SIMON KITURURU- MAWAZONI
-
USHUJAA wa KUKOPA!
Posted: April 25, 2008, 11:28 pm by SIMON KITURURU
Kukopa ni kazi ngumu, kwa sababu mkopo unakuja na kukutengenezea kasifa wengine wawezako kukaweka ndani ya sentensi kama:JAMAA kwa kukopa hata SERIKALI za AFRIKA hazioni ndani.
Kama si mzoefu, kijasho kitakutoka wakati unafanya maandalizi ya kukopa.
Ukizoea kukopa , unaweza kukopa kisirisiri pia au hata unaweza kukopa sehemu za siri za mwenzio.
Lakini....
....kukopa na staili yako ya kukopa , inategemea tu na ulivyoathirika kisaikolojia fulani.
Swali:- Hivi unakumbuka serikali ya Marekani a.k.a USA ndio miongoni mwa serikali zinazodaiwa mikopo sana duniani?
- Unakumbuka inasemekana sasa hivi MAREKANI haiwezi kumkoromea CHINA kwa vitendo kutokana na CHINA kuwa ndio nchi inayoongoza kwa kukopesha Marekani?
Staili yako ya kukopa , hutegemea sana kuathirika kwako kisaikolojia bado kuna kuhakikishia kuwa wewe unacho au huna.
Staili ya fundi viatu nje ya duka kumkopa mwenye duka, inaweza ikawa ya upole na unyenyekevu kuliko staili ya huyo mwenye duka kumkopa fundi viatu nje ya duka lake , ingawa wote wamechacha.
Swali:- Unajua unabadilika sauti wakati unakopa?
- Unajua unabadilika mwendo ukisha katashauri kumfuata umtongoze na lolote liwe a.k.a mwendo wa kumsogelea unayetaka kumkopa?
Lakini...
..inawezekana mkopaji aliye shujaa si yule aliyezoea kukopa.
Kukopa ni kitendo unaweza kukipamba kwa kusema umeazima.
Naweza kukubishia ukisema kuwa hujawahi kukopa halafu ukashindwa kunibishia ingawa kijiweni wewe ndiye usiokosa chumvi watu wakihitaji chai.
DUH!
NAACHA!
Baadaye , kesho , kesho kutwa au siku nyingine Mwenyezi Mungu akipenda iwe hivyo!
Si inasemekana hata nikifa ni mapenzi ya MUNGU?
Nakasikiliza kawimbo haka , kaitwako- To the Ceiling kalikopigwa na ISAAC BLACKMAN. Anza nako WIKIENDI ukipenda.
-
NAKUPENDA!Si nilikupigia SIMU?
Posted: April 25, 2008, 9:37 pm by SIMON KITURURU
Ukimya unatafsiri nyingi.
Kirahisi tu , unaweza kutafsiri ukimya wa mtu kutokana na nini ulishaanza kumfikiria utakaye jibu kutoka kwake.
Unaweza mpaka kupata jibu kutoka kwa uliye jaribu kuwasiliana naye bila mafanikio, kuwa jamaa ananikwepa au ananidharau.
Wajanja husema ukiwasiliana na jamaa atakusikia au hata kukusoma.
Lakini....
...ukisikia au kusoma cha mtu, inawezekana hajawasilisha au ujumbe wake kuhusu jiko , wewe ukaelewa anazungumzia choo kichafu ambacho kina funza funza fulani WANONO.
Lakini....
...funza funza wanono watutiao kinyaa, kichefuchefu au hata hamu ya kutapika, wanaweza wakawa ni watoto wapendwa jichoni kwa mama yao NZI.
DUH!
Ningependa kuchukua nafasi hii kuomba msamaha kwa wote ambao nimeshindwa kuwasiliana nao.Najua ni watu kibao ambao wamekata tamaa nami kutokana na ka-ukimya fulani.- Samahani kama sijakupigia simu wala kupokea simu!
- Samahani sijakujibu ile barua, e-mail wala labda sikugeuka uliponipigia ule mluzi!
Lakini..
.. kabla sijaondoka kabisa kwenye topiki ya kuwasiliana fulani,
nimefurahi kufanikiwa kukutana uso kwa uso na blogger wa Kitanzania ambaye tulikuwa tunajuana mtandaoni bila kuwahi kuonana uso kwa uso a.k.a EDO NDAKI
Pata baadhi ya picha zangu nilizozidaka baada ya kukutana na EDO NDAKI , pamoja na WADAU wengine.
Kwa wasio jua , huyu ndiyo Mzee EDO NDAKI:
Hapa nilijibanza naye.
MKUU wa Kikao a.k.a RAYMOND alikuwepo.
Powered by filmloop.myfabrik.com
Tulia na HEAVY D akikuambia NUTTIN but LOVE
-
Kuna WATU wakoKimYa lakini wameona na kusikia! UKIWAPA upenyo ,WATAKUULIZA kama USHAWAHI kuugua Ugonjwa wa akili.
Posted: April 25, 2008, 9:24 pm by SIMON KITURURU
Kuna topiki fulani watu hukwepa kuongelea kutokana na topiki ilivyokaa kushoto.
Ukimpa mtu nafasi au kianzio cha sentensi kuhusu topiki asiyo kuwa na uhakika inakuathiri vipi ingawa akilini mwake anaona inauhusiano sana na jambo la kutia aibu , atakuuliza .
Ukimpa nafasi au kumchekea mara baada ya kumpa tabasamu wakati anahamu na wewe, anaweza kupata nguvu ya kukutongoza.
Cha ajabu ni kwamba , asicho kuuliza uso kwa uso anaweza kuwa kasha jadili na wadau wengine mara mia kadhaa na kufikia kwenye uhakika kuwa lile gari lako umelikopa.
Kuteta, umbea au hata kumuongelea mtu kama hayuko kijiweni, ni BOMBA la SANAA kwa atakaye urahisi wa kuhakikishia ubongo wake alichosikia kwenye redio za mbao ni kweli.
Umbea na kutetana ni dalili kwamba unamuda zaidi katika maisha yako ambao huutumii kujishughulikia au kufanikisha yanayo kuhusu wewe binafsi.
Umbeya , kuteta, uzushi au hata kutungia watu vistori visivyo vya ukweli ni bomba la kazi nzuri kama una hobi ya UMBEA.
Si unaona mpaka PEREZ HILTON kawa milionea kwa kuongea umbea na uzushi?
Si umeona Tanzania kuna magazeti mangapi yanayokiri ni ya UDAKU?
Watu hupenda kuwa na taarifa zako ambazo wanahisi hutaki zijulikane.
Swali:- Unahisi ni kwanini humuulizi , wakati unataka kujua kama kweli ana mke mdogo pale mtaa fulani au kama bado ana kaudhaifu ka-mapenzi yake ya watoto wa sekondari ya KIFUNGIRO, kama usikiavyo?
- Unafikiri ni kwa nini huulizi ingawa unataka kujua?
...Ukiuliza aliye ulizwa anaweza kuhisi unajua tayari ,kitu ambacho kinaweza kufanya aanze kukukwepa.
....Ukiuliza maana yake umekiri kuwa hujui.
....Ukiuliza inaweza ukawa umetoa mwaliko wa kutaka kudanganywa.
INAWEZEKANA hujauliza kwa sababu hujapewa nafasi, kianzio cha topiki au kuchekewa, USIKONDE!
Unakumbuka lakini jinsi gani mazingira, topiki iliyokuwa hewani ....vilivyochangia ujisikie huru kuulizia au kutongoza?
Unajua mara nyingi ni wewe , mimi au yule tutengenezao mazingira ya kurahisisha mpaka kutukanwa?
DUH!
Inawezekana nimeshakutengenezea mazingira ambayo utataka kuniulizia ambacho nitakwepa kujibu!:-(
Inaruhusiwa kutojibu ingawa kwa mimi kutojibu unaweza kuondoka ukifikiria ni kweli mimi bado bikira.
NAACHA basi!
Nakutakia kila la KHERI katika maisha haya ambayo yanasababisha tutake kujua mpaka visivyo tusaidia kama vile :hivi yule msichana kavaa chupi au kaptura chini ya lile gwaguro.
Tulia na Mu-Itali (ambaye usipomuona unaweza kufikiri mweusi) kwa jina la Alberto D'Ascola A.k.a. AlBorosie
Au pata ujumbe wewe kama MTU MWEUSI kutoka kwa MORGAN HERITAGE wakimkumbusha MTU mweusi hali halisi ya MTU MWEUSI,
katika songi, FALLIN RACE
Blah blah blah
Fish cakes
Alas a fish cake.
Yet more fish cakes
Guess what ... yeah ... fish cakes.
The end of the fish cakes