SIMON KITURURU- MAWAZONI
-
Kama ampendeaye mtu TABIA bado naye atahitaji SEHEMU ZA SIRI ili penzi litimie!:-(
Posted: January 31, 2010, 7:00 pm by SIMON KITURURU
[Tahadhari: Wazo limepinda na LINAWEZA kukukwaza kama mtoto au tu kama weye ni Mzee wa kukwazika!:-(]
Kuna wagundulikao kuwa pamoja na kudai wamempendea mtu SURA au tu nyonyo,...
....bado walengacho na wahitajicho kutoka kwa mwenye HIYO sura nzuri wala sio HIYO sura na labda ni zake tu SEHEMU zenye NYETI.:-(
Na kwahiyo mara nyingine kumbuka kama hutachukulia hili kama ONYO,...
....kuwa pamoja na kwamba wako WASIFIAO HARUFU YA CHAKULA ambao hudai wamevutiwa na harufu ya chakula katika PENZI LAO LA HICHO CHAKULA,....
... lakini KUNA UWEZEKANO MKUBWA mapenzi YA harufu ya chakula kwa apendaye kula au MWENYE NJAA ni danganya toto kwa kuwa kwa yoyote mwenye njaa anajua kiliwacho katika chakula si HARUFU na afuataye harufu hata ya ubwabwa wa msibani ni KUGIDA MSOSI na sio KUSIKILIZIA HARUFU ndio SWALA NYETI.
Swali:- AU?
- Unauhakika kikufanyacho umpende mtu sio CHAMBO tu chakukurahisishia kukabiliana na vipengele vyake huyo mtu ambavyo labda vinanuka na vinasura mbaya ambavyo ndio unavihitaji katika huyo MTU?
- Unafikiri harufu ya wali sio tu msaada KWAKO wakukuwezesha ule wali ingawa mahitaji yako yangetimizwa na MATOKE au ugali wa mhogo?
Ndio....
.... labda kuvutiwa kwako na SURA au tu shepu ya matako ya mtu,...
.... ambavyo UKIFIKIRIA labda katika huyo mtu hivyo ndivyo vipengele vyake ambavyo hutavitumia na huna mahitaji navyo,...
... NI DALILI ya udhaifu wa UZURI wa uvihitajivyo katika huyo mtu vikiwemo TABIA YAKE au tu sehemu zake uzihitajizo katika shughuli nzima ya KUUJAZA ULIMWENGU a.k.a kuzalishana hasa kama SEHEMU HIZO huzitumii kimaridhawa kama VYOMBO vya burudani.:-(
Swali:- Unauhakika ni nini hasa umpendeacho wako MPENZI?
- Unafikiri katika kila PENZI hakuna lako hitaji ambalo unalipata kwa huyo mpenzi ambalo halina uhusiano na kifanyacho MPENZI kwako anavutia?
- Unafikiri mapenzi hayana UBINAFSI na ni kweli unampenda tu MTU kwa roho yote bila ubinafsi kwa kuwa tu ANA ROHO NZURI na hakuna chochote binafsi upatacho KIFARAJA ?
Ndio,...
... kuna MAPENZI ya aina nyingi,....
.... kwa mfano yale ya NDUGU kwa NDUGU au tu MTU na MBUZI.
Ndio,....
..... UKIFIKIRIA waweza kustukia hata MAPENZI ya mtu na MBUZI au KUKU aliyenona,....
... yawezekana ni DANGANYA TOTO hasa kama ASIFIWAVYO MBUZI na KUKU ni kimvutio WA MUONEKANO kama nia ya kuwafuga MBUZI au KUKU hao inalenga sana cha binadamu KITOWEO kuliko kupamba ya binadamu DUNIA.:-(
Swali:- Unauhakika MAPENZI yako kwa NDUGU yako nayo kiyakupavyo faraja , KWAKO hayana UBINAFSI ?
- Wakati kuna adaie amempendea MTU mwanya AU MATEGE,-kama sio tako,- unafikiri MWANYA au MATEGE ya apendwaye unateleza kitu gani muhimu katika PENZI la hao wapendanao?
NAKATIZIA HAPA katika hili WAZO Mheshimiwa nikiamini unaelewa hili ni wazo tu na kulibishia RUKSA!:-(
Hebu twende tu tena Ivory Coast Meiway aendelee na -Voila String
Au tu MEIWAY aweke tu na-DJ Tassouman
-
ANASA,...
Posted: January 31, 2010, 6:40 pm by SIMON KITURURU
... labda ni hata kunywa UJI wakati huna HITAJI la UJI.:-(
Na kwahiyo,...
....wakati KUMBIKUMBI wanakidhi mahitaji yaleyale ya SENENE ghali,...
.... LABDA kula SENENE ni ANASA pia.:-(
Swali:- Au?
Ndio,...
... anasa hutofautiana kutoka MTU na MTU,....
.... na anasa kwa wengine LABDA ndio maisha ya kawaida kwako.:-(
Swali:- Si kuna uwezekano kuwa na chupi zaidi ya mbili ni anasa pia, au unafikiri IKIBIDI chupi tatu hazikutoshi?
- Unafikiri kama UNA AKILI kufanya ujinga bila kutumia akili sio ANASA?
Ni wazo tu HILI Mheshimiwa na kumbuka blogu hii wala sio BIBLIA au Korani kibusara!:-(
Na moja kwa moja ngojea twende Nigeria Nkem Owoh aonye madhara ya kwenda shule katika - School Na Good Thing
Au tu twende Ivory Coast Meiway abadili hali ya hewa kwa kitu- Koundoum Beat
-
Jamani jamani SHIKAMOO MPENZI![Sentensi HII imebaniwa pua na demu mwenye mafua.:-(]
Posted: January 30, 2010, 3:21 pm by SIMON KITURURU
Na kuna watoao SHIKAMOO mpenzi ,....
... kama mkakati wa KISIRI wakumuambia MTU kiumri amezidi sana na KWA HILO kukwazwa asiombe PENZI.
LAKINI kwa kuwa HATA kama kwa UMRI ni mkubwa MPENZI,...
.... kumbuka lake laweza kuwa ni CHANGA na ndio kwanza limezaliwa tu PENZI.
Swali:- AU?
SHIKAMOO KIPENZI,..
... yaweza toka kwa AHESHIMUYE lako PENZI.
Na kwa kuwa anakua KIPENZI,...
...umri wako na wake waweza kuwa UNAANZA kufanana kama kipimo ni PENZI.
Kwa kuwa KIPENZI,....
.... wakati wengine PENZI LAO linakua, wapo ambao WANAPIGA MAKITAIMU kipenzi.:-(
Kwa kuwa KIPENZI,...
... wakati wengine PENZI LAO LINABALEHE, wapo ambao PENZI LAO linakufa MPENZI.
Na SHIKAMOO MPENZI,....
....inaweza kufikia kumaanisha tu``SHIKAMOO MPENZI bila PENZI´´ kwa kuwa labda ni kweli kwa kuwa PENZI HUZALIWA, ....
... basi labda pia HUKUA, hudumaa, hunywea, na KUFA tu kama vingine vizaliwavyo MPENZI.
Swali:- AU?
- Hivi SHIKAMOO maana yake ni nini vile?
- Sasa hivi ni MPENZI au PENZI lake listahililo SHIKAMOO?
- Tukiachana na PENZI na kuingia kwenye SALAMU TU,- NI mara ngapi weye MTZ utumiaye SHIKAMOO kama salamu huwa unamaanisha hiyo SHIKAMOO KISALAMU kwa umsabahiye?
NI wazo tu hili MKUU na NIMELIACHA ingawa kwako ni RUKSA kulifikiria kivyovyote vile UPENDAVYO Mheshimiwa!
SHIKAMOO basi!
Umefurahi eeh!
Jumamosi NJEMA!
Au hebu Frankie Paul abadili hali ya hewa Kijiweni kwa kumuongelea - SARA
Frankie Paul alete tena -SHUB eeN
Au tu Delinquent HABITS na Hurricane G wabadili zaidi tena kwa -Underground Connection [Tahadhari: lugha watumiayo haijaoshwa mdomo!:-(]
-
Kabla ya MUDA WAKO wa kueleweka KUFIKA, labda AKILI ZAKO na UFIKIRIACHO ni ukichaa kwa WENGINE!:-(
Posted: January 30, 2010, 4:12 am by SIMON KITURURU
Kuna watu mawazo yao yako mbele ya MUDA,....
..... na sasa hivi hawaeleweki ni nini WAZUNGUMZIACHO.
Swali:- Au?
- Unauhakika MAWAZO YA NYERERE ya siasa ya ujamaa na kujitegemea hayatakuwa ni MAWAZO na siasa inayotekelezeka mwaka 3000?
Na walio KIMAWAZO mbele ya MUDA,....
.......jamii inaweza kuwahukumu sasa hivi KAMA wafikiriacho wakikigeuza kuwa ndio WAKIZUNGUMZIACHO.
Swali:- AU?
Na ni mambo mengi katika huu muda,....
...... hayaeleweki ukiyachagua kuwa ndio UFIKIRIACHO,.....
.....na LABDA nikuanzia;- DINI,
- NDOA,
- SIASA,
- WOGA WAKO,
- ni nini LAANA,
.... au TU ni mpaka NI NINI ni aina ya gwaguro au chupi za wajanja,...
.... NA unayaona YANALETA MAANA kwa kuwa TU UNAFUATA MKUMBO WA watu wengi UWAHESHIMUO, utakao kuwa kama wao,NDUGU, au tu WALE TU udhaniao wameukata au tu wanaelimu kwa kuwa unajua waliposomea .:-(
Swali:- Au?
- Unakumbuka UKWELI wa jambo hauathiriwi na IDADI ya watu na labda ni kweli KWELI ya kitu mara kedekede waijuao ni wachache?
- Unauhakika na sababu za ujanja au tu mambo tu ya kileo kuleta maana kwa BINADAMU leo?
- Unauhakika mambo ya kileo ya mpaka ya JUHUDI ZA WAJANJA kumvalisha mpenzi pete wakioa YANALETA MAANA wakati inajulikana pete haizuii mpenzi kuonjwa au kuonja LAWALAWA NYAMA MTAANI ingawa anakitumbua nyumbani?
- Unauhakika wakati wa TANZANIA kupata uhuru haukuwa ni muda wa KAMBONA kuwa RAIS halafu wakati wa Rais MKAPA ndio ungekuwa wakati wa NYERERE?
Tukiachana na hilo,....
... naamini hata kisanaa TANZANIA ,...
... itafikia muda FULANI ndio ITAKUWA UJANJA kwa watu kustukia ni kwanini MORIS NYUNYUSA na ngoma ZAKE au tu Dr ZAWOSE ni mahiri kwa kuwa sasa hivi hawaeleweki kwa kuwa wafanyacho sio BONGO FLEVA.:
Tukiachana na hilo,....
Swali:- Si unakumbuka wengi wape kama tu zilivyokuwa demokrasia tuzisifiazo moja ya matunda YAKE ni kupotea kwa wengi hasa kwa kuwa NI KWELI lifuatwalo na wengi haina maana ndio usahihi wa hilo jambo?
- Unauhakika IKIWA kura za wengi TANZANIA ni za wasio elewa hata ni nini wanakipigia kura maana yake hao wengi ndio wapatiao jibu la matatizo ya TANZANIA?
- Hivi wewe MKUU unaeleweka?
- Hivi Mheshimiwa wewe HUMJUI HATA MTU MMOJA ambaye ni wale wafuatao mkumbo wa jambo kwa kuwa ndilo lielewekalo AU TU LIFUATWALO na wengi?
- Si unajua moja ya siri la urahisi wa kitu kuwa na wafuasi wengi ni MDHANIO wa urahisi wake kueleweka wakati tunajua MATATUZI ya mengi si rahisi?
- Si unajua wazo lako lisilo wezekana leo labda tu muda wake haujafika?
- Si wazo lihangaikiwalo NA MAARUFU leo linaweza kuwa ni wazo lililopitwa na wakati?
Naacha na ni wazo tu hili MHESHIMIWA !:-(
HEBU tu Fela andelee kwa kuleta another underground SPIRITUAL GAME kwa kitu - Beasts of no Nation.
Au tu FELA KUTI aendeleze SPIRITUAL GAME kwa hiyo hiyo- Beasts of no NATION
Au tu Phil Collins atulize kwa NENO kueleweka kirahisi kwa - Another day in Paradise
-
Kwa kuwa hata SAMAKI aringe vipi BADO ukweli uko palepale kuwa ana SHOMBO!:-(
Posted: January 29, 2010, 10:29 pm by SIMON KITURURU
Samaki weye kisura, na kwa ladha ni mtamu
Napenda yako sura, na kukugida mtamu
Kwa protini kinara, kukukaanga na hamu
Ila samaki kipenzi, we una harufu mbaya!:-(
Samaki we unanuka, vundo lako sina hamu
Harufu yako kunuka, shombo lako sina hamu
Na samaki unanuka, kwenye ya wali karamu
Hivi samaki kwanini, wanuka ila mtamu?:-(
Na siri yako nyingine, weye una miba ndani
Nje wapendeza vingine, kwa miba kuficha ndani
Wanikumbusha wengine, roho zao watu ndani
Kweli kipenzi samaki, wanuka bila kuvunda.:-(
Swali:- Hivi unapenda kunukia harufu ya samaki?
- Hakuna mtu KIROHO akukumbushaye samaki, kwa nje tamu ukimjua undani roho miba?
- Unafikiri samaki angenoga zaidi kama angenukia kama manukato?
- Unafikiri ni kwa nini samaki hunuka kama samaki?
- Unauhakika Mtu ananukaje ikiwa watu hutofautiana hata harufu ya ushuzi?
Ndugu Samaki;...
Kwa kunuka mwanawane ,....
..... wewe wanipagawisha. :-(
NIMEACHA na ni wazo tu dhaifu HILI Mheshimiwa NA halikuhusu kama wewe ni MPENDA SHOMBO YA SAMAKI na kwahiyo USIKONDE!
Nakutakia IJUMAA na WIKIENDI njema MKUU!
Hebu Keith Sweat abadili kwa kurudia -Twisted
Au tu Peter Tosh apoze mchecheto na kukumbusha- The poor man Feels it
Au tu Peter Tosh akumbushe tu kuwa tupo watu kama mie Simon Kitururu tunaugua- Reggae Mylitis
-
Udhaifu wa KUONA kabla ya KUPAPASA,....
Posted: January 27, 2010, 3:38 pm by SIMON KITURURU
.....kwa mwenye macho hapa DUNIANI ,....
..... ni bonge la udhaifu uponzao WENGI na ambao umesababisha mengi ikiwa pamoja na ya ;....- Ubaguzi wa rangi
- Baadhi ya embe dodo zisitomaswetomaswe
- Watu kuogopa giza na kuchagua kuwa nguvu za giza ni za shetani na za Mwanga niza MUNGU
Na unaweza kubisha, lakini KUONA pamoja na mazuri yake yote hapa DUNIANI,...
.... huleta udhaifu wa KUSIKILIZA na KUJISIKILIZA, kitu kisababishacho waonao wengi kusahau mapungufu ya wakionacho hasa kimtazamo wa muda mrefu KISA WAMEKIONA , na wamejiaminisha HICHO kitu kwa sasa NI kidude kizuri.:-(
Swali:- AU?
Na udhaifu wa `` KUONA KABLA´´ uathirivyo ,....
... usipoangalia waweza kukufanya ujiaminishe mwenyewe kuwa EMBE DODO ni TAMU kisa MUONEKANO WAKE na kusahau kuwa KUONA EMBE DODO na hata KULITOMASATOMASA embe dodo bado sio kipimo kizuri cha utamu WA EMBE DODO kwa kuwa ni LADHA ambayo huhitaji embedodo LIONJWE kwanza ndio kithibitisho cha UTAMU kipatikane,.....
..... na hapo ni kama hatufikirii MANUFAA YA EMBE DODO ni virutubisho vyake na wala sio muonekano WAKE , ..
....na wala sio hata ule wake UTAMU.:-(
Swali:- AU?
Na kuna UDHAIFU WA KUSIKIA kabla ya KUONA.
Udhaifu HUO wa kusikia kwanza pamoja na mazuri yake yote DUNIANI,...
... huweza kuathiri kwa ;...- Kudhoofisha makali ya kushuhudia kwako
- Kukuandaa woga
- Kukufanya udhani unajua ukweli kuwa Rais Mkapa Fisadi
- kukuandaa kuamini Maimuna havai chupi
....au tu kunaweza kukusababisha upende MTU au tu SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA kabla ya KUTHIBITISHA MTU HUYO au TARALILA HIYO ana/ina mbivu zipendekazo KWA VITENDO kwako.:-(
Ndio ,...
...sikatai kuwa ``UKISIKIA kabla ´´ unaweza kustukia ni nani KIRUKA NJIA au tu KIBAKA,....
..... au tu KUJIANDAA tu na UCHOCHORO kisa umesikia kuna majangili hapo,..
... au tu kuna MBUYU wenye majini kwa hiyo usipige teke vifuu,....
... na kwa hilo nasikia kuna wapatao faraja.
Na ,....
.. sikatai kuwa nasikia kuna wapatao faraja za ``KUSIKIA KABLA ´´ wengi ambao wanasaidia sana dunia hii iwe kama ilivyo KWA BAADHI YA MAZURI YAKE kwa kuwa tu WAMESIKIA BILA KUONA na sasa hivi WANAJIANDAA tu na;...- kwenda MBINGUNI walikokusikia tu
- kutofanya UASHERATI kwa kuwa wamesikia ya UKIMWI
- kuwa wafuasi wa siasa za CCM na kufanya TANZANIA tulivu
- kuwafanya waogope GIZA na kufanya usiku uwe mtulivu
....ila tusisahau tu kuwa moja ya UDHAIFU wa ``KUSIKIA kabla´´ ya kushuhudia ni kwamba faraja yake iko tu katika UWAZO(imagination) UBONGONI mwa mwenye kusikia tu bila kushuhudia kitu ambacho kirahisi husababisha;...- WATU kuhukumu watu kwa kusikia tu
- Watu kuhukumu vitu kwa kusikia tu
Swali:- Si inasemekana kuna waliosikia tu na kudhani ULAYA bomba kweli na mambo yake ni mswano sana tu?
- SI kunawasikiao tu na kung'ang'ania ni kweli fulani Malaya?
- Hivi unafikiri VIPOFU wa macho HAWAONI?
Ndio,...
...pamoja na yote mazuri,...
...KUNA UDHAIFU utokanao na ``KUONA kabla ya KUPAPASA´´ na ``KUSIKIA kabla ya KUONA na KUPAPASA´´,....- ... kwa hiyo UKIONA, - kumbuka KITU kina zaidi ya UONACHO na kwahiyo hata kama ni lako LIMCHUMBA lionekanalo NONO kimuonekano, ukiingia kichwakichwa labda lina UKIMWI na kwa hiyo ni vizuri ujue kabisa unalipenda LIMCHUMBA na umelipenda na MDUDU WAKE ili penzi lako lililo sababishwa na KUONA tu MBIVU inaelea, linoge na kusaidiwa kudumu kwa vitendo pia KWA KUWA unalijua LIMCHUMBA kwa zaidi ya lionekanavyo LIMCHUMBA.
- ...kwa hiyo UKISIKIA kabla ya KUONA kumbuka KITU kama tu GIZA liogopwalo, si lazima ni kweli GIZA linatisha hivyo ukikumbuka hasa isemekanavyo na ISHUHUDIWAVYO na mpaka NA watoto wengi wazuri uwaonao MTAANI ambao WENGI WAO walitengenezwa na wazazi wao vizuri GIZANI kwa kitendo kilichoenda shwari tu gizani na kwahiyo tu kumbuka aliyeoanisha GIZA na vitu vibaya si lazima aaminike kwa kumsikia tu kwa kuwa MABAYA mengi hufanyika kwenye MWANGA na kwahiyo labda nguvu za shetani ni NGUVU za MWANGA na wala sio NGUVU za GIZA.
Swali:- Au?
Tubadili kwa kwenda MALAWI kwa Lucius Banda alete - Tina
Au twende tu na MOZAMBIQUE ninmuache mwanamuziki mwingine aliye uawa Afrika Kusini na waliotaka kumuibia gari miaka michache iliyopita kwa jina GITO
-
Kwa kuwa kuna WAONGEAJI watumiao sauti ili KUKAA KIMYA!
Posted: January 27, 2010, 5:56 am by SIMON KITURURU
Wengi waongeao haki ya nani hawasemi KITU,...
....ndio maana usitishike na stori ndefu kwa kuwa kisemwacho chaweza kuwa kinajaa tu MSTARI.
Na ni kipaji kuwa KIMYA huku unaongea,...
..... na ajuliaye hicho kipaji NI mpaka baada ya kuagana naye ndio utastukia na kuanza kujiuliza:- Hivi jamaa lilikuwa linasema nini vile?
- Hivi Mheshimiwa kunachochote kweli alichokuwa anajaribu kutuambia?
... kwa kuwa watumiao SAUTI kukaa kimya na wenye kipaji KWA HILO wakati unawasikiliza unaweza ukajiaminisha mwenyewe kuwa kuna kitu unapata katika waongealo.:-(
Na KWA MTAZAMO MWINGINE labda ukweli ni kwamba,...
.... ukichunguza utastukia kuwa tunaishi katika JAMII ambazo hufunza watu kuongea kwa SAUTI wakati huo huo katika baadhi ya mambo kukaa KIMYA.
Na labda ni kweli ukiniuliza miye ,....
.... KWA ASIYELAZIMIKA KUONGEA NAWE AKIFIKIA kuongea nawe ,....
huyo kashapitia UCHAGUZI wa afikiriacho kinafaa kukuongelesha, MANENO atakayotumia asije akakukwaza weye MSWAHILINA kwa maneno ya KILOKOLE au tu hata jinsi ya KUKUONGELESHA ustukie mahaba wakati neno mahaba limekaliwa KIMYA.
Swali:- Si unajikumbuka tu WEWE MWENYEWE wakati unaongea na MTU ukwepavyo baadhi ya MANENO, MAMBO au tu vitu fulani kimsisitizo, KIKUVIDOKEZEA au hata tu ugusiavyo baadhi ya mambo ili tu kufanikisha kukalia kimya baadhi ya mambo?
- Si unajua stori yako ya kufeli mtihani iliyoko kichwani mwako itofautianavyo na umsimuliayo Mzazi?
- Ukikutana na mtu si unastukia ni mambo mangapi ya kupitiayo kichwani kuhusu huyo mtu na wawezakung'amua ni asilimia ngapi ya mambo yamuhusuyo huyo mtu ambayo huyaongelei?
- Kwani unafikiri kila unavyoongea kuna kitu hasa unachosema?
NI wazo tu HILI MKUU!
Samahani Caiphus Semenya yuko mawazoni tena na kitu - Angelina
Pat Shange naye arudie- Sweet Mama
-
UPROFESA wa nukuu za mstari mmoja MMOJA!
Posted: January 27, 2010, 2:24 am by SIMON KITURURU
Napenda kunukuu hasa nikitaka kulazimisha hoja nayoshindwa kuijengea HOJA.:-(
Na nawajua wapendao kunukuu kwa kuwa hoja yao ili iaminike kama ni hoja kuna WAWASIKILIZAO wapendao kusikia angalau jina maarufu ambalo kimtazamo lakubaliana na ya mdau mpya HOJA.
Na haki ya nani kama hoja yako ni ya magimbi,...
... na ukaingizia`; ``NA Yesu alisema ......,´´
...... halafu ukamalizia na hoja zako za magimbi ni matamu kuliko Mihogo kuna watakaosita kukubishia KUHUSU UTAMU WA MAGIMBI ingawa WANAPENDA MIHOGO kisa umemnukuu tu Yesu katika ya kutetea magimbi HOJA.
Na kama ni siasa za Tanzania za kujisifia unakula tu magimbi ...
... na ukaingizia na`` Nyerere alisema.....,´´
.... halafu ukamalizia na kula UBWABWA PEKEE MBELE YAO wakati kwenye SINIA KUNA MAGIMBI PIA kuna ambao hawatasita kukuunga mkono na HOJA YAKO kuhusu magimbi NDIO CHAKULA PEKEE kifaacho kuliwa wakati wanashuhudia wewe unalenga na unaonyesha kwa vitendo ni mtu wa UBWABWA kisa umemnukuu Nyerere na umeingizia magimbi katika HOJA.
Ndio ,...
...kunauwezekano kuwa nimepitiliza kudhaifisha kiunyambulisho hoja ya magimbi hapo juu !:-(
Swali:- Si unakumbuka lakini nukuu za mstari mmoja miwili katika STORI ya Bata Mjamzito inaweza ikafiti vizuri kuzungumzia au tu kujenga madhari kuwa stori ni ya mbuzi /BEBERU lisilo basha?
- Kama wewe ni Mkristo kwani hujawahi kufanikiwa kusikiliza mahubiri yaliyojengewa hoja na baadhi ya vifungu vya BIBLIA halafu baadaye ukaendelea kusoma vile vifungu na kugundua wala haviendani na hoja viliyoisaidia wakati mchungaji anashuka mahubiri Kanisani?
Ndio,....
... tuna nukuu na baadhi ya nukuu haki ya nani lazima umtishe mtu kuwa wewe MSOMI SANA kama ukipatia kunukuu,.....
....na si utani kuna mpaka MAPROFESA wa nukuu za mstari mmoja mmoja na katika kuipamba hoja utakuta mtu anaweza kukusimulia stori hata ya MBWA kiruka njia halafu akanukuliwa kuanzia Plato, Socrates, Nyerere, Rais Mkapa , Askofu Mkoba, mpaka MIMI katika kukuelezea kwa nini mbwa yule hajapata bado gono na mbwa wenzake wanafikiri ni mchoyo wa MIFUPA katika jamii ya MBWA katika tu kujenga HOJA.
NAACHIA HAPA nikiamini unajua hili ni wazo tu na labda halina hata UKWELI!
Na katika nukuu za tishatoto za ghafla hapa nami nanukuu bila sababu maalumu;
~Andre Gide akidai ´´Believe those who are seeking the truth. Doubt those who find it.´´
Na ~Alfred Lord Tennyson adai :``I am a part of all that I have met. ´´
Na ~Baba Ram Dass adai ``Only that in you which is me can hear what I'm saying. ´´
Swali:- Umestukia ni hoja mamilioni mangapi nukuu hizo zaweza kuingizwa bila mtu kujua wakati wanaziongea NILIOWANUKUU walikuwa wanaongelea nini?
Hebu tuamishwe kimawazo na RZA arudishe ya dunia katika -La Rumba
Au tu Zain Bhikha arudishe busara za Mungu katika- Allah knows
-
ASILI ya MIIKO kwangu, UHASISI wa ni nini MWIKO kwako!:-(
Posted: January 26, 2010, 11:15 pm by SIMON KITURURU
Asili ya vingi ambavyo ni mwiko kwangu ni KUTISHWA ,...
... na vingi ambavyo bado kwangu ni MWIKO na ambavyo sijatafuta sababu zake ni kwanini ni MWIKO, sababu za hiyo miiko bado SIJAPATA.
LAKINI pamoja na sababu ya MWIKO yaweza kuwa ni kutishwa BADO ni MWIKO !:-(
Na MWIKO kwako labda sio MWIKO kwa wengine hata kama hukutishwa,...
... na kwa hilo ukitafuta sababu ni kwanini , sababu UTAPATA.:-(
LAKINI pamoja na sababu ya MWIKO KWA WENGINE yaweza kuwa sio kutishwa BADO ni MWIKO !:-(
Na kwa wengine ni MWIKO kula KITIMOTO, au KUTAHIRIWA ,..
... wakati wengine MWIKO ni POMBE kama Uarabuni , au wengine ilivyokuwa sio mwiko katika mila baadhi kucheza ngoma matiti nje kama TANZANIA, au tu RUKSA bangi kidogo kama Uhindini,...
....ingawa NA kwa wengine Msichana mkubwa kuoga uchi na baba yake ni RUKSA na sio MWIKO kama Ufini, au tu Mwanamume kumuoa Mwanamume mwenzako ilivyo RUKSA na sio MWIKO Sweden ,....
... na ukitafuta sababu , UTAPATA.
Swali:- Unafikiri asili ya MIIKO ambayo kwako ni MWIKO ni nini?
- Unafikiri kushika MAKAA YA MOTO wakati wewe na kila MTU wanajua MOTO UNAUNGUZA ni mwiko?
- Unauhakika MIIKO ya wengine kwako inaleta MAANA?
- Unafikiri MIIKO yako kwa wengine INALETA maana?
Ndio KILA MWIKO unaasili zake,....
..... na labda kama kuna asiyevunja MIIKO basi kila MWIKO itafikia hakuna ajuaye kwa uhakika sababu ZA UZALIWA wake kitu ambacho kitasababisha KUNA KIZAZI CHA UMMA NA KIJIKO kitahitaji kuwe na PROFESA afanyaye utafiti wa KUVUMBUA ni kwanini baadhi ya JAMII ziliamua ni mkono wakushoto ndio wa kuchambia mavi na kufanya baadhi ya jamii kufanya ni MWIKO kuutumia MKONO HUO wa KUSHOTO kumsalimia mgeni au kuutumia kuchovyea tonge la UGALI WA YANGA kwenye bakuli moja la maharage swafi ya nazi,- na yote hayo IKIWA TU ni katika juhudi za kujaribu kuelewa MWIKO.:-(
Na ni kweli MWIKO unaasili yake,...
... na baadhi ya miiko ya hapo baadaye labda MWASISI ni wewe na tabia zako!:-(
Ni wazo tu hili Mheshimiwa USIKONDE!
Na hebu R. Kelly abadili kwa-Bump & Grind
Au tu Wu Tang Clan warudie- The heart gently Weeps
-
STAREHE ya kutumia MUDA BINAFSI kuhukumu WENGINE na maisha yao BINAFSI!
Posted: January 25, 2010, 8:31 pm by SIMON KITURURU
Ni kweli,...
... kunyoshewa vidole hainogi kama KUNYOSHEA wengine vidole hasa kama kilengwacho ni KASORO.
Na kunyoshea wengine vidole KUHUSU MAMBO YAO BINAFSI inasaidia sana kupunguza muda WA mtu kujichunguza mwenyewe BINAFSi hasa kama lengo ni kukwepa kujistukia zako KASORO.
Na mtu asipokuwa muangalifu anaweza akafikiri kutambua kasoro ni kitu rahisi mpaka itakapotokea AKAFIKIRIA na kustukia ukiwadadisi watu utagundua karibu kila kitu ukionacho hakina kasoro kuna AMBAO wanakikosoa kwa KASORO.:-(
Na haki ya nani uonacho kina kasoro kama tu MATEGE,...
.... kuna apendaye MTU kisa matege mpaka KWENYE ndoto zake za kikubwa za MCHANA ofisini WAKATI YUKO MACHO, ndoto zile za uasherati za kuombea siku moja afanikiwe kupata nafasi ya kufanya dhambi ya uzinzi na MTU mwenye bomba la matege ambaye atamsalimisha kutoka kwa wanaomfuatafuata KATIKA MAISHA HALISIA wenye miguuu imenyoka kama fito za kujengea kigenge cha kuuzia nyanya na vitunguu MIKESE,- na ni miguu iliyonyoka NDIO kitu ambacho kwake ndio KASORO.:-(
Swali:- Unafikiri kama mtu ana BONGE la pua kubwa kiuwiano na SURA YAKE imsaidiayo kupumua vizuri na kudaka harufu bwelele NZURI au tu za chooni, huyo anakasoro ya pua au ni yule mwenye pua UJAZO wa kawaida AMBAYO HAINUSI VIZURI na inazingua upumuaji , na ambayo inasababisha astukiwe ZAIDI kwa masikio kama Rais Obama ndio mwenye KASORO ya PUA?
- Hufikiri KASORO kwa asilimia kubwa ambazo SI UGONJWA zilalamikiwazo ni za KUBUNI kwa aliyenacho ndio maana mwenye aibu kwa midomo minene hushangaa watu wakilipia kujazwa midomo ili LIPS zijazie tako?
Ndio,....
.... kuna watumiao nyenzo ya KUHUKUMU WENGINE katika kuepusha wengine kuwachunguza yao yaliyojaa KASORO.
Na kwa bahati mbaya au NZURI, kwa ung'eng'e wanadai `` IT WORKS!´´,...
... kuhukumu wengine KWA KIPINDI KIFUPI inasaidia sana kukwepa KUJIHUKUMU wewe MWENYEWE.
Swali:- Wakati unahukumu wengine si unakumbuka kama kuna lako lihitajilo hukumu wala haliondoki na liko tu lakusubiri?
- Je, umefanikiwa kuhukumu mtu leo na kusahau kujichunguza yako yenye KASORO kwa muda leo?
Hebu Aaliyah abadili hali ya hewa kwa kurudia- One in a Million
Au tu Aaliyah adai -Age ain't nothing but number
-
UMEKIFIKIRIA unachokifikiria LEO?
Posted: January 24, 2010, 5:02 pm by SIMON KITURURU
Jinsi unavyofikiria ,....
.....HUWEZA athiri UNACHOKIFIKIRIA lakini.:-(
Swali:- Ni mangapi uliyoyafikiria jana AMBAYO HULAZIMIKI KUYAFIKIRIA LEO ambayo unakumbuka kuyafikiria tena leo?
NI HILO TU!:-( -
MANUFAA ya MAUMIVU!
Posted: January 24, 2010, 5:11 am by SIMON KITURURU
NDIO,....
...KUUMIA INASEMEKANA hatupendi.:-(
Swali:- Unafikiri bila kusikia maumivu unauhakika usinge haribu hata kikojoleo chako kwa kukiingiza vijiti au ANGALAU kuchoma TU tako lako kwa kukalia jiko la mkaa?
- Unafikiri bila maumivu maisha au hata vitisho vya JEHANAMU vingeleta maana katika kukudaka hofu?
- Hivi unajua adaiye roho inauma huwa anamaanisha anasikilizia maumivu wapi vile?
- Unauhakika hupendi kuumia?
BADO nafikiria hili swala MHESHIMIWA ingawa kunihukumu RUKSA!.:-(
BAADAYE Mkuu!
Au tu ngojea katika kubadili hali ya hewa KIJIWENI hapa Tabu Ley Rochereau alete - Mokolo Nakokufa
FRANCO & le T.P. O.K. JAZZ warudie - C'est Dur la Vie d'une Femme Célibataire
Au tu Too Short abadili kwa -The Ghetto
Na Skee Loo arudie- I wish
-
Jinsi watu watofautianavyo katika kusikia TUSI!
Posted: January 24, 2010, 4:11 am by SIMON KITURURU
Kunauwezekano kabisa UKIFIKIRIA,....
... utagundua UBUNIFU wa jinsi ya kustukia ni nini hasa ni TUSI haupo katika JAMII .:-(
Swali:- Huwa unafikiria ni nini hasa siri ya misingi ya fikira zako za UTAMBUZI WAKO WA ni nini hasa ni TUSI?
- UKIFIKIRIA unafikiri binadamu wenye busara na akili UWAJUAO HUWA wanapatia tusi la kulikasirikia?
Kuna uwezekano kabisa UKIFIKIRIA,....
..... utagundua labda tafsiri ya tusi katika mawazo ya wengi ni potofu ndio maana hawastukii TUSI HASA ila wanasikia WALILOFUNZWA KUTAFSIRI TU kuwa ndio tusi katika jamii NA JAMII ,....
..... ambalo laweza kuwa kwa mfikiriaji wala SIO TUSI na ni jinsi tu ya lipakuliwavyo na kuwekwa mbele za mtu kumfanyako mtu kuacha kufikiria na kukasirika kisa kaambiwa ana meno kama uchi wa kuku na haki yanani kapandisha mori kuwa alicho ambiwa ni TUSI.
Swali:- Ukifikiria kama BINADAMU AKIFIKIRIA unafikiri wengi wadhaniayo ni MATUSI yata faulu mtihani wa kuitwa ni MATUSI duniani ?
.. tusi la kweli ,....
.....KISIASA- ni lile la kubwa zima kufanywa mjinga kwa kuahidiwa AHADI ZA uongo na MWANASIASA KILA WAKATI WA UCHAGUZI MPYA ili umpigie kura KITU AMBACHO kirahisi kikiwekwa katika sentensi chaweza kuwa: ``Haya majinga kweli yani nikitunga TU stori kila wakati wa uchaguzi na kuahidi nisiyoweza hayaachi kunipigia KURA.Yaone vile kama vile haya stukii vile KUWA nalia ofisini na wala siwazi TATUZI la matatizo yao!´´
Na matusi KAMA hayo hutukanwa watu KIJAMII, KIDINI, KIUCHUMI au hata KIUTU tu WAO hata bila kustukiwa kwa kuwa kwa kiswahili watu wamefikia MPAKA kufikiria TUSI KUBWA ni mpaka tu jina la sehemu za siri za mtu.
Swali:- Si ushastukia moja ya tusi maarufu kwa kiswahili ni kutajiwa JINA LA SEHEMU ZA SIRI ZAKO halafu mbele ya jina la NYETI ZAKO ikaongezewa neno ``YAKO´´?
- Hujastukia watu wengi hukasirishwa na wayatambuayo kama MATUSI ambayo hayana kabisa UBUNIFU?
- Unauhakika ulishawahi kutukanwa au ni tafsiri yako tu ndio itafsiriyo na kulijenga tusi?
- Unauhakika hatuhitaji kuwa na somo mashuleni ya jinsi ya kustukia tusi halisi ni nini ili tuache kukasirikia tafsiri za tusi ambazo zina fanya watu wakosee kustukia tusi halisi ni lipi?
Kwa bahati mbaya,...
... NA WASIWASI kuna uwezekano mkubwa,...
...wengi wadhaniao wamewahi KUTUKANWA na kufanikiwa kulikasirikia TUSI,...
...walichofanya ni kukasirikia TAFSIRI tu zao ZA KILE walichojifunza kukitambua kama TUSI,....
....na wote twajua tafsiri ni mwanaharamu ndio maana hata sentensi ``BAISKELI WEE!´´- ikilengwa kwa mtu mwenye udhaifu na baiskeli anaweza akakurukia kichwa, kabla ya kukukaba kabali halafu akakukata ngwala huku yuko bize akikukutajia jina la kikojoleo cha mwanamke halafu akaongezea neno ``WE´´mbele yake kwa kuwa anaamini kwa kufanya hivyo ana KUTUSI .:-(
Swali:- Si unakumbuka kusikia au kutambua tusi ni kitendo cha kujifunza KUTAFSIRI TU ndio maana IRAKI kumrushia Rais George Bush KIATU ni tusi wakati kwa Mmarekani kumrushia mtu kiatu MAANA YAKE ni KUMRUSHIA MTU KIATU?
- Unauhakika jina la sehemu zako Nyeti chini kidogo ya kitovu ni MATUSI au ni kitendo tu cha kuzitumia hizo sehemu kabla ya kuhalalishiwa na Kanisa au Msikiti au VIBABU FULANI ndio matusi?
NI WAZO tu hili BINGWA na usikonde!:-(
Hebu FELA KUTI arudie-Mr Grammarticologylisationalism is the Boss
Au tu FELA KUTI aachie lawama kuhusu AFRIKA katika -Upside Down
-
KWELI si kila MTU anapenda KACHUMBARI,....
Posted: January 23, 2010, 8:29 am by SIMON KITURURU
...na kwa bahati mbaya,...
... huwezi KUMLAZIMISHA mtu upendacho AKIPENDE,...
....ingawa unaweza kumshikia KIBOKO asiyependa UJI KIFUNIKO akanywa UJI BILAURI na kukuchekea wakati ANAGUGUMIA huo uji wa muhogo ingawa UKWELI UKO PALEPALE KUWA kwa uji hana PENDO.:-(
Na kwa kuwa si kila mtu anapenda KACHUMBARI,...
....kwa hiyo mpenda kachumbari kama unajali watu wengine kumbuka kuangalia wenzio kama wananogewa KWELI NA KACHUMBARI YAKO KWELI kama wewe hasa ukikumbuka labda kachumbari yenyewe unogewayo nayo labda imezidi nyanya HATA KWAKO ila wanogewa zaidi na si kachumbairi hiyo , ila tu wanogewa na lako la KACHUMBARI pendo.:-(
Swali ndugu katika hoja kwa afikiriaye:- KACHUMBARI kama ni SHEREHE YA BIRTHDAY ambayo KWA kawaida hausherehekei kwa misimamo YAKO, unafikiri unaweza kulazimisha watu wasisherehekee birthday yako kwa kuwa wewe husherehekei?
Kwa kifupi,...
.....SI KILA mtu alaye kachumbari anapenda KACHUMBARI na ,...
... kama ASIYEPENDA KACHUMBARI alaye kachumbari bila kudhurika kwa kuwa kwa kitendo hicho wamuandaliao KACHUMBARI wanafarijika na kitendo zaidi ya utamu wa kachumbari ,..
.....UKINIULIZA naweza kudai LABDA hiyo ni moja ya VIITWAVYO kutokuwa MBINAFSI KWA AJILAZIMISHAYE KACHUMBARI ajuaye hadhuriki na kachumbari KWA kuwa anaheshimu WAPENDAO KACHUMBARI, ingawa asiyedhurika hapendi kachumbari NA anashiriki KACHUMBARI.:-(
Swali:- Unafikiri kunaapotezacho Mgogo akijiunga na sherehe ya Wamasai KATIKA kusherehekea kupoteza Umasai wao kwa kuwa ni Krismasi ambayo haihusiani na UGOGO na anaamini Wamasai hao hawadhuriki na shamrashamra zao za Krismasi ingawa KIMILA Krismasi haina uhusiano na Umasai?
- Tukirudi palepale kwenye kipele cha hoja, SI unakumbuka kuwa hata kama unapenda VIPI KACHUMBARI lakini BADO UKWELI UKO PALEPALE kuwa sio kila MTU anapenda KACHUMBARI?
NAACHA WAZO na ni RUKSA kutolielewa HASA KAMA wewe ni MVIVU KUFIKIRIA kwa kuwa haki ya nani HILI ni wazo tu MKUU!
Hebu tupooze kwa kwenda tena CUBA Ray Baretto na MONGO Santamaria warudishe- Congo Bongo
Au tu Santana Ft Rob Thomas warudie- Smooth
-
Umpendaye SANA HASA kwa uzuri wa TAKO, kwa bahati mbaya TAKO likidondoka!:-(
Posted: January 23, 2010, 6:40 am by SIMON KITURURU
[Tahadhari: Wazo limepinda!:-(]
Kwa bahati MBAYA,...
... UKIFIKIRIA ,...
....chochote kikufanyacho umpende mtu kimuonekano HAKIDUMU!:-(
Kwa bahati MBAYA,...
.... UKIFIKIRIA,...
...chochote KISABABISHACHO unampenda mtu NA kisichoonekana kwa MACHO pia hubadilika hata kama utadai kama tu pendo , KIMEDUMU.:-(
Swali kabla hujatafakari hoja :- Kwani unafikiri wewe wa jana ni wewe wa leo?
- SI unakumbuka kabla hujafa hujaumbika?
- SI unakumbuka KUNAUWEZEKANO MKUBWA kila umtamaniye kwakuwa KAUMBIKA hata kama ni kwa tamaa ya kutaka kumuonja tu KIDUDE, kama unajua alishaonjwa BASI si unajua kunauwezekano MKUBWA kuna aliyemchoka ingawa kwako bado MZURIII?
NDIO,...
....tunapenda kwa sababu LUKUKI!:-(
Lakini,....
....Upendacho cha MPENZI mpendwa,...
... kama hukuinacho kama akuavyonacho MPENZI basi KUNAUWEZEKANO MKUBWA kesho kishazeeka HICHO kwako.:-(
Na fikiria tu kuwa,....
...... umpendaye kwa kuwa CHUCHU saa sita,.....
.... kumbuka kuna saa ISHIRINI NA NNE katika siku,...
... na kama mapenzi yenu yananyegeleshwa na MUGONGOMUGONGO au tu BONGO FLEVA,...
... kumbuka kulikuwa na JAZZ BENDI kibao BONGO na KWASSAKWASSA pia sio muda murefu uliopita kimtindo ambo sasa hivi kuna watakao apia ni ZILIPENDWA.
Kwa kifupi,...
... KUMBUKA upendavyo KIKUPATISHACHO NYEGE kikupandishavyo nyege cha UMPENDAYE ,....
.... kuingiliana nacho kila siku KATIKA kutibu nyege ni tofauti na kuishi nacho jumlajumla kila siku MAISHANI kwa kuwa tu UKWELI NI KWAMBA katika MAISHA,...
......JUMLA YA MAISHANI na MTU ni zaidi ya tibabu la nyege.:-(
Swali:- Si unakumbuka KAMA UMESHAWAHI KUSIKILIZA WAHENGA , umpendaye kwa kuwa ANAKUVUTIA kwa mwanya , mkiingia MAISHANI unaweza kutokumbuka kumuangalia MWANYA kwa kuwa tu unajua ni wako na UNAMPENDA?
- Si unakumbuka sista DU mpenda mpiga CHUMA kwa kuwa ana SIXPACK unafikiri akipata mimba ni rahisi kumuacha ALIYEKUWA NA SIXPACK kwa kuwa kaota kitambi?
- Unakumbuka asilimia kubwa ya vilema hawakuzaliwa vilema?
- Ushawaza wewe bila tako ukoje na akupendaye siku ukiwa hauna tako utu wako unatosha kutunza pendo?
- SI unakumbuka mwenye mwanya aking'oka jino moja tu mvuto wa mwanya hufanana na mvuto wa kibogoyo?
NI WAZO TU hili MKUU na wala usikonde!
Hebu tubadili kwa Third World ft Bounty Killer & Shaggy wakileta - Reggae Party
Au tu VYBZ KARTEL Ft SPICE warudie -RAMPING SHOP
Nipo,...
.... na baadhi ya siku ni kama pichani ,
......na asanteni WADAU ambao hamkunitenga hizi siku za karibuni ambao baadhi mko PICHANI...:-(
-
Wakati na wasiwasi na ukweli wa msemo ``RASILIMALI YA MNYONGE NI UMOJA!´´.:-(
Posted: January 23, 2010, 5:58 am by SIMON KITURURU
NDIO,..
...UMOJA ni kitu cha ajabu,...
.... ndio maana umoja wa KUKU na jeshi lake la VIFARANGA vyao ni BONGE la sherehe ya ulaji laini kwa MWEWE.:-(
NDIO,...
.. kuna wanyonge afadhali hata wasiwe na UMOJA kitu ambacho sio ajabu ,...
... kwa kuwa matokeo ya umoja wao ni kuongeza UNYONGE tu kama wingi wa vifaranga vya kuku kwa MWEWE.
Kabla sijaendelea....
Swali:- Unafikiri Tanzania, CCM ni umoja wa vifaranga vya kuku au ni umoja wa MWEWE?
- Kwani hujastukia TANZANIA hata kama unyonge wa RAIS KIKWETE ni MZURI, unafikiri kundi lake lisipokuwa na aina kadhaa zenye nguvu tofauti na za unyonge wa RAIS KIKWETE , Rais Kikwete anaweza KUKIKWETELISHA?
- Si ulicheki HASA kama uliwahikucheki TANZANIA wakati wa RAIS NYERERE jinsi umoja wa WANYONGE alivyokuwa anapata tabu nao KUNYERERESHA nao?
Umoja ni NGUVU,...
.....si pingi hilo NG'O.:-(
Lakini umoja tu kwa kuwa wote chama chenu cha kuvizia UBWABWA MISIBANI ni kimoja na wote NYIE ni vifaranga,....
..... haki ya nani kwa mwewe -UMOJA HUO WAKATI HUO ni kitoweo ,..
....na KWA BINADAMU- labda WANADAMU wengine wanawasubiri TU vifaranga mkuwe wawachinjie WAGENI kuku MZIMA.:-(
Swali:- SI ushawahi kushuhudia baadhi ya ukarimu WA WATU WENGINE ni kukaa na njaa wakati mgeni akija atachinjiwa jogoo?
NIMEACHA WAZO na SI lazima uelewe naongelea nini MHESHIMIWA na ni WAZO TU HILI Mkuu!:-(
Hebu TUBADILI HALI YA HEWA KIJIWENI kwa kumpata General Larry Platt katika- Pants on the Ground
Au tu tumpate General Larry Platt katika -Pants On The Ground (TFG Remix)
- Unafikiri Tanzania, CCM ni umoja wa vifaranga vya kuku au ni umoja wa MWEWE?
-
Sura MIA za MTU MWENYE sura moja!
Posted: January 21, 2010, 7:44 pm by SIMON KITURURU
.....kuna WASAHAUO kuwa sura ,...
... waliyozaliwanayo SIO sura,....
.... watakayokufa NAYO hasa kama walizaliwa HAI.:-(
Na kwa mkao MWINGINE WA MAWAZO naweza sema ALILIACHO MTU wakati analilia KIWEMBE,...
....kwa kawaida sio KILEKILE aliacho MTU baada ya KUJIKATA na KIWEMBE.:-(
Swali:- AU?
- Unafikiri uifurahiavyo CHUPI dukani ni vilevile uifurahiavyo baada ya kuivaa?
Kumbuka Binadamu huyohuyo mmoja,....
..UKIMTAZAMA SURA,.....
... ndiye mwenye SURA ya:- HOFU
- UJASIRI
- KUJIDAI
- KUSHINDWA
- KUKATA TAMAA
- KUTONGOZA
- uijuayo ni ya KUKUKATAA USIMUONJE
- KUKUDHARAU
- KUTUBU dhambi ya mwaka jana
- KUJIDAI
- KISENGE
- KIJEBA mchovu tu
- UZURI kama kalamba limao
- UBAYA kama kunyanzi la tako la Kima mzee
- .....YENYE CHUNUSI
- ......NZURI KAMA MALAIKA
- KUHITAJI KUKUBALIKA
- KUKUBALI KAKOSEA
- HUZUNI
- FURAHA
- .....NK,...
..... WEWE ,...
....labda huyo MTU mmoja MWENYE SURA mia ni WEWE,....
.... kama sio MIMI.:-(
NAACHA WAZO HILI NYOKO MHESHIMIWA lakini kumbuka MHESHIMIWA hili ni wazo tu !:-(
Hebu tuangalie sura mbili za PAPA SAN Moja akilia.. katika -MADDY MADDY CRY
Au tu akiongelea enzi hizo -hippity hippity Hop
NA sasa msikilize sura yake nyingine akiwa KANISANI katika-Step Pon Di Enemy
Au tu endelea tu kumsikiliza akimsifu Yesu kanisani katika-God is for me
-
Hasira ni CHACHANDU ya maisha na kama hukasiriki , labda nenda KAMUONE daktari!:-(
Posted: January 15, 2010, 7:28 pm by SIMON KITURURU
Kuna mambo kama HASIRA utakuta kuna BINADAMU hujaribu sana kuyakimbia,....
.... labda kwa kuwa huo ni UBINADAMU.
Kuna mambo kama HASIRA ili binadamu awe BINADAMU hawezi kuyakimbia,...
....na hiyo ndio hali halisi ya UBINADAMU.:-(
Swali:- Si unakumbuka STAILI YA KUONYESHA HASIRA inaweza mpaka kutumika kama ushahidi kwa uliyewahi KUMSIKIA AKIDAI au mpaka hata uakaamini kuna mtu hana hasira?
- KIHISIA ZA BINADAMU SI umestukia kama KIFO kingekuwa kinapigiwa kura na BINADAMU au tu kinaweza kukimbiwa labda kufa kusingekuwepo duniani na kwa BINADAMU kujaribu kufa kwa uzee ingekuwa ni kitendo cha kuvunja sheria?
Lakini,...
....kama wewe ni BINADAMU ,ukifikiria HATA SIO SANA waweza kugundua kuwa HISIA zako zote kama binadamu zina umuhimu wake KWA BINADAMU na kwahiyo si kitu cha kipuuzi HATA KAMA HISIA ZENYEWE katika muda husika ni JIPU LINAUMA , na labda zinakupa tu shughuli ili maisha yako yalete maana KIBINADAMU yaletavyo sasa MAISHANI MWAKO.
Ndio ,...
......hisia zako ni MUHIMU.
Kwa mfano ,....
... hisia zako kama za:- Njaa- labda bila kusikia njaa wewe labda usingestukia ujivuniacho kuwa unaakili kwa kuwa tunajua tu kuwa unaakili kwa sababu ya ufanyayo kazi na labda kisa unafanya kazi hiyo ya utafiti wa mende NI kwa kuwa tu unalipwa mshahara ambao UNAUHITAJI ILI UNUNULIE CHAKULA,- na wala huzimii kiasi hicho mende , panya, au hata sehemu za siri za ng'ombe ambavyo vimekupa PHD kama mtafiti tukuzimiaye kwa MIAKILI.:-(
- Huzuni- hasa kama unastukia mchango wa kuwa na huzuni katika FURAHA yako.
- Kukasirika- hata kama hapa nikigusia kukasirika kwa wazazi WAKO kama umestukia mchango wake katika kukufunza abadu usiwe toto tukutu.
- Kuchoka- katika kukusaidia kupumzika ili baadaye ufikirie upya kwa akili iliyotulia.
- Au tu HISIA zikufanyazo uhisi UNANUKA KIKWAPA au tu sehemu za siri - zikusaidiavyo kukufanya utafute maji uoge , AU TU uwe msafi na mwenye AFYA zaidi kwa kuwa msafi.
Swali:- AU?
Tukirudi katika hoja ya kukasirika a.k.a HASIRA,....
.....kujinyima kukasirika mara kwa mara, kama tu matatizo ya kutunza sana nyege mshindo kwa wenye ukame ,- kwaweza kusababisha siku moja kikukeracho kidogo kikasababisha UKASIRIKE sana KUBWA KULIKO na kutuonyesha vioja bure MHESHIMIWA !
Kwa kifupi,...
labda jitahidi kukasirika mara kwa mara angalau ufanye mazoezi ya kujulia jinsi ya kuporomosha hasira kistaarabu au tu kuepuka KUKASIRIKA SANA ghafla kisa tu umejilundikia hasira kibao za vitu vingi na hapa siongelei umkasirikiacho Rais Kikwete au tu JIRANI.:-(
Swali:- Kutunza hisia KAMA WEWE ni MUUDHURIAJI MISIBANI si unakustukia KILIONI hasa ukistukia kuna waliao sana kupita kiasi KWA WASIYEMJUA na majina wayaliliayo hayana uhusiano na Marehemu aliyesababisha msibani hapo kuna mnuso?
Lakini,..
...JARIBU kumkasirikia akukasirishaye basi,...
... kwa kuwa ni uonevu kukuudhi akuudhi BOSI wako halafu HASIRA ZOTE unaziamishia nyumbani na kukasirikia watoto , BILA KUSAHAU na pia kumnyima unyumba MZAZI MWENZAKO.:-(
Jaribu kumkasirikia akukasirishaye basi ,...
.....sio iwe LIMZAZI lenzio limekuudhi nyumbani KWA KUKATAA KUFAFANUA, halafu unaleta fujo BAA - samahani- kwa watu wengine OFISINI ambao wala hata hawajui unawasiwasi MZAZI mwenzio ni mgawaji wa tendo la ndoa kwa wengine na labda MDUDU unao.:-(
Swali:- Unadhani ni kila wakati unauhakika ni nini kinachokukasirisha?
- Kwani utanibishia nikidai hasira zina utamu wake wewe?
- Unafikiri kwa TANZANIA haiwezi kuwa ni fasheni tu kuikasirikia CCM ikiwa bado inasemekana WATANZANIA wengi wasikikao wakiilalamikia CCM, ndio waipigiayo kura kwa siri?
- Au ni kweli fasheni ya hasira siku hizi TANZANIA ni kuwakasirikia MAFISADI kabla mkasirikaji naye hajawa FISADI?
NIMEACHA wazo MKUU, na kumbuka hili ni wazo tu MHESHIMIWA!
Ijumaa na WIKIENDI njema MHESHIMIWA!
Hebu BB KING na Tracy Chapman warudie- The thrill is gone
Au tu ngojea Sade azungumzie tu - King of Sorrow
- Si unakumbuka STAILI YA KUONYESHA HASIRA inaweza mpaka kutumika kama ushahidi kwa uliyewahi KUMSIKIA AKIDAI au mpaka hata uakaamini kuna mtu hana hasira?
-
UMESHAWAHI kujiuliza ni nani alitafsiri BIBLIA kwenda KISWAHILI?
Posted: January 15, 2010, 7:02 pm by SIMON KITURURU
Huwa natamani sana kuwajua walio tafsiri BIBLIA kwenda KISWAHILI kwa mara ya kwanza,...
.....NA,....
.....huwa natishwa na maneno haya:
``This Biblica translation of the Bible is for the Tanzanian dialect of the Kiswahili language, which is primarily used in the United Republic of Tanzania. This translation uses an informal language style and applies a meaning-based translation philosophy. It was translated consulting the biblical languages and was completed in 2006.´´
- kila nikiendea BIBLIA ya online ya BIBLICA
Kinitishacho sana ni maneno: ``.. This translation uses informal language style and applies a meaning-based translation philosophy. It was translated consulting the biblical languages...´´
Swali:- Wanamaanisha nini katika sentensi hiyo?
- Hiki kitu huwezi kuona kuwa kama wakitafsiri biblia WAKATOLIKI biblia HIYOHIYO itakuwa tofauti na ikitafsiriwa na WASABATO?
- Kwa kusoma sentensi hiyo huwezi kustukia misingi ya hoja ya nguvu ya Waislamu ya kutotaka KORANI itafsiriwe kwa lugha nyingine?
- Si unakumbuka tafsiri za kitu mara kedekede huathiriwa na mtu atafsiriye kitu?
Sitanii!
NISAIDIE Mheshimiwa kwa hilo kama unajua vizuri historia ya BIBLIA ya KISWAHILI na niakinani walihusika kuitafsriri hasa kama umeshastukia ki- meaning-based translation philosophy,- Mtakatifu Simon Kitururu akitafsiri BIBLIA kuna watakao kuwa na wasiwasi na dini zao.:-(
TUKO PAMOJA!
.... na moja kwa moja ngojea FELA KUTI abadili hali ya hewa KIJIWENI kwa kushauri- Let's Start
Au tu GEORGE NOOKS alete pambio- How Great Thou Art
-
R.I.P Brotha Teddy Pendergrass!
Posted: January 15, 2010, 3:14 am by SIMON KITURURU
Ingawa nimechelewa kustukia,...
... R.I.P Teddy.
[March 26, 1950 – January 13, 2010]
P.S :
Kama MAREHEMU HUWA wanasikia,...
... nakiri kuwa BADO nazinguka sana tu na kazi zako Mkuu,...
....kuanzia katika bendi ya Harold Melvin & The Blue Notes
katika ngoma kama - If You Don't Know Me By Now
...mpaka ulipokuwa solo katika ngoma kama -Close the door
Kwa msiyemjua Teddy Pendergrass mwaweza kukongoli HAPA
-
Binadamu yoyote AKINUKULIWA alichowahi KUFIKIRIA,....
Posted: January 14, 2010, 1:37 pm by SIMON KITURURU
..... waweza kuhakikisha ni jinsi gani BINADAMU wote ni sawa angalau hata kwa jinsi gani tu wafikiriavyo kwenda MSALANI.:-(
Na unaweza kustukia siri ya JENERALI wa JESHI aitwaye na kujulikana SHUJAA ni KWELI anaogopa GIZA,...
... na POLISI aheshimiwaye ni mwizi.:-(
Na ,...
....unaweza PIA kustukia MPAKA kumbe aonekanaye CHEKIBOBU, muonekano HUO ni kwa sababu TU aliwahikufikiria kitu na kujistukia kuwa ni MSHAMBA,...
.... kama TU ilivyokuwa kwamba kisa cha SISTA DU kuvaa mavazi mazuri na YA ghali sana ilivyo na UHUSIANO na matunda ya fikira zake zimwambiazo na KUMUHAKIKISHIA yeye mbaya UCHI .:-(
Swali:- Hivi ukinukuu MAWAZO ya PADRE asiyeruhusiwa kuoa wa KIKATOLIKI au tu hata PAPA si unaweza kukatishwa tamaa na jinsi anavyomfikiria demu ?
- Unauhakika kila mtu akinukuliwa alichowahi kufikiria kuna MHESHIMIWA duniani?
- Unafikiri hakuna uwezekano kila mtu ALIVYO ni matunda ya alichowahi kukifikiria ?
- Unafikiri ni lazima ufikirie Jehanamu ili uhusudu kwenda Mbinguni?
NI wazo tu hili MHESHIMIWA na USIKONDE!
Na nakutakia Alhamisi NJEMA Mkuu!
Ngojea DIDO arudie -Thank U
Au tu twende Cape Verde Cesaria Evora arudie-Sodade
Au tu Cesaria Evora arudie na -Angola
-
ANGOLA vs CABINDA ukifananisha na TANZANIA vs ZANZIBAR kwa Mtanzania!
Posted: January 14, 2010, 1:15 pm by SIMON KITURURU
Wakati tunaelekea kwenye UCHAGUZI Tanzania,.....
Swali:- Na kwa kuwa kuna wadaio Tanzania kuna Zanzibar kama Angola ilivyo na Cabinda, WATANZANIA kuna funzo lolote tunalojifunza kutokana na yalipofikia mahusiano ya Angola na Cabinda hasa wakati tunakumbushwa kwa baadhi ya busara ZA HIVI KARIBUNI za baadhi ya watu za kuishambulia timu ya mpira wa miguu ya TOGO ili kufikisha madai yao ULIMWENGUNI yagundulike AU TU yasikike?
Ndio,...
... ni rahisi kusema TANZANIA sio ANGOLA na ZANZIBAR sio CABINDA,....
....LAKINI?
Ni wazo tu hili MKUU na NIMEACHA!
Na moja kwa moja ngojea GEORGE NOOKS na COBRA wabadili hali ya hewa kwa - So excited
Au tu MAD COBRA abadili kabisa hali ya hewa kijiweni kwa kurudia- FLEX
-
Ibada fupi ya msiba wa marehemu Sophia Gerald Lusingu !
Posted: January 14, 2010, 1:10 pm by SIMON KITURURU
Ndugu jamaa na marafiki,
Tunapenda kuwatangazia kuwa, kutakuwa na ibada fupi ya msiba wa marehemu Sophia Gerald Lusingu itakayofanyika:
Siku: Alhamisi
Tarehe: 14 Jan 2010 Muda: 11 am to 1pm (saa 5 mpaka saa 7 mchana)
Mahali:address:
Warehouse
1 Cumberland road
Reading
RG1 3LB
Tafadhali mjulishe na mwenzako
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na simu zifuatazo:
07954563709, 07888841971, 07799212095,
Asanteni ,
TA Reading
--
Jumuiya Ya Watanzania Reading-UK
[www.tanzaniaassociation-reading.blogspot.com]
Nashukuru,
MK
-
Haiti,.....
Posted: January 13, 2010, 12:58 am by SIMON KITURURU
.... POLENI kwa yote yaliyokuja na TETEMEKO la ARDHI!
Au tu Michael Benjamin atukumbushe Haiti kwa wimbo ni upendao ingawa huzuni zake hapa ni za noel kwa -Nwel tristes
Lakini wakati tunamuachia yote Mungu hebu Sain Zahoor Ahmad atupe- Allah Hoo
-
MAISHA ya MALAYA yangekuwa kama UFIKIRAVYO yawe!
Posted: January 13, 2010, 5:42 pm by SIMON KITURURU
Maisha yangekuwa kama UNAVYOPENDA kuyafikiri watu WAYAISHI,...
.... labda HATA UBWABWA ungekuwa haunogi kwa MPENDA CHUMVI kwa kuwa kusingegundulika hata CHUMVI duniani kama weye cha muhimu katika MAISHA YA BINADAMU sio kula chakula chenye chumvi DUNIANI .:-(
Maisha yangekuwa kama UNAVYOPENDA kuyafikiria watu WAYAISHI,...
.. labda watu wasingestukia kuna MUNGU bado kitu ambacho kingewanyima watu muongozo muhimu uendeshao maisha ya wengi waishivyo sasa hivi ya kuogopa kufanya DHAMBI ilikukwepa kumuudhi Mungu hapa DUNIANI.:-(
Swali:- Unafikiria uwezekano wa KUWA jinsi uyafikiriavyo maisha yako LABDA NI KINYUME na wayafikiriavyo watu kibao uwajuao ambavyo wanafikiri wangeishi maisha yako?
- MAISHA ya MALAYA yangekuwa kama UFIKIRAVYO yawe unafikiri ungestukiaje AIDIA ya starehe ya limpenzi lako kwa kuwa ni lako tu NI TAMU?
- SI huwa kuna wakati unafikiri ni sahihi zaidi ufikiriacho maishani mwako ni sahihi?
- Maisha ayafikiriayo MSENGE yangekuwa kama ayafikiriavyo si kuna uwezekano kusingekuwa na asiye msenge?
- Unafikiri Maisha yangekuwa kama UNAVYOPENDA kuyafikiri watu WAYAISHI kuna ambaye angepata muda au wazo la kugundua chupi, ASPIRIN au tu kukaanga dagaa kwa kuwa vyote vyanzo vya wazo lake haviko katika staili ya maisha bora yako, MATUMIZI BORA YA MUDA KWAKO ?
Ndio,...
.... ukifikiria sana unaweza kugundua mpaka umuhimu wa cha muhimu kwako unapata msaada sana kutokana na ukweli cha muhimu kwako si kwa wote ni MUHIMU.:-(
Swali katokori:- Si umestukia wakati nafikiria zaidi kupata muda wa kwenda kucheza au kuangalia mpira kuna ambaye wakati huo ANAAMINI ni muda mzuri wa kujisomea kitabu?:-(
- Unafikiri kujua sana au kuelimika sana kunamanufaa au ni matumizi mazuri ya muda mfupi wa maisha ya mtu?
NI WAZO tu HILI MKUU usikonde!
Hebu Stevie Wonder alete-I don't know WHY
Au tu Stevie Wonder alete- I am FREE
Au tu Pavarotti na Stevie Wonder wamalizie kwa -Peace wanted just to be FREE
-
Kwa kuwa kuna afikiriaye ana MUDA wa kufanya AFIKIRIALO SASA HIVI baadaye!
Posted: January 13, 2010, 5:16 pm by SIMON KITURURU
Kama unachakufanya SASA HIVI,...
... na UNAMUDA SASA HIVI labda ni busara UKIFANYA SASA HIVI.
Ndio najua,....
.... labda unahisi una MUDA baadaye wa kufanya ambacho ungeweza kufanya SASA HIVI,....
... kitu ambacho kinafanya WAZO LAKO limekaa mkao wa sentensi ,...
-`` NAJUA nina muda baadaye HALAFU najisikia UVIVU KWELI kufanya kitu kingine wakati kwenye TV kuna bonge la ISIDINGO sasa HIVI´´ .
Swali:- AU?
Lakini ,....
.....hebu tuangalie pia madhara yawezayo kujitokeza IKIWA kila mtu atafanya atakacho kufanya sasa hivi:- Labda ungebakwa sasa hivi kwa kuwa labda kuna litokwalo na udenda KUHUSU WEWE ambalo litakalo kufanya ni kukuonja hata kinguvu SASA HIVI.:-(
- Labda Ungekufa sasa hivi kwa kuwa nia yako ni kujiua kwa kuwa unajisikia kufakufa kwa kuwa maisha magumu au tu unahisi ile siri yako ndio ishajulikana SASA HIVI .:-(
- Labda ungetajirika sasa hivi kwa kuwa ambacho ungefanya sasa hivi na sio kukifikiria TU ndio siri ya umilionea kwako kama utakivalia njuga SASA HIVI .:-(
- Labda ungestukia ujinga wa swala zima UFIKIRIALO NI BONGE LA BUSARA baada ya kulijaribu kwa kuwa ukweli ni kwamba ni la kijinga na kwako ni mpaka ulitende ndio utastukia ,kwa hiyo kwa kifupi unajichelewesha kustukia ujinga wako kwa kutofanya kitu SASA HIVI.
- Kuna uwezekano UKATALIWACHO ungekubaliwa sasa hivi kwa kuwa utakaye kumuomba anajisikia kukubali SASA HIVI.
- Hufikiri labda kuna umuhimu pia wa KUKOSA SABABU ZA kwanini hufanyi sasa hivi ingawa ungeweza kufanya KITU sasa hivi?
- Unafikiri hakuna WATANZANIA wajifunzalo kwa kutofanya sasa hivi kitu ambacho kinawawezesha kulisaidia TAIFA LA TANZANIA liendelee kuwa MASIKINI sasa hivi kitu ambacho ni funzo kubwa kwa WATANZANIA la somo muhimu la : ``Busara za MASIKINI katika umasikini muhimu ni nini kitu ambacho wananchi wa mataifa matajiri kibusara WANAKOSA´´?
NI wazo tu HILI na NIMEACHA mheshimiwa!
Ngojea DWELE alete- I'm CHEATIN'
Au tu DWELE na SLUM VILLAGE wazungumzie-Tainted
-
ELIMU ni moja ya SABABU kila mjinga umjuaye ni mjinga HIVYO!:-(
Posted: January 13, 2010, 4:29 pm by SIMON KITURURU
Unawezakubisha ,...
.....lakini kila mtu KAELIMIKA!:-(
Na kwa bahati mbaya ,...
....elimu IWEZACHO SANA KIRAHISI ni kuubadili tu JINA ujinga waidaiwaye AMEELIMIKA kuliko kitu kingine chochote kielimu.:-(
Na kwa bahati mbaya zaidi,...
... elimu yaweza kumzidishia UJINGA aliyeelimika ndio maana inafikia kuanzia aliyeshiriki kugundua BOMU la nyukilia, WAUANAO kwa KUTUMIA ELIMU iwashauriyo wapigane vita kuzuia mabomu ya nyukilia yasisambae, aliyegundua kondomu na asiyeitumia makusudi kondomu ukiwachunguza utagundua wote KIVYAO wameelimika kitu......
Swali:- Wakati unamtambua aliyeelimika huwa unakumbuka kufikiria ni mangapi hajaelimika?
- Si unakumbuka duniani , elimu itumikayo zaidi ni elimu dunia ambayo kila mtu anaweza kujiuliza hivi katika elimu hii hivi Profesa ni nani?
- Unafikiri kuna aliyeelimika kwa yote?
- Hivi baada ya kuelimika bado ulijistukia hujui kabla ya kupata uzoefu ?
NDIO,...
.... inajulikana kuwa kwa kawaida wale idaiwao WAMEELIMIKA SANA kwa mara nyingi huajiriwa na iaminikao NA wengi hawajaelimika sana hasa katika elimu ya kipimo ni VYETI ambao kwa bahati mbaya ndio waanzishao mahali watu WENGI wapaitapo KAZINI.
NA,...
....kisahaulikacho ni kwamba ELIMU ya yoyote YULE kuna eneo IMELENGA ndio maana Mganga wa MENO kwa kuwa na elimu kuhusu MENO si lazima anajua kutibu kichaa kama mwenye elimu ya VICHAA.
Na kibaya katika elimu,....
... kuna WAIJUAYO kwa nadharia WENGI kuliko kwa VITENDO ndio maana WADAIO wanajua matumizi ya kondomu katika kuzuia UKIMWI ni WENGI tu kama ambao ni rahisi kukiri kupata gono kuliko UKIMWI.:-(
Swali:- Unafikiri ni wangapi tujuao kufikiria tutakacho kuandika na kivitendo hatupatii kuandika ?
- Unafikiri ni wanasiasa wangapi wasioijua siasa kivitendo ambao unafikiri ni wanasiasa?
- SI unakumbuka kila mwenye elimu umtambuaye kwa hilo kuna kitu unamuunganisha nacho kielimu kama tu yule ufikiriaye mjinga na hajaelimika UMUUNGANISHAVYO na kitu fulani tu ambacho kwako kinapiga kelele kuwa hajaelimika ingawa UKWELI NI KWAMBA anaweza kukufundisha kitu?
NDIO,...
.....ELIMU ni aina ya kubagua nini unataka kukiacha ubongoni kiendeleze UJINGA au tu kibakie hakijaelimika,....
...na kuna uwezekano mkubwa aheshimiwaye kwa KUELIMIKA inategemea sana na ujinga au UDHAIFU wa mtu katika swala zima la ni nini KUELIMIKA na ni nini katika ubongo wake KIMEELIMISHWA.:-(
Swali:- Unafikiria kielimu hakuna profesa wa uchawi kwa kuwa wewe sio mchawi?
- Unafikiri elimu imekuzidishia ujinga upi wewe ?
- Umeshawahi kusikia kuwa kila isemekanaye kaelimika kuna ajiongezeacho KUTAKA katika asivyohitaji?
NI wazo tu HILI Mkuu!:-(
Hebu twende Afrika dauni anda , Penny PennY alete- IBOLA
Au tu PENNY PENNY alete na - Makantia Jive
- Wakati unamtambua aliyeelimika huwa unakumbuka kufikiria ni mangapi hajaelimika?
-
Mapungufu yajitokezayo katika NENO kutokana na UANGALIFU wa MTOA NENO!
Posted: January 9, 2010, 12:51 pm by SIMON KITURURU
....kwa bahati mbaya UANGALIFU wa kitu wahitaji UJUZI wa kitu ,....
...... na kama WEYE unalimaindi NENO lako na unataka LISIPOTEE bure,...
... kwa mafanikio zaidi basi angalau MJUE umlengaye kwa hilo NENO.:-(
Swali:- Lakini pia si unakumbuka kujua tumizi hata la kikombe haitoshi kama hujui jinsi ya kukihifadhi kikombe, kama unakitakia maisha marefu kikombe?
...na BILA kumjua umlengaye kwa NENO ambalo unafikiria KATIKA UMAANA lina kitu,...
....waweza KUMCHEKESHA utakaye KUMKASIRISHA hata kwa kumlenga kwa TUSI ambalo kwako unafikiri ni TUSI KALI katika LAKO neno.:-(
Swali:- Si umestukia hata maneno ya MWALIMU umuelewaye na kupasi MTIHANI ukimuuliza atakuambia anajua wanafunzi wake wanaofeli kwa kutomuelewa neno?
- Si umestukia hata MAHUBIRI ya ASKOFU au mawaidha ya SHEKHE yakugusayo kwa neno huwa hayagusi waumini wote ndio manaa inasemekana kunawatakao kwenda jehanamu kwa hilo?
- Na si unajua neno ulengwalo NALO likikukolea kwa kawaida mtu huanza kufikiri ndio kweli yenyewe KABISAAA kitu ambacho ndio kisa cha Papa WAKIKATOLIKI au tu Askofu wa Kilutherani kufikiri WASABATO kwa kusali jumamosi na kutokunywa mvinyo wenye KILEVI a.k.a pombe kanisani NI MATOKEO ya kuna neno la YESU hawajaelewa?
- Si unajua kwako usiyenielewa , neno langu hapa katika blogu hii mie SIMON Kitururu LABDA mlengwa sio wewe?
- Unabisha?
- Unafikiri YESU anaeleweka?
NDIO ,...
... kunauwezekano wakati WEWE ni muangalifu hata wa NENO akutazamaye na kukusikiliza anaweza akawa ni yule ambaye kwake UMEZIDISHA makali ya neno na unavyozidi KUMTONGOZA mwenzio anafikiri UNAMKARIPIA.:-(
Ndio,...
... neno lina ubinafsi KATIKA KULIELEWA na kipimo ni wewe mwenyewe ndio maana wakati mie Mtakatifu Simon Kitururu wakati nafikiri nahubiri NENO weye waweza kudhani NATUKANA kwa kuwa utumiacho katika kupima uzito wa neno ni chako binafsi.:-(
Ndio,...
... katika neno hata YESU hakueleweka na KWA HIYO kama WEYE MTANZANIA unawafuatilia wafuasi wa NYERERE Tanzania leo hii usishangae kustukia karibu wote neno lake pia hawakuelewa.:-(
Swali katokori:- Unanielewa naongea nini MHESHIMIWA katika hili neno?
- Unafikiri wewe wakati MWANGALIFU misingi ya uangalifu wako hata wa ili usijetukana bure ni nini?
- Si unakumbuka ukimtusi mwenye KICHWA kama DAFU kwa kukifananisha kichwa chake na`` Kichwa kama tako la MZEE´´ yawezekana ni tusi?
NIMEACHA wazo Mheshimiwa KIKORE na kumbuka hili ni WAZO tu MKUU na ni ruksa kutolielewa!
Ngojea nimuachie BOPOL MANSIAMINA katika gita na ASSAKA BABA LEY katika kipaza sauti au tu ORCHESTRE MODE SUCCES waje na -Pitie, Je veux la reconciliation
Au tu ngojea tuyarudi magoma moto kutoka kwa Mheshimiwa MCHUNGAJI MUNISHI ashushe kitu kizito kiitwacho-Nawaombea WANAHABARI
-
HIVI wasichana wa SIKU HIZI katika KUDENGUA bado kuna wabanao PUA?
Posted: January 9, 2010, 4:39 am by SIMON KITURURU
[Tahadhari: Taralila hii inahitajia ainafulani ya UKUBWA na labda haimfai mtoto au wewe kama unamchezo wa kukwazika na neno.:-(]
Ndio,....
.... kila kizazi kina staili zake za NATAKA SITAKI na mpaka tu fulu KUJISHEBEDUA.:-(
Ndio,...
.....kwa kawaida staili za jana si za leo ingawa kimini SKETI CHA MAWAZO au tu cha VAZI cha MWAKA elfu moja mia tisa SITINI chaweza kuwa kinalipa leo angalau katika staili ya kuonyesha mwanzo wa juu ya goti KATIKA kuchombeza dalili ZA paja zuri MWANAWANI lililosahaulisha mwenye paja ni UBONGO WAKE ndio katika staili yake ndio alichokuwa anatumia mlivyokutana katika KUJISHEBEDUA .:-(
Tukiacha utani na kwenda kwenye SWALI:- Hivi akina AKINA DADA/ KINAMAMA mnajua kuwa kwa akina KAKA/ AKINA BABA kabila yenu YA KIKE inahitaji mara nyingi ufundi sana KUFUMBUA FUMBO LA MNAWAZA NINI hata katika hata SWALA la kuhakikisha ni kweli wakati mnaonekana mnataka mafenesi ili twende kwenye SOKO LA MAFENESI kweli yenyewe HAIKO katika ukweli kuwa kihitajikacho ni VIATU VIPYA na tunaenda soko la mafenesi kwa kuwa liko mbele ya duka la viatu?
- Ewe usiye na UUME unauhakika unaongea LUGHA ambayo mwenye uume anaelewa, zaidi ya ile ya kulalamika NA KULIA KIDOGO ambayo kila kidume anaielewa?
- Na enyi vidume mnaelewa mara nyingine mtaka penzi mke wa ndoa anajisikia kutotoa tendo la ndoa lile lililobarikiwa na sio lile la kimada - kwa kuwa adaivyo pesa ya mboga haitoshi na au tu adaivyo kachoka mboga zile zile - maana yake kaichoka VITARA na BALUNI ya mwaka juzi na sasa anataka gari nyingine kama watumiazo mashoga zake?
- Kabla sijasahau MDENGUO,- ni staili gani siku hizi bongo inalipa kwa ZE demuz au ndio kila mtu na staili yake na wote hawamuigi RIHANNA?
NI wazo tu hili MHESHIMIWA usitishike ingawa mwaka huu demu akinielewa nimuelewavyo ntampa mimba haki ya nani!:-(!
Tuachane na hayo na hebu WERRASON abadili kwa -Operation Dragon
Au tu Yondo Sister arudie- Scandale
-
HIVI wasichana wa SIKU HIZI katika KUDENGUA bado kuna wabanao PUA?
Posted: January 9, 2010, 4:39 am by SIMON KITURURU
Ndio,....
.... kila kizazi kina staili yake ya TAKA SITAKI na mpaka tu fulu KUJISHEBEDUA.:-(
Tukiacha utani na kwenda kwenye SWALI:- Hivi akina AKINA DADA/ KINAMAMA mnajua kuwa kwa akina KAKA/ AKINA BABA kabila yenu YA KIKE inahitaji mara nyingi ufundi sana KUFUMBUA FUMBO LA MNAWAZA NINI hata katika hata SWALA la kuhakikisha ni kweli wakati mnaonekana mnataka mafenesi ili twende kwenye SOKO LA MAFENESI kweli yenyewe HAIKO katika ukweli kuwa kihitajikacho ni VIATU VIPYA na tunaenda soko la mafenesi kwa kuwa liko mbele ya duka la viatu?
- Ewe usiye na uume unauhakiki unaongea LIGHA ambayo mwenye uume anaelewa zaidi ya ile ya kulalamika NA KULIA KIDOGO ambayo kila kidume anaielewa?
- Na enyi vidume mnaelewa mara nyingine mtaka penzi mke wa ndoa anajisikia kutotoa tendo la ndoa lile lililo barikiwa na sio lile la kimada kwa kuwa adaivyo pesa ya mboga haitoshi na kachoka mboga zile zile maana yake kaichoka VITARA na BALUNI ya mwaka juzi na sasa anataka gari nyingine kama shoga zake?
- Kabla sijasahau MDENGUO staili gani siku hizi bongo kwa ZE demuz?
NI wazo tu hili MHESHIMIWA usitishike ingawa mwaka huu demu akinielewa nimuelewavyo ntampa mimba:-(!
Tuachane na hayo na hebu WERRASON abadili kwa -Operation Dragon
Au tu Yondo Sister arudie- Scandale
-
Staili YAKO!
Posted: January 9, 2010, 4:02 am by SIMON KITURURU
...staili YAKO ikifanana na ya WATU WENGI kivyenu ,...
.....kama unastukiwa KISTAILI kwa hiyo STAILI labda ni kwa kuwa UNAHARIBU SANA au weye BORA sana katika hiyo staili KISTAILI na haki ya nani kWA HIYO STAILI wakustukiao wanaweza kukuita weye MJANJA.:-(
Swali:- Si unakumbuka kwa wakoseao staili kuna mjanja wao pia?
....na staili YAKO ikizidi kutofautiana na staili nyingi za WENGI AMBAO kwako ni WENU,...
....hata ikiwa ni KWA SABABU YA KUFIKIRIA KWAKO TU hasa wakati weye katika KUNDI LENU HUSIKILIZWI FIKIRA ZAKO wala HUONEWI DONGE kistaili ,...
...bonge la staili yako yaweza kusababisha UONEKANE KICHAA wakati katika STAILI YAKO HATA KAMA NI YA KUONYESHA TAKO weye mwenyewe una bonge la tako bora NA STAILI YAKO ni BORA na kihesabu ni KUBWA KULIKO ,....
... ila kwa bahati mbaya wakati huo ni TITI na sio TAKO lililoko kwenye FASHENI na STAILI....
....NA YOTE NI KWA KUWA ukweli ni kwamba BINADAMU katika kuchagua ni nini BORA au KIZURI KISTAILI ukifikiria ,...
.....ZIKO UBONGONI ,....
... NA WENGI BINADAMU NI WAVIVU KUTUMIA UBONGO na KUFIKIRI .:-(
NDIO,...
..... sababu mojawapo isababishayo FASHENI na STAILI lazima zibadilike KILA MARA
... inaelezeka kirahisi hata bila kutumia AKILI KWA kuangalia KUCHOKA hata kwa WALI WA NAZI na MAHARAGE kama ukirudiwarudiwa ,...
.....KWA HIYO, ....
.....ili wapendao STAILI HII wasiboreke a.k.a kuchoka FARAJA ya staili hiihii KILA SIKU ,....
....kiakili INABIDI lazima WABADILI aina hata YA staili ya CHUPI hata kama chupi ya mwaka jana ya mauaua na ya mwaka huu ya NJANO zote zinateteza NYETI vilevile UKITUMIA AKILI ,....
...na kwa hili KISIASA ndio maana UKOMUNISTI ulizidiwa na UBEPARI hasa kwa kung'angania YALE YALE.:-(
Lakini pia tusisahau KUBADILI STAILI hata ya chupi KWA KUMNUNULIA MPENZI chupi nyingine za STAILI MPYA kama zawadi kwa LIMCHUMBA LAKO,....
...kinamna KWA LIMCHUMBA au hata LIMPENZI TU inasemekana HUWEZA kuleta MAANA kuwa UNALIPENDA KWELI LIMCHUMBA/limpenzi kwa kuwa tu au hasa tu kama LIMPENZI LITAHISI kuzipata HIZO ZA STAILI MPYA inabidi MWANAWANE uwe na bidii , unuie kweli AU TU uwe hasa MJANJA au tu staili yenyewe inasema...
- `` NAKUPENDA KWELI MPENZI´´!!.:-(
Swali:- Si unakumbuka staili ya zawadi hata ya bei poa inaweza kumaanisha unamfikiria kweli MPENZI wakati staili ya bei ghali ikawa inasema kwa mpenzi ngojea niondoe kero limpenzi liache kunikera?
- NA lakini SI unakumbuka WAJANJA SANA moja ya STAILI ya UJANJA WAO ni kufanya watu wasistukie wao ni WAJANJA?
NI HILO TU Mheshimiwa na NI WAZO TU ingawa limekatizwa!:-(
Hebu Angie Stone abague kwa kusifia wanaume weusi katika- Brotha
Boney M wabague kwa kumsifia- Brown Girl
Bob Marley akumbushe kuwa watu wasipoacha kubagua , kwa kuona rangi au hata MSHEBEDUO kama vile TABAKA ni nini kitatokea katika- WAR
-
Staili YAKO!
Posted: January 9, 2010, 4:02 am by SIMON KITURURU
...staili YAKO ikifanana na ya WATU WENGI kivyenu ,...
.....kama unastukiwa KISTAILI ni kwa kuwa UNAHARIBU SANA au weye BORA sana katika hiyo staili KISTAILI na haki ya nani wakustukiao wanaweza kukuita weye MJANJA.:-(
Swali:- Si unakumbuka kwa wakoseao staili kuna mjanja wao?
....na staili YAKO ikizidi kutofautiana na staili nyingi za WENGI AMBAO kwako ni WENU,...
....hata ikiwa ni KWASABABU YA KUFIKIRIA KWAKO TU hasa wakati weye katika KUNDI LENU HUSIKILIZWI FIKIRA ZAKO wala HUONEWI DONGE kistaili ,...
...bonge la staili yako laweza kusababisha UONEKANE KICHAA wakati katika STAILI YAKO HATA KAMA NI YA KUONYESHA TAKO weye mwenyewe una bonge la tako bora NA STAILI YAKO ni BORA na kihesabu ni KUBWA KULIKO ,....
....NA YOTE NI KWA KUWA ukweli ni kwamba BINADAMU katika kuchagua ni nini BORA au KIZURI ukifikiria ,...
.....ZIKO UBONGONI ,....
... NA WENGI BINADAMU NI WAVIVU KUTUMIA UBONGO ndio hasa sababu hasa FASHENI lazima zibadilike KILA MARA ili MJANJA na WASIO WAJANJA hata KIAKILI kwa kuwa AKILI KWA KUCHOKA hata WALI WA NAZI na MAHARAGE ukirudiwarudiwa ni RAHISI,...
.....ili wapendao STAILI HII wasiboreke a.k.a kuchoka FARAJA ya CHAI NA KITUMBUA KILA SIKU ,....
....kiakili INABIDI lazima WABADILI aina hata ya CHUPI hata kama chupi ya mwaka jana ya mauaua na ya mwakahuu ya NJANO zote zinateteza NYETI vilevile UKITUMIA AKILI ,....
...na kwa hili ndio maana UKOMUNISTI ulizidiwa na UBEPARI hata kama KATIKA HOJA HII HAPA hatutaingizia HOJA YA NGUVU ya chupi nyingine za STAILI MPYA kwa zawadi kwa LIMCHUMBA LAKO ziletavyo MAANA kuwa UNALIPENDA KWELI LIMCHUMBA kwa kuwa tu kuzipata inabidi MWANAWANE uwe na bidii , unuie kweli na uwe hasa MJANJA .:-(
Swali:- Lakini unakumbuka WAJANJA SANA moja ya UJANJA WAO ni kufanya watu wasistukie wao ni WAJANJA?
NI HILO TU Mheshimiwa!
Hebu Angie Stone alete ubaguzi kwa kusifia wanaume weusi katika- Brotha
Boney M walete ubaguzi kwa kumsifia- Brown Girl
Bob Marley akumbushe kuwa watu wasipoacha kubagua , kwa kuona rangi au hata MSHEBEDUO kama vile TABAKA ni nini kitatokea katika- WAR
-
Wakati NYANYA inaringia VITUNGUU!
Posted: January 8, 2010, 4:13 pm by SIMON KITURURU
Nyanya kwa maringo yake na KUJISHEBEDUA mbele ya KITUNGUU yaweza kudai INA sura nzuri zaidi kwa kuwa NYEKUNDUU halafu INABONGE la SHAVU nyororo kuliko KITUNGUU!
Swali:- Si unakumbuka lakini KITUNGUU kinalika peke yake kama tu NYANYA ilikavyo peke yake halafu bila CHUMVI?
Halafu NYANYA inaweza mpaka kujishebedua kwa jinsi ipatavyo JUA na haifukiwi udongoni karibukaribu na mavi ya kuku a.k.a MBOLEA kama kitunguu na INAPATA JUA tokea utotoni,....
...kwa bahati mbaya KWA BINADAMU ,....
... hata kabla KITUNGUU hakijaanza kufunua sketi ili kuisuta NYANYA kwa kujishebedua kisa ili iwe nyekundu haihitaji MKOROGO ingawa ina NDONYA angalau MOJA na siajabu kuikuta na CHUNUSI ikiingiliwa na VIMELEA,....
... na hata kabla KITUNGUU hakijaanza kutamba kwa jinsi iwezavyo kuliliza mpaka limtu KUBWA ,...
... Kwa BINADAMU aonacho na AFIKIRIACHO katika vyote vya NYANYA na KITUNGUU labda ni viungo tu vya MWIDU, chunga, MAHARAGE au sana sana kachumbari,...
..... na LABDA hata sikumoja hajawahi kufikiria kuna uwezekano NYANYA MSHUMAA inajiona yenyewe ni babukubwa kuliko NYANYA MVIRINGO na nyanya zote kwa pamoja zina ugomvi na VITUNGUU .
SASAAAAA....
Swali katokori:- Wakati huu ambao UISLAMU na UKRISTO vinalumbana unafikiri MUNGU anafikiria nini?
- Wakati Wakristo na Waislamu wanalumbana kuhusu nani ataenda mbinguni unafikiri BUDDHA anafikiria nini?
- Wakati wake wawili wa Rais ZUMA wa Afrika KUSINI wanagombana unafikiri Rais Zuma huwa anafikiria nini?
NI WAZO TU HILI Mkuu , na labda VITUNGUU na KABICHI , NYANYA na MABIRINGANYA wala havina UGOMVI kama UISLAMU na UKRISTO na ugomvi wa mambo uko KICHWANI TU mwa wanadamu HASA katika tafsiri ya MAMBO!:-(
Nakutakia IJUMAA na WIKIENDI NJEMA Mkuu angalau uwe na uhakika wakupata choo MHESHIMIWA!
Tararila HII ilitunga mimba mawazoni baada ya kusoma articles kadhaa zenye uhusiano na MALAYSIA katika :
``Minister in the Prime Minister's Department Jamil Khir Baharom today urged websites and blogs to refrain from carrying anything negative on the issue of the use of the word 'Allah' by the Catholic weekly magazine, The Herald.´´
Hebu tubadili hali ya hewa kijiweni kwa kupitia Cuba MONGO SANTAMARIA arudie- Me and U baby
Au tu Ray Barretto na MONGO SANTAMARIA waingie kazini kwa kitu- CONGO BONGO
Au tu turudi AFRIKA kwa mara nyingine OSIBISA watulize kwa -WOYAYA
-
Kama huna HESHIMA ulijuaje?
Posted: January 8, 2010, 2:01 pm by SIMON KITURURU
Jamii NI MPAKA ijue HUNA HESHIMA ndio itakupa adhabu .
Matokeo yake wanajamii wengi WASIONAHESHIMA wanaishi kinafiki katika kujaribu kutunza muonekano ambao JAMII inautambua kama ni HESHIMA!
Chakusikitisha,..
..... JAMII wakati HUO inaadhibu mtu inaweza kuwa ndio yenyewe HAINA HESHIMA.
Ila kwakuwa JAMII kwa ujumla ndio itafsiriyo kitu HESHIMA ni nini ,...
... ni rahisi kuwa kwa hilo la HESHIMA jamii yenyewe ni KIPOFU.
NA,...
.... JAMII ni watu na katika watu kuna mtu ambaye ni kiini katika MTAZAMO mzima wa HESHIMA ni nini.:-(
Kwa hiyo mtazamo mzima wa nini ni HESHIMA kwa kizazi cha BAADAYE mhasisi yawezekana ni WEWE usiye na heshima LEO.:-(
Ndio ,...
...kwa hiyo mtazamo MZIMA kama ULE wa ``KIZAZI cha sasa hakina HESHIMA kwa WAKUBWA´´ ni moja ya ishara kuwa HESHIMA ni kitu kilicho kwenye MWENDO na HAKIKUSIMAMA na muelekeo wa HESHIMA iendako kimtazamo ni MTU ambaye anaambukiza WATU mpaka kufikia kuwa ni mtazamo wa JAMII.
NA chakusikitisha ni kwamba MTAZAMO wako wa ni nini HESHIMA wa jana, LEO taka usitake kuna uwezekano umepitwa kwa SIKU moja ingawa mpaka ustukie kuwa yote udhaniayo sio HESHIMA yanaonekana ni KAWAIDA kama sio mfikiriaji utastukia hilo ikifikia PALE idadi kubwa ya JAMII IFIKIRIAYO KAMA WEWE itakapostukia.:-(
Swali:- Kwani kutoa kitu kidogo au RUSHWA TANZANIA unafikiri ilianza ghafla tu?
Ndio,...
....KAMA HUNA HESHIMA na UNATAKA KUTAMBULIWA KAMA MHESHIMIWA chakusikitisha ni kwamba WALA USIHOFU kwa kuwa KWA WATU WENGI inatosha WASIPOJUA tu kuwa WEWE HUNA HESHIMA!:-)
Ndio ,...
....KWA kuwa JAMII ni kipofu katika iliyoamua ndio KWELI YAKE, unaweza ukafikiri UNA HESHIMA mpaka UTOKE kwenye JAMII YAKO ,...
.....na hapo ndio utashangaa kumbe KUSONYA wazazi wako ni kukosa HESHIMA, au tu kustukia karibu wote UWAITAO WAHESHIMIWA katika JAMII ya waheshimiwa ni VIONGOZI waiibiayo serikali waiongozayo ulikuwa unakosea maana nzima ya HESHIMA ni nini.:-(
Swali:- Kwani HESHIMA ni nini?
- Mkuu hivi tukikusachi moyoni/ROHONI unaheshima au una heshima kwa kuwa unajulia muonekano na kauli za HESHIMA?
- Kwani weye kama MTANZANIA hujisikii ulikuwa huna heshima kwa ng'ombe kabla ya kukutana na MHINDU wa INDIA?
- Kwani unafikiri ni MTANZANIA ngapi haziheshimiwi mpaka na serikali yao ukilinganisha na jinsi MBWA waheshimiwavyo kama watu ULAYA na MAREKANI?
Swali zaidi katokori:- Si umeshastukia kukosa heshima HASA katika JAMII MASIKINI huwa kunawahathiri zaidi WANYONGE na walalahoi?
NDIO ,....
... kwa shingo upande labda NIKIRI,....
.... kama hali yenyewe ndio hii DUNIANI labda HESHIMA ni MUONEKANO na usikikavyo.
TUSIPOSHUHUDIA vitendo vyako vya kinyama na KUSIKIA kauli zako zisizo na heshima labda unahaki ya kuwa ndani ya JEDWALI la WENYE HESHIMA Mkuu!:-(
Nsikutishe MWANIWANE hili ni WAZO tu Mheshimiwa KIKORE!
Ngojea USA for AFRICA katika KUJIANDAA kujisaidia kujisikia vizuri kwa kusaidia AFRIKA tuwachungulie katika- DAY O
Au tu HARRY BELAFONTE mwenyewe adai-DAY O
-
Kwa wote mfuatao KALENDA ya JULIAN !
Posted: January 7, 2010, 11:08 pm by SIMON KITURURU
WOTE muifuatayo KWELI ya imani ipatikanayo katika MAKANISA ya KI-ORTHODOX,...
...HONGERENI kwa kuwa leo MWOKOZI YESU kazaliwa!
Na WENGINE nawatakieni wote shamrashamra MURWA za KRISMASI ya leo !
Samahani,...
....kwa wazingukao na KALENDA ya JULIAN kwa kuwa wamezoea ya GREGORIAN unaweza tu KU- GOOGLE mkero kama sio mvivu,....
.... au ukafananisha kuwa kwa KALENDA hii ya JULIAN ulitahiriwa tarehe gani kwa kukongoli-
Calendar converter HAPA
Au tu pata BEMBEYA JAZZ National kama utasherehekea kwa -Whiskey Soda
-
Happy Birthday Malick SUFIAN a.k.a KIKI!
Posted: January 7, 2010, 10:44 pm by SIMON KITURURU
Kila la kheri KIKI katika siku yako ya kuzaliwa MKUU!
....NA...
....nakutakia MAFANIKIO maishani katika kila upangalo na ujaribulo MKUU!
!
BILA kusahau, .....
....HERI ya KRISMASI MKUU!
Unajua tena KALENDA ya JULIAN inatuambia tena kuwa YESU kazaliwa tena leo!
Mpate JERU the DAMAJA kama chaguo langu kusindikizia salamu katika- The SUN TOUCHER
Na wanaokuzingua nawapa JERU tha DAMAJA katika - Ya playin' YASELF
-
...ijifichapo AJENDA ya SIRI!
Posted: January 7, 2010, 3:10 pm by SIMON KITURURU
[Tahadhari mwana tafsida: Tararila baadhi ya maeneo kitumizi la neno na kauli inapitiliza!:-(]
Mambo yangekuwa rahisi sana DUNIANI kama kila kitu kingekuwa tu kama CHOO kwa kuwa hata choo kiwe kisafi vipi hakuna siri kuwa kila mtu anajua kinaficha nini kunako SHIMO .
Swali:- SI inajulikana kwa kila mtu kuwa mwili wa choo, tumboni unanini?
Kwa bahati mbaya hata choo bado hakirahisishi sana MAMBO kwa kuwa ungejua choo kinashuhudia nini wafanyacho huko UWASHUHUDIAO waendao chooni ,...
...waweza kusikitishwa kwa kugundua kuwa ni choo pekee ndio chenye ushahidi kuwa ASKOFU au tu Shekhe umuheshimuye chooni ndiko avutiako UNGA a.k.a mihadharati wakati umuonapo akienda MSALANI na wala sio zile haja namba MOJA au ile nzito ya namba MBILI.:-(
Tukiachana na hilo na kurudi katika ijifichapo AJENDA YA SIRI...
...kwa MWENYE TABASAMU,....
... ajenda ya SIRI inaweza ikawa iko kwenye TABASAMU na wakati unafikiri tabasamu linashughulikia KUKUPA ukarimu,....
.... kwa CHUNA BUZI tabasamu linaweza likawa lina maana JIINGIZE mtegoni MWANAHARAMU WEYE nikufilisi , kwana lione vile MENO kama NGIRI.
...kwa BOSI tabasamu linaweza kumaanisha mie sikupendi ILA ukinitaka ntakubali na kama unataka kujua WAKUTETAO hapa ofisini wewe NIULIZE tu mie , mwenzio na tete ulaji wangu tu hapa ofisini.
NA,...
...ajenda za siri ya MTAKA ELIMU kwa wengi wala sio KUELIMIKA.:-(
......kwa Profesa MWINGINE elimu imetokea tu kwa kuwa TOKEA ALAZIMISHWE NA WAZAZI KWENDA SHULE UTOTONI ajuacho zaidi ni kujisomea na AJISIKIAVYO wakati akifanya MTIHANI ndio kulikomfanya hana hamu na NGONO kwa kuwa hakuna utamu MTAMU kama wakati anakokotoa MASWALA ili kutafuta JIBU na akipata jibu ukiusikiliza KWA MAKINI ubongo wake sauti uwezayo KUISIKIA unaweza kukumbushwa sauti uzisikiazo katika filamu za kikubwa a.k.a porno wakati unaziangalia kwa siri watu wasigundue kuwa ni wewe uliosababishaye neno SINEMA za NGONO kwenye search za google ni maarufu.
....kwa KIBOSILE na pamoja na watu LUKUKI WENGINE WENGI UWAFAHAMUO elimu ilikuwa ni CHAMBO TU cha kupata KAZI yoyote tu hasa baada ya kustukia VYETI na WAAJIRI ni kama INZI na MZOGA , na baada ya kupata kazi ni asilimia moja tu ya yaliyompeleka shule anayakumbuka na kuyatumia tena KIELIMU na hapa sigusii hata ile elimu ya kuvaa kondomu kabla ya kutumbuizwa na malaya.
Swali:- Unakumbuka vitabu vyako vya shule viko wapi mkuu?
NA,...
...ajenda za siri ziko mpaka kwenye DINI.
....kwa ASKOFU inaweza kuwa kisa kikubwa cha kujiingiza kwenye DINI ilikuwa ni kwa sababu tokea mtoto alikuwa anazimia magauni tu ya MAPADRE bila kusahau mapochoocho kutoka VATIKANI na hali halisi ya kwamba katika SEHEMU ZA dini ndio sehemu pekee unaweza kutoa SHOO inayoboa ila watazamaji wa shoo hawaondoki kama kwenye shoo nyingine kama za MDUMANGE au tu kwasakwasa zikiboa.
....na kwa Muimba kwaya dini inamsaidia sana kupata mademu wa KILOKOLE kanisani ambacho kwa kisiri ndio kimpelekacho kanisani .
Swali:- Si unakumbuka DINI kwa shekhe na Mchungaji ni kazi?
- Kwani ulifikiri kazi ya dini ni kupeleka tu watu mbinguni ?
- Unafikiri ni wangapi wakiwa kanisani au msikitini hawasikilizi kinachosemwa ila ni muhimu kwao kuonekana huko?
NA,
...kuna ajenda za siri za KUJIPENDEKEZA pia.
....kwa ajipendekezaye KWAKO moja ya siri usiyoijua INAWEZAKUWA ni kweli ANATAKA kikweli kuwa rafiki yako wa KWELI.:-(
...... kwa ujipendekezaye kwake ajenda ya SIRI KWAKO inaweza ikawa ni kutimiza busara idaiyo mjue vizuri ADUI YAKO kwa kuwa KARIBU YAKE kama unataka kuepuka KUCHEMKA katika swala zima la kukabiliana na UADUI WAKE au tu ile BUSARA idaiyo tu kuwa ADUI muweke karibu zaidi hata kuliko rafiki kwa kuwa anapigika ROBA kirahisi, au tu unaweza ukamrukia kichwa , kumkata ngwala AU TU KUMTEMEA BONGE LA KOOZI akiwa karibu.:-(
Na ,...
...kwa MMBEYA,..
....mara karibu zote ajenda ya SIRI katika MUONGEA UMMBEYA ni kutafuta habari zaidi zimuhusuzo mlengwa katika UDAKU a.k.a UMBEYA na chakusikitisha baada ya kupata UMBEYA mara karibu zote kunakuwa hakuna MANUFAA yoyote kwa MMBEYA.:-(
Swali:- Hivi ni kwanini hudhaniwa MMBEYA huwa afaidiki na UMBEYA?
- Hivi neno MMBEYA ni kiswahili fasaha au huwa linaandikwa MBEYA kama mkoa wa MBEYA kwa kiswahili?
- Heloooo MBEYA umejaribu kuuliza tu utakacho kujua CHA UDAKU bila kutunga kwanza kastori kakimbeya ili upate kujua fulani matako yake MUUMUKO WAKE ni wa bandia?
NAKATIZA wazo,....
... na kwa hili la kuamua KUKATIZIA WAZO HAPA lina ajenda za siri, moja wapo ikiwa ni kutaka tu ufikirie MWENYEWE ajenda zako za siri leo hii kwa uliye mnunia, mchekea au tu kumkarimu lunch zilikuwa ni nini na je zimezaa matunda au utalazimika uzibadilishie mkao kwa kuwa kwa mkao huu kimdako wa mchungulio chupi haionekani?
Swali zaidi katokori:- MHESHIMIWA unadhani hakuna ajenda za siri ambazo huzifikirii tu za karibu kila ufanyalo?
- Si unajua ajenda yako ya siri ifichwayo ndani ya umchekeavyo FULANI kwa nia ya kumuambia unampenda HUYO FULANI , kwa kuwa HUYO FULANI ni maarufu na watu kibao wanamchekea hovyo hudhani usingefanikisha DHUMUNI HILOHILO la yeye kukustukia KWANZA kabla HUJAMUINGIZA MKENGE kirahisi kwa kumgeuzia kibano ukawa ni weye tu UMNUNIAYE kila akija KAZINI/pale umtegeapo BILA SABABU kwa BONGE LA MNUNO mpaka ajiulize wewe unatofauti gani ya ladha?
- Kwani hujui kuwa ajenda za SIRI za baadhi ya Blogu ni KUJISHEBEDUA?
NI WAZO tu hili MAMA Kisebengo na USITISHIKE nimeliacha MHESHIMIWA!
Hebu ASWAD warudishe kitu -
Au tu ASWAD walete na -SHINE
-
UDHAIFU wa -``Kama tamu KWANGU itakuaje CHUNGU kwako?´´
Posted: January 7, 2010, 1:45 pm by SIMON KITURURU
[Tahadhari: Tararira hii ina ZIGZAG kimtiririko!:-(]
MAKALI ya mitazamo binafsi ya BINADAMU ni moja ya sababu DUNIA ni tamu na KILA LIMTU liamualo kuhangaikia penzi litapata MPENZI,...
...kwa kuwa hata mtazamo wako BINAFSI ule wa kuwa JAMAA LIMELOSTI a.k.a HALINA MPANGO ,...
... kwa BINTI YAKO mtazamo wake binafsi WA SWALA HILO HILO unaweza tu kuwa
- ``JAMAA halina MAKUU ndio maana linavaa MIDABWADA na halipendi MAGARI ndio maana kila siku linatembea kwa MIGUU hata DALADALA halipandi YANI kwa kutopenda makuu YANI´´ , ...
` `.... na LINAPENDA MAZINGIRA HILO na ili kutunza mazingira haliogi kwa SABUNI halafu napenda kweli harufu yake ya asilia ya jasho lisilokauka vizuri la uvundo wa KIKWAPA chake kizuri,.... ´´
.....-``YANI NALIPENDA HILO wewe we ACHA TU!´´[sentensi hii ya mwisho imebaniwa pua!:-(]
Swali:- Si unajua hata HITLER alikuwa na poozeo limpendalo mpaka kufa kwa jina Eva Anna Paula Braun?
MAKALI ya mitazamo binafsi ya BINADAMU ni moja ya sababu DUNIA ni chungu kwa kuwa WASIKIAO UTAMU mara nyingi hawachunguzi kama utamu wao si matunda ya wasikiao UCHUNGU.
Swali:- Kwani mara ngapi wakati unafurahia utamu wa UBWABWA huwa unafikiria atokwavyojasho na kuwashwa MVUNA MPUNGA ?
Kwa kifupi ILE KITU TAMU KWAKO mara nyingi ili iwe TAMU KWAKO kuna uwezekano umeiachanisha kifikira na swala zima la ni KWA akina NANI tamu kwako ni CHUNGU KWAO.:-(
Na MAKALI ya MITAZAMO binafsi ya BINADAMU hasa waliojiaminisha kuwa wao WANAAKILI na wafikiriavyo na WAISHIVYO ndivyo sahihi,....
....KIRAHISI, ....
......husababisha DUNIA izidi kuwa JINGA kwa IDAIWAO WANAAKILI , BUSARA, NA WANAUZOEFU WA MAMBO kung'ang'aniza kuwa KWELI waijuayo kivyao kwa kuwa KWAO iliwasaidia kufanikiwa waamini hiyo ndio KWELI PEKEE HATA MAISHANI MWA WATU WENGINE kwa kusahau kuwa DUNIANI kuna uwezekano kabisa hakuna WATU WAWILI wanogewao hata UBWABWA sawasawa.
Swali:- Unafikiri kama wewe HUWA unanogewa UBWABWA huwa unaogewa sawasawa na MAMA YAKO mpenda UBWABWA?
- Kama wewe ni MTANZANIA na umeshawahi kusimuliwa stori za JKT, unafikiri ushawahi kusikia stori mbili zilizofanana za jinsi WANAJKT uliokutananao wakidai walikuwa wanatoroka JESHINI au tu kazi sawasawa?
- Unafikiri ijulikanao WANAAKILI hajuilikani hivyo kwa kufuata mfumo huu tu wa sasa na tukibadili MFUMO tutastukia kuwa kuna bonge la UJINGA katika wenye akili wa sasa ndio maana lenye akili sana SASA HIVI DUNIANI ukichunguza labda liko bize linatengeneza bomu.
- Au unafikiri mwenye akili sana sasa hivi anafanya nini?
Pia kuna SAIKOLOJIA nyuma ya wenye wazo - ``KAMA SIFANYI MIMI NANIHII basi na NYIE WENGINE MSIFANYE!´´ ambayo chimbuko lake kwa wengi ni UBINAFSI ingawa inaweza ikafichwa katika hoja ya ASIYETAKA wengine wafanye ya ``NAWALINDA wengine kwa kuhakikisha nisichokiamini na kutokifanya basi na WENGINE MSIFANYE´´.
Swali:- Kwa kuwa hunywi pombe si ndio inaweza ikawa ndio hoja yako kuwa na wengine WASINYWE ingawa upendavyo ngono hovyo bado inawezekana ikawa bado hutaki na mke wako nae hovyo aonjwe?
Kwa kifupi wala usingehitaji kusoma yote niliyoandika hapa kwa kuwa nilichotaka kusema ni :
-Kama tamu KWANGU inaweza ikawa ni chungu kwako na BONGE la BUSARA na AKILI kwako labda lingenitia uvivu wa kuwa na hamu ya kuwa HAI KESHO.:-(
Swali:- Unafikiri ni wangapi hasa walioko kwenye dini ziahidizo PARADISO baada ya kufa ambao TAMU YAO imetiwa utamu na ahadi tu za PARADISO ila bila hilo TAMU yao ni BONGE la CHUNGU?
- Na si unakummbuka tamu kwako wakati unanjaa inaweza ikawa wala hainogi kama umeshiba na unajilazimisha kula?
...na MAKALI ya mitazamo binafsi ya BINADAMU ni moja ya sababu DUNIANI hakutaisha VITA kwa kuwa tu hata jinsi ya KUMPENDA MUNGU wa AMANI NA UPENDO ,....
..... iaminikao ndio wenye AKILI wanatofautiana MITAZAMO BINAFSI ya kusambaza dini au tu KUMTETEA MUNGU.
Swali zaidi kiduchu:- Kwa mtazamo wako ushawahi kumtetea MUNGU?
- Unadhani Mungu muweza yote kwa mtazamo wako anahitaji mtetezi BINADAMU?
- Huwa unafikiria kama tamu KWAKO inautamu gani KWANGU?
NI WAZO tu hili MHESHIMIWA na usikonde!
Tutulie na WASELA
Kwanza-CLOUDS Production enzi hizo za mwanzo wa Bongo FLEVA- Msela
Pili- Dopa MAN- Msela
Tatu -Mangwair -Msela
Nne- Nuru THE Light- Msela
-
Kwa Dada YASINTA NGONYANI!
Posted: January 5, 2010, 4:05 pm by SIMON KITURURU
-
Hongera Rais ZUMA kwa kuoa MKE wa TATU kiwaziwazi!
Posted: January 5, 2010, 3:10 pm by SIMON KITURURU
Pamoja na Rais Zuma wa AFRIKA KUSINI kulalamikiwa na baadhi ya watu kibao kwa uamuzi wake wa kujipatia JIKO la TATU kwa madai yapewayo nguvu na apendavyo kutunza MILA na DESTURI za KABILA lake,.....
....twaweza pia kupata changamoto kwa kujiuliza hivi ni MILA na DESTURI zipi ambazo ni busara kuzitunza.
Na wakati tunafikiria hilo kama tu kawaida ya WANYOSHEA VIDOLE wengine katika yao,...
..... twaweza pia kujiuliza HIVI watoto wazaliwao leo AFRIKA hasa mijini ni mila gani NA DESTURI za KIAFRIKA ambazo wanajifunza na kujivunia ili hapo baadaye angalau wawe na CHAKUJIVUNIA?
Halafu:- Kwani unafikiri ni watu wangapi ambao hawakiri tu kuwa na WAKE WENGI kisa kuna MILA na DESTURI labda hata zidaiwazo ni za KIKRISTO ambazo wanazitunza kinafiki kwa kuwa wanawasiwasi watu watawaonaje kwa hiyo nyumba ndogo zao a.k.a WAKE WENGINE wanawafanya siri?
- Kiislamu inajulikana kuwa kama unaweza ni ruksa kuwa na wake kadhaa LAKINI unafikiri KIKRISTO ni kipindi gani WAKE LUKUKI ilibadilishwa na MKE MMOJA ikawa ndio mswano wakati yajulikana akina King David , Solomon na watu kadhaa ambao wanaheshimiwa KIBIBLIA walikuwa na WAKE LUKUKI?
- Unafikiri huyu mke wa tatu wa Rais ZUMA alimuomba RAis ZUMA apimwe UKIMWI kabla hajamkubalia hasa kwa kuwa inajulikana na DUNIA nzima Rais ZUMA alisha ngonoka na Mwanadada mwenye UKIMWI na kudai ili kuzuia VIRUSI alioga chapuchapu?
HONGERA Rais ZUMA kwa kutoficha udhaifu wako kama wengine watusaidiao kueneza UASHERATI mtaani KISIRI wapendavyo kukaa viti vya mbele MAKANISANI na kujifanya NANIHII hawananihii!.:-(
Hebu ZE COMEDY wabadili kwa- SEGERE
Au tu FATUMA RAJABU alete -DOMO LA UPAWA
-
Jinsi HANITHI astukiavyo wake UHANITHI!:-(
Posted: January 3, 2010, 3:03 pm by SIMON KITURURU
....kwa VYOVYOTE kuna kitu HANITHI alikuwa anajaribu kufanya wakati alipostukia NA KUHAKIKISHA kuwa ni kweli katika shughuli NZIMA udhaifu wake yeye ni kweli ni UHANITHI!:-(
Swali:- Unafikiri kama mtu HAJARIBU ni MAMBO MANGAPI anauhakika katika shughuli YENYEWE yeye ni HANITHI?
- Si unajua kama moja ya NUIO la MWAKA HUU ni KUJARIBU, katika kujaribu moja la jambo ambalo MHESHIMIWA unaweza kustukia ni kwamba NI KWELI katika shughuli uliokuwa unasita kujaribu MWAKA JANA haki ya mjusi tena ni kweli MWAKA HUU UKIJARIBU katika shughuli hiyo utajihakikishia HUIWEZI na kikubwa katika hilo weye ni HANITHI?
- Lakini weye MTANZANIA si unajua ni kwa kujaribu tu ndio unaweza ukawa KIKWETE wetu wa baadaye KATIKA SHUGHULI na katika UHASISI wa nani atakuwa RAIS wa kikweli aletaye maendeleo ya kikweli TANZANNIA utasahaulisha watu weye SIO Rais NYERERE kwa kusababisha watu wasahau aliyofanya Rais Nyerere kwa kuwa yako yamesababisha mpaka PANYA na MENDE wanavitambi na wavivu kuingia katika nyumba za watu TANZANIA kudoea chochote kwenye masinki?
- SI unajua lakini labda ni weye ufikiriacho ukijaribu ndio JAWABU LISAWAZISHALO hata uzembe wa akina SIMON KITURURU ambao hata kumpa mimba mtu bado hawajafanikisha katika jamii iaminiyo moja ya shughuli ya walimwengu ni kuujaza ULIMWENGU?
Tukiachana na yote yasiyo GUSA KIPELE au kukuna kipele cha hoja hii;...
......FANIKISHA MKUU mwaka HUU kwa kuwa bila kujaribu KUNAUWEZEKANO hata wewe mwenyewe huwezi kujihakikishia ni JINSI GANI UNAWEZA.
-AU?
NIMEACHA hoja hii banangenge MHESHIMIWA na kwa MARA NYINGINE HERI ya MWAKA MPYA MKUU!
Na kama wewe ni MSICHANA na kisiri unanipenda ,....
...chukulia katika picha ifuatayo weye ni hilo doli NILILOJARIBU kulipa faraja ndani ya pendo.:-(
Au tu James Brown ashawishi kwa katika kurudisha ustaarabu hapa kijiweni kwa kudai-Get Up Off That Thing
James Brown aendelee kwa- I feel Good
Au tu Scarface abadili ustaarabu KABISAA kitu ambacho kinaweza kuwa sio ustaarabu kama KATIKA KUFIKIRIA hunajicho kwa kudai - Recognize
-
Kabla MATATIZO ya MWAKA JANA hayajajirudia tena MWAKA HUU!:-(
Posted: January 3, 2010, 1:59 pm by SIMON KITURURU
Swali:- Kama ulikuwa na tatizo mwaka jana UNAUHAKIKA UNAJUA kwa uhakika MWAKA JANA tatizo lilikuwa ni nini?
Lakini,.....
....KAMA HUBADILI ulivyokuwa au tu ULIVYOFANYA mwaka jana,...
..... nafikiri ni haki ya wapendao kulaumu WATU wengine ,....
.... KUKULAUMU ......
.....mpaka USIPOKUWA MJANJA WANAOKULAUMU unaweza kufikiri yao ya MWAKA JANA HAYAKUWA NA DOSARI na yalimchekesha YESU , Mohamedi, au tu KIMADA, hata kabla ya kuwafanya wajilaumu KITU waliokuzaa WAZAZI,...
...KWA kuwa LABDA NI KWELI .....
...kama hubadili ULIVYOFANYA mwaka jana , LABDA usitegemee sana MWAKA HUU kwa kuwa CHEUSI DAWA hupendi ulivyo kuwa mweusi mwaka jana basi kwa staili ileile ya MWAKA JANA ambayo mkorogo HAUKUKUCHUBUA SURA itakuchubua SURA MWAKA HUU.:-(
Na kwa BAHATI MBAYA,...
... haki ya nani tena LABDA ULIVYOFANYA mwaka jana MPENZI CHEUSI DAWA ambavyo HAVIKUZAA MATUNDA mwaka jana ,...
.. ni staili ileile IFANIKISHAYO VITU MWAKA HUU ambayo uliwahi tu KUIFANYA mwaka mmoja MZIMA kabla ya SHUGHULI ITAKIWAVYO KUFANYWA ,......
....na ukifanya vilevile vya MWAKA JANA, mwaka HUU italipa kweli mwaka huu hata kama MWAKA HUU cheusi dawa NIA YAKO sio TENA kujichubua sura kwa kuwa umeshastukia kuwa unalipa hivyohivyo ulivyo na BONGE LA MWANYA ambalo ulikuwa unafikiri limekaa kama PENGO mwaka jana ila umestukia KWELI KABISA KAMA NYOKO MWAKA HUU kuwa hilo ni MWANYA tokea enzi kama tu ILIVYO mwaka HUU.:-(
Swali:- Si unakumbuka MAJARIBIO ya mwaka jana ya KUFANIKIWA yaliyoshindwa haina maana katika yale majaribio ya MWAKA JANA kuna kitu ulikuwa UNAKOSEA?
- SI unajua ukijaribu kama mwaka jana labda MWAKA huu ndio utafanikiwa kupata hata kinamna uhangaikiacho labda katika PENZI kina UKIMWI?
- Unauhakika uhangaikiacho kufanikisha KIKIFANIKIWA huo hauta kuwa mwanzo wakustukia ndio kwanza inabidi uanze swala zima la uhangaikaji UPYA?:-(
NI WAZO TU HILI Mkuu na haki ya nani USIKONDE!:-(
Ngojea FLOETRY wadai katika mtongozo -SAY YES
Tantra Zawadi afikirishe.....
Tantra ZAWADI arudie kumuongelea- GIRL
Au tu twende tena GUADELOUPE ili FUCKLY arudie kitu -DOUDOU
Au tu ni kuache na Baadhi ya PICHA za kabla na BAADA ya MWAKA 2009 kitakatifu....
Blah blah blah
Fish cakes
Alas a fish cake.
Yet more fish cakes
Guess what ... yeah ... fish cakes.
The end of the fish cakes