SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • NIKIKUANGALIA wakati UNA-SHAbikia/CHEkelea/LIA TIMU yako IKISHINDA!

    Posted: April 30, 2008, 11:31 am by SIMON KITURURU
    Ukiwa na TABIA ya kumtazama binadamu, utastukia kuwa huhitaji televisheni wala kucheza bao ili ujiliwaze.

    Binadamu hakosi jipya la kukustaajabisha, kama unatabia au jicho la kumchunguza.

    Na....
    .....ukijenga tabia ya kumtazama sana binadamu , iko siku utastukia kuwa, kama ni kubwa zima halafu halitumii kinyoleo, linaweza likawa lina nywele nywele zinakua kuanzia mashavuni kama ni janaUME, au linakua manyoya mpaka maeneo ambayo kama halijavaa kificha nyeti, linaweza kuwa na kipilipili mpaka maKWAPAni. (Na cha ajabu ni kwamba ,inaweza ikawa ngumu kwako au kwangu kufumbua fumbo la umuhimu na madhumuni ya kwanini manyoya na nywelenywele hizi nyingine humuota huyu binadamu maeneo fulani fulani bila ya faida iliyouchi ).


    Binadamu kwa jina la ushabiki anaweza kulia, kupiga mtu au hata kujiua ,timu yake ikishindwa.

    Binadamu hata kama ni mchezaji na achukiaye tabia za kisenge, unaweza ukakuta kampiga busu, akamkatikia kiuno na kumkumbatia mwenziye mwenye sehemu za haja ndogo zilizo fanana na zake ,KISA, amefunga goli, bila kukumbuka kuwa tabia hizo hizo alizofanya kwa kufurahia na aina ya mtu aliyemfanyia vitendo hivyo, ukijumlisha ,ndizo tabia za kisagaji ambazo yeye na jamii yake kama ungeondoa mpira na kuweka muziki wa bluzi , basi angepigwa mawe mtu na wapambe kwa kosa la USHOGA.

    Inawezekana UMUANGALIAVYO mtu , unaOAnisha mahali alipo na nini kinafanyika,ili kuwa na uhakika na kitendo kuwa; ingawa anaguna, haiwezekani akawa anajisaidia haja kubwa sebuleni.
    Si agunaye chooni hata kama kajikwaa huko msalani , atashukiwa tu anaguna kwa sababu anakwenda starehe kubwa?

    Labda ni ka-ubinadamu kakupenda ushindani na kushinda, kamsababishiako binadamu afurahie timu yake ikishinda na ahudhunike akishindwa.
    Lakini si kufurahia kushinda na kuhudhunikia kushindwa , vyote ni vitu vya muda mfupi tu?

    Au labda ni kaudhaifu ka-kibinadamu kakutojua mwisho wa mchezo matokeo yatakuwaje, kamleteako binadamu tamu tamu ya kufuatilia mchezo mpaka mwisho.
    Lakini si wengine huwa na uhakika wakushinda au kushindwa katikati ya mchezo au kabla mchezo kuisha?

    Labda ni ka-utamu wa kushinda au uchungu wa kushindwa , kasababishako unaendelea kuwa mshabiki wa timu fulani.
    Swali:
    • Unajua ushabiki , inawezekana ni aina ya ugonjwa wa akili kama lilivyo penzi?
    • Ushastukia mshabiki , nukta kadhaa baada ya kushinda au kushindwa anaweza kufanya ambacho hawezi kukiri waziwazi amewahifanya maishani?
    • Ugonjwa wa akili ni nini?

    SAMAHANI nawaza tu!
    Si unakumbuka hiki ni kijiwe cha Simon kitururu-MAWAZONI?
    Siku njema!

    Tulia na Acoustic Blues vibes kutoka kwa Eric BIBB akikupa GOOD Stuff

    Au turudi tu kwenye Zouk Love ikija katika wimbo La Zouk Horay kama iletwavyo na Kaysha na kuwa remixed na DJ DUKA(samahani video inaweza kumkwaza mtu fulani au kuwa inamdhalilisha mtu fulani kwa mtazamo wa mtu fulani.Kama mtoto au mkwazika kirahisi, usiangalie .SAMAHANI!:-()
  • UKINUKUU BIBLIA/KORANI au .......kwa MTU asiyeamini MUNGU!

    Posted: April 30, 2008, 10:29 am by SIMON KITURURU
    Binadamu hupenda kunukuu watu, vitabu, matukio, ..... katika kujazia uzito au hata kuhalalisha kitendo au mtazamo wa mlolomo wao.


    Binadamu , kirahisi, husahau wengine hawafikirii wala kuamini ukweli wao ni ukweli hata kama unaitwa sayansi wakati wanamnukuu Einstein kuwa E=mc2

    Swali:
    • Unakumbuka kuna ambao E=mc2 ni= na ALbaMU mpya ya Mariah Carey na hakuna uhusiano wowote na Fizikia(Phisics)?
    Nachojaribu kunong'ona ni:
    ....Unaponukuu mwingine asichoamini , unaweza ukawa unajipotezea muda.

    Ukijikumbusha nukuu za mtoto.....
    .....LImwanaMKE LAKO au LIBWANA LAKO ufikirialo kuwa ni zuri na lina roho nzuri, na ni tamutamu kama lawalawa nyama, linaweza kumliza mtoto mdogo akalia kama vile kaumwa na manyigu , kutokana na kumuogopesha MTOTO, kwa sababu kwa nukuu za mtoto, huliona hilo LImTU LAKO kuwa lina sura kama Nundu na meno kama Ngiri.


    Ni rahisi kusahau kuwa kuna vitu vingi mtu umejifunza kuviogopa na hukuzaliwa unaviogopa, kitu ambacho mwenzio anaweza akawa bado hajajifunza kuviogopa na haogopi kama wewe.


    Sasaaaa......

    ....ukimtishia asiyeamini MUNGU, maswala ya MUNGU , anaweza akamtukania Mungu wako , halafu ukajikuta umempiga ngwala, mtama au hata kuMKOLIMBA , kabla hauja MSaddam Hussein.

    Lakini naamini kuwa....
    ......baada ya UBONGO WAKO kuamini kitu, tafsiri na wapi unanukuu viushahidi vyako au vikupovyavyo roho kuwa uko upande sahihi, HUATHIRIKA.

    Inawezekana umeathiriwa na ELIMU.
    Si ndio maana unanukuu vinavyotoka vitabuni ?

    Inawezekana umeathiriwa na dini.
    Si ndio maana karibu kila jambo utanukuu VITABU vya DINI ,mapenzi au hasira za MUNGU?

    Inawezekana umeaathirika na utamaduni fulani.
    Si ndio maana kuna mahali unanukuu mpaka wacheza Sindimba matiti nje, pale AIRPORT wakati Raisi wa nchi fulani ya Kiafrika kawasili,kuwa wako uchi na wafanyacho si utamaduni ASILI wa KIAFRIKA, iLA, unaamini pamba itokayo India inatengeneza nguo halisi za Kiafrika?

    DUH!

    Sehemu unanukuu, inaweza ikawa ni kama ujumbe uupatao kwa kuangalia sanamu.
    Sentensi uitoayo kwenye sanamu ,inaweza kutowakilisha kwa mwingine ilichowasilisha kwako.

    Swali:
    • Sanamu ni nini?
    • Sanamu huwakilisha nini kwako?
    • Unajua inawezekana kila mtu ANAABUDU sanamu?
    • Mwalimu asimamaye mbele yako darasani, na kuondoka bila wewe kujifunza au kuelewa kitu , hawezi tafsirika kama sanamu liwakilishalo kitu tu chenye jina MWALIMU?
    Kuna atakayesema sanamu huwa alifanyi kitu, linawakilisha tu kaujumbe kawakilishwako na sanamu.


    Lakini...
    ...wako watakao kumbuka, sanamu linaweza kukuangukia na kukuvunja nanihii!

    Naacha basi kukuzingua!
    Usitishike Nawaza tu hapa!

    Karibu tena MAWAZONI lakini!

    Pata basi TAP DANCE kutoka kwa Savion Glover

    Au....

    Mcheki tu Maraya Keri katika wimbo Touch my Body kutoka albamu E=mc2
  • MATANGAZO ya WADAU kiduchu!

    Posted: April 30, 2008, 10:08 am by SIMON KITURURU

    1.Filamu zinazowania tuzo ya Vinara wa Filamu Tanzania zatajwa!

    Filamu zilizoingizwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2007/2008 2007/2008 (Vinara Film Awards), zimetajwa.

    Katika taarifa kutoka mratibu wa One Game Promotion inayoaandaa tuzo hizo, Khadija Khalili, iliyotumwa kwenye vyombo vya habari zaidi ya filamu sabini zinawania tuzo hizo.

    Taarifa hiyo ilizitaja filamu hizo kuwa ni Crying Silently (Kilio Moyoni), Kolelo, Mwanahiti, Zawadi ya Fisadi, Oloboni na Layoni, Mmera (Jando) na Nyamaume.

    Nyingine ni Sumu ya Moyo, Segito, A Point of no Return I, A Point of no Return II, Dar to Lagos, Cross my Sin na Penina.

    Pia zimo Habari Kubwa, Fake Pastor, Chite Ukae, Surprise, Stranger, Fungu la Kukosa, Sea Man, Mzee wa Chabo, Donda Ndugu, I Love You, Miss Bongo I, Miss Bongo II, Revenge, Behind the Scene, na My Wife.

    Taarifa hiyo ilizitaja nyingine kuwa ni My Sisters I, My Sisters II, Machozi ya Nyamoma, Silent Killer, My Wife, Greena, Kiapo cha Damu, Valentine, Mwana Pango, Utata, Yolanda, Picnic, Uwanja wa Dhambi, Misukosuko II, Copy, Lugha Gongana, Mtoto wa Mjini, Nyuma ya Pazia, Macho Mekundu, Tanzia, Welcome Back, Karibu Paradiso, Swahiba, The Game of Love I, The Game of Love II na The Game of Love III.

    Nyingine ni Mahabati, Security, Itunyama, The Body Guard, Agano la Urithi, Ndani ya Gereza, Simu ya Kifo, My Heart, Malipo ya Kisasi I, Malipo ya Kisasi II, Mpasuko wa Moyo I, Mpasuko wa Moyo II, Kisasi na Diversion of Love.

    Taarifa hiyo ilieleza kuwa, majaji watakutana wiki ijayo kuanza kuziangalia tuzo hizo.

    Taarifa hiyo ilisema kuwa filamu zinazowania tuzo hizo ni zile zilizokamilika kutengenezwa Januari 2007 mpaka Machi 31, 2008.

    Filamu zinazowania tuzo za Vinara

    Vipengele vinavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo ni Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Muongozaji Sinema Bora wa Mwaka, Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu na Mtunzi Bora wa Filamu.

    Vingine ni Filamu Bora ya Kutisha, Muigizaji Mwandamizi Bora wa kike (supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Bora kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa Filamu ambao wote watapata tuzo na zawadi.

    Pia itatolewa tuzo ya heshima kwa wale waliotoa mchango wao kukuza sanaa nchini.

    Tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Mei zimedhaminiwa na bia ya Ndovu Special Malt, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Global Publishers.


    2.Kwa habari za ujerumani na historia yake tafadhali tembelea www.malumbosjr.blogspot.com





    3.MK MUSIC GALAXY

    Habari,
    Ule wakati tulio usubiria sasa umefika, Website ya pekee itakayo jishughulisha
    ktk kuutangaza muziki wa Tanzania ipo jikoni na ina karibia kuiva.

    Unataka kusikiliza muziki wa nyumbani? Basi watembelee wajuzi wa fani hii
    kupitia www.mkmusicgalaxy.com kwa miziki mipya na ya kizamani uburudike roho
    yako.

    4.Ushasikia.......
    FotoBaraza?


    --------------Mwisho wa MATANGAZO---------------------------------------

    Kama una muda kidogo, jifunze WAPAGANI wanafikiria nini kutoka kwa MWANABAOLOJIA Richard Dawkins aliyezaliwa NAIROBI , KENYA

Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs