SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • Kuhusu UGONJWA wa MAHITAJI hata kama MAHITAJI yenyewe ni PIPI kwa mwenye hitaji hasaaa la WALI!

    Posted: January 31, 2012, 10:14 pm by SIMON KITURURU
    PIPI huweza kugeuzwa kuwa HITAJI,....... hata kwa ambaye hitaji lake la  kweli kwa kihitajikacho ni NGUNA na MLENDA.Swali:
    • Unauhakika UNAHITAJI ufikiriacho kwako ni HITAJI?
    • Si unakumbuka kuna mahitaji watu hujifunza tu kuyachukulia kuwa HITAJI yasemekana?
    • Na UKIHITAJI UGALI na ukapata UGALI - si uleule UGALI yasemekana unakuwa MTAMU zaidi kitofauti?

    Na katika GONJWA la HITAJI,........kuna WAHESHIMIWA hubaka kuku,...... kisa wamegeuza kitu HITAJI,....... na kihitaji fulani MTU akiamini ndilo HITAJI,........labda ndio maana WATU huwa na mahitaji tofauti hata kama wako kwenye CHAMOTO KILEKILE,...
    ..... na labda ndio maana katika ``CHAMOTO UNAKIONA KILEKILE kwenye MAISHA´´  yasemekana  kuna wamkimbiliao YESU, MOHAMEDI, au hata MGANGA WA KIENYEJI hata kwenye hoja ambazo wangeweza kujitetea wenyewe bila NUKUU za MWALIMU NYERERE alisemanini kuhusu HILO kama tu jinsi ambavyo kuna wachaguao KUFA MOYO na kusubiria tu litokealo na LIWE!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na USIKONDE!







    Hebu KANDA BONGOMAN arudi tena na kuanzisha upya kwa-JT




    Halafu sijui kwanini ngojea KANDA BONGOMAN arudie-Wallow



    Burning Spear aingilie ghafla nakukumbushia - Identity


    Ili tu eti BURNING SPEAR apunguze spidi ya muwasho tena kwa-SHE IS MINE


    Au tu Burning Spear alainishe mzimo wakati anazima kwa-Reggae Physician
  • HISIA ni HALIHALISI ingawa sio lazima HISIA ni UKWELI kiuhalihalisi wa KITU!

    Posted: January 31, 2012, 10:04 pm by SIMON KITURURU
    Na LABDA ukihisi ,....... wewe labda UMEHISI TU na  hiyo kwako ni HALIHALISI,........ ingawa labda pia kuna umuhimu wa KUKUMBUKA,........ HISIA sio lazima ni UKWELI.

    Ni wazo tu hili BINGWA!

    Hebu tena SAM MANGWANA aingilie kati na kurudia mdinyo-AFRICA




    Halafu Kanda BONGOMAN azime la njugu live kwakuanza na -Isambe

  • Eti kuna watakao BABA kwenye MUME kama wageuzao MKE kuwa kama MAMA YAO!

    Posted: January 29, 2012, 9:08 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,....... inawezekana kuna wake za watu ambao MME kageuka BABA na wala sio MPENZI wala rafiki,......... kama tu isemekanavyo kuna MIDUME kwa MKE  inadeka kama MKE ni MAMA na sio limpenzi!:-(

    Swali:
    • Unabisha?

    Ndio,....
    .....UNACHOTAFUTA,.....
    ...... saaa nyingine unaweza kuwa unacho ila umekigeuza na wakummtongoza umemgeuza DADA au KAKA  ambayo ni hatua ya mbali zaidi ya ile BINAMU nyama ya HAMU!:-(
    Swali:
    • Unabisha?



    Ndio,...
    ......UNACHOTAFUTA,....
    .... saaa nyingine unaweza kuwa unakitafutia kwenye FIRIGISI wakati kiko kwenye MCHICHA  ambao UNAO.:-(
    Swali:
    • Unabisha?
    • Unauhakika kwako BABA ni BABA, Mama ni MAMA na RAFIKI sio PADRE kama HAUSIGELI /Hausiboi alivyo kisiri ni MPENZI?

    Ndio,....... kuna wageuzao ,......... ambacho KIPO hata kifudifudi MBELE ZAO!:-(
    Ni hilo tu na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

    Hebu Bassekou Kouyate arudishe mdinyo - Segu Blue




    Halafu ghafla The Commodores warudishe tena kile kitu fanki kile - Brick House
    Halafu The Temptations watubakize kwenye fanki na kuzima tena kwa -Shakey Ground


  • Huwa NAJARIBU!:-(

    Posted: January 29, 2012, 12:56 pm by SIMON KITURURU
    Hebu Kaka Joseph Hill anisaidie katika-I  TRIED




    Au ngoja tu Jean-Claude Naimro alainishe kwa - En Balaté
  • Kuhusu yule KISURA ambaye kwako LABDA ni KISURA tu mpaka ukiunganisha umfikiriavyo akiwa UCHI!

    Posted: January 29, 2012, 7:08 am by SIMON KITURURU
    Ndio,....... labda NGUO ukatizia denge katika kuficha kitu,...... na umtamaniye labda ni nguo tu ambazo zaongezea matamanio kwa kuwa ukimfumania chooni wakati anakunya labda hapendezi kama akuvutiavyo UKIMTAZAMA wakati ANALIA kisa unamemfumania USO UKO UCHI ingawa hata umjuavyo huwa hafuniki USO hadharani!:-(

    Swali:
    • Si unajua ni RUKSA kunibishia?
    • Na si wajua kuwa UCHI si lazima uvue NGUO?


    Ndio,...... labda kuna ambao unapenda mpaka mawazo yao,.......... LABDA kwasababu tu hata KIMAWAZO ,........mawazo yao yanakufikia wakati yameshavalishwa CHUPI,...... na yangekufikia  HAYO MAWAZO wakati yako UCHI kama walivyo UCHI,......... labda ungetafuta MWAVULI kujikinga ili usinyeshewe MAVI hata KIMAWAZO!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
    JUMAPILI NJEMA MKUU!



    Hebu Chaka Demus na Pliers waanzishe zaidi kwa-Gal wine




    Chaka Demus , Pliers na Jack Radics waingizie pia kamanyola bila jasho ile -Twist and SHout




    Halafu ghafla BUJU BANTON aingilie kati kwa-HUSH baby HUSH




    SHABBA RANKS ajaribu kuzima kwa tusi-Wicked in a bed




    Ila INNER CIRCLE ndio wazime tena kwa- SWEAT
  • Kabla HUJAONDOKA,....

    Posted: January 28, 2012, 3:57 pm by SIMON KITURURU
    ..... LABDA kuna MAHALI unaelekea TAYARI,......... hata kama unafikiria umekaa tu KITAKO kwenye eneo ulokalia HATA KAMA ni lile  uliitalo KIGODA.
    Swali:
    • Unabisha?

    Ndio,......... na KIMAWAZO,.........labda hata sasa hivi HAUKO ulipo hapohapo udhaniapo ndipo ULIPO!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


    Hebu tupate TUKUNYEMA kutoka kwa EDDY GRANT katika -WAR PARTY




    EDDY GRANT arudishe ile tukunyema-Walking On Sunshine





    EDDY GRANT arudie na tukunyema-HELLO AFRICA


    Adinye kiduchu tena -Gimme HOPE Joanna
    EDDY GRANT atungunyue kiduchu pana zaidi ile tukunyema-Killer on the RAMPAGE


    Halafu azime kwa-Living on the FRONTLINE

  • ....labda MTU hawezi kusema kaona aibu ya kuchungulia kabla ya KUCHUNGULIA!

    Posted: January 28, 2012, 12:32 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,......... na labda AIBU za MTU ,........ ni MATUNDA na FUNUNU za VIJULIKANAVYO vidude kwa MTU,....... na aoneacho aibu mtu ,...
    .... kwenye hicho LABDA kuna kitu ANAJUA kimfanyacho aone aibu.


    Swali:
    • AU?

    Ndio,........ labda UKIONEACHO aibu,....... umekiona hicho hata kwa kukichungulia!
    Swali la kizushi:
    • Unafikiri VIPOFU hawana aibu?
    • Na unafikiri VIPOFU hawaoni hata kwa jicho la ndani?
    Ndio,......na KIPOFU huchungulia pia ,.........kama ukiangalia kiundani!
    Ni wazo tu hili MKUU!
    Jumamosi Njema MKUU!

     Hebu Nit Doff aingilie kati kwa - Sunugal



    Halafu Kool & The Gang waingilie kati na kurudisha -Fresh



    Halafu Kool & The Gang wazime kwa -Hi De Hi Hi De Ho

  • Kwa kuwa ETI kunawadhaniao hakuna JINSI ya kuutafutia UTAMU jina JIPYA!

    Posted: January 27, 2012, 9:04 pm by SIMON KITURURU
    LAKINI,...
    ..... tokea enzi za kale LABDA,....
    ..... utamu ni uleule ila ni MAJINA tu unapewa MAPYA!

    Swali
    • Si wajua CHACHU , chungu, tofauti ya utamu wa uke na kachumbari, tamu kama WAZO LA  ngono .... au tu tamutamu kama sukari -ilikuwepo tu tokea enzi na LABDA ni majina TU inapachikwa tu ili JUMA na ROZA waelewane wanaongelea PILIPILI au BAMIA kiutamu katika hoja za KITUMBUA?

    Ndio,...
    .....ni wazo tu hili NGULI!
    Ijumaa na WIKIENDI NJEMA Bingwa!


    Hebu La Chepuya waingilie kati kwa - Checo Acosta


    UB40 wajaribu kupunguza spidi kwa kulalamikia ya PANYA FULANI katika -Rat in mi Kitchen




    Halafu BUSTA a busti kwa kuzima katika -HATARI

  • Wakati bado TUNAPENDA yale MAJIBU tuyapendayo!

    Posted: January 26, 2012, 10:27 pm by SIMON KITURURU
    Ndio unaweza kubisha,....... LAKINI,...
    ... labda ni kweli WATU WENGI hata UWAJUAYO hawapendi MAJIBU TU,...
    ... ila KIPENZI  ``KIJIBU ´´ kwao ni MAJIBU wasiyoyajua,...... na  ila MAJIBU ni  yale AMBAYO  yanaegemea kwa wayaaminiyo ndiyo MAJIBU  HAAAASAAAA kistaili ya WAAMINIVYO,....... kitu kifanyacho  katika ukweli wa ni nani kiudaku ni CHANGUDOA  waaminio hata KIHISIA TU  kabla  ,....
    .....kuwa ni CHANGUDOA,...
    .....watafurahia au hata kukubaliana nawe KIRAHISI ni CHANGUDOA hata kama hakuna USHAHIDI yule umsemaye ni kweli ni  CHANGUDOA  ambaye tayari wanahisi ni CHANGUDOA.
    Swali:
    • SI ni kweli hata kama majibu ni ya kihisia tu na hatuna uhakika kiushahidi au KISAYANSI- majibu yakaayo KIKRISTO yanaweza furahisha kama sio kukubalika na WAKRISTO kama tu yale MAJIBU ya KIISLAMU yawezavyo kukubalika na WAISLAMU kama sio kuwafurahisha  hata kama hayana UTHIBITISHO?

    Ndio,...
    ...labda TUNAPENDA majibu tuyapendayo,...
    .. na kwa MLEVI majibu yafagiliayo ULEVI hunoga zaidi kuliko yale yaonao WALEVI kuwa mambo zao DUKINAA tu!:-(
    Swali kiaina:
    • Hivi enyi wachawi WA  TANZANIA mbona Hamsifiwi wakati fani yenu  ya KICHAWI ni imara tu tokea enzi za mababu  TANZANIA na wengi wenu HAMJITOKEZI kunenepea fani yenu ilivyo nene TANZANIA mpaka muwe mnaumiza tu?
    • Halo MCHAWI hivi kweni MAZERUZERU mnawafanyia nini kikweli?
    Ndio,...
    ... jibu la nililouliza hapo juu naweza KUOGOPA JIBU,...
    ... ila NIMEULIZA!:-(

    Ndio,...... ni wazo tu hili MHESHIMIWA Kibanangenge!PAMOJA SANA BANDUGU BAPENDWA!

    Hebu tubadili kidude kwa msaada wa Bi KIDUDE kwa kuanzisha upya kwa -KIJITI



    Bi KIDUDE azime tena kwa-AHMADA
  • Stori za MTOTO Mzuri avutiaye KWA MBALI kwenye BAA kabla HUJAONGEANAYE!

    Posted: January 26, 2012, 9:54 pm by SIMON KITURURU
    Kuna MTOTO MZURI kwenye baa ambaye anavutia kabla hujaongea naye hata KITAFSIDA!Ila kuna MAMBO labda ongea na mtu NA utasahau mwanzo mapaja, KIFUA CHAKE KAMA SIMBA au sura yake ilikuwa ndiyo SUMAKU kimvuto ili uongee naye hata kuomba ambayo kimajina ni mazuri hasa bila kuya ita- KITAFSIDA!
    Swali:
    • Kwani hujastukia kwa mbali MVUTO unaweza kuuawa  na kusikiliza AVUTIAYE anaongea NINI baada ya kumsogelea?
    • Na si ushastukia saa nyingine  ni MIAKILI au TABIA zijitokezazo kwenye UONGEAYENAYE na wala SIO kwenye ndoto za utakaye kuongea naye - ndizo huua MVUTO wa MTOTO MZURI yule kwa nje anakalio kama malaika au MHESHIMIWA ambaye akifunga mdomo unakuwa unauhakika anamiakili na masuluhisho kuliko BULICHEKA na suluhisho la kujenga NYUMBA juu ya MTI?


    Ndio,...... fantansi zako hata za Rais KIKWETE  wa jamuhuri wa muungano wa TANZANIA labda zinamvuto zaidi kabla HUJAMSIKILIZA ,....
    .....na ukimsikiliza ASKOFU TUTU kama tu BABU wa LOLIONDO na SHEKHE YAHYA waweza kuhitimisha labda SURA ni NZURI kuliko waongeleayo!
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!Siku NJEMA!

    Hebu OffSide Trick na Baby J warudishe tena kidude- Kidudu Mtu



    OFFSIDE TRICK waongezee kipele-FATAKI



    OFFSIDE TRICK waongezee SHUGHULI kwa-Samaki





    Halafu hebu OFFSIDE TRICK na Mzee Yusuph wazime tena kwa jipu lawalawa-BATA



  • Katika TASNIA ya KIFICHO ile ya MHESHIMIWA kuonea aibu anachowaza HADHARANI!

    Posted: January 26, 2012, 9:48 pm by SIMON KITURURU
    Kuna tasnia ya AIBU,...
    ....NA LABDA ILE AIBU ya kuonea aibu hata UNACHOWAZA,....
    .....kisijulikane  unakiwaza HADHARANI bila sababu MAALUMU!:-(
    Swali:
    • AU?

    Ndio,.......na LABDA KUNA KITU katika  yasemekanayo HATA katika  kila KITU,....... kama katika ya kila KITU,........ inahitajika kukisema katika HADHARA  fulani hata kama HADHARA yako ni BAFUNI wakati unaoga na UKO PEKE YAKO kisa unakionea aibu ingawa wakati huo hicho ndicho KILA KITU!:-(

    Swali:
    • AU?
    • Kwani haujui kikusumbuacho rohoni moja ya dawa ni kukitamka?
    Na kama unajiheshimu na utakacho ni kutosikika katika ambacho wakati huo kiumuhimu ndicho kila kitu kwako,...
    ....labda BAFUNI  ukiwa peke yako ni MUHADHARA,...
    .... na peke yako kwenye kelele za maji SEMA KWA SAUTI utoe DUNGUDUNGUDUNGUNYIKO ROHONI  kwa kuwa hapo bafuni ni HADHARA yako ya kuongelea ambacho bado huna nguvu yakuongelea hadharani katika hata swala la kwanini chupi yako na sio MAWAZO YAKO ,.......ghafla NDIO  inachafuka zaidi NANIHII kuliko zamani INGAWA bado wataka hiyo iwe siri yako kwa watu walio HADHARANI kwenye wambea, WAZAZI uwaheshimuo mpaka kwa mpenzi wako kibogoyo bado wadhani ni busara iwe SIRI kwa siri ili utunze woga wako uliouzoea wakutotaka kuchafua NANIHII!:-(

    Swali:
    • Unabisha?
    • Na si unajua kuchafua hata hali ya hewa kimawazo au kiushuzi  maranyingi ni tatizo kubwa kisaikolojia kwa alipaye uzito chafuo hasa kwa kuwa kwa wengine labda wala sio CHAFUO?

    Ndio,...
    .... LABDA kuna tasnia za watu zilengazo ya KUONEA AIBU WATU ambayo usipoona aibu utatia AIBU kisa maswala tu ambayo JAMII imejijengea mpaka YAFANYA WANAJAMII BAADHI WALIO WENGI wanawazo MPAKA  la kuficha ndani ya CHUPI YA MAWAZO yale MAWAZO yahitajikayo kuwa UCHI HADHARANI katika jamii,....

    .... kwa kuwa ETI labda TU labda visivyosemwa HADHARANI ili MHUSIKA ATUNZE ADHANIAVYO NI HESHIMA hadharani,.........na labda ndio MAANA kuna watu wanaendelea KUFA BILA SABABU SASA HIVI PIA kisa WAVIJUAVYO WANAAIBU navyo  HADHARANI na wanajiheshimu navyo ambavyo visingewaua ila wanavionea AIBU ,...
    ....ila VYAWAUA  kwa kuwa WAHESHIMIWA  wale WAATHIRIKA wawaheshimuo ,...
    .....kwa matendo yao yametabiri YASIYOHESHIMIKA ni NINI- na yawafanya WAATHIRIKA wajisikie AIBU mpaka KUFA kwa yatibikayo kisa WANATAKA waheshimike KATIKA JAMII YA wawaheshimuo!:-(

    Ni wazo tu hili NGULI!Siku Njema Mkuu!
    Hebu Al Green abadili tena kwa KURUDISHA old schooL soul ile-Tired Of Being Alone




    Al Green aongezee ndude-Love and Happiness




    Halafu Aretha Franklin aongezee dozi kwa -Chains of FOOLS


    Aretha Franklin alainishe kwa makali-Respect


    Ila tu hebu SHAGGY , RIHANNA na Mr BEAN wajaribukuzima kwa -Bombastic



    Au tu SHAGGY mwenyewe ndiye azime kwa-Boombastic




  • Etta James!

    Posted: January 24, 2012, 7:12 pm by SIMON KITURURU
    Nimechelewa kidogo kukuaga rasmi!R.I.P Miss James! !
    Jamesetta Hawkins a.ka Etta James (January 25 1938-January 20 2012)



    Bado nasikiliza kazi zako MISS kama hii-AT LAST
  • Eti kisa ni kwamba KACHUMBARI huwa haisifiwi kuwa ni CHAKULA!

    Posted: January 24, 2012, 4:19 am by SIMON KITURURU
    KACHUMBARI ni CHAKULA,....... ingawa bado kuna wadaio  kama KILIWACHO  sio UGALI kwa kuwa ni WALI basi kiliwacho sio CHAKULA na alaye anapasha tu moto kabla hakijaletwa cha kikweli CHAKULA..


    LAKINI  ukikaa mkao wa kuchukulia KACHUMBARI kama CHAKULA,...
    .... kachumbari hushibisha  tu pekee hata bila chipsi dume au chipsi mayayi ambayo  kwa wengine ni kifungua kinywa tu  au  kionjo tu cha barabarani kabla hujaenda nyumbani  kwenye FULU KUBUGIA NANIHII kwa watazamavyo baadhi CHAKULA.
    Swali:
    • Si umestukia SHUKA ni nguo yakutosha  hata bila chupi kama ukiliangalia kimtazamo wa KILUBEGA Kimasai?
    • Kwani kwako chenye sifa fulanifulani hakiathiri ukipavyo sifa FULANIFULANI? 
    • Unafikiri KACHUMBARI PEKEE haishibishi?

     Ndio LABDA,.......ukigeuza mtazamo  ,.........KACHUMBARI ni chakula tosha TU hata kama hiyo sio SIFA YAKE ,........ na hata kama kachumbari yenyewe tuongeleayo hapa NI baiskeli  katika ya wafikiriao usafiri lazima iwe ni wa GARI na yabaiskeli hayaitwi SAFARI!


    Ni wazo tu hili kinanihii MHESHIMIWA!Jumanne NJEMA sana MKUU!

    Hebu UB 40 waingilie kati kwa - Please Don't Make Me Cry



    UB40 waongezee dozi kwa -The Way You Do The Things You Do



    Halafu hawahawa UB 40 wazime kwa -Here I am Baby





    Juzijuzi niliwadaka UB40 wakiwa live kama katika baadhi ya picha za juzijuzi zifuatazo...







  • Jinsi ya kuanza KUKALISHA Mawazo sio KIBIBLIA!

    Posted: January 23, 2012, 10:19 am by SIMON KITURURU

    Kuna MKAO fulani MAWAZO yako yamekaa,...... hata kama hayajakaa KIPAGANI au KIKURUANI!

    Swali:
    • AU?
    • Si yasemekana kunawasahauo kuwa mawazo yao labda yameegemea MRENGO fulani?

    Ndio,....... labda kukalisha MAWAZO ni jambo MTU ajifunzalo tu,......... na kuna uwezekano MAWAZO ya mtu hata yale yasiyokaa KIKURUANI au KISABATO bado yamekaa tu MKAO fulani ambao LABDA   ni wa KIVYAKOVYAKO!


    Ndio,... ... ni WAZO tu hili MHESHIMIWA!Jumatatu NJEMA Mwayego!

    Hebu Mighty SHADOW arudishe makalipso katika -Universal Language



    Mighty Shadow aongezee-I wish






    The Mighty Shadow atekenye pia - Doh Mix Meh Up


    Halafu ghafla Mrisho Mpoto na Maunda waturudishe Tanzania kwa pini - Samahani Wanangu


  • NI rahisi KUJENGEA MIPAKA uyajuayo kama tu UWAJUAO ingawa labda uhitajiyo ni yale USIYOJUA na wale USIOWAJUA!

    Posted: January 22, 2012, 12:35 pm by SIMON KITURURU




    Na siye TUSIOFITI kwenye UYAJUAYO na UWAJUAO,....... labda  usipoangalia  waweza kufikiri kwenye MAISHA yako UNATURUKA.
    Ila tusiofiti na YASIYOFITI kwenye ULIMWENGUWAKO,...... yapo tu AISEE na labda tuna na YANAKUGUSA hata kiusivyotegemea,.....
    ....ingawa hutustukiii hata katika tukojoayo pembeni ya BARABARA hadharani.:-(

    Swali:
    • SI unakumbuka YAKO na YA DUNIA YAKO labda bado nni nukta tu hata katika INSHA ya ULIMWENGU wako?


    Ndio,...
    ... YAKO  hata tukiyajumlisha na YANGU YOTE,...
    .... labda kihesabu bado sio YOTE!
    Na ni wazo tu hili MKUU!
    Hebu turudi ANGOLA ili David Zé aanzishe upya kipengele kwa - Mwangolé(O guerrilheiro)






    David Zé aongezee dozi kwa -Undenge Uami

    '
    Tuhame kidogo kwa msaada wa Stephen Marley katika kitekenyeo - Made In Africa




    Halafu hebu Damian Marley na Nas wazime kwa kuchezea wimbo wa DAVID Zé katika -Friends

  • UPOLE!

    Posted: January 22, 2012, 11:12 am by SIMON KITURURU
    UPOLE  labda ni ni SANAA tu ya kuficha HASIRA au tu HAMAKI!
    Swali:
    • AU?
    Ndio,...
    ...LABDA upole wa MTU ni tafsiri yako tu!


    Ni wazo tu hili BINGWA!Jumapili njema MHESHIMIWA!
    Hebu KASSAV waingilie kati tena kwa -Ave'w Doudou


    Halafu Ambelique azime kwa - New Sheriff In Town



Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs