SIMON KITURURU- MAWAZONI
-
Kwa kuwa KUNA NYIMBO MAMILIONI za MAPENZI DUNIANI ukilinganisha NA wingi wa NYIMBO ZILE za UMUHIMU wa jinsi ya KUBWIA UGORO!:-(
Posted: February 21, 2010, 10:33 am by SIMON KITURURU
....HASA ukilinganisha NA wingi wa NYIMBO ZILE za UMUHIMU wa jinsi ya KUBWIA UGORO!:-(
[Tahadhari: Taralila hii ina neno KUNYA!:-(]
Naanza;....
Kwa kuwa kuna NYIMBO MILIONI zizungumziazo MAPENZI katika kila wimbo mmoja uzungumziao KUNYA,....
... haina maana KUNYA hakuna sifa ziwezazo kutungiwa NYIMBO MILIONI katika kila wimbo mmoja UUSIKIAO wa MAPENZI.
Swali:- Si unakumbuka watu hufikiria KWENDA kunya mara nyingi maishani kuliko wafikiriavyo MAPENZI au wampendavyo MTU?
- Unauhakika ingawa huwezi kulazimisha watu waimbe NYIMBO ZA KILIMO wakulima wenyewe UKIWAACHIA WACHAGUE unadhani watasikiliza ZAIDI nyimbo zizungumziazo KILIMO?
Ndio...... usidanganyike na usikiacho kwa kuwa KINATAMKWA MARA NYINGI HADHARANI na kutungiwa nyimbo NYINGI ,...... NA UKAAMINI na kufikiri HICHO ndicho chenye umuhimu zaidi kuliko vingine kwa WATU.:-(
Ndio,...... usidanganyike na USIKIACHO kwa kuwa KINATAMKWA mara nyingi na kutungiwa NYIMBO nyingi,....... MPAKA UKAAMINI KWA KUSAHAU kuwa usichokisikia mara nyingi kina sifa nyingi tu za kutungiwa NYIMBO MARA NYINGI kama hichohicho ukisikiacho MARA NYINGI ,na watunzi HAOHAO watu.:-(
Swali;- Si unajua unaweza kuishi bila kupendwa lakini huwezi kuishi bila KUNYA ingawa nyimbo za HAJA KUBWA huzisikii vyakutosha REDIONI?
- Katika kuangalia ni kwanini kuna aina nyingi za nyimbo zenye neno HALELUYA kuliko zenye sentensi ``kudokoa MBOGA´´ , unafikiri wewe sio usababishaye hakuna nyimbo nyingi ziongeleazo umuhimu wa kunya vizuri kwa KUWA unasikiliza KIRAHISI zaidi nyimbo za ``Mpenzi nakupenda zaidi maungo yako´´?
NIMEMALIZA.:-(
NI WAZO TU hili MKUU na unaruhusiwa kulitukania mama!:-(JUMAPILI NJEMA MHESHIMIWA!
Au ngojea Peter Tosh akumbushie-U can't BLAME the YOUTH
Peter Tosh adai - ARISE Blackman
King YELLOWMAN anyambulishe kwa kitu- Fools go to church on Sunday
Au EEK a MOUSE abadili kwa kulainisha MSHAWASHA kwa stori ya -The man and the mouse
-
KWA kuwa njia NZURI ya KUTUNZA AHADI hata kwa MPENZI ni kutoahidi!
Posted: February 21, 2010, 10:07 am by SIMON KITURURU
AHADI ni faraja ya KITU kwa muda mfupi,........ kwa kuwa hata UKITIMIZA ahadi LEO hata bila KUDENGUA ,......... huo ni mwanzo TU wa kumuandaa mtu ULIYEMTIMIZIA AHADI kukaa mkao wa kuhitaji AHADI mpya UPYA .:-(
Swali:- AU?
- Kwani ulichoahidiwa kikitimizwa UNADHANI HUO ndio mwisho wako wa KUTAKA kuahidiwa TENA kidude?
AHADI mpya ni tamu KWELI,........kwa kuwa inatia faraja UPYA!
AHADI hujenga tegemeo la kuwa ingawa sasa hivi huna KIDUDE ,....
... ni muda tu kidogo ambao ndio tatizo kwa kuwa utakacho utakipata BAADA YA MUDA kwa kuwa UMEAHIDIWA tayari KIDUDE.
Swali:- AU?
NA AHADI ni tamu tu wakati IMEAHIDIWA,......... kwa kuwa utamu wa AHADI ni AHADI yenyewe ,....
...... hasa KWA SABABU ulichoahidi UKIKITIMIZA HUGEUKA KWA KUTIMIZWA na kuwa sio AHADI TENA ,...
...na KWA HILO ladha yake ni tofauti na AHADI ndio maana bado kuna WADAIO walinogewa na KILICHOAHIDIWA zaidi ya AHADI .:-(
NDIO,...
.....uhakika wa ladha ya AHADI uko zaidi katika AHADI tu na sio KILICHOAHIDIWA ,.......... kwa kuwa KITU ulichoahidiwa CHENYEWE ,....
.... kinaweza kuwa KINANUKA uvundo wa MKOJO au tu KIMEZIDI SUKARI kuliko ulivyoahidiwa na uifikiriavyo AHADI.:-(
Swali:- Unafikiri AHADI ya BUSU a.k.a kula denda ina utamu kama kula mate a.k.a KULA DENDA?
- Si unakumbuka utamu wa KUHISI UNAPENDWA ni tofauti na kitendo cha KUPENDWA CHENYEWE ndio maana uhisiye anakupenda wakati anakupa KIDUDE ili akuaambukize GONO na MDUDU unaweza kumpenda zaidi kuliko AKUPENDAYE na kukunyima KIDUDE kwa kukujali ili asikuambukize HERPES au tu FUNGUS ya kunako hata kabla hana GONO na MDUDU?
NDIO,....
.... KUAHIDI ni kujenga misingi ya KUVUNJA ahadi ,.........kwa kuwa KUAHIDI ni mimba ya MATEGEMEO ya ALIYEAHIDIWA ,....
.... na kitegemewacho KWA KUWA NI AHADI ndicho chenye misingi ya MAUMIVU yatakayopewa MOTISHA au kuvunjwa kwa AHADI hasa kwa kuwa wewe NI BINADAMU na hakuna BINADAMU mwenye uhakika na BAADAYE kiasi cha kuwa na uhakika asilimia MIA atatimiza AHADI.:-(
Na KWA BAHATI MBAYA kama HUJAAHIDI ,...
.... MKUU kumbuka kuwa haina maana kuwa,...... HAKUNA MTU aaminiye weye huna AHADI ya KUVUNJA kwake .:-(
Swali:- Si unajua kuna watu hata MSICHANA AKIOLEWA TU ni kama vile KAWAAHIDI na kahakikishia ukoo kuwa atapata mimba hivi karibuni kwa hiyo ni wakati wakumuangalia ujazo wa tumbo au tu katika mwendo anatikisaje matako , LA SIVYO itabidi kumuuliza MUME wake kuwa nini kinaendelea mbona KIMWANA HAJISIKII KICHEFUCHEFU ,kitambi hakikui, hali udongo, habanwi haja ndogo mara kwa mara au tu hatema mate ovyo?
- Si unajua PIA kumchekeachekea mtu ingawa ni kwa kuwa NI mcheshi TU kunaweza kumfanya MHESHIMIWA ACHEKEWAYE afikiri akitongoza atapewa kwa kuwa kicheko chako kimetafsiriwa ni KUJIGONGA na unaahadi kukubali?
Tahadhari,.......tafsiri za AHADI ziko nyingi kwa wengi na wala HIZO TAFSIRI hazitokani na sentensi - `` NA AHIDI´´.:-(
Lakini ,.........KUMBUKA kama hujaahidi ,...... wewe HUJATOA AHADI.
NA kama HUJAAHIDI ,....... MKUU kunauwezekano MKUBWA weye huna AHADI ya KUVUNJA,........ ingawa TU usisahau UWEPO wako tu labda unawapa watu AHADI ambazo usipoangalia unaweza mpaka KUJILAUMU kwa kudhani ULIAHIDI MTU kitu.:-(
Swali:- Unabisha?
Lakini kama unajua tatizo na SILIKA za MTU ,.........TIMIZA usivyoahidi,....
...kwa kuwa hakuna kitu kitamu KWA MTU kama kupata kitatuacho TATIZO LAKE ambacho hakutegemea na HAKUAHIDIWA!
Swali:- Si unajua jinsi gani utamu wa shilingi ulivyo mtamu zaidi ya shilingi kama ukigawiwa shilingi uliyokuwa na shida nayo bila kutegemea hilo?
- Ushawahi kusikilizia utamu wa kidude ulichopewa ghafla bila kutegemea wakati unahamu na kidude ulivyo tofauti?
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA !
Hebu King Yellowman abadili kwa - Wrong Girl To Play With
Au tu King Yellowman alete tena-Reggae Calypso
Au tu KING YELLOWMAN amalizie na pambio-Gimme vagina
Blah blah blah
Fish cakes
Alas a fish cake.
Yet more fish cakes
Guess what ... yeah ... fish cakes.
The end of the fish cakes