SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • JAMBO LISILOKUHUSU likikutia NYEGE!:-(

    Posted: August 29, 2010, 7:25 pm by SIMON KITURURU

    Ndio ,.........mara nyingi kimtiacho nyege mtu ni ambacho sio chake,...


    .......na INGAWA hata kama KINUNIA SHUGHULI  kina upele wenye usaha,...



    ....LABDA mwenye nyege KINUNACHO na KIKENUACHO  kikitekenywa  HATA KABLA YA SHUGHULI bado katika kupandisha JAZBA ya  hamu ya utamu  ya MHESHIMIWA KINUKA MKOJO ,....

    ....hicho KIDUDE  hata kama hakita kata makali  baada ya kuonja AU KUONJWA labda bado MHESHIMIWA mwenye nyege kama kina mgusa ANGALAU  MAWAZONI ,....
    ....labda hicho  KINAMHUSU.:-(




    Swali:
    • Unafikiri UNAUHAKIKA  kuna jambo lisilo KUHUSU ?

    NI WAZO TU HILI Mheshimiwa BI Mkora!:-(
    Hebu katika kubadili ndude tumsikilize mtoto wa NYERERE ambaye kwa jina ni ROSE -MARY NYERERE akijitetea kisomi....... na SAMAHANI kiswahili chake kinahitaji Kingereza katika baadhi ya pointi:-(




    Au tu Kanda Bongo Man achokonoe kidude kwa -Cantique



    Au tu Kanda Bongo Man arudishe mdinyo ajulikanao nao afrika kwa ndude-Wallow



    Au tu Kanda Bongo Man aendelee kushusha uji mzito katika.......

  • KINUKACHO, na kisababishacho HARUFU mbaya ya sehemu za siri za MHESHIMIWA labda havina uhusiano wa moja KWA moja.:-(

    Posted: August 29, 2010, 11:49 am by SIMON KITURURU
    Swali:
    • Unadhani CHAKULA na MDOMO vina uhusiano wa MOJA KWA MOJA?


     Turudi katika taralila:




    Wakati  umestukia MHESHIMIWA ananuka UCHI,...... labda ni kweli sio kosa lake ,....

    .... kwa kuwa ni kweli PIA kuwa UHESHIMIWA na MHESHIMIWA mwenye uchi labda hawana uhusiano wa moja kwa moja KAMA ufikiriavyo,...... na labda UCHI wake  MHESHIMIWA hauhitaji kuheshimiwa kama ufikiriavyo,....

    ....na  labda UHESHIMIWA wa mheshimiwa  MUUZA SURA  ukimnusa sehemu zake  za siri kabla HAJA JI SWAFI  uhakikicho katika ufanyakazi bora wenye hari MPYA labda sio  wa MHESHIMIWA kujiswafi bali ni jinsi tu  vitu vingine kama vile BAKTERIA zisaidiazo hata MHESHIMIWA KUJAMBA  zifanyavyo tu  kazi zao SWAFI.:-(

    SWALI:
    •  Si unajua KINUKACHO labda hakina uhusiano wa moja kwamoja na kisababishacho  UCHI  unanuka?

    Ndio,.......katika KUNUKA kuna bomba la DEMOKRASIA;......labda ndio maana  yoyote yule mazingira yakilipa atanuka KIKWAPA vizuri tu.:-(



    SAMAHANI kwa wazo lililopinda  na ni ruksa kunitukana SHENZI kama  sentensi  ZANGU katika hoja hii zina tako kubwa.:(
    Hebu NINA SIMONE abadili swala kwa kuachia ndude -I want a little sugar in my bowl





    Nina adunge -FOUR Women




    Nina Simone akojoe kisanii- MOOD Indigo




    Nina Simone aachie- My baby just cares for me



    Nina Simone amalizie kwa ndude-Feeling good



    Au tu anyuke hii kitu bomba iitwayo -FEELINGS


    Basi bwana labda tu naye  Eric Clapton azime jazba TU  kwa kitu-LAYLA

  • Kwa kuwa kuna UMADHUBUTI wa HATA chupi iliyochanika KIDOGO,....

    Posted: August 28, 2010, 12:13 am by SIMON KITURURU
    ..... KIFICHA NYETI  a.k.a kifumbisha jicho  ENEO ANUAI , huwa kinaweza kutimiza  HAJA ZOTE za kuficha UCHI kuliko hata chupi mpya  iliyoingia MNATO MFEREJINI  ambayo ni bonge la chupi kama la bibi kwa UZIMA.:-(

    NA inategemea unachungulia NINI kwenye tundu DOGO,...
    .... kwa kuwa  NI KWELI pia HATA  kwa kuchungulia kwenye TUNDU DOGO  unaweza kuona MZIGO WOTE  wa bonge la UCHI  UNUKAO wa mtu MZIMA.:-(
    Swali:
    • AU?

    Ndio,.......KIDOGO,......hata kama ni  KWA kuingiza tu kidogo,.......USISHANGAE kitendo hicho  kumfanya  apate mimba hata INZI  jike aliye na utu UZIMA.:-(




    Swali zaidi KIDUCHU:
    • Si unakumbuka CHUPI aka KIFICHA NYETI chenye tundu kinaweza kuwa kinafanya KAZI vizuri za CHUPI  kama tundu HALILENGI utakapo UTAMU ufichwe?





    TAHADHARI: Stori hii haina uhusiano na CHUPI wala UCHI wa mtu na ukifikiria utastukia HICHO!:-(
     NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA  na ni ruksa kutonielewa NA MKUU KWA HILO usikonde!:-(
    Moja kwa moja hebu Mchungaji MUNISHI abadili mkao kwa ndude nzito iitwayo- Michael Jackson is not DEAD just sleeping.




    Au hebu Lenny Henry na Rowan Atkinson aka MR BEAN wacheze na kumbukumbu ya Michael Jackson



    AU hebu tu FRESH JUMBE arudie ngoma nzito yenye tako kubwa katika -Ama zake AMA zangu

  • Kwa kuwa PROFESA MBELE sio ISSA MICHUZI!:-(

    Posted: August 28, 2010, 5:34 am by SIMON KITURURU
    Katika kijiwe  nilichopitia MUDA si MREFU,...
    .... moja ya hoja ilikuwa  ni UFANANISHAJI na umuhimu wa wafananishwao katika JAMII.:-(
    Kwenye MABLOGA wa ki -BONGO ambao wanatujumlisha na siyeMABLOGA ambao sio warefu,....
    .... ikaanza hoja ya kwa nini  kuna WABONGO  waendao zaidi katika BLOGU fulani fulani kuliko BLOGU NYINGINE  ambazo kuna wadaio ndizo zimeenda shule zaidi na kunasa  BUSARA ZAIDI kuliko BLOGU ambazo wanahisi labda hazina mchango muhimu sana  kwa JAMII .
    Swali:
    • Unafikiri ni kweli watu wote kwenye jamii, uonalo ni muhimu WEWE ni lazima na wao walione ni MUHIMU?


    Moja za BLOGU maarufu na wafananishwao ikawa ni pamoja na  blogu ya  Lady Jay Dee, Kaluse na busara zake, Profesa Mbele , Mjengwa na Anko Issa Michuzi  bila kumsahau Chemi che Mponda, Dina Marios, Dinah wa DINAHICIOUS, Matondo , Mubelwa Bandio,Muzee wa Lundu NYASA, Edo Ndaki,..,...,... Matiya  William Malkiory,...na wengine wengi.:-(




    Mengi yaliongelewa na kila MSHABIKI alikuwa na lake ni kwanini KALUSE ni zaidi ya BWAYA, au Yasinta Ngonyani ni zaidi ya Matondo Nzuzullima,.....
    .... bila kusahau kuwa mjadala ulinoga pale WASHABIKI wa Profesa Mbele walivyo kuwa wanadai kuwa Profesa Mbele Mchango wake ni mkubwa kuliko wa Issa Michuzi kitu ambacho kilijibiwa na hoja kama:......kwani mchango wa Issa Michuzi kama ni mdogo kwanini hata akilini kwako kanasa MPAKA kila ukitaka kujua YA BONGO  moja ya kifusi cha habari za bongo ukifukuziacho ni hichohicho cha Mkuu wa Wilaya aka Issa Michuzi....nk..


    Swali:
    • Kwa ni haiwezekani kuwa kila mmoja mchango wake ni muhimu  kwa auhitajio?
    • Kwani mchango wa Mama mzazi  na wa  Baba mzazi lazima ufanane  kwa kufananishwa kwa kipimo kimoja ki umuhimu wao?
    • Hivi ni kwanini watu hupenda kushindanisha  vitu NA WATU  hapa duniani , na kama napenda miziki ya Profesa J kwani inamaana  ni lazima Profesa J awe ni mkali kuliko Mwanafalsafa au AY ?

    Hoja hizi za nani zaidi ZIMENISHINDA na mpaka leo ukiniuliza siwezi kudai najua ni nani zaidi kati ya Peter Tosh na Bob MarleyLady Jay Dee na Ray C Tatunane na Watafiti, SINDIMBA na MDUNDIKO, ....:-(


    Swali kidogo zaidi:
    • Hivi Rais Mwinyi na Rais Mkapa nani zaidi?
    • Kwani unauhakika Nyerere alikuwa ni zaidi ya KAWAWA kwa Nyerere?


    NI wazo tu liendeleao kunikuna kwakuwa nimeondoka katika kijiwe ambacho bado  Wamshabikiao Issa Michuzi na Wamshabikiao Profesa MBELE wanaendelea kulumbana nani zaidi ingawa kwa mtazamo wangu ni kwamba wote  wawili{Profesa Mbele na Issa Michuzi }nauhakika kuna shule wamewapa na nashukuru kwa kuwa mie ni mshabiki wa wote hawa MABLOGA WAWILI WABONGO ambao ni hazina ya TAIFA.



    NI HILO TU MKUU!


    Na hebu  nijaribu tena kujaribu kustukia ni nani zaidi kati ya Bob Marley na Peter Tosh wakati najua hakuna watu wawili duniani wawezao kushindanishwa kwakuwa naamini hakuna watu wawili WALIO sawa.:-(

    Hebu Bob Malya arudie -Crazy Baldhead



    Au tu Peter Tesha akune kwa ndude-Mama Africa
  • Unafikiri UNAWEZA kuwa RAIS mzuri wa CHOO kama hata harufu za MAVI huzijui?

    Posted: August 28, 2010, 3:41 am by SIMON KITURURU
    Inaeleweka  kuwa ASIYEPENDA harufu mbaya za KINYESI ,....
    ....anaweza kuwa ni mfanyakazi bora tena wa kujituma katika kusafisha UPEVU wa tunda  MSALANI.:-(

    Swali:

    • AU?

    Na LABDA  kujulia KITU hata kama kujua huko ni kwa kitu kama  tu  KUKUNA kipele TU kitu ambacho kwa mtazamo wako NI shughuli IJULIKANAYO KIRAHISI  kuwa  ILI KUIFUDHU haihitaji MIAKA,....
    .....inabidi UFIKIRIE na KUANGALIA UPYA kuwa kuna uwezekano hata  pia KUJIFUNZA UFISADI kwa ambaye HAKUWA FISADI ni rahisi  na hakuhitaji WIKI MBILI kwa KABWELA KUUPATIA  ufisadi  .:-(
    Swali:
    • AU?
    • Unafikiri kujifunza UFISADI na kwa MTOTO kujifunza kuacha kunyonya KIDOLE ni NINI  ni kigumu ZAIDI?


    Na wakati TUNAELEKEA KWENYE UCHAGUZI TANZANIA,......na tunamatumaini ACHUKIAYE ufisadi  ataendelea KUUCHUKIA ufisadi hata akiwa katika nafasi imtiayo nyege ya UFISADI kwa kuwa KATIKA SEHEMU AMBAYO  kazungukwa na viwezavyo KUFISADIWA,....

    .....inawezekana kuna waondolewao BIKIRA ya UFISADI hata kwa kujichokonoa wenyewe chumbani wakati  WASHABIKI hakuna.:-(

    Swali:
    • Unafikiri unaweza kuwa RAIS mzuri  wa CHOO hata kama harufu za MAVI hujui?

    Samahani MHESHIMIWA  kwa kuwa KUNA UWEZEKANO   wazo limepinda na  haki ya mjusi tena hili ni WAZO TU na NIMEACHA!:-(





    Hebu katika kubadili hali ya hewa KIJIWENI Richard Marx arudie baladi nene iitwayo-Right Here Waiting For You






    AU ngojea Michael Bolton na Percy Sledge warudie ndude-When a MAN loves a Woman


  • BINADAMU ni MBAGUZI na asingekuwa MBAGUZI LABDA asingejali kuwa SURA ya KIMWANA MZURI ina pua kama JIPU!:-(

    Posted: August 26, 2010, 12:29 am by SIMON KITURURU
    Na haki ya nani tena BINADAMU huchagua ni nini  ni UBAGUZI wa kuulalamikia,....... ndio maana UBAGUZI wa VYUO au SHULE TU FULANI wa kuchagua waliopasi tu MTIHANI huwa hauonekani kuwa ni UBAGUZI.:-(


    Haki ya nani tena LABDA hata kuchagua wafanyakazi  kwa kudeku uzoefu wao katika kazi aka EXPERIENCE ambao WANAFUNZI huulalamikia,....
    .... ni ubaguzi tu  ingawa ampandishaye cheo MFAGIZI WA CHOO kuwa meneja wa CHOO CHA STENDI kisa siku hizi ni MZOEFU kuhusu maswala ya MSALANI NA HARUFU ZAKE huwa hadhani kitendo chake ni UBAGUZI.:-(

    Swali:
    • Unadhani wewe sio mbaguzi tukinyambulisha ni nini KIKUTEKENYACHO kunako kwa kupenda kikutekenye ENEO ANUAI kwa hiari yako?



    Ndio,....... labda hata uchaguzi wako wa kumpenda KISHTOBE mwenye tako jembamba kuliko  yule mwenye tako LILILOTUTUMUKA ni ubaguzi,...
    .... ingawa kwa sasa  unadhani UBAGUZI ni ule tu wa RANGI, kikabila  au tu KIDINI kwa kuwa tu dini yenu ya kuamini MBUYU  inadharauliwa na waaminio dini za PESA.:-(

    NI WAZO TU hili MKUU na wala huhitaji ukoko wa makande yaliyo ungwa kwa nazi ili KUPOOZA jazba!:-(
    Hebu ERIC DONALDSON abadili kitu kwa kitu-Traffic JAM




    Au tu Gregory Isaacs arudie-Material Man


    Au tu tena GREGORY akune kwa- Not the way



    Amwage-Hot Stepper




    AU tu aachie tu tena na ndude -Cool down the pace

  • STAFF BENDA BILILI!

    Posted: August 26, 2010, 11:13 pm by SIMON KITURURU



    Napenda tu hii BENDI,........STAFF BENDA BILILI!




    Idake katika -Je t'aime




    Staff Benda BILILI walete na ndude-MOZIKI




    Au tu wadinye na mkuno-Marguerite



    STAFF wamwage kitu -Mwana



    Jifunze tena kitu kidogo kuhusu STAFF BENDA BILILI kama huijui Bendi hii kutoka CONGO


    Au niachie tu baadhi ya picha za juzi ya jana wakati STAFF Benda Bilili wako kazini
























































































    Add caption
    Add caption
    Add caption
  • MIPANGO ya KIGOLI januari VS MIPANGO hiyo YA KIGOLI mwishoni mwa MWEZI WA NANE!:-(

    Posted: August 23, 2010, 2:29 pm by SIMON KITURURU
    Mwanzoni  mwa mwaka waweza kukuta kila MTU ana mipango kemkem MIPYA,...
    .....na hari MPYA.:-(
    Na asiye na KIPYA,....... angalau utakuta ana mori na matumaini kuwa MWAKA HUU atafanya juhudi hata ya kuacha kuvaa chupi za mtumba kwa kuwa kwa vyovyote vile mwaka HUU atanunua KIFICHA NYETI kipya.:-(


    Swali:
    • Lakini si inakumbukwa kuwa MIPANGO PEKEE bila mikakati ya utekelezaji na vitendo kuchukuliwa hatua, MIPANGO hufanana na ALINACHA tu?


    Na tusisahau tu kuwa,........KIBINADAMU,.......binadamu awezacho kuwa na uhakika nacho JANUARI cha weza kuwa kimekaa kinyume hata Februari.:-(

    Ubinadamu NISHAI kwa kuwa,....
    ... eti kwa LIBINADAMU,....... uhakika hata wa MIPANGO YA SASA HIVI ya kuwa baadaye ya leo HII , ... hilo  LIMTU  litakaa  uchi hadharani inaweza isiwe NI YA  uhakika kuwa  LABDA  ni  kweli BAADAYE hiyo HILO LIMTU  LINAUHAKIKA  hiyo baadaye LITAIFIKIA  na litakaa uchi  ,... AU hata likifanikisha BAADAYE HIYO KUIFIKIA ni kweli ILE shughuli ya kuachia DUKA LA MZUNGU LIWAZI ni kweli  kunauhakika LITACHUNGULIWA MAENEO kitu ambacho ndicho lengo la HUYO MTU katika mpango mzima wa kukaa uchi ya huyo MHESHIMIWA  ambaye anatabia nzuri tu na wala hata hana CHEMBE ya tabia mbaya au hata  kama wewe ANA   kiburi.:-(

    Swali:
    • Vipi mipango yako ya JANUARI inaendeleaje katika utekelezaji MWEZI huu?:-(


    NIMEACHA na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
    Hebu tu ZAP MAMA wabadili hali ya hewa kijiweni kwa ndude-Sweet Melodie



    Zap Mama wadunge na kitu-Kwenda




    Zap MAMA na Erykah Badu washushe-Bandy bandy



    Au tu Q-Tip amalize tu kwa-Vibrant THING

  • BLAH blah BLAH! Nyoooooo!blah blah BLAH!

    Posted: August 23, 2010, 1:52 pm by SIMON KITURURU
    Kisikilizwacho au hata kisomwacho chaweza kuwa tu ni:

    • Blah blah BLAH Rais Kikwete kaanguka ....Blah blah blah!


    • Blah blah blah Bi Ashura kakuza tako kwa dawa za mchina BLah blah blah .. na sasa anapata sida kwenda HAJA kubwa blah blah blah!

    • Blah Blah Blah Huzuni ni chanzo cha kusikilizisha MTU upya FURAHA... blah Blah blah!

    Swali:
    • Lakini katika BLAH BLAH BLAH si kunauwezekano mtu akaambulia angalau pointi moja ambayo inaweza ikajibu  kama umebanwa choo kiko wapi?
    • Umeshawahi kujiuliza MBWA huwa wanasikia ni nini asemacho BINADAMU  katika stori zake ndefu za BUSARA?


    Ndio,...... kidhaniwacho ni BLAH blah blah kinaweza kuwa ni cha BUSARA,....... ingawa chochote MTU asichokielewa kwake huweza kugeuka Blah blah blah.:-(


    Ndio,....
    ... blah blah blah ambayo kweli ni BLAH BLAH BLAH inaweza kujenga mtu busara,......... kama anaistukia Blah  blah kuwa ni BLAH BLAH blah.:-(Swali:
    • SI inasemekana kuna waongeao ya BUSARA  katika KUTONGOZA na WASIOPOE NGOMA na kushangaa wapiga BLAH BLAH BLAH katika mtongozo wakiina na kuinuka wanaokota kwa mtongozo KIDUDE?


    Labda jiulize mara mbili,........ kwamba udhaniacho  ni BLAH BLAH blah kweli ni blah blah blah  kwa kuwa unadhani ni blah blah blah...

    ... kwa kuwa  labda wengine sio WAPUMBAVU KAMA UDHANIAVYO kwa kuichukulia hiyo blah blah  kuwa ina UJUMBE MZITO kitu ambacho  kinawafanya  hata wamvulie mtu KIFICHA NYETI wakigawiwa KAULI ambazo kwako ni  Blah blah blah HATA katika MTONGOZO.:-(
    NI wazo tu hili MHESHIMIWA na ruksa kulibishia hasa kama halikupandishi mdadi wa kunielewa kwa kuwa WAZO HILI kwako  ni BLAH BLAH BLAH tu !:-(

    Hebu tu Harry Belafonte abadili harufu kwa kidude-Jump in the line





    Au tu Harry Belafonte arudie ndude-Coconut Woman


    Au tu Harry Belafonte amalizie tu kwa kitu- Mama look a booboo
  • ANGALIABONGO blog!

    Posted: August 23, 2010, 1:21 pm by SIMON KITURURU





    Kuna mabadiliko ya blog yangu kutoka www.angaliabongo.co.tz na sasa kuwa:
    www.angalia-bongo.com
    NATANGULIZA SHUKRANI ZA DHATI,SARAH.
  • Kama kuna mkutano wa MBU ili kutibu MALARIA!

    Posted: August 19, 2010, 1:54 pm by SIMON KITURURU
    Katika mkutano wa MBU,........ mbu wanaweza kukubaliana pia STAILI ya kukwepa kupigwa kofi na BINADAMU wakati wanapata msosi katika staili ya KUNYONYA damu.:-(


    Swali:
    • Kwani  mnyonge anategemea MAFISADI watajadili nini katika mkutano uliojaa MAFISADI Tanzania?
    • Kwani huwa unashangaa WABUNGE wakikubaliana kuongeza mshahara wa WABUNGE katika mkutano wa WABUNGE?:-(


    NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA Kigoli!


    Hebu twende unyagoni na Harry Enfield katika - Women Keep Your Virtue


    Au tu Harry Enfield achokoze watu kwa -Women know your limits



    Harry Enfield atupeleke jandoni kwa -The Conjugal Rights Guide


    Ok ngojea Tenor SAW abadili mkuno kwa kurudia sindimba-Ring the alarm




    Au tu Buju Banton aingilie shughuli katika ndude hiihi -Ring the alarm
  • Kwa kuwa katika shughuli ya kujamba, KIJAMBIO kwa kawaida huwa hakiombwi RUKSA!:-(

    Posted: August 19, 2010, 1:39 pm by SIMON KITURURU
    Ndio,....... katika shughuli AMBAZO hufanywa,....... kitumikacho kufanikisha SHUGHULI kufanywa kingekuwa na jeuri ,........LABDA usingekojoa.:-(

    Swali:
    • Unauhakika mikono ingekuwa na kibezi ingekubali kutumika katika shughuli zako za chooni za KUCHAMBA?

    NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA na wala huhitaji kubadili chupi kama HUNIELEWI nacholenga kwa hoja.:-(

    Katika kubadili wazo:
    • Kama WEWE ni MKRISTO au MUISLAMU , hivi unafikiri SHETANI naye anaungua JEHANAMU kama njemba zenye dhambi?


    Ok ngojea tu Manu CHAO abadili hali ya hewa kwa kidude-Desaparecido




    Manu Chao ashushe-Me gustas tu


    Au tu Manu Chao amalizie tu kukuna kipele kwa- Bongo Bong

  • NIKILEWA , labda wewe kirahisi tu ni MZURI!:-(

    Posted: August 18, 2010, 11:08 am by SIMON KITURURU




    KUMBUKA tu ,........ katika KULEWA,........ kuna walewao mpaka DINI!:-(
    Swali:
    • Unabisha?



    NI HILO tu Mheshimiwa na hili ni WAZO TU !:-(


    Hebu GNARLS BARKLEY washushe kitumbua - WHO'S GONNA SAVE MY SOUL





    SADE alainishe kipengele kwa-By Your Side




    Au tu SADE arudie kidude-Sweetest TABOO




    Au TU tumalize tu kipengele kwa kudeku Gnarls Barkley  wakishusha kitu - Crazy







    Ndio nilikuwepo MEI MOSI Morogoro:-(









































































































    Ndio,.......hakuna picha za MHESHIMIWA akitoa hotuba kwa kuwa KUNAUWEZEKANO nilikimbilia baa kabla ya HOTUBA kumwagwa.:-(
  • WASIWASI wa ambaye hana GOVI kutokana na MAFANIKIO ya utundu wa kukatwa JANDO!:-(

    Posted: August 18, 2010, 10:37 am by SIMON KITURURU
    Kama DUME ZIMA umetahiriwa aka UMEKATWA JANDO kama mimi ,........ hata ubishe ni kweli chako kionjea ukahaba kimekatwa.:-(


    Na kwa bahati mbaya JANDONI za siku hizi  za hospitalini zitumikazo kuleta utumishi  wa kupunguza kipengele bila MAFUNZO ambazo labda wewe unazishuhudia kama mimi,....
    .... LABDA ni kitu ambacho  ni ushahidi  WA KWELI  kwa asiyejua kukuna kipengele KAMA TU AJUAYE KUKUNA KIPENGELE  kuwa  labda shule yake ya MKUNO kuna kitu  imekatwa.:-(

    Swali:
    • Unabisha?


    Na unaweza kunibishia,........kwa kuwa ni kweli  KUKATWA GOVI na mpaka KUKEKETWA KWA MABINTI dhumuni lake halikuwa kuondolewa  TU katika KICHUGUU cha KUONJEA  baadhi ya  eneo la KUONJEA.:-(


    Unaweza KUBISHA,....
    .... lakini  ukifuatilia histori ya KUKATWA NGOZI YA KIPARA au tu  kwa wanawake kukatwa KIPELE  CHA KUNAKO  utastukia  SHUGHULI NZIMA iliendana na MAFUNZO ya mpaka  KUNANIHII ingawa yalilalia zaidi mpaka kwenye jinsi ya kuishi na LIMCHUMBA LAKO VIZURI  ,  staili ya kulizalisha/KUZALISHWA , staili ya kumwambia ANANUKA.... ingawa NDIO, ... pia shule ilifunza mpaka jinsi ya kukitunza KIFAA ili uwe na kifaa madhubuti cha MPENZI kumuonjea.:-(
    Swali:
    • Unabisha?



    Wakati kuna wanaharakati WAPIGAO VITA kukeketa MADEMU zaidi ya hata ya KUPIGA VITA YA KUTUNZA    ngozi ya KIPARA cha  KIDUME , .....



    ,,,,,umewahi kujiuliza ni kwanini kuna mashujaa waendelezao SHUGHULI HIII  kwa nguvu zote hata kama  kwa mtazamo wako SHUGHULI HIII sio ya KIPROFESA au KIBISHORORO inalipa aka ni MZUKA?Swali:

    • ........?

    Ndio,......... kama huna govi LABDA  NI KWELI  baadhi ya eneo lako la kupapasa sehemu za siri za ASHURA kwa ndani  NI KWELI zimekatwa.:-(

    Ndio,...
    .... kama umekatwa na staili za KUONJA au tu kumtunza mpenzi wako kwa KUMRIDHISHA hujui basi weye kona zote za SHUGHULI  jihadhari nazo kwa kuwa labda katika makali zote ZIMEKATWA.:-(



    NI WAZO tu hili MHESHIMIWA na wala usibanwe chupi kama hukubaliani NALO.:-(





    Ngojea SHOW OFF wabadili mtazamo kwa kidude-`li fe Cho



    Au hebu tu Don Carlos arudie sindimba -Ride on Christine



    Au tu Don Carlos aendelee kukuna kipele kwa pambio-Lazer Beam



    Nipo!:-(

































































































  • KUMBUKUMBU nishai - kwa kuwa inaweza KUGEUZA uhalisia wa kitu kwa kutanua hata UJAZO wa tako jembamba kukumbukwa kama LIMETUNA!:-(

    Posted: August 16, 2010, 6:07 am by SIMON KITURURU
    Kumbukumbu si lazima ni FACT aka kwa kindengereko UHALISIA wa kidude,....
    .... ndio maana TUKIO hilohilo  lililoshuhudiwa na WATU KUMI ukiwauliza hao watu kumi unaweza kupata STORI kumi tofauti za jinsi KIDUDE kilivyo tanuliwa.:-(


    Na kumbukumbu za KIDUDE,...... kuna wakati huathiriwa na UTAKAVYO TU kukikumbuka kidude,  na  wakati kidude kinatanuliwa UNAWEZA kujikuta unakumbuka jinsi tu kidude KILIVYOJARIBU kutotanuliwa.:-(

    Swali:
    • Hujawahi HATA kukutana na LIMPENZI LAKO LA ZILIPENDWA halafu ukastukia lina pua kama kibuyu  kitu ambacho ni tofauti na KUMBUKUMBU ZAKO ZA LIMPENZI  ambazo kabla hujakutana naye siku hizi  limpezi HILO MAWAZONI lilikuwa na kiuno kama n'ge na pua  LENYE utamu wa kwenye  macho ambao ni  MURUA?

    •  Kwani hujawahi kurudi mahali ambapo kwenye kumbukumbu zako palikuwa BOMBA na kustukia kumbe pako na palikuwa pakawaida tu  kama sehemu za siri  ulizozichoka?



    Ndio,....... katika WAKUMBUKAO,....... kuna wakumbukao kwa kuwa WANAKUMBUKA   na kuna  WAKUMBUKAO  tukio VIZURI.:-(


    Ndio,...
    ... katika WADAIO  WAO ni VIZURI wakumbukao,.......si lazima WOTE NI KWELI  wakumbukavyo vina UHALISIA na UHALIHALISI kama VIDUDE VYENYEWE HALISIA WADAIVYO KUVIKUMBUKA  hata kama wasimuliavyo makunyanzi ya kidude KWA MTAZAMO WAK O wanapatia vizuri.:-(


    Swali:
    • AU?
    Kumbuka tu ,...... kuna uwezekano  ukumbukavyo KIDUDE inategemea na ANGLE aka KONA YA sehemu uliyokuwepo wakati unakipigia chabo kidude.:-(

    Kumbuka tu,...
    ... kumbukumbu za aliyekipiga chabo kidude kwa juu na aliye KIPIGA chabo kidude kwa chini  WAKATI HUOHUO, kunauwezekano KUMBUKUMBU ZAO  za kidude wakati wa tukio LA MTANUO  zinaweza KUTOFAUTIANA ingawa ni kile kile KILICHOKENUA kidude.:-(

    NIMEACHA na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!Shikamoo basi kama UMENUNA!

     Hebu MOJA kwa moja kwa kuwa niko katika mudi ya BLUES  nimuachie Samuel L Jackson amwage  ndude - Stack -O -Lee katika kubadili hali ya hewa hapa KIJIWENI.:-(



    Au tu John LEE Hooker amwage hii ndude -Tupelo katika kuendeleza BLUES



    Au tu tulainishe kidogo NDUDE  kwakuingizia dalili za ULATINO  kwa kumuachia John Lee Hooker akija tena na SANTANA wakijamba kisanii kibuyu - The Healer





    Au tu na  JACOB F. DESVARIEUX alainishe kwa kunakishi BLUES kwa ZUKU MUZIKI katika mkito-Euphrasine's Blues




    NAKUTAKIA JUMATATU YENYE matako manene MHESHIMIWA hasa kama wewe ni mpenzi wa SANGARA WAMO!:-(
  • Kama kuna LA MUHIMU katika CHEMBECHEMBE za busara zilizoko kwenye UJINGA.:-(

    Posted: August 15, 2010, 6:01 am by SIMON KITURURU

    Operesheni za MJINGA,....... kwenye DARUBINI usishangae kustukia hazina UJINGA.:-(
    Na kwa WEREVU ukitafuta wao UJINGA,......... wawezakuta mpaka TANI ELFU za UJINGA.:-(

    Na katika UFIKIRIAYO ni mambo ya KIJINGA,.......... yaweza kuwa ni kweli TU KWAKO kuwa ni ya KIJINGA kwa kuwa TU umeshaamua HAYO ni ya KIJINGA.:-(
    Na labda UKITAFUTA busara na UEREVU  katika  yadhaniwayo ni ya KIJINGA,.........waweza ibuka MWEREVU na mwenye BUSARA na wala sio MJINGA.



    DUH! NASITISHA WAZO hapa  !:-(
    KUMBUKA hapa na spekuleti  tu HOJA katika WAZO KIJEBA na wala usibanwe chupi kama HUNIELEWI!:-(


    Hebu jikumbushe kitu katika -Think DIFFERENT


    Au hebu jikumbushe pia katika -Information Overload


    Au turudi tu CONGO ili LOPANGO ya BANKA warudie ndude -MPO NA KONGO

  • Unaweza kurahisisha KUWAUMIZA walio HAI waijalio MAITI kwa kuipiga bonge la teke MAITI!:-(

    Posted: August 14, 2010, 12:16 am by SIMON KITURURU

    Kulengwa,........ sio lazima moja kwa moja ULENGWE.:-(

    Swali:
    • Unabisha?


    Ndio,.......moja ya STAILI ya kumuumiza MAMA YA MTOTOO  wala labda sio kulipiga MBATA mama la toto,....... kwa kuwa inawezekana MAMA LA TOTO litaumia zaidi  kama utalibwenga bonge la konzi  LITOTO LAKE alipendalo.:-(


    Swali:
    • Si unakumbuka BAADHI ya maumivu uyapatayo wala haukuumizwa moja kwa moja WEYE?

    • Si inasemekana kuna watu weusi waumiao Rais OBAMA akitukanwa  kuhusu yamuhusuyo OBAMA na wala YASIYOWAHUSU wao walalahoi kisa wanajisikia yake yanawahusu kisa wanaamini naye MWEUSI?



    Ndio ,...... UKICHUNGUZA labda hata kilichokuumiza leo wala HAUKULENGWA wewe.
    Ndio,...
    ..... na labda wakati linalengwa TOTO kwa bonge la KONZI , kushikwa BONGE la  kibindo au TU  pamoja na TOTO  kufinywa lile BONGE LA MFINYO na LIBABA lake,....
    .... nia ya LIBABA LAKE  ili kuwa ni  KUMUUMIZA MAMA YAKE HUYO MTOTO  na wala sio KUUMIZA hilo  TOTO kinuka mkojo kama KWA HARAKA HARAKA ufikiriavyo WEWE.:-(

    Swali:
    • Ushawahi kuhisi utamu kwa kushuhudia mwingine anagawiwa BONGE la utamu?
    Ndio,......... inasemekana kuna watamanio hata MME wa mtu kisa stori tu ambazo zimewafanya wastukie utamu tayari wa lijitu ambalo sio lao na HAWAJA lionja.:-(

    Ndio,...
    ..... tamu kama CHUNGU  VILE labda kisaikolojia unaweza kusikilizishwa hata bila kuonja WEYE mwenyewe MOJA KWA MOJA  - kwa kushuhudia TU -  au tu kusikia waonja TAMUTAMU -  na kudhani unajua MAUMIVU ya ambao UNADHANI UNASHUHUDIA chungu wanaonja.:-(
    Swali:
    • SI unakumbuka kunauwezekano mkubwa MAITI haisikii maumivu?


    NI WAZO TU HILI KIJEBA na wala USIKONDE kwa kuwa kunauwezekano HALIKUHUSU!:-(

    Hebu tubadilishwe wazo hili na BIZMAN akirudisha ile ngoma ya mpwito ijulikanayo kama-MADEMU WA BONGO



    Au tu tubakie BONGO ili RAY C naye atupe pambio-Touch ME



    Au tu na Saida KAROLI anyuke-Ndombolo ya SOLO

  • Kuna walioko HAI wasahauo kuwa WANAHEMA,....

    Posted: August 14, 2010, 11:43 pm by SIMON KITURURU



    ..... na LABDA ingekuwa inabidi  ili KUHEMA inabidi MTU akumbuke KUHEMA,..........kuna NJEMBA ambazo zingekufa kwa kuwa TU zimesahau KUKUMBUKA kuhema.:-(

    Swali:
    • Si inasemekana KUNA WASAHAUO  kuwa BINADAMU wanakunya  mpaka wakumbushwe kwa wao wenyewe kubanwa HAJA KUBWA?


    NI WAZO tu hili BINGWA na wala usibanwe chupi MHESHIMIWA kama WAZO LENYEWE hili halikukuni wala kukutekenya FIKIRA!:-(

    NIMEACHA!

    Lakini katika kubadili hali ya hewa na tukikumbuka leo NI SIKU ya UHURU wa PAKISTAN  hebu tujikumbushe kirefu cha jina PAKISTAN kama lilivyobuniwa na  wanafunzi wa Cambridge Uingereza enzi hizo:
    P-unjabA-fghaniaK-ashmirI-ran S-indhT-ukharistanA-fghanistanN  BALOCHISTAN
    Ndio ,......jina la nchi hii lilibuniwa darasani Uingereza.
    Unauhakika ni akinanani walikuwa mezani wakitungisha mimba jina TANZANIA kabla jina TANZANIA halijazaliwa rasmi?
    Hebu tubadili zaidi hali ya hewa kwa kudungwa hii ngoma kutoka kwa The Bluesbusters iitwayo - Three Times A Lady



    Au tu Lionel Richie naye airudie ngoma hiihii -Three times a lady



    Tuhamie kwa Maxi Priest akidunga mkito-Golden Lady



    Au tu Stevie Wonder naye adunge mkito huu huu -Golden Lady



    Au tu Maxi Priest amalize tu kwa kutukumbusha kuhusu Marcus Garvey kwa ndude- Marcus

  • UMUHIMU wa kutokuwanacho KIDUDE!

    Posted: August 13, 2010, 2:50 pm by SIMON KITURURU
    Kama huna jiulize;....... HIVI wenye NAVYO wana nini  IKIWA  hulka ya BINADAMU hufanya wenye navyo kusahau au hata KUTOSTUKIA umuhimu wa walicho NACHO na hapo ni kama wanakumbuka  kidude WANACHO?
    ....HIVI hata  WENYE amani  maishani mwao YOTE kwani ni kweli wana AMANI kama  hawajawahi kustukia  ni nini kutokuwa na  amani MAISHANI?



    KUTOKUWA nacho KITU,.......yaweza kuwa ndio changamoto  imfanyayo MTU kustukia thamani  ya  KIDUDE.

    Na  wengi waliozaliwa na kukikuta KITU,....
    ..... yaweza kuwa hawapati hata motisha ya kujifunza ni nini thamani ya KIDUDE.


    Swali:
    • Au?
    • SI inasemekana hata thamani ya pesa ni tofauti kwa aliyezaliwa na kujikuta yuko kwenye familia ya wenye pesa  kitu kiwezacho kusumbua kujifunza kwake kubana matumizi?

    • Unafikiri mwenye tako analithamini tako kama asiye natako alithaminivyo tako ?

    Ndio,...
    ..... labda mpaka hata MSOSI huthaminiwa zaidi na wasio na chakula.:-(
    Ndio,......... labda moja ya tatizo la TANZANIA ni jinsi ilivyopata uhuru kirahisi  KWA POROJO ZAIDI  kitu ambacho LABDA kinaathiri UTANZANIA wa WATANZANIA hata katika kufikiria ni jinsi gani maendeleo ya TANZANIA yapiganiwe kwa vitendo  zaidi ya POROJO.:-(


    Swali:
    • Unafikiri WATANZANIA kwa kutokuwa nacho KITU wanajifunza kitu kweli kama haliyenyewe miaka yote tokea uhuru ndio hii?

    NI WAZO TU HILI lisilotimilifu MHESHIMIWA!

    IJUMAA NJEMA na WIKIENDI NJEMA NJEMBA!
    Katika kubadili hali ya hewa kijiweni labda USIANGALIE kideo hiki-Make Sure The Kiddies Are Sleeping Before .....usije kwazika.:-(






    Au turudi tena Kameruni -Sally Nyolo arudie -Tam TAM



    Tubakie hapa hapa Kameruni Bébé Manga arudie ngoma-Mota Benamaa



    Au tu Bébé Manga arudie tu na kitu -Amio


  • MAPENZI ni yaleyale hata kama WIMBO WA MAPENZI LEO ni mwingine!:-(

    Posted: August 12, 2010, 5:22 am by SIMON KITURURU

    MAPENZI ni YALEYALE  hata kama ni siku nyingine na MPENZI ni YULEYULE.:-(
    KITU mapenzi ni kile kile kwa kuwa HAKUNA PENZI hata wakati unapenda LINASALO TAMU YA PENDO LEO  ili iwe tamu VILEVILE kesho hata kama MPENZI ni yuleyule.:-(


    SWALI:
    • Unabisha?
    • Si labda MPENZI WAKO YULEYULE ASIYE NA KIBIONGO  ni juzi ndio alikuwa TAMUTAMU ZAIDI  kwa staili ileile ya kukuna NAZI katika kibinda nkoi?



    Umpendaye LEO kwakuwa MTAMU SANA leo,....
    ... kama unakumbukumbu nzuri tu  UNAWEZA KUSTUKIA siku moja KUWA  hata PENZI HILOHILO na MPENZI HUYOHUYO ,..........tamu ya JANA  labda haifanani na TAMU YA LEO  YAKE HUYO MPENZI  ingawa labda tamu ya KESHO KUTWA na MPENZI HUYOHUYO inaweza kuwa ina UTAMU wenye tako kubwa  zaidi kitu kitakacho kukufanya KESHO KUTWA iwe siku ya kufikiria kwako  KUMUOA au KUOLEWA NAYE  huyohuyo  ambaye mara ya kwanza ulistukia ananuka mkojo kwa mbali  INGAWA SASA YA KESHO KUTWA UNAJIAMINISHA KUWA  ni kweli MKUSANYIKO WA TAMUTAMU ZA TABIA mpaka KITUNZA UTAMU CHAKE  KIKUCHOCHEACHO USIKILIZIE UTAMU  kwa utamu wa kesho kutwa KINAFAA KWAKO kiwe ni chako  PEKE YAKO kibahiri.:-(
    LOH lione vile!



    Swali:
    • SI umestukia lakini kuwa HATA mpenda UKOKO kuna siku UKOKO ni MTAMU ZAIDI ingawa kuna siku chaguo lake la kuonja ni UTANDU ingawa UKOKO ndio kipenzi chake?

    NIMEACHA, na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

    Hebu EDDIE MURPHY aongee tena katika RAW 1987akiongelea-WOMEN



    Au hebu tupate Conspiracy theory katika- Moon Landing HOAX




    Tupate pia Conspiracy theory nyingine ya - 9 /11 hoax



    Au tu Public Enemy warudie -Dont believe the HYPE



    Au tu PUBLIC ENEMY wamalize mshawasha kwa -He got GAME

  • Wakati WAMAREKANI WEUPE inaaminika wanajua ULAYA kwenye asili yao,.......

    Posted: August 12, 2010, 4:49 am by SIMON KITURURU
    .... HEBU tusikilize BAADHI ya WAMAREKANI  weusi MAARUFU ,...
    ....ambao INAAMINIKA wanaweza kujua AFRIKA  ni asili yao,....

    ....ISIKILIZWE WAKATI KISIKILIZWACHO KINAFIKIRIWA  kiaina KATIKA KUJIFUNZA wafikiriavyo KIAINA Afrika.

    Kumbuka KUFIKIRIA kabla ya HUKUMU ni nini unachoangalia na KUELEWA!:-(



    Tuanze na EDDIE MURPHY akiongelea WANAWAKE wa KIAFRIKA




    Tubakie kwenye topiki ili baadhi ya miaka ya baadaye JAMIE FOXX aongelee kiania anavyofikiria  WANAWAKE WA KIAFRIKA


    Au tu tumsikilize Eddie GRIFFIN ajaribu kuelezea kitu katika mkao huohuo katika  afikiriavyo WAAFRIKA kinamna  katika -BACK TO AFRICA



    Au tu Tribe called QUEST walainishe kwa  kubadili mkuno kwa ndude -Hot SEX on a PLATTER





    NI HILO TU   MHESHIMIWA  na linahitaji fikira kama umedeku kitu kabla HUJAFURUMUA mkao wa hitimisho la FIKIR!!:-(
  • MTAZAMO kama SILAHA uwezavyo kumsaidia MALAYA kuvumilia maumivu ya biashara ya KUJIUZA!

    Posted: August 11, 2010, 12:37 am by SIMON KITURURU
    MTAZAMO wa mtu juu ya KITU,......... ni bonge la SILAHA,....
    ..... ndio maana hata kuruka KICHURA CHURA kukitazamwa kwa mtazamo wa kuwa KICHURACHURA NI MAZOEZI  huwa ni MAZOEZI ,....

    .... wakati ukirushwa KICHURA CHURA ukiwa na mtazamo ni ADHABU  hicho hicho KICHURA hugeuka kuwa ni ADHABU.:-(



    Swali:
    • SI umewahi kuona watu katika mazoezi wanapigishwa PUSHAPU  na wanaitikia wito wa KOCHA WA ZOEZI  kwa FURAHA?


    MTAZAMO ni kitu cha ajabu,.....
    .... kwa kuwa unaweza kukufanya URIDHIKE hata na UMASIKINI kwa kuwa kwa mtazamom wako hicho ni kitu cha kawaida  kwa kuwa jamii yenyewe yote uishinayo ni MASIKINI na  kuona ombaomba ni KAWAIDA.



    MTAZAMO ni kitu cha ajabu,........ kwa kuwa kwa MTAZAMO wako kama wewe unajihisi ni MBAYA hata uwe MZURI VIPI unaweza usijiamini KIUZURI kitu kiwezacho kukufanya upende kusifiwa mara kwa mara ni MZURI ili tu angalau ujiamini kuwa labda wewe sio MBAYA SANA kitu ambacho kinaweza kuhasiri hata ni NANI UNAFIKIRI NI MARAFIKI WA KWELI kwako kisa wanakusifia tako kitu ambacho kinafanya udhanie wasio kusifia kalio hao sio MARAFIKI WA KWELI na kwa kidhungu aka LUGHA YA KITAALAMU YA KIBISHOO  ukawaita MA- HATER  kama tu vile kutokusifiwa sio KAWAIDA.:-(


    MTAZAMO ni kitu cha ajabu,........ unaweza ukakufanya usistukie MUHESHIMIWA ni MALAYA ingawa afanyacho ndicho ukiiitacho UMALAYA kwa kawaida.:-(


    SAMAHANI NALIKATIZA WAZO HAPA kabla ya kuongelea kwa kina  ,....
    ....``MTAZAMO kama SILAHA uwezavyo kumsaidia MALAYA kuvumilia maumivu ya biashara ya KUJIUZA!´´



    Swali:
    • Kwani kwa MTAZAMO wako hujanielewa naongelea nini katika kudai MTAZAMO wako unaweza kuwa ndio ukuponzao kusikia maumivu wakati ungegeuza mtazamo CHUNGU ingekuwa TAMU?





    Hebu LOPANGO YA BANKA wadinye ndude kubwa KATIKA KUBADILISHA HALI YA HEWA KIJIWENI kwa kitu-MPO NA KONGO




    Bisso Na Bisso nao wanyokolishe kwa kitu - Le Reve Africain






    AU tu hebu tu BISSO na BISSO wamalizie na ndude-Bisso na BISSO


  • ASILIMIA ya UKWELI kwa kitu mtu afikiriacho ni KWELI;......

    Posted: August 11, 2010, 12:37 am by SIMON KITURURU
    ... mara nyingi KINAWEZA KUELEZEWA kwa kutumia mfano WA JINSI  mtu afikiriavyo NI KWELI  hana hajakubwa wakati anatembea kwa maringo ,.......... kwa kuwa tu ETI hajabanwa hajakubwa.:-(
    Swali:
    • SI unakumbuka labda kwa MTU labda mavi yapo hata kama ni kweli HAJABANWA choo?
    • Uongo si ni kweli ni UONGO kwa hiyo UONGO labda ni UKWELI?

    Ukweli ,....
    ......labda ni UKWELI pale tu kabla hujastukia uongo wake na ndio MAANA MPAKA  hata imani ziko nyingi na zote ni za kweli kwa aaminiye kwa kuwa  kwa KUAMINI  KITU labda ni kukiri KWA MTU  kuwa bado hajastukia DANGANYATOTO kitu.:-(


    Na  labda UONGO ni KWELI,....
    ..... kama ni kweli ni UONGO.:-(

    NI WAZO TU HILI MKUU na RUKSA kulitemea koozi kama halipandi mukichwa!:-(
    Hebu turudi HAITI  tena  ili Sweet Micky arudie ndude -Ou lala


    Au tu tubaki tu hapahapa Haiti Michel Martelly aka Sweet Micky adunge na ndude -Cocorico



    Na labda  tupitie tu tena Congo Tabu LEY alete ya kishtobe - Jolie Elie

  • Fafanuzi ya HOJA ya kwanini inasemekana Rais KIKWETE anamuigilizia Rais NYERERE kushindwa kwa kutumia kielelezo cha SEHEMU za SIRI!

    Posted: August 11, 2010, 12:37 am by SIMON KITURURU
    [Tahadhari: Wazo limepinda na linakonakona kimtiririko kwa hiyo shauri yako kama unanisoma halafu huelewi, Miye SIMO!:-(]

    Kabla sijakupotezea muda; KWA KIFUPI nachokilenga mjeledi  KINUNDU katika TARALILA hii ni kuwa:
    ´´Rais yeyote yule atakayechaguliwa TANZANIA awe kutoka UPINZANI au CCM hataweza kutimiza malengo ya WAMPIGIAO KURA kwa kuwa MIUNDO ya TAASISI za BONGO na UKIRITIMBA WAKE haufanyi kazi ipasavyo......

    Na kiongozi ambaye hataweza kulenga PAMOJA NA YOTE , miundo ya TAASISI ZA SERIKALI na ufanyakazi wa TAASISI kwa kuziboresha au kuzipamburua  ili kuondoa ukiritimba - na ambaye hata lenga kujenga Taasisi MPYA  ambazo zinalenga matatizo ya WATANZANIA na TANZANIA sasa, ..........hata weza kuondoa RUSHWA, umasikini, UJINGA, na kwa kifupi ataendelea kurudia yaliyomshinda NYERERE ambayo yanamshinda Rais KIKWETE.´´
    - Mwisho wa KINUNDU.


    HEBU tuliangalie swala aka KINUNDU  kwa kuangalia jinsi KUTOKA WAZO la kitu mpaka MAFANIKIO YA KITU yahitajivyo ufanisi wa MIUNDO ya TAASISI  kwa  kuangalia dondoo za miundo ya taasisi za SEHEMU ZA SIRI aka uchi  wa MNYAMA    ziwezavyo  KURAHISISHA uelewaji  hasa UKIZINGATIA;....

     ......mfano wa JINSI  mfikiria kupata mtoto awezavyo kufanikiwa kupata mtoto IKIWA TU  miundo mbinu  na miundo ya taasisi HUSIKA zinamuunganiko usababishao KIFIKIRIWACHO kizae mimba.ukikumbuka tu hapa KILENGWACHO KATIKA MFAN ULIOPINDA ni kuangalia jinsi  MKUU wa SERIKALI na WAFIKIRIAJI WENZAKE wahitajivyo miundo mbinu bora  na MIUNDO YA TAASISI  BORA ili WAZO lizae MATUNDA.:-(


    Mwanzo wa  mtazamo:
    MFIKIRIA kuzaa mtoto ili kiutekelezaji azae mtoto ,....
    ..... miundo mbinu ya taasisi za sehemu za siri hufanikisha tu anachofikiria- hapa na maanisha kumpa mimba au kupata mimba-   kwa kuwa miundo ya taasisi za sehemu za siri ipo na inafanyakazi bila ukiritimba ,....

    • ....kitu kifanyacho WEWE KAMA MWANAUME kinakuwezeshaKUFANYA UFIKIRIACHO kiamshe hisia , HISIA ZIAMISHIAZO MAJUKUMU katika MIUNDO YA  taasisi ZA CHINI YA KITOVU ambazo zina mfanyakazi mwenye support system aka miundo mbinu na shehena ambayo ingawa kuna ladha kama motisha kusaidia kazi ifanyike na kimiminika kisafirishwe mpaka katika mdomo wa KIFAA cha fani.

    • ....kitu kifanyacho wewe kama MWANAMKE kisaidie unachofikiria na kama muda ni sahihi KITAIMINGI miundo ya TAASISI zako za sehemu sehemu  itumie MIUNDO MBINU  BORA   ya taasisi za sehemu zako za siri  ILI ziwezeshe  malighafi YAI iliyotengenezwa katika moja ya TAASISI MWILINI  ifikishwe kwenye uchochoro  WA MAKUTANIO ya yai na mbegu hasa kama  miundo mbinu ya upelekwaji wa YAI lisilodariziwa na  LILILODARIZIWA TAYARI mahali maalumu yote ikiwa ni katika kuwezesha mchezo wa baba na mama uzae matunda.

    ..... kitu KITUKUMBUSHACHO PIA umuhimu wa mahusiano ya watu- IKIWA KATIKA MFANO ni mwanamme na mwanamke wajuao mchezo  - ingawa KISEREKALI ni WAFANYAKAZI BORA WAJUAO KAZI  hata kama kuna TAASISI BORA  KIMIUNDO ili matunda yatokee.
    KWA KIFUPI,....
    ....inahitaji ushirikiano wa MWANAMKE na MWANAUME  hata kama TAASISI ZAO ZA SEHEMU ZA UZAZI ziko bomba ili kusababisha matunda ya dunia kujazwa yafanikiwe kama tu ihitajikavyo TAASISI bomba ki miundo kitu ambacho TANZANIA HATUNA  ili kufanikisha MAWAZO YA RAISI  kufikia utekelezwaji murua  hasa ukikumbuka umuhimu wa TAASISI HIZO ZENYE MIUNDO MZUKA ihitajivyo wafanyakazi BOMBA..:-(


    SAMAHANI ngojea nilainishe lugha:

    Sasaaa....





    Tanzania kwa MIAKA NENDA RUDI imesifiwa hasa na WATANZANIA WENYEWE kuwa ni nchi ya amani. Cha kushangaza ni kwamba pamoja na amani yake maendeleo yake yanautapiamlo kiasi kwamba utakuta NCHI ZISEMEKANAZO kukosa amani huwa wala hazitishwi kimaendeleo na TANZANIA ambayo hata kwenye MPIRA wa miguu wenye washabiki wenye munkari au kwenye POMBE ambako kuna washabiki wenye motisha tumeshindwa kuwakilisha katika dunia kwenye fani.:-(

    Na wakati huu wa uchaguzi TANZANIA ni rahisi kushabikia KIONGOZI MGOMBEA mmoja au MWINGINE bila kujiuliza ni kwanini viongozi lukuki waliotangulia kuanzia Rais NYERERE mpaka Rais KIKWETE ,....
    .....siye na amani zetu bado hatuchezi mbali na UMASIKINI, ujinga, CHUPI ZA MTUMBA ,.. ...nk

    Na tunajua kuwa WATANZANIA wanaweza wakiamua hasa ukifuatilia jinsi tuwezavyo kufanikisha KICHENI PATI , harusi za ajabu, kushangilia timu za mpira wa ULAYA, mazoezi ya kupata na kumpa mtu mimba, kupata kilaji ,nk

    SWALI:
    • Umenielewa nalenga nini?
    • Umesikiliza ni hoja gani za MGOMBEA ambazo zinatekelezeka na umefikiria ni kwanini KILIMO kwanza haimfanyi BISHOO ajisikie kushika jembe KIUTEKELEZAJI?

    Ndio,....
    ...... labda TATIZO SIO NANI NI RAIS Tanzania kwa kuwa LABDA hata UMRUDISHE Moringe SOKOINE hakuna atakachofanya kama MIUNDO ya TAASISI zenyewe ambazo ni muhimu katika utekelezaji WA LILILOKUWA WAZO mambo yake  ni kama tako la Mzee aliyejisaidia kaba ya kuchambwa.:-(

    Ndio,...
    ....na LABDA hata kukiwa na TAASISI zenye MIUNDO bora, kama hazina WAFANYAKAZI wajuao kazi na wenye munkari wa kazi ni BURE kama tu Mbwa jike ALIYE KWENYE SIKU ZAKE mwenye taasisi zenye miundo bora ifanyayo kazi sawasawa lakini hajuikumgawia mbwa dume KISHUGHULI au tu Mbwa dume hapatii MSHUGHULIKO wawezavyo kusababisha TAASISI KUTOTIMIZA lengwa ya duninani kujae zaidi MBWA.:-(

    Swali:
    • SI unakumbuka ni KWANINI Waziri MREMA alifanikiwa kusababisha UJAMBAZI upungue kwa kustukia TAASISI katika miundo unahitaji vituo vya polisi vidogo karibu zaidi na WANANCHI?

    NIMEACHA!

    USITISHIKE MHESHIMIWA hili ni wazo tu    NA SAMAHANI kiduchu  KWA KURAHISISHA hoja ngumu na NZITO kwa kuiingilia kimtindo wa taralila za UJINGAbusara   MKUU !:-(

    Hebu Don Carlos arudie mkuno-Time


    Au tu DON Carlos arudie ndude-Just a passing glance





    Hebu nimuachie tu Tenor Saw enzi za 1985 arudie-Ring the Alarm na pia Fever




    Au tu turudi Senegal DAARA J wadunge tena kitu- ALLAH

  • IJUMAA NJEMA wajameni!

    Posted: August 6, 2010, 5:40 am by SIMON KITURURU
    Swali:
    • Unafikiri kuna UKWELI ukilitakia  LIJITU heri ni kweli LIJITU litapata heri?

    NDIO,....
    ..... labda kumtakia mtu HERI  hakuna kibadilikacho zaidi ya kumuandaa MTU  kustukia ya HERI ZAIDI ya ya KIBANO.:-(
    NI WAZO TU HILI MKUU!

    AU tubadili tu haliya hewa kwa kudeku hii ngoma-Can animals think like humans?





    SHOULD U let your man cheat?
  • Labda USIMTISHE MTOTO wako!

    Posted: August 5, 2010, 1:52 pm by SIMON KITURURU

    Kuna kitu WATU wengi hawajui kuhusu MIE Simon KITURURU,...... ila ukweli ni kwamba mkono wangu wa kulia haufanyi kazi vizuri kama inavyotakiwa ,...
    ... kwa KIFUPI hata UKIWA  sio mbali sana siwezi nikakurushia jiwe  kama nataka kukubwenga JIWE kirahisi na MKONO WA KULIA.

    Na tatizo lilianza kisa nilikuwa naficha siri eti kwa kumuogopa BABA.:-(

    STORI fupi laini na YA KWELI :
    Tulikuwa tunaishi SONGEA na moja ya vitu MDINGI alikuwa hapendi ikiwa pamoja na KUWA MCHAFU , kufeli mtihani enzi hizo nikisoma SHULE ya MSINGI MFARANYAKI (kitu ambacho nilikuwa sifeli) ,....
    ..... nilikatazwa kupanda juu ya MITI aka kuparamia miti kimichezo.
    Siku moja mie na marafiki zangu tukaenda  kuiba maembe  aka KUTUNGUA MAEMBE yasiyo yetu shambani  kwa  WANAFUNZI WA SONGEA GIRLS. Enzi hizo shamba la songea GIRLS lilikuwa kubwa  na sisi tulikuwa tunaingilia upande wa UWANJA WA MEDICAL  karibu na nyumba za mwisho mwisho za walimu enzi hizo za miaka ya NAINTINI EITEZ( (Kumbuka ni miaka mingi sijafika Ruvuma sijui maeneo hayo yakoje siku hizi)


    Basi BWANA katika kuwinda maembe bolibo na embe sindano  tukaupata mti ambao mbivu zilikuwa zimenona juu kabisa. Na mie ambaye hukatazwa kupanda miti nilikuwa kiongozi kuparamia juu kabisa kutikisa mti.

    Kilichotokea ni kwamba,...
    .... katika kutikisa tawi ili kudondosha maembe  tawi likakatika na kilichofuata nilijikuta chini nikijiuliza niko HAI au NIMEKUFA,.....

    .....na chaajabu hata marafiki zangu wakinisemesha nilikuwa siamini kama niko hai kwa KUWASIKIA kwa kuwa nilikuwa nahisi kuwa labda hata MFU akisemeshwa huwa anasikia.:-)


    Katika kufupisha stori hii ya kweli;...
     ....nilivyoanguka nilitegua mkono wa kulia na baadaye nikaja stukia labda na kitu kingine mkononi kiliharibika.:-(

    KIKUBWA:Kwa kuwa kwanza nilikatazwa kupanda miti na PILI miye na marafiki zangu tulikuwa tunaiba maembe ya wana SONGEA GIRLS nilifikiri sio busara kusimulia hicho kitu nyumbani. NILIFICHA maumivu na ugonjwa  kisa NAMUOGOPA BABA....
    .....na kwa bahati nzuri ilikuwa ni kipindi cha baridi SONGEA na maswala ya SWETA na JACKETI pamoja na MAIGIZO kuwa NIKO BOMBA  yaliniwezesha kuficha nimeumia mpaka mkono ukapona kinamna.
    TATIZO ni kwamba mkono ulivyopona mpaka leo hauwezi  kumlenga MBAJUWAYU  bila msaada wa mkono wa kushoto.


    Kwa kifupi :
    Nilijitia udhaifu wa mwili KWA KUFICHA UGONJWA kisa NAOGOPA KUCHAPWA. na BABA:-(Unajua tena AKILI ZA KITOTO!:-(

    NI moja tu ya stori ndogo ya KUJARIBU kukufanya MHESHIMIWA ufikirie kabla hujamfanya mwanao AKUOGOPE mpaka ashindwe kukutaarifu hana pesa za kutoa mimba kwa hiyo atajikorokochoa mwenyewe kisiri bafuni.:-(


    Na ni HILO TU MKUU!

    Hebu OCHESTRA MAKASSY wadunge ndude-MKE WANGU


    Hebu NDALA KASHEBA arudishe ndude-MARASHI YA PEMBA




    AU hebu tu DDC OCHESTRA Mlimani PARK wakite kwa -MTOTO AKILILIA WEMBE

    Baadhi ya PICHA zaidi...

































































































































  • MAISHA ya MBU ni magumu kama MBU BADO anaishi!

    Posted: August 5, 2010, 6:15 am by SIMON KITURURU
    Na mbu JIKE ndiye aumaye watu kisa anatafuta VIRUTUBISHO vya wanawe.
    Na jitihada za MBU JIKE aitwaye na wazungumzao ung'eng'e{  Anopheles}  za kutafuta PROTINI kwa kuwa ni mjamzito ndizo zimfanyazo apigwe vita na BINADAMU kwa kuambukiza watu MALARIA,....

    Swali:

    • Unafikiri ni wangapi wanawahurumia MBU  NA KUACHA KUWA BWENGA kwa kuwa WANAJUA ni kweli MBU JIKE ambao ndio wanyonyao damu za watu WANANYONYA  tu katika kutaka angalau watoto wao wapate virutubisho vilivyopo kwa watu damu?
    • Si unajua nia ya MBU sio kuambukiza mtu MALARIA?
    • Unafikiri ni mangapi ukiruka mimba kuna mtu angepigwa BONGE LA MBATA kama kitendo  kingejulikana pamoja na tamu ni kile kimuambukizacho BINADAMU MWINGINE bonge la gonjwa kuliko malaria?

    Ndio,....... labda MAISHA hata ya BINADAMU ni  lazima yawe magumu tu kama huyo BINADAMU anaishi.


    Swali:
    • SI Binadamu tuna mchezo wa kuamini MAREHEMU ni mtu mzuri kwa hiyo akifanikisha umarehemu  kapumzika kama hakuwa mzinzi , mdokoa mboga au tu zile zambi mhusika adhaniazo ni bonge za dhambi zenye tako kubwa?

    NAACHA wazo MKUU, na ni wazo tu hili BINGWA wala sio BIBLIA  !:-(

    Hebu Mbaraka Mwishehe aulize - MATUSI YA NINI?



    Kwa kubaraguza ngojea tudeku baadhi za MOVIE nilizo zirudia kwenye maktaba yangu ndogo ya nyumbani  kama:----
    Samuel L Jackson katika diner  ndani ya movie - Pulp FIction



    Samuel L Jackson katika Pulp Fiction - Ezekiel 25:17 ndani ya kazi ya Quentin Tarantino


    Goodfellas JOE Pesci arudie kitu katika kazi ya Martin Scorsese




    Nipo lakini...:-(
















  • NI kweli MBWA anajua kumnusa demu wa KIMBWA na kustukia demu huyo anafaa KUPANDWA ,....

    Posted: August 5, 2010, 5:33 am by SIMON KITURURU
    ... kuliko BINADAMU astukiavyo hata BINADAMU mwenzio mwenye kikohozi anaweza wakati wowowte KUBANJA.:-(

    Swali:
    • AU?





    Katika kunusa ,........ tunajua NGURUWE na MBWA wana pua kali kuliko BINADAMU.:-(

    Ndio,...... kuhusu kusikia ,...... tunajua hata TEMBO na PWEZA wanasikia  kuliko awezavyo kusikia BINADAMU.:-(

    Na sikubishii MHESHIMIWA ambaye unaweza kustukia mbwa kajamba kwakuwa unanusa,....

    .....HASA KAMA  wakati unamuona BINADAMU ni kiboko kwa kuwa wewe ni BINADAMU unashindwa kustukia KUNGUNI na chawa wana janja zao hata katika kujificha katika MAVUZI ya MHESHIMIWA MCHAFU HATA SIO SANA ambaye ni binadamu.:-(
    Swali:

    • UNauhakika BINADAMU ni mjanja KULIKO MINYOO kwa kuwa  kuna BINADAMU mwenye BENZI halafu aligundua tumizi la chupi?

    • Unauhakika MENDE wajuao JIKO lako MREMBO ni chafu hawana busara za utafutaji maisha kuliko WATANI zangu WACHAGA pale MOSHI stendi?

    LAKINI BINADAMU huyohuyo ukimsikiliza ,....... kwa kudai yeye ni mtu apendaye amani kwa JINA hata la yesu anaweza kukubwenga kisawasawa ili uelewe AMANI ni nini hutu akimtukania mama yako.:-(

    NI wazo tu hili MHESHIMIWA lililokaa KI-MAMA KISEBENGO!:-(Usitishike BISHOOO MHESHIMIWA ni wazo tu hili!:-(




    Hebu Tabou Combo adinye kitu - Pi Gro Pi Long





    Au tu Jean Philippe Marthely adunge ndude - Bèl kréati




    Au tu Patrick Saint Eloi akung'ute mkito -Chiré




    Na labda tu  Jean Claude NAIMRO amalizie KWA ngoma - Ave'w Doudou








    AU niache tu baadhi ya picha za juzi ya jana....:-(






















































Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs