SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • JINSI ya KUJIFUNZA kukitaka kidude ULICHONACHO!

    Posted: February 23, 2010, 2:57 pm by SIMON KITURURU
    Tatizo ni:

    ... WATU WENGI hufikiri  ILI WAWE NA FURAHA,...... wanahitaji WASICHONACHO,...

    .. wakati WALIVYONAVYO hawana hata MUDA  WAKUVIFIKIRIA kwa kuwa WAKO BIZE wanahangaikia WASIVYONAVYO.:-(



    MTU alichonacho tayari ,....
    ... kinaweza kirahisi kuwa NDICHO MUHIMU ZAIDI MAISHANI kuliko chochote ASICHONACHO ambacho kinamtoa raha kwa  jinsi tu ANAVYOHENYA kupigania KUKIPATA.


    NA usichonacho,......... hicho HUNA na labda huna nafasi yakukifikiria  na kujua kitakavyokupoza ROHO ukilinganisha na AMBACHO unacho TAYARI.:-(

    Swali:
    • Unafikiri umeshajifunza KUFURAHIA kikojoleo chako kabla ya KUTAKA  na kile kikojoleo  cha MWENZIO usichonacho?

    • Kwani  umeshajifunza KUHESHIMU elimu yako ya SHULE YA MSINGI ULIYONAYO TAYARI iliyokusaidia kujua kusoma na kuandika kabla ya KUJIKOSESHA FURAHA kwa kufikiria inahitajika  uende CHUO KIKUU au UWE PROFESA ili ufurahie KUELIMIKA?


    KUMBUKA,....... kunauwezekano MKUBWA,....... ukijifunza KUKITAKA na KUHESHIMU ulichonacho TAYARI,...

    .... unaweza kustukia WALA huhitaji cha ZAIDI kingine ili  MAMBO YAKO yawe DUKINAA,....
    .... kwa kuwa kuridhika hakuna uhusiano na ni kiasi gani UMEJILUNDIKIA ndude .:-(
    Swali:
    • AU?
    • Si unajua hata uelimike vipi utakufa wakati kunakitu HUJUI?
    • Unafikiri maishani mwako  UMEFANIKIWA kujifunza kuendelea   KUKITAKA ulichonacho?




    ...kabla sijaacha ngojea nibonge ung'eng'e kwa kudai,...
    .....FIKIRIA kwa kuwa labda ;...- ``HAPPINESS IS NOT what YOU WANT;.... its WANTING what YOU HAVE!´´.:-(

    NIMEACHA!
    SIKU NJEMA Mheshimiwa!

    Au tu ISASHA abadili tu kabisa kwa ndude-Don't U know?



    Au tu Dr Remmy arudie -NDUMILA KUWILI

  • TUKIACHANA na DUNIA tuishiyo SASA ambayo WENYE NGUVU ndio walindwao na MABODIGADI !:-(

    Posted: February 23, 2010, 10:49 am by SIMON KITURURU
    [TAHADHARI : Taralila HII  imelalia mtazamo wa KIUME ZAIDI  katika kugusia na kulishikashika SWALA!:-(]



    Hadithi Hadithi!
    Hapo zamani za kale kulikuwa na WENYE MABAVU na WANYONGE,......ingawa kwa kawaida ilikuwa WENYE MABAVU ndio wanalinda WANYONGE.
    Na ilikuwa ni jambo la kujivunia kweli  kama NJEMBA bode lako a.k.a MWILI lina mamisuli ya KIKULIMA na sio KITAMBI , kwa kuwa  WEYE USIYE na KITAMBI  ulijulikana unaweza kulima PUNDA KASINGIZIWA na kwa hilo tu  MADEMU warembo wa kijijini walikuwa hawakawii kukuchekea KISIMANI  na kukuchungulia ukienda kuoga MTONI ,wakati  ndoto zote zao hata zile za  wakati TU ndio wanavunjavunja  UNGO  zilikuwa zina DONDOO mpaka za  unavyonukia vizuri KIKWAPA CHA NGUVU  kwa jinsi  tu ulivyo na juhudi SHAMBANI.

     NGUVU ilikuwa inamaanisha NGUVU kweli na kama wewe KIDUME unalegalega a.k.a UMELEGEALEGEA   , wazee wazima  walihakikisha hutoki JANDONI  kwa hata kudai uliliwa na simba huko; kitu ambacho Wapare walidai umemezwa na MSHITU. JANDO lilikufunza  sehemu ya MWANAMKE na jinsi ya kumshungulikia apate kirahisi mbele yako kujisikia MWANAMKE.
    Na hapo zamani za kale  mwenye akili alikuwa ni yule ajaliye famili  na jamii yake. Mwenye akili alihakikisha familia na jamii yake INAPATA MSOSI , inalindwa, ina nyumba ambayo umejenga kwa nguvu zako MWENYEWE , na angalau kila mtu aliyepita UMRI WA KUCHEZA UCHI  WA KITOTO a.k.a kila aliyekaribia kuanza kuota  NYWELENYWELE KUNAKO umehakikisha  kavaa vazi la kisasa KIJIJINI  ; ambalo la weza kuwa ni chupi ya MKEKA au tu ile CHUPI ya  ngozi itokanayo na MNYAMA  uliye mdaka kazubaa msituni MWENYEWE , ambaye kitoweo chake  kingine bado kimekaushwa kwa moshi jikoni juu ya jiko la kuni.

    Hapo zamani za kale , ukishajulikana unamiguvu ya kutosha na umetahiriwa safi au tu KUFUNDWA VIZURI  kama unatoka katika  jamii yenu ishabikiayo  magovi, BADO NI WAZAZI  ambao walihangaikia swala la kukupatia  POOZEO LAKO  la maisha  a.k.a  kukutafutia MZAZI MWENZAKO.
    Na binti mzuri alikuwa SIO  yule mwenye bomba la tako au tu chuchu ya kutosha , kwa kuwa ilibidi kwanza WAZAZI wafanye utafiti kuangalia MASWALA YA FAMILIA YA KIGOLI ,  kama yale ya  UKOO wa  Kimwana MNONO mlengwa KUWA hawana KIFAFA kwao  , BIBI YAKE  hana UKOMA au tu  kama UCHAWI  KWAO  haupandi vizuri.

    Kwa hiyo MTOTO mzuri aliyenona kabisa  waliweza kumstukia DNA yake  ni ya KICHAWI  KABLA HUJADAKA KIMWANA , na  kwa  hilo ukastukia VIJANA BOMBA  wanukao kikwapa cha kutosha kukuhakikishia ni wakulima safi WAMEFUNGA BREKI ZA MATAMANIO na wakawa wana Mruka KIMWANA  MZURI  mwenye macho ya gololi, mashavu ya KUMIMINA, tako mtikisiko ´´SINGIDA-Dodoma´´,  kwa kuwa tu kwao  MAMA YAKE MKUBWA anakifafa na aliwahikuzaa MAPACHA kitu ambacho kwenye MILA zenu ni NUKSI..:-(

    Swali:
    • SI kunauwezekano MWENYE NGUVU siku hizi siye yule alindaye wengine, ila ni YULE alindwaye aepukane na wanyonge na  ASKARI?
    • Si mwenye nguvu siku hizi ni yule MWENYE PESA?
    • Si mwenye akili sikuhizi ni yule AJILIMBIKIZIAYE MALI wakati wengine hawana  , aliaye  katika ofisi ya UMMA mali za UMMA , na unaweza kumtambua KIRAHISI kwa kuwa kwa kawaida yuko katika KUNDI ambalo huitwa MHESHIMIWA?

    • Si Msichana  aonekanaye Mzuri siku hizi Tanzania ujazo wa TAKO  kipimo chake kimepunguzwa ingawa titi saa sita bado lakubalika?

    • Na si unajua kwa wadada  LIMJAMAA lao WALILENGALO au WALITEGEMEALO sasa hivi kwa kuwa ni jizi kwa kukusaini tu MAKARATASI   na lina MIPESA KEDEKEDE hapo zamani kuna uwezekano wangekufa -NALO kwa njaa?

    • Si unakumbuka PIA hapo zamani bonge la demu lazima linuke KIKWAPA vya kutosha ili KIJIJINI NJEMBAZ na WAZAZI WENU mjue ni bonge la mfanyakazi na likiingia shambani hilo ni BONGE la  TREKTA na  lafaa kuwa MKE?

    NDIO,........HAPO ZAMANI kulikuwa na MABAYA na MAZURI kama SASA HIVI.:-(
    Swali:
    • Unafikiri kizazi cha SASA hivi kimejifunza ni yapi MAZURI ya zamani yafaayo kutunza na ni yapi hayafai kuyang'ang'ania kwa kuwa tu bado yana tamu zake sasa hivi  kwa baadhi ya watu?


    Hapo zamani,...
    ...... kulikuwa na TAMU zake lakini pia  usisahau MABAYA kwa kuwa tu unajuakubonga UNG'ENG'E siku hizi na kamsemo ka ``OLD is GOLD ´´ umeshakakariri na KUKAAMINI kuwa NI KWELI TUPU.:-(
    Hapo zamani labda UNGEKEKETWA usikiliziacho tamu  wewe ,OOOHO  wee  SHAURI YAKO!


    Hapo zamani  kabla ya watu kuanza kuwa na NGUO na VIATU vya JUMAPILI au IDI ungekuwa unabonge la chupi la NGOZI au MKEKA wewe, Ohoo wee  SHAURI YAKO ! 

    Halafu HEBU LIONE VILE,...
    ....eti siku hizi linaturingia na chupi lake  la GUCCI na wala sio la KITENGE.:-(





    Tukiachana na mzaha,....Swali:
    • Unafikiri siku hizi si WENYE MABAVU ndio walindwao na MGAMBO , POLISI , MAHAKAMA  na mpaka JESHI wakati wanyonge hawana Mlinzi?
    • Na siku hizi si mpaka WIZI ni shughuli ya  asifiwaye kwa MIAKILI?


    Na katika HITIMISHO la hii HADITHI HADITHI,........ napenda kukukumbusha Mheshimiwa kuwa HIVI SASA bado kuna WENYE MABAVU na WANYONGE  ingwa labda kuna ukweli kuwa siku hizi mambo yote ni  MNYONGE  MNYONGENI na HAKI ZAKE CHUKUENI na sio MNYONGE MNYONGENI lakini HAKI zake MPENI.:-(

    NI HILO TU na ni Mwisho wa HADITHI HII!
    KUMBUKA TU,  NI  wazo tu HILI MKUU!



    Hebu Ringo Madlingozi na Oliver Mtukudzi wabadili kwa kurudia  kitu-Into Yami




    Au tu Sipho Hotstix Mabuse arudie tu -Shikisha


Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs