SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • NAOMBA UFUNGUO wa MOYO wako ili UJIDANGANYE kuwa sitaUMIZA roho YAKO.

    Posted: May 4, 2008, 5:58 pm by SIMON KITURURU
    Unaporuhusu mtu akujue, unampa huyo mtu ufunguo wa kiboksi cha UJUZI wa wewe ni nani.

    Akujuaye halafu atake kukuumiza, huwa habahatishi madoido au staili ya kukutomasa kidonda.
    Akujuaye ndio anaweza akawa anajua mpaka staili yako ya kulia, kupiga mayowe au hata ya kulamba kamasi lilengalo mdomo ukilia.

    Lakini...
    .. ni vigumu kukiri kuwa kama ufurahiavyo kumuona achekaye, kuna wachekeshwao na muonekano wako wa sura wakati unalia.
    SI unajua unaweza ukawa unakunja sura kama unanusa kimavimavi wakati unalia?

    DUH!

    Kama watu waogopavyo ngurumo ya radi wakati wanajua ukisikia ngurumo maana yake radi imekukosa, ndio wengine wahudhunikavyo kumuona anayelia bila kugundua kuwa tatizo ni kile kimlizacho mliaji na sio aliavyo.

    Kulia humsababisha mliaji asikie ahueni.
    AU?

    Tatizo ni kwamba, binadamu hapendi upweke kama anaishi maisha ya kawaida ya kibinadamu.
    Utajikuta umelazimika kumpa mtu fulani funguo ya moyo wako ili achokonoe roho yako.

    Nakutakia kila la kheri katika kusubiria uliempa ufunguo wa kiboksi cha ujuzi wa WEWE NANI afanye ubinadamu na kukuumiza kiduchu kabla haja pulizia.
    Ndio maisha!
    Kwani bila maumivu tungejua utamu ni nini?

    Kwa kherini kiduchu wadau wa blogu hii!
    Tutaonana tena kijiweni baada ya siku kadhaa wa kadhaa!
    Nakuacha na Patrice akupe EVERYDAY GOOD

    Au ngojea tu aseme HOW DO U CALL IT
  • SIKUPENDI kwa sababu WEWE MZURI!

    Posted: May 4, 2008, 5:18 pm by SIMON KITURURU
    Msichana mzuri kumzidi Khadija, inaweza ikawa ndio sababu ya Khadija kumchukia Zubeda.
    Kuna wengi ambao watakubali kuwa......
    ....... akisifika kwa mazuri kuliko wewe, na kama huoni hata jinsi yakukaribia mafanikio yake, anaweza akawa TISHIO KWAKO na sio faraja.

    Kuna ambao watakubali kuwa.....
    .....Uzuri wa unayefikiri mko sawa au umemzidi kakitu, ni jinsi asivyokutishia maisha na kukufanya ujihami na kujikuta unaanza kupiga mswaki, kuchana nywele, kubadilisha chupi au kuficha kile kitu uvunguni kabla hajatokea.

    Kuna wengi ambao ukifanana fanana nao wanaweza kukualika kirahisi UGAli ukiiva bila kujali njegere hazina vitunguu.

    Lakini....
    ....Tajiri na masikini ingawa wote ni watu wazuri , wanaweza kujisikia huru zaidi kula mbatata katika sebule au hoteli tofauti.
    DUH!

    Kuna watu husahau kuwa hata pendo huweza kuwa ni maumivu kwa umpendaye.
    Kuna watu wanaweza wakawa hawakupendi kwa vitndo vyao wafanyavyo kwa mapenzi yao ya dhati.

    Swali:
    • Hujawahi kumzimia mtu mpaka ukashindwa hata kuongeanaye akikuchekea?
    • Hujawahi kustukia karoho ka-kwanini yule na sio mimi baada ya kushuhudia na kuhisi labda yule umpendaye kila kitu utakacho kununua yeye anapewa bure?

    Kumbuka tu kwamba kipimo cha nani mzuri kubwa kuliko akilini mwako na katika jamii yako hutokana na mlivyoathirika kisaikolojia.

    Kumbuka.....
    ..... Mungu inawezekana ni mzuri kwako, lakini ni mbaya kwa jamii ya KISHETANI.
    ......Demokrasi ni nzuri kwa viongozi wa Marekani wenye pesa za kugombea Uraisi, lakini Ukomunisti mzuri kwa viongozi wa China.

    ......Wali mzuri kwa watu fulani, lakini wengine hawashibi bila ugali.


    Lakini...
    ....Kuna mtu anaweza kukupenda kwa sababu ya ubaya wako ambao unaweza ukawa unafaida zaidi kuliko uzuri wako kama mabepari walivyostukia.
    Swali:
    • Unakumbuka asilimia kubwa ya uvionavyo katika maduka fulani, viko dukani kujaribu kukukumbusha kuwa HUJAPENDEZA na wewe MBAYA ili ununue mafuta ya mgando,chupi fulani au raizoni ?
    DUH!
    Naacha topiki hii!
    Mpate Mighty Shadow akupe kibao WHATS WRONG WITH ME


    Au tulia na Arrow wakikupa HOT HOT HOT
  • WAKATI unamkana NDUGU yako aliyedakwa UCHAWI.

    Posted: May 4, 2008, 4:32 pm by SIMON KITURURU
    Kukana kitu ni jitihada za kutaka kuhakikishia wengine kuwa huhusiki kwa sababu kwa kisiri na kama wewe ni mkweli kwa wewe, ulichofanya kisha kuathiri na hata ukaneje ushaathirika nacho.

    Ukishaonja ukwaju , unaweza kushindwa kuelezea tofauti ya utamu wake na embe bolibo, lakini hata ukane kwa wengine hujui utamu wa ukwaju, unajua chini ya dhamira yako kuwa ukwaju na asali vinautamu tofauti.

    Nikikuudhi au kukutia aibu, unaweza kukana uhusiano wetu , undugu wetu , hata kama watu wanauhakika mimi fundi koroboi wako.

    Nikisifika, unaweza kusimulia mpaka jinsi babu yako mzaa babu na shangazi ya babu yangu walivyokuwa marafiki shule ya vidudu, ilikuonyesha ukaribu wako kwangu.

    DUH!

    Lakini....
    ......Hata ukikana, UKWELI uko palepale.

    Gari la zamani hata ulipake rangi bado ni baiskeli ya zamani.

    Kukana inawezekana , na watu wanaweza wasijue ukweli kwa muda fulani kwa sababu binadamu ni mvivu wa kufuatilia ahisiyo ugumu na ambayo hayamsaidii kupata utamu HATA AKIJUA sasa hivi.

    Unaweza ukawa unataka kujua kivipi BALOZI wa NYUMBA kumi kumi wako katajirika haraka haraka alipochukua ofisi kwa sababu zako binafsi za kuhisi KUTAJIRIKA KWAKE ni KUNYONYWA au kuibiwa kwako, la sivyo inawezekana usingejali kwanini ghafla tu, RAIS wako MTUKUFU kawa bilionea wakati nchi ina madeni.

    LAkini....
    .....jina lako likiwa linatajwa mara kwa mara likihusianishwa na uchawi, MCHAWI au Mama Ntilie, kuna watu kutokana na uvivu wa kufuatilia na urahisi wa kuhitimisha , watakua wanadhani wana uhakika kuwa wewe mchawi, ulilogwa au ni MAMA NTILIE.

    Mchezo wakuhitimisha bila ya kuwa na vigezo vithibitishavyo nani alimpa kuku mimba lililo rutubisha yai la kwanza, ningependa libakie tu katika sentensi; kati ya yai na kuku sijui nini kilitangulia kuwepo duniani.

    NAKUBALI unaweza kudai ni yai lilitangulia bila ushahidi zaidi ya kwamba katika kundi wewe ndio UNASAUTI KUBWA na wengine wameathiriwa na jamii kiasi kwamba katika mambo mengi kiduchu ya jamii, WAMEFIKIA kukubali tu kutokana na kutojiamini kama wewe ujiaminivyo katika hata mambo usiyojua.

    NAKUBALI unaweza kukana!
    Kana tu, hakuna noma!
    Swali:
    • Ushawahi kukana wewe sio wewe?
    • Unajua unaweza kukana kile kitu lakini ukaendelea kuona aibu kutokana na kitu hicho hicho ulichokuwa shupavu kukana?

    Usisahau kuwa, mara nyingi unakana kutokana na kujihami kuwa ukikubali utajiweka katika mazingira mabaya zaidi.

    Usisahau kuwa, hata usiyo yaelewa lakini ukahisi ukikubali utaenda paradiso, hukawii kukiri kuwa wewe Msabato au MUNGIKI.


    Naacha basi topiki hii usije ukanikana bure!
    Samahani lakini kwa kukutia aibu!

    LAkini....
    WHO wrote the BIBLE pt1?(msikilize basi Robert Beckford)


    Kuna mdau kanistua kuwa nagusia sana dini .Napenda kukiri naguswa sana na dini na ni mifumo yake tu inayonizingua....
    Lakini nasikiliza ya ulimwengu tu kama ya Timbaland na Magoo wakikiri INGAWA hawamuelewi......(samahani wanatumia lugha chafu!)

Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs