SIMON KITURURU- MAWAZONI
-
NDOTO nzuri, INAWEZA kumchafulia SHUKA mvulana!
Posted: April 17, 2008, 6:40 pm by SIMON KITURURU
Nami hushiriki katika kushawishi watu waote vitu vikubwa na kuvifanyiakazi vitimie.
Lakini....
.....Ndoto zangu zote zingetimia, ningekuwa bilionea , halafu ningeshakufa miaka kadhaa kabla sijabalehe , kwa sababu ndoto nyingine huitwa majinamizi au kwa kiswahili kingine kigumu, huitwa NDOTO MBAYA:
Watu hutukania kulala, ingawa kwa mwaka inawezekana ukawa umetumia miezi sita kulala.
Waliozubaa katika kugombania ubwabwa wa maisha, huambiwa au kutukaniwa kuwa wana ubongo uliolala.
Kulala bomba, kama hupati majinamizi!
Ukilala vizuri , ni rahisi kufanikisha majambo kutokana na utulivu wa akili yako na uwezo wako wakukabili jambo baadaye kama utafanikiwa kuamka. Kulala , si kuna watu wanadai ni nusu ya kifo?
Lakini...
..... nahisi wengine tunalala vizuri au vibaya na kupitiliza kulala mpaka yale maamuzi mazuri tunachelewa kuanza kuyafanyiakazi .
Nafikiri wengine tunalala zaidi , ndio maana ndugu , jamaa na hausigeli wa nyumba ya jirani, wanajiuliza:- Mbona hatuoni jamaa afanyalo?
- Mbona hatuoni hata baiskeli ya swala au ile mashine ya kukoboa pale sehemu sehemu?
Lakini.....
Martin Luther King Jr alisimulia ndoto yake na pia alitabiri kuwa atafariki kabla ya kuona ndoto yake ikitimilika.
Lakini....
...... ndoto yake inatimilika!
Si unaona mpaka Barrack Obama anagombea Urais katika nchi ambayo watu weusi walikuwa wananunuliwa kama KIFUNGU cha EMBENG'ONG'O miaka michache iliyopita?
Nisikufiche sijui sana maswala ya kulala wala ya NDOTO!
Si unajua tena wakati nimelala huwa nakua nimelala, na sifanyii kauchunguzi spidi ya udenda utokavyo mdomoni wakati nimelala ni kilomita ngapi kwa saa kabla haujagonga mto.
Lakini nasikia......
...inasemekana, ukilala kikawaida, unatumia angalau masaa mawili kila siku kuota.
Kumbuka pia , inasemekana kuwa ukilala , kwa wanaume sehemu za uume huweza kusimama na wenyeuke kinukta huweza kuvimba kiaina pia!
DUH!
Nakiri kuacha kuongelea swala nisilolielewa vizuri!
Nacho jua tu ni kwamba!
Ndoto hutimia hata kama ndoto nyingine zitatimia dakika kadhaa tu baada ya mimi na wewe kufa, kufariki au hata kukata roho.
Kama sisi si wachoyo.....- Tutimize tu, zile ndoto za kupanda miti ambayo tunauhakika itachukua miaka mia kukua, lakini ikikua itakuwa msaada kwa kizazi kijacho.
- Tusisite tu ,kufanyia kazi zile ndoto za kupigania haki ya masikini kusikilizwa na serikali yao na matakwa yao kufanyiwa kazi mpaka umasikini uwe ni jina limaanishalo:umasikini ni ile hali ya mtu kujilimbikizia maswala asiyoyahitaji.
- Tusisite kujaribu kufanyia kazi ile ndoto binafsi ya kuwa na maisha uyatakayo binafsi hata kama ni vigumu kueleweka jichoni mwa ndugu , jamaa, jamii au hata mchumba.
Swali:- Unakumbuka uliota nini jana?
- Hivi masikini na matajiri huota ndoto tofauti?
- Wanawake na wanaume je?
Ni kweli si ndoto zote nazikumbuka kama nikumbukavyo msosi baadaye kidogo baada ya kuamka..
DUH!
Naacha!
Inawezekana naota tu!
Si unajua tena?
AU?
NAKUTAKIA kila la kheri katika kufanyia kazi ndoto zako!
SIKU NJEMA!
Tulia na WAZIRI wa UTAMADUNI wa BRAZIL , Gilberto GIL
akija na kibao Imagine
Au Mpate tu katika kibao Aquele Abraço
-
WANAWAKE huoga TOFAUTI kwa sababu wana MAtiti. AU?
Posted: April 17, 2008, 4:53 pm by SIMON KITURURU
Wanawake na wanaume ndio binadamu awaonao kila siku ya MUNGU ibadilikayo.
Binadamu anaweza akajisahau kuwa kuna maeneo yamuathiriyo binadamu mwenye uume na mwenye uke ambayo hayajabadilika sana kimawazo hata ki.....ndani ya asilimia kubwa ya idadi ya binadamu waishio katika duniani hii ibadilikayo.
NI RAHISI kusahau kuwa , bado katika dunia hii , haki za wanawake na watoto hazina kipaumbele sana machoni mwa wanaume na hata wanawake pia. Watoto sitawazungumzia sana hapa sana leo hii, ingawa naamini kuna wanawake ambao wamefikia kuamini kuwa wanaume wafikiriavyo na watakavyo, ndivyo watakiwavyo kufanya, kufanyiwa au hata kuonekana.
Wanaume wametawala maeneo mengi hapa duniani mpaka unaweza kusahau kwa nini bado ni watoto wakiume wanaopendelewa kielimu na kikuwezeshwa kujitegemea kuliko watoto wadada.
Watu husahau kuwa katika dunia hii, asilimia kubwa ya watu wako katika nchi masikini na asilimia kubwa ya watu bado wanaamini mafanikio katika watoto wa kiume na si katika watoto wa kike.
DONDOO:(Pamoja na wachina kusifiwa wana akili sana, NAFIKIRI unakumbuka wamefanikiwa kupendelea watoto wa kiume, na kuwa na watoto wa kiume mpaka wanaanza kuishiwa wanawake wa kuoa au kumimbisha hivi sasa.)
Sasaa......
Dunia inabadilika kila siku, na binadamu inabidi abadilike kukabiliana na mabadiliko kama anataka kuhakikisha kizazi chake kuendelea kuwepo hapa duniani.
Ushirikiano wa mwanakaka na mwanadada katika kufanikisha mridhiko wa maisha haya mafupi binadamu aishiyo, unahitajika sana, hasa kama nia ni kujaribu kuishi haya maisha kwa mafanikio na furaha.
Mafanikio ya binadamu hapa duniani , hutafsiriwa na mtu mwenyewe kutokana na jinsi alivyo athiriwa kimawazo na mambo mengi yamzungukayo tokea azaliwe , kuanzia aonje chuchu, apate au akose elimu , mpaka mara yake ya mwisho kupumua.
SAMAHANI KIDOGO........!
Swali:- Hivi maisha ya mafanikio ni lazima yawe ya furaha?
- Hivi kujua kutokanako na elimu hakusababishi kumkosesha tu raha binadamu ambaye asingejua , asingetaka?
- Unataka kujua una UKIMWI?
- Hivi unataka mto wa kike au wakiume ukimimbisha au ukimimbishwa leo usiku?
Cha ajabu ni KWAMBA, mafanikio ya binadamu JAMIII iyazungumziayo, ni mafanikio YATAFSIRIWAYO na jamiii kuwa NI MAFANIKIO .
JAMII itasifia na hata vitabu kuandika kuhusu yale JAMII itambuayo kuwa ni MAFANIKIO hata kama HAYO mafanikio huweza kuwa si MAFANIKIO kwa muhusika binafsi..
Swali:- Unafikiri maisha ya Rais NELSON MANDELA, ya kuachika mara mbili na watoto kukua bila baba, kwa mtazamo wa jamii ni mafanikio?
- Unafikiri maisha ya MANDELA ya kutaka haki kwa kila mtu bila kuipendelea familia yake binafsi, JAMII kwa ujumla inatambua kuwa ni MAFANIKIO?
DUH!
WAKATI UNAMCHUNGULIA BINADAMU AKIOGA, kuna maeneo unayatolea macho kutokana kuvutiwa kwako wewe binafsi au kwa sababu yalikaa tu karibu na tundu la mchungulio.
Nakiri kuwa lazima utagundua zile tofauti uzionazo mbele yako na labda wakati huo huo , hautakuwa unafikiria au kujali binadamu umchunguliaye anawaza nini tofauti na wewe zaidi ya kugundua nini alicho nacho kilicho tofauti na wewe.
Kwa wanawake na wavulana , karibu kila mtu anakakitu kake ukitokea tu ,kanamsitua kuwa huyu jamaa mvuto wake divisheni ziro: lakini kwanini wengine wanampasisha mtihani?
Kwa wanaume pale kijiweni, kuna atakaye kuambia kuwa yeye ni mtu wa matako, macho , miguu , nywele au hata yule ambaye atasifiwa kwa busara zake na jamii, kwa sababu anasema anapenda tabia ya yule ampendaye kuliko yale macho ya gololi na mashavu ya kumimina.
Nahisi kwa wanawake pia unaweza kusikia kuwa anampenda jamaa kwa sababu anabomba la matege, ana macho kama bundi au hata kwa sababu ana kifua kama simba: si umecheki siksi paki zile?
Swali:- Unafanya nini kusaidia kuleta usawa wa haki za wanawake na wanaume?
- Umejichubua kwa sababu unafikiri wanaume wanapenda au unakubali kuchunwa buzi kwa sababu wanawake kazi yao ni kupendeza na kukupikia chakula kabla ya kukupa kifuko cha dhambarau ukitoka kazini / kabla ya kulala?
DUH!- Naelewa mafanikio yako yanaweza yakawa ni kujinyima hapa duniani kwa sababu unafikiri utafaidi mbinguni ukishafariki.
- Naheshimu kuwa wewe mwanamke ndio kungwi na mama ambaye unampeleka binti yako kutairiwa kinjegere, ili jamii ikukubali na wewe mwenyewe ufikie kukubali kuwa UMEFANIKIWA, kwa sababu umefikia katika uzani wa MAFANIKIO katika jicho la JAMII na umefikia JAMII itakavyo.
- Nakubaliana na wewe pia kuwa umejichubua iliupendeze na unapendeza katika jicho lako na jicho la yule.
- Nakubali kuwa , ukiniona sichani nywele , unafikiria kuwa nywele zangu chafu lakini ukisuka twende kilioni na kukaanazo wiki kadhaa bila kuziosha, wewe bado msafi.
Nakubali kuna wanawake na wanaume , wasenge na wasagwaji pia!
Nakubali hakuna binadamu wawili sawa!
Lakini.....
HUFIKIRII kuwa mimi , wewe, yule na yeye ambao tukotofauti , tunaweza tukawa katika ahueni zaidi kama WANAWAKE watapata nafasi sawa na wanaume katika dunia hii ya leo ya sayansi na tekinolojia ambayo haihitaji sana misuli kama enzi za ujima?
Hufikirii kuwa , ni mimi na wewe ambao tunachangia kutokuwepo kwa usawa wa binadamu wote kutendewa ubinadamu sawasawa bila kujali ni wanawake au wanaume?
Inawezekana unavyowaza ni sawasawa tu!
Si kuna MALIPO MBINGUNI?
Inawezekana unavyowaza ni sawasawa tu!
Si mwanamume ni kichwa cha familia halafu ana misuli uenye nguvu zaidi ya mwenye uke?
Inawezekana unavyofikiria ni sawa!
Kwani ni nani anataka au kuhitaji dume jike katika shughuli?
AU?
USITISHIKE!
Nawaza tu kibulicheka!
Hebu tuangalie jinsi wanawake na wanaume waogavyotofauti , kama maji yakitoka pale DAR-es-SALAAM, MOROGORO au pale SAME, MBAGA , Manka, KILIMANJARO kwa bibi, kama kuna bafu fulani.....
DUH!
Ngojea tu ni waachie Elana na KC wa Read My Hips dance troupe ,wazungumze kwa kutumia mwili....
BAADAYE BASI!
Blah blah blah
Fish cakes
Alas a fish cake.
Yet more fish cakes
Guess what ... yeah ... fish cakes.
The end of the fish cakes