SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • USHAWAHI kumtazama KWA MAKINI binadamu akikimbiza MWENGE?

    Posted: April 13, 2008, 10:53 pm by SIMON KITURURU
    Binadamu hupenda kuoanisha kitu na jambo.
    Ndio maana binadamu anajioanisha mpaka yeye na jina lake.

    Labda ndio maana anaitika ukimuita lile jina!

    DUH!

    Kuna vitu kibao binadamu anavioanisha na kakitu fulani.
    Ukimchorea mistari miwili kinamna, atakuambia, huo ni msalaba, halafu atadai unamkumbusha Ukristo au hata YESU.

    Ukimchorea kinusu mduara na mbwembwe fulani , atakuambia umemkumbusha MWEZI au hata UISLAMU.

    Ukamuonyesha sanamu fulani, anaweza akakuambia huyo ni Rais Nyerere , yule rais bomba sana au hata akakuambia huyo ni BIKIRA Maria, ingawa anajua kuwa, hakuna aliyewahi kumchora au hata kumpiga picha Bikira Maria au yule mwanaye ajulikanaye kwa jina maarufu kama YESU, wakati wako hai .

    Sasaaa.....!
    Hivi vitu viwakilishavyo majambo muhimu kwa binadamu, labda ni vizuri sisi binadamu kuwa navyo na kuvishabikia.

    Labda vinaleta mwamko wa maendeleo, vinatusababisha tujisikie tuko karibu na Mwenyezi Mungu, tuko karibu kama binadamu na binadamu au hata kujitambua kuwa sisi kabila letu ni Wagogo.

    Sasaaaa........!

    Narudia swali:

    • Ushawahi kumtazama KWA MAKINI binadamu akimbizaye MWENGE?
    • Unafikiri binadamu wakati anakimbiza mwenge, akilini mwake anafikiria nini?
    • Ushajistukia unaweza ukapigwa butwaa ukiona Mdau anakojolea kaburi?
    Mtu na kielelezo chake , hataki mchezo!

    Naweza kumshangaa Muiraki alivyokuwa anapiga sanamu la Saddam Husein kama vile linasikia maumivu , wakati mimi mwenyewe nakubali, naweza kukasirika nikisikia jamaa wanakojolea sanamu ya Rais wetu mtukufu JAKAYA KIKWETE.

    Sasaa.....

    MWENGE wa OLIMPIKI , au hata ule MWENGE mwingine , twendeni tu tukaukimbize!

    Lakini......, wakati naukimbiza MWENGE, naruhusiwa kuwaza ;` sijui watatulipa kweli baada ya mbio hizi?´ au `Nasikia baadaye kuna bomba la ubwabwa kwa wakimbizao mwenge´, na si lazima niwaze kuwa ni kweli tunahitaji umoja katika DUNIA hii.

    Lakini....., wakati tunaukimbiza ule mwenge, tujiulize:

    • Tofauti ya mwenge na kibatari pale nyumbani kwa bibi ,ni nini?
    • Ushawahi kutupa,kuchoma au hata kuchambia gazeti lenye picha ya Mheshimiwa ,Mtukufu au Hata PAPA Mtakatifu?
    DUH!
    JUMAPILI NJEMA!
    Tulia na PM DAWN
  • Maswala ya ,`HUYU demu asingekuwa AMEOLEWA, ningemtongoza!´:-(

    Posted: April 13, 2008, 9:20 pm by SIMON KITURURU
    DONDOO:
    • Hapa siongelei swala lililo karibu na swala kama la Raisi Mandela kumuoa mke wa rafiki yake Samora , baada ya Rais huyo wa Mozambiki kufariki.
    Inawezekana kabisa ukinyimwa ,ukataka zaidi!
    Inawezekana kabisa unataka na kinakufikirisha kwa sababu huna!
    Vile viatu ambavyo ushavisahau chini ya kitanda, inawezekana mwenzako anavitamani leo hii katika duka fulani.

    DUH!

    Unaambiwa, MAJANI huonekana yakijani zaidi kwenye bustani ya mwenzio.
    Ulichonacho , inawezekana umekizoea mpaka hustukii ni jinsi gani kilivyo kikali.

    Ukionacho mtaani , na haswa kile ambacho hukijui, kina weza kikawa kinakuvutia sana tu.
    Ukweli ni kwamba ukitamanicho chaweza kukukinaisha hata kabla hujavuka dakika tano yakuwa nacho.

    Cha mwenzako ambacho unauhakika huwezi kukipata kinabakia kama kipimo cha yale ambayo akilini mwako umependa kuyakubali kuwa ndio ukweli ukizungukacho hicho kitu ulicho amua kukiita kitu kizuri.

    Naamini si kitu kibaya kutamani cha mwenzio kama kinakusababisha upige hatua fulani mbele , katika kujijua au hata katika kukufanya ujitume kufanya mambo vizuri zaidi ilikufikia mwenzako alipo.

    Tatizo ni pale tu kama tamaa ya yale usiyonayo yatakujenga chuki kwa yule ufikiriaye anacho kukuzidi.

    Swali:
    • Unauhakika ulichonacho si kizuri kuliko cha mwenzio ikiwa kinakutosheleza?



    DUH NAACHA na moja kwa moja natoka nje ya TOPIKI!

    Huu wimbo hapa chini ni kwa wale (hasa Marasta) wasionielewa nikisema mimi si Rasta , hasa kutokana na ukweli sichani Nywele (kama ionekanavyo pichani) , hata baada yakujieleza mara kedekede kwanini mimi si RASTA.


    Tulieni basi na hawa MARASTA wanaojulikana zaidi katika PUNK ROCK kutokea miaka ya sabini, ambao wale MARASTA waaminio kuwa urasta unaendana na ROOTS REGGAE pekee, wanakwazika hata kwa kuwasikiliza.Wapate basi BAD BRAINS

    DUH!
    Usitishike!
    Niko na ERIC BIBB (niliyenaye pichani) ....masikioni.

    Tulia naye basi!

    Kwa mara nyingine , ASANTENI MARAFIKI wote popote mlipo kwa yote!

    Nawatakia kila la heri katika harakati za kuishi!

    Asanteni pia marafiki ambao tumebahati kukutana hivi karibuni !

    Mungu akipenda tutakutana tena!
    Baadhi mnaweza kujistukia katika picha zangu hizi katika filmloop....
    Powered by filmloop.myfabrik.com
    Tuko pamoja na BAADAYE basi!

Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs