SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • Manufaa MAKUBWA ya RAIS au KIONGOZI MJINGA!

    Posted: February 18, 2010, 7:12 pm by SIMON KITURURU
     [Tahadhari: Tafakari imepinda na ni fupi a.k.a imekatiziwa denge!:-(]

    Kama KIONGOZI  mjinga si mjinga vyakutosha kuharibu kabisa,......
    ...BASI labda ........KILA NCHI ili ijengwe na kuimarishwa MISINGI YAKE KIBUSARA labda inahitaji mara kwa mara kuongozwa na RAIS au Kiongozi MJINGA!

    Kiongozi  MJINGA hata wa KAMATI   YA KIJIJI na SIO  NCHI  ionekanayo inahitaji KIONGOZI asiye MJINGA kama TANZANIA ana manufaa yake katika kuamusha MORI WA WANANCHI  katika kustukia NA KUHESHIMU  ni nini umuhimu wa VIONGOZI BORA wajuao wanafanyanini na si WAJINGA katika UONGOZI  WAO  ambao matunda yake ndio kielelezo bora cha ubora wao wa kutoongoza mambo KIJINGA..


    Na Rais MJINGA ni msaada sana hasa akifuatiwa na RAIS MWENYE MIAKILI ya uongozi na bingwa wa  UTEKELEZAJI  kwa  BUSARA  ZAKE hasa katika kusaidia kukubalika kwake na SERA ZAKE baada ya WANAVIJIJI kuchoshwa na YALE YALE  ya danganya toto za KIJINGA..


    Swali:

    • AU?
    • Unafikiri HITLER hakuwa msaada kwa KIONGOZI aliyemfuatia UJERUMANI baada ya wananchi kushtukia alichemsha?
    • Unafikiri UONGOZI wa CCM  kama UNAKOSEA sio msaada na  funzo kwa CHAMA chochote kingine kitakacho ingia MADARAKANI Tanzania baadaye?



    Lakini.....
    • Hivi katika shughuli, KIONGOZI MJINGA na mtekelezaji swala na KIONGOZI MWENYE MIAKILI a.k.a SIO MJINGA  lakini PIA  si mtekelezaji unafikiri watoto watafanana na nani  kama uzalishaji watoto unahitaji MTEKELEZAJI wa shughuli?



    NIMEACHA!

    SAMAHANI ni wazo tu fupi hili MHESHIMIWA na ni ruksa kulipinga!
    SIKU NJEMA!

    Au badili kwa kupata stori ya ndoa na penzi kiduchu....


    The LAST POETS warudie tena -Take Your Time



    Au tu Fu-Schnickens na Shaquille O'Neal wabadili tena kwa -What's up DOC
  • Chandarua CHENYE manufaa NA CHA BUSARA kwako katika KUZUIA MBU ni nyavu nzuri za KUVULIA SAMAKI kwa MWENZIO!:-(

    Posted: February 18, 2010, 6:49 pm by SIMON KITURURU
    Wewe katika MAISHA sio WAO,........ kitu hicho hicho kikabiliwacho na swala la kuwa MIMI sio WEWE na  nipendacho MIMI ni kutokana na nikabilianavyo mimi KITU KISABABISHACHO  kwangu  kupenda upendacho wewe yawezekano inahitaji NIJIFUNZE.:-(

    Na kujifunza inahitaji SABABU,........ na tatizo linarudi pale pale kuwa SABABU ZAKO zilizokufunza  KUTOPENDA hata SINDIMBA na ujanja kwako ni BONGO FLEVA labda yabidi nikuelewe kwanini katika NGOMA nzito zote TANZANIA  wewe ikudakayo DAR es SALAAM kirahisi sio MDUNDIKO na ni KWASAKWASA ya kutoka kwa BABA MOBUTU ambaye ndio juzijuzi WANASIASA wetu TANZANIA wanastukia KUMUIGA katika UFISADI.


    Swali:

    • AU?
     Tukiachana na hilo, kumbuka tu .....
    Kwa aaminiye katika KUCHEZA peku  hata uumpe KONDOMU za BURE,....
    ......kama staili ya UMUHIMU uuonao hauangalii kwa jicho na ujuzi wa kunogewa UTAMU  kama wewe uchezaye MAMBO KWA SOKSI,....
    .....hata kama ATAKUFA atakufa wakati  anachezea kinjegele  PEKU kwa raha zake wakati UJUMBE wa UDAICHO NI MUHIMU alikusikiliza..

    Swali:
    • Kwani unafikiri  wangapi waambukizwapo UKIMWI walikuwa na KONDOMU na hawakuamua kuitumia tu?

    Na NDIO,........chenye manufaa kwako hata ukigawe bure kama wagawavyo VYANDARUA kuzuia MBU na MALARIA ,...

    .... CHANDARUA kinaweza geuzwa TU  kuwa ni nyavu za kuvulia SAMAKI ingawa ulihubiri na kupigiwa makofi  ukiongelea  CHA MUHIMU KWAKO ambacho  NI KUZUIA MALARIA wakati CHA MUHIMU KWA UWALENGAO NA MSAADA ni nyavu kama za CHANDARUA ambazo ni muhimu zaidi kwao KWA kuvulia SAMAKI.:-(

    Swali:
    • Unafikiri  ni kwanini kuna WANAWAKE wateteao umuhimu wa KUKEKETWA wakati wanogewao maswala kwa kuwa na kinjegere wanasimulia tamu za kutokeketwa?


    Ndio,......mwisho wa siku  LABDA ,...
    ... cha muhimu kwako  na ambacho unaamini kina umuhimu kwa wengine bado ni CHENYE manufaa ZAIDI  kwako kwa kuwa UMUHIMU WAKE una  MTAZAMO WAKO.:-(

    Na kama chako UAMINICHO kinamanufaa kwa wengine ,......... ukitaka WENGINE waambukizwe kunogewa kwako  katika hicho,...... labda kabla hujachukua HATUA YOYOTE ,....
    ...FIKIRIA wanogewavyo wengine kabla ya kuwapanulia hicho wengine WATU na  kufaidisha NZI  tu wakati uliotaka waonje ni WATU,......na wala sio hao INZI  wenye kunogewa na upanuacho vingine.:-(



    Swali:

    • Si unajua kuna uwezekano kabisa UFIKIRIACHO NI MSAADA KWA WENGINE ni kwa kuwa tu kwa kufikiria hivyo hicho ni msaada kwako?



    NI TAFAKARI tu HII Mheshimiwa! 
    Na MSOME,...
    .....Kadinali Chacha o'Wambura NG'WANAMBITI  aliyeiotesha TAFAKURI HII  kwa kuzungumzia jinsi VYANDARUA VIGEUZWAVYO    sehemu za kupoozea maisha magumu KUKU HAPA









    Au HEBU Mr.CHEEKS na STEPHEN MARLEY wabadili kabisa hali ya hewa kijiweni kwa kitu  - Guiltiness


    Mr CHEEKS alete-Double B Flow



    Au tu Mr.Cheeks amalizie kwa - Lights, Camera, Action

  • Labda umuhimu wa MTOTO kwa baadhi ni TUMIZI la MTOTO,.....

    Posted: February 18, 2010, 6:48 pm by SIMON KITURURU
    .....katika ajenda za WAKUBWA waliozaa kujisikia kuna kitu ANGALAU KIMOJA TU wamefanikiwa kufanya  KATIKA ya DUNIANI !:-(




    NA labda sio utani ,...
    ... kuwa umuhimu wa  MTOTO kwa binadamu waliozaa ni tumizi  la ya mtoto LIZIBALO na KUJAZIA  kizibwacho na hisia na shughuli zitokanazo na kuwa na MTOTO DUNIANI ambazo huanzia  tokea  mzazi ajue atapata  MTOTO.:-(
    Labda si utani ,......MTOTO kama tumizi kuna walikabilio kama ni SHUGHULI tu mojawapo iwasaidiayo WENYE MTOTO kujisikia tu kuwa pamoja na matatizo yote  ni kweli WAKO HAI na kithibitisho ni hata mwenye utapiamlo MTOTO.:-(

    Labda sio utani,...... mtoto ni MTAJI wa baadaye , wakati MKE ni trekta la sasa HIVI kama UNA SHAMBA  kubwa na pembejeo ni JEMBE shambani katika shughuli ya kilimo isiyo ya KITOTO.:-(


    Swali:
    • MTOTO wako ni wa nini wakati kwa MTAKA WAJUKUU anaweza zaa mtoto atakaye kuwa PADRE  wa KATOLIKI asiyeruhusiwa kuoa au kuzini kwa ruksa iletwayo kwa ndoa?


    • MTOTO wako ni wanini wakati kwa MTAKA WAJUKUU anaweza kuzaa mtoto tasa?

    Na kuna wenye WATOTO,...... kwa kuwa katika kuhusudu URODA mtoto ni ajali kazini.

    Kuna wenye MTOTO,...... kwa sababu  KUWA NA mtoto kwawasaidia tu KUWALETEA  maana ya maisha hapa duniani.

    Na kuna wahitajio MTOTO,...
    .... kama msaada wa MAISHA uzeeni.


    Swali:

    • Unauhakika ni wangapi wana watoto na hata siku moja hawakufikiri ni kwanini wana watoto?

    • Katika watoto waitwao wa mtaani duniani unafikiri ni wangapi wamezaliwa kutokana na wazazi wao kutofikiria yahusianayo na MTOTO kabla ya kuzaa mtoto?

    • Unafikiri matajiri kama akina OPRAH wenye mabiloni si kufuru kutokuwa na MTOTO au akina Rais Clinton kuwa na mtoto mmoja tu si kitendo cha upotezaji wa mbegu na mayai yashughulikiayo  mafanikio ya MMIMBISHO?

    • Hivi MTOTO kwako ni wa nini?


    Na kwa wengine ,..... LABDA mtoto UMUHIMU WAKE ni kama tu MWANASESERE kwa kuwa,....

    ..... SI MAMA YAKE YUPO atakaye mshughulikia ambaye yeye ni VIGUMU kumkimbia bila nyonyo kuvuja MTINDI akilia?




    Swali:
    • Unauhakika  ni kweli unahitaji WATOTO au hata  ndoa ukizingatia maisha yako ukiyatafutia MAANA kivingine yanaweza kuleta tu maana kama ya  MASISTA wa KIKATOLIKI ambayo bila ZE TOTOZ  yanalipa tu na hutabadili nepi rojo? 


    NI tafakari tu hii MHESHIMIWA wakati tunajua  MAZOEZI ya kitendo yanaendelea DUNIANI  na kwa kitendo  KUNA mtu kammegea MTU mahali fulani MIMBA !:-(


    Au hebu THE LAST POETS wabadili zaidi kwa tafsiri yao ya - Black is




    Au tu The LAST POETS wabadili tena mtazamo wao kuwa -NIGGERS are SCARED of REVOLUTION




    Au tu The Last Poets wamalizie kwa - When The Revolution Comes


Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs