SIMON KITURURU- MAWAZONI
-
TEKNOLOJIA IPO na katika ulimwengu wa FACEBOOK ,- kuna UJUMBE na status : ``Niko MSALANI!´´
Posted: February 16, 2010, 9:04 am by SIMON KITURURU
Katika ulimwengu wa GBuzz,....... MTONYO waweza kuwa ni ,....- ``Nimeenda KUCHIMBA dawa!´´
Katika ulimwengu wa TWITTER ,....... UJUMBE waweza kuwa ni ; .....-``Niko CHOONI!´´
Na katika ulimwengu ambao TEKINOLOJIA ni ala ya NGOMA katika enzi ZETU za MKOLONI,...
..... UJUMBE; Gdu du dududu du ,....
.. tafsiri yaweza kuwa ilikuwa ni ;...
-`` MKOLONI anakuja chimba choo kama hutaki kuchapwa HAMSA ishirini kwa kwenda haja vichakani!``
Swali:- Weye uliyebobea kwenye INTERNET na E-mail zako , UNAKUMBUKA jinsi ya kuandika BARUA lakini?
- Si unakumbuka hata teknologia ibadilike vipi haisaidii kutengeneza UJUMBE na ni MTU mwenyewe katika tumizi la tekinolojia aamuaye ujumbe autumao kwa wasio na CHAKULA kuwa ni jinsi CHOO cha kukaa kisafi kiongezevyo upotezaji wa muda wa watu CHOONI ?
Kumbukumbu:
Kuna kipindi barua ya MTU ya kwanza kwa MPENZI MLENGWA kutokana na elimu za vijiwe vya kitoto ,...
...ilifanikiwa kuchorwa mpaka MAUA na kunyunyiziwa poda KWA WENGINE huku yote hayo MTU kiroho kikimdunda kutokana na UZITO wa ujumbe ulioandikwa wa;....... ``Helo , mimi nakupenda na NAOMBA URAFIKI!``
Siku hizi MTU ZILIZOPIGA UMRI zinaweza onea wivu wale ambao WAMEZALIWA wakati maswala yote ni TEXT MESEJI za simu na MWALIMU ni TELEVISHENI ;....
.....halafu UJUMBE wa mtafuta MPENZI mwenyewe BADO ni;....... ``Helo , kunakitu nataka kukuambia NI DIP basi simu yangu haina hela!´´
Swali:- Unafikiri tekinolojia hizi mpya usipoangalia hazikuondoi hata ujuzi wa kupiga mluzi ili kuita MTU?
- Unafikiri pamoja na HIZI teknolojia kurahisisha upataji wa habari ukweli wenyewe si kwamba habari utakazo kuzipata ushazitengenezea mipaka na kwa mpenda habari za choo asilimia kubwa ya habari na ujumbe apatao ni wakuhusiana na CHOO kama tu mpenda BONGO FLEVA miziki kibao ailengayo na kuisikiliza isivyokuwa ni TAARABU?
- Si unakumbuka ni wewe na sio TEKNOLOJIA itoayo na kupokea UJUMBE na hata kwa kutumia tekinolojia gani bado BINADAMU atafariki akiwa amefanikiwa kujua tu machache katika duniahii yenye mambo zaidi ya KIDUCHU kilengwacho na mtu?
Ndio,....... kuna wakati madhumuni ya BARUA yalikuwa ni KUKUJULIA hali.
Na wakati tunaishi katika ulimwengu ambao MADHUMUNI ya kuwa ANONYMOUS MTANDAONI yanaweza kuwa ni KUTUKANA MTU, ...
.....tukumbuke tu TEKINOLOJIA haiongezi idadi ya UJUMBE zaidi ya KUFIKISHA tu HATA UJINGA kama UJUMBE ,....
....na kitakiwacho KUJULIKANA ni kwamba UJUMBE upo tu kama unania ya kuupata na matumizi yako ya TEKNOLOJIA yaweza kuwa ndio kwanza yanakusaidia TU kuchanganyikiwa kama si mahiri wa KUBAINI ni nini unakihitaji sasa hivi kwa KUKULUNDIKIA MASWALA mpaka ya ambacho kingekuwa KWAKO ni muhimu UKIBALEHE , na kusababisha MWINGINE akipate kabla hata hajavunja UNGO.:-(
NI HILO TU na ni wazo tu MHESHIMIWA!
Hebu Spike Lee joints ituletee Mo' BETTER BLUES ili akina Denzel Washington , Wesley Snipes,.... wamwage- DA BLUES
Au tu Tabi BONNEY arudie- YOU
Au tu TABI BONNEY aendelee tu kubadili kwa -The Pocket
Blah blah blah
Fish cakes
Alas a fish cake.
Yet more fish cakes
Guess what ... yeah ... fish cakes.
The end of the fish cakes