SIMON KITURURU- MAWAZONI
-
Mkusanyiko wa KINACHOFIKIRIWA ambacho kwa sababu MTUZ zinajiheshimu HAKISEMWI.
Posted: February 15, 2010, 11:14 am by SIMON KITURURU
MKUSANYIKO wa VIFIKIRIWAVYO visivyotamkwa,....... labda vina siri ya MATATUZI ya YADUNIA ambayo sio siri yaonekanayo hayana MTATUZI.
KINACHOFIKIRIWA ambacho KWAKO ni chepesi kutamkwa,...
... labda sio chepesi hivyo hata kama sio CHA KIJINGA kwa kuwa kunauwezekano mkubwa kimepitia MCHUJO uchambuao ni YAPI MTU AYAFIKIRIAYO anataka kuyafanya kwako iwe SIRI na aropokacho ni asilimia tu fulani la MROPOKO hata kama kwa kukuficha kitu anakucheleweshea muda wa kustukia staili ya kukaa kwako haimfai kimwana asiye vyaa kificha nyeti ambacho katika swala la kuchunguliwa ni TATUZI.
NDIO, kwa kujiheshimu kunavisivyo tamkwa,...
.... na matokeo yake labda ufikiriavyo ni siri wala SIO SIRI na kwa kukwepa kwako kutamka neno bado sentensi uifikiriayo isiyo na heshima yajulikana na kwa ukimya wako na ufikiriacho NI SIRI wala tatizo lako la kuficha siri zako HALIPO kwa kuwa HUNA SIRI na kwa hiyo halihitajipata ulilengalo TATUZI.
Swali:- Unafikiri kukwepa kwako kutamka baadhi ya maneno kwa kuwa UNAJIHESHIMU hakuchangii mkusanyiko wa SIRI MBOVU duniani?
- Madhumuni ya kukwepa kwako kudakwa unashabikia TOPIKI FULANI HADHARANI au tu kukwepa kwako tu baadhi ya maneno -kama mtu, - unafikiri hufanya ufikiriavyo SIRI kwa wakujuao kama mtu?
- Ukimuona mjamzito hata bila kutamkiwa kwani hujui jina HALISI AMBALO HULITUMII la KITENDO ambacho unafikiria au KUHISI alifanya ingawa mwenye mimba ni bonge la mpole?
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!JUMATATU NJEMA!
Hebu Milton Nascimento arudie-Travessia
Au tu hebu Gilberto Gil alete-Toda menina baiana
Au tuondoke tu BRAZIL na kurudi BONGO NYOSO kupata dozi kutoka kwa USWAZI waongelee-True Love
-
Madhara ya kufikiria VITU bila SABABU,....
Posted: February 15, 2010, 10:39 am by SIMON KITURURU
..... unaweza KUJIKUTA unastukia mpaka yasiyo KUHUSU.:-(
Ingawa KUFIKIRI ni bonge la shughuli ambalo mara nyingi wala halihitaji SABABU,....... matokeo yake MTU waweza jikuta unayapa umuhimu YASIYO na UMUHIMU kwa kuwa tu UNAMIAKILI na katika kuitafutia shughuli wabobea katika kufikiria mpaka ya wengine na kutafuta jinsi ya kuhalalisha yasiyo kuhusu YAKUHUSU.
Swali:- Unafikiri UNAFIKIRIA vya kutosha?
- Si inasemekana kuna waliogeuka vichaa kwa KUFIKIRI?
- Unafikiri MADHARA YA KUFIKIRI na FAIDA za KUFIKIRI kipi chema ingawa vyote vyaweza kufanikiwa kutokukupa JIBU?
NI WAZO tu HILI Mkuu!
Hebu binti ya ELIS REGINA , MARIA RITA alete- Encantada
Au tu MARIA RITA aendelee tu na kitu- CUPIDO
Blah blah blah
Fish cakes
Alas a fish cake.
Yet more fish cakes
Guess what ... yeah ... fish cakes.
The end of the fish cakes