SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • SANAA ya KUAHIRISHA ugomvi mpaka WAGENI WAONDOKE!

    Posted: March 13, 2010, 6:27 pm by SIMON KITURURU
    Ni sanaa kuutafutia UGOMVI muda na MAHALI pake,...

    ....NA labda  uaminivyo MAJIRANI ZAKO daima WANAFURAHA  ni kwa kuwa tu WANAPATIA  kuahirisha MUDA WA ugomvi  au tu hualikwi KATIKA sehemu yao MAALUMU  wapendeleayo kutekenyea UGOMVI.
    Swali:
    • Unabisha?

    Kwa bahati MBAYA,...
    ....wakati unatembea na ugomvi KICHWANI unaweza mpaka ukawa mchoyo  wa NANIHII kwa hata wasiohusika na UGOMVI wako na NANIHINO.
    Na  kwa bahati MBAYA,...
    ....ni sanaa kuahirisha UGOMVI mpaka wageni waondoke kwa kuwa  yaweza kusababisha TOPIKI zote uongeazo na wageni zijae KUBARAGUZA tu na wala hazikuchokonoi KUMAANISHA kweli kuwa nanihiii ina.NANIHINO.:-(
    Swali:

    • AU?


    Na kwabahati MBAYA,...
    .... labda kama WEWE unaweza kukaa MKAO  wa kusubiri WAGENI waondoke ili UGOMVI uendelee yawezekana ndicho kipimo kikubwa kuhusu USTAARABU wako.:-(

    Swali:
    • Unakumbuka sentensi ya kurudishia UGOMVI palepale ULIPOKUWEPO kabla WAGENI HAWAJAJA uitumiayo  baada ya wageni kuondoka?





    NIMEACHA hili wazo MHESHIMIWA na labda wala topiki haikuhusu na usikonde HASA  kama hujawahi kuahirisha UGOMVI kwa kuwa SHEKHE na PADRI au TU uwaheshimuo pamoja na MAMA wamekuja kukutembelea.:-(


    Hebu GEORGE MICHAEL abadili tena kwa -Careless Whispers



    Au Elton John amuongelee tena -NIKITA



    Na JIM REEVES akaribishe katika-Welcome to my WORLD
  • TATIZO la MJANJA akichumbia mtu AMUHISIYE ni MSHAMBA!:-(

    Posted: March 13, 2010, 4:12 pm by SIMON KITURURU
    Kirahisi MJANJA anaweza kujigeuza MWALIMU badala ya kuwa MPENZI kisa anahisi MAHUDUSHI -pangala wake ni MSHAMBA.:-(
    Swali:
    • AU?


    Ukihisiwa MSHAMBA waweza kujikuta unafundishwa mpaka unayojua,....
    .... na wanaokufunza WAJIDHANIAO NI WAJANJA kusahau kujifunza KUONA MAMBO kwa jicho lako kitu ambacho chaweza kuwa ndio KITATUA tatizo.

    Na tatizo la yeyote ajifikiriaye ni MJANJA na ndiye anayejua,.......LABDA  ni kujipa UALIMU kitu ambacho chaweza kuwa ndicho tatizo.
    Swali:
    • Unabisha?


    Ndio kila siku ni SHULE,....... lakini kuna sababu kila mtu SHULENI huwa kuna  MWALIMU amkumbukaye kwa UALIMU mzuri wa kusifika,.....
    .... na labda MAISHANI ukichumbia MSHAMBA jaribu kuchanganua kama ni kweli hilo lakufanya UFUDHU kuwa MWALIMU na si mwanafunzi katika PENZI.:-(


    Swali:
    • Hivi unafikiri UJANJA sio USHAMBA?
    • Hivi USHAMBA ni nini vile?


    NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!
    Hebu SIMBA WANYIKA katika kubadili wamwage ndude-SHILINGI YAUA tena ni MAUA




    Au tu Buena Vista Social Club warudie tena pia - Chan Chan


Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs