SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • MTOTO MZURI labda JAMBA tu usiahirishe,...

    Posted: February 27, 2010, 7:20 pm by SIMON KITURURU
    .... kwa kuwa  kama umewahi KUBANWA na kijambo,......... wajua  JUHUDI  na  JEURI za waliobanwa kijambo WASIOJAMBA HADHARANI  sana sana ni za kusogeza MUDA tu  WAKUJAMBA iliusisikie wakijamba  ,....... na AFYA YA KIJAMBO  CHAO kwa bahati mbaya bado huwa iko PALEPALE.:-(

    Na MTOTO MZURI  labda   NI BUSARA PIA  kijambo usilazimishe,...
    ....kwa kuwa ALAZIMISHAYE KUJAMBA  anaweza akafanikiwa KUHARISHA PIA juu ya kijambo hasa KWA KUWA  nukta ya kutolea uharisho NI ILEILE ambayo ukizidisha JUHUDI hewa itaongezewa CHEMBECHEMBE NA ROJO  katika MTOKO  utumiao tobo   ambalo wengi hutambua kuwa  HUWA linanunia shughuli  sehemu mbali mbali lakini katika tundu lililopo  PALEPALE.:-(


    Swali:
    • Unafikiri kwa kuahirisha UJUACHO utafanya WATU WENGINE wasipokuwepo kuna badili kuwa utakachofanya ni KILEKILE?


    • Unafikiri ukidokoa MBOGA bila kuonekana  kitendo chako hugeuka kuwa NI kuonja MBOGA?


    NDIO,...... moja ya BUSARA za BINADAMU ni kuficha  vitu vijulikanavyo SIO SIRI na  kuwageuza wavifanyao HADHARANI mahawayani ingawa LABDA uhawayani WENYEWE WENYE TAKO KUBWA  ni ule   UTU na HESHIMA ZA MTU   zenye misingi  ijengwayo kwa kuwa tu NI HESHIMA eti MJUACHO ANAFANYA kafanya SIRI.:-(



    NIMEACHA!

    Tahadhari: MHESHIMIWA  hii taralila HAINA uhusiano na KUJAMBA!:-(

    Hebu tubadili wazo HASA kwa kuwa kwenye taralila isiyona uhusiano na KUJAMBA inaneno JAMBA  lisilo la HESHIMA kwa  BAADHI YA WAUNGWANA WAJAMBAO  kwa kuwaachia En Vogue wadai- My Lovin' (Never Gonna Get It)



    Salt N Pepa wazungumzie - Shoop




    Au tu NAUGHTY by NATURE warudie tu.- FEEL me FLOW

  • Kwa kuwa , ...KUWA na DHAMBI ni tofauti na JINSI ya kujisikia una DHAMBI!

    Posted: February 27, 2010, 5:28 pm by SIMON KITURURU
    [ Tahadhari: JIHADHARI na WAZO hasa kama ULIVYO na unavyojisikia UNAFIKIRI  ni sawasawa!:-(]


    Kuna UWEZEKANO  kabisaaa...
    ...kuwa  MASIKINI ni tajiri kama hujamfundisha MHUSIKA  jinsi ya kuusikilizia UMASIKINI!:-(


    MATATIZO ya UMASIKINI ni MATATIZO tu kawaida  ,...... na LABDA mpaka uyaoanishe tu na UMASIKINI ndio matatizo AMBAYO NI MATATIZO kutokunya KIKAWAIDA kwenye jedwali la MATATIZO  kuna ambayo utayaambatanisha na  SEKSHENI a.k.a kipengele cha MATATIZO yaletwayo na kibano cha UMASIKINI na kuyafanya kuwa MATATIZO HAYO ni MATATIZO YA UMASIKINI.:-(


    Samahani,....
    ..... nimekumbuka , NIA na MADHUMUNI  ya taralila hii ni kuongelea DHAMBI.:-(


    DHAMBI ,...
    ....ni FIKIRA aliyokuwanayo MTU  hasa baada ya TENDO,...
    .... kwa kuwa DHAMBI inaweza ikawa ni TENDO LA NDOA  kabla HUJAFIKIRIA na kulioanisha kifikira na UZINZI.:-(

    Kwahiyo ;...
    ...DHAMBI usiishangae kama  ni  tamu!


    Na labda unajua  hata kama naheshimu kwamba HUTAKIRI,...
    ....  wala DHAMBI  hainauhusiano na UCHUNGU ingawa KIFIKIRA neno dhambi linamchezo wakufanya hata utamu wa ULICHODOKOA  ufikiriacho ni KISAFI  KIFISADI katika TAMU yake  YA MSHIKAKI  ukahisi KWAKE kunyunyiziwa chembechembe za kamasi la MPIGA CHAFYA ambalo husababisha utamu wa peremende usikilizwa kwa mikwaruzo ya ujuaji labda moja ya ifanyayo PEREMENDE tamu ni kamasi.:-(!


    Swali:
    • AU?



    Ndio,.......DHAMBI ingekuwa MCHICHA,.......kuna watu tungejaza TENGA!:-(

    Ila kwa jinsi DHAMBiI ilivyokuwa NYOKO,...
    .... ahubiriye DHAMBI mara karibu zote ndiye aliyekuwa na TAFSIRI FULANI  ya uhakika kwake YA DHAMBI ,.......kitu kifanyacho awe miongoni mwa WATU ambao kwa uhakika wanajua wafanyavyo ni DHAMBI.:-(



    Ndio ,...
    ...jinsi yako YA  kufanya DHAMBI  yaweza kuathiriwa na STAILI yako ya  unavyoisikilizia DHAMBI.
    Na kwa kuifikiria dhambi,...waweza kustukia  katika  dunia ya WENYE DHAMBI, watu wengi wanakustukia WEYE ni MWENYE DHAMBI kwa kuwa tu  NI KWELI  katika wafunikao kwa GWAGURO ,......WEYE unaikalia uchi na kuionyesha masharubu ya chini  DHAMBI .:-(


    Tukiacha MZAHA ;....Swali:

    • Unauhakika DHAMBI ni nini?
    • Unafikiri UMASIKINI USIKILIZIWAVYO kama tu DHAMBI  , unauhakika MASIKINI ni muda gani  HUWA anajisikia MASIKINI?
    • Unauhakika TAJIRI anajisikia tajiri wakati anakunya?
    • Unafikiri wewe kama ni MKRISTO ambaye  kwako ruksa ni kuonjeshwa kidude kimoja tu NA MKE WAKO  WA NDOA huwa unaelewaje na KUIGEUZA NI DHAMBI   ya MUISLAMU ambaye kwake SIO DHAMBI ,- ile ya KUONJESHWA VIDUDE VINNE  kutoka kwa WAKE WANNE WA NDOA  awawezao kuwapa huduma WAJISIKIE NI WAKE WA MTU  wapatao matekenyo yote ya NDOA   kwa maadili  ya KIISLAMU?
    • Unafikiri dhambi yako ya UZINZI  inafanana na dhambi ufikiriayo ni  HIYO HIYO kwa mwingine YULE aliyedakwa UGONI na wewe ambaye hafikirii kama WEWE?

    • Unafikiri kuna MTU anajisikia ana DHAMBI kama alivyo na DHAMBI?


    NI HILO TU!JARIBU TU  kukumbuka  ni TAFAKURI tu hii  MHESHIMIWA  na KUNAUWEZEKANO  kama WAZO HILI  limevalishwa chupi , basi chupi INATOBO!:-(

    Hebu ANDREW SAMUEL alainishe na kubadili HALI YA HEWA KIJIWENI kwa ndude-Pinacolada



    Maxi Priest abadili zaidi kwa ndude-Close to U



    Au tu MAXI Priest amalizie tu kwa ndude-Just a little bit longer

  • WAKATI kunauwezekano UFIKIRIACHO ni FIKIRA tu!:-(

    Posted: February 27, 2010, 5:12 am by SIMON KITURURU

    NDIO,...... ..labda kuna WATU unafikiri,.......wanakufikiria UNAVYOFIKIRIA unavyofikiriwa.:-(


    Swali:

    • Lakini unafikiri WATU wanakufikiriaje WEYE?

    Ndio,...
    ....kuna PADRI katika fikira haoanishwi na NYEGE  YA DHAMBI,....
    .....kwa kuwa  ni kweli ndani ya siku yake HUHUSIANISHWA  na mtekenyo ulazimishao baadhi ya watu WACHUMBIE malaya ambaye NI KWELI afanyacho kwa kawaida ndani ya siku SIO DHAMBI wala UMALAYA.:-(

    Swali:
    • Unafikiri MALAYA afanyacho ni UMALAYA  siku nzima?
    • Si unakumbuka wewe sio UNAVYOFIKIRIWA kwa kuwa kitu halisi sio FIKIRA?



    NIMEACHA tafakuri hii!Kumbuka hili ni WAZO TU   MKUU na labda  si AJABU  kujaribu KUPATA POINTI ya hoja YAKE  MHESHIMIWA!:-(

    Hebu Macy Gray abadili kwa -I TRY




    Au tu Corinne Bailey Rae abadili kidogo zaidi kwa -I'd Like To


Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs