SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • MINDSET a.k.a ULE MKAO UBONGO wa ANDUNJE wakufikiri na kukabili mambo ULIVYONG'ANG'ANIA.

    Posted: February 13, 2010, 1:38 pm by SIMON KITURURU
    Jinsi mtu AFIKIRIAVYO kitu ,....
    ....HUATHIRIWA na mkao wa BONGO LAKE  ulivyozoezwa  jinsi ya KUTUMIWA a.k.a MINDSET yake katika MAswala.

    Na aingiliaye swala moja  au kimoja  kitu,... .....waweza kujua staili yake ya KUFIKIRIA MAMBO mengi kwa kuchunguza tu  anavyofikiria  hasa STAILI  na VIGEZO atumiavyo kuongoza MUELEKEO wa anavyofikiri WAKATI  analiingia SWALA.

    MTU anavyofikiria kipya  kitu,...
    ... kuna  VITU VYA ZAMANI  ambavyo UBONGO ULISHAVING'ANG'ANIA  ambavyo  alishawahi kuvifikiria au  KUFUNZWA na kuviamini ndio kweli  ambavyo vinachangia  MKAO WA FIKIRA za  MTU katika vitu VIPYA kitu kisababishacho UDHAIFU au UMADHUBUTI  wa  staili ya kukabili fikra ya jambo jipya ambayo mara nyingine haihitaji kuoanishwa na la zamani ambalo liko ubongoni  SWALA.



    Swali:
    • Si unajua  BONGO lako likisha unganisha USIKU wa GIZA na UCHAWI  makaburini unaweza kusahau wajifichao makaburini  wanaweza kuwa ni MAJANGILI wajiandaao kupora mtu na wala sio WACHAWI?


    • SI umeshakutana na wacha MUNGU wenye akili ambao BADO kwao  ni vigumu kuelewa mtu yoyote ambaye matatuzi ya maswala yake hayahusishi kumcha Mungu au hata kumuomba Mungu kwa kuwa kwao UBONGO ndio ushang'ang'ania staili ya aina moja ya kukabili mambo na hakuna walionalo bila kuingizia ANGLE YA MUNGU  a.k.a  mchepuo wa  Padre au shekhe anasemaje katika swala?

    • Kwani hujawahi kukutana  AU KUSIKIA kuna mtu ambaye kwake BONGE la ugali ndio chakula na hata umpe wali kiasi gani haamini umempa msosi kwa kuwa KIFIKIRA kashaamini hivyo?



    • Kwani humjui angalau  MTANZANIA MMOJA  ambaye MINDSET a.k.a MNG'ANG'ANO wa KITEKENYA  STAILI YA AFIKIRIAVYO  KUKABILI MASWALA umemuaminisha  MWAFRIKA hawezi na MTANZANIA   hajui , ambaye hata awe Mkufunzi wa  CHUO CHA UAFRIKA  ambaye haki ya nani tena HAWEZI kutetea ajuacho HATA AMBACHO NI KWELI  katika UAFRIKA  hasa akibishiwa na Mzungu , Mchina, Muarabu,..... au  Mhindi ? 


    Tatizo la BONGO kukaa mkao fulani tu,.......ndio kisa  baadhi ya MATATIZO YAKO fulani uliyokuwa nayo mwaka juzi labda utakuwa nayo MWAKA kesho kisa tu  hata MWAKA KESHO utakuwa bado unayakabili kifikira a.k.a APPROACH YAKO,....
    ....katika swala kikutumia ubongo itakuwa ileile iliyosababisha ushindwe mwaka JUZI.:-(



    Swali:

    • AU?
    • Unafikiri huna staili moja utumiayo katika kufikiria kila jambo kiasi kwamba kama sasa hivi wewe ni KIBAKA kwa ufikiriavyo lazima ukiwa meneja wa choo cha stendi , Mbunge,  waziri au hata Rais tu wa KIBAHA au PEMBA  zikijitenga kutoka TANZANIA    utaiba tu? 
    • Si unajua kiruka njia sio mavazi lakini kuna mavazi fulani bado yanakufanya ufikirie usiye mjua ni kiruka njia kutokana na UBONGO wako ulivyojifunza yaliyopita NA KUYAKARIRI ambayo sio lazima ni sahihi leo?

    NI HILO TU na HILI  ni wazo tu MHESHIMIWA !:-(




    Au tu Richard Bona abadili kwa kitu- One Minute




    Au tu Richard Bona arudie- EKWA MWATO

  • MZAHA !

    Posted: February 13, 2010, 4:27 am by SIMON KITURURU
    MZAHA ni siriasi,....... kama kiguswacho kwa MZAHA kwako sio MZAHA.


    Na bila kujua mipaka ya USIRIASI,........waweza kukosea na kufikiri aliye SIRIASI analeta MZAHA .:-(

    Swali:
    • Unabisha?


    Kwa bahati MBAYA misingi ya MZAHA wowote ambao ni MZAHA mahiri,...
    ... ni hali halisi yake isababishwayo na kucheza karibu na KITU ambacho kwako sio MZAHA.:-(


    Swali:

    • Unafikiri asemaye ``ACHA MZAHA WEWE´´ mara kibao sentensi hiyo huitoa kutokana na MSUKUMO wa kitu gani?

    • Unafikiri ufikiriaye analeta MZAHA hayuko siriasi na MZAHA?

    NI HILO TU na ni wazo tu MHESHIMIWA!!


    Kama unapenda Jazz kama mie badili kwa John Coltrane katika -My favorite Things



    Au tu Miles Davis aendelee kwa -Round Midnight



    Au tu Richard Bona arudishe Jazz Afrika kwa -Eyando


Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs