SIMON KITURURU- MAWAZONI
-
Kama unasikia nachosikia na KUONA NACHOONA!
Posted: March 31, 2010, 8:29 pm by SIMON KITURURU
Waweza kustukia SIKU HIZI ,....
....Wanasiasa wanachukuliwa kama VICHEKESHO na WACHEKESHAJI wanachukuliwa siriasi!:-(
Kama unaona nachoona na KUSIKIA NACHO SIKIA siku hizi,....
...... unaweza kudhani MWISHO WA DUNIA umefika mpaka usome HISTORIA na kustukia dhambi nyingi zistukiwazo ZILISHA ANDIKWA KUWA ZINAFANYIKA tokea kabla ya enzi za kina YESU na kuna waliodai dunia imefikia mwisho enzi hizohizo wakiwa tu vilevile siriasi.:-(
Swali:- Unafikiri akina FARAO wa MISRI nao hawakuwa na kitu wakiitacho SIKU HIZI?
Kuna uwezekano IDADI YA WATU imekuwa sana siku hizi,...
... na ukichanganya KITU HICHO na TEKINOLOJIA ZA HABARI zisababishavyo mpaka UDAKU KUPATIKANA kirahisi ,....... labda kuna tunayoyasikia TU zaidi SIKU HIZI ingawa yalikuwepo tu hapa DUNIANI toka enzi za madanga chee.:-(
Swali watu wenye imani fulani :- Unadhani baada ya ADAMU na EVA kufanya dhambi ya kula tunda , dhambi yao iliyofuata ilikuwa ni nini?
- Ushawahi kusikia msemo hakuna jipa chini ya anga na kama KITU hakijafanywa na MTU basi kimefanywa na angalau mjusi?
Ndio,........ kama unasikia nachosikia na KUONA NACHOONA,...
..... labda kibadilikacho hapa duniani ni staili tu LAKINI MAMBO NI YALEYALE,.......kama tu salamu kubadilika KUTOKA ``Mambo dukinaa! ´´ kwenda ``Mambo POA!´´ na salamu YA KISASA kuwezakwenda mpaka kuwa ``Mambo Kukojolea dodoki!´´ - lakini zote zikimaanisha JIBU la salamu HIYO HIYO ya tokea enzi ya kuwa ``Mwenzetu hujambo lakini!´´.:-(
Ndio,........ kama unasikia na kuona nachoona,........ labda HATA udaku ni uleule kibadilishwacho ni MAHALI lugha tu itumikavyo au itumikayo.:-(
Na haki ya nani labda mambo ni kama SURUALI ,...
...iwe ni PEKOSI , kodrai au hata JEANS ya nailoni lakini vyote ni suruali na kupendeza au kutishwa na jinsi suruali imbinyavyo tako mtu HUKO KUKO tu machoni mwa mtazamaji na LABDA hakuna WATAZAMAJI wawili WAONAO na kuoanisha suruali na muonekano wa tako sawasawa.:-(
NI WAZO tu la GHAFLA MHESHIMIWA na wala usikonde kama unauwezo wa kula BAGIA !:-(
Namuachia SADIKI aendelee katika-Do You Hear What I Hear
Au tu Rick James abadili zaidi kwa ndude -Cold Blooded
-
Yakisikilizwa MALALAMIKO YA MPENDA KULA asiyependa kupika wala kuosha VYOMBO,....
Posted: March 30, 2010, 8:39 pm by SIMON KITURURU
.... yaweza KUSAHAULIKA kuna watu WASIOPENDA KULA pia DUNIANI.:-(
Na akisikilizwa KIDUME mpenda WANAWAKE,.....
.... kwa muda fulani UNAWEZA kusahau kuna wasenge pia DUNIANI.:-(
Swali:- SI unakumbuka katika kiwanja cha MPIRA WAMIGUU unaweza kusahau uwezekano wa kuwepo washabiki wa NETIBOLI hapo?
Ndio,...
.... kwa kuwa WATU WENGI wanaelekea upande wa kulia USIJE TU KUSAHAU kuwa kuna AMBAO kwa makusudi yao kabisaa wanaelekea KUSHOTO ndio maana wakati una sikiliza stori za waenda MSIKITINI au KANISANI usisahau kuna waendeao UCHAWI PIA duniani.:-(
Ndio ,....... labda APENDAYE kula ndio anaweza stukia matatizo ya KUPIKA na kuosha vyombo na KIRUKA NJIA aliye chacha ndiye atakuwa anastukia matatizo ya gesti za migombani LAKINI na wachawi yawezekana pia wana matatizo yao tu kitu ambacho ni MCHAWI tu atastukia ni hali ya hewa gani kupaa kwa ungo ni shwari zaidi DUNIANI.:-(
Ndio,...
... labda wakati unasikia MALALAMIKO ya hili kumbuka uwezekano wa kuwa kuna MATATIZO YALALAMIKIWAYO ya lile lisilo kuhusu pia hapahapa DUNIANI.:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na wala usikonde!:-(
Hebu Ray Barretto na Mongo Santamaria katika kubadili hali ya hewa kijiweni warudie - Congo Bongo
Au tu na Kofi Olomide arudie-Sylvie
-
KUWAZA!
Posted: March 30, 2010, 4:40 am by SIMON KITURURU
Kama ingewezekana kuchagua nini KISIWAZWE,....
...ningewazia chakula na kuruka kufikiria mpaka kama NI KWELI hakuna mavi yenye ulemavu .
Kama ingewezekana kuchagua nini KISIWAZWE,..........ningechagua kuwaza ya busara na kukwepa kuwaza kuwa moja ya alichonacho MWEREVU ni upumbavu.
Ningechaguliwa cha kuwaza,....
.....labda NI KWELI ningekuwa muda wote ni mpumbavu.
Lakini KWA kuwaza upumbavu,....
.....kuna astukiaye WEREVU wa watu JINSI ulivyotokana na upumbavu.
Na napenda neno ``PUMBAVU´´,....
..... kwa kusababishia KUNIIKUMBUSHA kustukia wale werevu.
NA ni wewe MWENYE busara na werevu ,....
....hasa kwa kuwa tu WEWE na sio MIMI katika yangu ya kipumbavu.
Swali:- Ushawahi kustukia kuwa upumbavu unavyowasaidia wengine hasa kama kwa werevu wako imesababisha unashindwa kufanya kitu kipumbavu?
- Mpumbavu afanyaye kitu na MWEREVU ajizuiaye kufanya kitu unafikiri ni nani mchango wake UTASTUKIWA zaidi na jamii?
- Unafikiri MPUMBAVU kwa kawaida anajistukia?
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!
Hebu The Roots wabadili zaidi kwa ndude- Proceed
Au tu The Roots warudie kitu - The Seed
Au tu A Tribe called quest watulize kwa - Oh my god
-
MIPAKA iwekwayo na UHESHIMIWA!
Posted: March 30, 2010, 4:37 am by SIMON KITURURU
Kwa kuwa jamii ndio inaweka MIPAKA ya nini kisemwe,......... WAHESHIMIWA ndio wafao kisabuni kwa kuwa KIHESHIMA kiwakeracho wamejifunza kuwa huwa hakisemwi hadharani.:-(
Ili kisichozoeleka kisemwe,...
....yawezekana WAHESHIMIWA wajuaji inabidi waangalie upya ni nini HAKISEMWI ambacho KINAFANYIKA kwa kuwa tu jamii imeamua kiheshima hicho kitu kisiongelewe HADHARANI.:-(
Swali:- Si unajua kuna aliyepata mimba au UKIMWI kwa kuwa tu WAHESHIMIWA hawaongelei ngono kwa kuwa HAWATAKI KUDAKWA wakiongelea waaminicho sio tpiki ya kiheshima hadharani?
- Hujawahi kuuonea wivu UHURU wa mtu apendaye kukusimulia ufikiriavyo ni vitu vya FARAGHA ambavyo wewe unavionea aibu mkiwa hadharani?
MIPAKA iwekwayo na HESHIMA,....
....kwa bahati mbaya inategemea mtu na mtu na ukiheshimucho kwa mtu mwingine wala HAKINA HESHIMA.:-(
Ndio ,...
.... kuna viheshimiwavyo kama tu TISHU CHOONI ambavyo hata TISHU IHESHIMIWEJE bado tumizi lake lisaidialo kuongezea heshima ya mtu hubakia ileile ya baada ya shughuli nzito TISHU ndio itakayogeuzwa kichambio.:-(
Swali:- Si unafahamu TISHU nayo inaheshima zake za kimakokoneo?
Hebu Erykah Badu abadili kwa kitu- Window Seat
Erykah Badu arudie ndude - Didn't Cha Know
Au tu Outkast na Slick Rick walete tena ndude- Da Art Of Storytellin
-
HISTORIA ya uchaguzi wa MCHUMBA TANZANIA iwezavyo kusaidia CCM Tanzania.
Posted: March 29, 2010, 3:38 pm by SIMON KITURURU
KIHISTORIA WATANZANIA walichaguliwa MCHUMBA !
Swali:- Unauhakika historia ya kujichagulia MCHUMBA ina muda gani katika familia yenu?
NI HILO TU wazo dhaifu MHESHIMIWA!!
Hebu Loray Misik wasaidie ndude - Gede
Au tu THE DON JOSE PACHANGA wanusishe sikio - SESTETO LA PLATA
-
Kama UMESHAWAHI kuosha uchi,...
Posted: March 29, 2010, 8:38 am by SIMON KITURURU
...kumbuka labda hicho KITU kimesha kupa uprofesa wa kuosha kitu chochote KILE.:-(
Swali:- AU?
- Si unakumbuka CHOO KINUKACHO ni matunda ya kazi za uchi hata zifanywazo kiheshima na MHESHIMIWA?
Ndio,...... sikubishii HASA kama umeshawahi kufikiria WAKATI ukipenga MAKAMASI ushikacho ni MAKAMASI.:-(
NAACHA MUELEKEO wa wazo nisije kugusia kugusia BURE mpaka nyanya za kachumbari uzipendazo zipendavyo kucheza na mbolea ilio oza kuliko kucheza na wewe.:-(
NI HILO tu na haki ya nani wazo hili la TARALILA halijafanyiwa utafiti wa kina na limeruka vyoo vinukiavyo vizuri bila kunyunyiziwa manukato .:-(
JUMATATU NJEMA MHESHIMIWA!
Hebu tubadili kwa kwenda YEMEN kuwasikiliza wanawake washabikiao kuoongezea shughuli kwa watoto katika ndude-The right to marry as a child
Au hebu Marijani Raajab na Fresh Jumbe waangushe ndude - Masudi
Ndio,...... aliyeandika taralila yenye neno lisilo LAKIHESHIMA kwa baadhi ya waheshimiwa ni huyuhuyu mimi kama HUYU MIMI aonekanavyo kwenye picha zifuatazo akijitafutia matatizo na halafu akinunia MATATIZO baada yakustukia alivyojiongezea.:-(
-
Uhusiano wa UKE na UUME WA PANZI usipochanganywa na UHUSIANO wa PANZI MWANAUME na MREMBO panzi JIKE!:-(
Posted: March 28, 2010, 4:28 pm by SIMON KITURURU
TUKIMGEUZA PANZI KUWA nzige au tu BIN -adamu MKUBWA,... ..... labda kuna BINADAMU anaweza kukumbushwa kwa HII TARALILA kuwa MWANAMKE na MWANAUME sio UBINADAMU kwakuwa pia kuna MBWA MVULANA ingawa labda ni BINADAMU ambao inabidi waoshe UANAUME au UANAUKE kwa kuwa wanamchezo kuwa wasipojiswafi watanuka zaidi ya KIKWAPA.:-(
SWALI banangenge:- Unauhakika UKE ungekuwa rafiki ya UUME kama PANZI asinge ugeuza kuwa ni MATUMIZI?
- Unafikiri CHAKULA kinaupenda MDOMO WA PANZI hata kabla ya kugundua hata kisichokuwa nia ya panzi ni kugeuza CHAKULA CHA PANZI mavi?
- Ushawahi kufikiria kuuangalia UKE WA PANZI kwa kuwa hata PANZI DUME havai chupi?
NI WAZO tu lililopinda MHESHIMIWA na kama umenisoma mpaka hapa SHAURI YAKO miye simo!:-(
JUMAPILI NJEMA MHESHIMIWA !
Ngojea Teddy Pendergrass adai - It Don't Hurt Now
Au tu The Isley Brothers warudie - Contagious
DUH Makassy MASIKIONI ananilazimisha niachie pia TENA ndude-Mambo BADO
-
FARAGHA!
Posted: March 27, 2010, 7:05 pm by SIMON KITURURU
[Tahadhari : Wazo limepinda!:-(]
Tatizo la FARAGHA,...... ni kwamba hurahisisha mpaka LILE TATIZO ULIJUALO LINAMKERA MHESHIMIWA liwekwe pembeni kwa kuwa kuna FARAGHA na kufanya lile tatizo ambalo hujui mtu analo likawa ndilo LINAPEWA KIPAUMBELE ambalo ni la MHESHIMIWA kujiangalia uchi kila nafasi ikitokea kutokana na kukwazika kwake ambako HADHARANI hakujulikani,...
...kuwa MHESHIMIWA anajihisi ana uchi wenye sura mbaya kitu ambacho ndicho kimpacho MOTISHA NA nguvu ya kukivulia gwaguro ilia KUJICHUNGULIA kuliko ILE MOTISHA YA KUDAI HAKI YA MNYONGE Mheshimiwa AJULIKANAYO KUITETEA kwenye hutuba zake zisizo kuwa faragha.:-(
LAKINI uzuri wa FARAGHA,...
...ni kwamba inaweza kukufanya UTULIE na kufikiri VIZURI jinsi ya kutatua MATATIZO YAKO na hata YA DUNIA kwa kuwa haubughuziwi na WAKUDA hapo KWENYE faragha.:-(
Swali:- Kwani unabisha kuwa kuna watu FARAGHA ZAO huzitumia zaidi kufanya vitu vyenye undugu na KUNUSA chupi zao ili kujihakikishia ni kweli mkojo wao ukivunda haunuki vibaya sana kuliko WAFIKIRIAVYO watajiinuaje KIMAISHA wakati maisha mazuri yanapendelea MAFISADI?
- Unauhakika aamuaye kuloga mtu huwa anawazia hilo FARAGHANI au katika kijiwe cha wachawi?
- Unauhakika FARAGHA yako huwa unaitumia kufanya vya faragha au unaitumia ZAIDI kuwaza maswala yenye undugu zaidi na kitu kama kati ya KITUMBUA na MAANDAZI nini ni TAMU TAMU KAMA SUKARI zaidi?
FARAGHAAAA!NI kweli mawazo YA MTU yasingekuwa YA FARAGHA labda tungestukia MHESHIMIWA sasa hivi umuaminiye kwa ufundi wa kusali,....
...SASA HIVI anafikiria kikojoleo na baada ya hapo wazo HILO ,...
....kitakacho hitimisha siku ni lile WAZO lake la kila siku la kufikiria UBWABWA na wala sio jinsi gani Tanzania itapata umeme wa kuaminika au wataunyimaje UKIMWI usinenepe kama ifikiriwavyo na wamheshimuo MHESHIMIWA wafikiriavyo ndivyo MHESHIMIWA anafikiria.:-(
HILI NI WAZO TU na halijafanyiwa utafiti wa kina kwa hiyo kifaraja unaweza kulitukania ZAIDI ya SHENZI.:-(
Hebu Matonya abadili kwa kuongelea-Spair Tairi
Diamond alainishe zaidi kwa ndude-Kamwambie
Hebu Isley Brothers waje live na kitu -Between the Sheets
Au nimuachie tu na Notorious B.I.G a sample Between the sheets na kuifanya kitu kiitwacho -Big Poppa
-
Moja ya WAZO LA MWANAMME kuhusu haki za MWANAMKE zikifikia kucheza karibu na mwanaume kunyimwa FARAJA za kike!
Posted: March 27, 2010, 5:30 pm by SIMON KITURURU
wali:- Umewahi kunyimwa wakati unataka?
Haki ya kutaka na inayoeleweka,.......KIBONGE cha mpinzani wake ni KUWA mtu mwingine NAYE anaweza kutoa madai hayohayo kuwa HAKI YAKE ni kukunyima.:-(
Na kwa bahati mbaya MWENYE haki anaeleweka,....... asipoelewa ni kwanini katika HAKI YAKE YA KUTAKA kuwe na mtu mwingine mwenye haki pia ya KUNYIMA.:-(
Na haki NISHAI,....
.... ndio maana wakati kuna ateteaye matumizi ya kikojoleo na bado haja fikiria kuwa KINYEO NACHO NI TAKWA kuna adaie haki ya matumizi ya kinyeo ambayo hataki yawe kisheria katika kifungu cha kimlazimishacho kisheria hicho kipengele kwa wakitakacho katika burudani au mahusiano KUKINYIMA.
Swali:- Unauhakika wakati unanyimwa unamfikiria akunyimaye ni kwanini ananyima saa nyingine kinukacho kipengele?
Na HAKI nishai,........ndio maana kuna wateteao DINI watakuambia mpaka ni upotofu wa maadili kwa jinsi HAKI ZA WATU ZIDAIWAZO KUKUBALIWA SIKUHIZI KUWA WANAPOINTI zinavyotukania maadili ya dini kwa jinsi wafuasi wajaribuvyo kuzielewa dini zenye maelfu ya MIAKA kwa taratibu za uelewaji wa IMANI wa isemekanavyo ni kileo.:-(
Na haki NISHAI,...
.... kwa kuwa haki za wengine zisipofanana na ZAKO wewe zaweza KUKUUMIZA NANIHIII na na kukupa nyege hata ile ya kilio.:-(
Swali la marudio :- Umewahi kunyimwa HAKI YAKO wakati unataka?
Kikubwa cha KUJIFUNZA ni kwamba ,...
.....baadaye BAADA YA KUNYIMWA unaweza kugundua ndio ilikuwa BONGE LA BAHATI NA MSAADA KWAKO,....
... uliosaidia HUKUGAWIWA UKIMWI kwa kuwa ulinyimwa na ndio sababu baadaye ukafaidi tamu zaidi MBIVU zile.:-(
Swali:- Umeshawahi SIKIA mtu aliyelalamikia kukosa USAFIRI anavyosifia BAHATI YAKE baada ya kusikia GARI LILILOMNYIMA LIFTI limeata ajali na wasafiri wote wame ZE DEDI a.k.a wamekufa na KUFARIKI?
Labda KIKUBWA CHAKUJIFUNZA ni kwamba,...
.....ucheleweshwaji wa HAKI za mtu waweza kuwa na fundisho angalau la nini hasa ni haki kwa ANYIMWAYE.
Si utani,...
... HAKI ZA WANAWAKE zicheleweshwavyo LABDA kuna kizazi cha VITUKUU zitafikia kusifia hilo kama sababu wanawake wamezidi NGUVU na UBABE WA NANIHII kuliko wanaume .
Swali:- Umeshafanikiwa wewe binafsi kumnyima MWANAMKE haki yake ?
- Unafikiri mwanamke hajawahi kukunyima haki yako wewe KIDUME?
- Umewahi kunyimwa?
- Haki ni nini?
Nimeacha na NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA na NI ruksa kulibishia!
Hebu Macka B na Dada Kofi wajiunge na makundi ya watu waliozoea kusifia kwa ndude - Proud Of Mandela
Hebu tupumzishwe kwa MANDELA ikisemekana akishabikia watu weupe wauawe
Au hebu Baby Cham na Carl Thomas wabadili mkao kwa ndude- Oh No
Asante WADAU wote tuliokutana juzi fulani ya hivi karibuni ambao baadhi ni hawa katika picha zangu...
-
Tukiangalia uwezekano wa kwamba labda KUNUNA NAKO kunaambukiza!:-(
Posted: March 25, 2010, 6:55 am by SIMON KITURURU
Tukiachana na kununa na kumuangalia MCHUMBA MWENYE SURA MBAYA TULIYEMPENDA KWA TABIA wakati KANUNA anavyotufanya TUJISIKIE ,...
... labda twaweza MPAKA kustukia ,....... kama una-HUZUNI jaribu kujichanganya na wenye FURAHA ili uambukizwe ANGALAU kuchekelea HATA kanyau bila sababu.:-(
Swali:- SI unajua FURAHA nayo huambukiza na ndiyo isababishayo HUWA UNASHUHUDIA hata baadhi ya uwajuao kwa busara nao wakichekelea pia ujinga kisa wako katika mazingira ambayo komedi babu kubwa ni MTU kajamba?
- Umefanikiwa kununa leo?
NI HILO TU MKUU na ni wazo tu!
SIKU NJEMA Mheshimiwa!
Au hebu tumsikilize mgomvi Winnie Mandela
Au tu wa mahaba SHAKILA arudie tu ndude -Moyo unalia macho yanacheka
-
Tufikirie tu UTAMU wa wimbo mzuri wenye MANENO MABAYA!
Posted: March 24, 2010, 8:53 am by SIMON KITURURU
Utamu wa wimbo una mambo yake,...... ndio maana ukichunguza utakuta MPAKA kuna mtu anapenda wimbo FULANI kwa kisa tu unaneno TAKO.:-(
Na avutiwavyo mtu na wimbo kila mtu staili yake,........na kuna wadaio WIMBO MZURI sio mirindimo wala maneno na ni jinsi uwakumbushavyo KITU au MTU na hata wakikuimbia huo wimbo hawafikirii maneno yanasema NINI na yana MAANA GANI na haiwaingii akilini labda huo wimbo ni matusi KWAKO.:-(
Swali:- Kwani kwako wataka kusema wimbo mzuri ni ule uuelewao maneno yake tu?
Ndio,...... kuna ambao uzuri wa wimbo ni VIDEO yake.
Swali zaidi kidogo:- Huwa unafikiria LAKINI ni kwanini unaupenda wimbo fulani?
- SI unajua ni kawaida maeneo fulani kusikia nyimbo za KANISANI kwenye baa na kuna wajipozao baada ya kuzini kwa kusikiliza nyimbo mpya za dini?
Ndio,...
.... labda unavyosikiliza wimbo unachosikia ni VIPENGELE VYA MAISHA katika MAISHA YAKO VIGUSANISHWAVYO na wimbo na wala huusikilizi wimbo kama idhaniwavyo kwa MIRINDIMO YAKE na MANENO YAKE kitu ambacho chaweza kuwa KIMESHASABABISHA umewahi kuukatikia kiuno wimbo wa msibani badala ya kuufanya ukusaidie kutoa BONGE LA mchozi.:-(
NIMEACHA WAZO MHESHIMIWA!
Hebu JOE ARROYO alete - YAMULEMAO
Hebu na Tshala Muana alete pia ndude-Sikila
-
Mazoezi ya KUSIKILIZA usichotaka KUKISIKIA!
Posted: March 24, 2010, 8:28 am by SIMON KITURURU
Jizoeshe kukumbuka ,.......kwa kawaida kunatofauti kati ya WEWE na kisemwacho kuhusu WEWE hasa kwa kuwa hakuna akujuaye kama unavyojijua WEWE.:-(
Jizoeshe kukumbuka,.......kuwa kukwepa kusikia USICHOPENDA KUKISIKIA hakibadili kuwa kinaendelea kusemwa USICHOTAKA KUKISIKIA - na kwa kuwa hata sasa hivi kinavyosemwa hakikuathiri LABDA hakina ATHARI SANA KWAKO KISEMWACHO hata kama sasa hivi ungekisikia kwa masikio yako MWENYEWE kwa kuwa hata sasa hivi KINASEMWA na labda asiyekisikia tu ni WEWE.:-(
Swali:- Si unajua labda sasa hivi kuna anayekuwaza vibaya na kukusema vilevile ingawa wala hilo halikuathiri?
Tatizo lijitokezalo ukisikia USICHOTAKA KUKISIKIA ni kwamba SASA UMEKISIKIA ,...
... lakini mambo yako vilevile kama tu kabla hujasikia KWA AJIAMINIYE kwa kuwa ni KWELI HUWA UNASEMWA hata kama KWA uwezo wa binadamu mdogo BINADAMU HUATHIRIKA pale tu agunduapo ANASEMWA.:-(
Kumbuka kama umefanikiwa mpaka KUSIKIA,....... kibaya kuhusu WEWE ambacho mpaka umekisikia labda HICHO hakina nguvu ya kukuua ndio maana mpaka UMEKISIKIA WAKATI UKO HAI na kupata muda wa kukionea aibu au kukiruhusu kukuumiza tu moyo kisa eti umekisikia KIKISEMWA .:-(
Swali:- Hufikiri kwenda KANISANI au MSIKITINI ni moja ya mazoezi ya waumini ya kusikiliza WASICHOPENDA kusikia kuwa kuna DHAMBI WAKATAZWAZO bado wao wanazisiki tamu?
- Huwa unafanya masoezi ya kuzoea kukosolewa au unafarijika na kumnunia au kumtukania uchi unayemsikia anakukosoa?
....ukimsikia kwa sauti yake anakuteta au tu anatukania matege yako wakati ulifikiri anafikiri unabonge la usafiri.:-(
Ndio,.......... yawezekana moja ya SIRI YA USHINDI KATIKA MAISHA YAKO ni kukabili usiyopenda KUSIKIA hata YASIYOKUHUSU WEWE KAMA MTU kwa mfano ya JINSI IDAIWAVYO KUWA tu Michael Jackson alidai Tanzania YAKO inanuka kwa kuwa labda kuumia tu roho hakutakusaidia kitu UKIFIKIRI.:-(
Swali:- Si unajua hutaathirika hata ukisikia likitajwa jina la kitendo wazazi wako walifanya mpaka ukazaliwa ingawa hupendi hilo KUSIKIA?
NAACHIA HAPA zoezi la kukuzoezesha kusoma maneno usiyotaka kuyasikia!.:-(
Twende kidogo Kenya tukajifunze ya kutoa mimba
Au tu Fally Ipupa abadili zaidi kwa ndude-Ko ko ko
-
UANDUNJE wa kujifunza kutoka katika matatizo WALIYOPITIA watu wengine!
Posted: March 23, 2010, 6:51 pm by SIMON KITURURU
Inasemekana ,......ni muhimu kujifunza kutoka kwa waliofanya HICHO KITU kabla yako.:-(
Ndio inasemekana,...
....unaweza kutopoteza MUDA kwa kuingilia BIASHARA ya chipsi mayai kwenye eneo kama UTAJIFUNZA kwa waliotangulia kuuza CHIPSI MAYAI kwenye eneo na kujua kuwa wateja hakuna na wapitao hapo huwa wana ulizia UGALI na sio CHIPSI MAYAI ambayo ndiyo biashara unaelekezea mtaji wako.:-(
Na inasemekana;...
....utatatua tatizo la KUTUNZA MUDA kwa kutegemea kujifunza kutoka katika MATATIZO YA WENGINE na kuepuka kufanya matatizo kama ya hao wengine yawepia ni YAKO.
Swali:- SI umesikia kuwa INASEMEKANA kuna msaada UNAOTOSHA FUNDISHO kwa kujifunza kuwa ukishika moto utaungua kutoka katika stori za wengine waliowahi kuungua kwa kushika moto kuliko weye mwenyewe kugusa moto ukaungua?
CHAKUKUMBUKA tu ni kwamba,...
....aliyetangulia kufanya KITU anaweza kuwa alikuwa MFUPI KULIKO WEWE na stori zake za ugumu wa kufikia KIDUDE unaweza ukawa uliongezewa ugumu kwa kuwa STORI YAKE KATIKA UGUMU ilijumlisha na KURUKIARUKIA KITU KUTOKANA NA UFUPI WAKE iliafikie KIDUDE kitu ambacho hakitakuathiri wewe ambaye NI MREFU VYAKUTOSHA na huhitaji kuhangaika na mihitaji ya msaada wa kigoda ili kujiongezea kimo UFIKIE kidude.:-(
Swali:- Si unakumbuka WEWE sio YULE kwa hiyo ingawa ngoma ya SINDIMBA ni ileile yawezekana kukata kiuno KWAKO ni rahisi zaidi kuliko YULE kwa kuwa wewe una kiuno kama NYIGU na ujazo wa MAKALI YAKO unatosha zaidi NAKUIFANYA SHUGHULI YA kuitingishia ngoma MAKALIO kwako kuwa rahisi zaidi kuliko wengine wenye kiono kama kabati na makalio chapati ?
Ndio,........ kuna stori za waliofanya UTAKACHO KUFANYA ambazo zaweza kukutisha kwa kuwa umeambiwa ni jinsi gani zilivyo washinda watu,....
.... lakini kumbuka labda walioshindwa SHUGHULI walishindwa kwa kuwa hawakuwa na kitu ulichonacho ambacho ni MTAJI WA PESA na wewe ukiingilia shughuli waliyoshindwa unachohitaji ZAIDI ni mtaji tofauti wa KUTUMIA AKILI ambao nao unao na SHUGHULI ZILIZOWASHINDA WENGINE ukiziingia kivyako mambo yatakuwa mswano.
Swali:- Hujastukia kujifunza kutoka kwa wengine NDIO MOJA YA SABABU watu wengi huhofu kujaribu wenyewe hata wawiwezavyo?
- Unauhakika hakuna CHA MANUFAA ujifunzacho kizuri kwa kuungua mwenyewe NA MOTO ili kujua maumivu ya MOTO badala ya kuogopa moto kwa kusikiliza stori za wengine za makali ya moto?
Kwa kifupi ,...... labda kunakitu ulichojifunza kwa KUSIKILIZA STORI NA UZOEFU WA WENGINE,...... ambazo ulihitaji kujaribu mwenyewe ili kujikwamua katika tatizo lakoLA SASA hata LILE la kuogopa KUTONGOZA MTU kwa kuwa anasifa za kunyima watu KUTOKANA NA STORI ZA WALIOJARIBU WENGINE ,....
....kwa kuwa labda KWA STAILI yako na kwa kuwa WEWE sio WALE ungekaribishwa katika ufalme na utukufu wa ukitakacho hasa ambao uko kwa UMUOGOPAYE kumtongoza.:-(
Kwa kifupi,...
....kwa kuwa CHIPSI MAYAI yasemekana haziuziki katika eneo yawezekana ni kwakuwa sio WEWE uziuzaye,...... na ungeanzisha biashara ya CHIPSI mayai wewe na KWA UKARIMU WAKO ,usafi wa mgahawa wako, BONGE LA BATASAMU LAKO, na jinsi tu uwafanyavyo wateja wanajisikia wako nyumbani , ungeweza kufanya mpaka WAPENDA NGUNA aka UGALI waanze kuja kula chipsi mayai mahali ambapo wengine wanadai hakuna wateja.:-(
Swali:- Umeshawahi kustukia KUJIFUNZA KUTOKA KWA WATU WENGINE haina maana ndio ujaribu KUWAIGA HAO MTUZ WENGINE?
Ndio,.........kujifunza katika MATATIZO YALIYO WAKUTA WENGINE,....... labda isiwe ni KUJITISHA TU kuwa kwa kuwa wengine walipata matatizo basi na MTU MWINGINE atakutana na MATATIZO hasa ukizingatia labda wengine waliona NI TATIZO kwa kuwa ilibidi waonge mwili wakati KWA MWINGINE ASITAYE KWA KUTISHIKA NA STORI ZA WENGINE tayari ni MALAYA kwa hiyo hilo la kuhonga mwili ili atatue tatizo la kupanda cheo wala si TATIZO kwake.:-(
Ndio,...
... matatizo uyasikiayo YALIYOWAPATA wengine ,......yana UANDUNJE hasa kama HUYASTADI katika kunyambulisha yatakuathiri vipi hasa kwa kuwa WEWE sio WATU WENGINE na staili na rasilimali zako za kuanzia AKILI mpaka ujiandaavyo tu kwa kuwa na kondomu au tu polishi ya viatu kabla viatu havijachafuka yawezavyokutofautisha TATIZO LILELILE kwako kutofautiana na hilohilo tatizo KWAKE.:-(
NIMEACHA na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu twende Beira Msumbiji Djaaka wapoze mchecheto
Tubakie hapahapa Msumbiji Djaaka warudie ndude-Djogoro
Au tu James Brown na Lenny Kravitz wabadili tu tena kwa ndude-Papa's got a brand new bag
-
UHUSIANO wa UNACHO WAZA na WEWE!
Posted: March 22, 2010, 9:47 pm by SIMON KITURURU
Anachokiwaza MTU kingekuwa ndicho pekee kitambulishacho UTU wa mtu ,...... labda wengine tusingeitwa WATU na WEWE.
Na ukisoma HISTORIA utastukia , HITLER aliamini mpaka WARUSI kuwa sio watu vizuri, WAJAPANI waliamini WACHINA SIO WATU, na bila kusahau AFRIKA KUSINI kuna waliohubiri mpaka makanisani kuwa WATU WEUSI sio WATU,........ na ukiwaza waweza kustukia ni jinsi gani misingi ya MAWAZO HAYO yawezavyo kuota mizizi ambayo chimbuko lake ni imani kuwa MIMI kwakuwa sifanani nawe basi sina uhusiano na WEWE.
Unachowaza ,...... labda sicho WEWE.
Lakini unachowaza,......... kinaweza kuwa kinachangia ulivyo WEWE.:-(
Swali:- AU?
Kwa bahati mbaya NACHO -kuwaza,....
..... pamoja na yote nijuayo yana kuhusu wewe bado nikiwazacho sio WEWE.
Labda akiwazacho mtu wakati anawaza,...... HICHO NI WAZO tu hata kama ndicho kifanyacho ufikirie unayekabiliana naye ni sio jini au MALAIKA na ni MTU kama WEWE.:-(
Swali:- Unafikiri katika tafsiri yako ya ni nini ni MTU ni asilimia ngapi inachukuliwa na ANACHOKIWAZA katika kukutambulisha kwako kuwa yeye ni MTU?
- Unauhakika kionekanacho kama mtu hakitoshi kuitwa MTU?
UKIWAZA,...... unaweza kuanza kuamini kuna watu uwajuao ambao wala SI WATU kwa kuwa labda wawazavyo na NGEDERE wawazavyo ni sawa.:-(
UKIWAZA,...
... waweza mpaka kuamini kuna BATA wanafikiria kama KUKU kama kipimo ni mwendo wao wakuvuka barabara wakati wanalikimbia gari lako kwa spidi sawa.:-(
Swali:- Unauhakika unachowaza sio kikufanyacho WEWE ni wewe au unafikiria ni sura lako zuri ndilo linauzito zaidi kuwa wewe ni WEWE?
- Unafikiri SURA LAKO halinamchango fulani katika UNAVYOWAZA ?
- Unauhakika sura yako haichangii unavyowazia MAHARAGE?
NIMEACHA na hili NI WAZO TU!
Hebu USTADHI Zakir Hussein atupigie-Tabla solo
Au tu turudi Msumbiji Mariza abadili kwa ndude-Barco Negro
Mariza alete pia - Oh gente da minha terra
Au tuamie tena Cape Verde ili LURA amwage kitu-Na ri NA
-
Leo JUMATATU kama siku ya kufikiria KAMA ulidanganya vizuri JUMAPILI uliyoipita!
Posted: March 22, 2010, 8:34 pm by SIMON KITURURU
Labda waongo wazuri LEO,.......ni wakumbukao walidanganya nini siku za JANA zilizopita.
Na labda mwenye AKILI ambaye anadanganya mtu LEO,...
....katika kusaidia kufanya uongo wake udumu vizuri anatakiwa kukumbuka ADANGANYACHO LEO na baada ya kumaliza kudanganya ADANGANYACHO LEO kuKIkumbuka ALICHODANGANYA LEO SIKU ZIJAZO kama anataka uongo huo WA LEO ubakie na sura ileile na asiugeuze kuwa NI UKWELI siku zijazo kwa BAADA YA KUDANGANYA kuchukulia alichodanganya KAMA NI kitu kilichopita.
Swali:- Unakumbuka mwaka jana muda kama huu ulijidanganya nini ambacho kinaathiri kitu maishani mwako ambacho kimaisha KAMA HUJIKUMBUSHI KUWA hicho ULIJIDANGANYA hutaweza kukipita?
- Kwani hujui KUDANGANYA vizuri kudumuko ni kazi ya WENYE akili wakumbukao kuoanisha uongo wao wa leo na ULE wa siku zilizopita?
- Unakumbuka labda leo kunakitu umedanganya na unakichukulia kitendo hicho kama kitu kilichopita?
NIMEACHA !
Kumbuka hili ni wazo tu MHESHIMIWA ambaye angalau katika KUTONGOZA hudanganya mtu!:-(
Hebu kwa kuwa leo ni JUMATATU tujikumbushe JUMAPILI kwa kuwasikiliza Maroon 5 wakiongelea-SUNDAY MORNING
-
STORI YA KAWAIDA inaweza kusaidia MTU kuisikia ikiongelea USENGE kama msomaji au ASIKILIZAYE STORI anafikiria USENGE.:-(
Posted: March 20, 2010, 7:42 pm by SIMON KITURURU
Katika stori ya kawaida ya MTU,...
... mtu anaweza kusahaulika katika SHUKURANI kama msikilizaji ni yule aaminiye ashukuriwa ye ni MUNGU KWA YOTE hata kama ni mtu ambaye ndiye akumbushaye ya MUNGU .:-(
Swali:- Unafikiri wakati unashida ya chumvi JIRANI akikusaidia chumvi naye hastahili SHUKURANI kwa kuwa unaamini awezeshaye yote ni MUNGU?
- Si unajua stori ya matatizo kwa atafutaye na afikiriaye MASHUJAA anaweza kuwa anasikia stori za kishujaa tu katika ZE HADITHI?
Ndio,...... stori ya KAWAIDA YA UHANGAIKALO NALO,...... unaweza kuigeuza kuwa ni YA MATATIZO ingawa uhangaikalo nalo na JINSI UHANGAIKAVYO NALO wengine huita HILO ni ``MAISHA TU`´hasa kama unaangalia uhangaikalo nalo kwa LENSI ya matatizo na sio kwa lensi YA MAISHA ambayo moja ya jinsi ya kusaidia jipu lipone NI KULIBINYA JIPU.:-(
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!
Hebu turudi MALI ili Mama Toumani KONE arudie ndude - Niemogo
Au tu turudi Tanzania Omar KOPA arudie ndude nzito iitwayo-UNYAGO
Au tu Omar Kopa aongee busara zilizo tafutiwa mpaka siku kwa WABONGO -Kitchen Party
-
UNAFIKIRI NI MARA NGAPI mtu aongeaye na wewe huwa ANAONGEA NA WEWE yakuhusuyo wewe na sio uliyompa nafasi tu KUYAONGEA ingawa alikuwa nayo kichwani kabla ya kukutana na WEWE?
Posted: March 20, 2010, 7:20 pm by SIMON KITURURU
Kuna waongeleao WALI ukiwapa nafasi ya kuongelea WALI ,...... wakati wakifikiriacho kabla ya wewe KUSAIDIA UWEZEKANO WA WALI KUONGELEWA kilikuwa ni UGALI.:-(
Swali:- Unabisha?
Aongeacho mtu kuhusu WEWE kinawezekana hakikuhusu wewe na kinatokana tu na UZOEFU WA YASIYO KUHUSU YA AONGEAYE hasa ukizingatia hakuna amjuaye mtu mwingine vizuri UKIFIKIRIA ingawa ni rahisi hata kudhania kwa kuwa mtu ni ndugu yako basi kuna kitu anajua katika wako UBINADAMU.:-(
Swali:- Lakini wewe unajijua?
- Unauhakika unawajua vizuri hata wazazi wako hasa ukifikiria hujui kwa uhakika walikutengeneza chumbani au migombani wakati wanatoka kwenye msiba wa jirani?
- Lakini si unajua kwa kutojiamini na kujijua kwako kunaweza kuwa ndiko kusaidiako KUAMINI KWAKO kuwa labda kuna mtu mwingine zaidi yako ndiye anaye KUJUA zaidi?
Ndio,....... baadhi ya tafsiri ya MATATIZO MENGINE YA MTU hutokea kwa kuwa MTU HUYO MHESHIMIWA kajifunza na kufudhu kutegemea WATU WENGINE WANAFIKIRIA NINI KUHUSU YEYE mpaka wanafikia kuamini hata kitu kidogo ambacho wanakijua kwa kujiangalia kwenye KIOO kinategemea watu wengine waseme uzuri wa MIDOMO YAO KAMA BIRIKA ni mizuri namna gani au tu ni watu wazuri vipi kwa kuwa hawakosi kwenda msikitini.:-(
NIMEACHA!
Hebu tubadili kwa SANCHEZ kurudi ndude- FRENZY
Au Tanto Metro and Devonte warudie kitu-Gal say Wooee
Tanto Metro na Devonte warudie-Everyone Falls in Love
-
Siku mtu akionjwa WAKATI kashadakwa na ugonjwa wa kichaa uitwao MAPENZI!
Posted: March 20, 2010, 4:50 pm by SIMON KITURURU
Penda,......... na waweza kujikuta unashabikia vijulikanavyo na wanao kujua kuwa huwa vinakutia KINYAA.:-(
Penda,.........na waweza kujikuta aibu zinakuisha na kukusababisha uonekawaida na kudhani ni moja ya kuonyeshwa penzi kuombwa kitengeneza watoto sehemu ambazo zilitengwa katika majengo ili bila BUGUDHA watu wajifungie na KUNYA.
Penda,...
.....na waweza kujikuta kwa mara ya kwanza KWA SAUTI UNABISHANA na wazazi wako ambao busara zao ulikuwa unazitegemea kama ndio misingi ya maamuzi yako ya hata ni kwanini wewe INJINIA SIKU HIZI wakati ungekuwa MPISHI MENYE FURAHA kama ungejisikiliza wewe mwenyewe kama ujisikilizavyo WEWE BINAFSI NA KUWA NA UHAKIKA NA BUSARA ZAKO KATIKA MAAMUZI YAKO kama hasa UJIAMINIVYO NA MAAMUZI YAKO katika kutiii ni muda gani ILIUSIJINYEE inabidi uende chooni KUNYA.:-(
Swali:- Unafikiri kama ungekuwa mtiifu kwa unaloliamini ni KWELI ,- kama ulivyokuwa MTIIFU KUHUSU YAKUHUSUYO WEWE BINAFSI kuwa iliusijikojolee ni muda gani inabidi uende kukojoa,... -unafikiri ni mangapi katika maisha yako yangefanana na wewe au picha yako ya dunia utakavyo iwe?
... kuna uwezekano ukiongea na mgonjwa wa MAPENZI busara zako hazina maana kwa kuwa zinatetea kitu KWA KUTUMIA AKILI ZAIDI YA HISIA wakati uongeaye naye anatumia HISIA ZAIDI YA KUJADILI SWALA KIAKILI kitu ambacho labda ni aina ya UKICHAA.:-(
Na kwa bahati mbaya naweza kusema pia; `` NDIO´´,.......UKICHAA uletwao na PENZI huweza kusababisha CHUNGU KIDOGO kuonekana tamu SANA na kwa hilo labda MAPENZI ni aina tu ya UKICHAA.:-(
NIMEACHA!
Kumbuka NI WAZO TU HILI Mheshimiwa na unaruhusiwa kulitukania!:-(
Hebu Ray Parker Jr abadili kwa kuwatetea wanaume katika ndude- I don't think MAN should sleep ALONE.
Au tu ASWAD warudie -Gotta find a way
Au tu ASWAD waendelee tu na ndude- I need UR LOVE
-
Kwanini ?: -(
Posted: March 19, 2010, 6:57 am by SIMON KITURURU
[Tahadhari: Katika wazo LILILOPINDA KWA WAVIVU WAKUFIKIRIA bado taralila ina neno CHUPI.:-(]
.......WAKATI kuna MPENDA KEKI alazimikaye KUGIDA MIHOGO wakati wengine kwa hiari yao WENYEWE hawaonji wagawiwazo KEKI kwakuwa wanasubiria MIHOGO,...
....yaweza kumtungishia MTU MIMBA ya swali;.......``KWANINI?´´:-(
Swali:- AU?
Ndio ,......KWANINI ,.......ni SWALI la kawaida la mtu!:-(
Swali:- Unabisha?
KWANINI katika taralila yaweza kuwa ,.......katika chupi YA KITABIA ivaliwayo siku ya MTU kupania kumuonjesha MCHUMBA utupu kwa mara ya kwanza ,......chupi HUWA imepaniwa iwe SAFI ZAIDI ya siku ambayo MCHUMBA HATA ANGALAU kwa mbali hatapewa nafasi ya kukodolea uwezekano wa ``MPENZI hajavaa KIFICHA NYETI ´´ kistaarabu ,... na labda NDIYO kiashiriacho kuwa MSTAARABU HUTAKIWI KUJUA kunasiku mtoto mzuri UMJUAYE KWA USAFI labda chupi yake sio safi sana kama KIBANGA ALIYEMPIGA MKOLONI ,...
.... NA inaweza HILO kuwa ndilo SWALI la MTU!:-(
NA kwanini,..........msibani AU HARUSINI kuna wahisio PILAU HUNUKIA vizuri zaidi kuliko KWA MAMA NTILIE YULEYULE ambaye ndiye aliyekuwa na TENDA MSIBANI na PIA ZILE HARUSI KADHAA ULIZO HUDHURIA ambazo ilibidi tu uende kwa kuwa hukuchangia pesa hata za kujionyesha tu KWA WAPAPARIKIAO WAJIONYESHAO kuwa wanapesa kweli kifisadi ,.......na LABDA hilo pia NDILO ni SWALI la mtu!:-(
Kwanini,......HATA ambaye kwa kawaida ndiye MWENYE NYEGE YA DINI AAMINIZO ZINAPELEKA WASIO WAJANJA DUNIANI kule MBINGUNI wakati KUMBE sio kila wakati HUYO NDIYE anajiamini kama ATAMKIAVYO WASIOJIAMINI hasa wakati atulizavyo manyanga ILI MEZA itulie,.......halafu ikitulia ndio mnastukia kumbe YEYE NDIYE yule mtu wa MIZOGA wakati anaokoa SIKU katika juhudi zake za wa ngono YA ufisadi,....
....ndio laweza kugeuka kuwa ndilo GUMU KINAMNA swali la MTU.:-(
Swali:- Kwa WATANZANIA unafikiri ni kwanini Mheshimiwa KIKWETE na sio Mheshimiwa PROFESA SARUNGI au Mheshimiwa RASHIDI KWAWAWA ndiye aliye tangulia kuwa MHESHIMIWA RAIS WA TANZANIA kabla ya Waziri mkuu MORINGE SOKOINE ?
- Unauhakika kwanini YESU hakuwa MWANAMKE?
- Umeshawahi kujiuliza NI KWANINI SIO kila lifanyikalo LIKUHUSULO HUWA UNAKUMBUKA kujiuliza KWANINI?
Ndio,.......LABDA ni kweli ,........KWANINI ni KIBONGE LA SWALI ndio maana SIO rahisi KUJIULIZA
ni kwanini inasemekana kuna MWINGINE aliyevulia mtu chupi mara moja tu na akapata KITU CHENYE THAMANI YA UWAZIRI wakati kuna aliyevulia chupi ZAIDI YA WATU WANNE NA NUSU na kutopata angalau BILAURI MOJA ya UJI WA MUHOGO wa asubuhi moja.:-(
Ndio,......labda kuna sababu ,........KWANINI ,.......ni SWALI la mtu.:-(Swali:- KWANINI?
- Tukiachana na UjingaBUSARA wa hiki KIJIWE huwa LAKINI unakumbuka kujiuliza KWANINI mara kwa mara MAISHANI?
DUH !NIMEACHA WAZO MHESHIMIWA lakini ni wazo tu HILI MKUU !:-(
IJUMAA na WIKIENDI NJEMA MHESHIMIWA!
Hebu Hugh MASEKELA abadili tu kwa kutukumbusha SOUTH AFRICA katika JAZZ katika ndude- Strawberry
Tubaki tu Afrika Jimmy Dludlu aendelee TENA kujaribu kulainisha wajanja kwa ndude -Tote
Au tuhame tu na tupate ndude -Casanova kutoka katika unajisi wa shughuli wa - Levert
- AU?
-
kWA bahati mbaya MUDA hauponyi MAUMIVU!:-(
Posted: March 18, 2010, 5:42 am by SIMON KITURURU
Ndio,.......kunauwezekano UFANYACHO NDANI YA MUDA baada ya kuonja UTAMU ndicho KIKUPONESHACHO kumbukumbu ZA jinsi ulivyowahi kuusikilizia UTAMU.:-(
Ndio,.......kuna wasemao kwa ung'eng'e ``TIME HEALS´´ a.k.a ``MUDA UNAPONYA´´ ingawa mimi ningependa kukualika ukae mkao wa kufikiria uwezekano wa kuwa - ``IT IS WHAT YOU DO within that TIME that DOES THE TRICK´´ a.k.a kwa lugha ya wajanja-``NI UFANYACHO baada ya KUUMIZWA au KUSIKILIZISHWA UTAMU ndicho kinaweza kukusahaulisha na KUPONYA uyakumbukavyo MAUMIVU au tu ule wa lawalawa UTAMU´´.:-(
Swali:- Kwani ni kweli ulifikiria maumivu na WIVU wa mwenye MPENZI aliyestukia MPENZI wake aliyekuwa anafikiri ni wake peke yake tu anagawia na wengine UJANJA huwa yanaponeshwa na MUDA TU bila kwa hilo lijamaa aka HILO lililostukia linadokolewa penzi na wajanja kujishughulisha na kitulizo kingine ambacho labda ni KWA kujisomea KORANI na kumsikiliza mchungaji wa PENTEKOSTE?
- Unafikiri ni MUDA TU na sio na michango ya vitu hovyo kama vile WALI , mikate na VIAZI ambao vitakusaidia kusahau UTAMU wa UGALI NA MAHARAGE hapo baadaye ukiamua kujisahaulisha tamu yake kwa kuwa inakukumbusha sana MBWA wako mpenzi alipozirahi na kufariki dunia?
Ndio,...... labda MUDA haukuponyeshi UKUMBUKAVYO utamu wa MAKANDE YALIYO CHACHA kama ndani ya muda baada ya kula PURE a.k.a MAKANDE yaliyochacha hautashughulika na kitakacho KURUDISHIA kumbukumbu ya UTAMU HALISI wa yale matamu MAKANDE.:-(
Ndio,...
....ukifikiria LABDA utastukia ni KWELI kuna kitu umefanya katika muda na sio MUDA TU ndicho kilichofanya hukumbuki vizuri ulivyotishika na DHAMBI baada ya kufanikiwa kwa mara ya kwanza kuifanya MAKUSUDI ndio sababu LABDA siku hizi unarudia HIYO dhambi makusudi KIRAHISI bila kujisikia vibaya sana.:-(
Ndio,.......MATUMIZI ya MUDA na labda WALA sio muda ndicho kisababishacho kuna aina ya UTAMU huisahau na kunaaina ya MAUMIVU labda unailenga makusudi ili kujikumbusha jambo FULANI ingawa bila kufikiria ndio maana kuna MPENZI husahau maringo yake.:-(
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA na haki ya nani tena NIMELIACHA!
Hebu tubadili kwa kwenda kiduchu BRAZIL Sergio Mendes atuletee tena kitu-Magalenha
Au tu Sergio Mendes na The Black Eyed Peas warudie ndude-Mas Que Nada
Basi bwana , tubaki tu na Black eyed Peas ya enzi ZILE katika kitu kitukumbushacho wikiendi bado haijafika kiitwacho-Weekends
-
BABA ntakusemelea kwa MAMA! OooooHO!
Posted: March 17, 2010, 8:16 pm by SIMON KITURURU
[Tahadhari: Wazo linatapatapa katika TARALILA HII!]
NIA ya kumsemelea MTU kwa mtu,....
..... inaweza kutoa SIRI ya MTU WA TATU ASEMELEAYE MTU ya anawafikiriaje hao watu wawili ajitahidio kuwaunganisha kwa MSEMELEO.:-(
Kuna wadaio PIA kuwa ukisemelea mtu,...
.... nia yako ni kutaka tu UKWELI ujulikane na SIO KINGINE,......na ikitokea kama unayemsemelea AKIPATA KIBANO basi hiyo huwa ni BONASI tu kama kwenye CHIPSI dume ilivyo KACHUMBARI ,....
....NA NI BONASI tu PIA kama UTAPATA FARAJA SANA TU hasa ikitokea ukashuhudia matunda yale YAKUSEMELEA KWAKO - yale ya KUGOMBEZWA kwa MTU, kubinywa KWAKE makende, KUFINYWA au tu KUDHALILIKA kukifanikishwa kutokana na wako MSEMELEO.
ILA kwa bahati mbaya ukiangalia tabia za watu,...
.... utastukia KWA KAWAIDA afikiriwaye ni MNYONGE ndio HUSEMELEWA kwa MBABE ili ikiwezekana ishuhudiwe akigawiwa MKONG'OTO au angalau KUGOMBEZWA kidogo baada ya MSEMELEO.:-(
Swali:- Unafikiri KIINI cha KUWASHWA kwa mtu mpaka ASEMELEE KITU kwa MTU huwa ni kweli ni NIA UKWELI UWE WAZI watu tumjue anyaye pembeni ya choo na KUFUTIA UTAJIRI kwenye ukuta wa choo ni nani au nia ni KUJIFAJIRI kwa MSEMELEAJI kwa KITENDO CHA KUSEMELEA?
- Unakumbuka mara ya mwisho uliposemelea MTU?
- Unafikiri kwa kawaida Tanzania , BABA akisemelewa kwa MAMA ina -nguvu?
NABADILI kidogo;....
Ndio,....
..... kunauwezekano hata ukiisemelea SERIKALI YA TANZANIA kwa WANANCHI,........ wananchi hushindwa kufanya kitu ingawa ndio wenye NGUVU na matokeo yake wengi twashuhudia WASEMELEAO WANANCHI kwa SERIKALI kwa kuwa wanajua SERIKALI ina polisi na MAGEREZA- bila kusahau vyombo vya habari ivitawalavyo ambavyo vyaweza kustua watu NCHI NZIMA wasiona HATA NA mpango na WEWE kuwa umekaa uchi bila kificha nyeti UDHALILIKE kwenye jamii na kwa ALIYEKUSEMELEA.
NARUDI PALEPALE;.....
Ingawa kirahisi katika JAMII ya KITANZANIA inaweza kuaminika ``MAMA ntakusemelea kwa BABA´´ inanguvu zaidi ya ``BABA ntakusemelea kwa MAMA´´,...
.... ukweli wenyewe waweza kuwa uko kinyume kwa kuwa labda MAMA ndio mwenye nafasi nzuri ya kumuadhibu BABA kama adhabu aamuayo kuitumia NI ITUMIAYO AKILI ZAIDI na sio ile ioanishwayo na MIGUVU ya MISULI na PESA za BABA.:-(
Swali:- Si unakumbuka achangiaye kuonekana MWANAMKE ni dhaifu inawezekana ni MIMI na WEWE hasa weye mwenyewe MWANAMKE?
- SI imekuwa kawaida kwa MWANANCHI kusemelewa kwa vyombo vya mabavu vya SERIKALI mpaka inasahauliwa ni WANANCHI HAOHAO WAOGOPAO SERIKALI ndio bila wao hakuna SERIKALI hata hiyo isiyowajali yaweza kujitutumua kwa MAGUVU?
- Unauhakika lakini BABA mwenye MIGUVU na MAMA wakianzisha vita baada ya wewe kumsemelea BABA kwa MAMA hawezi kudedi MDINGI ambaye kazoea kupikiwa na MAMA MWENYA AKILI na kutarajia MINOFU YOTE MIKUBWAMIKUBWA ya BATA apewa yeye kwenye ZE MLO ambao watoto huambulia mchuzi na mabakimabaki ya chembechembe za mnofu wa BATA kabla BABA hajarudi usiku KALEWA?
NIA ya kumsemelea MTU,......... inaweza ikawa ni kujisikia vizuri tu kwa ASEMELEAYE hasa kama anachokisemelea hakimuhusu ASEMELEAYE kuwa UNANANILIHIII ambacho hata KISIPONANILIWA hata afanyeje HATA KINANILII YEYE .:-(
Ndio,....
.... sibishi kuna ASEMELEAYE mtu,........ kwa nia ya kusawazisha kosa ili UNAYENANILII usijezoea tabia MBAYA ambayo itasababisha UNANILIWE hapo baadaye.:-(
NIMEACHA wazo MHESHIMIWA na kumbuka hili ni wazo tu ambalo ni RUKSA kutolielewa!:-(BWANA na BIBI wasifiwe!
Tupoze basi kwa kumsikiliza tena Mheshimiwa IDD AMIN
Tuendelee kidogo na Mheshimiwa Idd AMIN
Na tumsikilize kidogo tena Mheshimiwa KIBAKI
Sasa twende kwenye KIPELE nikilengacho bila utani-Where Will We Find Tomorrow's Leaders?
-
UBINADAMU DHAIFU uletavyo mapungufu mpaka katika kile KITU watu HUNUNUA!:-(
Posted: March 16, 2010, 1:42 pm by SIMON KITURURU
[Tahadhari: Taralila hii KUNAUWEZEKANO ina wazo lililopinda!:-(]
BINADAMU katika anunuayo:....
....katika CHAKULA,...
....LABDA katika MAPUNGUFU hununua msosi akifikiria UTAMU badala ya VIRUTUBISHO VYA MWILI ambavyo kwa BINADMU ndivyo muhimu kiafya na UZIMA.:-(
Katika WACHUMBA ,....
.... labda hununua hata kwa mizawadi LIMTU ZIMA na MITABIA YAKE MIBOVU wakati labda wahitajicho katika mtu ni SEHEMU ZAKE TU BAADHI au tu zile za siri , - kitu kisababisha BINADAMU huendelea kujikuta CHUMBANI yuko na Limtu LIZIMA.:-(
Katika fulani DINI,....
....kwa sadaka na MWENENDO labda MTUZ hujinunulia STAILI YA MAISHA kama IHESHIMIWAVYO NA BINADAMU badala ya kustukia havinunuliki VIKUZA IMANI vile vilainishavyo woga wa MUNGU MWEMA lakini ACHOMAYE VIUMBE alivyoviumba KATIKA wabadaye UZIMA.:-(
Swali:- Unafikiri KIBINADAMU ni rahisi kununua samaki bila shombo yake?
- Kwa BINADAMU unafikiri kuna anunuacho ambacho hakina makapi hasa ukifikiria hata katika chakula kitamu KILIWACHO ni asilimia ngapi huja na kile ambacho BAADAYE binadamu hukiita mavi?
Ndio,.......LABDA katika UDHAIFU WA KIBINADAMU huwezi kununua SAMAKI bila MIBA yake.:-(
Na NDIO,...
....labda kila BINADAMU anunuacho lazima kiwe KIKUBWA zaidi ya ahitajicho na akinunua GARI basi amenunua na matatizo YA GARI LAKE na akinunua CHAKULA kitamu basi HICHO lazima kije na uzito utakaogeuka mavi yake. .:-(
Swali:- AU?
Ndio,......labda katika kila kitu anunuacho BINADAMU ni KIKUBWA kuliko MAHITAJI YAKE,........na labda hata chupi inunuliwayo NA KIGOLI imezidi UKUBWA kama inaziba tako zima KAMA nia ya asili ya UTUMISHI WA CHUPI ili kuwa ni ili izibe matundu mawili tu YA SIRI ya KIGOLI yaliyo mbele na SEHEMUSEHEMU ZILE fulani katika ramani YA YALE makalio YAKE.:-(
Swali:- AU?
Ndio ,.......labda hata uendeayo SHULE ili ujisikie UMEELIMIKA yamezidi UKUBWA kuliko MAHITAJI YAKO ndio kisa katika MIA ya uyasomayo darasani labda ni moja KATIKA HAYO ambalo UKIKAA VIBAYA utakiona cha mtema kuni kikweli MAISHANI NA KUKIKUMBUKA UKIJUTIA kwa kuwa DARASANI hukuelewa hicho MAANA YAKE .:-(
.
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA !:-(
Au tu tumpate Ex Plantashun mwingine a.k.a 2FACE IDIBIA akija na Wyclef Jean katika ndude- Proud to be AFRICAN
Au tubaki tu hapahapa Nigeria Ex Plantashun Boiz 2FACE IDIBIA aje na R.Kelly waweke twist katika wimbo wa ya MAD COBRA katika -FLEX
Au tu MAD COBRA mwenyewe arudie classic -FLEX
-
UZURI wa HADITHI NZURI kwa TAKO ikiwa ni kwa kuwa ina stori mbaya kwa TAKO FULANI jingine!:-(
Posted: March 16, 2010, 1:42 pm by SIMON KITURURU
Misingi ya uzuri wa HADITHI NZURI kwa WATU hutofautiana,.....
... na kuna WENGI ili wanogewe na HADITHI basi HADITHI hiyo inahitaji kuwa na PANDE MBILI na moja ni ile yenye kuhakikisha USICHOKIPENDA au USIYEMPENDA stori HIYO inampa sifa MBAYA.:-(
Swali:- Si unakumbuka hata stori ya KIBANGA ampiga MKOLONI kwa waipendayo wengi ni kwa kuwa inapande mbili ile ya``KIBANGA´´ na ile ya ``MKOLONI´´ ,- na waipendayo hiyo stori hasa wamshangiliao ``KIBANGA`` ni kwa kuwa wanajua stori ina habari mbaya kwa ``MKOLONI´´?
- Si unakumbuka MOJA YA MISINGI ya stori za SUNGURA MJANJA na MWEREVU ili ziwe tamu huhitaji kumfanya FISI aonekane ZEZETA na anatabia mbaya?
Ndio,....... HADITHI NZURI za MUNGU hasa kwa wenye dhambi,....... zinaweza kuwa ni TAMU tu kwa washabiki wa MUNGU kwa kuwa kwa kawaida katika hadithi hizo MUNGU hushinda na UPANDE WA PILI WA HIZO HADITHI huwa zina stori zimpazo SHETANI sifa MBAYA.
Swali:- AU?
Ndio,...... kuna watu hata katika STORI IKUHUSUYO wewe na MTU MWINGINE ,......... ili STORI IWE TAMU watanogewa kama katika stori hiyo WEWE UNACHEMSHA, unapewa kibano au tu UNA SURA MBAYA kuliko huyo MWINGINE mwenye pua kama JIPU zuri.:-(
Swali:- Unafikiri kwa watu wengine ILI stori nzuri ya WAAFRIKA IFANE haihitaji kumgeuza adui YULE MWINGINE, yule MZUNGU, Mhindi au MUARABU?
- Si unajua ni kwanini kuna MA-HATERS duniani na ni kwanini inabidi stori NZURI ili iwanogee inabidi wachukue hatua mkononi na kusababisha stori nzuri ya CHUPI YAKO WAIHARIBU TU MAKUSUDI na kuitia UBAYA kwa madai unaipenda KWA KUWA mbele kidogo kwa chini imetoboka YOTE NI ili KUKUNUNISHA TU ujisikie VIBAYA?
....stori nzuri ya TAKO HILI zuri,.......labda imejengeka katika misingi ya kuwa apendaye stori hiyo ya tako,......NI KWA KUWA inamsaidia kujiaminishia TAKO LILE jingine asilolipenda ni BAYA.:-(
NIMEACHA!
Hebu twende NIGERIA tukutane na ex-Plantashun Boiz FAZE aongeleekuvunjika kwa kundi katika- Faze Alone
Au tubaki tu Nigeria FAZE aongee na mmoja wa ex-Plantashun Boiz 2FACE IDIBIA katika-
Letter to my Brother
-
ASILIMIA kubwa ya kitu watu waitacho SALAMU,....
Posted: March 15, 2010, 7:03 am by SIMON KITURURU
... labda sio SALAMU.:-(
Swali:- Wakati unasalimia mtu unauhakika na kitu ufanyacho zaidi ya kuamini tu UFANYACHO ni kusalimia?
- Unauhakika SALAMU ni nini ikiwa KUTIKISA KICHWA, kusonya, KUPIGA MAGOTI, kukonyeza na mpaka sentensi ; ``Shikamoo MWAAALIMU!´´na....,....``Sema wee Msenge!´´ kuna watu ni SALAMU?
NI WAZO TU hili MKUU!JUMATATU NJEMA! -
Wakati tunafikiria HISTORIA ya JINSI mtu anavyojifunza kuona AIBU kukaa uchi !
Posted: March 15, 2010, 6:14 am by SIMON KITURURU
[Tahadhari :WAZO limepinda na laweza lisikufunze kitu kama sio MFIKIRIAJI!:-(]
Mtu akizaliwa kwa taratibu huanza kujifunza,...
..... MPAKA nini kiko UCHI,....... na kwa kuigiliza hufikia mpaka kutafutia titi SIDILIA.
Mwalimu mkubwa katika swala LA KUFICHA PIA mtu ana-FUNZA,....
..... ni MACHO YA WATU na masura yao yageukavyo NAKUKUANGALIA VIBAYA wakati yanashuhudia unavyokatambuga huku miguu iko SAA TISA KASOROBO wakati sio riadha UNAKIMBIA.:-(
Macho ya watu hata kabla HUJAKEMEWA ubane miguu watu kwa bahati mbaya wasikuone NANIHII ndio yanafunza,....
..... kuwa kuna vitu onyesha MIJUSI na BATA lakini sio WATU kama heshima yako wataka kukuanayo ifanane na jinsi JAMII yako iaminicho ni heshima ukue vilivyo UKIISHIKILIA.:-(
Swali:- Lakini si unajua labda MACHONI mwa PAKA hakuna BINADAMU apendezaye UCHI?
- Si unakumbuka ulizaliwa uchi na labda ulisha wahi kumnyea mgeni pia BILA AIBUB ingawa hilo hukumbuki?
CHA kusikitisha ni kwamba,....
.....BINADAMU kimchekeshacho utotoni kutokana na udhaifu WAKUJIFUNZA ,........ mpe muda waweza kumkuta HUYOHUYO kimwana UKUBWANI kilekile eti kinamfanya ANALIA.:-(
Na LABDA binadamu badala ya kuona AIBU baada ya uchi KUJIFUNZA,.....
... angeweza kustukia katika MWILI wa binadamu labda UCHI ni kipengele ambacho ukijua KUKABILIANA NACHO kinakufundisha maisha kama hasa ukikumbuka kuwa UKIJISWAFI kipengele hutanuka na shughuli ya KUJISWAFI hata uchoke inahitaji kukumbukwa kwa KUACHA UVIVU kama wataka kipengele kivutie na wataka MWILI mzima usinuke hata kama nia sio watu wasistukie UNANUKIA.
Na baada ya hilo la uchi KUJIFUNZA,....
.... waweza kugundua wewe kama BINADAMU hata YAKO DHAMIRA au tu AKILI kama tu uchi unahitaji KUISWAFI mara kwa mara hata kama UNASIKIA UVIVU ili kuwa safi kama BINADAMU kiroho na KIMWILI na HASA kama wataka YAKUZINGUAYO uyatoke baruti na kuyapa MKIA.
Swali- AU?
Na kunauwezekano,...
....KUONEA aibu kitu ni kitendo cha KUJIFUNZA,........ na wote wachezao MUZIKI na nguo wakifuatilia HISTORIA YA WACHEZA MUZIKI wanaweza kugundua labda starehe halisi hata ya SINDIMBA ni kuicheza titi nje kwa kuwa labda vazi halisi la kuchezea muziki wala hata sio KIBWAYA bali ni kucheza uchi.:-(
Swali:- Si unakumbuka kunibishia RUKSA?
Lakini kuna waaminio kutokana na mafundisho ya DINI ZAO kuwa EVA yule demu wa ADAMU kama baadhi ya VITABU vya BAADHI YA DINI VIDAIVYO ndiye alianzisha mchezo wa kuona AIBU na kuficha uchi baada ya kula TUNDA alilopewa na MJANJA shetani ambalo alifanikiwa kumuonjesha ADAMU akasikia tamu ndio mpaka akajistukia yuko UCHI.
Na kama unaami HILO miye SIKUBISHII hasa kama umewahi KUFIKIRIA jinsi ulivyojifunza kuwa na AIBU kukaa UCHI na kufikia hitimisho ni kosa la EVA ndio sababu unaficha uchi.:-(
Na labda PIA ni kweli ,...
....katika HISTORIA fupi ya binadamu CHA KUSIKITISHA huwa inaambatanisha KUZALIWA uchi na mwisho kufa na kuoza mpaka uchi.:-(
SAMAHANI NAACHA WAZO MHESHIMIWA !:-(
Hebu tu PAPA WEMBA apoze shughuli NA KURUDISHA USTAARABU hapa KIJIWENI kwa ndude-YOLELE
Au tu tubaki hapahapa KONGO Papa WEMBA asawazishe shughuli kwa kitu- SHOW ME THE WAY
-
Tamu ya KUJIDANGANYA,.....
Posted: March 15, 2010, 4:37 am by SIMON KITURURU
.... inaweza KUSABABISHA kuwezesha kila UNACHOJISIKIA UKISEMA kukigeuza ni KWELI.:-(
Swali:- Si unajua INASEMEKANA ukirudiarudia kudanganya WATU KITU unaweza kuanza kukiamini mwenyewe HICHO KITU kuwa ni KWELI?
- Si unajua siri ya kukabili kutojisikia M-BAYA yenye mafanikio SANA inasemekana ni kujiaminisha mwenyewe KWA KUJIDANGANYA kila mara ukijiangalia kwenye kioo kuwa WEWE MZURI?
KUJIDANGANYA ni baabu kubwa,...... ndio maana kuna watu wengi INASEMEKANA wamefaulu mpaka KUFIKIA kuamini wataenda MBINGUNI kitu ambacho KWA MTU kunauwezekano kikawaida na KIUDHAIFU WA KIBINADAMU hawezi kufikia.:-(
Swali:- Unauhakika IMANI sio MBINU ya kumsaidia MTU KUJIDANGANYA ndio maana aaminiye N'GOMBE, mbuyu, YESU, BUDDHA, Kikwete, OBAMA , BIBI TITI, SHEKHE YAHYA , Simon KITURURU , HAWALA, BINAMU nyama ya HAMU, wote waaminicho kwa IMANI wanakigeuza UKWELI?
....kama wewe ni MTU kuna uwezekano hicho ndicho KIPIGACHO KELELE kuwa unaweza KUDANGANYWA .:-(
Kwanza kama utasifiwa leo kuwa UMEPENDEZA labda ni UONGO.:-(
NI WAZO TU HILI MKUU WA KITENGO!
Hebu twende MALI ili Mama Toumani alete mtekenyo uitwao- Niemogo
-
wakati mtu ANAHISI ANAKUJUA labda ndio huwa rahisi kukutukania KIPENGELE CHA SIRI shenzi!:-(
Posted: March 15, 2010, 4:26 am by SIMON KITURURU
KUHISI nishai kwa kuwa WATU,........huchanganya HISIA na ni nini ni KWELI.:-(
NA kwa kuwa kujua UKWELI ni shughuli na WATU ni wavivu kujishughulisha hasa na MAGUMU ya watu ,....... wapendayo kuyaamini kirahisi hutokana na HISIA tu na labda hasa zile zimuunganishazo mtu na MAMBO YA AJABU KIMPINDO au MAZURI KUPITA KIASI kama SIO MABAYA KUPITA KIASI yenye stori tamu ZITEKENYAZO HISIA KINAMNA ingawa hayana UKWELI.:-(
Swali:- Huwa unakumbuka kutofautisha unavyomuhisi ASKOFU au SHEKHE na halihalisi AMBAYO ndio ukweli ambao unaweza kuwa HUYO ni MWIZI na malaya kwa mbaaali kitu kisichokuwa na uhusiano na wadhifa wake wa DINI UUHESHIMUO ufanyao UMHISI na yeye vingine ?
- Si unakumbuka kama UNAHISI tendo hilo linatonya kuwa kuna kitu HUNA UHAKIKA kwa kuwa HUJADAKA MTU AKISHUGHULIKA na labda ndio kisa bado KUNA MTU hajamfukuza kazi hausigeli LEO ingawa anawasiwasi ni kiburudisho cha mmewe akiwa kazini?
- Unauhakika HUWA unajua UKWELI au hata uwaitao MAFISADI ni kwa HISIA tu ?
Na kwa KUHISI kuna wengi wanahukumu watu na VITU ,...
.... ingawa UKWELI wenyewe labda ni kweli BIKIRA Maria baada ya kujifungua alibakia bikira HATA KAMA hisia zako ZINAPINGA na TANZANIA kweli ina amani kama tu isivyo UKWELI.:-(
Swali:- Unabisha?
- Hivi hapa kwenye BLOGU huwa unahisi UNANIELEWA au unajua HUNIELEWI?
NDIO,....
....labda sio hisia zako tu,....... kuna uwezekano UKWELI wenyewe nilichoandika ni UJINGA hapa.:-(
Lakini SI UNAJUA kama unahisi una NJAA ,....
...kumbuka wewe hunanjaa KIKWELI kwa kuwa kwa kawaida MWENYE NJAA hujua na sio HUHISI kuwa ANA NJAA.:-(
NIMEACHA!:-(
Hebu twende ETHIOPIA ili TEDDY AFRO arudishe mambo mpwito kwa ndude- AYNE
Au tu TEDDY AFRO atulize manyanga kwa kitu-MUZIQA HIWETE
Au tusiondoke ETHIOPIA bila TEDDY AFRO kumwaga tena ndude-JAH
-
SANAA ya KUAHIRISHA ugomvi mpaka WAGENI WAONDOKE!
Posted: March 13, 2010, 6:27 pm by SIMON KITURURU
Ni sanaa kuutafutia UGOMVI muda na MAHALI pake,...
....NA labda uaminivyo MAJIRANI ZAKO daima WANAFURAHA ni kwa kuwa tu WANAPATIA kuahirisha MUDA WA ugomvi au tu hualikwi KATIKA sehemu yao MAALUMU wapendeleayo kutekenyea UGOMVI.
Swali:- Unabisha?
Kwa bahati MBAYA,...
....wakati unatembea na ugomvi KICHWANI unaweza mpaka ukawa mchoyo wa NANIHII kwa hata wasiohusika na UGOMVI wako na NANIHINO.
Na kwa bahati MBAYA,...
....ni sanaa kuahirisha UGOMVI mpaka wageni waondoke kwa kuwa yaweza kusababisha TOPIKI zote uongeazo na wageni zijae KUBARAGUZA tu na wala hazikuchokonoi KUMAANISHA kweli kuwa nanihiii ina.NANIHINO.:-(
Swali:- AU?
Na kwabahati MBAYA,...
.... labda kama WEWE unaweza kukaa MKAO wa kusubiri WAGENI waondoke ili UGOMVI uendelee yawezekana ndicho kipimo kikubwa kuhusu USTAARABU wako.:-(
Swali:- Unakumbuka sentensi ya kurudishia UGOMVI palepale ULIPOKUWEPO kabla WAGENI HAWAJAJA uitumiayo baada ya wageni kuondoka?
NIMEACHA hili wazo MHESHIMIWA na labda wala topiki haikuhusu na usikonde HASA kama hujawahi kuahirisha UGOMVI kwa kuwa SHEKHE na PADRI au TU uwaheshimuo pamoja na MAMA wamekuja kukutembelea.:-(
Hebu GEORGE MICHAEL abadili tena kwa -Careless Whispers
Au Elton John amuongelee tena -NIKITA
Na JIM REEVES akaribishe katika-Welcome to my WORLD
-
TATIZO la MJANJA akichumbia mtu AMUHISIYE ni MSHAMBA!:-(
Posted: March 13, 2010, 4:12 pm by SIMON KITURURU
Kirahisi MJANJA anaweza kujigeuza MWALIMU badala ya kuwa MPENZI kisa anahisi MAHUDUSHI -pangala wake ni MSHAMBA.:-(
Swali:- AU?
Ukihisiwa MSHAMBA waweza kujikuta unafundishwa mpaka unayojua,....
.... na wanaokufunza WAJIDHANIAO NI WAJANJA kusahau kujifunza KUONA MAMBO kwa jicho lako kitu ambacho chaweza kuwa ndio KITATUA tatizo.
Na tatizo la yeyote ajifikiriaye ni MJANJA na ndiye anayejua,.......LABDA ni kujipa UALIMU kitu ambacho chaweza kuwa ndicho tatizo.
Swali:- Unabisha?
Ndio kila siku ni SHULE,....... lakini kuna sababu kila mtu SHULENI huwa kuna MWALIMU amkumbukaye kwa UALIMU mzuri wa kusifika,.....
.... na labda MAISHANI ukichumbia MSHAMBA jaribu kuchanganua kama ni kweli hilo lakufanya UFUDHU kuwa MWALIMU na si mwanafunzi katika PENZI.:-(
Swali:- Hivi unafikiri UJANJA sio USHAMBA?
- Hivi USHAMBA ni nini vile?
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!
Hebu SIMBA WANYIKA katika kubadili wamwage ndude-SHILINGI YAUA tena ni MAUA
Au tu Buena Vista Social Club warudie tena pia - Chan Chan
-
Asante SHAHAWA,...
Posted: March 12, 2010, 6:00 am by SIMON KITURURU
...kwa kusababisha hata MAMBA MKALI kutaga MAYAI mbayo hayatakuwa VIZA kwa kukosa VIRUTUBISHO!:-(
Ndio,...
...kuna wasahauo KUMSHUKURU JOGOO na kushukuru TU kimiminika cha jogoo kimuingiacho KUKU kwa kuwa kimerutubisha MAYAI YA KUKU ili mayai YAPATE ujauzito yazae VIFARANGA kwa kuwa kimiminika cha JOGOO kilisaidia , ingawa JOGOO MWENYEWE ndiye aliye shikilia kiuno ambacho katika SHUGHULI ndio siri ya mafanikio ya mayai ya kuku kupata VIRUTUBISHO.:-(
Swali:- Si unajua kishukuriwacho MIMBA YA BATA IKIPATIKANA labda kimsaada wala sio kilichokuwa muhimu ZAIDI katika swala la BATA kupata mimba?
NDIO,......kwa bahati mbaya kuna WASHUKURUO kimiminika cha JOGOO na kumsahau KUKU na punje zake za kizazi ,...
... na katika hilo KUSAHAU bila KUKU hakuna kitakachototoleka kwa kuwa bila KUKU mwenye sehemu za ZA SIRI za kuingizwa kimiminika cha JOGOO MWENYE NYEGE ,... kile cha kuku chenye mchepuo wenye NANIIHII hakitajazwa mimba ambayo ili ijazwe ujanja,... UJANJA unahitaji KUKU NA MARINGO YAKE ili mayai yapate KIRUTUBISHO.:-(
Swali:- Unauhakika unapatia kulenga kihitajiwacho na ahitajiwaye KUSHUKURIWA?
- ASANTE zako unauhakika HUWA unashukuru kukatiwa kiuno au kisababishacho UWEZO wa kukata kiuno UWEPO uletao maana katika faraja zako?
- Ni mara ngapi kama wewe unaamini MUNGU umemshukuru MAJALIWA kwa kukuwezesha kupata nyege?
- SI unakumbuka labda sio MKULIMA aliyesababisha kulikuwa na chakula ulichokula leo?
NAKATIZA WAZO!:-(
ASANTE kwa yote WEYE na WOTE lakini,....... kwa kuwa labda naandika huu UjingaBUSARA kwakuwa LABDA NAHISI KUNA mtu anasoma!:-(
NIMEACHA na samahani kwa kupindisha WAZO na kwa matumizi ya LUGHA ambayo kwa MHESHIMIWA asiye ita BELESHI -beleshi ni NYOKO!:-(
IJUMAA na WIKIENDI NJEMA Mheshimiwa !
Au NGOJEA tubadili na twende kusikiliza ya MUNGU kikiristo kwa kupata wimbo mwanana kutoka kwa ROSE MUHANDO akitonya ndude-Mungu Wangu nitakushukuru
Au Zain Bhikha atonye kwa mkao wa KIISLAMU katika -A is for Allah
Na MAKASSY arudishe KITU NYUTRO nilivyo katika ndude -MAMBO BADO
-
KAMA unakumbuka BUSARA YA ulichofundishwa SHULE YA VIDUDU!:-(
Posted: March 12, 2010, 5:59 am by SIMON KITURURU
Labda ,......SHULE ya kuishi na WATU KATIKA MAISHA ulishaIMALIZA kwa ULIYOJIFUNZA shule ya VIDUDU a.k.a CHEKECHEA.:-(
Swali:- Unakumbuka CHEKECHEA wanafundishwa nini hata kama wewe hukuenda hizo shule ziitwazo za VIDUDU?
TWAWEZA KUJIKUMBUSHA lakini kuwa busara za chekechea hazina maringo katika KUTEKENYA UMUHIMU kwa kuwa ukiwa chekechea UTAFUNZWA yaleyale ya muhimu sana MAISHANI kama:- KABLA ya kula OSHA mikono
- UKIMALIZA kula osha MIKONO
- KABLA ya kuvuka barabara angalia pande zote uhakikishe hakuna gari
- KABLA ya kunya vua chupi na usinye pembeni ya choo
- UKIMALIZA kunya chamba na osha mikono
- USIMFINYE mwenzio
- KUJAMBA mbele za wenzio ni tabia MBAYA
- USIMUIBIE penseli, peremende AU KARANGA mwenzio
- KAMA unaumwa sema
- Waheshimu BABA na MAMA
- Na kama.....NA kadhalika kadhaa za nk...
SWALI- Umeanza kukumbuka MAFUNDISHO hayo?
- Unafikiri ukifuata hayo tu uwezi kula BINGO maishani hasa ukikumbuka digirii zako huruka somo la USIMFINYE MWENZIO?
NAACHA!
Lakini ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Lakini LABDA endelea nami KUSIKILIZA HAWA ambao wasemacho kama umefundwa weye utaendelea tu kuwa MHESHIMIWA hata wakati uwasikilizao ni DAS EFX kama tu enzi zile za ndude -ALRIGHT
AU Fu-Schnickens waendelee tu na wajanja wajuao hizi ndude wakiri kama wanajua nani ni - True Fuschnick
AU tu MAD LION abadili kidogo lakini AACHIE mchezo uleule katika -REAL TING
-
Kikubwa kifikiriwacho CHOONI,....
Posted: March 11, 2010, 8:10 pm by SIMON KITURURU
...kwa kawaida sio kile KIFANYIKACHO chooni.
Ndio,........kuna uwezekano ufanyacho chooni ULIKIFIKIRIA kabla hujaingia chooni.:-(
NI HILO tu na NI WAZO TU lisilo na uhusiano na CHOO Mheshimiwa!:-(
Ngojea KARAMA REGESU na MSONDO NGOMA wabadili kwa ndude -Nimebadilika Nini?
Au tu tena Jill Scott arudie ambavyo KIDUME angependa kukumbukwa katika ndude -CROSS My MIND
-
Ilivyo sura ya MAJUNGU KABLA hujapigwa MAJUNGU yanayokorokochoa KUNAKO!
Posted: March 11, 2010, 7:45 pm by SIMON KITURURU
Vitu vingi KUHUSU WEWE vinasemwa kila siku,....
..... na waweza kuvidharau kama VISEMWAVYO kivitendo havikuathiri na KISAIKOLOJIA uko ngangari kukabili ya watu maoni.
Na katika vinavyosemwa kila siku,....
..... vyaweza kuwa NI AMBAVYO UNAWEZA KUVIPUUZIA lakini yote hayo ni kwa kuwa ni VYA AINA zile zile ambazo UMEZOEA kusikiaWAKWARE WAKiPIGANIA mpaka kuchaniana chupi na gwaguro na ndio siri YAKO ya kujiandaa kuzoea na KUVIPUUZIA na labda umeshashiriki pia KATIKA KUTATUA mishemishe hiyo ISIYOKUGUSA ya aina hiyo kwa wahusika kuwapa VIDONGE VYAO angalau kwa maoni.
Swali:- Lakini si inasemekana ni kweli KABLA hujalogwa UCHAWI ni porojo?
- Na si inajulikana kila MTU ukimjulia huhitaji FIMBO kumpa adhabu?
Kila mtu ,....
.... ana kaudhaifu kake na kuna MWENYE SURA MBAYA ambaye watu wamezoea kumtukania SURA kitu alichozoea NA KIRAHISI ANAKIPUUZIA ,....
....wakati udhaifu wake uko kwenye MATEGE YA MIGUU ambayo bado hajazoea kutaniwa hasa kwa kuwa alikua NA KUKUZWA afikiri anabonge la USAFIRI na hilo lilifanikiwa mpaka alivyopenda MTU na huyo mtu akamuacha akimwambia hawezi kuwa na kishtobe MWENYE MATEGE na mwendo kama MJUSI mjamzito.:-(
Kila mtu,....
...... ana kaudhaifu kake na kuna adhaniwaye ni JASIRI KWA YOTE na MAJUNGU karibu yote yale ya kuwa yeye MWIZI , malaya, ANA kibiongo , NI JIRANI MBAYA kwa kuwa ni kweli anajambaovyo ananguvu za kukabili na ANAYAPUUZIA,...
.... lakini haki yanani akipigwa MAJUNGU yamuhusianishayo na kuwa yeye MCHAWI anakuwa kaguswa KIPELE cha UDHAIFU kwa kuwa hata yeye mwenye labda alihisi BABU YAKE alikuwa MCHAWI na maishani mpaka kilichomfanya KAOKOKA au tu kuwa MSWAHILINA , yote ni katika kuhakikishia UMATI kuwa yeye ni BONGE LA MTU MZURI na sio MCHAWI na kwa kumpiga MAJUNGU kuhusu uchawi kitu kihusianishwacho na kabila lake ambalo KAMODIFAI JINA usilistukie kabila lake , KWAKE unakuwa kama UNAFANYA watu wageuke kwa KWAKO kumpiga teke HADHARANI mjamzito.:-(
Swali:- Hujawahi kushuhudia jasiri wa kutania dini za wengine siku akisikia dini yake inatukaniwa au AKISIKIA tu stori za kujambiwa kwa kitabu aaminicho ni kitakatifu katika DINI yake ?
Ndio,....
.....KABLA hujalogwa labda stori za UCHAWI ni porojo,...
....NA kabla HUJABAGULIWA labda ubaguzi wa rangi ni porojo.:-(
Na kila mtu ana kaudhaifu kake,.......
....kama ni MWANAMKE usidanganyike ,...
....DUNIANI hakuna tako LAINI labda ndio maana MWANAMKE kwa MWANAMKE wakibwengana KATIKA KUTAFUTIANA MAUMIVU hushuhudii tako likilengwa kama vile NYWELE ZIVUTWAVYO na kikubwa husikii ugomvi wa wanawake ukosao matusi na kelele za maneno kwa kuwa UDHAIFU wa mwanamke ili kuuchokonoa vizuri MAUMIVU wahitaji kutumia neno .
Swali:- AU?
Kila mtu ana kaudhaifu kake,...
.... na kumbuka kwenye MWILI wa mwenye mijinguvu kama SIMBA ,...kwa kawaida kama ni DUME lazima kuna maeneo yenye KORODANI au MAKENDE laini na yenye kusikilizia MAUMIVU VIZURI tu hata kabla hujasema neno.:-(
Swali:- AU?
Na kama HUJAPIGWA majungu yakakuingia vizuri ,....... labda tu ZAMU yako bado na wakupigao MAJUNGU kuna kitu hawajui kuhusu WEYE.:-(
Na inaweza kuwa KIMAJUNGU KIMGUSACHO umjuaye kwa kuwa na mpenzi MWANANA WA JINSIA TOFAUTI yaweza kuwa ni kigumu kukibuni kwa kuwa HUAMINI kwake KIUDHAIFU BENDERA yake ni HUYO MPENZI MWANANA ALIYENAYE na ukweli ni kuwa BAFUNI akioga anamichezo yakujichezea mwenyewe KUNAKO ili KUTUNZA NGUVU za kutunzia siri yake kuwa anahusudu watu WA JINSIA YAKE,....
......na kamwe hastuki kwa yale majungu yaliyo MTAANI WATU WALIYO YAVALIA NJUGA kuwa eti yeye FISADI na anapata MITOTO MIZURI zaidi MTAANI kwakuwa anahonga hela za SHIRIKA.:-(
Kwa kifupi,...
...MAJUNGU kuna yanayowasaidia kitu ambacho WAPIGA MAJUNGU hawajastukia.:-(
Samahani NAACHA !Ila kumbuka HILI ni wazo tu MHESHIMIWA!:-(
Hebu Touré KUNDA arudishe USTAARABU hapa kijiweni DUH!
Aje kwanza na kitu-WAAR
Au tu Touré KUNDA amalizie na ndude-Wadini
Au tujifunze tu KUWA misosi ipo
-
MAHARAGE ni yaleyale YA JANA lakini si kila siku yana UTAMU ULEULE wa jana.:-(
Posted: March 10, 2010, 5:09 pm by SIMON KITURURU
UTAMU wa kitu ni tafsiri tu ya UBONGO,..........ulavyo maharage yaleyale si lazima unasikia UTAMU uleule.:-(
Na utamu wa MAHARAGE yaleyale waweza kuathiriwa na hali ya ULIMI wenye vionjo vipelekavyo umbea kuwa umekula tena maharage kwenye UBONGO,...
.... kwa hiyo labda KUNA SIKU usipounga maharage na UKIUNGA maharage HAKUNA TOFAUTI YA UTAMU na utamu uusikiliziao huwa ni MAZOEA TU yaleyale kuwa kwa kuwa maharage yana rangi ILEILE basi utamu wa matako yake ni uleule .:-(
Swali:- Si unakumbuka utamu wa hata PENZI lilelile NI KEMIKALI mwilini zitafsiriwazo na UBONGO na laweza sababisha penzi la juzi na jana la mpenzi huyohuyo kutofautiana makali ya usikiliziavyo ya chachandu ya penzi?
- Kwani HUSTUKII kama leo umekula chakula kile kile ulicho kula jana kunatofauti ya utamu?
Utamu ni michezo ya UBONGO,........ kama una njaa ya kutosha ,.......LABDA huo sio wakati wa kuamua UNAUHAKIKA na UTAMU wa kitu kwa kuwa MKAO wa UBONGO WAKO WAKATI UNA NJAA waweza kusababisha nyama ya KUNGURU kiutamu KWAKO ifanane na ya KUKU.:-(
Swali:- Unabisha?
Kwa bahati mbaya ,........WAKATI UNASIKIA TAMU ,........ukichunguza aina ya utamu nyuma yake KUNA SABABU.:-(
NI WAZO TU HILI MKUU!
Hebu tudeku porojo kuhusu UBONGO
Au HEBU tu GEORGE CLINTON na THE P FUNK ALLSTARS warudie- Atomic DOG
Au HEBU tu turudi tena ALGERIA ili CHEB KHALED alainishe kidogo kwa-DIDI
-
DOZI ndogondogo ZAKUMKUMBUSHA MWANAWANE wakati anaringia yake TAALUMA!:-(
Posted: March 10, 2010, 1:45 pm by SIMON KITURURU
Kuna wasahauo kuna WASUKUMA MKOKOTENI ambao,...
.... HAWAKUPATA tu bahati kusomea URUBANI lakini akili za kupaisha ndege wanazo.
Na kuna VIGOLI ambao,...... hawakujifunza tu TAALUMA YA UCHAWI lakini ukileta za kuleta uwezo wakujifunza KULOGA wanazo.
Na kuna MASISTA na MAPADRI ambao,........ WITO umefanya wapunguze BAADHI ya matumizi ya utupu na kibonyezo ambavyo WALIOOA na... au tu MALAYA wanaweza KUBOBEA na KURINGIA katika tumizi fulani , LAKINI ikumbukwe nguvu ya tumizi la HIVYO VIDUDE halafu wakatubu baadaye MASISTA na MAPADRE wasiooa AU kuolewa wanazo.:-(
Swali:- SI unajua KUJUA KITU na KUFANYA KITU vyote huhitaji nafasi ya kujua na MAHALI na muda wa kufanya kitu, KITU AMBACHO cha weza kufanya ambaye angekuwa INJINIA WA MELI kawa fundi bomba?
- SI unakumbuka KUJUA kitu ni nishai na MWANAFUNZI anaweza kumzidi MWALIMU katika kujua hicho kitu?
- Unauhakika ni wewe mwenyewe ndio uwezaye kuelewa kitu au ni mazingira tu ndio yawezayo kukufanya WEWE ndio uwe mwenye taaluma ya kitu?
LAKINI,....
...labda ,...... ni bahati tu kuwa na TAALUMA ambayo wengine hawana ingawa labda kuna mwenye KICHWA ZAIDI cha hiyo taaluma ambaye anaringiwa na mwenye TAALUMA.:-(
Swali katokori:- Hivi inawezekana KURINGA kwa dozi ndogo ndogo ni AFYA ndio maana binadamu anakipaji hicho au KURINGA ni kama tu nywelenywele NDEFU ZAKIKWAPA au zile za chini kidogo ya kitovu cha MKUBWA ambazo shughuli zake na umuhimu wake KUUJUA ni mpaka PROFESA fulani afanyie uchunguzi?
NI TAFAKURI tu HII MHESHIMIWA ambayo waweza kujikumbusha wakati unamnyolishia mtu TAALUMA YAKO na wala usikonde!SI unapata MSHAHARA?
NIMEACHA!:-(
Hebu tubadili kwa kuhudhuria harusi na vifijo WAKATI mdada akichukua mdada jumlajumla
Au tu twende KENYA kukutana na CANNIBAL na SHARAMA waongelee-KICHWA KIBOVU
Au tu tubaki TZ JHIKOMAN arudie ndude-MAPENZI
Au tu twende ALGERIA Khaled Hadj Brahim a.k.a Cheb Khaled aendeleze kwa -AICHA
-
SHULE POPOTE!
Posted: March 9, 2010, 4:14 pm by SIMON KITURURU
FUNZO la leo la KUJALI WENGINE halitoki kwenye kitabu kitakatifu bali latoka kwa DJ!
DJ mzuri ,........daima ni YULE alengaye ile kitu WASHABIKI WAKE na wamsikilizao wanajali NA kupenda ,......... na DAIMA hang'ang'anii kupiga miziki aipendayo yeye BINAFSI kwa kuwa ndio aipendayo .
Swali:- Unafikiri hakuna cha kujifunza katika hilo?
NI WAZO TU la HARAKA HARAKA Mheshimiwa !
Hebu tu Juliana Kanyomozi na Bushoke warudie- USIENDE MBALI
Au tu PROFESA J aulize tena -Hapo VIPI?
Profesa J na FEROOZ aendelee pia na -NIKUSAIDIAJE?
-
Kama humjui MLEVI ni uzembe KUWA NA UHAKIKA unajua anafanyanini BAA!
Posted: March 9, 2010, 3:24 pm by SIMON KITURURU
Kumbuka tu kuna WATU wako KANISANI kutafuta NYUMBA NDOGO na wala sio KUSALI kama WEWE au kama IFIKIRIWAVYO.
Na kuna walio BAA kazini na kazi yao ni USHUSHUSHU na wala sio kuuza BAA kama IFIKIRIWAVYO.:-(
Swali:- Unabisha?
NI kweli,......KAMA humjui MTU ni uzembe KUWA NA UHAKIKA unajua anafikiria NINI wakati unashuhudia anafanya NANIHINO mahali upafikiriapo na kupaunganisha na NANILIU.
Swali:- SI unakumbuka kila aendaye kazini HOSIPITALINI sio lazima ni NESI au DAKITARI?
- Unafikiri kila aliyeko CHOONI anajisaidia huko?
NI HILO TU!
Hebu tujikumbushe THE FRESH Prince
Mystic Revealers waongelee mtazamo wao katika- Religion
Na ma YOUTUBE STARS warudie -We are the WORLD
-
Tatizo la CHA sasa hivi ,...umuhimu wake KUUELEWA baadaye!
Posted: March 8, 2010, 8:49 pm by SIMON KITURURU
KIWEZEKANACHO kueleweka sasa hivi,.......... labda JARIBU KUKIELEWA hata kama huoni TUMIZI LAKE SASA HIVI kwa kuwa CHAWEZA kuwa kina msaada kwako BAADAYE!
Labda jifunze CHOCHOTE uwezacho kujifunza sasa hivi,....
.... kwa kuwa kama BINADAMU moja ya siri ya waliofanikiwa ni KUWA KWAO TAYARI KUKABILI TUKIO wakati TUKIO LINAJITOKEZA na hatujui nini kitatukabili ambacho tunakidharau sasa hivi ambacho ndio kitatatua ya BAADAYE.:-(
Na kuwa kwako tayari SASA hivi,........ kwa kawaida ni matunda ya kujifunza kabla ya tukio ulikabililo SASA HIVI ambalo kuna muda TAALUMA uitumiayo isingeonekana kipindi hicho kama ingekuwa na tumizi kwako BAADAYE .
Swali:- Ushawahi kukwepa kujua kitu ingawa uko katika MAZINGIRA ambayo yanaruhusu uwezo wa kujua kitu kwa kuwa tu huoni kitakusaidia NINI?
Haki ya nani kama uko CHINA jifunze Kichina na kama unakaa na mpika VITUMBUA jifunze kupika vitumbua kwa kuwa huwezi kujua lini uhitajicho katika kutatua kikusumbuacho ni kitu ambacho ungeweza kuwa unakijua tayari kama ungekipa shavu.
Swala hili linajidhihirisha kwangu mara kwa mara hasa tokea nilipostukia yale mambo yangu ya kuendekeza UTOTO WA MWISHO yaliponitokea puani kwa kujikuta naondoka NYUMBANI sijawahi kufua wala KUPIKA kisawasawa halafu niko mwenyewe na pesa za kimada ambaye PENZI LILE la kupenda mtu ili akufulie na KUKUPIKIA pesa sikuwanazo.:-(
Swali:- Si unajua kuna vijeba madhumuni ya kuoa ni kutafuta MPISHI , mfuaji na trekta mtu?
TUNAKUMBUSHANA TU hili MKUU lililonipitia MUKICHWA LEO baada ya kukosa ULAJI mnono ULIOHITAJI kitu ambacho ningeweza kukijua tokea MOROGORO SEKONDARI O'level MIAKA HIYO kama kisingekuwa kinaoanishwa na MASOMO ya WASICHANA ambayo kwetu VIDUME ENZI HIZO ilikuwa ni UJIKO kukwepa .:-(
Tubadili MSHAWASHA kwa kuwasikiliza I-Threes
Rita Marley aulize - Who colt the game
Marcia Griffiths alainishe tena kwa -Tell Me Now
Au tu RITA MARLEY arudie- One DRAW [Tahadhari: Maudhui ya wimbo yamepinda kama unamisimamo fulani:-( ]
Na Judy Mowatt amalizie kwa kumzungumzia- Black Woman
-
MPENZI nasogeza sikio UNIDANGANYE vizuri wakati unanichekea!:-(
Posted: March 8, 2010, 5:03 am by SIMON KITURURU
Kabla sijaanza,....
Swali:- Unafikiri ni kweli nahitaji kuambiwa UKWELI kila siku katika kutunza FARAJA zangu?
MAISHA ni mafupi na moja ya tumizi la muda KWA BAHATI MBAYA ni kuishi na UKWELI unaouma,...
.... kwa hiyo labda usinishangae nikiombea KUDANGANYWA.:-(
Lakini kwa kuwa umejifunza UONGO NDIO unaouma ,...
....unaweza kuamua kuishi kwa kuchunguza TARALILA AKUPAZO MPENZI kwa kuwa katika MAISHA YAKO MAFUPI NA MTU tamu UNATAKA IWE NI tamu kama katika HADITHI na kwa kuwa umefunzwa kuchukia UONGO tafiti zako zinaathiri usikiliziavyo KUDANGANYWA kitu kifanyacho KUDANGANYWA ijae uongo wenye bonge la misuli hasa kwa kuwa NI KITU ULICHOJIFUNZA KUKIKWEPA kwa kuambiwa UONGO NDIO UNANG'ATA na ukiusikilizia maumivu unauma,....
... kitu ambacho chaweza kuwa kimekuandaa na KUKUSAIDIA KUZIDI KUNISHANGAA nikidai naombea KUDANGANYWA.:-(
Swali:- Si unakumbuka UONGO na UKWELI labda vinanguvu sawa katika kutonesha KIDONDA kama unakidonda kitoneshekacho chenye kuleta maumivu?
- Na si unakumbuka moja ya shughuli ya WAZAZI ni KUDANGANYA WATOTO ingawa ni kwa kisingizio kuwa ni bado WATOTO na ukweli ni kuwa hawahitaji kujua kuwa MSHAHARA HAUTOSHI kwa hiyo kunabaadhi ya mambo huwanunulii kwa kuwadanganya na kwa hiyo HUO ni UKWELI ambao hawahitaji kuujua katika faraja zao za KITOTO?
Kwa hiyo MPENZI,........ nidanganye unanipenda SURA na sio PESA,......... na wakati UNANIDANGANYA usisahau kunichekea.:-(
MPENZI,...
....nidanganye UNASURA nzuri na LABDA usinistue kuwa UKWENI ni kwamba unasura kama PWEZA na wanidaka kwa sura nikuonayonayo HARUSINI kwa kuwa tu imenyunyiziwa rojo zihitajizo PESA,...
... na wakati unanidanganya HILO usilie MACHOZI yawezayo loanisha ungaunga usoni mwako na kwa hilo LABDA jaribu kunichekea.:-(
Swali:- Si unajua LABDA unadanganywa leo WEYE MHESHIMIWA MWENYE MIAKILI ndio kisa bado UNACHEKELEA?
Ndio,........ kama unaamini katika UKWELI ,....... ni kweli LABDA uongo nao unanafasi yake MAISHANI MWAKO katika kukuchagulia lini UTANUNA.:-(
Na ni KWELI,.......unaweza kuchagua kuchekelea porojo HATA CHUMBANI na sio tu KIJIWENI kama unajua JAMAA LINADANGANYA,.......badala ya KUNUNA.:-(
NI wazo tu HILI MKUBWA na usikonde!
Ngojea SHIHAN abadili tena kwa ndude- SICK & TIRED
Au hebu tumpate tena Maestro DEKULA KAHANGA VUMBI katika -Bamakonde
Au tu MAKASSY arudie ndude- MAMBO BADO
-
WAKATI unaongea na MLEVI na unafikiri kunauwezekano ni POMBE inaongea!:-(
Posted: March 7, 2010, 10:13 pm by SIMON KITURURU
KAMA wewe ni MSIKILIZAJI,...... kunauwezekano umeshamsikiliza MTU na kustukia kalewa DINI.:-(
Na tatizo hujitokeza tu kama weye MSIKILIZAJI,....
.... kwa kustukia kama huamini YESU kuna MSOMI utakaye kujua mawazo yake LAKINI hoja zake zote zisizo na uhusiano na DINI zinahitaji NUKUU za MWOKOZI YESU alisema nini katika mtongozo wa hoja hata za UMASIKINI wa MAMA NTILIE kimwana ASHURA wa karibu na soko la bwimbwi lenye MBILIMBI na halihitaji BUSARA zitokazo katika vitabu vya DINI.:-(
Swali:- Unauhakika umewahi kuongea na MTU ambaye hajalewa KITU?
- Unauhakika aongeaye ni wewe ikiwa uongeacho chahitaji unukuu BUDDHA alisemaje ili tuelewe stori zako za kungarisha UTU UZURI za hitaji midabwada?
ILA kwa bahati NZURI,.......wakati unaongea na MLEVI unaweza pia kupata JIBU LA TATIZO LAKO la jinsi ya KUBINYA JIPU kama weye ni MSIKILIZAJI,...
..... kwa kuwa pamoja na uongeaye naye kwako kufikiri KALEWA anaweza pia akawa NDIYE MWENYE JIBU zuri zaidi lihusianalo na JIPU hasa kwakuwa aweza akawa yeye ndiye MTAALAMU WA MAJIPU.
Swali:- Si unakumbuka kama hujui kupika MAANDAZI unaweza usiwe unajua siri ya SHAVU NYORORO LA ANDAZI ingawa HUJALEWA na si unajua kuwa MLEVI anaweza akawa ndiye ajuaye VITUMBUA vinapikwaje?
- Wakati unalalamikia walevi UNAUHAKIKA wasiolewa umewasikiliza kwa asilimia kubwa HUWA wanaongea nini?
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu LL COOL J abadili kwa KUPINDISHA aina za KIBUSARA kwa kitu-I'm That Type Of Guy
LL Cool J aendelee kwa ndude - Hush
Au tu LL Cool J amalizie na AMERIE kwa ndude- Paradise
-
Ingawa ni MKOJO wako LABDA kunasababu unachagua CHAKUKIKOJOLEA!
Posted: March 7, 2010, 9:48 pm by SIMON KITURURU
Kila kitu na mahali pake,......... na katika eneno KIUTU hata mavi huchaguliwa mahali pake.
Na kirahisi waweza kusahau kuwa KANISA SAFI lenye WAUMINI WASAFI moja ya siri ya WAKE USAFI ni lilihitaji choo pia KISICHO NA UHUSIANO NA DINI kisaidiacho walopendeza na KUNUKIA VIZURI waendelee kunukia vizuri NDANI YA KANISA kwa kuwa KINYESI CHAO kina mahali pake,...
Na kirahisi waweza kusahau kizuri kama DINI ndicho kikukumbushacho UNA DHAMBI na kukata makali ya utamu wa DHAMBI na katika USIKILIZIAVYO TAMU na kugeuza janja ya kidude ni ujinga kwenye UJINGA mahali pake,.....
Kabla sijasitisha WAZO hili banangenge,....
Swali:- Si unakumbuka SHILINGI ina pande mbili wakati unaitumia kununulia KIDUDE kimoja?
- Na si unakumbuka MAVI katika HISTORIA YAKE AMBAYO SIO NYINGINE yaliwahi kuwa CHAKULA kitamu?
Ndio,........ LABDA,.......... kuna sababu MKOJO wako mwenyewe unauchagulia JIWE na sio kitanda chako katika FARAJA YAKO ya kuukojoa.:-(
Na yawezekana mpaka HASIRA ZAKO labda ukifikiria VIZURI utastukia huwa kuna WATU UWACHAGUAO wakuwatolea MIKIKI YA HASIRA hasa kwa kuwa kama tu ulivyochagua KUTOLIA CHAKULA CHOONI kuna ambao UMEWACHAGUA waendelee kuamini wewe kwa kuwa PADRI basi INALIPA UKIENDELEA kutoonyesha zako hasira KWA kujulikana MPOLE ingawa wote twajua kama ni BINADAMU wahitaji dozi kadhaa za kukasirika na UNA HASIRA ULIZOZICHAGULIA MAHALI PAKE kwa kuwa kuna wageni ,...
.....kama huna kilema.:-(
Swali:- AU?
- Unafikiri kama una dhambi hakuna sehemu ulioichagua ambayo kirahisi unajisikia huru ZAIDI kurudia DHAMBI?
NI WAZO TU HILI MKUU na ni ruksa KULIBISHIA huku umetoa macho!
Hebu Sean Paul + Rihanna warudie- Break it OFF
Au tu Sean Paul na Blu Cantrell wabadili tu kwa -BREATH
Au tu Lady Saw na Beenie Man wabadili zaidi kwa -Healing
DAIMA nikipata muda huwa nipo na WADAU.....
-
MTU na KITU kichezacho karibu na AJISIKIAVYO VIZURI!
Posted: March 5, 2010, 4:04 pm by SIMON KITURURU
Aina yako ya KUJISIKIA VIZURI,.......... kama vile tu ilivyo uchaguavyo ni nini TAMU yawezekana staili zake UMEJIFUNZA tu.
Swali:- Si unakumbuka KUJISIKIA VIZURI baada ya kuangalia MPIRA wa miguu unahitaji UJIFUNZE kwanza ujue MPIRA WA MIGUU ndio nini na utamu wa BIA kuna walioona chungu kwanza kabla ya kufudhu KIFUNDISHO na kugeuza utamu uleule wa KILAJI kuwa ni MTAMU?
.....KUJISIKIA VIZURI ,...
..... ni bonge la sayansi NA USIPOANGALIA inawezekana UMESHAJIFUNZA NA KUKOMALIA kutaka UPATE KITU au MTU ndio ujisikie vizuri kuwa ni kweli UNAISHI na hauko hai tu.
Swali:- Unauhakika KUJISIKIA KWAKO VIZURI hakutegemei upate kitu hata chakijinga kama vile PETE?
Na ukichunguza waweza kugundua kabla ya kutaka uwe na KITU kama GARI zuri , CHUPI NZURI , baiskeli ngangari au tu NYUMBA NZURI ili UJISIKIE VIZURI,....
... ulianza kufanya mazoezi ya KUTAKA VITU ili UJISIKIE VIZURI kuanzia ULIPOZALIWA tu kwa kustukia ili UJISIKIE VIZURI ulihitaji KITU NYONYO la MAMA, halafu ukaelekea kwenye KULILIA kitu PEREMENDE ili UJISIKIE VIZURI , mpaka ukahamishia kuhitaji kitu - RABA MTONI aka LA KUCHUMPA , yote IKIWA ni katika kuendelea kuhitaji KITU katika shughuli nzima ya kujaribu kila siku KUPATA KITU ili ujisikie vizuri na hatimaye KUJISIKIA KWAKO VIZURI kunaweza kuwa SASA HIVI kunahitaji kilazima KITU FULANI tu ili angalau UJISIKIE VIZURI kiduchu tu.:-(
Swali:- AU?
Kama unabisha,.... ...jiangalie tu KUMOYO hali halisi kama ILIVYO ,.........waweza kugundua KUJISIKIA KWAKO VIZURI labda kunahitaji GARI ZURI leo ingawa HATA kwa hilo umejifunza GARI ni nini KWANZA hasa kwa kuwa KWENU sio maporini ambako bomba la HAIWEY ni UCHOCHORO,....
... na KUJISIKIA KWAKO VIZURI kwa kuwa una bonge la NYUMBA nzuri HUKO KWENU kumetokana na jinsi gani KABILA LENU siku hizi HAMHAMIHAMI kutafuta mihogo a.k.a MSOSI kila wiki kichaka cha pori la jirani nyingine , AU TU hamuhitaji tena kuhamahama ili kutafuta PAKUCHUNGIA MBUZI wa MAHARI na WALE ng'ombe zenu wa KISUSIO ambao ndio KITU ambacho kilikuwa kinawaletea KUJISIKIA VIZURI kabla yakugundua nyumba yenye choo cha ndani.:-(
Swali:- Unadhani hakuna kaukweli katika hilo na nimezidisha CHUMVI kwenye porojo?
Ndio ,....... ni kawaida kwa baadhi ya watu kuoanisha VITU na jinsi wajisikiavyo VIZURI, kitu kisababishacho watu kutafuta msaada mpaka wa kujinunulia vitu MURUA kama :- Raba la Kuchumpa
- Kitabu cha Juma na Rosa chenye bonge la jalada
- Bonge la CHUPI
- Isiyoya miti NYUMBA
- BAISKELI
- TOROLI na bonge la BELESHI jipya
- Bonge la Kibajaji
- GARI MOSHI kwa kuwa BENZI halikutoshi tena siku hizi
- nk. kadhaa wa kadhaa...
....NA WAPO pia wahitajio WATU WENGINE au tu DINI katika harakati zao za KUJARIBU kufanikisha KUJISIKIA KWAO VIZURI.
MIYE naamini kila MTU kivyake katika kusaka KUJISIKIA VIZURI ,...
...na LABDA vyote vinamsaada ikiwa tu UNAJIJUA UDHAIFU wako na katika KUVIBANJUA VIKUNAVYO UDHAIFU WAKO huumizi kwa makusudi watu WENGINE,....
... kwa kuwa WAJUA swala la KUJISIKIA VIZURI lilivyo NYOKO wanaojijua wanajua kuwa kuna watibuo TATIZO hilohilo lao BAA kwa kitu CHA BAA ambalo kwa mwingine dawa yake KATIKA KUCHOKONOA ni lazima SWALA aliendee KANISANI au MSIKITINI.
Swali:- Si unajua kuna watu kibao aka BWELELE ambao WAKO kwenye dini zao kwa sababu ya kutibu swala hili tu la KUJISIKIA VIZURI na wala huwa hawawazii kuogopa JEHANAMU kama wewe ndio kisa HASA wako MSIKITINI au KANISANI?
Ni kweli ,....
...ili kujisikia vizuri kuna watu WANAJIKATA a.k.a JICHINJA maeneo damu itoke wafarijike na KUJISIKIA VIZURI.
Lakini pia ,..
...UHAKIKA wa utambuaji wako wa UJISIKIAVYO VIZURI waweza kukuokoa KUNUNULIA SWALA GARI wakati kikunacho UJISIKIAVYO VIZURI ni BAISKELI na BWANA wa nje akunaye na kujazia majibu ya UDADISI wako wa nje ya ndoa KUNANI ambacho chamfanya MMEO asiache kuonja nje.:-(
Kumbuka tu,......... ni uungwana lakini kama wakati unajitafutia KUJISIKIA VIZURI basi cheza kwa stepu ,.......USIKANYAGE WENZIO.
Swali katokori:- Unajiasikia VIZURI lakini leo au unahitaji kitu kikune MSHAWASHA?
- Umewahi kufikiria ni nini siri ya KUJISIKIA KWAKO vizuri?
NIMEACHA wazo hili nyoko MHESHIMIWA na jaribu tu kukumbuka HILI ni wazo tu MKUU!
IJUMAA na WIKIENDI NJEMA!
Tupoze tu kwa kupata tena SINDIMBA kidogo kutoka kwa FIRST LADY, sasa tutafanyaje.:-(
Au tu DIANA ROSS na MICHAEL JACKSON warudie ndude-Upside down
-
UHUSIANO wa kosa LA PILI na misingi ya KOSA LA KWANZA la mtu.
Posted: March 5, 2010, 6:16 am by SIMON KITURURU
Kunauwezekano MAKOSA YA MTU yana UNDUGU,...... wa zaidi ya kuwa ayaunganishayo kindugu ni huyohuyo MMOJA mtu.:-(
Na kosa lile la TATU,.........linaweza kuwa limetokana na MISINGI ileile ya kosa la KWANZA.:-(
Swali:- Umewahi kufikiria MAISHANI MWAKO ni lipi lilikuwa kosa lako la kwanza?
- Unauhakika makosa yako hayana undugu?
- Unauhakika kosa la leo utalistukia kabla ya la kesho?
Ndio,...
...kosa la MTU la KUMI ,........ linaweza kuwa na uhusiano na lile la NNE ambalo lilitokana na misingi ya kosa LAKE la PILI.:-(
Ni wazo tu HILI MHESHIMIWA na wala usikonde!
Hebu ABETI MASIKINI abadilishe kwa kurudia ndude- AZIZA
Au tu Pepe Kalle arudishe kitu-Moyibi
-
DUNIANI- katika KUFIKIRIA YA YULE anayechaguliwa KUKUMBUKWA na WANADUNIA!:-(
Posted: March 4, 2010, 8:28 pm by SIMON KITURURU
[Tahadhari : Wazo limenuna a.k.a HALICHEKELEI kanyau!:-(]
Binadamu wanaweza kuchagua kumkumbuka MTU kwa SURA NZURI,...
....hata kama SURA ya mtu huyohuyo WAIPENDELEAYO KUIKUMBUKA ni sura ya kwenye PICHA za UJANANI wakati KIGOLI hajavunja ungo na bado anasura ya mduara nyeusi na KATIKA MASWALA ya uzuri hajachonga kidevu kama Michael Jackson na pia kuanza kujichubua.
Ndio,.........kuna waamuao kukukumbuka kwa MAZURI,........ kama vile kwa kuficha MABAYA katika KUMBUKUMBU yanageuza ukweli kuwa KIJEBA kuna muda na mengi tu alikuwa anatibua.
Swali:- Kwani hujastukia hata waliowahi kuwa wapenzi kuamua wakumbukalo ni yale tu mabaya katika penzi lao ambayo yamesababisha katika ndoa WAMEACHANA?
- Si unakumbuka kumbukumbu zilivyo nyoko kiasi kwamba labda MSIBA WA MWAKA JUZI kuna mtu KIRAHISI ambaye kasahau aliyefariki ALIKUWA ni nani lakini anakumbuka MENYU aka MSOSI na charanga zake ,- kuwa pilau lilikuwa lina bonge za nyama ya nguvu, MAJI YAKUNAWA YALIKUWA MACHAFU na kachumbari haikuwa ya kutosha?
- Unafikiri ni nini kinakujengea ukumbukayo?
Katika MARAISI wa Tanzania,......... na haki ya nani idadi yao ni KIDUCHU,........lakini kirahisi kuna ambaye kama sio NYERERE inahitaji ufikirie ni nini alichofanya usichokikumbuka ambacho NACHO hushindwa kukukumbusha jina lake na wahitaji msaada wa GOOGLE SEARCH ili KUMKUMBUKA.:-(
Ndio,...
...katika DUNIA kuna VIONGOZI wengi,......... lakini labda ni SADDAM HUSEIN na sio WAZIRI MKUU Sir John MAJOR wala MSUYA katika ambao kirahisi unawakumbuka.
Na taka usitake kuna NDUGU zako,....
...... ambao huwakumbuki hata wakati unajaribu NDUGU kuwakumbuka!:-(
Swali:- AU?
- Unauhakika KATIKA NDUGU ni asilimia ngapi ya NDUGU ZAKO ambao kwa jina unawakumbuka?
- Si unajua inaweza ikawa mtihani mkubwa kwa yeyote yule ukimuuliza akutajie jina la Mjomba wa BABU yake ukizingatia tayari shangazi ya BIBI na shoga zake waliokuwa wanacheza kujipikilisha kwa wengi kuwafahamu haileti maana?:-(
Labda MTU huchagua anaowakumbuka,........ na kunauwezekano KATIKA BINADAMU kwa asilimia kubwa ya watu mwisho wa kukumbukwa ni KIZAZI CHA WAJUKUU ZAO tu ambao kuna kitu kuhusu wao wanakikumbuka.:-(
Ndio,....... na kwa UMKUMBUKAYE labda unachagua cha kukumbuka,......... na KIRAHISI baada ya muda unaweza kukuta NELSON MANDELA anakumbukwa kwa mazuri tu ingawa amekiri mwenyewe alishawahi hata kuiba udogoni na NYERERE atakumbukwa kwa yote MAZURI wakati kwa SADDAM HUSSEIN na IDDI AMINI yaweza kuwa ni rahisi kukumbukwa kwa MABAYA TU ingawa taka usitake kuna MAZURI tu lukuki waliyowahi kufanya pia.:-(
Swali:- Unafikiri kwa kawaida ni mambo ya aina ngapi huwa Marehemu yoyote umjuaye huwa unakumbuka wakati unajua MTU kama MTU ana mengi ndani ya MAISHA kitu kifanyacho umjuaye kama MWIZI haki ya nani kuna mtu kwake huyo ni BABA tu MPENDWA ambaye anahakikisha familia yake haifi njaa?
- Unafikiri utakumbukwa na vizazi vingapi , kwa lipi na KWANI unamaindi hilo?
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA na wala USIKONDE!
Hebu twende tena Angola Carlos Burity arudie - Ojala Yeya
Au tupitie tu na CONGO Papa WEMBA arudie ndude-Awa Yo Okeyi
-
Labda ni JAMII NA MAZINGIRA YAKO tu ndiyo SIRI YA urefu wa UONYESHAVYO MASIKITIKO YAKO.:-(
Posted: March 4, 2010, 6:58 pm by SIMON KITURURU
[Tahadhari: Wazo limenuna!:-(]
Katika juhudi za MAISHANI kufupisha HUZUNI,........uonekanavyo UNAHUZUNI yaweza kuwa ndio moja ya yatafriwayo kuhusu wewe ni MTU wa namna gani.:-(
Lakini kwa BAHATI MBAYA yaweza pia kuwa kuna walazimikao KUCHEKELEA ya huzuni HADHARANI ,..........kwa kuwa tu JAMII inafikiri kikutiacho huzuni hakifai kuonewa HUZUNI.:-(
Swali:- Unafikiri wakati MTU kamalizia KUWA NA HUZUNI waweza kuwa ni MIONGONI MWA WAMFANYAO inabidi aongezee MAPOZI TU ya HUZUNI ili asijeonekana MTU mbaya na MAJIRANI?
KUHUSU kuhangaikia urefu wa KUONEKANA una- MASIKITIKO na katika juhudi za kufupisha za mtu HUZUNI,....
.....waweza kusababisha MTU achanganyikiwe hata MSIBANI kwa kuwa tu mategemeo ya JAMII yanataka alie wakati labda STAILI YAKE yakukabili mambo na HUZUNI haihitaji MTU ALIE MUDA HUO na yahitaji awe pekee ili kisahihi AHUZUNIKE na wala sio HADHARANI hata kama marehemu na ya marehemu HAYAJUI yanamgusaje NA kutokana na ukweli pia kuwa MAREHEMU alivyokuwa hai kutokuwa chochote muhimu kwa MTU MHUSIKA kwa hiyo ni vigumu kuitafutia mkao wa masikitiko na kujua AHUZUNIKE WAPI kinamna gani.:-(
KUHUZUNIKA hasa sehemu ambazo utahitaji michango ya watu ya MSIBA ni SANAA pia. :-(
Swali:- AU?
Na kwa bahati mbaya,....... kuna WAHITAJIO KUKUONEA HURUMA ambao huweza kulazimisha asiye na MASIKITIKO kuonekana mnyonge na mwenye MASIKITIKO kwa kuwa HURUMA YAO inatokana na wao kujijengea,....
... MAZINGIRA ambayo yanahitaji kama unahitaji HURUMA na huduma ZAO sharti tu uonekane katika MUDA FULANI una HUZUNI.:-(
Ndio ,...... wapo watu ambao JAMII IMEWAFUNDA kuonisha utiavyo HURUMA KIMUONEKANO ndio sawa na jinsi UNAVYOHUZUNIKA na kwa kurefusha muonekano KUWA UNAMASIKITIKO basi wewe ndio kweli MTU MZURI na umepata pigo kweli kitu ambacho huwapa faraja ya KUKUHUZUNIKIA KWA KUTO KUSUASUA kisawasawa katika hata yasiyowahusu sana wao KIHUZUNI.:-(
Swali:- Si unakumbuka kwa aliyefiwa KUCHEKELEA Msibani sio kithibitisho aliyefiwa hana HUZUNI?
- Unafikiri kwa mwenye FURAHA ni lazima ahakikishiye wengine kuwa ni mwenye FURAHA?
Ndio,.......LABDA.........ni MAZINGIRA tu na jamii ikuzungukayo AMBAVYO ni SIRI ya uonyeshavyo FURAHA YAKO,....
... INGAWA wajua akenuaye meno kwa kicheko,....
.... BADO sio ushahidi kuwa ACHEKAYE na kusababisha wengine nao WACHEKE PIA kuwa ni kweli ni MWENYE FURAHA.:-(
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!
Hebu Mbongeni Ngema abadili hali ya hewa hapa KIJIWENi kwa - Woza my fohloza
Au tu Mahlathini arudie- Kazet
Au tu tudie ya matumaini tu kutoka kwa SARAFINA kuwa pamoja na yote -FREEDOM is COMING
-
Kwa kuwa kunauwezekano MWIZI hajisiki ni MWIZI wakati anaiba!:-(
Posted: March 2, 2010, 4:36 pm by SIMON KITURURU
Kwa bahati mbaya,....... UWEZO WA KUNYA hauhakikishii MNYAJI kuwa wakati anakunya ANAJISIKIA anakunya:-(
Kabla sijaanza,....
Swali:- Unafikiri umjuaye kuwa ni MALAYA huwa ni kweli anajisikia MALAYA wakati anafanya umalaya?
Ndio,....... kuna uwezekano MJINGA hajisikii anafanya ujinga ,....... ndio maana LABDA ufanyikaji wa YAKIJINGA kwa kawaida ni rahisi.:-(
Ndio,....
.....YAFANYIKAYO Iringa,...... labda ni yaleyale ya DAR-es SALAAM kama hayaoanishwi na IRINGA kwa kuwa KIMPUMU au tu KONYAGI ileweshayo ni ileile ,...
...na kama UKILEWA HUFANYA UJINGA waweza kurudia ujinga uleule uliofanya SUMBAWANGA ukiwa KIBAHA kirahisi.
Swali:- Si unajua KUUA MTU ni rahisi kwa baadhi ya watu kama wafikiriacho WAKATI WANAUA MTU sio KUUA ila ni kwamba wanampiga tu MWIZI?
Ndio,....
.....kuna uwezekano unachofanya sasa hivi unakifanikisha kwa kuwa hujisikii na KUONANISHA wewe ULIVYO na WEWE UFANYACHO,...
... ndio maana kirahisi unaweza kuwa mahiri katika KAZI YAKO ya UZIBUA CHOO wakati unajisikia VYEMA TU kuwa wewe ni bonge la MKURUGENZI hasa kwa kuwa choo usafishacho ni cha IKULU nasio cha STENDI na jina la cheo chako ni AFISA USAFI.:-(
NI WAZO TU HILI Mheshimiwa na nimeliacha!
AU?
Hebu DOROTHY MASUKA abadili hali ya hewa kwa kitu- IMALI YAMI
DOROTHY MASUKA aendeleze kwa ndude-Kwa Nhingirikiri
Au hebu tu DOROTHY MASUKA arudie pia ndude- TEYA TEYA
-
BUSARA za kukwepa WENYE TABIA mbaya!:-(
Posted: March 1, 2010, 7:38 am by SIMON KITURURU
Kumbuka tu,.......UIMARA wa TABIA YAKO NZURI,......yaweza KUWA inahitaji UWEPO wa wenye TABIA MBAYA.:-(
Swali:- Unafikiri UNAUHAKIKA unamjua BINADAMU YEYOTE ambaye unauhakika KUWA hana sebene ifanikiwayo kueleweka nawe usiyemlokole KUWA NI tabia mbaya?
TABIA NZURI ya mtoto wa MNOKO uijuayo ,....... labda ni kwa kuwa WEWE ulilazimika tu KUJUA ni nini katika TAFSIRI ZA MASHUJAA WA TABIA NZURI ni nini katika tabia ,......DAWATI la wajanja wenye tabia LINA PIA tabia MBAYA .:-(
Ndio,...
... hata sura nzuri huhitaji unatafsirije sura MBAYA.:-(
NI HILO TU Mheshimiwa na hili NI WAZO TU MKUU!:-(
Hebu pata mshawasha wenye busara wa...
Au hebu COCOA TEA abadili kwa kutenga wadogo kwa ndude-18 and over
Blah blah blah
Fish cakes
Alas a fish cake.
Yet more fish cakes
Guess what ... yeah ... fish cakes.
The end of the fish cakes