SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • SAMAHANI! Nawakimbia tena wadau wa BLOGU HII kidogo!:-(

    Posted: April 22, 2008, 3:34 pm by SIMON KITURURU
    Samahani wadau wa blogu hii!
    Nimebanwa kidogo, kwa hiyo , saundi haitoki stirio....

    Lakini nafikiri kuanzia Ijumaa hii , pilau inaweza kunukia tena hapa kijiweni kama kawaida.
    Au ngojea niseme.....


    SASAA endelea kidogo tu na Lagbaja ambaye ndio baada ya FELA Kuti, katika AFRO BEAT, ananisaidia katika SUKUMA TWENDE wiki hiii, angalau katika wimbo FEYIN E.......akisisitiza utabasamu au kucheka hata kama nanihii ngumu:-(




    DUH!
    Au unaweza kujifunza kucheka au kutabasamu kitu kutoka kwa mchekaji huyu...
  • NAMKUMBUKA MPENZI KINUKA MKOJO!

    Posted: April 22, 2008, 2:28 pm by SIMON KITURURU
    Hakuna kitu kamili duniani!:-(

    Inategemea na engo au kona umuangaliayo au umchunguliayo kipenzi , kama hutaki kugundua huwa anajamba kama wewe na kijambo kingine kinachembechembe.

    DUH!

    Kinuka mkojo hanuki mwili mzima.
    Kuna maeneo kinuka mkojo ananukia kitunguu swaumu.

    AU?

    Kwa mpenzi Salome!
    Nakuonyesha penzi kwa kukununulia mkorogo wakati sipendi wajichubuao.

    Kwa mpenzi Zubeda!
    Nakuonyesha penzi kwa kukununulia manukato, wakati napata ashki kwa mnuko wako wa kikwapa.

    Kwa mpenzi Tanzania nchi ya amani mpaka inafungwa katika MPIRA wa MIGUU na RWANDA na BURUNDI katika kipindi nchi hizo ziko vitani.
    Nakupenda kwa kama kawaida ya Watanzania, nazungumzia penzi la bila vitendo vya kuzuia wafisadi hata kama najua siri zao kwa sababu :SI TUNA AMANI?
    Kwa mpenzi Tanzania, nchi yenye Mlima Kilimanjaro , lakini watalii watakao kuuona mlima Kilimanjaro bado wanajisikia vizuri wakija kutokea Kenya na wakishuka mlimani, wanarudi Kenya kwa sababu wanauhakika zaidi ndani ya Kenya.

    Bado nakupenda kwa dhati ingawa najua sisi wengi Watanzania hatukiri kuwa Makaka na Madada zetu Wakenya, kunakitu wamefudhu au kwa sababu fulani fulani wanafanikiwa kitu ambacho tunaweza kujifunza kutoka kwao kiridhishao wageni a.k.a. watalii.

    Usitishike, kila mtu kuna kitu anaweza kujifunza kutoka kwa mwingine!
    Ujanja ni kukiri kuna kitu mwenzio anakijua zaidi yako.

    AU?

    Swali:
    • Kupenda ni nini?
    • Nikisema nakupenda unaridhika kwa sababu umesikia nimesema nakupenda?
    • Kwa mpendwa, je, nikuache kwa sababu wewe ni kinuka mkojo ingawa unanikojolesha?
    Kwa mpenzi fulani!
    Najua wengi hulalamika, kusema, na nahisi labda hata mimi hufanya hivyo ilikujisikia vizuri kwa sababu sitendi!:-(
    Mawazoni , sisi Watanzania nahisi tumelewa kusikia kuwa tuna amani kiasi kwamba kinuka mkojo nahisi hatukinusi.
    AU?

    DUH!
    Naacha wazo hili, nisije nikajifunga bure halafu ukapata cha kunidaka.
    Msikilize tu Mmoja wa wanamziki wa AFRO BEAT niwapendao KUBWA kuliko, Lagbaja akikupa kitu ROCK ME GENTLE

  • CHUPI, BAISKELI, BIRINGANYA, ......Majina ya sehemu ZA SIRI,Harage MOJA au PIA neno lisilo BISKUTI.

    Posted: April 22, 2008, 7:45 am by SIMON KITURURU
    Naheshimu neno!

    Toto la binadamu likizaliwa, baadhi ya maneno ya kwanza kujifunza ,ni neno baba au mama linatamkwaje.

    Jitu zima likishakua , baadhi ya maneno ya kwanza kujifunza katika lugha fulani mpya, ni matusi, kutukana au kama halina aibu kama mimi, litajifunza kwanza mpaka majina ya sehemu za siri kwa Kichina.

    Lakini....
    ....inasemekana kuna maneno, kubwa zima halitakiwi lisikike limesema kama linataka kuonekana lina busara au kama linataka kuheshimika.

    MANENO ni kitu cha ajabu sana!

    Unaweza ukajikuta umeyatumia kumwambia mtu kitu , ingawa unauhakika kumng'ong'a kungefikisha ujumbe!
    SI unajua maneno mengine jamii imeamua kuwa ni matusi?


    Lakini....
    ... ukitukana sehemu sehemu fulani , kuna ambao wataamini wewe ni mtoto wa mjini.

    Kuonekana mtoto wa mjini ni dawa ya kisaikolojia ya muda kwa mtoto wa mjini, kuhalalisha njia zozote za kufanikisha yale watoto wamjini wafikiriayo ni bomba na ni ujanja bila kuona aibu ingawa inaaibisha.

    Ufundi wako wa kutumia neno kutukana, ni moja ya kipimo cha jinsi gani unakumbuka maneno uliyojifunza ukubwani.

    Kama wewe ni kubwa zima kama mimi na unakumbuka matusi, basi akili yako inafanya kazi vizuri kukumbuka hata jinsi ya neno liwezalo kutumika kuomba msamaha au hata kuhakikisha lugha yako si chafu kama yangu katika uwasilishaji wako wa ujumbe .


    Najua kama wewe unatoka Afrika ya mashariki na lugha yako ni Kiyao , Kikwere au hata Kijita kama mimi, unajua kutukana kwa kingereza.......

    ......Lakini.....
    ... ushawahi kumtukana mtu kwa kumkonyeza?

    Tokea enzi za mababu, lugha inabadilika, na huzaliwa maneno mapya karibu katika lugha zote duniani karibu kila siku.

    Maneno na tafsiri ya maneno ni dalili ya jinsi ilivyokuwa vigumu kwa binadamu kutumia neno kufikisha ujumbe au kujaribu kufikisha kauli.

    DUH!
    Ningependa kutumia neno kufikisha ujumbe hapa leo!
    Lakini mbona hata nikitumia neno sieleweki?

    Ningependa kutumia neno kuelimisha hapa leo!
    Lakini mbona walioelimika bado hubakia na kutokuelimika kwa kibinadamu kama hatuoni elimu yao kutatua siri ya nini muhimu kwa binadamu?

    Swali:
    • Unakumbuka jinsi wanaojua au pia wanasiasa wetu ambao wengine tunawaita MUHESHIMIWA Raisi, watumiavyo neno kuwatusi wananchi kwa kuwaahidi neno ambalo hubakia kuwa ni neno tu bila vitendo?
    • Unakumbuka neno ulilotumia kudanganya kakitu ambako kamesababisha uwe na amani rohoni leo hii kutokana na watu kukaaamini kaneno na kuacha kufuatilia kwa vitendo unafanya nini?
    • Unakumbuka kuwa utamu wa neno, ni uwezo wake wakutumika kudanganya au kusema ukweli?
    • Uongo mwingine si huitwa fiksheni au porojo na huchukii ukisimuliwa?
    DUH!

    Naheshimu neno na maneno, lakini kumbuka vitendo inasemekana ndio huongea kwa sauti kubwa kama unataka kumpa mimba au kupewa mimba ambayo matunda yake , ndugu jamaa na maadui wataweza kupotezea muda kwa kunyoshea kidole.

    Vitendo vingine hata ukiviona , unaweza kujifanya hujaona ili usitamke neno.

    Hebu tumuangalie mbwa akifanya kitendo...(samahani kama utatafsiri kitendo cha mbwa huyu kwa neno matusi au PUNYETO!SAMAHANI lakini kwa FIKIRA zako POTOFU au NZURI!)

    DUH!

    Siku hizi inasemekana wajanja hutumia neno hata kwenye nyimbo, neno ambalo mwingine ataita ni matusi na kudhalilisha mtu au watu hasa wa jinsia fulani.

    SWALI:
    • Umestukia kila kizazi hutumia neno kusema kizazi kipya kimepotea kutokana na matumizi na tafsiri ya neno?
    • Umestukia ni miziki ya aina fulani tu ndio ina asilimia kubwa ya wasanii watumiao neno ambalo laweza kutafsiriwa kama tusi?
    • Kwanini?
    NAACHA BASI!

    NAWAZA TU USIKONDE!

    AU?

    Msikilize RAY J akikuimbia huuu wimbo ,(samahani ,hatumii lugha nzuri kwa watu fulani!Sishauri usikilize maneno katika wimbo kama wewe ukosensitivu na neno liwezalo kuwa tusi au wewe ni mtoto. Sikiliza kama kwa kawaida wewe si mfuatiliaji wa nyimbo zinasema nini.)...............
  • SIKO KWENYE MUDI YA KUONGELEA TOPIKI fulani.

    Posted: April 22, 2008, 6:29 am by SIMON KITURURU
    Unaweza kuongelea jambo kwa kutoongea.

    Lakini....
    ..... nahisi unajua kuwa kwa siku nzima , ni mambo mengi yapitayo kichwani ambayo binadamu wewe na mimi tunachagua kutoongelea au hali halisi inatukosesha bahati ya kumnong'oneza yule fulani.

    Lakini...
    ...binadamu achaguayo kuongelea au ajikutayo kaongelea , inaweza kuwa ni kwa sababu kuna kitu haongelei.

    Swali:
    • Unajua unaweza ukawa unanisoma na kuelewa nisichoongelea?
    • Hujawahi kutishika na kile kilichokupitia mawazoni ambacho hujawahi kukiongelea na hautakiongelea?
    DUH!

    Ambacho unakipenda na ungependa kumuuliza nanihii, wakati mwingine ni vigumu kukiomba kwa sababu hakiongelewi.

    Ambacho kwa kawaida hakiongelewi ,ukikiongelea, jamii na wewe mwenyewe hutumia kajicho fulani kukuangalia na kujiangalia kama tafsiri au jibu lake ni chachu au ni: umelizwa kibuyu na chumvi hupati.

    DUH, samahani kidogo!
    (``Unajua kama umefika mpaka mstari huu, inawezekana unaendelea kusoma nisichoongelea?´´)

    Tuendeleee....

    Labda...
    ...kile kitu ufikiriacho naongelea, unaweza kushindwa kuniuliza au kuuliza kwa sababu hakiongelewi!:-(

    DUH!

    Swali:
    • Unafikiri ni kwanini uliongea ulichoongea leo na kwanini kuna kakitu hujawahi kuongelea ingawa kanakupitia MUKICHWA?
    • Huongelei kipengele kwasababu hujawahi kutukana eeh?
    • Hivi wakati mwingine ukitukana ,huwa unatumia maneno uyatumiayo katika maongezi?



    SAMAHANI lakini kwa KUKUZINGUA kama umezinguka kiduchu kwa nisichoongelea , ambacho ungesikia , ungekibatiza kuwa si au ni kitu muhimu!

    HIVI kwa mwenye akili, inawezekana akagundua umuhimu wa kuongea ujinga?


    NAACHA basi!
    Tulia na BOB Marley akikukumbusha maswala ya maisha kama vile UGUMU wa KUBADILIKA ndani ya wimbo STIFF NECKED FOOLS

    Au turudi tu BONGO nakukutana na big 4 the GZ ft NgwearBIG 4 the GZ wakiwa na NGWAIR wakikusimulia maswala ambayo yako katika maisha na ambayo kwa watu fulani huweza kuita ni muhimu na ukashindwa kuwabishia kama vile maswala haya wayaimbayo ya PATI FULANI


Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs