SIMON KITURURU- MAWAZONI
-
Kijiwe kiko PUMZIKONI,...
Posted: November 28, 2011, 10:04 am by SIMON KITURURU
-
TANZIA
Posted: November 27, 2011, 11:57 am by SIMON KITURURU
FAMILIA YA MWAKIPUNDA WA NGAMANGA IPINDA KYELA MKOANI MBEYA WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MPENDWA WAO ANNEL MWAKIPUNDA MWAISUMO KILICHOTOKEA TAREHE 26/11/2011 DAR ES SALAAM. MAZIKO YATAFANYIKA MOROGORO TAREHE 28/11/2011.
HABARI ZIWAFIKIE FAMILIA YA MWAKIPUNDA,FAMILIA YA MWAISUMO,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI POPOTE WALIPO.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE NA MILELE
AMEN -
Haya tena:Jesus was a Buddhist Monk( BBC Documentary )
Posted: November 26, 2011, 8:15 pm by SIMON KITURURU
-
VIVA KAMANDA LOWASSA
Posted: November 26, 2011, 4:17 pm by SIMON KITURURU
LOWASSA KUANZA KUANIKA UKWELI KUHUSU RICHMOND KWA KWELI NAONA ANAFANYA KILE NILICHOWAHI KUTABIRI KWENYE MAKALA YANGU YA "LOWASSA SEMA NENO MOJA TU"
...NIMEAMUA KUMTUNGIA SHAIRI HILO HAPO CHINI...
Kalamu yangu nashika, shairi nakutungiaKamanda umeongea, kiwingu umeondoaHukutaka kusinzia,makosa kuyarudiaJibu umetupatia, viva kamanda Lowassa
Mwananchi nimesoma, la jana nilinunuaMachoya yakatuama, dukuduku umetoaUliyosema Dodoma, Kwakweli yanavutiaJibu umetupatia, viva kamanda Lowassa
Richmond kupasua, mapema uligunduaKikwete ukamwambia, mkataba kuondoaRais akakataa, nini alitegemea?Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa
Nape akashikilia, lile asilolijuaMikoani kaambaa, uzushi kang’ang’aniaJinalo kulichafua, wewe ukavumiliaJibu umetupatia, viva kamanda Lowassa
Mapema nilitabiri, falsafa nikapingaMagamba sikukariri, kuvuana sikuungaUkweli niliukiri, mantiki iso kungaJibu umetupatia, viva kamanda Lowassa
Beti sita nakomea, kalamu naweka chiniMengi nimeongelea, soma tena kwa makiniYatazidi kutokea,kusini kaskaziniJibu umetupatia, viva kamanda Lowassa.
Shairi limetungwa na Nova Kambota Mwanaharakati,+255717 709618novakambota@gmail.comwww.novakambota.comTanzania, East AfricaJumamosi, November 26, 2011
Nimetumiwa hii nanihii na:Nova Kambota -
Kama NCHI iumwayo inahitaji TIBA ya haraka , labda DEMOKRASIA sio DAWA .
Posted: November 26, 2011, 3:22 pm by SIMON KITURURU
Mifumo ya KIDEMOKRASIA inakamchezo ka KUCHELEWESHA mgonjwa kupewa DAWA hata ijulikanayo kuwa inatibu GONJWA,...
... kisa DEMOKRASIA inafanya WATU hata WASIOJUA KINACHOENDELEA kuruhusiwa KULUMBANA hata kuhusu dawa wasizozijua wakati mgonjwa anaendelea kuugua ,......kisa KIDEMOKRASIA kila KIMBULUKUTU inabidi KISIKILIZWE ili iaminike hata dawa sahihi aijuaye ni MTU MMOJA imeamuliwa na WENGI.
Swali:- SI unakumbuka WENGI WAPE lakini kama wengi watakacho kupewa kinavimavimavi bado MMOJA ajuaye hao wengi wanakosea bado ndio MWENYE dawa sahihi hasa kama vimavimavi sio sahihi hata kwa hao wengi waliochagua bila KUJUA wanachagua nini?
NI wazo tu hili MKUU!Hebu tupumzike kiwazo zaidi kwa kudeku...
China's Capitalist Revolution - BBC (6.2009)
http://www.bbc.co.uk/programmes/b00lfcz6
Producer: Robert Coldstream
Executive Producer: Nick Fraser.
Aired: June 20, 2009, July 25, 2009 -
Twanga Pepeta wavamia jiji la London
Posted: November 26, 2011, 12:15 pm by SIMON KITURURU
[www.youtube.com]
Bendi ya Twanga Pepeta imewasili leo mjini london tayari kwa makamuzi katika
ukumbi wa Silver Spoon London kwa ajili ya Kuadhimisha miaka 50 ya
uhuru wa wa Tanganyika. Usikose show hii ya Ukweli
Asanteni,
Urban Pulse Creative
Nimetumiwa na:Frank Eyembe wa Urban Pulse -
Leo katika Mtonesho: CHINA ndani ya Bongo / AFRIKA/The Chinese Are Coming
Posted: November 26, 2011, 10:05 am by SIMON KITURURU
China's Investments in Africa
BBC Documentary - The Chinese Are Coming
Hebu tudeku mahali pengine ambako sio AFRIKA kwa kina WAZUNGU OBAMA katika kidude:The CHINESE are not COMING, They are ALREADY here
Ni MTONESHO tu huu MKUU! -
Ya DUNIA: Mwanamke ampika MUMEWAKE!
Posted: November 25, 2011, 10:55 pm by SIMON KITURURU
Haya DEKU mwenyewe stori,...
-
Kikuchekeshacho chakuchekesha kwa kuwa kuna kitu katika hicho unajua Mshikaji!
Posted: November 25, 2011, 1:20 pm by SIMON KITURURU
Na vichekesho kwa kawaida havina maana ,....... kama havibebi unalojua Mshikaji!
Swali:- Mshikaji si unakumbuka lakini kuwa huhitaji kujua kikulizacho ili ulie?
Ni hilo tu MSHIKAJI!Na Ijumaa na WIKIENDI njema MSHIKAJI!
Hebu BARON aturudishe Trinidad & Tobago katika-Somebody
Eddy Grant aturudishe Guyana tena kwa SUGAR BUM BUM
Halafu azime tena kwa -Hello AFRIKA
-
Watanzania wawili kucheza ligi daraja la pili Sweden
Posted: November 25, 2011, 12:13 pm by SIMON KITURURU
William John Joseph Kaniki (Golota)
Wachezaji wawili wa kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) na William John wamefanikiwa kujiunga na timu ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio( Trials). Majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya thelathini ambapo wachezaji watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF)
Habari hii imeletwa kwenu na:http://www.africa4life.com/
Nimetumiwa na:Nancy Mtunga -
Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone Awarusha Wakaazi wa DMV
Posted: November 25, 2011, 10:57 am by SIMON KITURURU
Mwana muziki wa kizazi kimpya ndani ya Washington DC, AJ Ubao wa kwanza (kushoto) pamoja mzee wa kuwachanganya Dmk global Dickson Mkama. wa kwanza( kulia) wakiwanyumba ya jukwa na mwana muzingi aliekuwa anasubiriwa kwa hamu siku ya jana Jumatano Nov23, 2011 katika sherehe za Thanksgiving Muimba Jose Chameleone katikatia, akisubiriwa kwa hamu na wapenzi wakeNyuma ya jukwa mwana dada Luren akipata flash ya pikee kabla ya unyesho kuanzaaMuimbaji Ana Lov akipata flash ya pamoja na rafiki yake kwenye onesho hilo la Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone.Cheif wa swahilivilla Abou Shatry akipata picha ya pamoja na kundi zima la muimbaji kutoka Uganda Jose Chameleone.Aj Ubao alikuwa ni mumbaji wa pili kuimba katika onyesho hilo waliosherikiana na mwanamuziki wa kutoka Uganda Jose Chameleone, wakiwa nyuma ya jukwa akipata flash ya pamoja na mdhamin wake wapendoWapenzi wa tazamaji wakisubiri kwa hamu onyesho hilo kuazarasmi ndani ya ukumbi wa Rendezvous mitaa ya Parklawn Dr, Rockville Maryland U.SMwana muziki wa kizazi kimpya kwa muziki wa R&B ndani ya Washington DC, AJ Ubao akiwarusha vibaya sana wapenzi wa muziki wa nyumbani wanaoishi hapa DMV Jana jumatano Nov 23, 2011 Nchini Marekani. Wapenzi wa muziki wakinyumbani wakiwa wanamshangaa Msanii wa hapa Washington DC, AJ UbaoMwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone akifanya vituz vyake ndani ya Rendezvous Hall mitaa ya Parklawn Dr, Rockville Maryland U.SMamia ya watu jana walifurika kuja kumuangali Msanii kutoka Nchini Uganda kwa jina maarufu la Jose Chameleone, ana nyimba zake, ikiwemo mama roda, Jamalila analia, na nyingi nyenginezo.Mamia ya warembo waliohudhuria kwenye Show hiyo ya Mwanamuziki wa Uganda Jose ChameleoneWarembo mikono juu wakiwa wamevudiwa na uwimbaji wa mwanamuziki huyo ndani ya ukumbi uliofurika warembo wa Kiafrica.Juu na chini full warembo wakipata hisia za muziki wa muimbaji maarefu kutoka nchini Uganda Jose Chameleone. Sauti ya muimbaji Jose Chameleone inayofurahisha warembo wamuziki wa kinyumbaniKama kawaida yake akiwa na kundizima ndani ya Washington DC Jana Jumatano Nov 23,2011Wakati mwengine warembo hupandwa na jazbaba wale wanaposhindwa kujizuwia na kuomba mic ili kuchombeza wimbo uliokuwa unaimbwa hewani wa kipepo Mambo ya jana hayo cheza ni kucheze ndani ya Rendezvous HallMapozi na wewe: mrembo akipata picha kutoka kwa mpiga picha wetuHivyo ndiovyo ilivyoo hakuna fitinaCheza nikucheze juu na chini warembo wa Kiganda ndani ya Nyumba Mrembo aleehudhuria ndani ya unyesho hilo kabambe la Muimbaji Kutoka Nchini Uganda Jose ChameleoneKwakweli ilikuwa sho ya aina yake wapenzi wengi ambao ni Waganda aliofurika na kumuunga mkono jamaa yaoMwana mitindo wa Uganda jina lake hatujaweza kulipata vyema lakini ni Mwanamitindo wa Uganda!Cheza ni kuche hiyo huku warembo wakipata flashi ya pamoja kwenye show hiyo ya Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone Alivyo warusha Wakaazi wa DMV Jana Nov 23, 2011 kwenye siku kuu ya Thanksgiving Nchini Marekani. Picha zote na [swahilivilla.blogspot.com]
Nimetumiwa hii na:Juma Issa -
Twanga Pepeta Wakamata Pipa
Posted: November 25, 2011, 10:13 am by SIMON KITURURU
Bendi ya Twanga Pepeta wakijiandaa kuingia kwenye PipaChalz baba akiwa tayari kuingia kwenye PipaFull Mzukakikosi cha Twanga kikijiaandaa kuingia Katika Uwanja wa Julius NyerereKutoka Kulia Amigolous akiwapa Mikoba Jojoo, Jumanne, Baby Tall na Luizakutoka kushoto Shalapova, Charles Baba na ShakashiaMaria Soloma akiwaaga mashabiki wake NyumbaniVictor Mkambi mpiga kinanda wa Twanga akiwa na Maria Soloma ambae ni dancer wa twanga
Salam,
Twanga Pepeta ''KISIMA CHA BURUDANI'' wameondoka leo asubuhi kutoka uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea kuvinjari katika Jiji la London ili kusugua kisigino na wapenzi wao walioko nchini Uingereza na nchi jirani ikiwa ni katika kusherehekea maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Kundi hilo lililokamilika katika safu zake za waimbaji, wapiga vyombo na wacheza show linatarajiwa kuwasha moto wa burudani yao siku ya Jumamosi, tarehe 26 Novemba 2011 katika Ukumbi wa Club 2000 Savoir Banqueting Suite, Popin Building Southway, Wembley HA9 0HB kuanzia saa Tatu Kamili Usiku mpaka alfajiri (9pm til late).Mheshimiwa Balozi Peter Kalaghe atakuwa mgeni rasmi. CD za album mpya na za zamani zitauzwa na vinywaji pamoja na vyakula vya kitanzania vitakuwepo vya kumwaga. Viingilio vitakuwa £20 (singles) na £35 (couples) kabla ya saa sita (mid night) na £25 (singles) na £40 (couples) baada ya saa sita usiku.
Njoo tujumuike, njoo usugue kisigino, njoo usherehekee uhuru wa nchi yako, njoo ule na kunywa kitanzania. Burudani ni watu na watu ni pamoja na wewe. Tanzania itajengwa na watu wenye moyo kama wewe. Karibuni sana.
Shughuli hii imeandaliwa na Urban Pulse Creative wakishirikiana na Miss Jestina Blog, chini ya maelekezo thabiti ya Ubalozi wa Tanzania, London. Tumethubutu, Tumeweza na Tunaendelea Mbele
Nimetumiwa na :Frank Eyembe -
Katika KUMBUKUMBU:George Washington Carver
Posted: November 24, 2011, 7:00 pm by SIMON KITURURU
-
ASANTE KOTOKO in DAR
Posted: November 24, 2011, 5:48 pm by SIMON KITURURU
TIMU ya soka ya KUMASI Asante kotoko ya Ghana inatarajiwa kuwasili nchini Desemba 9 tayari kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya kombaini ya timu za Yanga na Simba siku ya Desemba 11 kwenye uwanja wa Taifa.Mchezo huo ni sehemu ya kukamilisha maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Future Century Limited, Helen Masanja.Masanja alisema kuwa timu hiyo itafikia Zanzibar na baadaye kuja jijini Dar es Salaam kwenye hotel ya Lamada tayari kwa mchezo huo ambao umedhaminiwa na PPF, Kenya Airways, Vanedrick Tanzania Limited, Lamada Hotel na Vanne Fashion Tabata. Alisema kuwa wanatarajia kuwa na burudani ya aina yake kwani tayari kombaini ya timu ya Yanga na Simba itaundwa na wachezaji nyota wanaocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.Aliongeza kuwa makocha wawili, mkongwe, Abdallah “King Mputa” Kibaden na Fred “ Minziro” Felix ndiyo watakuwa wakuu wa benchi la ufundi la timu hiyo ambayo itaundwa na wachezaji 20 watakaotangazwa hapo baadaye. Wengine katika benchi la ufundi na meneja, Boniface Pawasa na daktari wa timu, Juma Sufiani.Alifafanua kuwa uteuzi wa timu hiyo hautajali uraia wa wachezaji hivyo kama wachezaji kutoka nchi za nje ambao wanachezea timu hizo watateuliwa, basi watacheza mchezo huo.Masanja alisema kuwa Yanga na Simba zimekubaliana na kuweka historia kwa mara ya kwanza tangu timu hizo zitengane mwaka 1935. Alisema kuwa historia inaonyesha kuwa timu hizo zilikuwa pamoja kuanzia mwa 1922.Mwenyekiti wa Yanga Lyod Nchunga alisema kuwa mechi hiyo itaondoa tofauti iliyopo baina ya mashabiki wa Simba na wale wa Yanga hasa zinapotokea timu hizo zinacheza mechi za kimataifa ambapo imekuwa ni kawaida mashabiki wa timu hizo kushangilia timu pinzania.Wakati Nchunga akisema hayo, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kuwa muungano huo utaleta tija kwa timu hizo ambapo mashabiki wa Simba na Yanga siku hiyo watakuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuishangilia timu yao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.Alisema kuwa huu ndiyo mwanzo wa kuanza kushirikiana katika mechi za kimataifa na kuwataka mashabiki kufika kwa wingi na kutoa sapoti kubwa kwao.
Nimetumiwa taarifa na:Shaffi Dauda -
Kwani MTANDAONI unastukiaje ANONYMOUS ni MWANAMKE au MWANAUME kimaandishi yake TU?
Posted: November 24, 2011, 12:45 pm by SIMON KITURURU
Najiuliza tu baada ya kukutana na baadhi ya WADAU WAWILI JANA ambao mtandaoni nilikuwa nadhani ni WANAUME ,....
.... na kumbe ni vigoli bomba tu!(Msinitusi kama mwanisomalakini leo)
Na katika kuongeanao tukatofautiana kidogo kuhusu EMU THREE ,...
....wa DIARY YANGU
... wao wanadai ni demu na mimi tokea enzi hana BLOGU yake na nakutana na comment zake kwa DINAHICIOUS wa MAHABA HUKU,...
... kuwa huyu NGULI ambaye nakiri simjui jina lake halisi ni DUME.
Kwa M3:
Ambiere M3 EEEH!,.....jana kuna katopiki ambako kamefanya nipende zaidi staili yako kwani mpaka leo niwafahamuo kila mtu anauhakika kivyake TOFAUTI kuwa wewe ni JINSIA GANI.
Ila mie niko pale pale kuwa weye ni (kwa kipare)MGHOTHI aithee!
Tukiachana na hilo:- Wewe unastukiaje JINSIA ya mwandishi asiye jitambulisha mtandaoni?
- Na kwani ni lazima kujua MWANDISHI KIJINSIA ni yule akojoaye kirahisi kasimama au ni yule achuchumaye kiusataarabu ili kukojoa kirahisi ili kulenga shimo la choo cha shimo wakati MADA iongelewayo labda haina uhusiano na jinsi ya kukaa kistaarabu kwa aliyevaa sketi fupi kwa kuwa ni ile ya hivi DAR -ES- SALAAM ile posta mpya itaitwa POSTA mpya mpaka LINI wakati labda wala sio MPYA tena siku hizi?
Ni MTONESHO tu huu MHESHIMIWA na usikonde!
Hebu Kleptomaniacs watunishe- Tuendelee
Mashifta warudishe - System ya Majambazi
Mashifta waongezee-Pesa ,Pombe, SIASA na Wanawake
Halafu LONGOMBAS wazime kwa kukumbusha-Vuta pumzi
-
Labda wenzetu WAZURI na wale wenye MIAKILI SANA watuachie kwanza siye wengine NDIO tuwastukie kwanza kuwa wao ni WAZURI au ndio WENYE MIAKILI sana!
Posted: November 24, 2011, 11:17 am by SIMON KITURURU
YATUMIAYO AKILI SANA ,...........labda ni YA KAWAIDA kwa MWENYE akili,.......a.k.a yatumiayo akili sana KWAKE ni kawaida !
Na kwa isemekanaye ni MZURI SANA,... ... labda yatakiwa UZURI wake uwe kwake ni KAWAIDA kwa kuwa umemng'ang'ania na kwake huo sio kitu cha kutia akili,...
....a.k.a UZURI kaumbwanao kwa hiyo huo kwake ni KAWAIDA.
Swali:- AU?
NDIO,...
... labda kustukia yatumiayo sana AKILI,...
... labda hiyo ni shughuli ya WENGINE ambao hustukia nani ni mwenye AKILI,...
... kama labda kama MTU ni MZURI labda hiyo ni shughuli ya wengine wastukio kwanza !
LAKINI:- Si labda mtu akisubiria WENGINE , wengine wanaweza wasistukie anamiakili na pia haki yanani labda ni kweli yeye ni mzuri kweli hata bila nguo kitu ambacho JAMII kwa jamii IJIFUNDISHAYO miakili na UZURI wake unaweza USITAMBULIWE?:-(
Ndio,..... kuna WENYE akili wajijuao wanamiakili WASIOTAMBULIKA na JAMII kwa kuwa jamii inakipimo tofauti cha nini AKILI SANA na usipopasi mtihani wa jamii basi weye hutambuliki,...
... kama tu ijulikanavyo kuwa JAMII ikijifunza kupenda wenye tako lililopigwa pasi WAZURI wenye tako kubwa huondoka kwenye kipimo cha wazuri katika jamii kisa tako kubwa na matege kwa mbaaaaali!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu DIDO aingilie kati na kulainisha kwa-THANK YOU
Ghafla Youssou Ndour aingilie kati kwa-Medina
Halafu Youssou N'dour azime kwa -Africa, Dream Again
-
Kuna wadhaniao UJINGA KISIRI CHOBISI unanafuu kuliko UJINGA HADHARANI kwenye UMMA!
Posted: November 24, 2011, 10:00 am by SIMON KITURURU
Lakini,........ labda MJINGA,....... ni MJINGA tu kama kitafsiri za wadaio kuna BINADAMU mwenye pumba za KIJINGA,...... hata kama ujinga wake MHESHIMIWA kafanya SIRI.
Swali:- Kwani KUHUSU YA SIRI-unafikiri HATA kwa kuficha HATA nyege KISIRI inamaana mwenye nyege hana NYEGE kisa anazificha na hiyo nni SIRI?
Na ndio ,........ hata kwa KISIRI,.......... labda kifanyacho MTU hufanya hicho ni SIRI,....... ni kwa kuwa UKWELI NI KWAMBA jambo lifanywalo siri hilo SIO SIRI na lipo PALEPALE na ndio maana mwangalifu katika kumdeku mficha SIRI ,...
...yasemekana jinsi MTU afichavyo siri ndio KIFICHUA SIRI.:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu MCHUNGAJI Solomon MUKUBWA abadili wazo na kurudisha hali ya hewa laini kwa watu baadhi kwa kudinya pini la kikristo lile-Mfalme Wa Amani
Halafu Zain Bhikha aingilie kati mchezo kwa - Give Thanks to Allah
-
...ndio HERUFI hujenga NENO na MANENO hujenga SENTENSI....
Posted: November 23, 2011, 6:43 pm by SIMON KITURURU
...... ila maswala ya UJUMBE,............ hata sentensi iwe ni ipi LABDA hilo ni swala JINGINE!:-(
Swali:- Na si unakumbuka maswala ya UJUMBE umuhimu wake labda UNATEGEMEA apataye UJUMBE anastukia au tu anahitaji UJUMBE GANI?
Ndio,.........na SENTENSI zozote zile labda zina UJUMBE,........ kama tu KWAKO katika hizo unastukia UJUMBE,.........ingawa bado swala la UMUHIMU wa UJUMBE HUO kwako,....... hilo nalo ni SWALA JINGINE.:-(
NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu Zap Mama, Talib Kweli, Common wabadili kwa - Yelling Away
Au tu Talib Kweli azime kwa-Move Somethin'
-
Swala la kuwa na ``UHAKIKA NA KITU´´ labda ni jambo la kufanyia kazi KILA SIKU....
Posted: November 23, 2011, 4:14 pm by SIMON KITURURU
....kwa kuwa SWALA la UHAKIKA,...
.... laweza kuwa lahitaji IMANI..........na kwa bahati mbaya labda IMANI,....... moja ya misingi yake ni KUTOKUWA na UHAKIKA baadhi ya nyakati.:-(
Swali:- Si unajua ulichonauhakika nacho LEO sio LAZIMA kila siku zijazo/KILA WAKATI utakuwa na UHAKIKA nacho kwa KIPIMO HIKIHIKI cha LEO?
Na USICHO na UHAKIKA wala IMANI nacho LEO,...... labda ni swala la kukipa MUDA tu HICHO.
Ni wazo tu HILI MHESHIMIWA!:-(
Hebu Asa arudie - Jailer
Halafu Seu Jorge aturudishe kidogo brazil kwa - Pretinha ao Vivo
Halafu CEU hapahapa Brazil azime kwa- Malemolencia
-
Wakati kuna SARESARE MAUA -Weye UNAOGOPA nini na WENZAKO wanaogopa NINI?
Posted: November 23, 2011, 3:17 pm by SIMON KITURURU
Na labda huhitaji hata HISTORIA kujua,....... labda wengine hawaogopi hata KUFIA wanachokiamini ,...... kiwe ni SIASA au hata DINI.
Na wajua wengine HAWAOGOPI MTU wasiyemjua au hata kufia NCHI ambayo kwa walivyo nyong'onyea labda ni nchi isiyo wajua angalau hata KWA kuwaunga mkono angalau nao wafaidike angalau na yake MADINI.
Swali tena:- Je wewe UNAOGOPA nini?
Na ni ndio ,........kuna ambao waogopacho sana ni VIBOKO,mitihanin, mende au tu kuparuriwa na KUKU.
Na ndio,...
.... kuna waogopao vifo ingawa wanapoteza muda kwa kuogopa visivyoua kama vile vya majungu rasharasha aka ``JE WATU WENGINE WANAWAWAZAJE TU ´´ kitu ambacho HAKIUI MTU labda.:-(
Je waogopa NINI?Ni wazo tu hili NGULI!
Hebu Nneka Egbuna aanzishe tena kwa-Beautiful
Nneka aongezee- Lost Souls
Halafu Nneka ,Ziggy Marley na Eeday wazime kwa-Express Yourself
-
LABDA hakuna MTOTO awazaye akikuwa atakuwa mfanyakazi wa MOCHWARI kuosha MAITI!
Posted: November 23, 2011, 2:13 pm by SIMON KITURURU
Swali:- Au unafikiri kuna MTOTO atamaniye akikuwa ofisini kwake kuwe kunalazwa WAHESHIMIWA MAREHEMU?
Ndio kuna ya UTOTO,....... na ya UTOTO ya mpenda UDEREVA ,......... mara nyingi sio yale ya UKUBWANI ambayo huweza geuza MTOTO aliyependa kuendesha apende KUENDESHWA!:-(Swali:- SI umestukia UKUBWA nuksi hasa pale kama MTU ni mwenzangu na mimi asiye na MIURITHI ya KITAJIRI astukiapo inabidi afanyie kazi MSHAHARA na ofisi labda ni popote?
- Na kazi si ni KAZI tu ingawa bado ukweli uko palepale kuwa kazi nyingine MUHIMU ni zile za kupima wingi wa minyoo kwenye kinyesi cha Mheshimiwa MAABARA ili kuhakikisha kama kweli MHESHIMIWA ana MINYOO?
NDIO,....... na MAITI wanahitaji WATAALAMU husika ambao ni muhimu tu,....... ndio maana MOCHWARI ni ofisi tu za kawaida za WATU tena labda wale waliokuwa wanaogopa stori za vifo UTOTONI.:-(
NI WAZO TU HILI MKUU!
Hebu AKON aanzishe upya kwa-Mama Africa
Halafu Céu azime kwa - Roda
-
Amigolous na Saleh Kupaza walonga.
Posted: November 23, 2011, 1:38 pm by SIMON KITURURU
Salam,
[www.youtube.com]
Wanamuziki Amigous na Saleh Kupaza kutoka bendi ya Dansi Twanga Pepeta "KISIMA CHA BURUDANI" wakiongelea kuhusu maandalizi ya ziara yao Nchini Uingereza Katika Kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania yatakayofanyika tarehe 26 Novemba 2011 katika ukumbi Club Club 2000 Banqueting Suite(Former Silver Spoon) Popin Building Southway. Wembley HA9 0HB kuanzia saa 9pm- 4am. Kiingilio ni £20.00 kwa single na couple £35.00 kabla ya saa sita Usiku
Asanteni
URBAN PULSE CREATIVE wakishirikiana na MISS JESTINA BLOG
Nimetumiwa hii na:Frank Eyembe -
Afrika KUSINI na vyombo vya HABARI!
Posted: November 23, 2011, 1:24 pm by SIMON KITURURU
Ya: ``STATE SECRETS´´ law.......na dalili za WANAHABARI kufungwa midomo.....
-
Na ni mstari mwembamba kati ya KUFAULU na KUFELI!
Posted: November 22, 2011, 5:36 pm by SIMON KITURURU
Na kama UMEFAULU,...
.....labda kumbuka kufeli kupo tu ,...
.... na kuna uwezekano ALIYEFAULU hajisikii kafeli kwa kuwa kaegemeza mitazamo yake mbali na YALE aliyofeli.
Na kama MTU anajisikia KAFELI,....... akumbuke tu KUFAULU kupo tu,....... .... na kiendeleacho ni labda kabobea katika kuangalia zaidi ayatambuayo kama KUFELI.
Swali:- Si katika MTU alilofaulu akijichunguza bado MAISHANI anaweza kustukia nini alichofeli na ndio maana hata mtu ajulikanaye kwa kufaulu KISIASA kama NELSON MANDELA bado anakiri wakati anafanikiwa KISIASA , kifamilia ALIKUWA anafeli kitu kilichofanya ndoa zake mbili kufa na watoto kulelewa bila BABA?
- Na si unakumbuka hata MOTHER TERESA yasemekana alikuwa anaona wale WALIOONEKANA na JAMII kuwa ndio waliofeli kimaisha na kuwa masiki kupindukia ndio ambao KIIMANI walionyesha kufaulu zaidi kuwa karibu na MUNGU?
- Na si nasikia hata katika LIFAULIWALO/Lifaulwuo moja ya siri ya wafauluo HILO ni kufeli katika hilo bila kukata tamaa nakulifanyia kazi hata kama ni kimazoezi mara kwa mara kitu kisahauliwacho na washabikiao KUFAULU tu ?
Ndio,...... labda tukumbuke hakuna AFELIYE au KUFAULU kila kitu,....... na ni tabia tu zawatu kuruka baadhi ya mambo kufanyacho hapa DUNIANI kuna wenye lebo za kuwa wao WAMEFAULU,...
.... autu ni wale WALIOFELI:-(
Ni wazo tu hili MKUU!
Hebu BONEY M warudie-MALAIKA
Au tu Anjelique KIDJO naye arudie-MALAIKA
Halafu tu tena BONEY M wazime kwa-JAMBO BWANA/Hakuna MATATA
-
Anayenipa motisha fulani leo ni: HELEN OYEYEMI!
Posted: November 22, 2011, 5:15 pm by SIMON KITURURU
Kama unahusudu kusoma au unahamu yakuandika,...
... cheki kazi za huyu mdada Helen Oyeyemi.......ambazo kiaina zimenianzishia wiki kisababu mbalimbali:
Msikie kidogo akiongea....
Habari zake zaidi HUKU
Kwa kifupi:
Helen Oyeyemi was born in Nigeria in 1984 and has lived in London since the age of four.
She completed her book The Icarus Girl just before her 19th birthday while studying for her A-level exams. She is now a student of social and political sciences at Cambridge University.
AU:
Helen Olajumoke Oyeyemi (born 10 December 1984) is a British novelist. She was born in Nigeria and raised in London.
She wrote her first novel, The Icarus Girl, while still at school studying for her A levels at Cardinal Vaughan Memorial School.
Oyeyemi studied Social and Political Sciences at Corpus Christi College, Cambridge, graduating in 2006. Whilst at Cambridge, two of her plays, Juniper's Whitening and Victimese, were performed by fellow students to critical acclaim and subsequently published by Methuen.
In 2007 Bloomsbury published her second novel, The Opposite House which is inspired by Cuban mythology.
Oyeyemi is a lifelong Catholic who has done voluntary work for CAFOD in Kenya[1].
In 2009 Oyeyemi was recognised as one of the women on Venus Zine’s “25 under 25” list. [2]
Her third novel, White is for Witching, described as having "roots in Henry James and Edgar Allan Poe" was published by Picador in May 2009. It was a 2009 Shirley Jackson Award finalist and won a 2010 Somerset Maugham Award.
Her fourth novel, Mr Fox, was published by Picador in June 2011. -
YA PAKISTANI:Kutuma meseji ZA SIMU zenye matusi mwiko kuanzia hivi karibuni !
Posted: November 22, 2011, 12:55 pm by SIMON KITURURU
PAKISTANI yataka kampuni za simu kuzuia meseji zenye maneno ya matusi.
... na maneno kama ,Jesus Christ, Satan, TAXI, Idiot, yakiwa ni miongoni mwa ambayo itakuwa mwiko kumtumia meseji rafikiyo ukitumia sentensi yenye maneno hayo..... DEKU ndude,...
-
ASHA BARAKA na AMOSI wazungumzia kuhusu 50th Independence Tour
Posted: November 22, 2011, 11:01 am by SIMON KITURURU
Salam,
[www.youtube.com]
Mkurugenzi wa African Stars ASHA BARAKA pamoja ofisa wa Ubalozi nchini Uingereza AMOSI MSANJILA wanazungumzia kuhusu maandalizi na matayarisho kwa ajili ya ziara ya Twanga Pepeta "KISIMA CHA BURUNDANI'' nchini Uingereza katika Kuazimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Show hii itafanyika jumamosi Tarehe 26 November 2011 katika Ukumbi wa Club 2000(Silver Spoon)Savoir Banqueting Suite, Popin Building Southway, Wembley HA9 0HB.
Asante,
Urban Pulse Creative
-
Ngumi kupigwa Desemba 18,MZALENDO PUB
Posted: November 21, 2011, 12:23 am by SIMON KITURURU
Na MWANDISHI WETU
WASANII mbali mbali hapa nchini wanatarajiwa kutoa burudani katika pambano la mchezo wa ngumi lisilo na ubingwa litakalowakutanisha bondia, Mada Maugo na mpinzani wake Suleimani Saidi 'Toll' Desemba 18 mwaka huu katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama JIjini Dar es Salaam.
Akizungumza na kona hii ya burudani Raisi wa shirikisho la ngumi za kulipwa hapa nchini (PST) Emanuel Mlundwa alisema, maandalizi kwa ajili ya pambano hilo yamekamilika.
Aliwataja wasanii watakaotoa burudani siku hiyo kuwa ni Kundi la mapacha watatu Khalid Chokoraa (Halidi Chuma)pamoja na msanii wa mziki wa bongo fleva Mwana FA (Hamisi Mwinjuma).
Alisema licha ya kuwepo kwa burudani hizo vile vile atakuwepo kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila Super D kwa ajili ya kutoa mafunzo kupitia Dvd pamoja na kuzisambaza.
Aliwataka mashabiki wao wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani hiyo, licha ya kuwa mchezo huo haupewi kipaombele watahakikisha wanasonga mbele katika kuazimisha miaka 50 ya uhuru.
aidha katika mapambano ya ngumi ya utangulizi mabondia Yohana Miyayusho na Shadrack Juma, Doto Kipacha atazidunda na Saidi Muhidini na kwa upande wa mchezo wa Kick Boxing ambao utatuwakilisha kimataifa Tanzania Muaythai Academy of Combat watawaletea mpambano kwa mara ya kwanza nchini kati ya bondia Emanuel Shija kutoka Tanzania na Munyeshyaka Vincent kutoka Rwanda Mpambano huo utakuwa wa kimataifa kutokana na ushiriki wake wa nchi hizo mbili nchini zitakuwa zikipeperusha bendera zao.
Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930 +255774406938 Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
Nimetumiwa hii na:Super D -
Mahojiano Maalum na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda Part 3
Posted: November 21, 2011, 9:23 am by SIMON KITURURU
Salam,
[www.youtube.com]
Urban Pulse Creative inakuletea sehemu ya tatu katika Mahojiano maalum kutoka kwa Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
.
Asanteni,
Urban Pulse Creative
Nimetumiwa hii na :Frank Eyembe wa Urban PULSE -
Ngumi kupigwa Desemba 9 DDC Keko Dar es Salaam
Posted: November 21, 2011, 9:19 am by SIMON KITURURU
Ramadhan Nassib kulia
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Ramadhan Nassib, anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na mpinzani wake Antony Kariuki wa Kenya, katika pambano la maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru litakalopigwa kwenye Ukumbi wa DDC Keko Dar es Salaam, Desemba 9 mwaka huu.
Akizungumza Mratibu wa pambano hilo, Pius Aghaton, alisema kuwa pambano hilo linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na rekodi zilizopo kwa mabondia wote.
Alisema kuwa pambano hilo litakuwa la uzito wa Fly ambalo litapigwa katika raundi 10.
“Tumeandaa pambano la aina yake kwa ajili ya kusherekea miaka 50 ya Uhuru na pia kuweza kuwajengea mabondia wetu uwezo wa kucheza mapambano ya kimataifa” alisema.
Mratibu huyo alisema kuwa katika pambano hilo, kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo bondia Juma Fundi atazichapa na Juma Seleman katika pambano la uzito wa Fly la raundi sita, Fred Sayuni atazipiga na Bakari Dunda katika pambano la uzito wa Feather la rfaundi sita.
Pambano jingine litawakutanisha mabondia Rashid Ally pamoja na Daud Mhunzi katika pambano la uzito wa Feather la raundi sita na Faraji Sayuni atazichapa na Alpha George katika pambano la uzito wa Fly la raundi nne.
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.
'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,
DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
Mob;+255787 406930
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
--
Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930 +255774406938 Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
Nimetumiwa hii na:SUPER D -
LABDA hakuna PENZI liishilo bila UCHIZI wa wapendanao WAPENZI!
Posted: November 20, 2011, 11:19 am by SIMON KITURURU
Ndio,....... labda kama hakuna UCHIZI kwenye PENZI LAKO,.........labda kumbuka kwa wengi ukitumia akili penzi tamu sana kwa kutumia akili hushushwa dozi KIUTAMU na kuna washushwao dozi WAPENZI mpaka penzi lao hata likichunguliwa halitawezwa kutofautishwa na PENDO LA DADA na KAKA hata ingawa pendo la DADA na KAKA ni chanya tu hata katika maisha ya wasio DADA na KAKA kibinamu .
SWALI:- Au?
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!JUMAPILI NJEMA Mkuu!
Hebu WILLIE BOBO asigine kidude kwa-GUAJIRA
Au tu azimaye awe ni Oliver N'goma apenyezaye tena ya- Lili
-
Wakati MHESHIMIWA labda sasa hivi ana hamu kweli ya KUMA leo!
Posted: November 20, 2011, 10:50 am by SIMON KITURURU
Na yasemekana,........TATIZO la kuma ni kuwa hicho kidude huja na MWENYE kuma.!
Na nasikia,...... kuma na mwenye kuma ,........ maringo yao kwa watu wakawaida ambao ni wahitajio tu chakula kama kitu muhimu zaidi kimtazamo,...... yasemekana kuma na MWENYE kuma ni vitu viwili tofauti sana kama unaujasiri wa KUTOFAUTISHA. vitu:-(
Swali:- AU?
- Na si unakumbuka yasemekana MBOO haifanani na mwenye MBOO?
Ndio,...... ni wazo tu hili MHESHIMIWA ,....... hata kama kwako wazo hili labda halijavaa chupi!:-(
Hebu SEAL aanzishe upya kisiri kwa-SECRET
SEAL aendelee kurudisha ustaarabu kwa - Fly Like An Eagle
Au tu SEAL asitishe dozi kwa- Kiss from a Rose
-
Safari ni NDEFU,...
Posted: November 19, 2011, 1:47 pm by SIMON KITURURU
... lakini,......UKISAFIRI kuelekea ufikiriako ni utakako KWENDA,........ waweza kuja kustukia utakalo kwa unakotaka kwenda lipo palepale TAYARI ulipo.:-(
Ni wazo tu hili MKUU!Jumamosi njema MKUU!
Hebu turudi MALI ili Oumou Sangaré aingilie tena kati kwa - Seya
Halafu huyuhuyu Oumou Sangaré azime kwa -Ahn diyah
-
Hamu ya KUGUSAGUSA kidogo kidude HUWEZA KUWA ndiyo ianzishayo yajulikanayo kuwa ni ya MAKUBWA ya KUSHIKASHIKA NDUDE!
Posted: November 19, 2011, 1:33 pm by SIMON KITURURU
NDIO,....... LAKINI na DOGO lichukuliwalo kuwa ni LA PILI,...... labda ndilo lilianzia kwenye lile dogodogo lile LA MOJA kikutambulika tu,....... kwa kuwa kiukweli labda dogo tokea mwanzo ni KUBWA!:-(
Swali:- Kwani unafikiri MAKUBWA hutokea ghafla tu kwa kawaida?
- Na katika DOGO si labda ni MTAZAMO wa MTU tu hasa kwa kuwa labda DOGO KWANGU ni KUBWA KWAKO?
Ndio,..
.... labda mpenda MAKUBWA agusagusaye DOGO ambalo laweza zaa MAKUBWA,...
.......huyo kiaina hata kama atadai sio tafakari zake dogo HILO halikuwa lamkumbusha MAKUBWA....
..........yawezekana hata kuvutiwa kwake na dogo hilo hata bila yeye kujua ni kwa sababu DOGO hilo hata kama sio kiudogo wa kugusagusa kiaina kuna kimstuacho kuwa hapo kuna lake apendalo kubwa hata kama sio lile la KUSHIKASHIKA!:-(
Swali:- Unafikiri ukiangalia DOGO hustukii kubwa kama dogo hilo UNAHISI laelekea kuwa KUBWA?
Ndio,...... na UWEPO wa hamu ya kugusagusa KIKUBWA kwa mwenye DOGO,....... inawezekana ni kwa kuwa tu kuna MAKUBWA na pia kuna kishikikacho KIDOGO!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na si lazima ulielewe!:-(
Hebu Africando waanzishe upya ili tubadili mawazo kwa - Aicha
Africando waongezee dozi kwa - Sabador La Bamba
Africando wadinye - Gombo
Halafu hapahapa Senegali Wasenegali hawa wa Africando wajaribu kuzima kwa - Yay Boy
Halafu tu BALOJI na Konono N°1 ghafla waturudishe KONGO na ndio wazime tena kwa-KARIBU YA BINTOU
-
AFRIKA BAMBAATAA recklessly!
Posted: November 19, 2011, 11:12 am by SIMON KITURURU
Hebu UB 40 na Afrika Bambaataa warudie tu kutonesha- Reckless
Na mie CHICHEMI sasa hivi ila kama tamu muhimu,......labda fanya iwe TAMUKUNOGA leo hata kama si ki-RECKLESS...!:-(
Tuko Pamoja na siku njema mkuu! -
Hebu USENGE utetewe kiduchu tena UGANDA!
Posted: November 19, 2011, 5:55 am by SIMON KITURURU
... hebu tudake hii ndude,........Uganda gay rights.....
...wakati FRANK MUGISHA kutoka UGANDA akinyambulisha haki hizi ambazo yasemekana kuna wengi wazibaniazo mapaja....
Swali:- Si nasikia kama tumizi la kinyeo ni la MTU mwingine kinyeo cha mwingine hata bila PENZI labda hilo swala sio dili lako utumbuaye kwa mbele?
Ni nanilii tu hii alwatani KIHESHIMATU kabisaa! -
LEO baada ya Rais wa zamani wa PHILIPPINES yule GLORIA ARROYO kudakwa kwa wizi wa kura za mwaka 2007
Posted: November 18, 2011, 9:13 pm by SIMON KITURURU
Kama Mtanzania:- Unahisi ipo siku mambo kama haya ya kujaribu kumuwajibisha kiongozi baada ya kuondoka madarakani yatakuja tokea BONGO?
Ndio,....... Rais Gloria Arroyo leo kadakwa tena akiwa anaumwa hospitalini kisa maswala ya wizi wa kura ya mwaka 2007 akiwa Rais.
Na kikubwa kisa cha kudakwa kwake wala hakuhusiani na kura zake mwenyewe kama Rais ,........ bali kwakuhusishwa na kuhusika kwake katika kufanikisha mpambe wake anashinda kiti cha useneta kwa kufanikisha wizi wa kura za mpambe wake huyo.
HABARI zaidi HAPA
Swali tena kimarudio:- Unafikiri ipo siku KATIBA YA BONGO itaruhusu kuwajibishwa kwa watawala washirikio kuhaini nchi baada ya wao kuondoka katika hatamu?
Nawaza tu kwa SAUTI!
Hebu tujaribu kubadili wazo kwa uchokozi kutoka kwa mtoto mzuri JOSEY PRISCILLE
Haya basi NIMEACHA MKUU! -
KOZI YA MAKOCHA WA NGUMI MKOA WA PWANI YAOTA MBAWA
Posted: November 18, 2011, 8:54 pm by SIMON KITURURU
Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa Kibaha Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuhuzuria kozi ya makocha iliyotarajia kuanza jumamosi ya kesho ata hivyo kozi hiyo iliota mbawa baada ya mkufuzi alieteuliwa na chama cha ngumi cha dunia (AIBA) kupata dharura kozi hiyo iliyoandaliwa na kamati ya Olimpic (TOC) iliota mbawa na kufanya makocha hao kutojua hatma yao baada ya kufika Pwani bila kupewa stahiki zao walizoahidiwa katika barua ikiwemo usafiri wa kwenda na kurudi pamoja na chakula ambavyo hawajapatiwa na kujitafutia usafiri kwa njia yao wenyewe kurudi mikoani kwao.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Makamu wa Rais wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini (BFT), Michael Changalawe (kulia) akizungumza na makocha wa ngumi nchini wakati walipowasili, Kibaha Mkoa wa Pwani Juzi kwa ajili ya kozi ya mchezo huo na kuambiwa kozi hiyo iliyoandaliwa na kamati ya Olimpic (TOC) imehairishwa kutokana na mkufuzi wake aliyeteulia kupata dharura . Hata hivyo, makocha hao kutoka mikoa mbalimbali ya nchi walinyimwa stahiki zao hususani maladhi na posho za nauli za kuwarudisha mikoani walikotoka na kupatiwa kwa makocha wachache tu kinyume na barua walizopewa makocha ya kuwa watalipiwa gharama zote za kwenda na kuwarudisha mikoani kwao.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930 +255774406938 Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
Nimetumiwa taarifa na:SUPER D -
Dawa CHUNGU saa nyingine NDIYO mgonjwa AHITAJIYO!:-(
Posted: November 18, 2011, 12:02 pm by SIMON KITURURU
NDIO,....... saa nyingine kwa mpenda UTAMU,...... huweza kuchanganya kila TAMU na UZURI wa kitu ,......kitu kifanyacho kwa kupenda kwake UTAMU kuathiriwa kutostukia kuwa TIBABU la RIDHISHO kwake ni ndude CHUNGU.
Swali:- AU?
ILA yasemekana kwa bahati mbaya TAMUTAMU KUNOGA inamchezo saa nyingine kwa BAADHI YA WATU kiladha zao kunasia,...
.... kwa MALAYA wa kulipia MTAANI zaidi ya kwa MAMA WA NYUMBANI,........kwa totoz la kilokole ambalo ni MALAYA CHUMBANI kama liliopolewa disko vile ZAIDI ya BONGE la totoz la kilokole ambalo chumbani liko kama KANISANI ambalo linaheshima za kilokole zote kwenye mpaka ya UNYUMBA HALALI usio DHAMBI chumbani,.......kitu ambacho labda ni swala la kuchunguza ni kwanini kwa mtu saa nyingine anasahau maji ni matamu SANA kiladha na kuongelea juisi kama ndizo TAMU kwa kuwa hazina maji mengi KILADHA.
Swali:- Si unakumbuka kuna watu hawana LADHA mdomoni?
- Na si unakumbuka PILIPILI sio kionjo kitamu kwa kila mtu MDOMONI?
Ndio,.......KIDAWA,....... MCHUNGU saa nyingi HUYO ndiye DAWA,...... na kihitajiwacho kisichopendwa ladha mara nyingi labda NI DAWA na NDICHO MUHIMU ZAIDI hata kama kwa kuwa kitibiwacho hakiitwi UGONJWA basi na TIBABU hata lile lisilo na mahaba nalo haliitwi DAWA .
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu kwenye GITAA LA BEZI aingilie kati VICTOR WOOTEN nimuheshimuye kwenye chombo ili aanzishe vita mpya kwa -U can't hold no groove if U aint got no pocket
Turudi KAMERUNI ili mpiga bass nizimiaye kazi zake Richard Bona aanzishe upya kwa - Djombwe
Halafu Richard Bona azime tu dozi tena kwa- Ekwa Mwato
-
Twanga Pepeta 50th Tanzania independence Tour
Posted: November 18, 2011, 11:08 am by SIMON KITURURU
Salam,
African stars Entertainment Tanzania wanakuletea Bendi nzima ya Twanga Peteta ili iweze kufanya Makamuzi Live ndani ya Nchi ya Uingereza. Terehe 26.11.2011.
[www.youtube.com]
Asante sana!
Nimetumiwa TANGAZO na:FRANK Eyembe wa Urban PULSE -
Swala la ``KUFAIDI´´ ambalo huwezazalisha mpaka ``LABDA anafaidi zaidi alalaye na RAIS!´´
Posted: November 18, 2011, 10:47 am by SIMON KITURURU
Swala la KUFAIDI,...... laweza hitimishwa kwa kudhaniwa ``WENGINE wanafaidi zaidi ´´´......na nakama kwa wengine wana`` URAIS `` kama kipimo cha juu cha KUFAIDI hufanya hata yahusianishwayo na URAIS kuwa ni kigezo kizima cha nini ni KIPIMO cha juu cha KUFAIDI,...
... na kufanya mpaka twaweza kusahau labda kuna mengine ni hausi boi wa MWENYEKITI WA KIJIJI ndiye ajinomayo KIKUFAIDI na na sio RAIS.:-(
Swali:- Unabisha?
Na kwa kuwa labda inahitaji kwanza MTU awe na tafsiri yake BINAFSI yakuwa KUFAIDI ni nini,...
... labda ikitafsiriwa vizuri WATU huweza kuhitimisha KIDUDE ni KIDUDE tu hata kama kimemnasia BINADAMU MWINGINE asiyelengwa na FANTASI za mtu zilizojengwa na tafsiri zake za nini ni KUFAIDI.:-(
Swali:- AU?
Ndio,......katika swala zima la KUFAIDI,...... labda faidi tu ulichonacho KINGUNGE ,........ kwa kuwa labda ni FANTASI tu ambazo zafanya MENGINE na YAWENGINE kwako kitafsiri ni KUFAIDI,....... na waweza kujikuta unapoteza muda kwa kutamani nyama ya kuku wa kizungu USIYONAYO kikufaidi ambayo ukiipata matokeo yake ni kustukia unanogewa zaidi na nyama ya kuku wa kienyeji ambayo ulikuwa nayo tokea zamani na hukuifaidi kwa kuwa ulikuwa huipi chansi kinafasi ili UIFAIDI kwa kuwaza usiyo nayo ile ya paja la kuku wa KIZUNGU.
Swali:- AU?
- Si wajua ukichunguza labda kila MTU kuna afaidicho kuliko wengine ?
... labda KUFAIDI,...
.... ni tendo la kustukia ni kitu gani MAISHANI mwako weye hicho UNAKIFAIDI zaidi ya WENGINE!:-(
Ni wazo tu hili KAMANDA na usikonde!Ijumaa na WIKIENDI NJEMA MHESHIMIWA!
Hebu turudi KONGO ili Staff Benda Bilili waanzishe upya kwa - Je t'aime
Hapahapa KONGO hebu KONONO No. 1 Waingilie shughuli kwa....
Konono No 1 waendelee---
Au tu KONONO No.1, Herbie Hancock ,India Arie na wengine wazime tu kwa-IMAGINE
-
Kuna ambao kwao KILADHA ni idadi ya SHILINGI hasa kwa kuwa LADHA hunogeshwa na GHARAMA!
Posted: November 18, 2011, 10:08 am by SIMON KITURURU
Kuna wanogewao na kitu ,...... kisa hicho kidude ni GHALI!Swali:- AU?
Na pamoja na kuwa kuna wadaio kuna wengi DUNIANI ambao kwao GHALI SANA NDUDE ni ile igawiwayo BURE,...
...bado ni kweli pia kuna wanogewao na NDUDE na kuapia ni tamu kisa hicho ni kitu GHALI.
Swali:- Si yasemekana kuna wavutiwao na GHARAMA kitu kifanyacho kwao kitu cha thamani wakikipata BURE huwa hawakithamini kisa TAMU ZAO zimebobea katika kuunganisha GHARAMA ya KITU KISHILINGI DUKANI na TAFSIRI kuwa kama ni BEI KUBWA basi hicho BABU KUBWA kitu kifanyacho wanaruka kustukia thamani ya kweli ya KITU?
Ndio,...
....labda kuna TAMU,...
... na kwa watu wengine hiyo ni TAMU tu kwa kuwa ni GHALI!:-(
NI wazo tu hili KINGUNGE!
Hebu tupate zilipendwa ya KIBRAZIL kwa msaada wa Gilberto Gil aturushaye studio mwaka 1979 kudinya - Back in Bahia / Aquele abraço
Sijui kwanini hebu Gilberto Gil arudie tena-Aquele abraço
Gilberto Gil hapahapa BRAZIL apenyeze - Kaya n Gan Daya
Halafu ajaribu kuzima tu kwa -Waiting in vain
Halafu ghafla Bob Marley aingilie na kurudia-Waiting in vain
Halafu huyuhuyu WACHAGA wadaio ni MCHAGA BOBU MALIYA azime kwa-BAD CARD
-
Kwa kujitahidi SANA kuna wafikiao KUCHUNGULIA mpaka ambavyo WANGEANGALIA tu kwa kuwa DUKA la MZUNGU li WAZI!
Posted: November 17, 2011, 10:54 pm by SIMON KITURURU
Yasemekana,...
....UKIJITAHIDI SANA,...
.... mara lukuki yawezafikia kuwa JUHUDI SANA ziko katika KUJITAHIDI SANA kuliko hata katika ni nini kwa KUJITAHIDI UNAFANYA.:-(
Na yasemekana,..... tuko wengi tu ambao kwa KUJITAHIDI SANA mpaka tunapofuka na kufikia KUCHUNGULIA mpaka zile IHANA,...
...ambazo labda tungeziangalia tu na KUSHUHUDIA mpaka ya firigisi na kitumbua makunyanzi na kiponzacho ni JUHUDI!
Swali:- Unafikiri wakati unajuhudi na HIKI hilo sio kikwazo kwako kifanyacho huoni KILE?
Ndio ,...
.... LABDA,...
..... au tu ni LABDA saa nyingine LABDA,...
...... kifanyacho MTU au tu hata WEWE hustukii mengine,........ni JITIHADA ZAKO na JUHUDI zako kwenye VITU ambavyo labda sio hicho KITU kiwezacho kuwa ni muhimu KABISAAA kwako !:-(
SWali:- Unabisha?
Ndio,...... ukijitahidi,..........LABDA saa nyingine labda UNAJITAHIDI SANA mpaka hata katika YAFANYIKAYO KIVIVU weye wayafanyia JUHUDI mpaka yanaanza kuonekana ni MAGUMU hata kwa wasio WAVIVU wa kufanya.:-(
Ni wazo tu hili NGULI!:-(
Hebu Inner Circle wabadili kwa - Games People Play
Inner Circle wachokoze zaidi mpaka wale WAKRISTO wa siku mojamoja kalika WIKI hata kama hiyo ni JUMAPILI na sio JUMAMOSi katika mtuno- One Day Christian
Halafu tu INNER CIRCLE wazime kwa -BAD BOYZ
-
MATANGAZO mengine BWANA!
Posted: November 17, 2011, 3:57 pm by SIMON KITURURU
-
TWANGA PEPETA independence tour
Posted: November 16, 2011, 7:56 pm by SIMON KITURURU
Nimetumiwa na :Urban Pulse -
Bado kiwezeshacho``KUPENDA´´ chaweza kugeuka TATIZO,...
Posted: November 16, 2011, 3:42 pm by SIMON KITURURU
.... kwa kuwa CHOCHOTE kile chaweza KUPENDEKA ukikaa vizuri,...... na KUPENDA kwa MTU,........kwa wengine labda tayari ni TATIZO.:-(
Swali :- AU?
NDIO,...
.... ``NAPENDA´´,...
.... hata kama ni ile ``NAKUPENDA´´,...
.... kuna watakaodai hubobea maudhaifu ya watu husika WAPENDAO ambayo si lazima kwa mtazamo wa asiyehusika kuonekana kama ni CHANYA au hata TATUZI hata kwa PENZI,....
... na labda ndio maana MAPENZI yamejaa WAPENDAO MTU wasio pendwa na huyo WAMPENDAYE.:-(
Ni wazo tu hili MKUU!
Hebu turudi NIGERIA kwenye ile zilipendwa Easy Motion Tourist kama ilivyodungwa na Fatai Rolling Dollar / Harbors Band
Au tu Fatai Rolling Dollar aongezee - Allah Na Tu Ba
-
KWA WALE WAPENZI WA SWAHILIVILLA FACEBOOK PAGE
Posted: November 16, 2011, 3:01 pm by SIMON KITURURU
KWA WALE WAPENZI WA SWAHILIVILLA FACEBOOK PAGE
TUMEVUMBUA MTINDO WA KILA SIKU KATIKA [swahilivilla.blogspot.com] KUWEKA (WAPENZI WETU WA FACEBOOK PAGE KWA KILA SIKU )
NITUMIE PICHA ZENU NDANI YA INBOX YANGU AU HATA KATIKA PROFILE YANGU. PICHA ZIAMBATANE NA MAELEZO PAMOJA NA SALAMU KWA WAPENZI UWAPENDAO. KUFANYA HIVYO KUTATOA CHANGAMOTO YA UKUWAJI WA JAMII YETU KATIKA MAZINGIRA UA UPENDO KWA JAMII YETU HII TUIPENDAYO SHKRAN! TUPENDANE
ANGALIA MFANO HAI NEANI YA: http://swahilivilla.blogspot.com
JIUNGEA NA FACEBOOK PAGE HAPA [www.facebook.com] -
MASHINDANO YA NGUMI YA KAMANDA KOVA YANAENDELEA
Posted: November 16, 2011, 2:55 pm by SIMON KITURURU
Bondia Mussa Mohamedi (kulia) kushoto akioneshana ufundi wa kutupa makonde na John Christian wakati wa mashindano ya Kova Cup Dar es salaam jana Mussa alishinda kwa point.
(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Bondia Sunday Elius akipambana na Abdallah Kasimu wakati wa mashindano ya Kova Cup Dar es salaam jana Kasimu alishinda kwa point.
(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.com www.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930 +255774406938 Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania -
Hebu tumsikilize TAJIRI kuliko wote DUNIANI kingawira PESA!
Posted: November 15, 2011, 10:15 am by SIMON KITURURU
OOOOKEI,........ ngojea Carlos Slim ambaye ndiye mwenye pesa kuliko wote DUNINANIN,......aongee,...
-
MALIKA NDLOVU na The BADILISHA Poetry X-Change
Posted: November 15, 2011, 3:26 am by SIMON KITURURU
Turning & Returning
Showreel
BADILISHAAn African Poetry Exchange
-
Nigeria's YouTube poet /Mshairi wa Kinaijeri CHIEDU IFEOZO ananilie USHAIRI katika YOUTUBE.
Posted: November 14, 2011, 7:23 pm by SIMON KITURURU
Chiedu Ifeozo,..... yuko ONLINE.
WASHAIRI wa BONGO mpo?
Ni changamoto KIAINA tu hii NGULI na wala usikonde!
Au tu tupate Ushairi kutoka kwa Wayne Visser uitwao- I am an African
-
MABONDIA WAPIMA AFYA ZAO
Posted: November 14, 2011, 6:04 pm by SIMON KITURURU
Daktari wa Mchezo wa ngumi, Josefu Magesa akiwapima mabondia watakaoshiriki mashindano ya kova Cup yaliyoanza Dar es salaam leo katika ukumbi wa PR hotel zamani IMASCO CENTER mashindano hayo ya siku mbili yanamalizika jumanne ya 15/11/2011.
(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com) --
Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.com Mob;+255787 406930 +255774406938 Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
Nimetumiwa taarifa na:Super D Boxing Coach -
....labda TATIZO ni RAIS NYERERE kufanikiwa zaidi kama MTU binafsi NYERERE katika mfumo uathirio zaidi ya mtu binafsi HATA asiye mchumba wa NYERERE!:-(
Posted: November 14, 2011, 12:15 pm by SIMON KITURURU
Yasemekana,....... kama mafanikio ya Mheshimiwa NDUGU ZITTO KABWE yatakuwa ni yale ya mtu BINAFSI kama yalivyokuwa ya GADDAFI,...
.... yahitajio MFUMO MZIMA au tu yale yafanikishwayo kwa msaada wa ki(kwa KI-ung'eng'e )``INSTITUTIONS´´ ili wengi waendelee kufanikiwa hata aliyefanikisha ambaye ni Rais MWINYI kwa kuwa bado sio ZITTO KABWE akiondoka ,...
....yahitajiyo MFUMO MZIMA au tu hata ``INSTITUTIONS BOMBA´´ ili yaendelee ,...
....aliyefanikiwa binafsi kama Rais DOKTA BABA WA TAIFA Mwalimu NYERERE aking'atuka hayo hufa kwa kuwa misingi ya yakuyaendeleza kimfumo au hata ki vyombo vya UMMA kiidara ambavyo vyaweza kuendelea na mchezo uleule,......hushindwa kucheza mchezo uleule VILEVILE kisa mtu binafsi hata KIMKAPA hayuko tena katika HATAMU.
Swali:- Kwani unafikiri baada ya NYERERE - ile ndude CCM bado ni ileile KIVILEVILE?
- Na si yasemekana kama kuna MISINGI MIZURI ya mfumo katika idara za KIKWETE yeyote asiye kikwete , KIKWETE akiondoka anaweza kujikuta kirahisi tu ana KIKWETESESHA?
- Si unakumbuka labda mtu mmoja ni chachu tu na huhitajika KIJIJI KIZIMA ili kutunza kijiji KIZIMA?
Ndio,....... yasemekana SABABU MOJAWAPO ifanyayo ya GEORGE BUSH yafanane na ya BARRACK HUSSEIN OBAMA ni mfumo na idara zichezazo vilevile MCHEZO ULEULE na ndio maana VITA za GEORGE BUSH huchezeka vilevile hata kama ashikiliaye kiuno ni OBAMA.:-(
Ni wazo tu hili lililopinda KIDOOOOOGO MHESHIMIWA !:-(
Hebu tu tena Baaba Maal na wenzake wabadili WAZO kwa kurudia tena- Three Little Birds
Au tu tena Herbie Hancock na Céu waingilie tena kati na kuzima kwa - Tempo de Amor
-
UKWELI labda ni KWAMBA,...
Posted: November 14, 2011, 11:15 am by SIMON KITURURU
.... hakuna atakaye kuweka HURU,....... na kama unataka kuwa HURU kiuhuru ,........ hiyo ni shughuli yako MWENYEWE kujiweka HURU.:-(
Swali:- Si starehe JIPE MWENYEWE?
- Kwani unafikiri kuna kitu kusaidiwa kuwa HURU?
Ndio,...
.... uhuru labda ni JAMBO la kujitakia MWENYEWE,...
... kama tu ilivyo kuwa labda UHURU ni jambo tu pia la mpaka KUJITAFSIRIA mwenyewe.:-(
Swali:- Kwani kwako kuwa HURU maana yake ni NINI?
- Unafikiri TANZANIA ni NCHI huru?
- Watanzania je?
- Wewe je?
Ndio,...... labda ni swala la MTU aliye huru,...... kuwa HURU hata katika swala la KUFICHA hayuko huru ujue alikuwa anafanyanini MSALANI!:-(
Ni wazo tu hili MKUU!Jumatatu njema!
Hebu Toni Braxton alainishe kwa-Spanish Guitar
Au tu TONI BRAXTON alainishe zaidi kwa-Unbreak MY heart
-
YA DUNIA: Human echolocation lets blind man 'see' /Kuona kwa KIPOFU kwa KUSIKIA.
Posted: November 14, 2011, 10:51 am by SIMON KITURURU
Swali:- Kama unaona-JE wakumbuka wasioona wanadinyaje wasiyoyaona ?
Cheki moja ya mbinu ya wasioona KUONA,...... katika -Human echolocation lets blind man 'see'
-
UMUHIMU wa KITU kwa MTU asiye WEWE uwezavyo kuwa ni CHIPSI MAYAI!
Posted: November 14, 2011, 9:58 am by SIMON KITURURU
Cha MUHIMU kwa MTU asiye WEWE,....... labda ni kile ambacho kwa apaye umuhimu NYAMA,...... hicho ni MCHICHA.:-(
Swali:- Na si unakumbuka KIPEWACHO UMUHIMU na MTU , na kitu MUHIMU kwa kustahili UMUHIMU vyaweza kuwa kwa kawaida ni vitu viwili TOFAUTI?
- SI unakumbuka labda umuhimu wa KITU hata kwako ni PIPI kwa kuwa unahitaji sukari mwilini na wala sio MCHICHA usifiwao kwa kutohusishwa na MHESHIMIWA anukaye mdomo kuoza MENO?
Ndio,..... labda bado ni KWELI,....... la MUHIMU kwako ni MUHIMU kwako tu,....... hasa kwa sababu tu UMELIPA umuhimu!:-(
Ni wazo tu hili MKUU!
Hebu Rick James arudie-COLD BLOODED
Au tu Ol' Dirty Bastard arudie tu - Cold Blooded
Halafu tena Ol' Dirty Bastard azime kwa -Baby, I got your money
-
Leo baada ya kutoka KANISANI: Helloo dhambi -MAMBOZ vipi aisee!
Posted: November 13, 2011, 8:56 pm by SIMON KITURURU
Ndio,....... labda DHAMBI MPYA ya ufikiriaye hana DHAMBI kanisani kwa kaupole kake ,.....UCHUNGAJI WAKE ulivyo KIASKOFU... ...uimbaji KWAYA WAKE,........au tu hata kwa akuangaliavyo kwa MAHABA katika jina la BWANA kiuchumba,.......na wala hata sio kwa jazba yake ya kunena kwa lugha ,...
.... labda ni kweli DHAMBI MPYA za walio KANISANI huanziaga hukohuko KANISANI lakini!:-(
Swali:- Si MAHALI popote na WAKATI wowote ni wa CHAI hata katika ya CHAI?
SAMAHANI NILITAKA KUSEMA:- SI labda mahali POPOTE na WAKATI WOWOTE MPEKECHO -dhambi KIMPENYEZO inaweza kupenyeza na kugusagusa eneo au tu kutekenya hata kidude hata kwa watiwao majaribuni na PAJA bila kuona PAJA?
Ndio,...... labda ni kwa MAPENZI YA MUNGU TU,...... kuna atakaye piga kambi au kuchezea midoli MBINGUNI!:-(
Ni wazo tu hili KAMANDA na samahani kama kimkwazo nimefanikisha!:-(
Hebu R.E.M waachie- Losing My Religion
Au tu R.E.M wapunguze kwa kitu kwa-Everybody HURTS
-
TISHA TISHA ina MIPAKA na LABDA ndio maana HATA utishie UKIMWI ,ngono hatuachi NG'OOO!:-(
Posted: November 10, 2011, 3:15 pm by SIMON KITURURU
Funzo kutoka kwenye TAHADHARI za hatari za UVUTAJI SIGARA ziwekwazo kwenye PAKETI za SIGARA , sigara yenyewe au hata kwenye MATANGAZO ya SIGARA zaonyesha kuwa ,...
......WATAKAO KUVUTA SIGARA asilimia za kutosha TU,...... watavuta tu SIGARA hata kama wanajua na WAMETAHADHARIWA kuwa uvutaji wao SIGARA utawapatia SARATANI ya MAPAFU.:-(
Swali:- Kwani unafikiri WAVUTA BANGI wangapi huacha kuvuta bangi kwa tahadhari wapewazo kuwa BANGI huleta KICHAA?
- SI walevi wanajua POMBE si CHAI?
- Na kwani unafikiri swala la NGONO PUMBAVU kuwa chanzo cha uenezaji UKIMWI latisha wahusudu NGONO asilimia ngapi ambao wanafanya kazi katika N.G.O . za ``TISHATISHA UKIMWI UNAUA´´ ambao kazi yao ni kinyume na NGONO pumbavu waendekezazo wakati wako katika ZIARA za kikazi ya KUELIMISHA watu watishike na UKIMWI?
Ndio,....... na labda TISHATISHA inamipaka yake KIMAFANIKIO,...... kwa kuwa kwanza WATU TWATISHIKA kwa vitu tofauti kitu kifanyacho hata UCHOCHORO ukutishao ule wenye GIZA kwa mwingine ndio mahali pazuri pakujibanza BILA WASIWASI kiofisi ya kazi maalumu kwake ya UPORAJI waogopao HUO uchochoro.:-(
Swali:- AU?
Ndio,...... TISHATISHA ina MIPAKA katika KUTISHIA kitu mtu,...... kwa kuwa labda pia kwa baadhi kilengwacho kutumika kama TISHIO ilikusitishwa ,...... hichohicho ndicho kifanyacho MAISHA ya MLENGWA kuleta MAANA.:-(
Swali zaidi:- Na si wakati mmoja anatishia mtu atakufa labda kuna ambaye ALENGWAYE NA KUTISHIWA KIFO ambaye kufa ndio kitu kiletacho maana KWAKE na ni poa kwa kuwa NAAMINI ndio staili ya kwenda mbinguni kiaina?
Ndio,....... ukikosea WAKULENGA na ulengacho kama TISHIO ,.......... KITISHO CHAKO chaweza kuwa ni KICHEKESHO kwa kuwa UTISHACHO NACHO kwake hukitambua kama Ze COMEDY.:-(
NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu DJ JESUS aanzishe kwa-Homem Casado
Tuga Agressiva na Titica waongezee dozi ya pambio kwa - MOTO
Halafu Gata Agressiva wazime kwa - Fula Mupepi
-
Ya KINYAA CHA MTU kisa katika STORI na PICHANI bata kaharisha!
Posted: November 10, 2011, 2:30 pm by SIMON KITURURU
KINYESI kwenye PICHA itiayo KINYAA mtu ,...... kama tu kwenye STORI za WATU zitiazo KINYAA mtu ,........huwa HAKINUKI ingawa kwa kuwa kuna wenye KINYAA,......... hata stori za USHUZI TU kuna wakunjao USO utafikiri wamenusa harufu MBAYA,.......eti WANAKINYAA.:-(
Swali:- SI umestukia harufu nyingi ni za KUFIKIRIKA kutokana na MAZOEA tu yafanyayo watu hata KISAIKOLOJIA WANUSE na kufananisha na wajuavyo VYATIA KINYAA kitu kifanyacho wafanikiwe kusikia KINYAA?
- Na si umestukia YA PICHANI bado KIAINA labda yako kwenye hiyo PICHA TU kama ya SIMULIZI yawezavyo kuwa kwenye SIMULIZI TU na kihalihalisi kwako hayapo na hutakutananayo?
Ndio,.......KIAINA,...... ya SIMULIZI kama tu yalivyo kwenye TV/LUNINGA,....... ayapayo MAISHA na kuyafanya yawe HALIHALISI / YA KWELI hata kwa KIKUHUZUNISHA kama sio KIKUTIA KINYAA,...
.... labda ni WEWE mwenyewe kwa jinsi uyaoanishavyo na HALI HALISI itiayo KINYAA.:-(
Swali:- Si ili hata utishike na SINEMA ya KUTISHA labda yahitaji uoanishaji wako wa UONACHO na KUSIKIA na ujuacho KINATISHA kwenye UBONGO WAKO?
Na ndio,...
.....LABDA kinyesi kisipooanishwa na mavi na MKULIMA ,.......kwa MKULIMA hicho hugeuka MBOLEA NZURI tu na wala isiyotia kinyaa na itafutwayo kwa juhudi KABISAAA BILA KINYAA kwa ajili ya bustani ya NYANYA za KACHUMBARI uipendayo!:-(
Ni wazo tu hili MKUU!
Meiway hebu aanzishe upya kwa - Les Genies Vous Parlent
Halafu hebu tu Vusi Mahlasela arudie-When You Come Back/Ndakupenda Sana
-
Katika TAFAKURI za wafikiriao KUISHI MIAKA MINGI ni KUFAIDI MENGI kiaina!
Posted: November 10, 2011, 2:13 pm by SIMON KITURURU
Ndio,...... kuna WAHURUMIWAO pia na KUHUZUNIKIWA kwa kuwa,...... hawakula CHUMVI nyingi kabla ya kuanza kivyao kwa staili ile ya KUDEDI.:-(
Swali :- Si kuishi MIAKA MINGI kwa WENGINE maana yake ni``JAMAA LILIFAIDI LILE ?´´
- Katika HAMU YA KUISHI miaka MINGI umewahi CHUNGUZA matatizo ya WALA CHUMVI NYINGI?
- Lakini si KUISHI miaka MINGI maana yake pia ni KUZEEKA sana kitu ambacho kuna WASIOPENDA?
- Si kwa kula chumvi nyingi kuna warudiao NEPI tena?
Na labda,...
.... kuna WASAHAUO kuwa KUISHI KUREFU labda wala sio TIJA na FARAJA kwa AISHIYE MAISHA MAREFU hasa kama AFYA na HALIHALISI ya KIMAISHA ndio HIVYO TENA kitu kifanyacho labda KUISHI KUREFU kukawa maana yake ni KUTESEKA kwa muda MREFU kiaina.:-(
Swali KIAINA:- Unakumbuka kufaidi VIWEZEKANAVYO sasa hivi hasa UKIZINGATIA miaka izidivyo labda VIWEZEKANAVYO SASA uviwezavyo kuvipindia mgongo yawezekana ikawa ni tatizo kuwezananavyo baadaye kisa UMRI wafanya mgongo unauma?
Ndio,....... kuishi kwingi ni KUONA mengi,........ kitu ambacho pia LABDA ni kuongezea muda wa KUJUTIA URUKAVYO kufanya sasa hivi UVIWEZAVYO SASA HIVI ambavyo havitawezekana siku UKILA CHUMVI NYINGI.:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu Baaba Maal abadili wazo na aanzishe upya kwa - Miyaabele
Baaba Maal azime - Three Little Birds
-
Jumuiya ya Afrika yang'ara ndani World Trade Market Uingereza
Posted: November 10, 2011, 1:30 pm by SIMON KITURURU
Salam,
Leo ilikuwa ni siku ya jumuiya ya Afrika mashariki ambayo hufanyika kila mwaka katika maonyesha ya WTM hapa nchini Uingereza. Kwa kawaida sherehe hizi hufanyika katika banda la nchi ambayo ni mwenyekiti wa Afrika Mashariki, kwa hiyo mwaka huu tafrija hii ilifanywa kwenye banda la ndugu zetu wa Kiburundi.
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVEAsamoah Gyan alipotembelea Banda la Tanzania Asamoah na wapenzi wake kutoka Tanzania Bw Meena. Bw Issa. Mh A. Jihad Naibu Balozi Chabaka, Jonathan Frank, Bw Issa na Bi Jestina Mwenyekiti wa bodi ya utalii ya Uganda akiwa na Bw William Byeruhanga Mh Jihad akiwa na wafanyakazi wa Bodi ya utalii ya Zanzibar Waheshimiwa Ephraim Kamuntu, Najib Balala na Victorie Ndikumana Waziri Maige na Naibu Balozi Chabaka wakipokea zawadi ya mpira Waziri wa Utalii na Mali asili Mh Ezakiel Mahige
Nimetumiwa na:Frank Eyembe wa Urban PULSE Creative -
Tangazo:TEENSPOT MAGAZINE !! ON SALE .. WE DO IT FOR THE YOUTH
Posted: November 10, 2011, 1:27 pm by SIMON KITURURU
-
DR. REGINA KAPINGA AIPEPERUSHA VEMA BENDERA YA TANZANIA NDANI YA BILL AND MELINDA GATE FOUNDATION.
Posted: November 9, 2011, 5:25 pm by SIMON KITURURU
DR. Regina Kapinga
Mama Regina (Program Officer of Bill & Melinda Gate Foundation) ni Mtanzania wa kwanza kuchaguliwa kuwa Staff wa Bill and Melinda Gate Foundation.
Kutokana na Elimu na uzoefu aliokuwa nao katika kufanya kazi kwenye Taasisi za kimataifa, Taasisi ya kimataifa inayomilikiwa na Tajiri mkubwa Duniani Bill Gate ambaye ni mmiliki wa kampuni kubwa ya technolojia ya Microsoft ikaona imtumie katika kuweza kusimamia shughuli zote zinazohusu misaada mbali mbali katika mabara maskini Duniani, yaani Afrika na Asia.
Watanzania tunakutakia afya njema ili uweze kuitangaza zaidi Nchi yetu, tunaamini kupitia wewe Taifa letu litafaidika na misaada mbali mbali kutoka kwenye Foundation hiyo.
Nimetumiwa na:Henry KAPINGA wa KAPINGAZ Blog. -
PSPF YAPEWA TUZO KWA KUTOA MIKOPO YA NYUMBA KWA WASTAAFU
Posted: November 9, 2011, 5:04 pm by SIMON KITURURU
Wafanyakazi wa PSPF wakifurahia tuzo waliyoipata baada ya kukabidhiwa na wazirei wa kazi na Ajira Bi. Gaudensia Kabaka wakati wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii iliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam jana tuzo hiyo ni kwa kutambua juhudi za mfuko huo katika kutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama wake wanaokaribia kustaafu.
(Picha na Mpigapicha wetu)
Waziri wa Kazi na Ajira Bi. Gaudensia Kabaka akimkabidhi kaimu Mkurugenzi wa PSPF .Bw.Adam Mayingu tuzo ya kutambua juhudi za PSPF katika kutoa mkopo wa nyumba kwa wanachama wake wanaokaribia kustaafu wakati wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii iliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam jana
(Picha na Mpigapicha wetu)
Waziri wa Kazi na Ajira Bi.. Gaudensia Kabaka akijaza fomu ya uhakiki wa wastaafu wakati alipotembelea banda la PSPF katika maonesho ya Wiki ya hifadhi ya Jamii Mnazi Mmoja Dar es salaam jana Kabaka ni mmoja wapo wa wastaafu wa PSPF kushoto ni Ofisa wa Fedha Mwandamizi Bw. Victor Luvena
(Picha na Mpigapicha wetu)
--
Rajabu Mhamila 'Super D'Photojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930 +255774406938 Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
Nimetumiwa na :SUPER D -
KOCHA WA MCHEZO WA NGUMI SUPER D KUHUDHURIA KOZI YA KIMATAIFA YA NGAZI YA JUU YA MCHEZO HUO
Posted: November 9, 2011, 4:27 pm by SIMON KITURURU
Rajabu Mhamila 'Super D'
Na Mwandishi wetu
KOCHA wa timu ya ngumi ya Ashanti ya Ilala na Mkoa wa Kimchezo Ilala, Rajabu Mhamila 'Super D', ameteuliwa kuhudhuria mafunzo ya ngumi yaliyoandaliwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).
Miongoni mwa makocha wa ngumi watakaoshiriki mafunzo hayo, ni mpiga picha wa Magazeti ya Business Time inayochapicha Magazeti ya Majira, Sports Starehe na jarida la Maisha, Mhamila ambaye maarufu kwa jina la Super D.
Super D mbali na kuwa kocha wa ngumi na mpiga picha, pia ni bondia wa zamani wa ngumi za ridhaa na kulipwa.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, alisema kozi hiyo itawahusisha makocha wa mchezo wa ngumi nchini kuanzia Novemba 12, mwaka huu hadi 20, ambapo itafanyika wilayani Kibaha, Pwani.
Mashaga alisema Mkufunzi wa kozi hiyo atatoka nchini Algeria, ameteuliwa na Chama cha Ngumi Ridhaa cha Dunia (AIBA), ambapo makocha 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara, wameteuliwa kushiriki.
Mashaga alisema makocha hao wamechaguliwa kwa kuzingatia mchango wao katika ushiriki wa matukio mbalimbali ya BFT, hasa mashindano kwa kuleta timu au mikoa yao kushiriki mashindano mbalimbali yaliyoandaliwa na BFT.
"Baadhi ya makocha hao, walipata mafunzo ya awali yaliyoandaliwa na BFT, watakaofuzu mafunzo haya, watatambuliwa na kuingizwa katika kumbukumbu za AIBA," alisema Mashaga.
Alisema makocha hao wataweza kufundisha mchezo huo popote duniani na kuruhusiwa kushiriki mashindano yote ya kimataifa kama makocha katika mashindano yatakayoandaliwa kwa kufuata sheria za AIBA.
Alisema kwa uzoefu wao BFT, wanategemea mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo, kutakuwa na ushindani wa uhakika kutoka kwa makocha hao.
Mashaga alisema kwa msingi huo, wanatarajia kupata ushiriki wenye tija katika mashindano kufuzu kushiriki katika mashindano ya Olimpiki 2012, London Uingereza.
Nae Super D aliongezea kwa kusema kozi hiyo imekuja wakati muafaka kwa kuwa dhamira yake ni kukuza na kuendeleza mchezo wa ngumi kimataifa Super D ambaye sasa ni muandaaji wa mafunzo ya ngumi kwa njia ya DVD ambazo huwa anaweka matukio mbalimbali ya mapambano ya ngumi za Dunia wakiwemo Floyd Mayweather, Manny Pacquiao,Mohamedi Ali, David Haye, Mike Tyson na wengine wengi . DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi Ilala na klabu ya Ashanti nayo ya ILala.
Ciao...
--
Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930 +255774406938 Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
Nimetumiwa habari na:Super D -
R.I.P HEAVY D!
Posted: November 9, 2011, 8:44 am by SIMON KITURURU
Dwight Arrington Myers aka HEAVY D(May 24, 1967 – November 8, 2011)
R.I.P Dwight Arrington Myers!Kazi zako bado nazisikiliza!
Hebu tujikumbubshe moja ya kazi zake-Nuttin' But Love
-
Je tukubali moja ya sifa ya UTANZANIA ni kuwa WOGA na sio tu wa SERIKALI na VYOMBO vyake?
Posted: November 8, 2011, 9:32 pm by SIMON KITURURU
Moja ya kisababishacho asilimia kubwa ya watu kuwa ma-ANONYMOUS kwenye hata michango ya maendeleo mitandaoni ni WOGA wa kuhusishwa na wawazacho.
Watu huogopa VISASI hata bila kujua kama kuna ukweli kutakuwa na kisasi kama uwazacho kinatofautiana na WATAWALA wawazavyo kitu kilichozaliwa enzi za Rais Nyerere ambapo ilijengeka kuwa ukipingana naye hukuweka nje ya mtandao usisikike . Ingawa kuna waliofika kutumia maneno kama ``Uta KOLIMBWA wewe) ikimaanisha mpaka uhai wako huweza kuwa hatarini kama ikijulikana hukubaliani na UTAWALA.
Watu huogopa kuonekana WAJINGA kwa kusema kitu hadharani labda kutokana na tokea watoto tunaimbiwa madhara yakuwa wajinga na labda na mpaka viboko kuchapwa kosa likiwa ni ujinga. Madhara yake hata wajuao vizuri yenye hekima na busara wako KIMYA kwa kutojiamini na WAJUAVYO ili wajije hakikishia umma kuwa WAJINGA.
Na moja ya sababu karibu MAJUKWAA yote ni wachache huchukua muda kuchangia hoja pamoja na kwamba labda mtandao ni ghali na muda hautoshi,... sbabu kubwa bado mimi naamini ni WOGA. Woga wa kujiharibia kitu ingawa nasikia kujiharibia kazi aka MLO ni kitu kiongozacho.
Na yasemekana hata kwa kisingizio cha Utamaduni/Mila na desturi . Watanzania ni waoga hata kuonyesha wamempenda mtu hadharani ingawa UKIMWI na magonjwa ya zinaa bwelele yanaonyesha PENZI kivitendo linagidwa kimadhubuti
Kuna ule uoga wa hata kumsema/kumtukana mtu hadharani ingawa vifanywavyo kwa siri vina ushahidi HADHARANI hata kwa kupitia mapenzi yetu ya UDAKU yafanyayo vyombo vya udaku kushamiri. Kupigana majungu ambayo ni moja ya dalili za WOGA, .....nk
Tukiachana na hilo:- SI nasikia ni MPIRA wa miguu tu ambao WATANZANIA wengi sio waoga kuambatanisha MAJINA yao na Wafikiriacho kuhusu YANGA na SIMBA?
- Si nasikia kisiasa bado ni swala liogopwalo na wengi bado hata kujulikana vizuri wanawaza nini kwa kuhofia isijeharibu ulaji?
- Na ni kiadoado tu maswala ya JAMII mengine huamsha MIJADALA na hasa yakiongozwa na swala la kijamii la MALAVEDAVE ingawa staili ipendwayo katika mijadala hii pia ni ile ya mtu kutotaka kujulikana ni nani?
Naendelea kuwaza!:-(
Hebu Pepe Kalle arudie- Simplicite
Au tu Tshala Muana azime kwa- Benga Nga Na Respect
-
Action! Developing the Commonwealth's cinematic culture -HORACE OVE na ZINA SARO WIWA
Posted: November 8, 2011, 8:53 pm by SIMON KITURURU
Kwa apendaye sinema zitengenezwazo na Watu weusi,...
.... deku,...
Katika nanihii:
Ndio ,.... ZINA SARO WIWA ni binti ya Ken SARO WIWA yule jamaa mwanaharakati aliyeuawa na Jenerali Sani ABACHA kwa kuwa mwiba katika swala la uharibifu wa mazingira ufanywao na SHELL.
Horace Ové pamoja na mengine,...
.... yeye ndiye (kwa ung'eng'e) Guinness World Record HOLDER for the first Black British film-maker to direct a feature-length film, Pressure (1976)
Kipengele katika kazi za Zina Saro WIWA,......kazi iitwayo..
This Is My Africa.
Ni mtonesho tu huu KAMANDA! Siku NJEMA! -
R.I.P Joe Frazier
Posted: November 8, 2011, 5:53 pm by SIMON KITURURU
Joseph William "Joe" Frazier (January 12, 1944 – November 7, 2011)
R.I.P Smokin' Joe!
Bado mie nacheki kazi zako za enzi za ...
Habari zaidi cheki HUKU
...au ..
Joseph William "Joe" Frazier -
Sherehe za siku ya Kuzaliwa Mwanzilishi wa Dini Ya Sikh Guru Nanak
Posted: November 8, 2011, 5:07 pm by SIMON KITURURU
Salam,Maelfu ya wafuasi wa dini ya Sikh walijitokeza siku ya Jumapili tarehe 6 Novemba 2011 katika mjini wa Southall, Middlesex UK ili kusherekea siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa dini yao Guru Nanak aliezaliwa mwaka 1469 nchini Pakistani.Wakati akiwa na umri wa miaka 30 alipotea kwa hali ya miujiza kwa mda wa siku tatu. Alipo rejea alianza kuhubiri, kufundisha na kuandika dini ya Sikh wakati maisha yake yote. Pia Guru Nanak alisafiri dunia nzima kuitangaza na kujadili dini hii kwa waumini wengine kama waislamu pamoja na HindusKwa Miaka zaidi 550 wafuasi wa dini hii wamekua na desturi hii ya kusherekea siku moja kabla ya kuzaliwa kwake Guru Nanak kwa kuandaa maandamano haya makubwa ya Sherehe hii ambayo hufanyika India pamoja na baadhi ya sehemu za nchi ya Uingereza. Kwa kawaida sherehe hizi huongozwa na wafuasi wakuu watano wanaojulikana kama ''Panj Piare'' wakiambatana waimbaji, wanamuziki na timu ya wacheza upanga (Martial Arts) kuelekea hekaluni kwao ''Gurdwara'' Sri Guru Singh Sabha, hapa Southall hekalu lao ndio kubwa kuliko yote katika bara la ulayaSherehe hizi huanza mapema asubuhi kwa kuimba, kuomba kwa pamoja. Baadae chakula cha kitamaduni kinachojulikana kama ''Langar'' hutolewa bure kwa kila mtu.Maandamano ya Southall yanaitwa Nagar Kirtan,Asanteni,URBAN PULSE CREATIVE
chakula kilikuwa bure kwa kila mtu.halaiki ya kubwa ya waumini wa dini ya Sikh wakisherekea .Hata watoto nao walikuja kusaidia kutayarisha chakula.Southall Palikuwa hapatoshi.wadau wakiwa kazini kutayarisha chakula.wakati wa kupata mapocho pocho.Frank akiwa katikati ya mitaa ya Southall kushuhudia sherehe hii .Maandamano yakiendelea.Waumini wa dini ya Sikh wakiazimisha siku hii .Frank akipata chai ya tangawizi na iliki kutoka India.Muasisi wa Dini ya Sikh Guru Nanak.
Nimetumiwa na :Frank Eyembe -
Tuff rec yafanya wimbo wa miaka 50 na wasanii wa Morogoro
Posted: November 7, 2011, 8:27 pm by SIMON KITURURU
Studio ya Tuff Records iliyopo mjini Morogoro,Katika kushehelekea Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.katika sherehe hizo Tuff Records yawakusanya wasanii wa kizazi kipya ambao ni wapya katika tasnia ya muziki,ikiwa kama kuonesha umoja wao katika taifa.Wimbo huu ni kwajili ya watu wote wenye upendo na inchi hii. Ni kwa ushilikiano na blog ya CHUMA (BFL) http://bongoflavalink.blogspot.com
WASANII WALIO SHILIKI KATIKA NYIMBO NI:
NellyTuff Rec Ft Nelly Crizy, Man Fair, Nasreal, Malale,GS, Big Poppa, Raz Q, Roberly &Young Steve
Mtayalishaji wa muziki
GQ- 0657659969
WIMBO:
TUNAWEZA(MIAKA 50)
STUDIO:
TUFF RECORDS
kwa mawasiliano: +225 712 222244Tuff Rec Ft Nelly Crizy, Man Fair, Nasreal, Malale, GS, BIG Poppa, Raz Q, Roberly & Young Steve - Miaka 50 Ya Uhuru (Prod By GQ).mp3
9320K Play Download
Nimetumiwa na:Salim Chuma -
Unamkumbuka CARLOS the JACKAL?
Posted: November 7, 2011, 6:14 pm by SIMON KITURURU
Carlos the Jackal
Kuna kipindi ilikuwa ukiongelea maswala ya ugaidi au hata ya ``Terrorism´´ jina lake lilikuwa maarufu kuliko Bin Laden maeneo fulanifulani .
Naona anakesi mpya tena huko UFARANSA huyu jamaa iliyoanza leo.
Jikumbushe kama umemsahau huyu Ilich Ramírez Sánchez aka Carlos the Jackal.
Katika kujikumbusha zaidi kiaina kisimulizi za Wamagharibi kuhusu Carlos,...
-
CHAMA CHA NGUMI DUNIA (AIBA) KUWAPIGA MSASA MAKOCHA WA TANZANIA
Posted: November 7, 2011, 6:00 pm by SIMON KITURURU
BOXING FEDERATION OF TANZANIA (BFT)
SLP 15558 DAR ES SALAAM 6/11/2011 Email; bft.tanzania2009@gmail.comTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI; YAH;KUFANYIKA KWA MAFUNZO YA KIMATAIFA KWA WALIMU WA MCHEZO WA NGUMI ZA RIDHAA TANZANIA 12-20 Nov 2011 KIBAHA PWANI.Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) wameandaa mafunzo kwa walimu wa mchezo wa ngumi Tanzania.Kozi hiyo itafanyika kuanzia tarehe 12-20 Nov 2011 Kibaha, Pwani katika shule ya Filbert Bayi.Mkufunzi katika kozi hiyo ni kutoka Algeria,aliyeteuliwa na Chama cha ngumi cha Dunia (AIBA)Jumla ya washiriki ni 30 wamechaguliwa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara kuja kuhudhuria mafunzo hayo, kwa kuzingatia mchango wao katika ushiriki wa matukio mbali mbali ya BFT hasa mashindano kwa kuleta timu au mikoa yao kama makocha na kujihusisha kikamilifu katika shughuri mbalimbali zinazohusu kuendeleza mchezo wa ngumi TanzaniaZaidi makocha hao tayari walishapata mafunzo ya awali yaliyoandaliwa na BFT.Baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo washiriki watakaofuzu watatambuliwa na kuingizwa katika data base za Chama cha ngumi cha Dunia [AIBA]Pia wataweza kufundisha mchezo wa ngumi popote Duniani na kuruhusiwa kushiriki mashindano yote ya kimataifa kama makocha kwa mashindano yote yatakayo andaliwa kwa kufata sheria za AIBA.Kwa uzoefu sisi kama BFT tunategemea mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo,tunategemea kupata ushindani wa uhakika kutoka katika mikoa iliyopata nafasi ya ushiriki,na tunategemea kupata timu ya Taifa ya ngumi yenye sura ya kitaifa tofauti na awali ambapo wachezaji wengi walitokea DAR ES SALAAM na hasa katika vyombo vya ULINZI NA USALAMA.Kwa msingi huo sasa tutategemea kupata ushiriki wenye tija katika mashindano mbalimbali ya kimataifa hasa kufuzu katika ushiriki wa timu yetu ya Tanzania katika mashindano ya Olimpiki 2012 London Uingereza.Na mashindano mengine ya kimatafa.Makore Mashaga.KATIBU MKUU BFT. Mob; 0713588818. Email;mashagam@yahoo.com
--
Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930 +255774406938 Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania -
THREE DAYS REMAINING CAST YOUR VOTE NOW FOR SWAHILI FASHION WEEK 2001 AWARDS / ZIMESALIA SIKU TATU PIGA KURA YAKO SASA KATIKA TUZO ZA SWAHILI FASHION WEEK AWARDS 2011
Posted: November 7, 2011, 5:35 pm by SIMON KITURURU
THREE DAYS REMAINING CAST YOUR VOTE NOW FOR SWAHILI FASHION WEEK 2001 AWARDS / ZIMESALIA SIKU TATU PIGA KURA YAKO SASA KATIKA TUZO ZA SWAHILI FASHION WEEK AWARDS 2011
FEW DAYS HAVE REMAINED FOR THE VOTING LINES OF SWAHILI FASHION WEEK AWARDS 2011 TO BE CLOSED, VOTE FOR YOUR FAVORITE TIME RUNS OUT SO QUICKLY. DON'T EVER TRY MISS THIS FASHION EVENT AS IT IS BEING THE BIGGEST FASHION EVENT OVER EAST AND CENTRAL AFRICA
ZIKIWA ZIMESALIA SIKU CHACHE HADI KUFUNGWA KWA NJIA ZA KUPIGA KURA KWA AJILI YA TUZO ZA SWAHILI FASHION WEEK 2011 WEWE KAMA MUWEZASHAJI WA TUZO HIZI MPIGIE KURA YULE UMPENDAYE NA UNAYEONA ANAFAA KUSHINDA. USIJARIBU KUTOKUWA MMOJA WA WASIOPIGA KURA JIVUNIE MAVAZI YA KIAFRIKA KWANI HILI NI ONESHO KUBWA LA MAVAZI AFRIKA MASHARIKI NA KATI
PIGA KURA YAKO SASA HAPA: www.swahilifashionweekawards.blogspot.com
Nimetumiwa habari hii na:Esi Mgimba -
PSPF YAKABIZI MSAADA KWA KIKUNDI CHA WALEMAVU CHANG'OMBE
Posted: November 7, 2011, 5:30 pm by SIMON KITURURU
Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma PSPF, Bi.Fatma Elhady (kushoto) akimkabidhi msaada wa hundi ya shilingi milioni 1.5 Bi.Dominion Apiyo wa Kikundi cha Walemavu cha Little cha Chang'ombe wilayani Temeke,Dar es Salaam jana(.Picha na mpigapicha wetu)
--
Rajabu Mhamila 'Super D'Photojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930 +255774406938 Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
Nimetumiwa habari na : Rajabu Mhamila. -
Boko Haram
Posted: November 7, 2011, 10:10 am by SIMON KITURURU
Najaribu sana kuwaelewa hawa jamaa wa NIGERIA wa Jama'atu Ahlis Sunna Lidda'awati wal-Jihad
...ingawa mpaka sasa ni kwa bila mafaninkio.
Cheki moja ya kazi zao...
Naendelea kuwaza! -
SIKU ALIYOFARIKI BIBI TITI MOHAMED, MMOJA WA WANAWAKE WALIOKUWA WANAHARAKATI WA UKOMBOZI WA TAIFA LETU
Posted: November 7, 2011, 9:27 am by SIMON KITURURU
Bibi Titi Mohamed enzi za uhai wake.
Hapa akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Bibi Titi Mohammed (1926 - 5 Novemba, 2000) alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania. Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika.Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere.
Juu ya kutolewa kwake, Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wa kisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlani.Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi ameonekana kwenye makaratasi ya chama tawala kama "Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".Mnamo tar. 5 Novemba, 2000 Mohammed amekufa kwenye hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.Moja kati ya mabarabara makubwa ya mjini Dar es Salaam yamepewa jina la Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.
Nimetumiwa na:Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog. -
ALFEO SILUNGWE AKIITANGAZA TANZANIA KATIKA MOJA YA PRESENTATION ZAKE INDIA.
Posted: November 7, 2011, 9:17 am by SIMON KITURURU
Alfeo Silungwe Mtanzania anaye piga Nondo ya Masters of Statistic ndani ya Nchi ya India akiwa anafanya presentation katika moja ya kozi anayo isomea chuoni hapo.
Nimetumiwa na:Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog -
Mahojiano Maalum Kutoka Kwa Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Posted: November 7, 2011, 9:06 am by SIMON KITURURU
[www.youtube.com]
Salam,
Wakati tunapokuwa tunajiandaa kuelekea katika sherehe za miaka 50 ya uhuru Urban Pulse Creative watakua wanakuletea mtiririko wa Mahojiano maalum kutoka kwa Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili kutuelimisha na kutupatia changamoto mbalimbali zinazozikabili taifa letu. Hii ni sehemu ya kwanza ya Mahojiano hayo.
Asanteni Sana,
URBAN PULSE CREATIVE
Nimetumiwa na:Frank Eyembe -
Jinsi jina la SEHEMU ZA SIRI za BINTI FULANI lilivyogeuka kuwa TUSI!
Posted: November 7, 2011, 3:02 am by SIMON KITURURU
Tupo wengi tupendao sehemu za siri za mabinti fulani,...... lakini SEHEMU ZA SIRI za wanawake tuwapendao bado KIJINA ni TUSI.
Swali:- Na si nasikia mapaka kwa baadhi ya WANAWAKE hutumia jina la sehemu maridhawa ya sili ile ya chini ya kitovu yenye kusaidia mapaka kukojolesha binti kama TUSI?:-(
Na sehemu za siri za kike zile nizipendazo kama wengine tu wapendao kunanilii kama mimi mara kwa mara halihalisi ikiruhusu,...
.... hizo zinamajina mengi ingawa kwa bahati mbaya ili utukane KWA MAFANIKIO ,.......sio kila jina la KIPENGELE HIKI ni TUSI.:-(
Swali :- Si unakumbuka ili kitu kizuri kama UKE ilikigeuke TUSI labda yahitaji atukanwaye kutafsiri mpaka jina la ANDAZI kuwa sio ANDAZI kihivyo?
NDIO,....... labda tusi ni TAFSIRI,....... ndio maana maka kitafsiri za watu kipengele TAMUKUNOGA ni tusi pia.:-(
Ni wazo tu hili KAMANDA!Jumatatu njema MKUU!
Hebu Mighty Sparrow aanzishe kwa - Wood in De Fire
Mighty Sparrow aongelee yaonglewa kuwa - Sparrow Dead
Mighty Sparrow adai - No, Doctor, No
Mighty Shadow a- Roll de Bumbalum
Shadow aachie-Obeah
Mighty Shadow amwage -Tabanka
Baron aingilie kati kwa-Come By Me
Baron adai-Sweetness is My Weakness
Au tu turudi tu TANZANIA ili Dr Remmy azime kwa-Nalilia MTOTO
-
Katika kufupisha`` SHENZI´´
Posted: November 6, 2011, 8:17 pm by SIMON KITURURU
``KIREFU´´ kuna wasiosikiliza,...... na pia hata WASIOSOMA ya MUHIMU kwa kuwa tu eti yako ``KIREFU´´.:-(
Swali:- Si kama REFU lahitaji UREFU basi labda acha tu liwe REFU?
Na kwa kuwa kuna WAFUPISHAO ``kifupi´´,...... isije tu kuwa ``KIFUPI´´ maana yake nayo KIMAANA imefupishwa na kuwa fupi!
Swali:- SI kifupi bado huhitaji kuwa bado ni kitu kizima?
Ndio kuna vipufishwavyo ,....... na labda ni vifupi kwakuwa sio vitu vizima kiujazo!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu tu BILAL aanzishe tena kwa-SOUL SISTA
Bilal aongezee - Fast Lane
Halafu tu BILAL azime kwa - Sorrow Tears and Blood
-
KWA KUWA si kila avutaye SIGARA hufa na SARATANI ya MAPAFU,.....
Posted: November 6, 2011, 5:56 pm by SIMON KITURURU
..... Lakiiiiniiiii!
Na sio kila MALAYA hupata magonjwa yaambukizwayo kwa UASHERATI,........... Lakiiiiniiiiii!
Na sio kila KICHAA alaye majalalani huugua kipindupindu,....
..... LAKINIIIII!
Swali:- SI nanihii isababishayo NANIHII si kila ANANILIYE hufanikiwa kuwa na NANIHII na ndioa maaana sio kila mfanyakazi bora ana MSHAHARA MZURI na sio kiala ananiliwaye hupata MIMBA?
NI nanilii tu hiii BINGWA na wala usikonde.
Hebu AL GREEN abadili NANILII kwa ndude- Love and Happiness
Al Green kwa kuwa ni JUMAPILI kikristo adinye pia - Too close to heaven
Hebu Extra Large waingilie kati na kuturudisha ZIMBABWE kwa - Muti Wemusango
Xtra Large waongezee ya - House Girl
Wadodose ile ndude -MUROORA
Au tu hapahapa ZIMBABWE Xtra Large wazime kwa -Kushamura Newe
-
Sayansi ya KUCHAPA m-TOTOZ!
Posted: November 6, 2011, 5:26 pm by SIMON KITURURU
Ndio,....... naamini VIBOKO Wabongo wengi wamekula katika makuzi yao..
...hebu tudeku .....Science behind physically disciplining children.
Fundamentalism & Corporal Punishment
Breaking the Will of the Child
Social Science & Corporal Punishment- Introduction
Cultural Attitudes Toward Children
Scientific Evidence
Denial-"I was spanked & I'm Okay."
Spanking: Spare the Rod or Spare the Child
Discipline Without Hitting
Training Parents
Spanking kids in Zambia
Swali:- Ushawahi kulichapa totot lako?
- Kwani ni MIKUBWA mingapi ushawahi kufikiri inafaa kutandikwa?
- Ushawahikulichapa kubwa zima na kama hujawahi ni kwanini?
- Unafikiri ZE MZUNGUZ na Ze WABONGOZ ki kifimbocheza hufundikishwa tofauti kitu kifanyacho ze MBONGOZ kuchapwa na Ze MZUNGU kuchapwa ni vitu tofauti?
Ndio,...... kuna mikubwa MIZIMA ichapanayo PIA,....... na eti kisa katika matumizi hayo ya mikanda au fimbo ni KITENDO ndani TU tendo la penzi.:-)
NI mtonesho tu huu MKUU! -
Katika HAMU ya VIJISENTI!
Posted: November 4, 2011, 5:02 pm by SIMON KITURURU
Ndio,...... yasemekana hakuna BINADAMU aliyezaliwa FISADI,...... na yoyote yule anaweza kuwa FISADI kitu kiwekwacho uzito na ukweli kuwa karibu MAFISADI wote uwajuao wenye VIJISENTI vya WIZI au hata tu ambao wanalia ofisini huku bado hawajastukia kuwa waliavyo ofisini ni WIZI;...
... bado ukweli uko palepale kuwa WAINGIAO OFISINI ambazo zina FWEDHA,......huwa yasemekana hujistukia HUMOHUMO ofisini kuwa wanapenda VIJISENTI na kama KIUHASIBU wamestukia hawatastukiwa WAKIDOKOA ,...
....hujichukulia vyao MAPEMA huku wengine wakiahidi WATAENDA KUTUBU makanisani au tu kwa MIUNGU YAO baadaye!:-(
Swali:- Unauhakika hutaki VIJISENTI?
- Unauhakika VIJISENTI vikigalagala mbele zako hutadokoa kama hatutajua?
- Lakini si unakumbuka pia hata yaliyowazi kama TITI na MWANA kuwa sio kila mtoto azaliwaye hupenda TITI la MAMA na ili ale kikunyonyeshwa ni bonge la shughuli kwa MAMA mnyonyeshaji?
Ndio,..... labda kumbuka tu tena kuwa,......karibu asilimia mia ya mafisadi hawakuzaliwa MAFISADI,...... na hustukia tu kuwa wamegeuka MAFISADI baada ya kuanza kuitwa MAFISADI,........LAAAKIIIINIIII!!:-(
NDIO ni wazo tu hili NGULI!Ijumaa na WIKIENDI NJEMA Mheshimiwa!
Hebu COSTULETA aanzishe upya kwa - Do Milindro
COSTULETA apenyeze kachumbari zaidi tena na - LADJUM
Costuleta apandishe mita za dozi zaidi kiujazo kwa - Tchiriri
Au tu tusiende mbali Dj Anjo Negro aingilie kati na kuzima kwa miondoko hiihii ya KUDURO kwa ndude pana kikishimo ile -Chuco Chuco
-
Katika CHANGAMOTO zaidi : Hawa washindi wa NOBEL akina BERTRAND RUSSELL na EINSTEIN kuhusu Sir GOD/MUNGU
Posted: November 4, 2011, 4:30 pm by SIMON KITURURU
Bertrand aanzishe
Einstein amalizie...
-
Leo katika CHANGAMOTO:Stephen Fry
Posted: November 4, 2011, 3:44 pm by SIMON KITURURU
Getting out of the I-Mode
Philosophy, Logic And Reason /Importance of unbelief
Au cheki pia kuhusu SELF- PITY -
Leo katika UCHOKOZI: Hebu KARY BANKS MULLIS ( Nobel Prize winning American biochemist)adai hakuna ushahidi H.I.V inasababisha A.I.D.S.
Posted: November 4, 2011, 2:59 pm by SIMON KITURURU
Kuhusu jamaa huyu NGULi kisayansi,...
.. mgugo tuu au kiaina bofya hata HAPA
Hebu tumsikilize yeye na wengine...
Blah blah blah
Fish cakes
Alas a fish cake.
Yet more fish cakes
Guess what ... yeah ... fish cakes.
The end of the fish cakes