SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • OYAAA mliosoma MAZENGO Dodoma!

    Posted: February 10, 2010, 8:19 am by SIMON KITURURU
    Oyaa,.....Naomba niwajulishe rasmi kuwa mail group ya wanaMAZENGO wa zamani imefunguliwa.

    So far kuna members 19 mpaka sasa!

    Gilbdert DedanMike MungureAdelino LifaAsupya NFredddy LiundiVitus MpandaAdoplh KasegenyaZephaniaSimon KitururuJesse KokaSamuel KeenjaSalum SeifMohdyFortune MkonyAmani MashayoAlex NgwanduKweba BulemoMwombeki BareguEbenezer Kimaro.
    Haya wazee...ukitaka kutuma email kwenye group wewe andika :
    Mazengo@googlegroups.com

    Then inabidi kuanza kufanya mkakati wa re-union kubwa hapo mjini.

    So many nice ideas are coming up.....so lets
    get this rolling !

    Kidumu,-Kweba


    Kongoli HAPA ,........kuideku Mazengo ambayo siku hizi ni St John's University of Tanzania.----------------______________________________________------------------------------




    Au badili tu nami kwa kuendelea na I Jahman Levi kama enzi hizo nikiwa MAZENGO katika-Ancient Lover


    Au tu arudie na -JAH Heavy Load

  • TUKO PAMOJA - ila labda KIMAWAZO mwenzio niko CHOONI!:-(

    Posted: February 10, 2010, 7:42 am by SIMON KITURURU
    Kamsemo ; ``TUKO PAMOJA !´´ ......... ni KATAMU kwa kuwa kanawezakumficha asiye PAMOJA NAWE  ULIYENAYE  kwa kukufanya UDHANIE alivyo pamoja na POCHI LAKO  yuko nawe.:-(


    TUKO PAMOJA!,...

    .....LABDA kama MTETO au MSEMO  yasaidia  KUJAZA  tu jazba  ya kuamini  kaudhaifu kako KAKUTAKA KUAMINI uliyenaye ana  HAIBA za kufanya  ni kweli   YUKO  NAWE.:-(
    Swali:
    • Hivi wakati unatamka kale kamsemo `` TUKO PAMOJA´´ si kuna uwezekano kuna siku huwa unatudanganya?

    • Au?
    Ndio ,...... ukiniuliza ntakwambia kuna uwezekano MKUBWA TU  siku nyingine KUWA  uliyenaye pamoja  OFISINI  au DARASANI,..........labda HAYUKO  HAPO na YUKO NAWE  kimawazo GESTI na wala  sio KANISANI .:-(
    Swali:
    • Unauhakika sasa hivi kuwa uko hapo ulipo eti mwenyewe udaiko umeketi kitako  na hauko Mtandaoni?



    NI HILO TU na ni wazo tu hili MKUU!TUKO PAMOJA na ubarikiwe sana tu Mheshimiwa !

    Hebu SOUKOUS STARS wabadili kwa kitu  -SOFIA



    Au tu I Jahman Levi atulize manyanga kwa kukumbusha kitu katika -Master of my Mind



    Autu I Jahman adake kihitajicho ngangari akidakacho katika hii nyundo aiitayo- I want to be free

  • Misingi na siri ya UJANJA WA MTU ni dhaifu ndio maana DUNIANI kuna MJANJA mpaka kwa kutovaa chupi PIA!:-(

    Posted: February 10, 2010, 7:42 am by SIMON KITURURU



    [Tahadhari: Wazo hili linamwendo wa kusuasua kimtiririko!:-(]





    Kitu kidogo tofauti chaweza tafsiri kwa watu MTU ni MJANJA ,...
    .... na kwa wacheza SINDIMBA uchi chaweza kuwa ni kitu kidogo kama TU ni nani ULINGO kauvalia chupi!


    Na kwa wengi siri ya wamstukiavyo MJANJA,........ ni utofauti wake tu na wengine katika MIKAKATI hata kama mikakati yake yenyewe  ifanikishacho ni kwenye mitumba ya suruali kudaka zilizojichanganya HUMO  zilizotumika chupi.:-(


    Misingi ya tafsiri ya UJANJA umtofautishao katika kundi aliye MJANJA,...
    ... yaweza kuwa ni UJINGA wa TAFSIRI ya ni nini UJANJA ndio maana utekelezaji wa JAMBO LILELILE LA KIJINGA hata kama laumiza HATA BILA KUJUA WENGINE kwa kukwepa miundo mbinu ambayo watu wanaitumia kutekeleza jambo LILELILE ,.......kuna watakao APIA ni UJANJA hata kama shughuli yenyewe ni kudaka mteja kwa kumkalia uchi na MODO MJANJA shughuli hiyo kaivulia chupi.:-(
    Swali:

    • Si unajua siri ya misingi ya kimfanyacho MJANJA aonekane ni MJANJA KWAKO  labda ni kasumba zako tu?


    NA kama BINADAMU angekuwa kwa kawaida anaishi MILELE,....
    .... HAKI YA NANI TENA,...
    ....labda WAJANJA wangekuwa ni wale waishio maisha mafupi KWA KUJIUA na moja ya mjanja AMBAYE angesifiwa sana ni yule KATIKA STAILI YA KUFA  alijinyonga:-(

    Samahani kidogo:

    • Lakini si kuna wajanja tuliowapa USHUJAA  kwa KUWA walijiua VITANI ili wasidakwe na adui na kudhalilishwa ?
    • Lakini kwa tafsiri fulani si MAISHA ni vita?


    ....kwa hiyo LABDA  ni UJANJA kukwepa kudhalilika,......... ingawa LABDA bado kama wote WATAKUWA WANAKWEPA kudhalilika ,....

    .....MJANJA  MPYA ,......
    ....atapatikana  KATIKA  WADHALILIKAO  ambaye angalau kabla hajafa anaweza akawa anajulikana KATIKA WALIOFARIKI  na KUFA angalau YEYE  ndiye wa kwanza kujua na kuwa na UZOEFU wa SWALA ZIMA la  ni nini KUDHALILIKA kabla ya kukwepa  kibano na KUFA..:-(



    NDIO ujanja MPYA  waweza kuwa sio KUDHALILISHA wadhalilika,....
    ..... kwa kuwa kama kila MTU anadhalilisha  basi labda imeshafikia kuwa KUDHALILISHA SIO TENA UJANJA  na atakayeibuka kama MJANJA atatokea kwa  wapendwa wadhalilishwao a.k.a WADHALILIKA.:-(
    Swali:
    • Si  inasemekana Rais Obama  kama RAIS wa KWANZA kuwa na baba MWEUSI  Marekani ni mjanja?
    • Si kuna uwezekano Rais Obama kama RAIS ASIYE KUWA WAKWANZA KUWA NA MAMA MWEUPE Marekani bado hilo lilimsaidia UJANJA?


    Ila taka usitake MAISHA ya UJANJA ,....
    ...... ni mafupi ndio maana WAJANJA wa kweli huwa hawakatizii denge SHUGHULI.
    Na ukikosea kutafsiri UJANJA,...
    .... wajanja MAISHANI mwako wanaweza wakawa wala katika UJANJA hawapatii SHUGHULI.:-(



    NDIO,........Misingi  na siri ya UJANJA  WA MTU  ni dhaifu SANA ,.......ndio maana DUNIANI  kuna MJANJA mpaka kwa KUNG'ANG'ANIA faraja za  NEPI  hajastukia BADO duniani kuna jeuri ya chupi PIA!:-(


    Swali:

    • Si inakumbukwa ujulikanao kwa sasa kuwa ni  USHAMBA ni uleule ulioonekana  UJANJA  zamani?
    • Unafikiri unajua  MISINGI ya tafsiri yako ya Ujanja kwako ni nini na imeegemea wapi?
    •  Ujanja unafikiri ni nini?
     Kama unajua kikweli ni nini UJANJA,...
    ....NA  unajua SIRI ya utafsirivyo nani MJANJA,......weye ushatatua moja ya UDHAIFU WAKO!:-(
    Swali moja zaidi katokori:
    • Unafikiri  kujua UDHAIFU wako sio kujiponza pia?






    NIWAZO tu hili MHESHIMIWA!:-(NA nakutakia kila la kheri uwe na uhakika wa kupata  choo leo MKUU!




    Hebu tubadili kwa kumdeku Mjasiliamali-







    Au tu hebu Chick Corea, Bobby McFerrin na Bela Fleck walete kitu -Spain





    Au tu OUTKAST warudie- Rosa Park


Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs