUNISIA yalianzishwa na MMACHINGA aliyejichokea na sio WANASIASA au WASOMI wale FULU kujifanya WANAJUA KILA KITU?

    Posted: October 23, 2011, 3:32 pm by SIMON KITURURU

    WATUNISIA wakibeba picha ya mchoro ya Mohamed Bouazizi(29 Machi 1984 – 4 Januari 2011)




    Desemba 17 Mmachinga Mohamed Bouazizi aliyekuwa na miaka 26, alijichoma moto kupinga ukandamizaji katika mji wa Sidi Bouzid na kufia kwenye hospital huko Ben Arous, Tunisia baadaye.

    Machinga huyo aliamua kujichoma moto mbele ya ofisi za serikali baada ya kunyang'anywa MATUNDA na MBOGAMBOGA alizokuwa anauza na kunyanyaswa na maafisa wa mji na mgambo wao kwa madai kuwa hana kibali cha kufanya umachinga kitu kilichomfanya aone hakuna haja ya kuishi katika mazingira ambayo kujitafutia riziki kihalali kwa kufanya biashara ndogondogo bado mtu ananyanyasika na kuporwa hata kamtaji.

    Kujichoma kwake ndiko kulifanya Wananchi karibu Tunisia nzima kuamua wamechoka na matokeo yake ni mpaka serikali ya Rais Zine El Abidine Ben Ali ikaanguka -kitu ambacho kikaeneza wananchi kudai mapinduzi karibu Uarabuni kote.

    MADHUMUNI ya TARALILA hii ni KUKUMBUSHIA TU kuwa:
    • Saa nyingine cheche za mageuzi huanzia usikokutegemea na usishangae kuwa labda si WANASIASA watakao geuza nchi hata ya TANZANIA.
    • Na labda uwadharauo wanaweza kuwa ndio kiini katika ukombozi wako.

    Ni angalizo tu hili MHESHIMIWA!JUMAPILI NJEMA KAMANDA!


    Vyanzo vya stori ya Mohamed Bouazizi unaweza kugugo tu au nenda kwa Aljazeera;
    ...donoa HAPA,...
    ....au hata bofya
      HUKU

    Hebu MICHAEL JACKSON atutie majaribuni kwa kumsifia KIDOSHO wa KILIBERIA katika-Liberian GIRL


    Au tu Michael Jackson azidi kubembeleza kidosho kwa - Give In To Me

  • JERRY NASHON na MOHAMED GOTAGOTA jukwaani

    Posted: October 22, 2011, 11:07 pm by SIMON KITURURU
    ``Mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni mwa 90, ungefika kuanzia saa nane mchana, siku ya Jumapili, katika Ukumbi wa Vijana Hostel (ukumbi unaopakana na Mango Garden), ungekuta vijana wameanza kukusanyika wakisubiri saa tisa mchana ambapo Vijana Jazz walikuwa wakianza muziki. Siku hiyo ilifahamika kama.....´´

    ...DUH endelea ,.......HUKU



    Kundi zima la VÍJANA JAZZ  Jumapili moja wakiwemo Mohamed  Gota Gota......... bila kumsahau .Jerry Nashon Dudumizi ,..... kwa  ya zaidi tena BOFYAAAA--
    www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.comwww.johnkitime.blogspot.com
    Nimetumiwa na NGULI:John Kitime
  • Umestukia kuwa ukweli ni kwamba kibinadamu ,BINADAMU labda hawezi kusaidia kila MTU?

    Posted: October 22, 2011, 9:00 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,......unaweza kujitahidi uwezavyo  LAKINI,...
    .... na ukigundua KUSAIDIA  haki ya nani tena  kuwa  ni KUJISAIDI mwenyewe...
    ... waweza kukuta UCHOYO mtu afanyao  wa hata kumnyima MTU mwingine kubenjuka au kubenjua kidude  ,...... LABDA ni jinsi tu mojawapo ya MTU kujinyima kutobenjuka mwenyewe!:-(
    Swali:
    • Si unakumbuka  mmoja wa ahitajiye MSAADA  wa WATU wengine  ni yule idhaniwaye ndiye asaidie  kitu kifanyacho MIMI au WEWE  ... au hata YULE  aaminiye  anaweza yote la bda kwa hilo ndio hasa kidhihirisho kuwa anakwalifai aka ndiye MUHITAJI MSAADA zaidi ambao  labda  tena ule mkubwa ambao ni wa MAWAZO kama tu si o tu jinsi ya  KUWAZUA wazo?
    • Kwani unaamini ni kweli STAREHE ni kujipa MWENYEWE?

    Ndio,...... ukichunguza  au hata KUJICHUNGUZA ,...... unaweza kustukia labda unakosea kustukia ni nani ahitajiye MSAADA kwa kuwa  pamoja na YASIYO MATATIZO yako ,......labda BADO AISEE astahiliye msaada  kwako kiwewe KABISAA ,.......sio MBWA na wala sio PAKA wako kwa kuwa bado tatizo ni LAKO!:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


    Hebu tena Isley Brothers waingilie  tena kati kwa -Summer Breeze

    MC Hammer aulizie tena - Have You Seen Her

    Mc Hammer abadili kwa kukumbushia-U can't touch this


    Naughty By Nature waingilie kati tena kwa -OPP

    Naughty By Nature waongezee kipengele kwa - Hip Hop Hooray

    Au tu Naughty By Nature wazime tena kwa -Feel me flow

  • MAISHA ni MIKIKIMIKIKI na Ray Njau!

