SIMON KITURURU- MAWAZONI
-
Jifunze UFISADI- KOZI ya KWANZA.
Posted: May 16, 2008, 8:18 am by SIMON KITURURU
Mbinu moja maarufu sana ya kumshinda adui ni kumjua adui.
Si utani , ufisadi ni bomba la kitu maarufu duniani na waongeleao ufisadi mara nyingi ni wale wasiofaidika na UFISADI.
Siwezi kusema kuwa na utaalamu na somo hili ingawa nadhani kuwa, inawezekana hili somo halihitaji uende chuo chochote ili kufudhu jinsi ya KUMFISADI Mtu , Nchi au Kanisa.
Swali:- Ushawahi kujiuliza kwanini unaweza kuona jinsi gani MFISADI anavyofanikisha UFISADI hata bila kwenda kusomea popote wakati huoni taaluma ya PROFESA wa UCHUMI au wa KILIMO atatuavyo matatizo ya kiuchumi wa Tanzania utegemeao kilimo?
- Unafikiri kwanini katika silabasi za shule ,hakuna kozi ya UFISADI?
Naamini UMIMI uko ndani ya binadamu tokea atokee duniani au enzi hizo binadamu walivyofikia wawili hapa duniani.
Naamini chembechembe za ufisadi zilianza kujijenga ndani ya binadamu kuanzia pale alianza kuamini uwepo wa uchache wa vitimiza mahitaji yamuwezeshayo binadamu kuishi.
Mahitaji ya binadamu na jinsi ya kuweza kuyatimiza yanaendelea kutofautiana kulingana na upeo wa akili ya binadamu ulivyo, hasa ukikumbuka enzi za KUTUMIA TREKTA na zile za KUVAA KIBWAYA , mahitaji ya RAIZONI, kunatetesi yalikuwa au bado yanatofautiana.
Kipindi cha kuishi kwa kuokota mizizi na matunda, mjanja alikuwa ni yule atakayeweza kuwa na mizizi na matunda wakati kuna uhaba wa mizizi na matunda. Lakini wakati hivi vitu(mizizi na matunda) viko vingi , ilikuwa huwezi kumtisha Mr Kidume, kwa kumnyolisha eti una mapera mengi kuliko yeye, wakati anajua kuwa hata pale apendapo kumuangushaga Binti Kitoweo jua likizama, ni chini ya mti wa mpera uliojaa matunda.
Ukiruka kutoka enzi za kupigania embeng'ong'o na mihogo mpaka kipindi hiki ambacho bado wengi hapa duniani tunaweza kupigania embeng'ong'o na mihogo ingawa wengine wanaendesha magari aina ya FERARRI na WANA VIJISENTI BILIONI kadhaa katika benki kadhaa hapa duniani, unaweza hata ukakubaliana kuwa AKILI za BINAADAMU ni UJINGA uendao na AKILI za kiBINAADAMU, hasa katika staili yake ya kusikilizia ladha ya kuridhika au MAFANIKIO.Inashangaza jinsi binadamu awezavyo kujilimbikizia wakati wengine wana njaa, kama unaweza kusahau UBINADAMU.
Unakumbuka NGAZI za MAHITAJI kwa mujibu wa Maslow (Maslow's hierarchy of needs?)
DUH!
Naachia hapa kufundisha somo hili la UFISADI .
Unajua TENA, naweza kukudanganya bure!
Ila kumbuka kuwa chembechembe za ufisadi zipo tu hata ndani yako.
Usipoangalia , unaweza ukajikuta umeamsha chembechembe za UFISADI na ukazirutubisha pia kiaina.
Katalisti za kuamsha mshawasha wa KUFISADI ziko bwelele, zinakuzunguka hadi msalani pale ustukiapo maji hayatoki na pesa za kununulia karatasi za kujipakaza mavi sehemu zifichwazo na chupi hauna. Halafu unajua kufutia kinyesi ukutani nishai na mchanga unaweza kuwa na minyoo.
DUH!
Usitishike lakini! Labda tusipoharibu mazingira tunaweza kuwa na majani bado au mawe yafaayo kutumika kama MAKOKONEO.
LAKINI......!
Baadhi za Katalisti ziwezazo kuathiri ashki za UFISADI wako ni:- Utu WAKO
- Umasikini wako au jinsi ufikiriavyo kuwa wewe ni masikini hata kama si.
- Uelewaji wako wa staili yako ya kuridhika .
- Udhaifu wako wa Muonekano au sehemu(status) yako katika jamii
- Udhaifu wako ukuwezeshao kudokoa mboga ukiachwa jikoni peke yako au Ukiwekwa kwenye ofisi ishughulikiayo VITOWEO ;kwa mfano kama wewe Raisi ofisini , Mjumbe wa Nyumba kumikumi au kama VIJISENTI tu vinakatizakatiza kwenye kona yako halafu unahisi hutadakwa ukidokoa.
- nk......kadhaaa wa kadhaaa.
JIADHARI!
DUH!
Samahani kwa simulizi chafu!
Hebu tumsikilize Ngozi Okonjo-Iweala akigusia maswala ya UFISADI au mambo ya : How to help Africa? Do business there
Au Angalia tu ujinga kama vile DUME ZIMA liwezavyo kutumia muda wake MUHIMU wa dakika kadhaa KULIA katika BIG GIRLS DONT CRY
DUH !
WIKIENDI NJEMA!
Mpate tu PAPA WEMBA au VIVA la MUSICA
-
Kilema cha MAANDISHI , PICHA, TV,sinema au KUSHUHUDIA , hata katika kusaka habari za MPENZI KIBOGOYO.
Posted: May 16, 2008, 5:41 am by SIMON KITURURU
Nasikitika kuwa maandishi , picha na hata ushuhuda wa macho inaweza kuwa si msaada kwa binadamu katika kukabiliana na ubinadamu au dunia hii, ingawa unawezakusema unajifunza kitu kwa kuangalia picha za nanihii au kusoma maandishi.
Ubinadamu nishai!
Karibu kila agusacho au kutumia kama binadamu, kina udhaifu.
Ndio maana hata kama huamini Mungu, ni vigumu kuwa na uhakika kuwa hakuna Mungu au angalau LIKIUMBE ambalo linasababisha binadamu huyu mwenye mapungufu, pamoja na mende, wawepo hapa duniani.
Usitishike sana!
Inawezekana nilivyovitaja vinakusaidia.
Na ni ukweli naheshimu maandishi, picha , picha zitembeazo na pia , ushuhuda wa macho.
Naandika hapa leo hii kwa sababu nimeshangaa kujikuta nabishana na watu kuhusu umuhimu wa vitu hivi, kitu ambacho sikudhani kinaubishi.
Au nisemee...
Naamini kabisa kujisomea hasa vitabu, ni bomba la ujanja katika kutekenya akili.
Ila sipingi umuhimu wa picha au picha malaya(moving pictures, TV,Videos,etc.) kwa jinsi zisaidiavyo uelewekaji wa jambo kwa kutumia kona nyingine. Pia sisahau msaada wa maswala ya shuhuda za kuona papo hapo.
Nachojaribu kusema ni.......
1. Maandishi huhifadhi taaluma vizuri sana, ingawa stori za paja la kuku, kama hujui kuku yukoje, akilini lawezakufanana na paja la kicheche uliyemzoea baada ya kumalizia kusoma stori za kuku.
Utamu wa kusoma maandishi ni pamoja na jinsi ukupavyo uhuru wa utalii wa ubongo
( imagination).
Katika maandishi na kama hujawahi kuonyeshwa michoro ya picha za shetani mwenye mapembe, basi shetani anaweza kuonekana anasura kama yule kidume au kijike umuogopaye, ambaye anaweza hata akawa ni mwalimu au mme wako.
Swali:- Kama usingeonyeshwa michoro ya kubunia ya shetani au YEsu , unafikiri mawazoni kwako Yesu na Mkwawa wangekuwa wanasura au wamevaa ulimbwende aina gani?
- Tukiachana na maandishi katika barua kwa Baba:Wakati unaongea na simu na LIMTU lako , ushawahi kufikiria unayeongea naye ananukaje mdomo?
2. Maswala ya video na picha ni kiboko pia!
Usipoangalia unaweza kusahau kuwa si lazima yarahisishe kwako kuelewa kuwa hiki ni KIJIJI cha MATOMBO au hivi ndivyo jinsi BATA wafanyavyo MAPENZI.
UKiona picha au video ya kijiji ,ni mpaka uambiwe kuwa hiki ni kijiji cha MATOMBO ili uelewe kuwa hapa si kijiji cha KIABAKARI.
Ukiona picha au video za Bata wanafanya mapenzi, kama hujui kinachoendelea, unaweza kufikiria kuwa BATA wanapigana.(Kwani hujawahi kusikia waliofumaniwa na mtoto wao wakati wanafanya mchezo wa baba na mama halafu mtoto akalia kuwa BABA ANAMPIGA MAMA?)
Swali:- Ushastukia kuna watu duniani , picha ipigwayo Tanzania au GINI ya Ikweta(Equatorial Guinea) kwao ni sawa tu, hasa kutokana na kufikiria Afrika ni nchi moja?
3. Mwisho ....
Nakiri tuko tunaohusudu taaluma na ujinga tuufyonzao kwa kushuhudia jambo kwa macho yetu wenyewe.Lakini swala la kushuhudia jambo, ni rahisi kujidanganya kuwa utaelewa au hata kuweza kuwa mtoa ushuhuda mzuri zaidi kwasababu ulikuwepo wakati kitendo kinafanyika. Cha ajabu ni kwamba, kama hujui mchezo wa Kriketi , hata uutolee macho kama bundi, huwezi kuelewa daktari anafanya ninikatika operesheni yako ya jando, kama huna taaluma husika.
DUH!
Kuelewa ni nini kinaendelea kunahitaji tetesi za kujua unachoangalia ni nini, la sivyo ,UTABUNIA.
Katika vita zetu za kutumia SILAHA za mkuki na mapanga , hili likitu ambalo jamaa anakunyoshea bila kulirusha au kwa jina jingine BUNDUKI , mtu unaweza kulidharau kuwa si SILAHA na wala haliui kirahisi tu kama au kuliko mshale wako wenye sumu ya nyongo ya kenge, kama hujawahi kusikia duniani kuna hata kitu bomba kama GOBOLE.
Sasa cha kujiuliza tu ni kwamba.....
.....Haya yote tuyatafutayo au kuhifadhi katika maandishi , picha au ubongoni baada ya kushuhudia,si ni maswala tu yasaidiayo tu kujazia muda wa binadamu hapa duniani akiwa safarini kutoka kuzaliwa kuelekea kufa?
.......Haya mavitu tuhangaikayo kuyatafuta hata kwenye dini , pombe au moshi wa majani ya mpapai, si ni majivitu ya kujaribu kujazia tu haya maisha ladha tamutamu kunoga ili katika ujazo, yazidi kupunguza kusikia kwetu uchungu au yajaribu kurahisisha kutupatia kanjia kakuendeleza tamutamu kunoga baada ya wewe ,mimi na yule kukata roho , kufa au kuanza?
EE BWANA EEH!Naaacha basi kitopiki!
Kumbuka Mimi Nawaza tu hapa!
Hebu twende KANADA tukamsikilize tena RUSSEL PETERS akishauri WAZUNGU waanze KUPIGA WATOTO WAO.....
Au Ngojea twende NIGERIA tuangalie mambo ya KIDUNIA kama VILE ya akina DADA wakipigana....
Tulia tu na ERIC SERMON akija na kibao REACT
Blah blah blah
Fish cakes
Alas a fish cake.
Yet more fish cakes
Guess what ... yeah ... fish cakes.
The end of the fish cakes