SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • Na kwa kuwa LEO yaaminika ni JUMATATU kwa wengi!

    Posted: October 24, 2011, 4:39 am by SIMON KITURURU
    Kumbuka tu kuwa,....... KALENDA ifanyayo jana ni JUMAPILI na juzi ilikuwa ni JUMAMOSI,......... ni kitu kilichotungwa tu na WATU kama WEWE,......... kitu kifanyacho labda bado kama tu enzi za mababu zilizokuwa hazifuati KALENDA hizi,......JUMATATU HII kwako ni JUMATANO ya mwaka jana kwa mwingine.

    Swali la kizushi:
    • Unakumbuka KIISLAMU leo ni MWAKA gani?

    Ni angalizo tu hili MHESHIMIWA na usikonde!:-(

    Hebu BILAL aanzishe upya kwa-FREE


    Nottz aingilie kati kwa - Shine So Brite


    Shafiq arudi na Bilal katika pini- Cheeba

    Nottz na Bilal warudi tena kwa- Right Here


    Au tu tena Amerie azime kwa - 1 Thing

  • WAMAREKANI bwana kwa kukasifia kanchi kao bwana- ETI kanchi kao ni ``THE GREATEST PLACE on EARTH!´´

    Posted: October 23, 2011, 6:35 pm by SIMON KITURURU
    Haki ya nani ukisikiliza WANASIASA wa MAREKANI wakisifia MAREKANI,...... unaweza kudhani MAREKANI ni nusu MBINGUNI kwa jinsi wanavyopasifia na pia kusifia WAMAREKANI kama wao ni watu bomba sana na SPESHO hapa DUNIANI ,...
    ....mpaka unaweza kuelewa fununu ZA KITU  hata bila ya  kuhoji WAENDEKEZAO UMAREKANI hata bila kufika MAREKANI kwanini labda kuna  uwezekano WAPO waaminio  WAMAREKANI wakienda haja zitengenezwazo na malighafi CHAKULA,...... labda watoacho kihaja kubwa ni  karibu na keki au angalau kwa wapenda ubwabwa wanaweza hisi tokeo lao la ya msalani AREKANI AKIENDA KUJISITIRI ni PILAU.
    Lakini: 
    • Umestukia ukiongea na MSWISI ,.....au MFINI hata tukiruka nchi nyingine unaweza kukuta na wao wanaamini nchini kwao ndio BOMBA zaidi na wanafundishana hivyo hata katika porojo za hapa na pale na kama kunakasoro wanaamini ni kwa sababu WAGENI nchini kwao ndio wanawaharibia NCHI?
    • Na si unastukia sie kwetu hata kitu kirahisi kujivunia kama Mlima KILIMANJARO tunashindwa kuutetea kuwa uko Tanzania na  nasikia kuna Watanzania kibao kama hailazimiki wanakwepa kujitambulisha kuwa ni Watanzania huko ughaibuni kisa hata waowenyewe wanashindwa kujivunia TANZANIA?



    Ndio ,..... na labda ni JANJA moja wapo,........ kujisifia wenyewe hata ki-PROPAGANDA kama wafanyavyo WAMAREKANI,...
    ...lakini:
    • Ukijivunia TANZANIA ya leo si kunawatakaoamini tu kirahisi UNADANGANYA?
    Ndio,....... wenzetu hata KIPOROJO za uongo kikuombea KURA ,........wanajivunia sana KWAO na kudai kuwa kwao ni ``THE GREATEST´´!

    Ni wazo tu hili kiangalizo MHESHIMIWA!:-(



    Hebu Kassav waingilie kati na kubadili mchezo kwa ndude kimchanganyiko yenye -OH, MADIANA


    Kassav bado kipaza sauti kikishikiliwa na Jacob Desvarieux wapandishe dozi kwa - Mwen Malad Aw

    Hebu ndani ya KASSAV huyu Jean-Claude Naimro ashike kipaza sauti tena katika- Ave'w Doudou


    Ndani ya KASSAV mdada Jocelyne Béroard zamu yake ashike kipaza sauti na kurudisha-SIWO



    Au tu kundi zima la KASSAV wazime tu manyanga   kwa-Tim Tim Bwa Sek
  • UNAKUMBUKA Mapinduzi ya TUNISIA yalianzishwa na MMACHINGA aliyejichokea na sio WANASIASA au WASOMI wale FULU kujifanya WANAJUA KILA KITU?

    Posted: October 23, 2011, 3:32 pm by SIMON KITURURU

    WATUNISIA wakibeba picha ya mchoro ya Mohamed Bouazizi(29 Machi 1984 – 4 Januari 2011)




    Desemba 17 Mmachinga Mohamed Bouazizi aliyekuwa na miaka 26, alijichoma moto kupinga ukandamizaji katika mji wa Sidi Bouzid na kufia kwenye hospital huko Ben Arous, Tunisia baadaye.

    Machinga huyo aliamua kujichoma moto mbele ya ofisi za serikali baada ya kunyang'anywa MATUNDA na MBOGAMBOGA alizokuwa anauza na kunyanyaswa na maafisa wa mji na mgambo wao kwa madai kuwa hana kibali cha kufanya umachinga kitu kilichomfanya aone hakuna haja ya kuishi katika mazingira ambayo kujitafutia riziki kihalali kwa kufanya biashara ndogondogo bado mtu ananyanyasika na kuporwa hata kamtaji.

    Kujichoma kwake ndiko kulifanya Wananchi karibu Tunisia nzima kuamua wamechoka na matokeo yake ni mpaka serikali ya Rais Zine El Abidine Ben Ali ikaanguka -kitu ambacho kikaeneza wananchi kudai mapinduzi karibu Uarabuni kote.

    MADHUMUNI ya TARALILA hii ni KUKUMBUSHIA TU kuwa:
    • Saa nyingine cheche za mageuzi huanzia usikokutegemea na usishangae kuwa labda si WANASIASA watakao geuza nchi hata ya TANZANIA.
    • Na labda uwadharauo wanaweza kuwa ndio kiini katika ukombozi wako.

    Ni angalizo tu hili MHESHIMIWA!JUMAPILI NJEMA KAMANDA!


    Vyanzo vya stori ya Mohamed Bouazizi unaweza kugugo tu au nenda kwa Aljazeera;
    ...donoa HAPA,...
    ....au hata bofya
      HUKU

    Hebu MICHAEL JACKSON atutie majaribuni kwa kumsifia KIDOSHO wa KILIBERIA katika-Liberian GIRL


    Au tu Michael Jackson azidi kubembeleza kidosho kwa - Give In To Me

  • JERRY NASHON na MOHAMED GOTAGOTA jukwaani

    Posted: October 22, 2011, 11:07 pm by SIMON KITURURU
    ``Mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni mwa 90, ungefika kuanzia saa nane mchana, siku ya Jumapili, katika Ukumbi wa Vijana Hostel (ukumbi unaopakana na Mango Garden), ungekuta vijana wameanza kukusanyika wakisubiri saa tisa mchana ambapo Vijana Jazz walikuwa wakianza muziki. Siku hiyo ilifahamika kama.....´´

    ...DUH endelea ,.......HUKU



    Kundi zima la VÍJANA JAZZ  Jumapili moja wakiwemo Mohamed  Gota Gota......... bila kumsahau .Jerry Nashon Dudumizi ,..... kwa  ya zaidi tena BOFYAAAA--
    www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.comwww.johnkitime.blogspot.com
    Nimetumiwa na NGULI:John Kitime
  • Umestukia kuwa ukweli ni kwamba kibinadamu ,BINADAMU labda hawezi kusaidia kila MTU?

    Posted: October 22, 2011, 9:00 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,......unaweza kujitahidi uwezavyo  LAKINI,...
    .... na ukigundua KUSAIDIA  haki ya nani tena  kuwa  ni KUJISAIDI mwenyewe...
    ... waweza kukuta UCHOYO mtu afanyao  wa hata kumnyima MTU mwingine kubenjuka au kubenjua kidude  ,...... LABDA ni jinsi tu mojawapo ya MTU kujinyima kutobenjuka mwenyewe!:-(
    Swali:
    • Si unakumbuka  mmoja wa ahitajiye MSAADA  wa WATU wengine  ni yule idhaniwaye ndiye asaidie  kitu kifanyacho MIMI au WEWE  ... au hata YULE  aaminiye  anaweza yote la bda kwa hilo ndio hasa kidhihirisho kuwa anakwalifai aka ndiye MUHITAJI MSAADA zaidi ambao  labda  tena ule mkubwa ambao ni wa MAWAZO kama tu si o tu jinsi ya  KUWAZUA wazo?
    • Kwani unaamini ni kweli STAREHE ni kujipa MWENYEWE?

    Ndio,...... ukichunguza  au hata KUJICHUNGUZA ,...... unaweza kustukia labda unakosea kustukia ni nani ahitajiye MSAADA kwa kuwa  pamoja na YASIYO MATATIZO yako ,......labda BADO AISEE astahiliye msaada  kwako kiwewe KABISAA ,.......sio MBWA na wala sio PAKA wako kwa kuwa bado tatizo ni LAKO!:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


    Hebu tena Isley Brothers waingilie  tena kati kwa -Summer Breeze

    MC Hammer aulizie tena - Have You Seen Her

    Mc Hammer abadili kwa kukumbushia-U can't touch this


    Naughty By Nature waingilie kati tena kwa -OPP

    Naughty By Nature waongezee kipengele kwa - Hip Hop Hooray

    Au tu Naughty By Nature wazime tena kwa -Feel me flow

  • MAISHA ni MIKIKIMIKIKI na Ray Njau!

    Posted: October 22, 2011, 8:19 pm by SIMON KITURURU


    Ndio ,..... RAY NJAU  yupo ,...... na ukitaka kujua zaidi kwanini MAISHA NI MIKIKIMIKII...bofya HUKU

    Ni hilo tu MUUNGWANA!
    Tukiachana na hilo ,......hebu Patrick Balisidya,...... aturudishie MIKIKI  kikusiliba  NANIHII kwa kipengele kile cha   -WIKIENDI

    Au tu MAKASSY adai tena-MAMBO BADO

  • EMU THREE na DIARY YANGU --Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-40

    Posted: October 22, 2011, 8:06 pm by SIMON KITURURU

    Adamu alibakia kwa muda ameshikilia simu mkononi, utafikiri bado anasubiri kuongea na huyo mtu aliyekwisha kuongea naye karibuni, lakini walikuwa wameshamaliza kuongea, ….kilichomfanya aduwae kwa muda ni hzio taarifa alizozipokea kwa huyo aliyempigia simu, …ilikuwa kama mtu kamtonesha kidonda kilichokuwa kimepona…Hakuamini kabisa kuwa Rose kawa na mwanaume mwingine, …

    ...ENDELEA na stori tamutamu ,...HUKU ,...... ambako ndio KIJIWENI KWAKE huyu NGULI .
    NI HILO tu MKUU!

    Tukiachana na hilo ,...... kimselebuko tuendelee,...... tu na  Linton Kwesi Johnson aanzishe upya kwa ushairi -More time

    Linton Kwesi Johnson aulizie tena - Want Fi Goh Rave ?



    Linton Kwesi Johnson akumbushie - It Dread Inna Inglan


    Linton Kwesi Johnson aongezee kukumbushia - Sonny´s Lettah

    Mutabaruka aingilie kati nakuongelea tena -Dis Poem


    Mutabaruka apandishe dozi jazba kwa -It no GOOD


    Gregory Isaacs alainishe kwa - Out Deh



    Halafu huyu huyu  Gregory Isaacs ajaribu kuzima kwa - Good Morning


    Halafu tu eti  Barrington Levy ndiye azime kwa - Black Roses
  • JONAS SEGU na DEO NJIKU wapima uzito kwa ajili ya KUZIDUNDA JUMAPILI HII MOROGORO.

    Posted: October 22, 2011, 7:22 pm by SIMON KITURURU








    Bondia Deo Njiku wa Morogoro akipima uzito uwanja wa Jamuhuri leo kwa ajili ya mpambano wa kuwania
    ubingwa wa taifa wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) utakaofanyika kesho..

    Kushoto ni mpinzani wake Jonas Segu na promota wa mpambano uo Alifa Kipao..


    ( Picha na HABARI :  www.superdboxingcoach.blogspot.com)





    Kocha wa mchezo wa ngumi Nchini Rajabu Mhamila ' Super D Boxing Coach' katikati akiwainua mikono juu mabondia Deo Njiku wa Morogoro kushoto na Jonas Segu wa Dar es salaam baada ya kupima uzito katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro leo kwa ajili ya mpambano wa kuwania ubingwa wa taifa wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) utakaofanyika kesho jumapili.

    (Picha na habari : www.superdboxingcoach.blogspot.com)





    Nimetumiwa PICHA na HABARI na:

    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.com Mob;+255787 406930         +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
  • Video nyingine ya enzi za TANCUT ALMASI ORCHESTRA(1989)

    Posted: October 22, 2011, 5:00 pm by SIMON KITURURU




    ´´Ninakwenda safari, safari yenyewe safari ya kikazi,
    Ninakwenda safari, safari yenyewe ya masafa marefu,
    Najua hapa utabaki, watasema mengi,
    Pia wabaya wetu mama watafurahi.
    Chorus
    Safari sio kifo mama iyeeo
    subiri ntarudi mama iyeoo




    Nikirudi mama nipokee kwa mikono miwili
    Nikirudi mama nitakuletea zawadi
    Zawadi nono mama watototo
    Iyee mama iyee...``

    Haya tena TANCUT ALMASI ORCHESTRA(1989), wakiwa jukwaani live Tancut Club Iringa wakiporomosha kibao MASAFA MAREFUBofya HAPA--
    www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.com
    www.johnkitime.blogspot.com


    Nimetumiwa na:John Kitime
  • Watakacho WATU hata kama hakileti MAANA kwako, LABDA maana iko ndani ya lao TAKWO!

    Posted: October 22, 2011, 4:30 pm by SIMON KITURURU
    Na tatizo kubwa la WASOMI au tu wajuao mpaka  wanapitiliza na kudhania wanamiliki kujua hata TAKWO  la watu wengine,...
    ..... yasemekana ni kutumia miakili yao  KUOANISHA  KULETA MAANA kwa KITU  na  KUTAKWA kitu.:-(

    Swali:
    • Unabisha?
    • Hujastukia kuna watu wanaamini watakavyo na wewe inabidi kiaina uvitake hivyo vidude?
    • Si kuna vielewekavyo  na kuleta maana kwa wengine tu hasa kwa kuwa wao sio wewe?

    Ndio,...
    ... utakacho,...
    ... labda  ni muhimu kukumbuka kuwa labda hicho kidude hata kama ni DINI au tu tako kuwa  kwa wengine haki ya nani  hicho kidude HAKINA MAANA.:-(
    NI wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

    Hebu Keith Sweat aanzishe tena upya kwa - Twisted



    Marving Gaye arudie-Sexual Healing


    Donell Jones adai- U know what's up

    Au tu R. Kelly azime tena kwa - Ignition
  • Leo katika CHAKULA cha AKILI!

    Posted: October 22, 2011, 4:00 pm by SIMON KITURURU
    Think Different



    Bob Marley - Redemption Song


    Jumamosi njema MKUU!
  • 1st FASHION AWARDS TO BE DONE IN EAST AND CENTRAL AFRICA FROM SWAHILI FASHION WEEK 2011- VOTE FOR YOUR FAVORITE

    Posted: October 22, 2011, 3:30 pm by SIMON KITURURU



    Hello everybody, Swahili Fashion Week 2011 introduce to you Fashion Awards. Please we have mention the Categories at the Right side of the website Vote for your Favorite. Is simple go to the Box tick on the dialog box of your favorite nominee, then down click vote,you canonly vote once to any Category of your choice . Votes start now until 10th November 2011. Please invite others to vote too. Thank you all in advance and for being part of SWAHILI FASHION WEEK

    To vote click this Link : www.swahilifashionweekawards.blogspot.com
    Nimetumiwa na :Esi MgimbaSwahili Fashion week 2011
  • PRESHA za WEWE kuwa kama WALE na MIMI kuwa kama WEWE zivalishavyo chupi UHURU binafsi!

    Posted: October 22, 2011, 3:00 pm by SIMON KITURURU
    Kuwa HURU ASILIMIA MIA kwa MIA wakati uko hai,....


    .....labda  hilo ni ALINACHA tu a.k.a JAMBO la kufikirika tu,........ hasa  kwa kuwa  WEWE ni WEWE na uhuru wako labda wahitaji  uhuru kwa kuwa kuna watu WENGINE!!:-(
    Swali:
    • Umestukia  kuwahuru  NI SWALA  lakufanyia kazi SIKU  hadi SIKU, dakika hadi DAKIKA  hasa kwa kuwa  WEWE ni WEWE  na  uhuru WAKO unasababishwa pia na uwepo wa wengine ambao huna MAMLAKA ya WAFIKIRIAVYO au hata uwepo wao?

    Ndio,........ labda MOJA  ya kifichacho watu  kuwa  hawako huru,...  ... ni  imani zao tu  kuwa WAKO HURU  na ya WENGINE  hayawaathiri  kitu ambacho labda nacho ni ALINACHA tu KIHALIHALISI!:-(


    Ni wazo tu hili KAMANDA!:-(






    Hebu tena The Isley Brothers waingizie - Contagious


    The Isley Brothers waongezee dozi tena kwa - Secret Lover


    Au wazime tu tena kwa -Between the sheets
  • Kwenye FANI,...

    Posted: October 22, 2011, 2:25 pm by SIMON KITURURU
    .... labda wasioko  ndani ya FANI waongeleao fani   kiaina ni WAZUSHI!:-(
    Swali:
    • Si labda ya KILOKOLE  ayajuayo vizuri  hata kuyaongelea kiundani  ni MLOKOLE ayaishiyo hayo ya KILOKOLE  kilokole?

    Ndio,....... labda  hata ya KIMALAYA,......mtaalamu wa fani ni MALAYA,....... na abwabwajaye ya KIMALAYA asiye MALAYA  kwa asilimia nzito tu  yawezekana  afanyacho na aongeleacho  kina  UZUSHI!
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na ni  ruksa kulibishia!:-(
    Hebu Mick Jagger na Lenny Kravitz wadai -God give me everything I want

    Led Zeppelin waingizie - Black Dog


    Halafu AC /DC wazime kwa -Thunderstruck

  • Katika jitihada za kutofautisha WATU na WANYAMA PORI wakati bado LIBYA iko MAWAZONI!

    Posted: October 21, 2011, 5:14 pm by SIMON KITURURU
    Kuna wakati wanyama wanaeleweka ni kwanini,...
    ... wanafanya wafanyavyo  hata kama wafanyacho KIBINADAMU ni  unusaji wa bonge la kinyeo.:-(,...
    Hebu tuwadeku  na kushuhudia  kielewekacho,....

    Na WANADAMU  na UTASHI wao,....... kuna waelewao labda  na kutetea kuwa kifanyikacho na WANADAMU mara kibao ni UTU kwa kuwa wafanyao ni WATU na sio UNYAMA  kwa kuwa kuna vigezo   watendao wanaongea na kuvaa chupi na suruali kama sio sketi  huku wakijiita WATU kwa kuwa wanadai wanaakili kuliko WANYAMAPORI  wanajua hata KIMANENO kuwa MATUSI  akitukana Simon Kitururu NI NINI ingawa kiutu  ukifikiria unaweza  kutokwa ladha ya CHAKULA kama kitendwacho na WATU KINYAMA  kimdhuruye ni wewe ,...
    .... hebu tu tutembelee nchi ya  ZANZIBAR  iliyo jirani na TANGANYIKA kupata kifungua kinywa kwa kuwa kinapanda na atendwaye unyama sio sisi ,...
    ...na  kwa Breakfast  kutoka Zanzibar   tupate,...


    Kachumbari tupatie IRAN

    Dina ya Mchana  kiaina tupatie huku huku  IRAN


    Kianzio cha dina ya usiku twende Iraki kuchekelea Mtu anauawa:-(

    Dina yenyewe kwa furaha za kibinadamu tupate Libya wakati bado ya moto,...


    Ndio,...... kimkao fulani labda ,......TOFAUTI ya WANYAMA PORI na BINADAMU ,...... kiutu WANYAMA PORI wanaeleweka KIRAHISI na wafanyayo yana UTU kuliko WATU!:-(Swali:
    • AU?
    • Si unakumbuka kunibishia RUKSA?
    Na ni wazo tu hili MHESHIMIWA wala USIKONDE!
    Na labda tubadili wazo tu  HILI  NYOMI KIHUZUNI -``sasa tutafanyaje!?´´........ kwa ndude ``Napenda matako makubwa a.k.a Baby got back ´´,..........kama idadavuliwavyo kibinadamu  na -Sir Mix-A-Lot


    Halafu au tu Tone Loc aloki kipengele kwa - Funky Cold Medina

  • SWAHILI FASHION WEEK in ANGOLA ON 15/10/2011

    Posted: October 21, 2011, 3:50 pm by SIMON KITURURU
    Designer Gabriel Mollel from Tanzania during the Fashion Bussiness in Angola on 15th-oct-2011


    Designer Manju Msita from Tanzania during the Fashion Bussiness in Angola on 15th-oct-2011

    Mustafa Hassanali from Tanzania during the Fashion Bussiness in Angola on 15th-oct-2011

    Tanzanian Consul in Luanda HE Mziray Mbwana with Team Tanzania at Fashion Business Angola on 15 Oct 2011







    Nimetumiwa na:Esi Mgimba
  • AJALI YA NDEGE ILIYO TOKEA KILOMETA 15 KUTOKA UWANJA WA NDEGE WA KIA JANA USIKU.

    Posted: October 21, 2011, 2:41 pm by SIMON KITURURU



    Picha ya ndege iliyo dondoka ikitoka KIA usiku wa jana ambapo kulikuwa na Pilot aliye fariki dunia papo hapo anatambulika kwa jina la Ally na abiria mwengine ambae yupo KCMC kwa matibabu zaidi.

    Picha na HABARI:
     Latest news Tz Blog
    Nimetumiwa na:MDAU  wa Latest news Tz Blog
  • Kuna sababu Kichwa, NYONYO au hata KORODANI ingawa ni nzito kwa kawaida kwa MTU hivyo sio MZIGO!

    Posted: October 21, 2011, 1:30 pm by SIMON KITURURU
    KAWAIDA! Na  kwa kawaida kama mdada anaanza kuumwa MGONGO kisa  uzito wa NYONYO,....
    ... kama tu  kwa ALWATANI  ambaye kikorodani  mwendo siku hizi taratibu  kisa BUSHA  na  makende yamegeuka MZIGO,........ huo ni ushahidi tu  huyo Bin'ADAM abebacho  huyo  si KAWAIDA.:-(
    Swali:
    • SI kwa kuwa ni kawaida ndio maana Bin' Adam huwa hastukii kwa kawaida uzito wa hata  KICHWA  chake ingawa  kwa kawaida BICHWA ni kilo kadhaa kiuzito?

    Ndio,...
    ..... kama kwako hicho KITU  kwako ni MZIGO,...
    .... hata kama kwa jina hicho kitu ni MME WAKO,...
    .... labda  tayari hicho kitu  si KAWAIDA na JIVUE GAMBA Mwanakwetu  hasa kama  kwako  hilo si DHAMBI.
    Swali zaidi:
    • Lakini  si  inakumbukwa kuna mambo mengine kusikia UZITO kwayo ndio KAWAIDA?
    • Lakini si NZITO  ni kawaida ikiwa NZITO pia?

    Ndio,....... labda pia kama KITU kimebebeshwa mpaka MIMBA na bado uzito ni uleule,...... katika hilo   sio KAWAIDA,...
    ... kwa kuwa kuna vitu hata kama KIUZITO ni kimaumivu,...
    .... labda BINADAMU huhitaji kukumbuka kuwa hiyo ndiyo kawaida,...
    .... kama tu ilivyokuwa kama unaungua na husikii MAUMIVU hiyo si KAWAIDA!:-(

    Ni wazo tu hili  lilipopinda na kupiga U-turn kiaina  MHESHIMIWA!Ijumaa na WIKIENDI njema KIMAHUDUSHI PANGALA Mheshimiwa!
    Hebu  tubadili wazo tena kwa msaada wa SAM Mangwana katika kibao-Bana ba CAMEROUN


    Sam Mangwana aongezee tena dozi kwa -KABIBI


    Samba Mapangala aingilie kati kwa ku- Vunja Mifupa

    Pepe Kalle akatizie tena denge nakuachia  tena-MOYIBI


    Halafu PEPE KALLE azime kibatari kwa -Gérant

  • TWANGA PEPETA kusugua VISIGINO nchini UINGEREZA

    Posted: October 21, 2011, 12:02 pm by SIMON KITURURU
    Mkurugenzi wa Twanga Pepeta katikati Asha Baraka Akiongea na waandishi wa Habari Kuhusu Uzinduzi na Ziara UK




    Salam,

    Baada ya kufanya na Kumaliza uzinduzi wa albamu yao kabambe tarehe 6 Novemba 2011 ASET wakishirikiana na URBAN PULSE CREATIVE Wanatarajia kuwaburudisha wapenzi wa Bendi Maarufu ya Twanga Pepeta Nchini Uingereza mwishoni mwa Mwezi wa Novemba.

    Show Hii Maalum ni kwa ajili ya kuazimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Tarehe pamoja na maelezo ya Ukumbi yatafuatia mda sio mrefu. Hivyo wadau kaeni mkao wa Kula.

    Asanteni,

    Urban Pulse Creative.

    Nimetumiwa HABARI na :Frank Eyembe wa Urban Pulse Creative
  • Tamaduni za KUCHEKELEA KANYAU kwa kuwa MTU kafa ZIPO hata kwa uliowahi kuwaona katika MSIBA mwingine wanalia!

    Posted: October 21, 2011, 4:05 am by SIMON KITURURU
    Ndio,...... labda sijawahi kuchukia vizuri MTU,...... lakini kifo cha mtu mpaka leo hii hakijawahi kunifanya nirukeruke kwa FURAHA kisa mtu KAFA!:-(
    Swali:
    • Si umestukia watu huchekelea kanyau MTU akifa  kama wakiamini wanasababu kuwa MAREHEMU ni MTU mbaya?
    KIUNGWANA lakini,..... MAREHEMU daima  alikuwa ni MTU MZURI!:-(

    Swali:
    • AU?
    Naendelea tu KUWAZA!:-(

    Hebu Zap Mama aanzishe upya kwa - Mupepe


    Zap Mama aanzishe kuvimbisha mtekenyo kwa- Cou Cou


    Halafu labda Zap Mama atulize kwa - Yaku


    Kabla tu tena sijui kwanini Zap Mama hajazima kwa - Sweet Melodie

  • Katika ya watu yazaniwayo RAHISI, labda SI rahisi kwa kuwa ``THe deVIL iS in thE DetaiLS!´´.:-(

    Posted: October 21, 2011, 4:02 am by SIMON KITURURU
    Ndio,...
    ... MENGI kama huhusiki  katika kuyatimiza na unategemea MTU MWINGINE atimize huku ukidhania ni rahisi,...... labda  kumbuka tu USICHOKIJUA  hata kwa UMJUAYE,.......kama unadhania ni rahisi kwako haimaanishi kwa mwingine ni KIBONDE,.......kitu ambacho labda ndio maana SIO RAHISI wasiojua ``DETAILS´´ kuelewa  wafikiriavyo ni RAHISI kutimizwa na wawatumainiwao  watatimiza,...... kama tu labdaWATANZANIA wajuao miakili ya Rais MKAPA  halafu wakastukia hatimizi,......hutokea HAWATIMIZIWI huku wanashangaa hata KISIRI  kwa kuwa labda KIUKWELI  katika DETAILS labda katika shughuli za kiume kumshughulikia MWANAMKE kuna msenge ASIYEJULIKANA KATIKATI YA SHUGHULI ya KUMCHANUA MWALI  ki-DETAILS  aisee ikichunguzwa!:-(



    Swali:
    • Unabisha?

    Ndio,......  kuna vipengele kwenye MUWA,...... na kama  vipengele  aka VIFUNDO havipo,.......KIDETAILS labda ndio siri kwanini  MUWA hushindikana kuwepo  pia AISEE!:-(
    Ni wazo tu hili lilopinda kiduchu KAMANDA!:-(

    Hebu Gregory Isaacs abadili ndude KIWAZO kwa kugusia tena - My Only Lover




    Aguseguse- Substitute


    Atekenye -Hush Darling


    ...apapasepapase na ku- Cool Down The Pace



    Gregory Isaacs huyuhuyu ajaribu ku - Confirm Reservation


    Asiruke-Front DOOR


    ...abembeleze tena  kwa-Objection Overruled



    Au tu tena kiaina azime kwa -Not The Way

  • R.I.P MUAMMAR GADDAFI

    Posted: October 20, 2011, 9:12 pm by SIMON KITURURU
    Muammar Gaddafi  (7 June 1942-20 October  2011)


    R.I.P ,........na utakumbukwa na Wakupendao NA wakuchukiao PIA!
    Habari zaidi,.......HAPA





  • Kwa kuwa PILIPILI iliyoshamba yaweza kuwasha walio NYUMBANI kabla ya kuletwa NYUMBANI!

    Posted: October 20, 2011, 7:00 pm by SIMON KITURURU
    Swali:
    • SI kwa walioonja uchungu wa KLOROKWINI  katika mchakato wa kutaka  kutibu MALARIA walikuwa wanajua watasikia uchungu au mpaka kutapika kabla hata ya kuweka KIDONGE mdomoni kwa kuwa wanajua uchungu wake kitu kilichofanya baadhi wagundue kuchomeka vidonge vya KLOROKWINI kwenye NDIZI kabla ya kuonja UCHUNGU?
    • Na si ajuaye uchungu wa kuumngua na MOTO unaweza kumfanya asikie uchungu na kuanza kulia kwa kumtishia tu utamuunguza kwa kusogeza kaa la moto karibu na jichole?

    Ndio,..... labda unaweza kuwashwa na WASHAWASHA hata kwa mbali kama unajua tabu za kuwashwa,.......au TU TUKIRUKA MENGINE bado unajua finyofinyo kiwashawasha kinyoko ni NINI  kwako!:-(
    BADO ni wazo tu hili KAMANDA:-(
    Hebu Bruno M arudishe mtekenyo katika kutubadili wazo kwa -Dança dos Comba




    Bruno M aongezee dozi kwa - Thubilla

    Au tu sijui kwanini  Burning Spear akatizie denge,.......na kubadili mchezo kwa kusifia kwao kwa-Land of my birth


    Halafu huko huko kwao  Eric Donaldson aingilie kati kwa - Are you thinking of him



    Halafu  tu Eric Donaldson azime tu kwa -More love


  • FRANSIC MIYAYUSHO ajiandaa kumkabili MBWANA MATUMLA

    Posted: October 20, 2011, 6:24 pm by SIMON KITURURU


    Bondia Fransic Miyayusho (kulia) akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi na Badi Sachedina wakati wa mazoezi ya mwisho ya MIYAYUSHO  kabla ya kumvaa Mbwana Matumla katika mpambano wao wa ubingwa mwishoni mwa mwezi huu.
    ( Picha na habari: www.superdboxingcoach.blogspot.com)




    Bondia Fransic Miyayusho (kulia ) akiongoza mazoezi katika kambi yake ya lazima ukae iliyopo Kinondoni , Dar es salaam jana.  Miyayusho anajiandaa na mpambano wake wa ubingwa na Mbwana Matumla litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu.
    ( Picha na habari: www.superdboxingcoach.blogspot.com)




    Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) akielekezwa jinsi ya kutupa masubwi na Doi Miyayusho wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wa kuwania ubingwa na Mbwana Matumla utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu.
    ( Picha na HABARI: www.superdboxingcoach.blogspot.com)








    Nimetumiwa PICHA na HABARI na:

    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania
  • Trailer kuhusu Mahojiano ya Mh Waziri Mkuu MIZENGO PINDA

    Posted: October 20, 2011, 6:00 pm by SIMON KITURURU
    Salam,[www.youtube.com]Urban Pulse Creative wakishirikiana na Star tv wanakuletea Trailer ya Mahojiano Maalum na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofanya ziara nchini Uingereza hivi karibuni. Mahojiano haya yalikuwa yamelenga zaidi kupata ufahamu na uchambuzi wa namna serikali yetu ya Tanzania inavyofanya kazi pamoja na changamoto zake.
    Mahojiano haya yalifanywa na Baraka Baraka  Kutoka Urban Pulse na yatarushwa Hewani kupitia  kituo cha Star TV Jumapili ijayo Tarehe 30 octoba 2011 kuanzia saa 10.30 katika kipindi cha Medani za siasa.Tafadhali usikose kuangalia kipindi hiki ili upate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Tanzania na Serikali yetu.Asanteni,Urban Pulse Creative
    ...au deku...


    Nimetumiwa hii HABARI na:Frank Eyembe wa Urban Pulse Creative
  • AJALI MBAYA MKOANI MBEYA MAENEO YA MLIMA NYOKA KUELEKEA UYOLE

    Posted: October 20, 2011, 5:30 pm by SIMON KITURURU
    MAJERUHI WA AJALI HIYO MBAYA ILIYOTOKEA MBEYA JANA.
    MWILI WA MAREHEMU YUDA AMBOKILE UKIWA UMENASA KWENYE GARI.
    MAJERUHI MWENGINE ALIYE NUSURIKA KIFO





    STORY
    ..na Ezekiel Kamanga-MBEYA YETU.

    Jinamizi la ajali mbaya limeendelea kuusakama mkoa wa Mbeya ambapo usiku wa kuamkia jana imetokea eneo la Mlima Nyoka Uyole Jijini humo na kuua watu watatu akiwemo dereva wa gari hilo dogo Yuda Ambokile Jeshi la Polisi limethibitisha.

    Kaimu kamanda wa polisi Anacletus Malindisa anesema Marehemu wengine ni Peter Kishimba mwenye umri wa miaka 47 mkazi wa Tazara Iyunga na Joshua Sanga mwenye umri wa miaka 2 mkazi wa Uyole jijini Mbeya na ajali hiyo ilitokea majira ya saa Moja na nusu kwa kuhusisha gari Nne ambazo zote zilijeruhi watu waliokuwemo ndani yake.

    Wakizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kuharibika kwa gari aina ya Toyota Dyana yenye namba za usajili T 660 AUX ambayo ilikuwa imeegeshwa katika mlima huo.

    Walisema kuwa kutokana na kuharibika kwa gari hiyo ndipo gari dogo aina ya Suzuki Escudo yenye namba za usajili T 425 BAZ , iliyokuwa ikitokea barabara ya Mbarali kwenda Mbeya mjini ambayo ilikuwa na abiria watano iliigonga gari hiyo na kusababisha kifo cha Dereva wake Yuda Ambokile na wengine kujeruhiwa vibaya na magari mengine Toyota Cheser T 512 BCT na Nissan T 991 BAK.

    Baada ya gari hiyo kugonga gari iliyokuwa imeegeshwa na kusababisha madhara hayo ndipo gari nyingine aina ya Baloon ikagongwa na gari hiyo aina ya Escudo kisha Baloon hiyo ikatumbukia korongoni na kusababisha majeruhi wawili waliokuwemo ndani ya gari hiyo ambao wote walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na Mmoja wao akaruhusiwa baada ya hali yake Kiafya kuimarika.

    Ajali hiyo haikuishia hapo bali gari nyingine aina ya Pickup yenye namba za usajili T 991 BAK nayo ikakumbwa na dhahama hiyo ambapo iliharibika vibaya bila kusababisha majeruhi kwa watu waliokuwemo ndani yake.

    Majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutembelewa na waandishi wa habari leo, wengi wao walikutwa wakiwa na hali mbaya na kushindwa kuzungumza chochote bali baadhi yao waliokuwa na nafuu walisema kuwa walikuwa hawakumbuki chochote juu ya ajali hiyo zaidi ya kujikuta wamelazwa wakiwa na majeraha katika miili yao.

    Majeruhi hao ambao baadhi yao waliweza kuzungumza na waandishi wa habari ni pamoja na Denis Untwa (24) ambaye ni dereva wa Baloon, Laina John Sanga (35), Michael Mteve (20), Anania Simbeye(35) ambaye ni dereva wa Escudo, Emmanuel Tambikeni na mmoja aliyejitaja kwa shida jina moja la Boniface..

    Habari na (www.mbeyayetu.blogspot.com)


    Nimetumiwa HABARI na:Mdau wa MBEYA YETU Blog


    Poleni jamani MLIOKUMBWA na JANGA!R.I.P Marehemu Wapendwa!-Simon Kitururu
  • Kwa bahati mbaya TUKO WENGI tupendao kumsikiliza au hata KUMSOMA aongeleaye TUTAKAYO KUSIKIA!:-(

    Posted: October 20, 2011, 2:00 pm by SIMON KITURURU

    Na yasemekana UKWELI ni kwamba,...... kama tayari unajua UPENDAYO kusikia,........ labda hayo tayari unayajua kiasi cha kutosha kama ukiyafikiria MWENYEWE kiundani,..... na labda wakati huo ingekuwa busara KUSIKILIZA au hata kusoma usiyotaka KUSIKIA,...... kama nia ni kutaka kuendelea kujifunza kitu KIPYA!:-(

    Swali:
    • AU?
    Ndio,...... labda kuendelea kunogewa kusikia utakacho kusikia hata kama hicho ni kuwa WEWE ni MZURI KWELI,...
    ..... wakati huo yawezekana unajijua TAYARI wewe ni MZURI mwenye sura tamu kama PIPI na huo MUDA uendeleao kuutumia kurudia kusikia sifa zilezile za uzuri wako,....... KIBUSARA labda ungekuwa ni wakati wa kujifunza kwa uzuri wako HUO uchuneje buzi KIMALAYA au tu uuficheje ki SISTA wa KIKATOLIKI ili usidoewe na Wakware.:-(

    Swali zaidi:
    • AU?

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

    Hebu turudi UGANDA ili PHILLY LUTAAYA aanzishe upya kwa-Ndabye Ennake



    Philly Lutaya atukumbushe tena -Tugende e kampala



    Kabla tu huyuhuyu Philly Lutaaya hajazima kwa -Entebbe Wala
  • Kwa kuwa UTOTO wa MTU MZIMA ni kitu cha kuficha!

    Posted: October 20, 2011, 12:29 pm by SIMON KITURURU
    Watoto eti ni MALAIKA,...... lakini kubwa zima likiendekeza UTOTO sio tena UMALAIKA.
    Swali:
    • Unamkumbuka Michael Jackson?

    Ila lakujiuliza vizuri ni kwamba;.....
    ...Je utoto HUMUISHA Mtu MZIMA au utu uzima ni shule tu ya kumfanya MTU mzima ajizuie kufanya UTOTO?
    Ndio,.,...
    .....NAKUBALI,...
    ....kuna WADAU hunipa vidonge vyangu kuwa BLOGU hii imejaa UTOTO katika staili hii niitumiayo kuandika ya UjingaBUSARA.
    Swali zaidi:
    • Je si waliozeeka sana nasikia mambo zao hurudia kuwa kama ya kitoto?
    • Kwa hiyo Je UTOTO uzeeni  ni jambo la kujifunza tena au ni swala la kutojizuia tu tena kufanya yaaminikayo ni ya kitoto ?
    • Ushawahi kuona Mzee sana mambo zake halafu yakakukumbusha Mtoto?

    Ndio,......... labda UTOTO na UZEE  vyote ni MALAIKA.:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na Usikonde!:-(
    Hebu turudi KAMERUNI ili Sandra NKaké aanzishe tena kwa -Higher

    Sandra Nkake arudie pia - I miss my land


    Au tu Sandra Nkake azime kwa-H.A.P.P.Y

  • WASANII MNAVYOKAA KWENYE VIKAO VYENU NA BASATA NA HILI PIA MNALIONGELEA?

    Posted: October 20, 2011, 12:01 pm by SIMON KITURURU
    Msanii wa maigizo ya vichekesho JOTI akitoa changamoto ambazo anakutana nazo katika sanaa yake hiyo ya maigizo.
    Mzee Kipara hii ndio hali aliyofikia hivi sasa.
    Mzee Kipara ni msanii wa muda mrefu ambaye alikuwa katika sanaa ya maigizo kwa muda mrefu, kipindi cha hivi karibuni vyombo mbali mbali vya habari vilitoa hali ya afya yake.

    Kwa sasa hali yake bado ni mbaya, napenda kuwakumbusha tena wasanii wote msimtupe mzee huyu na mnavyoendelea na vikao vyenu na BASATA pia muweze kumuongelea Mzee huyu, ili kwa pamoja na Serikali mumsaidie. Napenda kuwashukuru wale wote waliojitahidi kumsaidia kwa namna moja au nyingine ili kuweza kumfanya Mzee huyu ajisikie ana watu ambao wanamjali, Mungu atawarudishia.

    Nimetumiwa HABARI na:Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog

    UGUA POLE Mzee Wetu!Na MUNGU akujalie Upone haraka!-Simon Kitururu
  • Tatizo la MAJIBU,....

    Posted: October 19, 2011, 6:47 pm by SIMON KITURURU
    ......huwa hayajibu kitu  baada ya MTU kujibiwa kama ajibiwaye,.........hayayafanyiikazi!:-(


    Ni angalizo tu hili  MKUU!

    Hebu Mbaraka Mwinshehe  arudie - Urafiki Mwisho Wa Mwezi


    Au MBARAKA MWINSHEHE aongezee dozi kwa  - Shida


  • Zawadi ya MAUA na WAAFRIKA!

    Posted: October 19, 2011, 6:40 pm by SIMON KITURURU


    Baada ya kukuta ZAWADI hiyo hapo  ya UA kwa DADA YASINTA,......HAPA..... .... nimejikuta najiuliza:
    • Hivi ni kwanini WAAFRIKA wengi UA kwao sio ZAWADI na kwa Wamagharibi ni lini MAUA yalipamba moto kuwa ni ZAWADI MWANANA?
    • Kwako UA ni Zawadi?
    • Kama sio KWANINI na kama ndio -Kwanini?




    Nawaza tu kwa SAUTI!
    Hebu tubadili wazo kwa kumuachia Wiz Khalifa  katika- Fly Solo



    Au Wiz Khalifa azime tu kwa - Black And Yellow

  • Matumaini katika kinga ya MALARIA!

    Posted: October 19, 2011, 2:00 pm by SIMON KITURURU



  • Wengine WAKUZUNGUKAO inawezekana sio tena WATU bali ni LUNINGA ,kompyuta na MAGAZETi ya UDAKU.

    Posted: October 19, 2011, 1:50 pm by SIMON KITURURU
     Wengine WAKUZUNGUKAO ,.... ... yawezekana ndio waathirio YAKO  UFIKIRIAYO na yakuzungukayo sasa hivi,...... hata ki uyatafsirivyo.

    Swali:
    • Kwani unafikiri WENGINE kwako bado NI WATU au tu  ni  VITU tena vya wengine hasa katika DUNIA HII ya leo ambayo VITU na MALI vyajaliwa kuliko UTU ? 
    • Si umeshawahi kusikia kuwa kuna watu kibao hata nchi zilizoendelea  WANYAMA kama Mbwa au paka na WATU  hakuna tena tofauti  kiwawafikiriavyo?
    • Na si  pia ukitaka kupima thamani ya MTU na KITU labda chunguza ni kwanini KIBAKA anaweza kutolewa roho  kwa kosa la kuiba  ndizi kitu kifanyacho labda MTU na NDIZI  au hata tukiita kidhaniwacho KIBAKA kakwapua ni POCHI - kwa watu wengine kiuthamani  UHAI  na KITU hakuna tofauti au kwa kuwa KIBAKA huuawa basi UHAI haunathamani kama KITU?

    Ndio,...
    ... labda ukifikiria,...
    .... WENGINE wakuzungukao na kuathiri ufikiriavyo,....
    ..... sio WATU tena moja kwa moja kwa kuwa UTHAMINICHO labda wala sio MTU.
    Katika kumbukumbu:
    • Unakumbuka  msemo HAPENDWI MTU pochi lako tu!?:-(
    Ndio,....... kwa wengine MTU  na KITU ,....... labda kiuthamani  hakuna tena tofauti kitu kifanyacho KITU kuthaminiwa ZAIDI.:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(





    Hebu  tupitie tena TOGO ili Afia Mala amwage - Baila Mi Musica


    Afia Mala aongezee dozi kwa - Ten Homte


    Halafu hapahapa TOGO hebu tena Afia Mala azime kwa- Segne

  • Daktari Mtanzania Julie Makani apokea tuzo kutoka Royal society Pfizer London

    Posted: October 19, 2011, 1:00 pm by SIMON KITURURU
    Salam,          

    Dr Julie Makani kutoka Tanzania amepokea Tuzo  jumanne tarehe 18 octoba 2011 ya Royal Society Pfizer nchini Uingereza. Dr  Makani amepokea tuzo hii ya utafiti alioufanya katika gonjwa hatari la Sickle Cell (SCD) ambaye makazi yake ya kazi ni kwenye Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi cha Muhimbili katika idara ya Haematology. Kutokana na utafiti wake kumeonekana ushahidi kuwa, chanzo kikuu cha magonjwa na vifo vitokanavyo na sickle Cell nchini Tanzania husababishwa na Arnemia (upungufu wa damu)

    Dr Makani pia amefanya mchakato wa matibabu katika majaribio ya Hydroxyure chemotherapy agent inayo gusa Bone marrow katika matibabu ya  Anaemia kwenye  ugonjwa wa Sickle Cell

    Ni matumaini yake  kuwa utafiti huu utapelekea kuboresha uchunguzi na matibabu ya ugonjwa huu ili kuweza kuimarisha afya za watu, mfumo mzima wa afya  na jamii kwa ujumla.

    Kwa niaba ya Watanzania  wote  Urban Pulse tunapenda kumpongeza  DR Makani kwa mafanikio hayo.

    Asanteni

    Urban Pulse Creative



    Dr Julie Makani akitoa machache

    Wageni waalikwa kwenye Royal Society Pfizer Awards London


    Kutoka Kulia Balozi Kallaghe, Mama Makani, Dr Makani, MP O'Brien, Naibu Balozi Chabaka na Mr Simba

    Dr Julie Makani akiwa na familia yake

    Dr Julie Makani Akipokea Tuzo yake


    Dr Julie Makani akiwa na Baba yake Mr Bob Makani pamoja na Mama Vicky Makani

    Parliamentary Under Secretary of State, International Development Stephen O'Brien. akimpongeza Dr Julie Makani

    Dr Julie Makani. akiwa na Cleo, Paul na Frank baada ya kupokea Tuzo.
    Nimetumiwa na :Frank Eyembe wa Urban Pulse Creative

    Hongera Dr Julie Makani!-Simon Kitururu
  • Katika KUMBUKUMBU: Hotuba ya January Makamba kijijini Tamota.

    Posted: October 19, 2011, 12:31 pm by SIMON KITURURU

  • Ya duni: UZURI

    Posted: October 19, 2011, 12:10 pm by SIMON KITURURU

  • YA DUNIA: Mwanamama KIUNO kama NYIGU!

    Posted: October 19, 2011, 11:56 am by SIMON KITURURU

    The Smallest waist in the World on a Living Person
  • Amka Kumekucha

    Posted: October 19, 2011, 10:49 am by SIMON KITURURU
    Ndio,...
    .....ni MAROON COMANDOS hao wakikuamsha

  • Leo katika konsipirasi: Did William Shakespeare write his own stuff?

    Posted: October 18, 2011, 9:30 pm by SIMON KITURURU
    Film claims William Shakespeare did not write his plays



    Excerpt from a mock trial of Shakespeare for literary fraud. James Boyle, Shakespeare's "lawyer," has just released a literary mystery called "The Shakespeare Chronicles" about the question -- Who Wrote Shakespeare.




    Ndio,...... kuna wadaio William Shakespeare siye aliyeandika ndude zijulikanazo kuandikwa naye ila kuthibitisha ndio KASHESHE.

    Ndio,...... SWALA hili NALO,......nimoja tu jingine nililokutananalo KIJIWENI !:-(
  • Kuna sababu WATU huongea tu,....

    Posted: October 18, 2011, 9:17 pm by SIMON KITURURU
    .... kwa wengi kugeuza kivitendo waongeleavyo ,....... hiyo ni shughuli nyingine kabisaa!:-(

    Swali:
    • Lakini umestukia si kila kitendo chahitaji ushawishi na kujituma sana kama ukichukulia mfano wa walevi katika kugeuza maongezi ya pombe kuwa kitendo cha kunywa pombe au wapendao uasherati kimaongezi kuyasawazisha kwa ufanisi na umakini kivitendo?

    Ndio,....... labda kuna sababu sie wengine kwa MENGINE ,....... tunaishia kuongea tu,...... kitu ambacho kirahisi huishia kuwa ni MANENO MATUPU tu!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
    Hebu turudi Haiti ili Michael Benjamin arudie - Ou Pati



    Au tupitie tena Madagascar ili MAMEHY wadinye-Madranto valin'olo



    Halafu hapahapa MADAGASCAR Vaiavy Chila azime kwa - Nagnini Anao Moa Zaho

  • Leo moja ya kilichozungumziwa katika pitapita zangu:Mormon religion and its roots.

    Posted: October 18, 2011, 8:42 pm by SIMON KITURURU
    Leo moja ya kilichozungumziwa katika pitapita zangu:Mormon religion and its roots.
  • YUSTA MSOKA, MWANASHERIA ALIYEFANIKIWA KUTIMIZA MOJA YA NDOTO ZAKE.

    Posted: October 18, 2011, 7:19 pm by SIMON KITURURU
    Advocate Yusta Msoka
    Yusta Msoka akiwa amesimama nyuma, mbele ya dirisha la pili upande wa kulia, akiwa katika picha ya pamoja na Wanasheria wenzake baada ya kula kiapo cha kuwa Advocate (Wakili)
    KAPINGAZ Blog inapenda kumpongeza sana Dada Yusta kwa kufanikiwa kufika hapo alipofikia, vile vile inamshauri asiishie hapo aendelee zaidi mpaka aweze kufikia level ambayo ni ya kimataifa.
    Kwa kutambua uhaba mkubwa wa Mawakili katika Taifa letu tunapenda kuwapongeza wale wote walioweza kufanikiwa kuwa Mawakili, tunawaomba wakafanye kazi zao kwa uadilifu na kuliletea sifa na mafanikio mazuri taifa letu, hasa hasa kuwa makini katika mikataba mikubwa ambayo taifa letu sasa linaangamia kutokana na mikataba hiyo. Nimetumiwa habari hii na:Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog

  • Mahojiano Maalum kati ya Mh Waziri Mkuu na Urban Pulse kurushwa na STAR TV

    Posted: October 18, 2011, 7:15 pm by SIMON KITURURU
    Mh Waziri MKuu Akifanya mahojiano na Baraka Baraka


    Salam,Urban Pulse Creative wakishirikiana na Star tv wanakuletea Mahojiano Maalum na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofanya ziara nchini Uingereza hivi karibuni. Mahojiano haya yalikuwa yamelenga zaidi kupata ufahamu na uchambuzi wa namna serikali yetu ya Tanzania inavyofanya kazi pamoja na changamoto zake.Mbali na hapo tulijadiliana kuhusu Majukumu ya Waziri mkuu, Chakula, Nishati, Jumuiya ya Afrika Mashariki na mchakato wa katiba Mpya kuelekea kuazimisha miaka 50 ya uhuru.Mahojiano haya yalifanywa na Baraka Baraka  Kutoka Urban Pulse na yatarushwa Hewani kupitia  kituo cha Star TV Jumapili ijayo Tarehe 30 octoba 2011 kuanzia saa 10.30 katika kipindi cha Medani za siasa.Tafadhali usikose kuangalia kipindi hiki ili upate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Tanzania na Serikali yetu.Asanteni,Urban Pulse Creative.


    Nimetumiwa na:Frank Eyembe wa Urban Pulse Creative
  • Leo katika kumbukumbu:EUGENICS

    Posted: October 18, 2011, 1:39 pm by SIMON KITURURU
    War on the Weak: Eugenics in America


    Dr. William Shockley on Race, IQ, and Eugenics


    Eugenics

    Kuna wadaio BILL GATES na misaada yake aangaliwe pia kwa jicho la waangaliao wanaoshabikia EUGENICS ,....

    ....Depopuation: Bill Gates And His Eugenics Lie



    Kama umesahau kuhusu hii NDUDE kwa jina EUGENICS ambayo ilitumika sana na HITLER pia katika kuamua ni WATU wa aina gani wanafaakuruhusiwa kutengeneza MIMBA ,...
    .... unaweza kuigoogle tu au BOFYA,.....HAPA
    JUA kitu,...... kama unataka kukabili KITU.Ni hilo tu MKUU!
  • AIBU GANI HII BADO INAENDELEA KULIKUMBA TAIFA LETU!

    Posted: October 17, 2011, 10:35 pm by SIMON KITURURU
    Jeshi la Polisi nchini (PT) kupitia Inspekta Generali wake Said Mwema(Pichani) imetangaza dau la Shilingi Milioni 5 kwa mtu yeyote atakaefanikisha kupatikana kwa mtu aliyemjeruhi mtoto Adam Robert (14) ambaye ni Albino huko Geita ambapo mtu asiyejulikana alimvamia mtoto huyo na kuanza kumkata kata mikono na kisha kutoweka na vidole vya Albino huyo.Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia mwishoni mwawiki katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang’hwale ambapo mlemavu huyo, Adam Robert (14), mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono wa kulia na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kushoto.Ni jambo la kusikitisha sana kuona vitendo hivi vinaendelea kutokea na mwisho wa siku jeshi linataka kutumia fedha za walipa kodi kwa ajili ya kuwapata wahalifu hao, mi nadhani hii njia sio sahihi, sidhani kama Jeshi la polisi wanashindwa kuwapata hawa wanaowatuma wahalifu kwenda kuwadhuru maalbino hawa. Jambo la msingi hapa sio kutangaza dau ni kuhakikisha wale wanaowatuma ndio wanakamatwa na ninaamini jeshi la polisi likishirikiana na usalama wa Taifa inawezekana kuwakamata hawa na kuwatokomeza kabisa, usalama wa Taifa wanafanya kazi gani kama sio pia na kuangalia usalama wa Watanzania hawa! Ni aibu kubwa kwa Taifa letu vitendo hivi vinavyoendelea.

    Nimetumiwa na:Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog
  • WAREMBO WA CHUO KIKUU KUTOANA JASHO JUMAMOSI HII

    Posted: October 17, 2011, 7:55 pm by SIMON KITURURU
      Shindano la kumsaka mrembo wa chuo kiu cha Kmpala International University 2011 litarajiwa kufanyika jumamosi hii katika ukumbi wa Savanna Lounge (quality center) uliopo barabara ya Pugu,jumla ya warembo 12 wamejitokeza kuwania taji hilo siku ya tarehe 22 octoba.Shindano litapambwa na wasanii wa kizazi kipya kipya Dully sykes,D-nob,Ngoma za asili na vijana wa kutikisika(shers),mabali ya burudani hizo kutakuwa na suprize ya majai pamoja masupastaa wa movie.Miss Kampala Internationa 2011 imeandaliwa na serikali ya wanafunzi ikishirikana na wadau maarufu wa mabo ya urembo na mitindo nchini Tanzania,tiketi za fainali hizi zinapatikana CLOUDS fM,CHUONI KWAO,JB BELMONT HOTEL,SAVANNA LOUNGE(quality center)kitchen hut (mlimani city) kwa iasi cha 10,000/= (regular) na V.I.P 30,000/=   Shindano hili limedhaniwa na Savanna Lounge hotel,Belmont hotel,clouds fm,Air Uganda na uniqueentertz blogspot.com


    NB:
      Bloggers wenzangu naomba tuwape sapoti wanachuo wenzetu udhamini wao haukidhi sana kila gharama hata mimi najitolea tu kwaajili ya jamii yangu





    Nimetumiwa na muhusika wa:http://uniqueentertz.blogspot.com/
  • SAKATA LA MGOMO WA WANACHUO WA IMTU UNIVERSITY HATMA YAKE LINI?

    Posted: October 17, 2011, 7:49 pm by SIMON KITURURU
    Geti kuu la kuingia Chuo kikuu cha Afya IMTU kilichopo Mbezi Beach.
    Wanachuo hao hapa wakiwa katika moja ya maandamano ya mgomo huo.
    Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr Shukuru Kawambwa
    Sakata hili lilitolewa miezi michache iliyopita na vyombo mbali mbali vya habari kuhusu mgomo huu wa wanachuo hawa.
    Ni jambo la kusikitisha sana kuona nchi ambayo ina upungufu mkubwa wa Madaktari, kushindwa kuumaliza mgomo wa Madaktari Wanafunzi ambao sasa umekamilisha miezi miwili, kundi hili la wanachuo limekuwa likikusanyika nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Elimu kwa vipindi tofauti bila hitimisho la mgomo huu.
    Kwa kutambua umuhimu wa wataalam hawa tunaziomba mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia na kuongoza  ziumalize mzozo huu ambao madai yao ya msingi ni kulipa Ada kwa Tshs na si US Dollar na pia kulipa ada kubwa tofauti na vyuo vingine vya binafsi (private).
    Sisi kama wanafunzi ambao tunaathirika na mgomo huu Bado tuna imani na Serikali ya Mh.Jakaya kikwete na watendaji wake wote, Katibu Mkuu Wizara ya elimu,Tanzania Commision of Universties na Higher Education Student Loan Board tunawaomba waumalize mzozo huu. Pesa nyingi zimetumika za walipa kodi kupitia loan board kuwakopesha wanafunzi hawa Tunahitaji sasa wote kwa pamoja kulishughulikia hili tatizo ili tuweze kuendelea na Masomo na mwisho tuende kujenga taifa letu changa lenye upungufu mkubwa wa Madaktari.

    Nimetumiwa na :Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog
  • Invitation for Bids - Meru Residential Apartments

    Posted: October 17, 2011, 7:41 pm by SIMON KITURURU
    SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
    KUKARIBISHWA MAOMBI YA KUNUNUA NYUMBA 30 ZILIZOKO MJINI ARUSHA
    Shirika la Nyumba la Taifa linawakaribisha watanzania wakazi na wasio wakazi  kuleta maombi ya kununua nyumba zake zilizojengwa mjini Arusha. Nyumba hizo ambazo zinaitwa “Meru Residential Apartments” zinatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu (siku 90) kuanzia tarehe 1 Oktoba,2011.MRADI WENYEWE:Meru Residential Apartments zimejengwa kwenye mandhari murua inayokupatia maisha bora katika jamii yenye usalama. Zimepewa jina hilo kama ishara ya kuuenzi Mlima wa Meru ambao ni mlima wenye Volcano hai nchini Tanzania wenye urefu wa mita 4,566 (futi 14,980), ukiwa ni mlima wa kumi kwa urefu barani Afrika.MAHALI ZILIPO:Meru Residential Apartments ziko mjini Arusha kwenye eneo la katikati kabisa, kwenye mtaa wa  Wachaga, Kiwanja Na. 565/I. Eneo hilo liko umbali usiozidi kilomita mbili toka ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), nyumba hizo zimepakana na hospitali ya Selian na Chuo cha Ufundi, na kwa upande wa mashariki inakupatia muonekano mzuri wa Mlima Meru.MAELEZO YA NYUMBA HIZO.
    Idadi ya Nyumba 30
    Ukubwa eneo la nyumba 169.45
    Idadi ya Majengo 2
    Idadi ya ghorofa kwa kila jingo Ghorofa nne
    Idadi ya vyumba kwa kila nyumba 3 (kimoja kinajitegemea)
    Sifa nyingine za nyumba hizo Sebule kubwa, chumba cha kulia, jiko,stoo,bafu na choo [ Nyumba zinauzwa bila samani (furniture)]
    Kila nyumba ina  maegesho maalum ya gari, pamoja na tanki la maji la lita 1000.












    BEI ZA NYUMBA HIZO:Bei ya chini kabisa ya kila nyumba ni shilingi za Kitanzania 175,314,366.48 bila kujumlisha kodi ya ongezeko la thamani. Mwombaji atakayetoa bei ya juu zaidi na kutimiza masharti yote yaliyoelezwa hapo chini ana nafasi kubwa zaidi ya kuuziwa.TARATIBU ZA KUOMBA:Waombaji wanatakiwa kuzingatia utaratibu ufuatao:
    1. Wanaopenda kununua nyumba wachukue fomu za maombi kutoka Makao Makuu ya Shirika, kwenye ofisi za Shirika zilizopo Arusha, au kwenye ofisi yoyote iliyo karibu nao. Fomu zinapatikana pia kwenye tovuti wa Shirika (www.nhctz.com).


    1. Fomu za kuomba kununua zijazwe na kuwekwa saini na kurejeshwa kwenye ofisi za Shirika pamoja na barua ya kuonyesha kiasi ambacho mwombaji yuko tayari kulipa. Shirika litahitaji pia ushahidi wa malipo ya shilingi 10,000/=(Malipo yasiyorejeshwa) kama ada ya maombi na malipo ya asilimia kumi (10%) ya awali zilizolipwa kupitia benki kulingana na thamani ya nyumba uliyochagua.


    1. Waombaji wote waliofanikiwa wataandikiwa barua kujulishwa hivyo. Watapewa siku 90 toka tarehe ya barua hiyo kukamilisha malipo ya asilimia tisini (90%) iliyosalia kulipia nyumba husika. Utaratibu wa kulipa unaweza kuthibitishwa kwa kulipa pesa kwenye akaunti ya mradi au kuonyesha hati ya mkopo toka benki.


    1. Kama uthibitisho wa malipo hautawasilishwandani ya siku 90, mnunuzi atanyang’anywa na nyumba hiyo kuuziwa mtu mwingine toka kwenye orodha ya waombaji. Mnunuzi aliyeshindwa kulipa hiyo asilimia tisini (90%) ataruhusiwa kutumia asilimia kumi (10%) ya awali kulipia nyumba kwenye mradi mwingine. Aweza pia kurejeshewa fedha zake kwa kukatwa asilimia mbili (2%) ya kiasi hicho.


    1. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni Jumatano tarehe 4 November, 2011 saa 4:00 asubuhi.


    1. Maombi yapelekwe ndani ya bahasha yenye rangi ya hudhurungi/kahawia iliyoandikwa juu;”Maombi ya Kununua Nyumba za Meru-Arusha”.


    1. Maombi yote yapelekwe kwa: Meneja wa Mkoa, Shirika la Nyumba la Taifa, S. L. P 883, ARUSHA
  • KIDUM

    Posted: October 17, 2011, 2:30 pm by SIMON KITURURU


    BURUNDIAN MASTER DRUMMER and Singer:...Jean Pierre Nimbona a.ka.KIDUM..............NAHUSUDU tu  mambo zake ninihino kwenye ngoma.


    KIDUCHU kuhusu Mjamaa HUYU  angalau kimoja ya alubamu  zake kwa ung'eng'e:

    This long awaited album is Kidum’s fourth offering after YARAMENJE, SHAMBA and ISHANO. It is perhaps the most acclaimed release produced by Kidum, featuring his much sought-after chart-topping hit, Mapenzi. He collaborates with Tanzanian songstress lady Jaydee in Nitafanya, Ugandan princess of song Juliana Kanyomozi (Haturudi Nyuma), Kenyan maestro Nameless (Greedy) Sara Mitaru (imara) and compatriot Frankie Joe (Kipenda roho). If you are looking for dance and melody, then you will find sumptuous amounts of zouk and blues on this album.





    Hebu adatishe KAMANYOLA bila JASHO tena katika-MAPENZI





    Akiwa na Juliana Kanyomozi wanyokolishe -Haturudi Nyuma



    Au tu na Komandoo LADY JAY DEE waweke pia kimadangachee pini-NITAFANYA



    Habari zake za zamani kidogo,....... bofya HAPA

    NA wavuti yake iko: HUKU
  • SAHARAN vibe,...

    Posted: October 17, 2011, 2:01 pm by SIMON KITURURU
    ....ni blogu niipendayo sana.

    Itembelee kwa kubofya :SAHARAN VIBE.
    NI HILO TU Mdau!
  • Baraka CHUMBANI labda bado ni ile kitu MATUSI!:-(

    Posted: October 17, 2011, 7:25 am by SIMON KITURURU
    Na MATUSI kwa kuwa ni tafsiri tu za WATU,...... na ile tu MATUSI lakini  aisee MHESHIMIWA,...... labda BADO hata KIHESHIMA TU  bado hiyo ni ile kitu  iitwayo MATUSI TU MAISHANI ,...... na  ndio maana kitu hiyo mshikaki huweza  ITWA  pia  labda  bado hata na MTU fulani  hata asiye KIJEBA haki ya NANI VILE kuwa hiyo ndude ni PENZI hata pasipo CHUMBA na ya yajulikanayo kuwa huru CHUMBANI ambayo hata kama sio  kisiri  HAYO ni kujikojolea.:-(
    Swali:
    • AU?
    • Unabisha?:-(
    • Na si CHUMBANI  kimsingi ni CHUMBA kitu kifanyacho BAFU , sebule  na mpaka chumbani labda bado vyote ni VYUMBA tu ukitafsiri kiaina fulani bila kugusia ufikiriayo yanaukarimu zaidi CHUMBANI na si CHOONI?

    Ndio,..... na labda mpaka kifikiriwacho ni  BARAKA ni tafsiri tu za MTUZ,...... kwa kuwa waliobarikiwa kitafsiri za watu labda ndio  akina RAIS KIKWETE au Rais NYERERE ambao kwa wengine hata huko kwenye  CHUMBA wakiitacho OFISI kwa  yao yawatesao   WAO,..... kwa watesekao  na YAO  hata kama si ya kama MORISI NYUNYUSA KUTOKUMBUKWA NA WAO ingawa taarifa za HABARI  ZAO miaka lukuki zilianza na NGOMA ZAKE  ambaye na ambao wako kwenye vyumba ambavyo  kiunene sio IKULU,..
    ...labda ya viongozi hao bado sio BARAKA pia.:-(
    Ni wazo tu hili KAMANDA!:-(Jumatatu njema MKUU!


    Hebu Curtis Mayfield aanzishe ndude upya kwa kudunga tena mbilimbi-Move on up


    Curtis Mayfield adinye pia kipengele - Superfly



    Bob Marley aingilie kati na kubadili kidude kwa -Dance Do The Reggae


    Au tu Bob Marley azime kidude kwa - Reggae On Broadway




    Na sijui kwanini lakini labda hebu Curtis adunge tu  pia kidonge -Pusherman

  • Katika ya Uganda eeh! AMERIKA hiyoooooo!

    Posted: October 16, 2011, 9:00 pm by SIMON KITURURU
    Katika ya Uganda eeh! AMERIKA hiyoooooo!
  • Unachoogopa usiku GIZANI,.....

    Posted: October 16, 2011, 4:15 pm by SIMON KITURURU
    ... kumbuka huwa unakiogopa tu hata kwenye MWANGA pale mchana,........ na kifanyacho LABDA hustukii kuwa woga wako wa KITU uko palepale yaweza kuwa ni kitu kingine kama vile kuna WATU WENGINE hapo na kwa kuwa unaona vizuri kwa kuwa KUNA MWANGA na kisaikolojia uko shwari,....
    ... lakini hilo BADO KWA BAHATI MBAYA haliondoi kuwa AOGOPAYE MENDE wakati hakuna mende haimaanishi kwa hilo basi haogopi MENDE wakati huo.:-(
    Swali:
    • SI unakumbuka apendaye UBWABWA huwa anapenda UBWABWA hata wakati UBWABWA haupo?

    Ndio,....... labda kama UOGOPACHO ni WACHAWI na KUKABWA na vibaka GIZANI katika ule USIKU,...... kumbuka kuwa hivyo vitu unaviogopa MCHANA PIA  kwenye MWANGA ingawa LABDA kwa kuwa kuna watu wengine LUKUKI MCHANA PEMBENI YAKO  na pia kwa kuwa UNAONA VIZURI kwenye MWANGA na kujisahau ugopavyo kwa kuwa huvioni kwenye mazingira ya VIONEKANAVYO mchana,...
    ... labda usisahau tu kuwa KUJISAHAU unaogopa DUDU  haimaanishi kutokuwepo kwa  WOGA WA dudu   kwa MTU  HUYO ambaye bado labda ni WEWE  kumefutika.:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

    Hebu Muddy Waters aanzishe kwa-Mannish Boy (I'm A Man)


    John Lee Hooker adai - I'll Never Get Out of These Blues Alive


    Jimi Hendrix aingilie kati kwa -Crosstown traffic


    Au tu hebu Jimi Hendrix azime tena kwa - All Along the Watchtower

  • MAJIBU ya KITU labda MTU huwa nayo MBELE YAKE tu ,....

    Posted: October 16, 2011, 4:06 pm by SIMON KITURURU
    ... na yasemekana tatizo liko  kwenye kuyastukia TU kuwa  hayo ni MAJIBU,.......na baada ya kuyastukia  ,...... kuyafanyia KAZI ili yawe kikweli ni JIBU!:-(
    Swali:
    • Unabisha?

    Ndio,...... katika tatizo lako LABDA ni wewe mwenyewe UNAJIBU sahihi,...... ..kwa hiyo labda jiamini tu na chukua hatua kwa ufikiriacho ni JIBU hasa kwa kuwa ajuaye unatatizo gani vizuri ni WEWE MWENYEWE na  hilo pekee YASEMEKANA NI KIGEZO TOSHA  kama sio  ni moja ya misingi ikufanyayo kuwa WEWE ndio MWENYE jibu zuri  zaidi kuwa kipele chako cha siri MAISHANI kikunwe au kibinywe!:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!Jumapili njema KAMANDA!:-(
    Hebu Lou Reed aanzishe kipengele upya kwa- Walk on the Wild Side



    Pink Floyd wapenyeze- Wish You Were Here


    Lou Reed aongezee dozi kwa - Perfect Day


    Au tu hebu U2 wazime kwa-Sweetest thing

  • NGUMI KULINDIMA PANANDIPANANDI ILALA JUMAPILI HII MABONDIA WAPIMA UZITO

    Posted: October 15, 2011, 11:38 pm by SIMON KITURURU


    Kocha wa mchezo wa ngumi Habibu Kinyogoli akiwaelekeza vijana toka klabu mbalimbali jinsi sheria za mchezo wa ngumi zinavyokua wawapo ulingoni.Michuano ya mchezo wa ngumi inatarajiwa kulindima kesho jumapili katika ukumbi wa panandi panandi Ilala Bungoni.

    (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)






    Baadhi ya wachezaji wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano utakaofanyika jumapili hii.

    (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)




    Kocha wa mchezo wa ngumi Habibu Kinyogoli akiwaelekeza vijana toka klabu mbalimbali jinsi sheria za mchezo wa ngumi zinavyokua wawapo ulingoni . Michuano ya mchezo wa ngumi inatarajiwa kulindima kesho jumapili katika ukumbi wa panandi panandi Ilala Bungoni.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania

    Nimetumiwa na:Super D
  • DEO NJIKU AJIANDAA KUMKABILI JONAS SEGU WIKI IJAYO

    Posted: October 15, 2011, 11:26 pm by SIMON KITURURU





    Kocha wa Mchezo wa ngumi, Boma Kilangi (kushoto) akimsimamia mazoezi bondia Deo Njiku wa Morogoro wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake wa ubingwa zidi ya Jonas Segu wa Dar es Salaam  litakalofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro wiki ijao.

    (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)




    Bondia Deo Njiku akifanya mazoezi ya misuli ya tumbo kwa kutumia vifaa vya kisasa kwa ajili ya  kujiandaa na mpambano wake wa ubingwa zidi ya Jonas Segu wa Dar es Salaam  litakalofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro wiki ijao.

    (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)










    --
    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania

    Nimetumiwa na:Super D
  • Kwa kuwa MOJA ya janja ya MAZINGAOMBWE ni kukuonyesha hiki ili USIONE kile!

    Posted: October 15, 2011, 11:01 am by SIMON KITURURU
    Hebu tuanze kupapasa ndude kwa KISWANGLISH:

    Janja za wanamazingaombwe zinawekwa katika makundi matatu;Misdirection, Illusion and Forcing.
     
    Katika MISDIRECTION siri ya tumizi hilo ni kwa kuwa  yajulikana kutokana na udhaifu wa UBONGO wa Binadamu,...
    .....na focusing on one thing can make a person  oblivious to other things that would otherwise be obvious.

    Kwa hiyo,...
    ....misdirection lies at the heart of magic. It is the art of diverting the audience's attention away from  the act itself. In neuroscience terms, misdirection relies on the fact that the brain has a very limited supply of attention.
    Ndio,...
    .....na kuchekelea kanyau ni noma kwa kuwa ,.......
    ....  another mysterious way of manipulating attention of a person  is with humour.


    Na achekaye wakati anacheka,...
    ... wakati huo  hawi makini katika kuangalia hata vya wazi mbele yake.
    .........kwa hiyo  akuchekaye wakati anachekelea kanyau huo ndio wakati  rahisi kumficha kitu  cha wazi mbele yake hata kwa mfano  badala ya kujifuta mdomo unaweza wakati huo kuchokonoa pua na kuondoa kamasi lililokuganda bila kustukiwa.:-(
    Na another key tool in the magic repertoire is ILLUSIONS, particularly cognitive illusions. Hizi zina  rely on the fact that much of what you think you see is actually invented by your brain.

    Na,.......perception is not about capturing a full picture of reality, but taking snapshots of the world and making the rest up.

    Kwa hiyo,.......MENGI  ufikiriayo unayaona MKUU ,..... inasemekana hutungwa tu UBONGONI mwako.:-(
    Sasa tukiacha kuzunguka MBUYU ngojea tu niingie katika nataka kusema nini katika UjingaBUSARA huu:

    Okei,...... nachojaribu kusema,.......kumbuka UONACHO kama kuna mtu anakuonyesha hata KISIASA labda ota machale kwa kuwa labda uoneshwacho ni silaha tu ya kukufanya USIONE jambo kwa kuwa bize katika kuangalia jambo jingine.
    Swali:
    • Wabongo mnakumbuka BABU wa LOLIONDO alivyoondoa makali ya hata mambo mengine katika siasa za Tanzania?

    Okei,........ nachojaribu kusema,....... kumbuka  wakati MTU anacheka kuna wafumbao mpaka macho na hapo tukiruka kitendo cha kuchekelea hutuliza mtu katika kustukia mambo.

    Swali:
    • Huja stukia ZE VICHEKESHO hata kama sio vya ZE Comedy ni muhimu kwenye mihadhara fulani yenye waheshimiwa KUHUTUBIA ambayo hutumiwa hata katika HOTUBA na Waheshimiwa akina Rais NYERERE wenyewe pia kwa dhumuni hilohilo kiaina?
    • Na kama umeenda kwenye mazingaombwe si ushastukia huwa unachekeshwa mara kwa mara na mwana mazingaobwe ?

    Okei,....... nachojaribu kusema,.........kumbuka kuwa ukishawishiwa na kushawishika  wala huhitaji kuona picha nzima kuwa jamaa aingizaye mkono mfukoni afanyacho ni kufungua zipu tayari kuchojoa.:-(
    Swali:
    • Kwani unafikiri ukishahisi unaibiwa KURA unahitaji kuona kabisa kura ziitolewavyo kwenye kisanduku cha kura au tu kumuona uhisiye ni mwizi wa kura pembeni ya kiboxi  manyoya cha KURA inatosha?

    Ndio,....... wazo limepinda na sijajadili kikugusagusa kitu FORCING kama itumikavyo na WANAMAZINGAOMBWE ingawa wote twajua Mwanamazingaombwe hata achezaye na KARATA huwa akimuambia mtu achague KARATA bila yeye kuiona ,...... afanyacho ni kum-FORCE achaguaye KARATA kuamini afanyacho ni chaguo lake na Mwanamazingaombwe hajui kuwa kifanyikacho na KADI ya karata atakayochagua Mwanamazingaombwe anaijua kwa kuwa ni yeye aliyemchagulia hiyo kadi  MTU hata wakati anamwambia mtu achague Hiyo KADI ya KARATA!:-(
    NIMEACHA na ndio ni RUKSA kutonielewa!:-(
    Jumamosi NJEMA Mheshimiwa!

    Hebu tudeku-Selective attention test ile iliyoandaliwa na Daniel Simons and Christopher Chabris.


    Au ghafla Ferro Gaita waturudishe Cape Verde kwa kuingizia ghafla -É si propi




    Halafu Mdada Denise Belfon apenyeze tena -Licks

  • Kwa kuwa aachaye KINYESI bila kuvuta MAJI MSALANI labda kwake hilo si TATIZO!

    Posted: October 14, 2011, 10:53 pm by SIMON KITURURU
    Lisilo TATIZO kwa ZUBEDA  na lisilo muhusu MWANAISHA,.....

     ... likimtatiza  MWANAISHA ,........ basi yawezekana ni  NI TATIZO tu kwa MWANAISHA kwa kuwa  kaligeuza kuwa TATIZO TU kwake.

    Swali:
    • Lakini  si labda bado LISILOKUTATIZA laweza kuwa ni tatizo halali kwa wengine?
    • Si tatizo la choo kichafu labda sio kali kwa aliyeacha choo kichafu kama ilivyo kwa ambaye baadaye  akutaye timba pembeni kwenye choo kichafu?

    Ndio,...
    ... tusisahau labda kuwa bado kuna UKWELI,...
    ... lisilo TATIZO kwa NYERERE na halikumusu KIKWETE bado laweza kuwa ni moja ya misingi ya matatizo kwa Rais KIKWETE.!

    Ni wazo tu hili na RUKSA kutolielewa!


    Hebu Red fox aanzishe upya kwa-Ghetto gospel



    RED FOX apandishe dozi kwa - BORN AGAIN BLACKMAN


    Halafu Red Fox ahamishe tu kipengele  kwa -Dem A Murderer

  • SHABAZZ PALACES

    Posted: October 14, 2011, 8:47 pm by SIMON KITURURU


    Haya ,..
    ... tuendelee,...
    .... mie naanza mwisho wa Ijumaa kiaina  na Shabazz Palaces



    NAKUTAKIA Kamanyola bila JASHO Mkuu!

    Ndude hiyo hapo juu ilirekodiwa  tarehe 6/28/11


    Tracks:Bop HardAn Echo From The Hosts That Profess InfinitumA Mess, The Booth Soaks In Palacian Musk...Free Press And Curl
    Host: Cheryl Waters
    Audio: Kevin Suggs
    Cameras: Jim Beckmann, Scott Holpainen & Justin Wilmore
    Editing: Scott Holpainen

    www.kexp.org
    www.youtube.com/kexpradio
    www.subpop.com
  • ISSA SEWE AJIFUA KUMKABILI RAMADHANI SHAULI

    Posted: October 14, 2011, 7:10 pm by SIMON KITURURU
    Mbunge wa Ilala Mussa Zungu atashughudia ZAIDI ya mabondia 42 wanatarajia kushiriki katika mashindano ya mchezo wa ngumi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba16 mwaka huu Dar es Salaam.

    Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha wa Klabu ya Ashanti ya Ilala, Rajabu Mhamila, 'Super D' alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha Klabu 12 kutoka katika maeneo mbalimbali.

    Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala.

    Super D alisema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuhendeleza kuhamasisha mchezo wa ngumi nchini ikiwa ni pamoja na muendelezo wa mchezo huo unanaofanywa na Kinyogoli Foundation.

    “Tumeandaa mashindano ya ngumi ambayo yatashirikisha vijana mbalimbali na lengo letu ni kuhamasisha mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuuendeleza ili uweze kutuletea faida hapo baaye” alisema.

    Kocha huyo alisema kuwa vijana watakaoshiriki watakuwa katika uzito mbalimbali kuanzia Unyoya mpaka uzito wa juu.

    Alisema kuwa pia wanatarajia kushirikisha mabondia wa kike kutoka katika klabu hizo hizo Aliongeza kuwa katika mapambano hayo mgeni mwalikwa ni Mbunge wa Ilala Mussa Zungu ambaye kwa mara ya kwanza atangalia mchezo huo ukipigwa katika jimbo lake

    Aliongeza kwa kusema kuwa wanaitaji wadau mbalimbali wajitokeze kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya vijana ikiwemo maji kwa ajili ya mchezo huo kwa siku hiyo wenye nia ya kutaka kusaidia au kushiliki kwa kuchangia chochote wanaweza kuja katika ukumbi wa mazoezi uliopo Amana Ilala au kufika Ashanti Boxingi clabu kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwa siliana na Kocha Mkongwe, Habibu Kinyogoli kwa simu 0655928298 au unaweza kuwasiliana na Super D Boxing Coach O713,0787-406938 Email.superdboxingcoach@gmail.com wadau mbalimbali mnakalibishwa


    Kocha mkongwe wa mchezo wa ngumi , Habibu KInyogoli (kulia) akimwelekeza jinsi ya kutupa masubwi bondia Issa Sewe wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Dar es salaam jana Sewe anajiandaa na mpambano wake na Ramadhani Shauli litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania

    Nimetumiwa na:Super D
  • MAISHA YA KUJIPENDEKEZA kwa MSHINDI huishi kufuata ukumbukwavyo USHINDI,...

    Posted: October 14, 2011, 4:44 pm by SIMON KITURURU
     ... na ushindi ukiisha UMAARUFU  kwa wengi wajipendekezao kwa MSHINDI,...
    ... humsahau MSHINDI kwakuwa tokea mwnzo  hakuwa anapendwa MTU kama MTU,...... bali kilichopendwa ni USHINDI  na MTU alikuwa  kitu tu kiwakilishacho KUSHINDA.
    Swali:
    • Si unakumbuka kuna  wapendao GARI ambao huonekana hadharani kama wampendaye ni MWENYE GARI?
    • Si kuna wapendao UTAJIRI  na ukiwa TAJIRI hata kama unasura na tabia  kama tako wewe ni BONGE la dili?

    Ndio,....... kuna idhaniwao ni  WAJIPENDEKEZAO kwa MTU,...... ila ukichunguza utastukia kuwa hawapendi MTU bali tu kile kiwakilishwacho na huyo MTU kitu ambacho  huweza kufanya apendaye URAIS  akajikuta kama  wadaivyo alivyo Mke wa MANDELA kuwa Rais yeyote hule awe SAMORA wa MSUMBIJI  au tu IDI AMIN   kwake  atakuwa  ndiye afaaye kuwa MME hata kama ni yule Mzee kama MANDELA aliyemshinda WINNIE .:-(


    Swali:
    • SI mpenda NYANYA  anaweza akajikuta anapenda zaidi bustani ya NYANYA kuliko ile ya KAROTI?

    Ndio,...... MAISHA ya uwepo wa KUJIPENDEKEZA,...... labda hauhitaji uwepo wa MTU  kwa kuwa kwa ajipendekezaye ,........sababu za kujipendekeza  kwa MTU labda wala hazina misingi ya kweli ihitajiyo huyo MTU.:-(

    Ni wazo tu hili MHESHINMIWA!Ijumaa na WIKIENDI NJEMA MKUU!

    Hebu Mzee Yusuph aanzishe upya kwa-Naksh Naksh


    Ali Kiba naye aingile kati kwa - Nakshi Mrembo

  • OYAA wapenda NGONO,....

    Posted: October 14, 2011, 3:38 pm by SIMON KITURURU
    ...deku listori ukiweza...katika-CAN great sex lead to memory loss?

  • Wakati unamuangalia MWENYE MATUSI ambaye hajatamka bado TUSI!

    Posted: October 14, 2011, 1:57 pm by SIMON KITURURU
    Mtu huweza kuchagua kukaa KIMYA  ili ahisiwe au hata aonekane kuwa   ana BUSARA,...
     ... tatizo LABDA  ni pale WASIO NA BUSARA wakaao KIMYA kuanza kuamini ni kweli wanabusara kwa kuwa wanahisiwa na WENGINE wasio jua kitu kuwa ,...... WANABUSARA.

    Swali:
    •  MKuu yeyote umfikiriaye sasa hivi hatakama ni MSWAHILINA  si unakumbuka kuwa ana matusi?
    • SI unajua MWENYE matusi anayo tu hayo MATUSI hata kama kakaa kimya?

    Ndio,...... na labda KUMBUKA TU kuwa  mwenye haja kubwa,....... anayotu hajakubwa mwilini hata kabla hajastukia haja kubwa imembana au WATU wengine  kushuhudia hitaji lake linamuelekeza CHOONI!:-(
    Ni wazo tu hili MKUU!:-(


    Hebu Singing Sandra aanzishe upya kwa - True Colours


    Singing Sandra aendeleze kwa -Crying


    Halafu Ella Andall azime tena kwa - Rhythm of A People

  • Women Their Own Worst Enemy-adai Mwanamama SINGING SANDRA

    Posted: October 14, 2011, 1:06 pm by SIMON KITURURU


    Si nishasikia kuwa pia:
    • Black PEOPLE their Own Worst Enemy?
    Ni mtonesho tu huu MKUU na usikonde!:-(
  • Remmy Ongala Tribute Night Event In London

    Posted: October 14, 2011, 4:10 am by SIMON KITURURU


    Greetings,

    We are honoured to invite you to a very special tribute night for one
    of Africa’s greatest singers, the mighty Remmy Ongala who sadly passed
    away on 13th December 2010.

    “He was a superstar in East Africa, and in the 1980s and 1990s he
    reached European and American audiences with albums for Real World, a
    label founded by Peter Gabriel, and international tours that included
    many appearances at Mr. Gabriel’s Womad (World of Music and Dance)
    festivals.” - New York Times, January 18, 2011.

    To celebrate Remmy’s music and life we have invited the original members of his band Orchestra Super Matimila to perform live on stage on Saturday 22nd October lead by Kawele (AfricaJambo) and featuring soukous superstars Saidi Kanda, Fiston Lusambo,Rama Kayimanda, Billy Mwangura, and Malinga, Kiniki, Rissa Rissa,
    Eugene Makuta, and Claudia Bakisa.

    Also very special guests on the night include Baba Adesose Wallace
    (Ibile/ Tribe Of Doris), and Torera Mpedzisi (Mbira legend)!!

    Your DJs on the night are: African music don DJ Wala Danga (Africa
    Centre/ Limpopo Club), Mister K (Africa Centre) and Planetman (Little
    Blue Ball/Passing Clouds).

    =========================

    Live on Stage:

    Orchestra Super Matimila & guests (Soucous)

    Baba Adesose Wallace & Torera Mpedzisi

    DJS:

    Wala Danga
    Mister K
    Planetman
    ==========================
    money raised on the night is going to the DK Remmy Ongala Foundation
    to help children in Tanzania with music scholarship.
    [www.thedkremmyongalafoundation.com]
    ==========================

    Passing Clouds
    1 Richmond Rd. Dalston E8
    corner Kingsland Rd.
    8pm-3amDate 22 October 2011
    £5 before 10pm, £8 after
    entrance at the back.

    Train: Dalston Kingsland, Dalston Junction (new station)
    buses: 242, 38, 76, 67, 149, 56, 30, 243Please come to support the Course and inform your friends.ThanksPosted By Urban Pulse Creative

  • ZE Documetary

    Posted: October 14, 2011, 4:09 am by SIMON KITURURU
    Salam [vimeo.com] Urban Pulse Creative inakuletea Mini Documentary ya Msanii wao Mish Ze Fyah Sis kuangalia safari yake katika ulimwengu wa muziki na maoni yake kusuhusu mziki. Asante URBAN PULSE CREATIVE
  • TANGAZO:Image Profession

    Posted: October 14, 2011, 4:08 am by SIMON KITURURU





    Nimetumiwa tangazo na:Dimo DebweImage Profession
  • HISTORIA ni KATILI kwa ASHINDWAYE!

    Posted: October 13, 2011, 7:25 pm by SIMON KITURURU
    Swali:
    • Si unakumbuka ni WASHINDI mara nyingi stori zao ndizo  HUSIKILIZWA?
    Ndio,...
    ... labda ota JICHO la tatu ,...
    ... hata katika stori nzuri za historia  UZISIKIAZO za ya VYAKO kama sio hata ya KIKIJIJI  chako,...
    ..... kwa kuwa  yawezekana katika stori TAMU kuna yaliyorukwa kwa MAKUSUDI na mtoa stori ASIKILIZWAYE :-(


    Ni wazo tu hili kimstuo  tu MHESHIMIWA!:-(
    Hebu turudi BENIN ili Kiinzah aendeleze kwa - Femi


    Fafa Ruffino atubakize hapahapa BENIN kwa -ILE


    Au tu tukatizie GUINEA  ili  Mory Kante akiwa na  SANTANA wairudishie uhai -YEKE YEKE


    Halafu turudi KAMERUNI ili MANU DIBANGO azime tena kwa-Soul Makossa
  • Kumbukumbu ya kifo cha FRANCO LWANZO MAKIADI

    Posted: October 13, 2011, 6:30 pm by SIMON KITURURU





    Miaka 51 iliyopita siku kama ya leo ndipo jabali Franco Lwambo Lwanzo alipofariki huko ubelgiji.
    Soma historia yake:HAPA--


    R.I.P!


    www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.comwww.johnkitime.blogspot.com

    Nimetumiwa na:John Kitime
  • KATIKA KUMBUKUMBU:Tam Tam pour L'Ethiopie

    Posted: October 13, 2011, 5:30 pm by SIMON KITURURU
    Mwaka 1985 ,...
    ....akina Lema Adé ,Hugh Masekela, Manu Dibango, Mory Kante, Salif Keita, Toure Kunda, Youssou N'Dour, King Sunny Ade, Yves N'Djock,....
    ... na wengine wengi walishuka na ndude kadhaa kinguli ikiwemo hii,.......katika kuchangia Ethiopia iliyokumbwa na NJAA kipindi hicho.



    Ni kumbukumbu tu hii  KIBOSILE na wala USIKONDE!:-(
  • NGUVU ya MTU MMOJA katika ya HELKOPTA:Igor Ivanovich Sikorsky

    Posted: October 13, 2011, 3:42 pm by SIMON KITURURU
    Kuna wengi husahau  kuwa ,.......LABDA ni  MCHANGO wao kama mtu MMOJA,..... ndio siri ya  JIBU kwa maswala yasumbuayo ULIMWENGU.
    Na  ukisikia stori za watu kama STEVE JOBS,Thomas Alva Edison,Henry Ford, Albert Einstein, Mwalimu Nyerere, MANDELA, na wengine wengi,....
    ... unaweza kustukia ni JINSI GANI mtu mmojammoja pia kimchango wake anaweza kuwa chachu yakutosha .
    LEO hebu tumcheki :
    ... katika-Sikorsky: Father of the helicopter

  • Mbunge wa MVOMERO Ndugu AMOS MAKALLA atembelea eneo la mgogoro wa ardhi KINYENZE

    Posted: October 13, 2011, 1:56 pm by SIMON KITURURU
    Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla (mwenye suti) akiangalia uzio
    uliowekwa na mwekezaji katika Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji chaKipera, Wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro na kuziba njia inayokwendakatika mtaa wa Mwanga na katika mashamba.
    Pia mwekezaji huyo raia wa kigeni amechukua sehemu ya mashamba ya wananchi hao bila ya taarifayeyote kwa Halmashauri ya Kijiji na wananchi.











    Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla  akiwa na Hamis Maguo , alipotembelea hivi karibuni Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera , kufuatilia mgogoro kati ya wananchi wa Kijiji hicho na mwekezaji












    Nimetumiwa na :
    Mroki Mroki/FATHER KIDEVUDirector MD Digital CompanyGeneral Secretary PPATProfessional Photojournalist & BLOGGERP.O.BOX 110097,Mob: +255 755 373999 /+255 717 002303,
    Email: mrokim@gmail.com.
    Blog: www.mrokim.blogspot.com
    DAR ES SALAAM, TANZANIA
  • TAARIFA YA MAZISHI ya Marehemu MZEE SAIDI MUHAMMAD SIKAMKONO.

    Posted: October 13, 2011, 7:24 am by SIMON KITURURU


    Rejea taarifa ya msiba wa Mzee Said Muhammad Sikamkono.

    Mazishi yatafanyika LEO   tarehe 13/10/2011 katika makaburi ya Hainalt Garden of Peace saa nane mchana. 

    Ila kabla ya makaburini tunaombwa wote tufike msikiti wa Sakina Walthamstaw (basi namba 179) saa sita na nusu mchana.

    Msiba uko nyumbani kwa marehemu Woolwich Dorkyard ambako wote tunakaribishwa muda wowote kujumuika na familia ya marehemu wakati huu wa majonzi .

    Wakina mama pia wanaweza kufika msikitini au nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kutoa pole.
    Address ya sehemu ya msiba ni;

    Woolwich Ferry405,Frances Street, London.SE18 5JU.
    Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:

    Haruna Mbeyu:07813539025 AU Abdallah Mdidi: 07766454596 
  • MAPENZI ya watu wawili hayana DISPLINI WEYE bwana,...

    Posted: October 13, 2011, 5:33 am by SIMON KITURURU
    ... na kama una DISPLINI  katika penzi LAKO  HILO lenye MPAKA  mtu wa PILI,....... labda stukia uwezekano labda WEWE au huyo mwenzio afanyaye kwenye penzi muwe WAWILI  kimapenzi hamfanani  na labda katiyenu WAWILI kuna MMOJA  hanogewi sana kihilo PENZI weye!:-(


    Swali:
    • Si inajulikana kuwa PENZI  la kweli halihitaji matumizi sana ya AKILI  kikutafakari kinini ni PENZI kiakili ndio maana  KIMAPENZI hata UKIMWI  kama MIMBATU ni oyee kwa mpenzi wakati kapenda?
    • Na si unajua siri kubwa ya CHANGUDOA katika KUCHUNA BUZI  KIMAFANIKIO  ni kwa kuwa anadisplini ya kucheza na engo tu  ajuazo zinaweka kuchuna buzi MSWANO kisa ni kwakuwa katika hili PENZI yeye hajapitiliza KIPENZI?
    • Kwani unafikiri waambukizwao na MPENZI gono kikaswende    hata kabla  hawajakubali kutoa jicho katika kalio-kikalio  huwa hawajui madhara ya kugawa bahati nasibu za shehena kinyeo?

    Ndio,...... MAPENZI ni kikohozi  ndio maana  LABDA hayazuiwi  hata na kwa  kizuizi cha MPENZI  kunuka uchi,....... na kama  kiakili unajizuia MPENZI asifaidi,...... labda hujapenda kisawasawa  WEYE,......na UNADISPLINI weye,...
    .. kitu ambacho chaweza kuwa ndio ilipo JANJA  YA MDOEZI na yawezekana UTAIBIWA NA WAJANJA weye!:-(


    Ni wazo tu hili kitishatoto MHESHIMIWA!:-(




    Hebu tu turudi Senegal ili kigoli  Aby Ndour abadili ndude kwa ndude-Fouta



    Au tu ghafla Marcia Griffiths na Bounty Killer waingilie kati kwa - Tell Me Now


    Halafu Judy Mowatt azime tena kwa-BLACK WOMAN

  • MSIBA WA MTANZANIA MWENZETU MZEE SAID MUHAMMAD SIKAMKONO

    Posted: October 13, 2011, 4:20 am by SIMON KITURURU


    Tunaskitika kuwataarifu kuhusu kifo cha Mtanzania mwenzetu Mzee Said Muhammad Sikamkono kilichotokea juzi tarehe 11/10/2011 mchana katika hospitali ya Queen Elizabeth, Woolwich, London.
    Mipango ya mazishi inaendelea na mtaendelea kujulishwa. Kwa wakati huu ambao tutakuwa tunasubiri kupata taarifa ya mazishi, mwenye kuweza kuchangia chochote au mwenye kuhitaji kujua zaidi kuhusu msiba huu, tunaomba awasiliane na;
    Sheikh Ayub kwa namba; 07944930708
    AU
    Said Surur kwa namba; 07538063536
    AU
    Mr. Haruna Mbeyu kwa namba; 07813539025.
    “MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU SAID MUHAMMAD SIKAMKONO MAHALI PEMA. MUNGU AMETOA NA MUNGU AMETWAA, JINA LAKE LIBARIKIWE”
  • Mpigie KURA Miss JESTINA GEORGE wa Miss Jestina George Blog

    Posted: October 13, 2011, 4:04 am by SIMON KITURURU


    Hello to all you lovely people,

    Miss Jestina George Blog has been nominated for the Blog of the Year category at the 2011 (BEFFTA) Black Entertainment Film Fashion Television and Arts Awards.

    Please show your support by voting through this link, [www.beffta.com], under category select News 4. Blog Of the Year & Under Nominee select Miss Jestina George then submit your vote.

    Voting closes on 14th October and your vote would be very much appreciated.

    Thank you for your time,

    --


    Jestina George CEO & Founder : MISS JESTINA GEORGE BLOG
    Telephone: +447404332910
    Website: www.missjestinageorge.blogspot.com
    Twitter: [https:]
    Facebook: JestinaGeorge
  • Taarifa ya mabadiliko ya mtandao wa MATUKIO na WANAVYUO.

    Posted: October 12, 2011, 7:00 pm by SIMON KITURURU

    Sasa Blog hii imeungana na WANAVYUO WATANZANIA WANAOSOMA NJE YA TANZANIA.




    Kwanza kabisa tunapenda kuwasalimu wadau wote popote Duniani,tunatumaini ya kwamba bado mnaendelea na ujenzi wa taifa letu.

    Kwa heshima na Taadhima tunapenda kuchukua nafasi hii kuwapa taarifa kwamba mtandao wenu wa Matukio na Wanavyuo(www.tzwanavyuo.blogspot.com) sasa tumefanya mabadiliko makubwa ambapo tumewaunganisha wanavyuo watanzania wanaosoma Tanzania na walio Nje ya Tanzania.

    Tumefanya hivi kutokana na malalamiko na maombi ya Wanavyuo waliopo nje ya Tanzania kutaka kuanza kutuma matukio yao ambayo yanajili huko waliko.

    Tumelipokea ombi hili na sasa mwanachuo yeyote ataweza kutuma habari zake ama habari zao hapa. Pia kwa watumishi wa vyuo hapa nchini Tanzania mnakaribishwa sana kuleta matangazo yenu ikiwa ni nafasi za masomo ama kama kuna habari ya haraka mnataka iwafikie wanafunzi basi mtutumie moja kwa moja nasi tutaiweka muda huo huo.

    Mabadiliko mengine tuliyo yafanya kwa faida ya watu wote ni kwamba sasa tuna panel upande wa kulia ambapo tumeorodhesha tovuti za vyuo vyote vya Tanzania. Pia tumeweka na mambo mengine mengi ya msingi ambayo yatapata kuwasaidia.

    Mtandao wa wanafunzi ambao unafanya kazi kama Facebook (Social network)upo hewani mnakaribishwa kujiunga www.tzuniversitiesconnects.tk mnakaribishwa sana na pia mtakutana na wanavyuo wengine hapo.

    Tunatanguliza shukrani zetu za Dhati!
    Tumumie matukio na habari zozote zihusuzo vyuo hapa:twanavyuo@live.comTembelea Mtandao wa Matukio na Wanavyuo hapa:www.tzwanavyuo.blogspot.com
    Kwa niaba ya wanavyuo wote,Matukio na wanavyuo Crew.
  • NDIO !..labda UFIKIRIAVYO TU ndio kitu kiwezacho geuza neno KIDUDE kiwe TUSI au LA!:-(

    Posted: October 12, 2011, 6:58 pm by SIMON KITURURU
    Na ni RUKSA kubisha,....... ingawaje hata neno ´´KUBISHA``,...... yategemea tu na MTU unavyofikiria kwa kuwa neno KUBISHA nalo halina MAANA MOJA na halitekelezwi kiaina MOJA.:-(
    Swali:
    • SI mwenye kuwaza uchafu  chochote kisemwacho huweza kugeuka na kuwa na maana CHAFU?
    • Si hata  ubepari wa KIULAYA (  Social Capitalism)kwa MAREKANI ni matusi ukioanishwa nao kama afanyiwavyo Rais Obama?
    • Na si umeshasikia siku hizi HAPA DUNIANI imeshafikia  hata JUMA na ROZA  kitafsiri na wafikiriavyo baadhi ya watu  ni kuwa wote wanapatikana katika JINSIA  moja kitu kifanyacho  kuna nchi ni halali  kukuta NDOA za JUMA na ROZA ambao mmoja katafsiriwa ni wakikekike na kuitwa MKE  na mwingine ni wakiumeume ajitambulishaye katika mahusiano hayo kama MME  na kitendo cha kufunga pingu za maisha kati ya wanaume hao au wanawake hao  wawili bado tafsiri yake ni ileile ``NDOA´´ kama itafsiriwavyo kwa wale wenye mahusiano ya  MWANAMKE na MWANAMME kindoa?

    Ndio ,...... siku hizi mpaka NDOA hapa duniani,...... labda hutegemea tu na  afikiriavyo kama sio ATAFSIRIVYO mtu.
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

    Hebu Bobby McFerrin aanzishe upya kwa - Turtle Shoes

    Bobby McFerrin aongezee dozi kwa  - Invocation


    Au tu tena FLOETRY waingiliekati na kukuna tena kidude kwa-FLOETIC
  • HALI YA MTOTO CECILIA NI MBAYA ARUDI BILA KUFANYIWA OPERESHENI

    Posted: October 12, 2011, 5:30 pm by SIMON KITURURU
    Mtoto Cecilia wakati akiwaomba wasamalia wema waweze kumsaidia.
    Hapa Mtoto Cecilia akitoka Hospital ya Regency Dar akiwa ameshikwa mkono na afisa mmoja wa Channel Ten tayari kwa kuelekea Airport kuanza safari ya kwenda India.
    Mtoto Cecilia alitangazwa hivi karibuni na Vituo mbali mbali vya habari akiomba msaada wa kusaidiwa pesa za matibabu ambazo zingeweza kumwezesha kufanyiwa operesheni ya moyo ambao umempelekea mpaka Tumbo lake kuvimba kama unavyoliona.
    Taarifa za Cecilia ziliweza kutolewa na Miss Tanzania wa mwaka 2006 Bi .Hoyce Temu pale alipoamua kujitokeza na kumtangaza Cecilia akiomba msaada huo. Wasamaria wema walijitokeza na kumsaidia Cecilia mpaka akaweza kwenda India kwa matibabu, cha kusikitisha sana ni kwamba matibabu yake kwa njia ya operesheni yameshindikana kutokana na moyo wake kwa upande mmoja kuathirika na sumu ambayo madaktari wa India wamesema inasababishwa na Sumu ambayo ipo kwenye Mihogo, sumu hiyo huwaathiri sana watoto wenye umri kama wake.
    Kwa hiyo imekuwa ni vigumu kumfanyia operesheni hiyo, wakashauri atumie dawa tu ili kuweza kuitoa sumu hiyo, Mtoto Cecilia mpaka sasa hali yake sio nzuri anawaomba watanzania mumuombee ili aweze kupona na aweze kutimiza azma yake ya kuwa Mwalimu. Watanzania tunashauriwa tukiona hali ambayo ni tofauti kwa watoto wetu tuwawaishe Hospitali mapema kwa uchunguzi tunaweza tukawaepusha na hali kama hii aliyofikia Cecilia.

    Nimetumiwa HABARI na:Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog
  • Shukrani: DR.SHANAMESIA ELISHIWAKWE MUSHI

    Posted: October 12, 2011, 5:21 pm by SIMON KITURURU
    DR.SHANAMESIA ELISHIWAKWE MUSHI  (27/7/1927-13/08/2011)




    FAMILIA YA BWANA NA BIBI GEORGE ISRAEL MNYITAFU KWA NIABA YA FAMILIA YA MAREHEMU DR.SHANAMESIA ELISHIWAKWE MUSHI ,TUNAPENDA KUTOA SHUKRANI NYINGI NA DHATI KWENU NINYI WOTE MLIOKUWA NA SISI WAKATI WA KUUGUZA BABA YETU MPENDWA HADI PALE BWANA ALIPOMWITA KATIKA NYUMBA YA MILELE 13/08/2011 NA KUZIKWA TAREHE 16/08/2011 MACHAME KISIKI.

    SHUKRANI ZIWAENDEE MADAKTARI NA WAUGUZI WA HOSPITALI YA MACHAME,KCMC,REGENCY NA MUHIMBILI,WAFANYAKAZI WA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA-DAR ES SALAAM,MOSHI NA ARUSHA),UONGOZI WA KANISA LA AZANIA FRONT(MCHUNGAJI C.MZINGA,A.KIBONA NA E.LWIZA),VIKUNDI VYA KWAYA(AZANIAFRONT-KWAYA KUU,KWAYA YA VIJANA NA KWAYA YA AGAPE),MSAIDIZI WA ASKOFU DAYOSISI YA KASKAZINI MCHUNGAJI SHOO,MKUU WA JIMBO,MCHUNGAJI GLADNES SHAYO WA USHARIKA WA KALALI,PAMOJA NA WOTE WALIOSHIRIKI KWA NAMNA MOJA HADI NYINGINE KATIKA KUUGUZA HADI KUMZIKA BABA YETU MPENDWA.

    ASANTE NA BWANA AWABARIKI!BWANA ALITOA NA BWANA ALITWAA JINA LAKE LIIMIDIWE!
  • Haya WAMAREKANI WEUSI, Ni MWEUSI gani MBAGUZI zaidi wa RANGI?

    Posted: October 12, 2011, 4:59 pm by SIMON KITURURU
    Swali:
    • Si inakumbukwa WEUSI kwa WEUSI, WAAFRIKA kwa WAAFRIKA wenye asili ya KIAFRIKA hubaguana pia kwa RANGI? 
    • Au?

    Haya  turudi MAREKANI  kwa mgombea URAIS yule Herman CAIN:......Is Herman Cain a racist?

    Ndio,...... kwenye msosi wa mchana leo topiki ya watu weusi kutoko MAREKANi niliojichanganya nayo ilikuwa hiyo hapo juu!:-(

    NI hilo tu MKUU!
  • PATRICK BALISIDYA akiwa jukwaani 1996!

    Posted: October 12, 2011, 4:00 pm by SIMON KITURURU
    Patrick Balisdya ni moja ya nguli wa muziki Tanzania.Ilikumuona akiwa jukwaani mwaka 1996,.. INGIA HAPA

    www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.comwww.johnkitime.blogspot.com
    Nimepigiwakrosi na:John Kitime
  • Kila KIGUNDULIWACHO kikiwekwa kati kitafiti,....

    Posted: October 12, 2011, 3:30 pm by SIMON KITURURU
     ... kina uwezo  wa kuwa na U-HASI  na pia  U-CHANYA,......... hata  kama  JICHONI  mwa MTUZFULANI   kimtazamo kimeegemea UPANDE MMOJA  TAYARI ambao  huwa ni CHANYA  ,vuguvugu au HASI tayari kiaina.:-(

    Swali:
    • Si inajulikana kuna WAGUNDUAO hata kitu CHANYA  MAISHANI MWAO kama vile MUNGU   kupitia kitu  kijulikanacho kwa U-HASI kama KUUGUA GONJWA hasi au tu KUCHACHA?
     Ndio,....... SHILINGI  inapande mbili,....... na labda KUMBUKA  TU upande mmoja wa shilingi  kikitu  huweza kuwa bado na vipengele vingi vyenye pande nyingi kimtazamo na tafsiri!:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(


    Hebu N.W.A wanzishe tena kwa -Express Yourself



    Public Enemy waendeleze kwa - He got game



    Halafu sijui kwanini hebu Charles Wright ,..
    ... arudie tu tena kitu  kwa -Express Urself

  • TIMBULO, wimbo wako ``DOMO LANGU´´, umeiba au umeibiwa?

    Posted: October 12, 2011, 3:00 pm by SIMON KITURURU
    Kamata mwizi !
    Je Timbulo wimbo wa ``DOMO LANGU´´ kaiba au kaibiwa,Hebu angalia video hizi kwaku;... BONYA HAPA

    www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.comwww.johnkitime.blogspot.com

    Nimetumiwa na:John Kitime
  • JICHONI MWAKO unajionaje?

    Posted: October 12, 2011, 2:30 pm by SIMON KITURURU
     SIKIONI mwako ,........ unajisikiaje?

    Katika moyo wako KIHISIA zako,........unajihisije?


    Na kwa kuwa  hapa DUNIANI kuna WENGINE,....

    JICHONI mwa WENGINE,......unafikiri ukoje?
    SIKIONI  mwa WENGINE ,.......unafikiri unasikikaje?

    Katika HISIA  za WENGINE ,....... unafikiri WANAKUHISIJE?
     Na hata tukiruka  vipengele mpaka  vya kipua zako AU ZILE ZA WENGINE unafikiri unanukiaje kwa kawaida,........ SI KIBINADAMU inawezekana KILA MTU kuna mtu ambaye anapandishwa ainafulani tofauti ya HISIA  ambayo inawezekana KIBINADAMU kitu ambacho ,...... APENDWAYE  kuna AMCHUKIAYE,...... ANUKIAYE VIZURI -kwa MWINGINE hiyo ndiyo harufu MBAYA,....... IAMINIKAYE ana sauti TAMU kwa MWINGINE huko ni KUKOROMA,... nk.!?:-(

    Naendelea KUWAZA  na USIKONDE!:-(


    Hebu JAMES BROWN aanzishe mchezo upya kwa-Papa Don't Take No Mess / My Thang


    En Vogue waingilie kati na kudai wafanyacho ni- Giving Him Something He Can Feel


    Au tu tena TLC walete madai ya - Creep
  • Kuna MAMBO ambayo kuna WATU labda wako MBELE YA MUDA,....

    Posted: October 12, 2011, 1:49 pm by SIMON KITURURU

    ... na katika HAYO iliwaeleweke LABDA yahitaji MUDA na hata kizazi kingine ili YAELEWEKE ili kieleweke.:-(
    Swali:
    • SI labda kunauwezekano akina MWALIMU Nyerere na siasa zao za UJAMAA na KUJITEGEMEA , Ukomunisti, mpaka maswala ya nyani kutovaa nguo ni VIDUDE vilivyotokea kabla ya MUDA ambao waelewao WANGEKUEPO?
    • SI labda hata MAMBO ZAKO yasiyoeleweka ni waliopo tu na nyezo zao za kuelewa hazijaenda sambamba kitu kifanyacho kuna ambayo kwako yanaleta maana na kwa wengine ni ushuzi mtupu?



    Ndio,........ labda kuna MAMBO jibu ni MUDA tu ,.......... kwa kuwa baada ya MUDA wako watakao kuja kuelewa kitu kifanyacho haki ya nani tena hapa DUNIANI kuna waenziwao baada ya MUDA ingaw labda wakati huo hawapo tena DUNIANI !:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na usikonde!:-(

    Hebu Leadbelly arudie-Black Betty



    Leadbelly aongezee -Irene Goodnight


    Gotan Project waingizie na- Queremos Paz



    Halafu Charlie Wilson azime  kwa - There Goes My Baby

  • Jamani binadamu , VICHAKANI kama tu MAPORINI ni haiwei za watu!

    Posted: October 12, 2011, 4:10 am by SIMON KITURURU

    Swali:
    • Si kichawi  yasemekana WANYAMA ni watu?
    Ni mzinguo tu huu MKUU!Nakutakia KAMANYOLA bila JASHO!
  • Kama akili ni NYWELE, si nywele hupukutika?:-(

    Posted: October 12, 2011, 4:02 am by SIMON KITURURU
    Ndio,....... labda chunga ya aliyekuwa na akili JANA,....... hata kama huyo  aliye kuwa na akili jana kwako kijina alikuwa ni Simon Kitururu.:-(
    Swali:
    • Si wakati mtafiti anachunguza ujinga , mwenye akili jana  katika utafuti wa leo anaweza kuonekana hana akili?
    • Na si yajulikana hata kwa wasifiwao ya jana kiakili kama Albert Einstein hata juzi ya miaka hiyo hawakuwa wanafaulu kila kitu  kitu kifanyacho kuna utakayotafiti kuhusu wao na kustukia UJINGA?


    Ndio,....... usisahau kuna BUSARA za waliopukutika nywele,...... hata kama siri ya kupukutika kwao nywele ni UMRI!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(






    Hebu LESEGO aingizie -Africa Viva


    Lesego aongezee-Usindile


    Au tu ngoja Ini Kamoze azime kwa - Pirate

  • Kama HUJAUMIZWA na dharau za HILI.... ! Kama hujasikilizishwa UNAFUU na uelewa wa LILE...!

    Posted: October 11, 2011, 11:18 pm by SIMON KITURURU
    MAUMIVU ya dharau ni ya KILA MTU ,...........na na hapo ni hata kwa kuwa  chochote chaweza kuwa chanzo cha MAUMIVU!Swali:
    • Si unajua MAISHANI  ujisikiavyo huweza kuathiri USIKILIZIAVYO  mengine?
    • Na kwa  sababu DHARAU hutegemea tafsiri za MTU, si kila MTU  kawahi kufikiri kadharauliwa?
    • Na siunakumbuka hata toto lako mwenyeweulilolizaa MWENYEWE huwezeshwa kukuwezesha  ujisikie KUDHARAULIWA?

    Na kama  kwa kuwa CHOCHOTE huweza kuwa ni chanzo cha kumsikilizisha MTU vibaya,........ kisaikolojia CHOCHOTE kile huweza kuwa ni chanzo cha UAHUENI ,...........kwa kuwa MARA KIBAO  yote hutegemea MTU anajisikiaje kabla ya kuathirika na KITU hata  kama hicho kidude ni DHARAU,....... kitu kifanyacho kuwa CHOCHOTE KILE huwezakugeuka ndicho FARAJA ya MTU na ndio maana  kuna wafarijikao hata kwa kupata taarifa kuwa KAFA mtu.:-(
    Swali:
    • Si kuna wafarijikao hata kwa kusikia VITA imeanza kama wafarikavyo  wasikiapo umeshinda na njaa au sikukuu yako ilikuwa MBAYA na DAGAA hawakutosha?
     Ndio,...... labda kama una HILI,....... yaweza kuwa ndio misingi ya UATHIRIKAVYO na LILE,...... kitu kiwezachokuwa ndicho kikusaidiacho unatafsirije hata nini ni DHARAU.:-(Ni wazo tu hili MKUU!:-(

    Hebu Jackie Chan na Chriss Tucker wabadili kwa -WAR


     Edwin Starr mwenyewe afankifai katika hilihili pini- War


    Halafu  Jerry Butler asoulifai kwa - Only The Strong Survive


    Kisha NATALIE COLE azime tena kwa-This will be

    .
  • Sio LAZIMA kila kitu kiwe SIRIASI!

    Posted: October 11, 2011, 6:00 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,....... pamoja na kuwa kuchukulia vitu SIRIASI ni moja ya kitu BINADAMu awezacho,....... labda yasiyo SIRIASI na wasio SIRIAZI wanaumuhimuwake pia  hapa katika hii DUNIA pia.
    Swali:
    • Unabisha?
    • Je unaweza kuafodi kutokuwa SIRIASI?!
    Ndio,...... maisha ni MAFUPI,....... na labda si kila kitu lazima kiwe SIRIASI kila wakati ,....
    ........LAKINIIII!:-(Ni wazo tu HILI Mheshimiwa !:-(


    Au tu Admiral Tibet,Shabba Ranks na Ninja Man walete usiriasi kwa - Serious Time

    Shabba Ranks arudi na Debroah Glasgow katika-DON'T TEST ME


    Shabba Ranks aongezee- Telephone love

    Au tu Maxi Priest aingilie kati kwa - House Call

  • Ukisifiwa na UMPENDAYE hata kiuongo , labda SIFA ZILEZILE ZA WAKWARE kiutamu NI tamu zaidi!

    Posted: October 11, 2011, 3:10 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,....... kuna WATU KWAKO  hata kisifa ziitwazo matusi   WAKIKUTUKANA ,.........tusi LILELILE hukolea zaidi pilipili kimfurukuto wa MAUMIVU kuliko WENGINE.:-(Swali:
    • Si labda hata WEWE MWENYEWE umeshastukia si kila akuchekeaye  HUWA unajisikia vizuri  kakuchekea  kistaili ya ujisikiavyo ukichekewa na ujingongaye kwake?
    Ndio,.......  hata kijambo a.k.a USHUZI wa MPENZI  ,...
    ....kwa MPENZI yasemekana huvumilika kirahisi zaidi!:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(Nakutakia JUMANNE  KIBONGE  Mkuu!

    Hebu Mpume Sikakane aingilie kati kwa - Baba ka Mdudu


    Au tu tena Bisso na Bisso wazime na - Bisso na Bisso

  • Tatizo kubwa la ajali isababishwayo na MLEVI aendeshaye GARI,....

    Posted: October 11, 2011, 2:41 pm by SIMON KITURURU
    ... waathirikao na AJALI mara nyingi huwa ni pamoja na WALE ambao hawajalewa ,...... na hapo ni kama tutaruka kipengele kuwa hao  WAUMIZWAO na MLEVI wala hawakuwa kwenye gari liendeshwalo na MLEVI.
    Swali:
    • Si umestukia kuwa labda kikuumizacho chaweza kuwa wala hukuhusika nacho kimtengenezo?
    • Si unakumbuka YAKO yanauhusiano hata usiouona na WENGINE?
    Ndio,....... labda pamoja na kwamba swala ni lako,......... yaweza kuwa lina MCHEZO wa kuumiza mpaka wasio husikanalo kivyako,.......kitu kifanyacho kuwa labda kumbuka kuwa na huruma  ya  KITU  kihusucho WENGINE kama unampango  KIVYAKO uwezekanao ambao huwezakunyea kisima ujuacho hutachota maji kwa kuwa wakitumiao  ni wengine,....... kwa kuwa  WENGINE kwa WENGINE kimengine,...
    ....ni WEWE mwenyewe HUYO.:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
    Hebu turudi UGANDA ili Radio &Weasle wanzishe upya kwa - Kuku


    Jose Chameleone aendeleze kitu kwa - Vumilia


     Radio & Weasele warudi tena na -Nakutamani


    Halafu tu wazime kwa -ZUENA

  • Kunawadaio UZURI ni BOMBA la NGAO ya WENYE TABIA mbaya kutostukiwa!

    Posted: October 11, 2011, 11:12 am by SIMON KITURURU
    Ndio,....... yasemekana ili WATU waone MAKALI ya TABIA MBAYA za mwenye SURA NZURI,....... inabidi kwanza waruke SURA na UMBILE zuri la KIDOSHO ili wastukie anatabia mbaya au hata waanze kuingiwa WAZO kuwa labda PAMOJA na kuwa KIDOSHO  ni MREMBO kisura , tako , usafiri  pamoja na vikorokocho vingine vya kudakia WATOKWA UDENDA bado labda  anamchezo wakujikojolea KITANDANI bado mpaka ukubwani  na mara ya mwisho  KIDOSHO kujilowanisha akiwa  usingizini labda ni siku hiyohiyo aliyowekwa kwenye lensi  ya macho ya avutiwaye na sikioni  mwa aliyedakwa kwa sauti nzuri utafikiri ni ya malaika kiruka njia .

    Swali:
    • AU? 
    • Na si kwa SILAHA ya UZURI yasemekana WAREMBO husamehewa UJINGA  kuliko siye wenye SURA mbaya?
    • SI unajua DUNIA yetu imejaa watu waaminio na kuthamini ya JUUJUU tu kitu kifanyacho kuwa kama YA MTU YALE MAZURI yamejificha chini ya LISURA lake baya kama ramani ya kipenyo kwenye tako la nguruwe, hayo yake mazuri anaweza mpaka kufariki hayajagunduliwa wala kustukiwa?

    NDIO,...
    ... kuna wenye mambo BOMBA SANA  hapa DUNIANI  wakwepwawo na WATU  kisa tu KISURA imeaminika ni MAKATILI au tu sio watu wazuri.
    Swali:
    • Si inasemekana kuna wadaio wapo watu WAZURI tu wenye tabia za KIMALAIKA waliokaa KIVIBAKA kitu kifanyacho wakisogelea tu WATU, mtuz huanza kujipapasa kama bado POCHI wanalo kwa kuamini KISURA tu wanajua KIBAKA ni nani?
    • Na sinasikia hata KIKUKOPA MTU kuna ambao kisura tu kuna wawakopeshao kisa wamekaa kama vile ngawira pesa wanazo kitu ambacho ni moja ya siri zao kwanini KITAPELI wao ni washindi?
    • Na si inasemekana kuna WAJUAO na ni muonekano wao tu hufanyao HAWASIKILIZWI  hata wakati wanatoa suluhisho?
    • Na siinasemekana kuna waliompigia mpaka Rais Kikwete kura kisa wanampenda SURA?

    Ndio,....... labda SHETANI hajakaa kishetani afikiriwavyo,........ na labda ukitaka kustukia kuna uwezekano hapo au katika hilo yupo SHETANI,....... moja ya kitoacho siri ni kama hapo ni PATAMU kunoga na unajisikia vizuri sana hapo au katika hilo hata kama ni la KIZINZI  unajiaminisha  kuwa hilo ni KITENDO TU CHA NDOA na unogewavyo sio KIZINZI.:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
    Hebu Checo Acosta waingilie ghafla na kubadili mchezo kwa-La Cinturita



    Choubou alainishe kidogo kwa-Andrea


    Halafu WANAUME waturudishe tu tena- DAR mpaka MORO




    Halafu T Pain azime kwa-5 O'Clock

  • KARIBU DUKA LAKO (DUKA LA KUUZA NA KUNUNUA)

    Posted: October 10, 2011, 8:26 pm by SIMON KITURURU
    Duka Lako


    Habari za leo Mabibi na Mabwana... Ni matumaini yetu nyote mu wazima. Tunapenda kuchukua nafasi hii ya pekee kabisa kuwakaribisha sana katika mtandao huu wa kipekee,kisasa na waina yake ambapo mmiliki wa mtandao huu sio sisi lakini ni wewe ndio maana ukaitwa DUKA LA KUUZA NA KUNUNUA. www.dukalako.blogspot.com . Duka lako ni mtandao ambao umetengenezwa kwa nia na madhumuni ya kukurahisishia wewe mfanya biashara mtanzania popote pale Duniani, au wewe mtu binafsi kuweza kununua au kuuza bidhaa yako yoyote ile kupitia mtandao huu wa DUKA LA KUUZA NA KUNUNUA.

    Bidhaa hizo ni pamoja na Computers,Simu za mkononi,vifaa vya majumbani, Vifaa vinginevyo mbali mbali, Magari nyumba na kitu chochote ambacho unataka kukiuza kiwe ni kipya au chazamani utaweza kukiweka hapa na kitauzwa moja kwa moja. Kama ni Second hand mwenye mali atatakiwa kusema kabisa.

    Yafuatayo ni maelezo ya jinsi ya kutumia mtandao huu:
    1. Hii ni fursa ya mtu yoyote yule anaetaka kuweka bidhaa yake ipate kuuzwa na kununuliwa hapa,ndio maana ikaitwa Duka lako(Duka la kuuza na kununua). Utatakiwa utume bidhaa yako ukiambatanisha na bei zako pia mawasiliano ya barua pepe ama namba yako ya simu.

    2. Ni muhimu unapo leta bidhaa yako iwe ni picha halisia kabisa ambayo umepiga wewe mwenyewe na sio ambayo umeitoa Google ili kuepusha usumbufu wakati unawasiliana na mteja wako anaetaka kununua bidhaa hizo.

    3. Mtu anaetakiwa kuweka bidhaa hapa anatakiwa aweke specification ya bidhaa yake kama zipo mfano Kompyuta,simu na vitu ambavyo vitahitajika kuweka maelezo yake, atatakiwa kifanya hivyo ili kumrahisishia mteja wake kufanya maamuzi yaliyo sahihi na ikumbukwe kwamba duka hili ni lako wewe ambae utaweka bidhaa zako hapa.

    4. Kwa wafanya biashara ambao wanamiliki tovuti za makampuni yao tunawaomba sana mtuwekee na link za tovuti zenu ili mtu akiingia apate kuona zadi kuna nini ndani ya duka lako.

    5. Katika kuweka Bidhaa hizo katika duka Lako mteja atachangia kiasi kidogo cha fedha ili kuendeleza ufanisi wa kazi zetu,pia atatangaziwa bidhaa zake katika njia mbali mbali.

    6. Tunaomba Baada ya mteja kupata mteja na bidhaa yake kuuzwa awasiliane nasi ili tuweze kuitoa bidhaa hiyo na kuwapisha wengine wanao weka bidhaa zaidi.

    Wateja wetu kumi wa kwanza ambao tutapata barua pepe zao kupitia (dukalako@live.com) baada ya kumaliza kusoma hapa, watauza bidhaa zao hapa Bure kabisa kwa muda wa wiki moja kuanzia leo, kuwa wa kwanza sasa kuweka bidhaa yako hapa na kuuza na kupata wateja mapema iwezekanavyo. tunawahakikishia kuwa kwa njia hii mtaweza kuuza vitu vyenu kwa haraka na uhakika zaidi. kwa maelezo zaidi na kuona zaidi Tembelea Duka lako sasa. Tunatanguliza shukrani zetu pia ukiona hii mwambie na mwenzako pia asipitwe na Duka hili muhimu kabisa kwa watanzania wote popote Duniani.

    Tuma Bidhaa zako kupitia Barua Pepe: dukalako@live.com
    Wasiliana nasi kabla ya kutuma bidhaa au baada ya kutuma bidhaa kupitia namba ya simu hizo chini:
    +255 762039028 au +255 714233895



    Tembelea Duka hili hapa: www.dukalako.blogspot.com
  • Katika KUMBUKUMBU: I have a DREAM- Dr Martin Luther King Jr

    Posted: October 10, 2011, 2:14 pm by SIMON KITURURU

    Swali la kizushi:
    • Una NDOTO?



  • Hivi ni WATANZANIA wangapi wamewahi kufikiria kukwea MLIMA KILIMANJARO ?

    Posted: October 10, 2011, 1:07 pm by SIMON KITURURU
    Kuna mambo  yako tu JIRANI ,........ kama MUBGA za WANYAMA Tanzania au Milima ya ULUGURU,........ ambayo ni WAGENI  waonao thamani zake na  watambuao hata tamutamu zake kimahudhurio.
    Hebu tumdeku  MGENI  akijipima  kwa kukwea ndude ya BONGO,...... bila MIKONO wala MIGUU .....




    Au tusikie ya Neil Duncan, Dan Nevins, Kirk Bauer wa Disabled Sports USA,...
    ... katika yao ya Mlima Kilimanjaro,....


    Ndio,....... kuna wadaio MAISHA ni magumu BONGO,........ kitu ambacho tayari ni kigumu tayari na kifanyacho mengine ni ya KITALII kuwa ni LAKSHARI.

    Swali la KIZUSHI kwa FISADIZ:

    • Vipi WAHESHIMIWA Fisadiz ambao labda muna MUDA na PESA, ..... mshawahi tembelea hata MIKUMI kujua angalau KIBOKO JIKE uso kwa uso anapendelea wanja ya rangi gani?
    Usitishike MKUU labda nazingua tu!:-(Jumatatu NJEMA!
  • Bendi ya akina mama, WOMEN Jazz BAND 1966

    Posted: October 10, 2011, 6:34 am by SIMON KITURURU
    Kijakazi Mbegu kwenye solo gitaa



    Je unajua kuwa 1966 kulikuwa na bendi ya akina mama watupu hapa Tanzania?
    Angalia picha zao wakiwa kazini kwa,.....

    .......kubonyeza HAPA-- www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.com
    www.johnkitime.blogspot.com

    Nimepigiwa krosi hii na:John Kitime.
  • URBAN PULSE yaibuka kidedea ndani ya SPORAH SHOW

    Posted: October 10, 2011, 4:45 am by SIMON KITURURU
    Salam



    URBAN PULSE CREATIVE ikiwakilishwa na Frank pamoja na Mish Ze Fyah Sis walipata fursa ya kushiriki katika Game show ilioandaliwa na Sporah Show kwa ajili ya kutafuta mshindi ambae atabuni Slogan Nzuri ya Kampuni yao pamoja na Sporah Show.
    Katika Game show Hii ,Urban Pulse waliibuka washindi., Asanteni,URBAN PULSE [www.youtube.com]

    Nimetumiwa ndude HII na:Frank Eyembe wa Urban PULSE Creative
  • Ambayo ni kama utani kwa asiye mwenye uanamke wa hata JIKE la MJUSI,...

    Posted: October 10, 2011, 4:40 am by SIMON KITURURU
    ... ila ikiingia kwenye  kipengele kihusishacho  YA HASI ya yalioingilia kwenye mpaka  UKE wa MJUSI ambayo yanamhusu huyo MJUSI JIKE au waathirikao na  yamtokeayo MJUSI JIKE hata kwa aathirikavyo na kilichoingilia kwenye wake UKE,......unaweza kugundua  chenye kuoanisha UKE  na MWENYEUKE labda kinamchezo wakuathiri mpaka wasio na UKE  hata kama hapa hatuwaoanishi na MJUSI dume!:-(

    Swali:
    • Si unakumbuka kutonielewa RUKSA?
    Na katika yadhaniwayo ni UTANI hata  kwenye UUME,...
    .... yanaweza kuwa yanakata makende hata ya MWANAUME kujisikia ni MWANAUME,...... kitu kiwezacho kuwa ndicho kiathiricho wengi wenye kuhusiana na huyo KIDUME hata kama mahusiano naye hayana uhusiano na UUME au tu UKE wa waathirikao na AATHIRIKAVYO kidume,...
    ... na labda sio UTANI HUU katika hili aisee!:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na  ni ruksa kulitemea koozi. :-(
    Hebu Issa BAGAYOGO aingilie kati na kurudisha-DIARABI


    Halafu hebu tu Erykah BADU arudishe TENA heshima hapa kijiweni kwa kudunga tena pambio-Annie don't wear no PANTIES

  • HARUFU nzuri ya MPENZI labda SI ile tu ya PAFYUMU ya kikojoleo kizuri cha MWANABIBI aisee!

    Posted: October 9, 2011, 7:34 pm by SIMON KITURURU
    Na kama unampenda mpenzi kwa ANUKIAVYO,....... kumbuka HUYO  MPENZI  anajamba tu ki-SIO PAFYUMU  PIA  na  LABDA pia  kwa hilo ananuka kikwapa  TU kama KAWA tu kijeba MWANABIBI  baada ya kujiswafi,...... kitu kifanyacho,........ kama moja ya misingi ya umpendavyo MPENZI ni jinsi anukiavyo,......LABDA aisee jichunguze kuwa upendacho ni MANUKATO au ni huyo MPENZI ambaye UPENZI WAKE KWAKO NI KWAKUWA TU UNAMUITA MPENZI  ambaye asipojiosha kidude wote twajua atanuka hata kama baada ya kujinyunyuzia manukato hanukii kwa kila pua  ya mtu  kisio KIMAVIMAVI ,...
    .....ni MPENZI wako hata kikushikana tu mikono mbele za watu KATIKA JAMII UIOGOPAYO kwakuwa ina BABA na MAMA na WASENGE FULANI ambao hata HAWAKUHUSU ,...
    ...waaminio nyie ni WAPENZI .:-(
    Swali:
    • Si unajua kuna wapendao ANDAZI  ambao wafikiriacho ni kuwa wampendaye NI  yule tu katika MAPENZI YA MAANDAZI ni   mwenye ANDAZI ?

    Ndio,...... ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(


    Hebu RAY CHARLES ajaribu kubadili kwa-A song for U


    Halafu Whitney Houston arudie ndude hiihii -A song for U


    Whitney ajaribu tena -I will always love U


    ....halafu tu BOB Marley aingilie kati  tena  nakubadilisha kipengele kwa -Concrete Jungle




    Halafu tu huyuhuyu KIJEBA  Bob Marley azime tu MSHAWASHA  kwa -HEATHEN


  • Wakati BINADAMU anahangaishwa mpaka na UHURU wa kujamba!

    Posted: October 9, 2011, 7:00 pm by SIMON KITURURU
    Labda ni KWELI,....... ipo siku BINADAMU anaweza kuwa HURU akiwa HAI!:-(
    Swali:
    • AU?
    Ndio,...... katika yasiyo HURU,...... labda ndio utastukia nani ni HURU!:-(

    Hebu BILAL aendeleze somo kwa-Someday We'll All Be Free



    NI hilo tu KAMANDA!
  • Kutoka kwa Mheshimiwa Rais Jomo KENYATTA with Love: Kumamaye zenu!

    Posted: October 9, 2011, 3:05 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,...... labda ni LUGHA tu,...... lakini msikilize na ni kweli Mheshimiwa Jomo Kenyatta kama siye tu alikuwa anakatizia denge kwa SENTENSI kama hizo kwenye mpaka HOTUBA ZAKE,...



    Swali:
    • Si umestukia ukiondoa kumamaye kuna mengine aongeleayo?


    Ni hilo tu  MHESHIMIWA!:-(
  • MAHITAJI ya JEMADARI KIGOLI ya kuongozwa na KIPOFU!

    Posted: October 9, 2011, 1:37 pm by SIMON KITURURU
    Ndio labda ni MATUSI kufikiria WATUONGOZAO  wanaona kisa wana macho yaonayo,...
    .... hasa  ukiwa na USHUHUDA waonao ambao WENGI  ndio waitwao VIONGOZI katika DUNIA hii yetu  mpaka LEO HII watupelekako sie tutakao kwenda SEBULENI  ni kawaida kwa kufuata macho yao hujikuta tunaishia CHOONI!:-(
    Swali:
    • Unabisha?
    • Na si umestukia labda hata katika kudaka matamu huhitaji JICHO  wala kuona kitu kifanyacho labda KUONA  kumezidishiwa tu sifa wakati utamu kwa wengi labda kikufaisdi huufungia macho?


    Ndio,....... labda  tuhitajiye KIUONGOZI  ni KIPOFU,......ambaye haangalii sura bali  hisia za nini ni sahihi  kitu ambacho HII miviongozi yetu  kwa kutumia MIJICHO YAO haioni !:-(

    Ni wazo tu hili  MHESHIMIWA!:-(Jumapili njema MKUU!

    Hebu ghafla Lokua Kanza aingilie kati kwa- Le Bonheur / Gib Mir Ein Wunder


    Au tu EDDY GRANT azime tu  kwa-Hello AFRICA

  • Nyerere Day 2011 in Washington DC

    Posted: October 9, 2011, 1:06 pm by SIMON KITURURU
    Maadhimisho ya nne ya kuenzi maisha na kazi za Mwl Julius K. Nyerere yatafanyika Oktoba 15, 2011 hapa Washington DC. Mmoja wa waasisi wa Julius Nyerere Comemoration Bwn Rick Tingling akielezea maandalizi ya siku hiyo katika video hapa chini

    http://www.youtube.com/watch?v=dfp2o_kTmyw

    NYOTE MNAKARIBISHWA!Itafanyika:
    Howard University Basement Auditorium725, 2225 Georgia Ave, NW, Washington, DC 20059FROM 3PM-6PM
    MAELEKEZO KUELEKEA Howard University Hospital Basement Auditorium:

    • Ingilia mlango wa mbele wa Hospitali unaotazamana na Georgia Avenue.
    • Pita kwenye dawati la maelezo kwa utambulisho
    • Endelea mbele mpaka kwenye "lift" zilizo kama yadi 50 toka dawati la mapokezi.
    • Chukua "lift" / elevator kuelekea sakafu ya chini (basement).
    • Elekea upande wa kulia ukifuata alama zinazoelekeza ulipo ukumbi.



    BARAKA KWAKO NA ASANTE KWA USHIRIKIANO!http://www.changamotoyetu.blogspot.comhttp://www.youtube.com/user/mutwiba



    AMBATANISHO: MAELEZO KUHUSU MAADHIMISHO HAYO.
    NOTE: Mabadiliko pekee niliyojulishwa ni kuwa Balozi Mwanaidi Maajar hataweza kuhudhuria kwa kuwa atakuwa nje ya mji.




    4th Annual Julius K. Nyerere Commemoration
    On Saturday, October 15, 2011, the Julius K. Nyerere Commemoration committee will convene its 4th Annual program commemorating the life and work of Julius Kambarage Nyerere at Howard University Hospital auditorium from 3:00 – 6:00 pm. The Tanzanian Ambassador Her Excellency Manaidi Maajar was a featured guest at last year’s program and has been invited to address the commemoration again this year. The exciting program will feature drumming by Ngoma Na Rafiki, as well as performances by Maryland’s Taritibu Youth Association. Featured speakers will include, among others, Dr. John Rutayuga of Ukimwi Orphans Assistance, Dr. Baruch of Everlasting Life Health Complex, Wisson West of Serengeti Gallery, Elvira Williams of AHEAD and Jessica Mushala of S.H.I.N.A. will be Mistress of Ceremonies. The program will also feature a Tanzanian style auction of African art, and for the 3rd year in a row be catered by Caroline’s Kitchen.

    Who was Julius Kambarage Nyerere and why should we commemorate his life and work? Simply put, he was a man who built a political career fighting poverty, ignorance and disease – and winning.

    This program was begun by local activist and admirer Rick Tingling-Clemmons in collaboration with a number of Tanzanians to commemorate the life and work of Julius Nyerere, the first President of Tanzania, who was a visionary leader – kind, astute, a dedicated educator who led the nation to adopt Swahili as a national language and embraced the title Mwalimu, which means teacher in Swahili, and implemented Ujamaa – Swahili for collective work and responsibility. He authored several books; was a tactician and a pan-Africanist who materially supported many of his fellow African nations’ liberation movements.

    Commemorating his life should be seen as one of the keys that will unlock the miseries of today’s woes as we fight against poverty, ignorance and disease the world over.

    We encourage you to attend this family-friendly life-affirming event.



    Nimetumiwa na:Mubelwa T. Bandio
  • Nini cha kufanya katika ku::Create FREE Green Card photos online, AND fill out the U.S Diversity Visa Form

    Posted: October 9, 2011, 4:03 am by SIMON KITURURU
    Msaada kwa wanaotaka kujua pa kuanza na nini cha kufanya:

    1. Follow this link to create required photo: www.egreencardphoto.com
    2. Follow this link to validate the photo size: [https:]
    3. Follow this link to fill out the 2013 Diversity Visa program (DV-2013): https://www.dvlottery.state.gov

    Maelezo yametoka/source:www.wavuti.com/4/post/2011/10/how-to-create-free-green-card-photos-online-and-fill-out-the-us-diversity-visa-form.html
    el fin! Recalculating...
    Subi|wavuti.com

    Nimepigiwa Krosi na:Subi wa WAVUTI
  • Ukinywa MAJI jiandae kukojoa!,...

    Posted: October 8, 2011, 8:27 pm by SIMON KITURURU
    Swali kwa ung'eng'e:
    • Sounds simple and straight foward, right?
    Ndio,...... kuna washangazwao na ufikiriayo yako wazi aisee,.........na moja ya lililowazi ni kuwa MTU chini ya nguo yuko uchi.Swali:
    • Si umestukia kuna washangaao MTU akiwa uchi hata kimawazo wayajuayo yapo?
    Ndio,....... katika kuwa UCHI ,....... labda  kishangazacho ZAIDI ni kuwa kuna washangaao!:-(


    NI wazo tu hili MHESHIMIWA!Tubadilishiwe wazo na Joti katika - Jibwa Koko


    Halafu Ferre Gola na Heritier Watanabe wabadili tena kwa - Nostalgie



    Halafu Pepe Kalle azime tena kibolingo  zaidi kwa -Pon moun paka bouger
  • MAMA WA KICHINA AGOMA KULIPA USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI KISA JUMAMOSI SIYO SIKU YA KAZI

    Posted: October 8, 2011, 7:15 pm by SIMON KITURURU
    Mama wa Kichina akiwa amechachamaa na kuelekea katika Jengo la NMB Tawi la Mbalizi Road Mjini Mbeya kuomba msaada kwa mapolisi.
    Moja ya watumishi wa kampuni ya AAICO ambayo ndiyo wamepewa dhamana ya kukusanya ushuru wa maegesho ya magari jijini mbeya akitoa mnyororo kulifunga gari ya wachina hao huku mama wa kichina akilia kwa hasira
    Mama wa kichina akimtolea maneno makali binti Eliza mkusanya ushuru wa maegesho ya magari huku mchina huyo akiendelea kugoma kuwa hawezi lipa ushuru siku ya jumamosi na jumapili kwani ni siku za mapumziko siyo siku za kukusanya ushuru


    Mume wa mama mama wa kichina akijaribu nae kuwaelewesha wakusanyaji waushuru wa maegesho yamagari kuwa wameshazoea hivyo kutolipa siku ya jumamosi na jumapili kwani ni siku za mapumziko


    Picha zaidi ya tukio hili tembelea: www.mbeyayetu.blogspot.com

    Nimetumiwa na:Fredy Tony ICT wa MBEYA Yetu BLOG
  • Wakati kuna ambao KUTESTI ZALI kabla ya NDOA ili kucheki kama MIMBA inashika ni OYEEE kisana tu yani!

    Posted: October 8, 2011, 7:03 pm by SIMON KITURURU
    Yasemekana  SIKU HIZI  ni UJANJA  kabla KIDUME hajaoa,...
    .... kutesti zali KWANZA!:-(
    Swali:
    • AU?

    • Lakini ,....JE ?
    ....kwani ni mangapi  inabidi tuamini  tu bila kutesti zali?.... tunakoenda si itafikia WATOTO WA MAMAM KISEBENGO KILA MAHALI  kila wakati kutaka kucheki kuwa lile liaminikalo kuwa -NI siri ya MAMA KISEBENGO KIUHAKIKA ndiye ajuaye nani hasa  ni baba ya  MIMBA ya MAMA KISEBENGO  labda aijuaye si MAMA KISEBENGO pekee kwa UHAKIKA  kwa kutesti kuwa kitu cha kawaida katika DUNIA HII ambayo hakuna IMANI tena?
    Ndio kunatuyajuayo yale ya UKIGUSA MOTO utaungua LAKINI ,....... na labda haihitaji  mtu mwenyewe KUTESTI zali kama umeona tayari  jinsi  mwingine  alivyogusa moto akaungua.


    Swali :
    • AU?


    Ndio,...
    ..... na labda kuna ambao  hata kwenda MBINGUNI  wangetaka kutesti ZALI kwanza ,...
    ... ili kucheki kama ni kweli kuna MBINGUNI kabla ya kuamini DINI zao.
    Swali:
    • Kwani huoni  jinsi IMANI  ilivyopungua DUNIANI kitu ambacho  labda kuna watakao UHAKIKA tu na kusahau utamu wa KUAMINI tu?


    Ila kama WEWE ni miongoni mwa waaminio ni UJANJA kutesti zali kwanza  kabla hujachukua JUMLAJUMLA,........ kumbuka kuna ambao katika kutesti zali kwa nia ya kucheki kama MIMBA inashika kishughuli ambazo kwa kawaida hufanyika PEKUPEKU,.......kuna waibukao na gono, kaswende na UKIMWI na wakati huo bado MIMBA haijashika pia!Swali:
    • Unabisha?

    Ndio,....... ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

    Hebu tu tena Patricia Faria abadili wazo kwa kurudia tena-Fofoca Joaquina



    Yuri da Cunha arudie-Homem é bom



    Buju Banton aingilie kati nakubasili mchezo kwa-Love Me Browning



    Buju Banton apitilize kidogo na kuharibu kwa - Over Di Dickie



    Mad Cobra ajaribu kulainisha tena kwa kurudia -Flex


    Halafu Ray Barretto arudishe tena ustaarabu kijiweni kwa-El Watusi



    Halafu Willie ROSARIO azime kistaarabu pia kwa -WATUSI Boogaloo


  • MBWANA MATUMLA ajifua kumkabili FRANSIC MIYAYUSHO.

    Posted: October 8, 2011, 3:20 am by SIMON KITURURU


    Mabondia Mbwana Matumla (kushoto) na Mussa Sunga wakipigana wakati wa mazoezi ya kambi ya Ilala, Dar es salaam jana. Kulia ni kocha Mohamedi Chipota.

    Matumla anajiandaa na mpambano wake wa ubingwa na Fransic Miyayusho litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu.

    (PICHA na HABARI na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
    --
    Super D Boxing Coach
    Photojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania



    Nimetumiwa na Rajabu Mhamila, SUPER D
    wa SuperD Boxing Coach
  • Wakati Rais KIKWETE leo anatimiza Miaka 61

    Posted: October 7, 2011, 7:55 pm by SIMON KITURURU
    Swali la kizushi:
    • Hivi ni WATANZANIA wangapi hawajui tarehe ya siku waliyozaliwa?



    Rais Kikwete alizaliwa tarehe SABA mwezi wa KUMI mwaka 1950  ,........kijijini Msoga, BAGAMOYO , TANGANYIKA.
    Happy Birthday Mr Rais!
    NI HILO TU!






    Au tu tena Mighty SHADOW aingilie kati na kubadili mchezo mzima  kwa-You looking for horn



    Mighty Sparrow akatizie denge kwa - Water de Garden


    Au tu Mighty ARROW ajaribu kuzima kwa-Hot Hot Hot


    Kabla  tu Lord Kitchener  hajazima tena kwa - Sugar Bum Bum


  • Hongera WANAWAKE wa shoka ELLEN JOHNSON SIRLEAF, Leymah Gbowee na TAWAKKUL KARMAN kwa kutunukiwa tuzo la NOBEL!

    Posted: October 7, 2011, 6:30 pm by SIMON KITURURU
    Ellen Johnson Sirleaf RAIS wa LIBERIA

    Mwanaharakati  wa Ki-Liberia  Gbowee

    Mwanaharakati, Mwanasiasa na Mwanahabari waki-YEMEN Tawakkul Karman



    HONGERA ZENU  akina MAMA!Habari zaidi kongoli  HAPA



    Ngojea nilolome kidogo!

    Tukiachana na kuwa hili TUZO  la NOBEL kama tu kwenye sinema lilivyo la OSCAR mie huzinguka nalo  kwa kuwa huwa naamini kuna ajenda za chinichini ZIKIWEMO zile za KISIASA na KIMIKAKATI ZAIDI  ambazo hufanya maamuzi ya nani ashinde na kwa hilo kufanya  kuna mpaka akina Rais OBAMA kutunukiwa NOBEL  kitu ambacho siamini kama walistahili,....
    .... bado  labda lina mchango wake kiaina ukizingatia BINADAMU akihusika katika chochote kile labda bado kitakuwa na mapungufu ya KIBINADAMU!
    MWISHO wa MLOLOMO!:-(

    Hebu  tubadili  mshawasho kwa kumuachia Dama Ludmila aturudishe tena Luanda ,ANGOLA na kuanzisha upya kwa - Acaba de Dar o Toque





    Dj Sottão aingilie kati na -Sentido Silencio


    Dj Sottão aendeleze mwanzo wa wikiendi hii kidhambidhambi tena kwa-Moço direito



    Au tu dhambi ikae njenje tu katika siku hizi ambazo labda nizamwishomwisho,...:-(

  • Wakati TONY MELENDEZ asiye na MIKONO anapiga GITAA kwa MIGUU!

    Posted: October 7, 2011, 3:33 pm by SIMON KITURURU
    Swali:
    • Si kuna wafikiriao unahitaji mikono kupiga GITAA?

    Hebu baada ya kusikia kifupi kuhusu yeye  ashushe pini:-Let it be

    Tudeku tu  pia  na yaliyojiri    PAPA John Paul akiwepo kushuhudia  katika kibao,....- Never Be The Same

    Ndio,...
    .... labda kuna GITAA  lako KIMAISHA  ambalo limezoeleka kupigwa mimba  hata  KIPESA au tu KIVYETI  vya ELIMU KUBWA ,........lipigikalo bila PESA wala ELIMU  kama utatumia kitu kingine  kulipa mimba tu LIZAE NEEMA kwa kutumia visivyozoeleka!

    Swali:
    • AU?

    Ndio,....... labda UNAWEZA udhaniacho huwezi,........ ila JARIBU kwa njia nyingine  kama NJIA watumiazo wengine kwako HUNA jinsi ya KUWANAZO!
    Ni hilo tu MKUU!Ijumaa na WIKIENDI NJEMA!
  • Video ya KASHASHA ikiporomoshwa na TANCUT ALMASI ORCHESTRA 1989

    Posted: October 7, 2011, 2:19 pm by SIMON KITURURU
    Kuanzia album ya kwanza ya Tancut Almasi Orchestra , bendi iliendelea kutoa vibao vilivyoweza kudumu katika kumbukumbu za wote waliovizisikia kuanzia enzi hizo.

    Album ya kwanza ilikuwa na nyimbo kama vile:
    Nimemkaribisha nyoka(Kasaloo Kyanga), Kashasha(Kyanga Songa), Tutasele (Kasaloo), Mtaulage(John Kitime), Big Four (Utunzi wa wimbo huu ulileta utata kwani ulianza kwa ugomvi kwa Mamado Kanjanika kudai kuwa aliutunga yeye wakati akina Kasaloo na Kyanga wakidai wameutunga wao. Lakini hatimae akina Kasaloo waliacha ugomvi huo na Mamado hutajwa kama mtunzi wa wimbo huu. )
    Hebu angalia mambo yalivyokuwa wakati KASHASHA likipigwa.John Kitime niko hapo na miwani kubwa nikiungurumisha rhythm guitar
    -- BONYA HAPA

    www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.comwww.johnkitime.blogspot.com

    Nimetumiwa na :John Kitime
  • BABA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA KOSA LA KUMSHINIKIZA MKEWE KUNYWA SUMU HADI KUFARIKI

    Posted: October 7, 2011, 1:16 pm by SIMON KITURURU
    Mweyekiti wa kijiji cha Ijumbi kata ya Ruiwa wilaya ya Mbrali Bwana John Mkalimoyo akimfariji dada wa marehemu Nuru Masuba aitwaye Stumai Wilson ambapo marehemu alikuwa akiishi naye Kijiji cha Mapogolo kapunga.







    Na mwandishi wetu

    Mohamed Mwawipa mwenye Umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Ijumbi kata ya Luwiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya ameshikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa tuhuma za kumshinikiza mkewe kunywa sumu baada ya kumtuhumu kumwibia shilingi laki nne na elfu hamsini.

    Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa marehemu Nuru Masuba alikuwa na ugomvi kwa kipindi kirefu na mumewe hali iliyopelekea wakatengana lakini October 4 walirejeana upya mahusiano yao hadi kifo kilipomfika.

    Akiongelea tukio hilo mwenyekiti wa kijiji cha Ijumbi John Kalikumoyo amesema mtuhumiwa alikiri kutenda tukio baada ya kuhojiwa na uongozi wa kijiji na kwamba endapo mwanamke huyo asigekubali kunywa sumu angetumia silaha ya jadi aina ya kisu kumuangamiza kama fedha hizo hazitoonekana.

    Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alipomuulizwa juu ya kukamatwa kwa Mohamedi Mwawipa alisema kuwa taarifa hizo bado hazijamfikia na kwamba atazitolea ufafanuzi pindi atakapo pata taarifa kamili kutoka kwa mkuu wa polisi wilaya ya Mbarali.


    Mtuhumiwa Bwana Mohamed Mwawipa ambaye alimshinikiza mkewe Nuru Masuba kunywa sumu baada ya kumtuhumu kuwa amemwibia fedha taslimu shilingi laki nne na elfu hamsini akionesha askari wa upelelezi eneo alilonywea sumu mkewe



    Mwili wa marehemu Nuru Masuba aliyeshinikizwa kunywa sumu baada ya kutuhumiwa kumwibia fedha shilingi laki nne na elfu hamsini na Mumewe Mohamed Mwawipa akipelekwa kuhifadhiwa kaburini, baada ya uchunguzi wa daktari na polisi kukamilika.


    PICHA  na HABARI  na- Mbeya yetu Blog


    Nimetumiwa na :Fredy Tony ICT wa Mbeya Yetu Blog
  • Heri ya siku ya kuzaliwa Askofu Desmond Mpilo Tutu!

    Posted: October 7, 2011, 4:01 am by SIMON KITURURU
    Desmond Mpilo Tutu (Alizaliwa  tarehe  7 October 1931)
    HAPPY BIRTHDAY MKUU!Kivyako umejitahidi aisee!



    Hebu tumsikie tena akiongelea kitu kama kawaida yake,....

    Au tu hebu Rais MUGABE amtusi kidogo ,....

  • Watu huwa na MCHEZO wa kukubaliana na MWIZI wa PIPI kuwa PIPI ni TAMU,...

    Posted: October 6, 2011, 10:50 pm by SIMON KITURURU
    .... na tofauti ipo tu  kwakuwa MWIZI huamua KUIIBA pipi hiyo!:-(
    Swali:
    • Au?
    Ndio,....... labda  kunakufanana kwingi tu  ,...........ndani ya  MBAYA na MZURI pamoja na kuwa  watu hubobea kwenye tofauti ndogo tu  iwezayo kufanya MZURI  na MBAYA kufikiriwa ni WATU tofauti sana!:-(

    Swali:
    • Si unakumbuka KIMWANA mwenye bonge la KALIO kisangara wamo na yule ambaye ana KALIO tepwetepwe si bado wote wawili  ukweli ukopalepale kuwa wana MAKALIO ingawa kimapenzi ya watu  mmoja nundu zake za kukalia au kutikisa katika mwendo hupendwa zaidi?

    Ndio,...
    ..... ukifananisha,...
    .... KILA MTU  kwanza kabisa ana UBINADAMU  hata kama  kuna wasifiwao  ni wazuri kama MALAIKA!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

    Hebu Quincy Jones aingilie kati na kurudisha nyundo -The Secret Garden ... ndio Barry White ,Al B. Sure, James Ingram na El Debarge walitoavokoz kipedejee




    Quincy Jones abadili kidogo kwa - SOUL BOSSA NOVA



    Quincy Jones abadili zaidi kwa - Quintessence


    Quincy Jones amrudishe Tevin Campbell katika-Tomorrow



    Halafu Tevin Campbell amalizie tu kwa -Can We Talk?

  • UTABIRI: Hakutakuwa na U.S.A kama TAIFA ifikapo mwaka 2020 -Prof.Johan Gultang

    Posted: October 6, 2011, 6:02 pm by SIMON KITURURU



    Kama una muda ,..............msikilize Prof.Johan Gultang akitonya KITABIRI,...
    ...kuhusu kuanguka kwa TAIFA KUBWA lijulikanalo kama United States of America




    Kirefu kiduchu,....


    Ndio,...... labda ni MTAZAMO wake tu huu,....................LAKIIIIINIIII!
  • MH. JOHN MNYIKA TAARIFA ZA VITENDO HIVI VINAVYOENDELEA KATIKA SHULE ZA MSINGI JIMBONI KWAKO UNAZO?

    Posted: October 6, 2011, 5:21 pm by SIMON KITURURU
    Mh. John Mnyika Mbunge wa Jimbo la Ubungo Dar es salaam.
    Kuna taarifa saa hizi zimetufikia kupitia kipindi cha Redio ya Clouds FM cha Leo tena, kuhusu shule moja ya Msingi Jimbo la Ubungo.
    Shule ya Msingi Tuliani iliyopo katika Kata ya Kilungule Wilaya ya Kinondoni kuna vitendo vichafu vinaendelea kufanywa na Vijana wahuni wa maeneo hayo vya kuwalawiti wanafunzi wa Shule hiyo ya Tuliani.

    Vitendo hivyo mpaka walimu wanavijua na wanashindwa la kufanya kwa sababu nao Walimu wa kike wanaogopa wanaweza kubakwa. Vitendo hivyo hufanywa na vijana hao katika vyoo vya shule hiyo, kutokana na hali ilivyo mbaya mpaka walimu pia wakienda Chooni ni lazima wasindikizane kwa kuwaogopa Wabakaji hao. Kwa taarifa pia kupitia Leo tena, Polisi wa kituo cha jirani wanalijua hili lakini hawalifanyii kazi.
    KAPINGAZ Blog kwa kutambua utendaji wako wa kazi tunakuomba ulifanyie kazi haraka sana, ili kuweza kuokoa vizazi vyetu visije vikaangamizwa na Wabakaji hawa. Vitendo hivi vimekuwa vikikua kwa kasi sana hasa katika Shule nyingi za Dar es salaam. Tunaomba Serikali kupitia Wizara husika nao walifanyie Kazi haraka sana.


    Nimetumiwa na:Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog
  • R.I.P Steve JOB!

    Posted: October 6, 2011, 9:21 am by SIMON KITURURU



    Kwa wapenda tekinolojia,......mpaka wa waliopata MOYO ,...... kuwa MTU mmoja anaweza kuwa changamoto kwa WENGI,......weye STEVE  ulikuwa bonge la CHANGAMOTO na ni bonge la CHANGAMOTO bado!

    R.I.P Steve!
    Tugewe zaidi kitu ,....... kwa kumkumbuka mwaka 1984 katika:-Steve Jobs demos Apple Macintosh, 1984


    Tujikumbushe kiduchu ya Steve JOBS zaidi,...



    Tumsikilize,...



    Au tu  stori ya kifo chake ishushwe,...



    Ndio,...... labda STEVE JOBS,......ni miongoni mwa WAYU wawaliochangia kuwezesha kuna tuliojuana MTANDAONI!

    Habari zaidi unaweza kukongoli HUKU au hata HUKU
  • Kwa kuwa NGUVU za NYONYO , paja au KALIO labda ni zilezile MILELE,....

    Posted: October 6, 2011, 4:08 am by SIMON KITURURU
    ...... tatizo LABDA bado ni kwamba  yasemekana wenye TITI ,bomba la usafiri KIPAJA, goti ,MAGIMBI   au tu hata TAKO walewale,......... vifaa vyao hivyo vya mpaka  kudakia WAJANJA  KIJANJA hivyohivyo hunywea baada ya MUDA kabla ya milele KIBINADAMU ,...... kwa kuwa eti kuna fununu hivyo NAVYO huwa haviishi milele KIKUNONA KIUNONO kama pale vilipowawezesha WARINGIAO UZURI kimaringo kutembea wakitingisha tako au chuchu bila sidilia KIUZURI  kwa kuwa hao bado ni BINADAMU.:-(

    Swali:
    • SI yasemekana ingawa SANGARA wamo ila nao hao sangara kama perege HUFA ukifuatilia maisha yao hata kama si kimilele?
    • Na si UA  ZURI LA PENDEZA  nasikia  bado lamaisha mafupi hata LABDA hata ki-UA?

    Ndio,....... MILELE kibinadamu LABDA  haiwezekani,...... ndio maana stori za KIBINADAMU zenye MILELE labda kuna  WENYE BUSARA imebidi wasingizie katika  hizo hata kiramli kuhusika mpaka kwa MIUNGU ya kipedejee itoayo mpaka MABENZi ukitoa sadaka!:-(


    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(


    Hebu Angela Ferrao ajaribu KIANGOLA  kulainisha kwa - Wanga


    Perola ajaribu KIANGOLA kuongezea - Omboio



    B.M.F waingilie kati kwa kugusia ukristo kiswanglish kwa KIKENYA katika  - Njoo


    Au tu B.M.F wajaribu kuzima ndude KIKENYA kikanisakanisa bado  kwa-I LIVE FOR YOU



    Halafu PAPA SAN alie tu tena na kuturudisha mtaani huko KARIBIANI kwa - Maddy Maddy Cry

  • LEYMAH GBOWEE-Mwanamke MWAFRIKA wa SHOKA

    Posted: October 6, 2011, 4:05 am by SIMON KITURURU
    Mchungulie,...... na ukihitimisha sio washoka ,.......SASA mimi  .....just fikiria......NIFANYEJE?

    Ndio,...... ingawa SHOKA sio BUNDUKI,...... LABDA kuna mengi yangenitoa BARUTI huyu MMAMA kakomalia!:-(

    NI HILO TU MKUU!
  • HALIHALISI inamchango katika uamuzi ANDUNJE anapigana kwa kutumia MKUKI , gobole au MANENO gani ya matusi katika VITA!

    Posted: October 5, 2011, 7:59 pm by SIMON KITURURU
    Halihalisi  ina MCHANGO WAKE pia,........ na inaweza kuwa ndio iamuayo  WATU wanakula KIMA au NGURUWE.:-(
    Swali:
    • Si ni mpaka KIMA awepo kihalihalisi ndio anaweza kugeuzwa KITOWEO?
    • Si halihalisi labda ndio huchagulia hata kichaa ni chupi ya aina gani atakayovaa kichwani?
    • Halihalisi si ndiyo  hugeuza kwenye mchwa  watu wagundue kumbikumbi wanalika?


    Halihalisi KIBOKO,....... kwa kuwa inaweza kuwa na mchango hata KATIKA aelewavyo KITU mtu ,......... hata kama KIHALIHALISI  hilo ni shule ya mazingira TU  atokayo MTU na sio CHUO kitoacho VYETI  kafunzacho  nyuma ya udhaniwao ni UJINGA kuna cha busara  awezachojifunza mwerevu MTU.:-(
    NI wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(Hebu tu Jimmy Dludlu arudie -Tote


    George Benson arudishe - Breezin'


    Au tu tena Mafikizolo wazime kwa -Nisixotshelani

  • VAZI TATA! KUNANI MWENZETU?

    Posted: October 5, 2011, 7:55 pm by SIMON KITURURU

    Picha ya juu ni Katibu Mkuu Mwenezi wa CCM Nape Mnauye, na picha ya chini wa kushoto ni Mh. Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA.


    Hilo vazi lako Nape linanichanganya, mie sijakupata vizuri. 
    Mbona linafanana na hilo lililovaliwa hapo chini kushoto?Au upo pia na kule nini kwenye vidole?

    Nimetumiwa na:Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog
  • NGUMI kurindima ILALA Oktoba16

    Posted: October 5, 2011, 2:46 pm by SIMON KITURURU

    ZAIDI ya mabondia 42 wanatarajia kushiriki katika mashindano ya mchezo wa ngumi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba16 mwaka huu Dar es Salaam.

    Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha wa Klabu ya Ashanti ya Ilala, Rajabu Mhamila, 'Super D' alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha Klabu 12 kutoka katika maeneo mbalimbali.

    Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala.

    Super D alisema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuendeleza kuhamasisha mchezo wa ngumi nchini ikiwa ni pamoja na muendelezo wa mchezo huo unanaofanywa na Kinyogoli Foundation.

    “Tumeandaa mashindano ya ngumi ambayo yatashirikisha vijana mbalimbali na lengo letu ni kuhamasisha mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuuendeleza ili uweze kutuletea faida hapo baadaye”
    -alisema.

    Kocha huyo alisema kuwa vijana watakaoshiriki watakuwa katika uzito mbalimbali kuanzia Unyoya mpaka uzito wa juu.

    Alisema kuwa pia wanatarajia kushirikisha mabondia wa kike kutoka katika klabu hizo hizo.

    Aliongeza kwa kusema kuwa wanahitaji wadau mbalimbali wajitokeze kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya vijana ikiwemo maji kwa ajili ya mchezo huo kwa siku hiyo wenye nia ya kutaka kusaidia au kushiriki kwa kuchangia chochote wanaweza kuja katika ukumbi wa mazoezi uliopo Amana Ilala au kufika Ashanti Boxing club.

    Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na Kocha Mkongwe;
    Habibu Kinyogoli kwa simu 0655928298  .

    Au unaweza kuwasiliana na ;
    Super D Boxing Coach kwa simu O713,0787-406938 
    Email: superdboxingcoach@gmail.com

    Wadau mbalimbali mnakaribishwa.

    --

    'Super D'

    Photojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania


    --
    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania

    Nimetumiwa na:Superdboxing coach
  • Barua ya Wazi Kwa Dr Kafumu; Ushindi Wako Igunga na Maswali Yasiyojibika

    Posted: October 5, 2011, 1:59 pm by SIMON KITURURU
    Dr Kafumu


    Na Nova Kambota Mwanaharakati,

    Mara kwa mara huwa nasema tatizo kubwa la Tanzania yetu ni kupenda kupindisha ukweli, hii imetufanya kuwa watu tusiopenda kufikiri kiasi kwamba tunalambishwa kila linalokuja “tumekuwa madodoki kila uchafu tunasomba”. Naandika hivi kwa nia ya kujenga si kubomoa, naandika hivi kwa mustakabali wa Demokrasia yetu ambayo nathubutu kusema imetikiswa kupita maelezo huko Igunga na tusipokuwa makini Taifa litadondoka siku za usoni.

    Kwako Dr Kafumu ambaye umetangazwa kuwa mbunge wa Igunga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), naomba unaposhangilia ushindi wako nikiamini wewe ni msomi na mzoefu katika Nyanja za uongozi wa Taifa hili napenda usome maandishi yaliyo ukutani kisha malizia kwa kuunganisha dots za ushindi wako halafu niambie ikiwa ni kweli unaamini kuwa umeshinda kihalali? Au la niambie kile ambacho kinaitwa “changamoto za uchaguzi Igunga” ni nini kama siyo “mizengwe?”Kama mchambuzi nisiyeegemea upande wowote nisingependa kutia mwaa mtiririko huu wa hoja zangu kwa hiyo sitaegemea upande wowote bali nitajadili kwa misingi ya hoja ili ikibidi kujibiwa pia nijibiwe kwa misingi ya hoja vivyo hivyo, nataka kuibua hoja zenye mashiko ili zitufikirishe na kutupa majibu ya kisayansi badala ya kumezwa na mawimbi ya watu wenye mkatiko wa mirija ya fikra ambao wamebaki na ushabiki badala ya hoja kiasi kwamba wanatoa majibu ya zamani kwa maswali mapya. Yafuatayo ni mambo manne ambayo yanatia doa ushindi wa Dr Kafumu;
    Kwanza Tume Ya Uchaguzi; 
    Tume ya uchaguzi ya nchi hii haina sifa nzuri na haiwezi kuwa na sifa nzuri mpaka iwe huru, hata I gunga hali ni hivyohivyo tumesikia malalamiko dhidi ya tume hiyo lakini hasa kwa aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa uchaguzi huo ambaye pia ni mteule wa rais na bila shaka kwa kuunganisha mantiki haina shaka kuwa naye ni mwanachama wa CCM au basi anaipenda kimoyomoyo. Uchaguzi wa Igunga ukipimwa kwa mizania hii ya aina ya tume ya uchaguzi tuliyonayo ni vigumu sana kwa mtu mwenye kufikiri kwa mantiki kuridhia matokeo ya uchaguzi huo.

    Pili Siasa Uchwara;
    Hapa inahitaji moyo mgumu kuyasema lakini kwa vile tangu awali nilishasema kuwa lengo si kufukua makaburi bali kuweka shada la maua juu ya makaburi basi acha niseme hiki ambacho nakiita ni siasa uchwara. Kwanza kabisa jinsi serikali ya CCM ilivyoruhusu kubofywa kwa kile kinachoitwa “kitufe cha udini”, ikumbukwe kuwa hata wakati wa uchaguzi serikali bado ina jukumu la kuilinda katiba na kuhakikisha amani haivurugwi aidha kupitia mirija ya udini wala ukabila, nayasema haya kutokana na baadhi ya viongozi wa dini kuirushia makombora CHADEMA tena wakaenda mbali kwa kutoa wito kwa baadhi ya waumini wa dini Fulani kutompigia kura mgombea wa chamna hiko, lakini cha ajabu hata hiyo hoja ya DC kuvuliwa hijabu imekwama kama gazeti nguli la Mwanahalisi lilivyofunua kuwa Mama Fatuma Kimario uislamu wake una mashaka kutokana na yeye kuwa ni mke halali wa Bw Kimario ambaye ni mkristu wa madhehebu ya Kikatoliki ambapo hata mwanazuoni mashuhuri wa kiislamu nchini Sheikh  Issa Ponda amenukuliwa akisema kuhusu mwanamke au mwanaume wa kiislamu kubadili dini Sheikh Ponda amesema “Hilo ni kosa kubwa sana”.  Lakini cha kusikitisha kuwa wakati haya yote yanatokea CCM walikaa kimya kana kwamba “hawakuliona kosa”, je tukisema kuwa hii ilichangia Wana Igunga kupiga “kura za chuki” dhidi ya CHADEMA tutakuwa tumekosea? Haya ni maswali magumu kuhusu ushindi wa Dr Kafumu.Jambo la pili ambalo linaangukia kwenye siasa uchwara ni pamoja na vitimbi vya rushwa na vitisho vya “kipuuzi” mfano gazeti la Dira linamtaja mwenyekiti wa mtaa wa Nkokoto huko Igunga Bw Abed Motomoto (CCM) kuwa amekutwa akigawa rushwa “live”kwa wanawake wa mtaa wake kwa lengo la kuwashawishi kumpigia kura mgombea wa CCM (Dr Kafumu), lakini kama hili halitoshi kuna hili la Mh Ismail Aden Rage kupanda na bastola ikining’inia kiunoni halafu tunaambiwa kapewa adhabu ya kulipa laki moja, sasa ladda nitumie fursa hii kumuuliza ndugu yangu Aden Rage kuwa alikuwa anamtisha nani na bastola yake? Au nani kamwambia kuwa ni utamaduni wa kitanzania kuonyeshana vyombo vya moto? Haya ni machache kati ya mengi yanayokinzana na maana ya demokrasia pia kupoteza mantiki nzima ya “uchaguzi huru na wa haki”

    Tatu kuchelewesha matokeo;
    Hili ni  tatizo linalotia huzuni sana kiasi kwamba nashawishika kuamini kuwa “bado tuna safari ndefu”, nayasema haya kwasababu kwanza idadi ya watu waliojiandikisha ni tofauti sana kwasababu waliopiga kura ni wachache wanaokadiriwa kuwa elfu sitini (60,000) lakini cha ajabu hata kiasi hiki kichache cha kura kimechukua masaa kibao zaidi ya kumi kuhesabu, hiki kama si kiroja ni nini? Au tuamini kuwa kuna lililojificha nyyuma ya pazia hapa?
    Nne Matumizi Ya Nguvu;
    Nalazimika kuyaandika haya kutokana na tabia inayozidi kukua siku hizi ya polisi kutumia nguvu dhidi ya wananchi , matukio ni mengi lakini hebu tutupie macho kwenye hili sakata la Igunga ambapo nasema kulikuwa na matumizi ya nguvu yasiyo na msingi, mabomu ya machozi ya nini? Watu walitawanywa kwasababu gani? Kwa mamlaka ya nani? Na faida ya nani? Je hii ndiyo demokrasia tunayoitaka? Huu ndiyo tunaouita ushindi halali? Uhalali uko wapi hapa?Baada ya kuona upungufu huu , sasa tuone nini ambacho Dr Kafumu anaweza kufanya ili kuienzi Demokrasia na kuwapa haki yao Wana Igunga;1. Awe wa kwanza kulaani matumizi ya nguvu dhidi ya Wana Igunga2. Awe wa kwanza kuhakikisha Ismail Aden Rage anachukuliwa hatua kali za kimaadili3.Awe wa kwanza kulaani harakati zozote za wanasiasa kuingiza udini kwenye siasa4.Awe wa kwanza kuomba radhi kwa niaba ya chama chake kwa kukaa kimya au kushabikia siasa uchwara.5 Awe wa kwanza ndani ya CCM na Tanzania kukataa ushindi huo na kuitaka Tume kuitisha tena uchaguzi wa jimbo dogo la Igunga , hili lifanywe pasipo kuangalia gharama za zoezi hilo, bali lifanywe ili kuuonyesha Ulimwengu kuwa Dr Kafumu na CCM wameamua kusiamamia misingi ya Demokrasia pasipo kujali gharama za hatua hiyo.Haya ni mambo ya msingi kwa Dr Kafumu kuyasoma na kuyafanyia kazi, hii itamjengea heshima sio tu ndani ya CCM bali kwa watanzania wote na Ulimwengu mzima. 
    Tafakari! A luta Continua!  Nova Kambota Mwanaharakati,+255717 709618novakambota@gmail.comwww.novakambota.comWesneday, 5october,2011Tanzania, East Africa.
    Nimetumiwa na :Nova Kambota.
  • MDADA wa KIKONGO anikunaye kisauti sasa hivi ni :JOSEY PRISCILLE

    Posted: October 5, 2011, 1:24 pm by SIMON KITURURU
    Msikilize akichokoza kidogo,...


  • MISH akamua ndani ya SPORAH SHOW

    Posted: October 5, 2011, 10:55 am by SIMON KITURURU
    Salam

    Msanii wa Urban Pulse Creative Mish Ze Fyah Sis akifanya makamuzi ndani ya Sporah Show

    Asanteni
    Urban Pulse Creative
    http://www.youtube.com/watch?v=-ZolaNe7mTM



    Nimetumiwa na :Frank Eyembe wa URBAN PULSE CREATIVE
  • London Model Network Video

    Posted: October 5, 2011, 10:47 am by SIMON KITURURU
    Greetings,

    Robert De Niro (Enclosure Catwalk Show) - Presentation by London Model - Backstage London Model Network

    londonmodelnetwork.co.uk. 

    Fantastic show all the Paparazzi doing a wonderful job and Robert De Niro with all has Enclosure guests arrived at Aura Mayfair In London on friday 30th September 2011.

    Thanks,
    This is An Urban Pulse Production in Association with Jestina Blog
    http://vimeo.com/30051232

    London Model Network from Urban Pulse CreaTV on Vimeo.

    Nimetumiwa na :Frank Eyembe wa URBUN PULSE CREATIVE
  • Kama hupendi KUZEEKA-``HONGERA za SIKU YA KUZALIWA labda ni MATUSI aisee!´´

    Posted: October 5, 2011, 4:02 am by SIMON KITURURU



    Swali la KIZUSHI:
    • Kwani  MTU huwa anapongezwa nini katika BIRTHDAY ukizingatia labda hana mchango wowote katika kufanya awepo hapa DUNIANI katika siku hiyo hasa kama unaamini katika MAPENZI ya MUNGU mwanadamu hawezi kuingilia?
    • Na je ni kwanini kuna BINADAMU hufikiria MUNGU muwezesha yote NDIYE ahitajiye KUSHUKURIWA  kwa kuachia limtu likue wakati MAPENZI yake labda ndio yaondoayo wengine MAPEMA  kisababu zake?
    • Hudhani pongezi nyingi za watu katika siku ya kuzaliwa MTU labda ni kukosa chakusema?

    Ndio,...
    ... labda si kwa kila MTU ni furaha MIAKA kuongezeka,....... hasa kwa kuwa MIAKA kuongezeka ndio siri ya UZEE,......ambao sio kila mtu yuko huru nao KIHIVYO.
    Swali  zaidi kizushi:
    • Kwani wewe unapenda KUZEEKA?
    • Si nasikia kuzeeka kwa mpenda UZINZI huja na MZINZI kushindwa kuendelea kujinoma KIZINZI kirahisi?
    • Na si kuna waaminio MIAKA izidivyo mvuto wa MREMBO hunywea na sio kwa titi tu kulala?

    Ndio,...... umri huja na faida zake KIBUSARA,......... lakini  bado kuna walalamikao kwa kuwa UMRI huja na meno kung'oka kitu kifanyacho ni WAZEE wengi ndio VIBOGOYO  kitu kifanyacho mpenda KITIMOTO kushindwa kugida nyama UMRI ukienda!:-(

    Na ni wazo tu hili la kizushi MHESHIMIWA!
    Jumatano njema MKUU!

    Hebu turudi KENYA ili Gidi Gidi Maji Maji warudie - Unbwogable


    ...DJ ariwaindi and come back again,...


     Gidi Gidi Maji MAJI na Wikimosh waongezee dozi kwa - Atoti


    Halafu tena Eric WAINAINA amalizie na-Nchi Ya Kitu Kidogo

  • KITENDO TULICHOKILAANI KUTENDEWA MKUU WA WILAYA IGUNGA CHAJIRUDIA TENA, NANI WA KULAUMIWA?

    Posted: October 4, 2011, 8:45 pm by SIMON KITURURU
    Mwanamke mmoja jana aliyesadikiwa ni mwanachama wa CHADEMA alibebwa mzobe mzobe na Askari wa kutuliza ghasia Igunga baada ya kutokea mtafaaruku kati ya wanachama wa CHADEMA na Polisi muda mfupi kabla ya kutangazwa matokeo ya mshindi wa kiti cha Ubunge igunga.
    Napenda wadau tuliangalie hili, hasa taasisi zote za kijamii na kiserikali, hivi majuzi Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mama Fatuma Kimario alidhalilishwa kwa kuvutwa na kuvuliwa kilemba na wafuasi wa chadema, kitendo ambacho kililaaniwa na taasisi zote za kijinsia, kijamii na kiserikali. Leo hii linatokea tena tukio kama lile, la mama huyu kuzalilishwa kijinsia kwa kushikwa mwili wake bila ridhaa yake, naziomba taasisi zinazohusika na haki zitueleze je huyu mama hii ni haki yake kutendewa kitendo kama hiki au kwa sababu ni kutoka chama cha upinzania au kwa sababu ni mwanamke asie na madaraka yoyote? La hasha! nadhani hapo hiyo siyo haki.
    Naamini jeshi la polisi linao askari wa kike, kwa nini hawa wasitumike kuwakamata waandamanaji wa jinsia yao! mpaka askari wa kiume anadiriki kumbeba huyo mama! Je angekuwa ni mama yake angeweza kumbeba hivyo?
    Mi kwa mtazamo wangu nadhani kuna haja ya kuundwa taasisi maalum kwa ajili ya kuwapa elimu ya jinsia hawa askari wetu nadhani itaweza kusaidia udhalilishaji huu usiwe unajitokeza.
    KAPINGAZ Blog haifungamani na chama chochote cha kisiasa, Tungependa kuwasikia TAMWA, TGNP na Taasisi nyingine za kijinsia  mkikemea na kuvilaani vitendo hivi.  Tulitegemea kitendo kile kilichotokea kwa Mkuu wa Wilaya kinaweza kikawa funzo pia kwa askari wetu lakini tunaona bado kinarudiwa tena.


    Nimetumiwa na :Henry Kapinga wa KAPINGAZ blog
  • Karibu KONA YA MANGOMA "It's all about East African Flava"

    Posted: October 4, 2011, 8:21 pm by SIMON KITURURU




    Habari zenu wadau wote...

    Tunapenda kuchukua nafasi hii ya kipekee kabisa kuwakaribisha katika Libeneke jipya kabisa la KONA YA MANGOMA .

    Ambapo mtapata kutazama video mpya na nyenginezo nyingi kutoka pande zote Afrika Mashariki yani Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

    Pia tunaomba wasanii wote ambao mnatoa Video mtutumie link kupitia barua pepe hii (konayamangoma@live.com) ili tuweze wape sapoti ya juu.

    Kwa pamoja tunaendeleza Muziki wa Afrika.

    Tunatanguliza Shukrani zetu za dhati kwenu!

     Ukiona link hii mpe na mwenzako.Jina la Blog: Kona ya Mangoma Link:  www.konayamangoma.blogspot.com




    Nimetumiwa na :Dj Kali Flava wa KONA YA MANGOMA
  • KIMISHENI TAUNI kuna WAJANJA huishi MJINI!

    Posted: October 4, 2011, 12:28 pm by SIMON KITURURU
    Tatizo,....... yasemekana KIMISHENI TAUNI ,....... mafanikio yake ni ya MUDA hasa kwa kuwa MISHENI tauni hazina MISINGI YA UHAKIKA ijengayo alivyofanikiwa jana kuingiza watu MJINI ataendelea kwa staili hiyohiyo ya kuingiza mjini washamba kwa kuwa hata mshamba aliingizwa mjini hakawii kustuka kitu kiuacho ofisi MJINI.:-(

    Swali:
    • Na sinasikia kuna wadaio mpaka serikali ya Tanzania moja ya kiikwamishacho ni kufanya kazi KIMISHENI TOWN ambapo wajanja hula kimisheni tauni /KIJANJA?


    MISHENI tauni KIBOKO katika kufanikishia wajanja yale ya CHAPUCHAPU,....... lakini  labda  kwa kuwa CHAPUCHAPU labda sio TUISHIVYO,....... mjanja anaweza akajikuta KIMISHENI TAUNI kakwama baada ya muda!:-(

    Ni wazo tu hili MKUU!




    Hebu ghafla tena  Dj Sottão aturudishe tena ANGOLA na kuanzisha upya kwa pini- Sentir Moça



    Noite e Dia waingilie kati kwa - Bondenda

    Au tu Noite e Dia waongezee tu dozi ..(Sasa tutafanyaje?) ..kwa -Tá maluca



    NIMEACHA!:-(
  • Eddy Sheggy na akiimba Shakaza

    Posted: October 4, 2011, 12:25 pm by SIMON KITURURU
    Unakumbuka wimbo wa Shakaza?Hebu jikumbushe HAPA
    --
    www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.com
    www.johnkitime.blogspot.com




    Nimepigiwa krosi na:John KITIME.
  • Yajadiliwayo kuhusu NDOA huko MEXICO!

    Posted: October 4, 2011, 11:55 am by SIMON KITURURU
    Deku kitu katika,......Temporary Marriages Coming To Mexico


  • Utalipia zaidi kodi DENMARK kama UNATAKAKUNENEPA kwa FINYANGO zenye MAFUTA!

    Posted: October 4, 2011, 11:50 am by SIMON KITURURU
    Deku  mtonyo uhathirio hata wapendao BREKIFASTI fulani mfukoni katika ,.......Denmark introduces fat tax


    Matatizo ya wengine BWANA,....... ukiwa SOAMLIA sasa hivi huwezi kabisa KUYAELEWA!:-(
  • Katika majaribio ya KUCHUNGA wengine WANAVYOFIKIRIA,...

    Posted: October 4, 2011, 9:54 am by SIMON KITURURU
    ... kuna WATISHAO mtu!
    Swali:
    • Si unakumbuka LAANA kwaasilimia kubwa ni  VITISHO vya ajaribuye KUCHUNGA  mtu hata KIFIKIRA kama tu woga wa KUKUFURU utishiavyo watu?

    TATIZO TU ni kwamba,...
    .... hata MTU atishweje,....... afikiriacho ni vigumu KUKIKONTROO hata kama JAMII  ya VITISHO hugeuza MENGI yafikiriwayo  kugeuka SIRI.:-(Swali:
    • SI mengi UFIKIRIAYo labda moja ya sababu ni SIRI  ni kwa kuwa unaogopa kitu hata kama hicho kitu ni KUDHALILIKA machoni mwa jamii iliyojaa WANAFIKI?

    Ndio,...
    .... na kwa kuwa wengi WANACHUNGIKA kwa vitisho katika jamii yetu,........ ndio maana labda wenye MAJIBU ya MATATIZO yetu wako KIMYA hasa kama KIJIBU  suluhisho lapingana na JAMII iruhusuvyo KUFIKIRIA hadharani kitu kifanyacho hata ambako kuna PANYA  tujuao CHINA wanalika tu au KONOKONO ambao UFARANSA ni bonge la maakuli   kuna wafao na njaa kisa  hayo MAAKULI   hata kuyafikiria KIMAAKULI  ni mwiko katika fulanifulani JAMII!:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA !
    Hebu tu turudi Angola ili Yuri da Cunha arudie kibao - Kuma Kwa kié


    Yuri da Cunha aongezeedozi kwa - Homem é bom


    Au tu PATRICIA FARIA aingilie kati kwa - FOFOCA JOAQUINA


    Nicol Ananaz aingizie - Bomba


    Halafu  tumalize tu mkuno hapahapa Luanda Angola kwa Dj Sottão katika ndude- Moço Direito

  • London Model Network Yafana!!

    Posted: October 3, 2011, 12:05 am by SIMON KITURURU
    Salam


    URBAN PULSE CREATIVE na MISS JESTINA BLOG wanakuletea picha za London Model Network show iliyofanyika jijini London ijumaa tarehe 30 septemba 2011 ndani Ukumbi wa  AURA uliopo MAYFAIR  ikiwashirikisha warembo kutoka pande zote za Dunia, Make up Artist, Stylist, na Designers.
    Mojawapo Wageni Rasmi walikuwa ni Celebrities Superstar Robert DeNiro na Rebbeca Black.
    Show Hii iliandaliwa na SEE LI
    Asanteni,
    URBAN PULSE Wakishirikiana Na Miss JESTINA BLOG
    Wadau wakibadillishana mawazo kabla ya show

    Baada ya Show ilikuwa full Kujiachia

    Cat walk

    Cat walking ikiendelea

    Frank akila Pozi Na Robert DeNiro

    Live Perfomance

    Maonyesho ya Mavazi yakiendelea

    Model Akiwa mzigoni

    Model Kutoka Ethiopia katika miondoko ya Cat walk

    Model, Stylist Na Make up artist wakila pozi baada ya show

    Photo Shoot

    Photo shoot zikiendelea na model

    Sanamu Zinazotembea

    Tina (Katikati)Akiwa na SEE LI kutoka kushoto na Mdau



    Nimetumiwa na :Frank Eyembe wa URBAN PULSE CREATIVE
  • Video ya Joseph Mbilinyi aka MR2

    Posted: October 3, 2011, 10:44 pm by SIMON KITURURU
    Unamkumbuka MR2 ,...
    .....hebu angalia video yake ya mwaka 1996
    BONYA HAPA 


    -- www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.comwww.johnkitime.blogspot.com
    Nimepigiwa krosi hii na:John Kitime.
  • Umeme wa JUA : HEBU tucheki SPAIN

    Posted: October 3, 2011, 10:06 pm by SIMON KITURURU
    Umeme wa JUA : HEBU tucheki SPAIN
  • YA IGUNGA: CCM moja CHADEMA na vimburukutu vingine BILA!

    Posted: October 3, 2011, 4:40 am by SIMON KITURURU
    Tetesi ni kwamba mpaka saa hizi CCM imeshinda MCHEZO  Igunga !

    HONGERA zenu CCM! 
    Hongera Dr. Kafumu!

    Hongera na wote wengine wa VYAMA VYOTE VINGINE  mlioSHIRIKI katika KINYANG'ANYIRO!
    Habari itaendelea kiaina  KESHO,...... data zote zikiwa uchi!!

    UPDATE:

    CCM KURA 26,484 sawa na 47%

    CHADEMA 23,260 sawa na 41%

    CUF 2,104 sawa na 4%

    AFP 282 sawa na 0.5%

    CHAUSTA 182 sawa na 0.3%

    SAU 83 sawa na 0.1%

    DP 76 sawa na 0.1%

    UPDP 63 sawa na 0.0%

    Waliojiandikisha ni 171019

     Kura kwa ujumla  56072 sawa na asilimia 33%


    Matokeo katika kila kata:

    Mboto CCM 730- CHADEMA 302
    Nguvu moja CCM 694 CHADEMA 284
    Nkinga CCM1479. CHADEMA 1085
    Itumba CCM1079 CHADEMA 590
    Nanga. CCM 897. CHADEMA 645
    Igurubi CCM 925 CHADEMA 592
    Mwisi CCM 926. CHADEMA 992
    Mbutu. CCM 1186. CHADEMA 1426
    Kinungu. CCM 505 CHADEMA 268
    Ngulu CCM 622 CHADEMA 412
    Igunga CCM 3181 CHADEMA 3358
    Choma CCM 1227 CHADEMA 918
    Kining. CCM 700 CHADEMA 451
    Mwashiku. CCM 798 CHADEMA 484
    Nsimbo CCM 738 CHADEMA 1016
    Itunduru CCM 738 CHADEMA 784
    Mwamashimba CCM 1224 CHADEMA 1421
    Mbutu CCM 1335 CHADEMA 1427
    Bukoko CCM 1136 Chadema 931
    Nyandekwa CCM 691 Chadema 631
    Ndembezi CCM 866 Chadema 806
    Chabutwa CCM 545 Chadema 581
    Ziba CCM 1053 Chadema 860
    Igoweko CCM 1051 Chadema 880
    Sungwizi CCM 1225 Chadema 718
    Isakamaliwa CCM 525 Chadema 593

    Source:  Tume ya TAIFA ya UCHAGUZI.
  • Kwa kuwa PAKA anapenda PANYA!:-(

    Posted: October 3, 2011, 4:04 am by SIMON KITURURU
    Ndio,...... lakini sababu za PAKA kumpenda PANYA,....... zaweza kuwa ndio vigezo vya PANYA kufikiria  PAKA anatabia MBAYA kiadui!:-(

    Swali:
    • AU?
    • Si hata kwa WATU kupenda NYAMA YA KUKU inamaana KUKU auawe?

    Ndio,........ sababu za kwanini  ZUBEDA anafaa kwa  kuendekezwa lake TITI lililosimama,........ labda hiyo ni siri ya TITI kutoendekeza wampendao ZUBEDA kwa kuwa  hilo ndio liadhibiwalo kikunyonya na kufanya ZUBEDA asivutie likilala!:-(
    Ni wazo tu hili lililopinda kiduuuchu  MHESHIMIWA!:-(
    Hebu Gladys Knight na The Pips warudishe -Friendship Train

    STEVIE Wonder arudishe-Uptight



    Au tu Stevie Wonder azime tu tena mtonesho kwa  - Master Blaster
  • MSAGAJI yasemekana hastukiwi kirahisi kama astukiwavyo MSENGE!

    Posted: October 3, 2011, 4:02 am by SIMON KITURURU
    Ndio,....... sifa ya upendo kwa WANAWAKE ,...... labda yaficha MENGI!:-(

    Swali:
    • AU?
    • Si  msichana kumshika tako  msichana hadharani haistui sana kama DUME likishikwa tako na DUME?
    Na labda BASHA hastukiwi KISENGE,....... katika michezo ishirikishwayo WASENGE kiulazima.:-(

    Ndio,...... hili ni swala rafiki yangu kanitonya leo kwa kuwa KIPENDA ROHO  chake,...... kumbe kinapenda WANAWAKE wenziye hata KINANILII na katika hilo KIDUME hana pakuanzia VITA!

    Ni hilo tu MKUU kimtonyo!
    Tujaribu kubadili kwa kuchungulia NIGERIA,.......katika-Nigeria's brain gain


    Au tu SALIF KEITA abadili kwa- Tekere

  • Muone Marijani Rajabu akiwa jukwaani 'live'

    Posted: October 2, 2011, 11:58 pm by SIMON KITURURU
    Wengi wamekuwa wakimsikia tu Marijani Rajabu ,......angalia katika video hii akiwa jukwaani akiimba na kupiga gitaa  kwa kuingia HAPA:
    http://wanamuzikiwatanzania.blogspot.com/2011/10/muone-marijan-rajabu-katika-onyesho.html--
    www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.com
    www.johnkitime.blogspot.com

    Nimepigiwa krosi na:John KITIME
  • MIKANDA YA MCHEZO wa NGUMI ZA KULIPWA TPBO yabakia Mkoa wa TANGA

    Posted: October 2, 2011, 11:05 pm by SIMON KITURURU



    Bondia Said Mundi wa Tanga  akimwadhibu bondia Mohamedi Bakari wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa uzito wa kilo.52 uliofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga jumamosi iliyopita, Mundi alishinda kwa T.K.O raundi ya pili na kuwa bingwa wa ngumi za kulipwa TPBO.


    Bondia Said Mundi wa Tanga akinyoshwa mkono juu baada ya kumtwanga Mohamedi Bakari wakati wa mchezo wa kugombania mkanda wa ubingwa wa taifa wa chama cha ngumi za kulipwa TPBO viwanja vya Tangamano TANGA.




    Bondia Alan Kamote  wa Tanga akinyoshwa mkono juu na Refarii Yasina Abdalah baada ya kumshinda Yohana Robert wa Dar kwa pointi na kutangazwa kuwa bingwa wa kg.60 wa chama cha mchezo wa ngumi za kulipwa TPBO katika pambano lililochezwa viwanja vya Tangamano mjini Tanga mwishoni mwa wiki.







     Bondia Haji Juma wa Tanga akinyoshwa mkono juu na Refarii Yasina Abdalah baada ya kumtwanga bondia  Juma Selemani na kutoa ubingwa wa ngumi za kulipwa TPBO katika viwanja vya Tangamano mkoa wa Tanga

    (Picha na HABARI  www.superdboxingcoach,blogspot.com)
    --
    Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania

    Nimetumiwa na :RAJABU MHAMILA( SUPER D)
  • JAPHET KASEBA awa bingwa wa NGUMI ZA KULIPWA NCHINI.

    Posted: October 2, 2011, 11:00 pm by SIMON KITURURU

    Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Iddy Azani akimvisha mkanda wa ubingwa unaotambuliwa na chama cha mchezo wa ngumi za kulipwa PST bondia Japhet Kaseba baada ya kumtwanga Maneno Oswald kwa Point  jijini Dar es salaam jana.


    Mabondia Japhert Kaseba (kushoto) akipambana na Maneno Oswald wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa PST uliofanyika Dar es salaam jana Kaseba alishinda kwa pointi..





    (Picha na HABARI  kutoka  www.superdboxingcoach.blogspot.com)-- Super D Boxing CoachPhotojournalist at Majira, Business TimesEmail.superdboxingcoach@gmail.comwww.burudan.blogspot.comMob;+255787 406930        +255774406938         Po.Box. 15493Dar es Salaam Tanzania


    Nimetumiwa na :RAJABU MHAMILA (SUPER D)
  • SIKIO likizidi KICHWA kinaniliii!

    Posted: October 2, 2011, 6:00 pm by SIMON KITURURU
    Asikilizaye,...... yasikilizwayo bila MCHUJO,...... huweza kuwa ndio siri ya KHADIJA kwa chini ana kipele KUAMINIKA kisa yamesikiwa tu,...
    ...hata kama KIUSHAHIDI hayana KICHWA wala migugu!:-(Swali:
    • Si sikio labda HALIZIDI kichwa?
    • Si umestukia KANISANI kama MSIKITINI ni fulu tumio la SIKIO?

    Ndio,..... SIKILIZA,........ lakini!:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
    Hebu MANGWAIR aanzishe kufunua chupi mpya kwa - MSELA MSELA



    Nuru achezee afikiriayo ni ya-MSELA



    Toniks ,Amani , CJ , Nuru ,Juliana Kanyomozi na nguli KIDUM wadinye ia kidude - Haturudi Nyuma



    Au tu hebu Majek Fashek aihamishie pembeni kule NIGERIA na - Promised Land





    Majek Fashek aongezee tena dozi kwa - So long


    Au tu Majek Fashek azime manyanga kwa - I'm Not Tired


    Halafu M.O.G na Mr SEED wafunge kabisaaa ukurasa kwa- PAPA GOD OOH!

  • Kama UNACHEZEA nanihino,...

    Posted: October 2, 2011, 4:00 pm by SIMON KITURURU
    ...... basi  LABDA kuna kizidicho kwenye YAKO katika hilo kisiriasi,...
    ....na LABDA ndio maana NDUDE HIYO uichezeayo ,...
    ....imegeuka MCHEZO!:-(Swali:
    • Si unajua KICHEZEWACHO  chochote kile  labda kimetengenezwa au chahitajiwa katika isiyo MICHEZO?

    Ndio,...... kama  unachezea KIMAISHA  hata mboo au kipenyo KIKIPENGELE ,....... labda huna haja sana ya MIMBA au KUMTUNGISHA MJUSI MIMBA hata kama  HATA KIHIVYO hiyo  kimuonekano MUHIMU ni MDOLI kimdoli!:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


    Hebu urudi MADAGASCAR ili Rasoa aweke  ustaarabu tena kwa - Tramaraindry


    Maikoro Manan DAza adinye -AMBONY AMBANY



    Huyuhuyu MAMADA atekenye -Toujours Choc


    Au tu turudi BONGO ili Tanzanight wapindishe kwa-KAFARA



    Orijino ComedI kivideo warimiksi ile  Mbagala ki - KAFARA


    Sasa tufanyeje?
    Hebu DIAMOND mwenyewe ahamishe kwa-Kamwambie


    Bado,...
    ...nipo aisee!:-(















  • IGUNGA OYEEE!

    Posted: October 2, 2011, 1:30 pm by SIMON KITURURU
    Nawatakieni wote wapiga KURA Igunga,....... kila la kheri  na pigeni KURA ki KHERI wajameni!


    Tutajua baadaye nani MSHINDI,........ na MSHINDI wa  kikweli ,........HONGERA!
    Au hebu tuhamishe wazo kwa kumsikiliza DENISE BELFON katika - Saucy Baby


    GhettoFlex aingilie ndude ya Denise Belfon katika-Wine Bend Over

    Jack Radics ajaribu kuzima  kwa - No matter


    Jack Radics aungane na CHAKA DEMUS na PLIERS wote waongelee yatokeayo kitandani  kwa -TWIST and SHOUT


    Au tu Jack Radics azime kabisaaa kwa -This Time I'll Be Sweeter

  • Katika KUTESTI ZALI kwa ALAMBAYE nanihii!

    Posted: October 2, 2011, 4:02 am by SIMON KITURURU
    Katika kutesti DHARI,...... kuna MPAKA waingizao mguu kwenye maji ya MOTO,....... ili kucheki tu kama ni kweli YANAUNGUZA au LA,...
    .....kama tu kwenye simulizi!:-(


    Swali:
    • Si yaaminika  ALIYEOGA labda  bado ni MCHAFU na ndio maana kwa wasafi hawatakuwa kimbelembele kumlamba kila eneo hata KIKUTESTI dhari?
    • Ushawahi KUTESTI zali?
    Na katika kutesti DHARI,...... labda kuna MPAKA ambao hupata ushahidi BASHA ni MSENGE,........hata kama kwenye KITU jamaa alikuwa anatesti tu ZALI  kuwa BATA ni mtamu  au analadha tu kama ya MCHICHA.:-(


    Ni  wazo tu hili MHESHIMIWA hata kama lina KIBIONGO!:-(
    Duh!:-(
    Hebu Gregory Isaacs aamshe MTU kwa-GOOD MORNING




    D'Angelo aanzishe kupindisha vita upya kwa - Everybody Loves The Sunshine


    D'angelo atoe SIRI kuwa kuna watiao ambao wana- Feel Like Makin' Love


    D'Angelo na Lauryn Hill waongezee -Nothing Even Matters


    Au tu sijui kwanini  Gregory Isaacs arudishe  tu kitu halafu azime tena  kwa-GOOD MORNING

  • Kwa kuwa MUDA TULIONAO UNAPITA,....

    Posted: October 1, 2011, 7:21 pm by SIMON KITURURU
    ..... mengi YA LEO yatakujakuwa tu ni NUKTA  katika stori  NZIMA ya ulimwengu,.......NDIO MAANA labda hata MKE wa MKWAWA hakumbukwi jina.:-(
    Ndio,...
    ... ni MIAKA MAELFU imepita na katika hiyo ni MAELFU yamepita,...
    ...... na ukizingatia  kuna wengi   zaidi ya BABU na BIBI  ZAO hawajui ndugu zao waliopita ni akina nani na walifanya nini  hata katika kuchangia  ugunduzi wa MSHALE au  jiko la  MAFIGA ,...
    ....ndio ni MIAKA MAELFU yamepita katika uwepo wa BINADAMU hapa DUNIANI  hata kama uwakumbukao ni WATU WAWILI  na MAMBO SITA tu.:-(

    Swali:
    SI unajua labda ni KWELI binadamu ni fulu KUSAHAU kirahisi tu?

    Ndio,.......MENGI  hata udhaniayo  ni MUHIMU SANA KWAKO labda yako kimkao wa MPITO,...... na katika MPITO HUO  kwa wengi hata wakati huohuo unadhania hayo ni MUHIMU ,......wengine wanayaona hayo HAYANAMPANGO kama tu  mpenda KITIMOTO  athaminivyo MCHICHA  wakati  kwake kilipacho ni nyama ya nguruwe!:-(

    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

    Hebu turudi BRAZIL ili Milton Nascimento aanzishe kwa-Francisco


    Hapahapa Brazil Gilberto Gil na Milton Nascimento waongezee dozi kwa-Andar com Fé



    Kabla hatujaondoka Brazil Seu Jorge amwage- Te Queria


    Seu Jorge aongezee dozi kwa - Mania de Peitão

    Au tu Seu Jorge azime tena madungurudu kwa-Carolina

  • Adolf Hitler; Ukweli Uliofichika…..(1)

    Posted: October 1, 2011, 7:02 pm by SIMON KITURURU


    Na Nova Kambota (Mwanaharakati),


    Nimekuwa nikifanya utafiti kuhusu maisha ya Adolf Hitler kupitia
    maandiko mbalimbali  na niseme wazi katika dunia ya leo  “mwendawazimu
    mkubwa”  ni mtu anayepingana na fikra za kimagharibi ndiyo kwa wasomi
    wetu wa sasa wenye mtazamo wa kizungu ni vigumu kuyaona mambo katika
    uhalisia wake bali katika mtazamo wa kiulayaulaya na Marekani.
    Maandiko na mtiririko wa mantiki unabainisha kuwa fikra za anayeitwa
    dikteta Adolf Hitler zingalipo mpaka leo hii tena zinaongoza sio tu
    Ujerumani bali Ulaya na Marekani, pengine kuna watu watapinga hili ,
    ila sina hofu, najua kwanini watanipinga? “hawasomi” na “hawapendi
    kusoma” na zaidi wamefumbwa wasione vinavyoonekana, naam! Naandika
    kuibua mjadala, naandika kunyoosha palipopinda, naandika ili tujifunze
    kufikiri.


    Kama unadhani fikra za Adolf Hitler zimekufa au wazungu hawapendi
    mawazo yake nasema basi hesabu “Maumivu” narudia tena hesabu maumivu,
    kabla hujaendelea kubisha hebu tafuta kitabu cha Adolf Hitler
    kinachokwenda kwa jina la “Mein Krampf” kilichopigwa chapa mnamo mwaka
    1925. Mwenyewe Adolf Hitler alikiandika kitabu hiko akiwa gerezani
    mnamo mwaka 1923, inaelezwa kuwa kitabu hiko ndiyo ulikuwa mwongozo wa
    utawala wake baadae kuanzia mwaka 1933 mpaka 1945.


    Baada ya vita kuu ya pili ya dunia mnamo mwaka 1945 pengine kwa
    kukusudia au kwa hulka yao ya kuficha ukweli wazungu na wamarekani
    wamefanikiwa kuficha ukweli kwa zaidi ya miongo mitano kuwa “fikra za
    Adolf Hitler ndiyo mwongozo wa mataifa hayo ya kibeberu” na vyovyote
    itakavyokuwa ukweli utabaki hivyo kuwa Mein Krampf(My Struggle) au kwa
    Kiswahili kinaitwa “Mapambano Yangu” ndiyo mwongozo wa Ulaya na
    Marekani kwa maana nyingine tunaweza kunyumbulisha mantiki kwa
    kuhitimisha kuwa “Mawazo ya Hitler yanaitesa Afrika mpaka leo”.


    Ukipitia kitabu hiko utakutana na kauli hii “Those who want to live,
    let them fight, and those who do not want to fight in this world of
    eternal struggle do not deserve to live.Adolf Hitler
    Mein Kampf”  kwa tafsiri nyepesi ya Kiswahili Adolf Hitler hapa
    anamaanisha wanaohitaji kuishi hawana budi kupambana, na wale
    wasiotaka kupambana basi hawastahili kuishi Dunia hapa.  Naam! Haya
    ndiyo mawazo ya kiongozi wa Manazi Adolf Hitler , sasa je hebu tuone
    undani wa kauli hii na je nani anaitekeleza kwa vitendo? Na kwa mapana
    yapi?


    Mpaka leo hii hakuna ubishi Ulaya na Marekani wako katika mapambano ya
    kufa na kupona kuhakikisha ubeberu wao unazidi kuimarika na zaidi ya
    yote mirija yao ya kunyonyea inazidi kufyonza maliasili za Afrika .
    Mapambano ya wazungu ni kuhakikisha kuwa Afrika inaendelea kuwa
    masikini, haya ndiyo mawazo ya Adolf Hitler ambayo yanakumbatiwa na
    mabeberu wa Ulaya na Marekani, wasiyapende vipi wakati yanawasaidia?
    Sasa kwanini wadanganye dunia kuwa hawampendi Hitler? Waswahili
    wanasema “ukipenda boga sharti upende na ua lake”, Je iwapo ni kweli
    Hitler ni mbaya kwanini wakumbatie na kuzisujudu fikra zake?  Kuna
    nini hapa?

    Naam! Hii ndiyo kwanza sehemu ya kwanza ya mfululizo wa makala hii ya
    kusisimua , jiandae kusoma sehemu ya pili itakayoeleza kwa undani
    uhusiano kati ya mawazo ya Adolf Hitler na ubabe wa mataifa ya Ulaya
    na Marekani. Asante kwa kusoma!




    Nova Kambota Mwanaharakati,+255717 709618novakambota@gmail.comwww.novakambota.comTanzania, East Africa
    Saturday, October1, 2011.
    Nimetumiwa na:...Nova Kambota
  • Dakika ni SAA akihusishwa MPENZI !

    Posted: October 1, 2011, 6:29 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,....... labda DAKIKA ni SAA,....... kama unangojea  MPENZI,......au tu  kama unaharaka.:-(
    Swali:
    • AU?
    Ila DAKIKA ni MWAKA pia,...
    .... kama uko kwenye KIBANO na nia ni kukikimbia KIBANO,...... hata kama KIBANO hicho ni MPENZI!:-(
    Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
    Hebu tugewe na BANDA CALYPSO ndude- MEU ENCANTO


    Madonna arudie- La Isla Bonita


    Halafu sijui kwanini Peter Tosh abadili mchezo tena kwa - Why Must I Cry
  • Leo ni siku ya WAZEE!

    Posted: October 1, 2011, 11:18 am by SIMON KITURURU

    Hongera na HESHIMA zenu WAZEE!Nawatakia MAISHA MAZEFU,...... yasiyo na dozi kubwa KIKUKEREKA!!

    Habari ndio HIYO!Uchokozi:
    • Wazee wa JUMUIYA  ya AFRIKA MASHARIKI mshalipwa?
  • Kama WEWE ni KIJANA,....

    Posted: October 1, 2011, 4:06 am by SIMON KITURURU
    ... kumbuka tu VIKONGWE uwajuao waliwahi kuwa ,.......Ze TOTOZ!

    Swali:
    • SI umestukia ni rahisi kujisahau EEEH?

    Ndio,........ ZE-TOTOZ,...... zitazeeka tu MUDA ukila MUDA!:-(


    Tunakumbushana tu MKUU!Jumamosi NJEMA!
    Hebu tuanzie tena TANZANIA ili Anastazia Mukabwa na Rose Muhando wadai - Kiatu Kivue



    Tukatizie ITALY ili AlBorosie aongelee - Kingston Town


    Au tu General LEVY aongezee tu uzito kwa- Incredible



    Au azime tu kwa -HEAT


Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs