SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • Labda UKWELI bado ni UONGO!:-(

    Posted: February 17, 2010, 8:01 am by SIMON KITURURU
    Ukweli  ni nishai kweli,....... kwa sababu  hubakia kwako kuwa ni UKWELI mpaka uustukie kuwa HUO  ni UONGO.:-(

    NA  kama uongo ambao hujaustukia BADO, kwako ni UKWELI ,.......... haki ya nani  KWAKO huo ni  UKWELI  kwa kuwa tu UNAUAMINI, na ndio kifanyacho huo KWAKO bado sio UONGO.:-(

    LAKINI  tatizo la UONGO ambao KIGOLI au NJEMBA ITAKUFA / imekufa a.k.a KUDEDI ikiamini ni UKWELI,.....
    ... bado hataufanyeje ni UONGO.:-(

    Swali:
    • Unabisha?
    • Kwani unafikiri UKWELI ni UKWELI kwakuwa mwaniwane  unaamini tu ni UKWELI?





    UKWELI ni KIBOKO ,........ndio maana ukiwauliza WAAMINIO utastukia kila mtu ana kweli yake,.....
    KWA MFANO;...

    ... Wakatoliki watadai Kanisa lao ndilo la KWELI,....

    .....Walutheri nao watadai KANISA lao ndilo la kweli,.....

    ......WAPENTEKOSTE  nao watadai lao ndilo la KWELI ndio maana wanawanenaji kwa lugha zaidi kanisani mwao,.....

    .....WASABATO watadai pia wao mpaka kwa kusali Jumamosi  na kula chakula cha BWANA kwa juisi ukiachilia mbali KITIMOTO kwao mwiko , wao ndio wanapatia zaidi na ndio wao BIBLIA wanaielewa KIKWELI, ...
    .... halafu ukiwakuta WAISLAMU ndio watakustua kuwa WAKRISTO wanakosea kuelewa na UISLAMU ndio dini ya KWELI, ....

    ....na WAYAHUDI ndio kabisa  wao watakuambia  ndio KWELI waliochaguliwa na MUNGU na huo ndio UKWELI  ,....

    ..... bila kusahau wasio amini MUNGU ambao kwa KUTOKUAMINI Mungu  ndicho waaminicho  ndio ni KWELI  YAO ,........nao wanadunda TU  mtaani  kama tu wacha MUNGU wadundavyo wakiwa na faraja kwa KUWA WANAAMINI   waaminicho ndio KWELI.,  tukiachiliambali  waaminio Mungu wawafikiriavyo ...,....

    .....na ..... .:-(




    Swali:
    • SI unajua kuwa udhaniaye na kumsifia kikweli kuwa ni KISURA a.k.a  MZURI kwelikweli  bado kuna mtu kwake huo ni UONGO KWELI KWELI  na ukweli wenyewe KWAKE  ni kwamba  LIKISURA  lako a.k.a UNALOLIMEZEA MATE  ni BAYA kwa ujazo wa kutosha tu?

    • Unauhakika na siri ya nini kinafanya kuna vitu VINGI TU MAISHANI MWAKO ambavyo hujawahi hakikisha  ila unaviamini ni KWELI?

    • Unauhakika kuna MTU anaweza akawa MPAKA na uhakika YUKO HAI wakati hajui AU HANA UHAKIKA  WAFU WANAJISIKIAJE na wakishadedi a.k.a KUANZA hawajisikii wako HAI kama mtuz tu uzijuazo ziendelezazo UFISADI tu Kimswano tu maeneo?



    Lakini UONGO PIA  ni bonge la kitu kwa kuwa limesaidia wengi kufanya KWELI.:-(
    Na haki ya Mama Kisebengo tena!...,...
    .....kunauwezekano NDOA NYINGI  ZA WATU UWAFAHAMUO ukizifuatilia kutokea enzi za MCHUMBIO mpaka Urais wa Rais Nyerere, Kikwete, OBAMA au tu uchaguzi wa MWENYEKITI wa kikao cha KICHENI PATI ya BINTI UGONI ,.........nyuma yake WAWEZA STUKIA KULIKUWA NA BONGE la dozi ya UONGO iliyofanikisha.:-(


    Na narudia,........KWA BAHATI MBAYA,...........inawezekana kabisa KUWA uongo ni UKWELI mpaka aliyedanganywa ASTUKIE.:-(



    Swali:
    • Sasa hudhani kama kuna KWELI za aina nyingi hivi duniani basi kuna uwezekano KWELI yako bado ni UONGO?

    • SI unakumbuka ilikuwa ni KWELI kabisa kuwa DUNIA inaumbo la MEZA na waliodai NI ya mduara waliuawa mpaka na kanisa KATOLIKI kwa kupotosha watu mpaka UKWELI ulipo geuka kuwa ni kweli DUNIA ni ya duara na inalizunguka JUA na sio JUA linaizunguka DUNIA? 





    NIMEACHA!NI WAZO tu hili MHESHIMIWA KUMBUKA na wala usikonde hasa kwa kuwa  weye HUDANGANYI!


    Hebu mcheki mwenye uhakika na KWELI yake ....


    Au hebu Raheem DeVaughn abadili kwa kweli yake ya  - She's not you



    Au tu Raheem DeVaughn alete pia-Try again

Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs