SIMON KITURURU- MAWAZONI
-
USHAWAHI kuiona au KUPIGA PICHA ya MUNGU?
Posted: April 11, 2008, 4:51 am by SIMON KITURURU
Swali:- Mungu wako wa upendo , anaweza kuwahurumia wale ambao kwa uwezo wao dhaifu wa kibinadamu wamefanikiwa kufa bila kumstukia au kumuelewa na kumfuata?
- Hivi Mungu wa mwenzio ni wa uongo eeh?
Ukiongelea maswala yahusuyo Mungu, kama unaimani fulani, utaamini kuwa Mungu haonekani.
Ukiongelea maswala ya Mungu, ni rahisi watu kuhisi unakufuru au unacheza mpakani na kupitiliza.
Lakini, ukimuongelea Mungu kinamna sikio la fulani linaamini kuwa ni Mungu atakiwavyo kuongelewa, huyo mtu fulani anaweza akawa mfuasi wako kama umenuia kuwania kuwa msikilizwaji katika maswala ya imani.
Binadamu karibu katika jamii zote duniani, huamini kuwa kuna kitu, vitu au........ ambayo ina/zina/..ana nguvu na uwezo kuliko binadamu yoyote yule.
Mara nyingi huyu/hiki/....huogopwa ,ingawa wengi huamini katika msaada wake kwa binadamu.
Swali:- Kwa nini hata yule Mungu wa upendo, anaogopwa?
Kuna werevu fulani ambao tunawasifia siku kibao kwa jinsi watumiavyo akili zao na kufanikisha mambo kibao ambao wanaweza kukufanya ushangae wakikuonyesha au kukusimulia kuhusu Mungu wao.
Nafikiri kwa kifupi unaweza kuwakumbuka Wamisri waliotuachia mpaka Mapiramidi jinsi walivyo kuwa wanamuabudu Farao wao kama yule Ramesses II
Nafikiri unaweza kukumbuka Wajapani wakati wanatawala Asia karibu yote , namaanisha mpaka China, walikuwa na Mungu Mfalme, kama vile huyu Emperor Shōwa aka Hirohito.
Au unaweza kumkumbuka yule mtoto aliyezaliwa juzi juzi India aka LALI ambaye anasura mbili asujudiwaye kama Mungu na watu ambao itakuwa vigumu kuwaita wajinga.
Hebu tujikumbushe baadhi ya Picha fulani ambazo zinaweza kukupa baadhi ya......:- Mtoto aitwaye Lali ambaye kashaanza kuabudiwa
Picha kwa hisani ya AP- Mungu Farao RamessesII
Picha kwa hisani ya Hajor- Yesu
Picha kwa hisani ya Google images- Mungu Jua
Picha kwa hisa ya Tinka Sloss- Mungu Mfalme Hirohito
Picha kwa hisani ya Google images- Hapa weka picha ya Msichana fulani aabudiwaye ( Unaweza kufuatilia hata mitaa ya Nepal kama humuabudu msichana fulani wewe)
- Hapa weka picha ya mvulana fulani....
Picha kwa hisani ya ULI SEIT
DUH Naacha basi hii topiki!
Unajua niko mawazoni tu lakini!
Usitishike wala kuchukia, fikiria tu!
AU?
IJUMAA NJEMA!
Samahani kwa ambao nimewakwaza au kuwapa vibes za kufuru!
Msisahau kuniombea kwa Mwenyezi MUNGU wenu!
Pata wimbo wa Injili kutoka kwa Bob Marley!
-
TANGAZO kwa WADAU walioko HELSINKI !
Posted: April 11, 2008, 4:50 am by SIMON KITURURU
UNAKARIBISHWA katika ile PATI YA WAAFRIKA yaKILA mwezi
ndani ya HELSINKI.
Tarehe: 12.4.08
Saa: 21:00 mpaka 04.00
Mahali:Ravintola Kaisaniemi
Anuani ya sehemusehemu: Kaisaniementie 6
Kiingilio: 5 Euro
Kutunziwa Jacket: 2 Euro
DJS: EDDO the MAN akiwa na ALIKO aka Altunes
Karibu Mmoja !Karibu Wote!
Kwa habari zaidi nenda: www.africannight.org
DUH!
Haka kawimbo kamtajako mende aka Kaka ROACH (Kakaroach in meh petty coat), kamenikaa kweli kichwani mwangu leo....
Naona nimemzidisha LORD KITCH !
DUH!
Usisahau kuwa pati hii mpaka Msondo Ngoma ni mbele kwa mbele.
Basi tulia na mwanadada nimzimiaye aka Lady Jaydee akikuambia USIUSEME MOYO
Blah blah blah
Fish cakes
Alas a fish cake.
Yet more fish cakes
Guess what ... yeah ... fish cakes.
The end of the fish cakes