SIMON KITURURU- MAWAZONI
-
UJUMBE MZURI ni kama UGALI,saa nyingine ni MPAKA uwe na MBOGA tamu ya kusukumizia TONGE ndio kitaeleweka!:-(
Posted: February 22, 2010, 1:19 pm by SIMON KITURURU
UJUMBE MZURI labda hautoshi kwa kuwa tu ni UJUMBE MZURI,...... ukizingatia walengwao wanaweza wasiupokee USIPOSINDIKIZWA na kulainishwa na NJIA ambazo walengwa hawafikirii ni MBAYA.:-(
Swali:- Si unajua kuna watu bila TAARABU mahubiri yako YENYE UJUMBE MZURI WA BUSARA kuhusu mapenzi hawatayaelewa?
UJUMBE MZURI ,..
....kwa kawaida hausikilizwi kwenye WIMBO MBAYA.:-(
Na kuna wengi WASIKILIZAO matusi vizuri,...
... ambao ni UJUMBE WASIOUPENDA kwa kuwa tu wanapenda mrindimo wa muziki AMBAO KWAO ni wenye UJUMBE MBAYA .:-(
Ndio,.......kuna wamsikilizao pia MTU vizuri ,....... kisa WANALAZIMIKA kuwa watulivu nakusikiliza KWA KUWA wanatishwa na sura lake BAYA.:-(
Swali:- AU?
- Si unakumbuka ugali unaweza usiliwe kama hauletwi mezani na MBOGA tamu?
- Si unakumbuka UGALI mbaya unaweza kuliwa kama mboga tamu?
- Kwani wewe hakuna wimbo uupendao ambao unajua UJUMBE WAKE NI NYOKO lakini hata hivyo unaurudiarudia NA MPAKA KUUKARIRI WIMBO huo wenye UJUMBE MBAYA KWAKO na kwa MATOTO YAKO huku ukitingisha bichwa lako kisa mirindimo ya MUZIKI na SAUTI ya muimbaji vinakukuna nanihii kunako?
Ndio,.......TATIZO ni ,......ujumbe MZURI katika hata HOTUBA ,....... labda inahitaji SURA fulani au tu SAUTI fulani ili walengwao na UJUMBE wasikilize UJUMBE bila kushikiwa VIBOKO.:-(
Swali:- Si nasikia kuna wamsikilizao Barrack Obama Marekani kisa wanapenda sauti na WANAOMSIKILIZA Rais KIKWETE Tanzania kisa wanampenda sura?
- Si unakumbuka kuna sababu si kila mtu WEWE unamsikiliza ?
- Si unajua kuna uwezekano majibu ya matatizo yako ulishapewa ila hukuyasikia kisa hukupenda wimbo au sura tu ya MTOA suluhisho?
- Si unajua upendaye kumsikiliza unaweza kunogewa kufuatilia azungumziavyo jinsi ya kutatua matatizo ya kujisaidia kwa bata kuhitajivyo bata wavalishwe chupi kuliko USIYEPENDA kumsikiliza akizungumzia jinsi ya KUTATUA matatizo yako?
Ndio,..... labda HATA MAANDISHI usiyopenda KUYASOMA yanasomeka bado,...... na husomi hata BIBLIA na KORANI ingawa unajua vina UJUMBE MWEMA tu,...
....kama tu kwenye kitabu cha KAMASUTRA ubobeavyo kwenye PICHA na sio MAANDISHI kisa kwa ladha yako VITABU hivyo banangenge vimekosewa kuandikwa VIZURI katika mirindimo ikupandishayo MDADI WA KUSOMA kama vile yaandikwavyo MAGAZETI YA UDAKU katika mirindimo iwezayo kukufanya uone HABARI ya KHADIJA hapendi kuvaa chupi ni HABARI MUHIMU SANA kuliko habari ya KUNA MAFURIKO Ludewa. .:-(
Swali:- AU?
- Si unakumbuka pia kuwa UJUMBE MZURI NA WA BUSARA kwa MTU MWINGINE inawezekana ni KILE ukiitacho wewe MATUSI?
Staili ya MUANDISHI wa habari,...... yaweza kusababisha usomee UANDAJI wa UDONGO walao wajawazito, HISTORI au tu angalau upende kujisomea stori za UCHAWI uziogopazo,.......kisa STALI YA UANDISHI kukufanya usiyependa kusoma uhusudu KUHAMIA mstari unaofuata katika HADITHI kisa kanogewa na SENTENSI ya kwanza ,...
..... kama tu kwa ASIYE PENDA UGALI WA MUHOGO kujikuta kamaliza bonge la sima kisa MBOGA tamu kusababisha tonge la kwanza kumshawishi MLENGWA kukata TONGE la pili na mpaka kumaliza MAAKULI bila kukumbuka huwa HAPENDI UGALI wa MUHOGO kwa kuwa yeye ni MUTU ile inapenda YUGALAI (Ugali kwa Kizungu) iliyopikwa kwa kutumia UNGA WA SEMBE.:-(
Ndio,...
... UGALI bila MBOGA unalika bado .:-(
NI wazo tu HILI MHESHIMIWA!:-(
Hebu India.Arie, Dobet Gnahore, Idan Raichel na Blue Miller walete- Palea
Au tu India Irie na Dobet Gnahore waendelee na -Pearls
Bila kumsahau ALI KIBA katika kibao-Mac Muga
-
HIARI IPO hata kama kwa HIARI atendwavyo MWINGINE yachokoza na kuchokonoa HURUMA YAKO kwa kuwa ANAVYONANILIWA hupendi!:-(
Posted: February 22, 2010, 9:14 am by SIMON KITURURU
NDIO hata ubishe ,...... katika KUNANILIU ,.......kuna WANANILIWA pia ,....... ambao WANANANILIWA VIZURI kwa bidii TU kwa hiari yao wenyewe.:-(
Swali:- Kwani unafikiri WATANZANIA katika kunaniliu a.k.a KUCHAGUA CCM na sio vyama vya UPINZANI unafikiri WENGI TU hawafanyi hivyo kwa HIARI yao tu hata kama WEWE hupendi CCM Mkuu?
- Kwani unafikiri ni MANGAPI utendewayo ambayo unasaidia WEWE MWENYEWE yafanikiwe UTENDWE VIZURI TU kwa faraja?
Kuna yalazimishwayo,....... lakini HATA KAMA HUPENDI haiondoi ukweli kuwa kuna WAUMIZWAO,...... ambao yaumizayo ni ya HIARI KWAO.:-(
Kuna yalazimishwayo,... ....lakini hayohayo usipostukia hasa KAMA WAUMIZWAO NI WAJANJA unaweza kushabikia mchokonoo UNAOUMIZA bila kujua kwa kuwa WAJANJA wanaweza tu kutungia jina tofauti MCHEZO wakati KITENDO NA maumivu ni YALEYALE.:-(
Swali:- Si unajua adhabu nyingi tu wapewazo watu kama tu KURUKA KICHURACHURA , zikifanywa kwa HIARI wajanja HUZIBADILI JINA na kuziita ni MAZOEZI?
- Si unajua KUBAKWA, na MAMA WATOTO kulazimika kuwa kiburudisho kwa baba watoto bila kuandaliwa kwa kuwa baba watoto SAA HIYO anataka kula mali zake alizozitolea MAHARI ,kwa MDADA kunaweza kukawa na maumivu sawa kimwili , ingawa moja MDADA kabakwa MIGOMBANI na JINGINE ni IMEBIDI KWA HIARI mdada avumilie MAHITAJI YA MUME WAKE kwa kutii MAFUNDISHO YA SOMI wake KWENYE UNYAGO kuhusu HIARI YA MWANAMKE ni MAAMUZI YA MUMEWE , na kwahiyo haliitwi KUBAKA?
NIMEACHA !
HILI ni WAZO tu MHESHIMIWA!Jumatatu NJEMA!
Au tu Jean-Claude Naimro na KASSAV wabadili tena kwa-Ave'w Doudou
Au tu JOCELYNE BEROARD wa KASSAV alete -Kay Manman
Au tu Jacob Desvarieux na KASSAV wapoze pia zaidi kwa -Malad aw
-
SHOGA njoo pembeni TUMSENGENYE MAMA MWENYE NYUMBA kwa kuwa HAUSIGELI ni kibonde , TUTAMSUTA uso kwa USO!:-(
Posted: February 22, 2010, 8:50 am by SIMON KITURURU
Katika dunia yenye WENYE mabavu,....... kwa kawaida WABABE HUSENGENYWA kwa SIRI ili wasije kubwenga MTU bure wakisutwa USO kwa USO,....
....na ASUTWAYE uso kwa uso ni ambaye inaaminika katika tukio hana MABAVU na akileta za kuleta wakati anapandishiwa sketi a.k.a ANASUTWA hata MBATA na KONZI anawezabwengwa kama nyongeza juu ya MSUTO.:-(
Swali:- SI unakumbuka mara nyingi HATA WEWE ufanikiwaye KUMSUTA uso kwa uso KWA KAWAIDA ni YULE ambaye humuogopi VIZURI?
- SI unakumbuka UMSENGENYAYE na KUMTETA na MASHOGA ZAKO hasa yule rafiki yako bado ni ISHARA ya KUOGOPA KUZUNGUMZA NAYE UFIKIRIACHO na ndio sababu INGAWA UNAMSENGENYA NA MASHOGA ZAKO WENGINE bado KWA KUMUOGOPA una kahofu kakutotaka ajue ni wewe UMTETAYE kisa unajua ana mimba ya PADRE na wala si ya HAUSIBOI kama walivyohisi WAMBEYA wa nyumba ya jirani waliovalia njuga ufala wa MUME wa rafikiyo kabla huja waongezea MSENGENYO kwa kuwa tonya ishu?
- Si unakumbuka kuna WAPINZANI wengi wa Rais KIKWETE ambao ni mabingwa tu ya KUMSENGENYA na KUMTETA wakati hayupo lakini akitokea KIJIWENI kumsuta HAWAWEZI?
Kwa mtazamo huo usishangae mahusiano YA ASUTWAYE na ASENGENYWAYE na KUTETWA yakiwa na MWALIKO uliokaa mkawai :
Njoo tumsute MLALAHOI,...... kwa kuwa FISADI inabitumsengenye tu na kumteta kwa siri kwa kuwa mpaka POLISI ni hawala zake.
Njoo tumsute, KUMTETA na kumpiga makonzi MSENGE,...... kwa kuwa NJEMBA RIJALI yenye wake wengi hata kuisengenya tu kwa hilo KIMILA nyingi za KIAFRIKA bado haiwezekani.
Njoo tumsengenye MAMA MWENYE NYUMBA na sio HAUSIGELI,........ si unajua kumsuta MAMA MWENYE NYUMBA unaweza kuchochea kubwengwa na mpaka BABA MWENYE NYUMBA ingawa kwa kumsuta HAUSIGELI yaweza kuonekana sawa TU ingawa HAUSIGELI na wala sio MAMA MWENYE NYUMBA ndiye kiburudisho cha Baba Watoto.
Swali:- Lakini si unakumbuka asengenywaye kama hastukii asengenywacho MSENGENYAJI labda anapoteza tu MUDA?
- Si ulishawahi kufikiria kuwa mara nyingi UMSUTAYE unaweza pia kumsengenya lakini si kila UMSENGENYAYE unaubavu wa kumsuta kwa kuwa kusuta mtu huhitaji umuangalie machoni?
Ndio,.......labda hata katika ya VIONGOZI wako MAFISADI kuna uwezekano yote uyasikiayo ni MISENGENYO na kuteta tu kwa wasio na MABAVU ,.......kwa kuwa hakuna wa KUWASUTA uso kwa USO.:-(
CHA ajabu ni kwamba,...
....wengi waogopwao KUSUTWA uso kwa USO mabavu yao MISINGI YAKE inatokana na kitu hicho hicho ``KUOGOPWA´´.:-(
Swali:- Unauhakika weye MTANZANIA Rais Lowasa Mkapa akiwa mbele zako utaongelea Richmondi kama utetavyo kijiweni na washikaji?
Ni wazo tu DHAIFU HILI Mheshimiwa lakini pamoja na yote NI WAZO!
Hebu FALLY IPUPA abadili kwa -Cadenas
au tu tulia na Awilo Longomba - Awa Imani - African Tonic katika- C'est pas Complique
Blah blah blah
Fish cakes
Alas a fish cake.
Yet more fish cakes
Guess what ... yeah ... fish cakes.
The end of the fish cakes