    Posted: October 22, 2011, 8:19 pm by SIMON KITURURU


    Ndio ,..... RAY NJAU  yupo ,...... na ukitaka kujua zaidi kwanini MAISHA NI MIKIKIMIKII...bofya HUKU

    Ni hilo tu MUUNGWANA!
    Tukiachana na hilo ,......hebu Patrick Balisidya,...... aturudishie MIKIKI  kikusiliba  NANIHII kwa kipengele kile cha   -WIKIENDI

    Au tu MAKASSY adai tena-MAMBO BADO

  • EMU THREE na DIARY YANGU --Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-40

    Posted: October 22, 2011, 8:06 pm by SIMON KITURURU

    Adamu alibakia kwa muda ameshikilia simu mkononi, utafikiri bado anasubiri kuongea na huyo mtu aliyekwisha kuongea naye karibuni, lakini walikuwa wameshamaliza kuongea, ….kilichomfanya aduwae kwa muda ni hzio taarifa alizozipokea kwa huyo aliyempigia simu, …ilikuwa kama mtu kamtonesha kidonda kilichokuwa kimepona…Hakuamini kabisa kuwa Rose kawa na mwanaume mwingine, …

    ...ENDELEA na stori tamutamu ,...HUKU ,...... ambako ndio KIJIWENI KWAKE huyu NGULI .
    NI HILO tu MKUU!

    Tukiachana na hilo ,...... kimselebuko tuendelee,...... tu na  Linton Kwesi Johnson aanzishe upya kwa ushairi -More time

    Linton Kwesi Johnson aulizie tena - Want Fi Goh Rave ?



    Linton Kwesi Johnson akumbushie - It Dread Inna Inglan


    Linton Kwesi Johnson aongezee kukumbushia - Sonny´s Lettah

    Mutabaruka aingilie kati nakuongelea tena -Dis Poem


    Mutabaruka apandishe dozi jazba kwa -It no GOOD


    Gregory Isaacs alainishe kwa - Out Deh



    Halafu huyu huyu  Gregory Isaacs ajaribu kuzima kwa - Good Morning


    Halafu tu eti  Barrington Levy ndiye azime kwa - Black Roses
  • JONAS SEGU na DEO NJIKU wapima uzito kwa ajili ya KUZIDUNDA JUMAPILI HII MOROGORO.

    Posted: October 22, 2011, 7:22 pm by SIMON KITURURU








    Bondia Deo Njiku wa Morogoro akipima uzito uwanja wa Jamuhuri leo kwa ajili ya mpambano wa kuwania
    ubingwa wa taifa wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) utakaofanyika kesho..

    Kushoto ni mpinzani wake Jonas Segu na promota wa mpambano uo Alifa Kipao..


    ( Picha na HABARI :  www.superdboxingcoach.blogspot.com)





    Kocha wa mchezo wa ngumi Nchini Rajabu Mhamila ' Super D Boxing Coach' katikati akiwainua mikono juu mabondia Deo Njiku wa Morogoro kushoto na Jonas Segu wa Dar es salaam baada ya kupima uzito katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro leo kwa ajili ya mpambano wa kuwania ubingwa wa taifa wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) utakaofanyika kesho jumapili.

    (Picha na habari : www.superdboxingcoach.blogspot.com)





    Nimetumiwa PICHA na HABARI na:

    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.com Mob;+255787 406930         +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
  • Video nyingine ya enzi za TANCUT ALMASI ORCHESTRA(1989)

    Posted: October 22, 2011, 5:00 pm by SIMON KITURURU




    ´´Ninakwenda safari, safari yenyewe safari ya kikazi,
    Ninakwenda safari, safari yenyewe ya masafa marefu,
    Najua hapa utabaki, watasema mengi,
    Pia wabaya wetu mama watafurahi.
    Chorus
    Safari sio kifo mama iyeeo
    subiri ntarudi mama iyeoo




    Nikirudi mama nipokee kwa mikono miwili
    Nikirudi mama nitakuletea zawadi
    Zawadi nono mama watototo
    Iyee mama iyee...``

    Haya tena TANCUT ALMASI ORCHESTRA(1989), wakiwa jukwaani live Tancut Club Iringa wakiporomosha kibao MASAFA MAREFUBofya HAPA--
    www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.com
    www.johnkitime.blogspot.com


    Nimetumiwa na:John Kitime
  • Watakacho WATU hata kama hakileti MAANA kwako, LABDA maana iko ndani ya lao TAKWO!

    Posted: October 22, 2011, 4:30 pm by SIMON KITURURU
    Na tatizo kubwa la WASOMI au tu wajuao mpaka  wanapitiliza na kudhania wanamiliki kujua hata TAKWO  la watu wengine,...
    ..... yasemekana ni kutumia miakili yao  KUOANISHA  KULETA MAANA kwa KITU  na  KUTAKWA kitu.:-(

    Swali:
    • Unabisha?
    • Hujastukia kuna watu wanaamini watakavyo na wewe inabidi kiaina uvitake hivyo vidude?
    • Si kuna vielewekavyo  na kuleta maana kwa wengine tu hasa kwa kuwa wao sio wewe?

    Ndio,...
    ... utakacho,...
    ... labda  ni muhimu kukumbuka kuwa labda hicho kidude hata kama ni DINI au tu tako kuwa  kwa wengine haki ya nani  hicho kidude HAKINA MAANA.:-(
    NI wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

    Hebu Keith Sweat aanzishe tena upya kwa - Twisted



    Marving Gaye arudie-Sexual Healing


    Donell Jones adai- U know what's up

    Au tu R. Kelly azime tena kwa - Ignition
  • Leo katika CHAKULA cha AKILI!

    Posted: October 22, 2011, 4:00 pm by SIMON KITURURU
    Think Different



    Bob Marley - Redemption Song


    Jumamosi njema MKUU!
  • 1st FASHION AWARDS TO BE DONE IN EAST AND CENTRAL AFRICA FROM SWAHILI FASHION WEEK 2011- VOTE FOR YOUR FAVORITE

    Posted: October 22, 2011, 3:30 pm by SIMON KITURURU



    Hello everybody, Swahili Fashion Week 2011 introduce to you Fashion Awards. Please we have mention the Categories at the Right side of the website Vote for your Favorite. Is simple go to the Box tick on the dialog box of your favorite nominee, then down click vote,you canonly vote once to any Category of your choice . Votes start now until 10th November 2011. Please invite others to vote too. Thank you all in advance and for being part of SWAHILI FASHION WEEK

    To vote click this Link : www.swahilifashionweekawards.blogspot.com
    Nimetumiwa na :Esi MgimbaSwahili Fashion week 2011
  • PRESHA za WEWE kuwa kama WALE na MIMI kuwa kama WEWE zivalishavyo chupi UHURU binafsi!

    Posted: October 22, 2011, 3:00 pm by SIMON KITURURU
    Kuwa HURU ASILIMIA MIA kwa MIA wakati uko hai,....


    .....labda  hilo ni ALINACHA tu a.k.a JAMBO la kufikirika tu,........ hasa  kwa kuwa  WEWE ni WEWE na uhuru wako labda wahitaji  uhuru kwa kuwa kuna watu WENGINE!!:-(
    Swali:
    • Umestukia  kuwahuru  NI SWALA  lakufanyia kazi SIKU  hadi SIKU, dakika hadi DAKIKA  hasa kwa kuwa  WEWE ni WEWE  na  uhuru WAKO unasababishwa pia na uwepo wa wengine ambao huna MAMLAKA ya WAFIKIRIAVYO au hata uwepo wao?

    Ndio,........ labda MOJA  ya kifichacho watu  kuwa  hawako huru,...  ... ni  imani zao tu  kuwa WAKO HURU  na ya WENGINE  hayawaathiri  kitu ambacho labda nacho ni ALINACHA tu KIHALIHALISI!:-(


    Ni wazo tu hili KAMANDA!:-(






    Hebu tena The Isley Brothers waingizie - Contagious


    The Isley Brothers waongezee dozi tena kwa - Secret Lover


    Au wazime tu tena kwa -Between the sheets
  • Kwenye FANI,...

    Posted: October 22, 2011, 2:25 pm by SIMON KITURURU
    .... labda wasioko  ndani ya FANI waongeleao fani   kiaina ni WAZUSHI!:-(
    Swali:
    • Si labda ya KILOKOLE  ayajuayo vizuri  hata kuyaongelea kiundani  ni MLOKOLE ayaishiyo hayo ya KILOKOLE  kilokole?

    Ndio,....... labda  hata ya KIMALAYA,......mtaalamu wa fani ni MALAYA,....... na abwabwajaye ya KIMALAYA asiye MALAYA  kwa asilimia nzito tu  yawezekana  afanyacho na aongeleacho  kina  UZUSHI!
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na ni  ruksa kulibishia!:-(
    Hebu Mick Jagger na Lenny Kravitz wadai -God give me everything I want

    Led Zeppelin waingizie - Black Dog


    Halafu AC /DC wazime kwa -Thunderstruck

  • Katika jitihada za kutofautisha WATU na WANYAMA PORI wakati bado LIBYA iko MAWAZONI!

    Posted: October 21, 2011, 5:14 pm by SIMON KITURURU
    Kuna wakati wanyama wanaeleweka ni kwanini,...
    ... wanafanya wafanyavyo  hata kama wafanyacho KIBINADAMU ni  unusaji wa bonge la kinyeo.:-(,...
    Hebu tuwadeku  na kushuhudia  kielewekacho,....

    Na WANADAMU  na UTASHI wao,....... kuna waelewao labda  na kutetea kuwa kifanyikacho na WANADAMU mara kibao ni UTU kwa kuwa wafanyao ni WATU na sio UNYAMA  kwa kuwa kuna vigezo   watendao wanaongea na kuvaa chupi na suruali kama sio sketi  huku wakijiita WATU kwa kuwa wanadai wanaakili kuliko WANYAMAPORI  wanajua hata KIMANENO kuwa MATUSI  akitukana Simon Kitururu NI NINI ingawa kiutu  ukifikiria unaweza  kutokwa ladha ya CHAKULA kama kitendwacho na WATU KINYAMA  kimdhuruye ni wewe ,...
    .... hebu tu tutembelee nchi ya  ZANZIBAR  iliyo jirani na TANGANYIKA kupata kifungua kinywa kwa kuwa kinapanda na atendwaye unyama sio sisi ,...
    ...na  kwa Breakfast  kutoka Zanzibar   tupate,...


    Kachumbari tupatie IRAN

    Dina ya Mchana  kiaina tupatie huku huku  IRAN


    Kianzio cha dina ya usiku twende Iraki kuchekelea Mtu anauawa:-(

    Dina yenyewe kwa furaha za kibinadamu tupate Libya wakati bado ya moto,...


    Ndio,...... kimkao fulani labda ,......TOFAUTI ya WANYAMA PORI na BINADAMU ,...... kiutu WANYAMA PORI wanaeleweka KIRAHISI na wafanyayo yana UTU kuliko WATU!:-(Swali:
    • AU?
    • Si unakumbuka kunibishia RUKSA?
    Na ni wazo tu hili MHESHIMIWA wala USIKONDE!
    Na labda tubadili wazo tu  HILI  NYOMI KIHUZUNI -``sasa tutafanyaje!?´´........ kwa ndude ``Napenda matako makubwa a.k.a Baby got back ´´,..........kama idadavuliwavyo kibinadamu  na -Sir Mix-A-Lot


    Halafu au tu Tone Loc aloki kipengele kwa - Funky Cold Medina

  • SWAHILI FASHION WEEK in ANGOLA ON 15/10/2011

    Posted: October 21, 2011, 3:50 pm by SIMON KITURURU
    Designer Gabriel Mollel from Tanzania during the Fashion Bussiness in Angola on 15th-oct-2011


    Designer Manju Msita from Tanzania during the Fashion Bussiness in Angola on 15th-oct-2011

    Mustafa Hassanali from Tanzania during the Fashion Bussiness in Angola on 15th-oct-2011

    Tanzanian Consul in Luanda HE Mziray Mbwana with Team Tanzania at Fashion Business Angola on 15 Oct 2011







    Nimetumiwa na:Esi Mgimba
  • AJALI YA NDEGE ILIYO TOKEA KILOMETA 15 KUTOKA UWANJA WA NDEGE WA KIA JANA USIKU.

    Posted: October 21, 2011, 2:41 pm by SIMON KITURURU



    Picha ya ndege iliyo dondoka ikitoka KIA usiku wa jana ambapo kulikuwa na Pilot aliye fariki dunia papo hapo anatambulika kwa jina la Ally na abiria mwengine ambae yupo KCMC kwa matibabu zaidi.

    Picha na HABARI:
     Latest news Tz Blog
    Nimetumiwa na:MDAU  wa Latest news Tz Blog
  • Kuna sababu Kichwa, NYONYO au hata KORODANI ingawa ni nzito kwa kawaida kwa MTU hivyo sio MZIGO!

    Posted: October 21, 2011, 1:30 pm by SIMON KITURURU
    KAWAIDA! Na  kwa kawaida kama mdada anaanza kuumwa MGONGO kisa  uzito wa NYONYO,....
    ... kama tu  kwa ALWATANI  ambaye kikorodani  mwendo siku hizi taratibu  kisa BUSHA  na  makende yamegeuka MZIGO,........ huo ni ushahidi tu  huyo Bin'ADAM abebacho  huyo  si KAWAIDA.:-(
    Swali:
    • SI kwa kuwa ni kawaida ndio maana Bin' Adam huwa hastukii kwa kawaida uzito wa hata  KICHWA  chake ingawa  kwa kawaida BICHWA ni kilo kadhaa kiuzito?

    Ndio,...
    ..... kama kwako hicho KITU  kwako ni MZIGO,...
    .... hata kama kwa jina hicho kitu ni MME WAKO,...
    .... labda  tayari hicho kitu  si KAWAIDA na JIVUE GAMBA Mwanakwetu  hasa kama  kwako  hilo si DHAMBI.
    Swali zaidi:
    • Lakini  si  inakumbukwa kuna mambo mengine kusikia UZITO kwayo ndio KAWAIDA?
    • Lakini si NZITO  ni kawaida ikiwa NZITO pia?

    Ndio,....... labda pia kama KITU kimebebeshwa mpaka MIMBA na bado uzito ni uleule,...... katika hilo   sio KAWAIDA,...
    ... kwa kuwa kuna vitu hata kama KIUZITO ni kimaumivu,...
    .... labda BINADAMU huhitaji kukumbuka kuwa hiyo ndiyo kawaida,...
    .... kama tu ilivyokuwa kama unaungua na husikii MAUMIVU hiyo si KAWAIDA!:-(

    Ni wazo tu hili  lilipopinda na kupiga U-turn kiaina  MHESHIMIWA!Ijumaa na WIKIENDI njema KIMAHUDUSHI PANGALA Mheshimiwa!
    Hebu  tubadili wazo tena kwa msaada wa SAM Mangwana katika kibao-Bana ba CAMEROUN


    Sam Mangwana aongezee tena dozi kwa -KABIBI


    Samba Mapangala aingilie kati kwa ku- Vunja Mifupa

    Pepe Kalle akatizie tena denge nakuachia  tena-MOYIBI


    Halafu PEPE KALLE azime kibatari kwa -Gérant

  • TWANGA PEPETA kusugua VISIGINO nchini UINGEREZA

    Posted: October 21, 2011, 12:02 pm by SIMON KITURURU
    Mkurugenzi wa Twanga Pepeta katikati Asha Baraka Akiongea na waandishi wa Habari Kuhusu Uzinduzi na Ziara UK




    Salam,

    Baada ya kufanya na Kumaliza uzinduzi wa albamu yao kabambe tarehe 6 Novemba 2011 ASET wakishirikiana na URBAN PULSE CREATIVE Wanatarajia kuwaburudisha wapenzi wa Bendi Maarufu ya Twanga Pepeta Nchini Uingereza mwishoni mwa Mwezi wa Novemba.

    Show Hii Maalum ni kwa ajili ya kuazimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Tarehe pamoja na maelezo ya Ukumbi yatafuatia mda sio mrefu. Hivyo wadau kaeni mkao wa Kula.

    Asanteni,

    Urban Pulse Creative.

    Nimetumiwa HABARI na :Frank Eyembe wa Urban Pulse Creative
  • Tamaduni za KUCHEKELEA KANYAU kwa kuwa MTU kafa ZIPO hata kwa uliowahi kuwaona katika MSIBA mwingine wanalia!

    Posted: October 21, 2011, 4:05 am by SIMON KITURURU
    Ndio,...... labda sijawahi kuchukia vizuri MTU,...... lakini kifo cha mtu mpaka leo hii hakijawahi kunifanya nirukeruke kwa FURAHA kisa mtu KAFA!:-(
    Swali:
    • Si umestukia watu huchekelea kanyau MTU akifa  kama wakiamini wanasababu kuwa MAREHEMU ni MTU mbaya?
    KIUNGWANA lakini,..... MAREHEMU daima  alikuwa ni MTU MZURI!:-(

    Swali:
    • AU?
    Naendelea tu KUWAZA!:-(

    Hebu Zap Mama aanzishe upya kwa - Mupepe


    Zap Mama aanzishe kuvimbisha mtekenyo kwa- Cou Cou


    Halafu labda Zap Mama atulize kwa - Yaku


    Kabla tu tena sijui kwanini Zap Mama hajazima kwa - Sweet Melodie

  • Katika ya watu yazaniwayo RAHISI, labda SI rahisi kwa kuwa ``THe deVIL iS in thE DetaiLS!´´.:-(

    Posted: October 21, 2011, 4:02 am by SIMON KITURURU
    Ndio,...
    ... MENGI kama huhusiki  katika kuyatimiza na unategemea MTU MWINGINE atimize huku ukidhania ni rahisi,...... labda  kumbuka tu USICHOKIJUA  hata kwa UMJUAYE,.......kama unadhania ni rahisi kwako haimaanishi kwa mwingine ni KIBONDE,.......kitu ambacho labda ndio maana SIO RAHISI wasiojua ``DETAILS´´ kuelewa  wafikiriavyo ni RAHISI kutimizwa na wawatumainiwao  watatimiza,...... kama tu labdaWATANZANIA wajuao miakili ya Rais MKAPA  halafu wakastukia hatimizi,......hutokea HAWATIMIZIWI huku wanashangaa hata KISIRI  kwa kuwa labda KIUKWELI  katika DETAILS labda katika shughuli za kiume kumshughulikia MWANAMKE kuna msenge ASIYEJULIKANA KATIKATI YA SHUGHULI ya KUMCHANUA MWALI  ki-DETAILS  aisee ikichunguzwa!:-(



    Swali:
    • Unabisha?

    Ndio,......  kuna vipengele kwenye MUWA,...... na kama  vipengele  aka VIFUNDO havipo,.......KIDETAILS labda ndio siri kwanini  MUWA hushindikana kuwepo  pia AISEE!:-(
    Ni wazo tu hili lilopinda kiduchu KAMANDA!:-(

    Hebu Gregory Isaacs abadili ndude KIWAZO kwa kugusia tena - My Only Lover




    Aguseguse- Substitute


    Atekenye -Hush Darling


    ...apapasepapase na ku- Cool Down The Pace



    Gregory Isaacs huyuhuyu ajaribu ku - Confirm Reservation


    Asiruke-Front DOOR


    ...abembeleze tena  kwa-Objection Overruled



    Au tu tena kiaina azime kwa -Not The Way

  • R.I.P MUAMMAR GADDAFI

    Posted: October 20, 2011, 9:12 pm by SIMON KITURURU
    Muammar Gaddafi  (7 June 1942-20 October  2011)


    R.I.P ,........na utakumbukwa na Wakupendao NA wakuchukiao PIA!
    Habari zaidi,.......HAPA





  • Kwa kuwa PILIPILI iliyoshamba yaweza kuwasha walio NYUMBANI kabla ya kuletwa NYUMBANI!

    Posted: October 20, 2011, 7:00 pm by SIMON KITURURU
    Swali:
    • SI kwa walioonja uchungu wa KLOROKWINI  katika mchakato wa kutaka  kutibu MALARIA walikuwa wanajua watasikia uchungu au mpaka kutapika kabla hata ya kuweka KIDONGE mdomoni kwa kuwa wanajua uchungu wake kitu kilichofanya baadhi wagundue kuchomeka vidonge vya KLOROKWINI kwenye NDIZI kabla ya kuonja UCHUNGU?
    • Na si ajuaye uchungu wa kuumngua na MOTO unaweza kumfanya asikie uchungu na kuanza kulia kwa kumtishia tu utamuunguza kwa kusogeza kaa la moto karibu na jichole?

    Ndio,..... labda unaweza kuwashwa na WASHAWASHA hata kwa mbali kama unajua tabu za kuwashwa,.......au TU TUKIRUKA MENGINE bado unajua finyofinyo kiwashawasha kinyoko ni NINI  kwako!:-(
    BADO ni wazo tu hili KAMANDA:-(
    Hebu Bruno M arudishe mtekenyo katika kutubadili wazo kwa -Dança dos Comba




    Bruno M aongezee dozi kwa - Thubilla

    Au tu sijui kwanini  Burning Spear akatizie denge,.......na kubadili mchezo kwa kusifia kwao kwa-Land of my birth


    Halafu huko huko kwao  Eric Donaldson aingilie kati kwa - Are you thinking of him



    Halafu  tu Eric Donaldson azime tu kwa -More love


  • FRANSIC MIYAYUSHO ajiandaa kumkabili MBWANA MATUMLA

    Posted: October 20, 2011, 6:24 pm by SIMON KITURURU


    Bondia Fransic Miyayusho (kulia) akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi na Badi Sachedina wakati wa mazoezi ya mwisho ya MIYAYUSHO  kabla ya kumvaa Mbwana Matumla katika mpambano wao wa ubingwa mwishoni mwa mwezi huu.
    ( Picha na habari: www.superdboxingcoach.blogspot.com)




    Bondia Fransic Miyayusho (kulia ) akiongoza mazoezi katika kambi yake ya lazima ukae iliyopo Kinondoni , Dar es salaam jana.  Miyayusho anajiandaa na mpambano wake wa ubingwa na Mbwana Matumla litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu.
    ( Picha na habari: www.superdboxingcoach.blogspot.com)




    Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) akielekezwa jinsi ya kutupa masubwi na Doi Miyayusho wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wa kuwania ubingwa na Mbwana Matumla utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu.
    ( Picha na HABARI: www.superdboxingcoach.blogspot.com)








    Nimetumiwa PICHA na HABARI na:

    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
  • Trailer kuhusu Mahojiano ya Mh Waziri Mkuu MIZENGO PINDA

    Posted: October 20, 2011, 6:00 pm by SIMON KITURURU
    Salam,[www.youtube.com]Urban Pulse Creative wakishirikiana na Star tv wanakuletea Trailer ya Mahojiano Maalum na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofanya ziara nchini Uingereza hivi karibuni. Mahojiano haya yalikuwa yamelenga zaidi kupata ufahamu na uchambuzi wa namna serikali yetu ya Tanzania inavyofanya kazi pamoja na changamoto zake.
    Mahojiano haya yalifanywa na Baraka Baraka  Kutoka Urban Pulse na yatarushwa Hewani kupitia  kituo cha Star TV Jumapili ijayo Tarehe 30 octoba 2011 kuanzia saa 10.30 katika kipindi cha Medani za siasa.Tafadhali usikose kuangalia kipindi hiki ili upate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Tanzania na Serikali yetu.Asanteni,Urban Pulse Creative
    ...au deku...


    Nimetumiwa hii HABARI na:Frank Eyembe wa Urban Pulse Creative
  • AJALI MBAYA MKOANI MBEYA MAENEO YA MLIMA NYOKA KUELEKEA UYOLE

    Posted: October 20, 2011, 5:30 pm by SIMON KITURURU
    MAJERUHI WA AJALI HIYO MBAYA ILIYOTOKEA MBEYA JANA.
    MWILI WA MAREHEMU YUDA AMBOKILE UKIWA UMENASA KWENYE GARI.
    MAJERUHI MWENGINE ALIYE NUSURIKA KIFO





    STORY
    ..na Ezekiel Kamanga-MBEYA YETU.

    Jinamizi la ajali mbaya limeendelea kuusakama mkoa wa Mbeya ambapo usiku wa kuamkia jana imetokea eneo la Mlima Nyoka Uyole Jijini humo na kuua watu watatu akiwemo dereva wa gari hilo dogo Yuda Ambokile Jeshi la Polisi limethibitisha.

    Kaimu kamanda wa polisi Anacletus Malindisa anesema Marehemu wengine ni Peter Kishimba mwenye umri wa miaka 47 mkazi wa Tazara Iyunga na Joshua Sanga mwenye umri wa miaka 2 mkazi wa Uyole jijini Mbeya na ajali hiyo ilitokea majira ya saa Moja na nusu kwa kuhusisha gari Nne ambazo zote zilijeruhi watu waliokuwemo ndani yake.

    Wakizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kuharibika kwa gari aina ya Toyota Dyana yenye namba za usajili T 660 AUX ambayo ilikuwa imeegeshwa katika mlima huo.

    Walisema kuwa kutokana na kuharibika kwa gari hiyo ndipo gari dogo aina ya Suzuki Escudo yenye namba za usajili T 425 BAZ , iliyokuwa ikitokea barabara ya Mbarali kwenda Mbeya mjini ambayo ilikuwa na abiria watano iliigonga gari hiyo na kusababisha kifo cha Dereva wake Yuda Ambokile na wengine kujeruhiwa vibaya na magari mengine Toyota Cheser T 512 BCT na Nissan T 991 BAK.

    Baada ya gari hiyo kugonga gari iliyokuwa imeegeshwa na kusababisha madhara hayo ndipo gari nyingine aina ya Baloon ikagongwa na gari hiyo aina ya Escudo kisha Baloon hiyo ikatumbukia korongoni na kusababisha majeruhi wawili waliokuwemo ndani ya gari hiyo ambao wote walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na Mmoja wao akaruhusiwa baada ya hali yake Kiafya kuimarika.

    Ajali hiyo haikuishia hapo bali gari nyingine aina ya Pickup yenye namba za usajili T 991 BAK nayo ikakumbwa na dhahama hiyo ambapo iliharibika vibaya bila kusababisha majeruhi kwa watu waliokuwemo ndani yake.

    Majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutembelewa na waandishi wa habari leo, wengi wao walikutwa wakiwa na hali mbaya na kushindwa kuzungumza chochote bali baadhi yao waliokuwa na nafuu walisema kuwa walikuwa hawakumbuki chochote juu ya ajali hiyo zaidi ya kujikuta wamelazwa wakiwa na majeraha katika miili yao.

    Majeruhi hao ambao baadhi yao waliweza kuzungumza na waandishi wa habari ni pamoja na Denis Untwa (24) ambaye ni dereva wa Baloon, Laina John Sanga (35), Michael Mteve (20), Anania Simbeye(35) ambaye ni dereva wa Escudo, Emmanuel Tambikeni na mmoja aliyejitaja kwa shida jina moja la Boniface..

    Habari na (www.mbeyayetu.blogspot.com)


    Nimetumiwa HABARI na:Mdau wa MBEYA YETU Blog


    Poleni jamani MLIOKUMBWA na JANGA!R.I.P Marehemu Wapendwa!-Simon Kitururu
  • Kwa bahati mbaya TUKO WENGI tupendao kumsikiliza au hata KUMSOMA aongeleaye TUTAKAYO KUSIKIA!:-(

    Posted: October 20, 2011, 2:00 pm by SIMON KITURURU

    Na yasemekana UKWELI ni kwamba,...... kama tayari unajua UPENDAYO kusikia,........ labda hayo tayari unayajua kiasi cha kutosha kama ukiyafikiria MWENYEWE kiundani,..... na labda wakati huo ingekuwa busara KUSIKILIZA au hata kusoma usiyotaka KUSIKIA,...... kama nia ni kutaka kuendelea kujifunza kitu KIPYA!:-(

    Swali:
    • AU?
    Ndio,...... labda kuendelea kunogewa kusikia utakacho kusikia hata kama hicho ni kuwa WEWE ni MZURI KWELI,...
    ..... wakati huo yawezekana unajijua TAYARI wewe ni MZURI mwenye sura tamu kama PIPI na huo MUDA uendeleao kuutumia kurudia kusikia sifa zilezile za uzuri wako,....... KIBUSARA labda ungekuwa ni wakati wa kujifunza kwa uzuri wako HUO uchuneje buzi KIMALAYA au tu uuficheje ki SISTA wa KIKATOLIKI ili usidoewe na Wakware.:-(

    Swali zaidi:
    • AU?

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

    Hebu turudi UGANDA ili PHILLY LUTAAYA aanzishe upya kwa-Ndabye Ennake



    Philly Lutaya atukumbushe tena -Tugende e kampala



    Kabla tu huyuhuyu Philly Lutaaya hajazima kwa -Entebbe Wala
  • Kwa kuwa UTOTO wa MTU MZIMA ni kitu cha kuficha!

    Posted: October 20, 2011, 12:29 pm by SIMON KITURURU
    Watoto eti ni MALAIKA,...... lakini kubwa zima likiendekeza UTOTO sio tena UMALAIKA.
    Swali:
    • Unamkumbuka Michael Jackson?

    Ila lakujiuliza vizuri ni kwamba;.....
    ...Je utoto HUMUISHA Mtu MZIMA au utu uzima ni shule tu ya kumfanya MTU mzima ajizuie kufanya UTOTO?
    Ndio,.,...
    .....NAKUBALI,...
    ....kuna WADAU hunipa vidonge vyangu kuwa BLOGU hii imejaa UTOTO katika staili hii niitumiayo kuandika ya UjingaBUSARA.
    Swali zaidi:
    • Je si waliozeeka sana nasikia mambo zao hurudia kuwa kama ya kitoto?
    • Kwa hiyo Je UTOTO uzeeni  ni jambo la kujifunza tena au ni swala la kutojizuia tu tena kufanya yaaminikayo ni ya kitoto ?
    • Ushawahi kuona Mzee sana mambo zake halafu yakakukumbusha Mtoto?

    Ndio,......... labda UTOTO na UZEE  vyote ni MALAIKA.:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na Usikonde!:-(
    Hebu turudi KAMERUNI ili Sandra NKaké aanzishe tena kwa -Higher

    Sandra Nkake arudie pia - I miss my land


    Au tu Sandra Nkake azime kwa-H.A.P.P.Y

  • WASANII MNAVYOKAA KWENYE VIKAO VYENU NA BASATA NA HILI PIA MNALIONGELEA?

    Posted: October 20, 2011, 12:01 pm by SIMON KITURURU
    Msanii wa maigizo ya vichekesho JOTI akitoa changamoto ambazo anakutana nazo katika sanaa yake hiyo ya maigizo.
    Mzee Kipara hii ndio hali aliyofikia hivi sasa.
    Mzee Kipara ni msanii wa muda mrefu ambaye alikuwa katika sanaa ya maigizo kwa muda mrefu, kipindi cha hivi karibuni vyombo mbali mbali vya habari vilitoa hali ya afya yake.

    Kwa sasa hali yake bado ni mbaya, napenda kuwakumbusha tena wasanii wote msimtupe mzee huyu na mnavyoendelea na vikao vyenu na BASATA pia muweze kumuongelea Mzee huyu, ili kwa pamoja na Serikali mumsaidie. Napenda kuwashukuru wale wote waliojitahidi kumsaidia kwa namna moja au nyingine ili kuweza kumfanya Mzee huyu ajisikie ana watu ambao wanamjali, Mungu atawarudishia.

    Nimetumiwa HABARI na:Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog

    UGUA POLE Mzee Wetu!Na MUNGU akujalie Upone haraka!-Simon Kitururu
  • Tatizo la MAJIBU,....

    Posted: October 19, 2011, 6:47 pm by SIMON KITURURU
    ......huwa hayajibu kitu  baada ya MTU kujibiwa kama ajibiwaye,.........hayayafanyiikazi!:-(


    Ni angalizo tu hili  MKUU!

    Hebu Mbaraka Mwinshehe  arudie - Urafiki Mwisho Wa Mwezi


    Au MBARAKA MWINSHEHE aongezee dozi kwa  - Shida


  • Zawadi ya MAUA na WAAFRIKA!

    Posted: October 19, 2011, 6:40 pm by SIMON KITURURU


    Baada ya kukuta ZAWADI hiyo hapo  ya UA kwa DADA YASINTA,......HAPA..... .... nimejikuta najiuliza:
    • Hivi ni kwanini WAAFRIKA wengi UA kwao sio ZAWADI na kwa Wamagharibi ni lini MAUA yalipamba moto kuwa ni ZAWADI MWANANA?
    • Kwako UA ni Zawadi?
    • Kama sio KWANINI na kama ndio -Kwanini?




    Nawaza tu kwa SAUTI!
    Hebu tubadili wazo kwa kumuachia Wiz Khalifa  katika- Fly Solo



    Au Wiz Khalifa azime tu kwa - Black And Yellow

  • Matumaini katika kinga ya MALARIA!

    Posted: October 19, 2011, 2:00 pm by SIMON KITURURU



  • Wengine WAKUZUNGUKAO inawezekana sio tena WATU bali ni LUNINGA ,kompyuta na MAGAZETi ya UDAKU.

    Posted: October 19, 2011, 1:50 pm by SIMON KITURURU
     Wengine WAKUZUNGUKAO ,.... ... yawezekana ndio waathirio YAKO  UFIKIRIAYO na yakuzungukayo sasa hivi,...... hata ki uyatafsirivyo.

    Swali:
    • Kwani unafikiri WENGINE kwako bado NI WATU au tu  ni  VITU tena vya wengine hasa katika DUNIA HII ya leo ambayo VITU na MALI vyajaliwa kuliko UTU ? 
    • Si umeshawahi kusikia kuwa kuna watu kibao hata nchi zilizoendelea  WANYAMA kama Mbwa au paka na WATU  hakuna tena tofauti  kiwawafikiriavyo?
    • Na si  pia ukitaka kupima thamani ya MTU na KITU labda chunguza ni kwanini KIBAKA anaweza kutolewa roho  kwa kosa la kuiba  ndizi kitu kifanyacho labda MTU na NDIZI  au hata tukiita kidhaniwacho KIBAKA kakwapua ni POCHI - kwa watu wengine kiuthamani  UHAI  na KITU hakuna tofauti au kwa kuwa KIBAKA huuawa basi UHAI haunathamani kama KITU?

    Ndio,...
    ... labda ukifikiria,...
    .... WENGINE wakuzungukao na kuathiri ufikiriavyo,....
    ..... sio WATU tena moja kwa moja kwa kuwa UTHAMINICHO labda wala sio MTU.
    Katika kumbukumbu:
    • Unakumbuka  msemo HAPENDWI MTU pochi lako tu!?:-(
    Ndio,....... kwa wengine MTU  na KITU ,....... labda kiuthamani  hakuna tena tofauti kitu kifanyacho KITU kuthaminiwa ZAIDI.:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(





    Hebu  tupitie tena TOGO ili Afia Mala amwage - Baila Mi Musica


    Afia Mala aongezee dozi kwa - Ten Homte


    Halafu hapahapa TOGO hebu tena Afia Mala azime kwa- Segne

  • Daktari Mtanzania Julie Makani apokea tuzo kutoka Royal society Pfizer London

    Posted: October 19, 2011, 1:00 pm by SIMON KITURURU
    Salam,          

    Dr Julie Makani kutoka Tanzania amepokea Tuzo  jumanne tarehe 18 octoba 2011 ya Royal Society Pfizer nchini Uingereza. Dr  Makani amepokea tuzo hii ya utafiti alioufanya katika gonjwa hatari la Sickle Cell (SCD) ambaye makazi yake ya kazi ni kwenye Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi cha Muhimbili katika idara ya Haematology. Kutokana na utafiti wake kumeonekana ushahidi kuwa, chanzo kikuu cha magonjwa na vifo vitokanavyo na sickle Cell nchini Tanzania husababishwa na Arnemia (upungufu wa damu)

    Dr Makani pia amefanya mchakato wa matibabu katika majaribio ya Hydroxyure chemotherapy agent inayo gusa Bone marrow katika matibabu ya  Anaemia kwenye  ugonjwa wa Sickle Cell

    Ni matumaini yake  kuwa utafiti huu utapelekea kuboresha uchunguzi na matibabu ya ugonjwa huu ili kuweza kuimarisha afya za watu, mfumo mzima wa afya  na jamii kwa ujumla.

    Kwa niaba ya Watanzania  wote  Urban Pulse tunapenda kumpongeza  DR Makani kwa mafanikio hayo.

    Asanteni

    Urban Pulse Creative



    Dr Julie Makani akitoa machache

    Wageni waalikwa kwenye Royal Society Pfizer Awards London


    Kutoka Kulia Balozi Kallaghe, Mama Makani, Dr Makani, MP O'Brien, Naibu Balozi Chabaka na Mr Simba

    Dr Julie Makani akiwa na familia yake

    Dr Julie Makani Akipokea Tuzo yake


    Dr Julie Makani akiwa na Baba yake Mr Bob Makani pamoja na Mama Vicky Makani

    Parliamentary Under Secretary of State, International Development Stephen O'Brien. akimpongeza Dr Julie Makani

    Dr Julie Makani. akiwa na Cleo, Paul na Frank baada ya kupokea Tuzo.
    Nimetumiwa na :Frank Eyembe wa Urban Pulse Creative

    Hongera Dr Julie Makani!-Simon Kitururu
  • Katika KUMBUKUMBU: Hotuba ya January Makamba kijijini Tamota.

    Posted: October 19, 2011, 12:31 pm by SIMON KITURURU


Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs