SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • Fomu za tuzo za Vinara zatolewa!

    Posted: March 30, 2008, 9:35 pm by SIMON KITURURU
    Habari yako ndugu...
    Ifuatayo ni taarifa kwa vyombo vya habari. Tunategemea ushirikiano wako.
    Asante!


    Fomu za tuzo za Vinara zatolewa!

    Fomu za ushiriki katika kinyang'anyiro cha kuwania Tuzo za Vinara wa
    filamu Tanzania 2007/8 zimeanza rasmi kutolewa jana katika vituo
    mbalimbali nchini ikiwa ni hatua ya kwanza kabla ya kutolewa kwa tuzo
    hizo.
    Tuzo hizo zitakazotolewa kwa mara ya kwanza nchini, zimeandaliwa na
    kampuni ya One Game Promotions na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia
    Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya dovu Power Malt.
    Mratibu tuzo hizo, Khadija Khalili, amesema kuwa, kutokana na sababu
    zilizo nje ya uwezo wao, fomu hizo zilichelewa kutoka kwa tarehe ya
    awali hivyo kusababisha kuongezwa kwa muda wa kurejeshwa fomu na
    kupokea filamu zitakazoshiriki katika tuzo hizo hadi Aprili 18 badala
    ya Machi 31 kama ilivyotangazwa awali.
    Alisema watengenezaji wa filamu nchini wanakaribishwa kutuma nakala za
    filamu zilizotengenezwa kati ya Januari 2007 hadi Machi 31, 2008, kwa
    ajili ya kuwania tuzo hizo.
    Khalili alisema kuwa, jopo la majaji litakutana baada ya Aprili 18
    kuchagua watakaowania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2008.
    Alisema fomu za kushiriki kuwania tuzo hizo zinapatikana katika vituo
    vilivyotangazwa awali ambavyo ni ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa
    (BASATA) kwa Omari Mayanga, pia zinapatikana kwa wasambazaji wa filamu
    ambao ni Wananchi Wote, GMC, Kapico na Game First Quality.
    "Fomu zilizojazwa na nakala ya filamu iliyopo kwenye mfumo wa VCD na
    DVD zitumwe kwenye ofisi za BASATA zilizopo Ilala Bungoni jijini Dar
    es Salaam au ofisi ya One Game Promotion," alisema.
    Vipengele vitavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo kuwa ni Filamu
    Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa
    Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji
    Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Mwongozaji Sinema Bora wa Mwaka,
    Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu, Mtunzi Bora wa
    Filamu, Filamu Bora ya kutisha, Muigizaji Mwandamizii Bora wa kike
    (supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Bora
    kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa
    Filamu ambao wote watapata tuzo na zawadi. Pia itatolewa tuzo ya
    heshima kwa wale waliotoa machango wao kukuza sanaa nchini.

    DUH!
    Tulia na Mighty Sparrow... baada ya kupata ujumbve hapo juu....

    Endelea na COCOA TEA akizidi kukumbusha kuhusu .....BARACK OBAMA

  • ILE KITU NATAKA!

    Posted: March 30, 2008, 7:15 pm by SIMON KITURURU
    Binadamu tajiri......!
    Hapungukiwi ILE KITU NATAKA

    Umasikini humfanya mtu awe na busara katika
    uchaguzi wa ILE KITU NATAKA

    Matajiri wenye uhakika na dengu, malazi na...,
    utacheka uchaguzi wao wa ILE KITU NATAKA

    Ferarri kwao ni ILE KITU NATAKA,
    wakati Corolla ni aina ileile ya ILE KITU NATAKA

    Kabla ya kufa binadamu...,
    hupungukiwi ILE KITU NATAKA

    Kwa sababu......
    Ukweli ni kwamba unataka ILE KITU NATAKA.

    JUMAPILI NJEMA!
    Twende Kameruni kumalizia na msanii MANU DIBANGO

    Akikupa CADANCE


    Au endelea na MANU DIBANGO katika staili hiii, akiwa na LES LITTLES...
  • ZILE NYIMBO ZIIMBWAZO KATIKA LUGHA TUSIZOELEWA!Duh!

    Posted: March 30, 2008, 6:15 pm by SIMON KITURURU
    Starehe za miziki, mara nyingi ni jinsi ikusuuzavyo roho.

    Hebu mpate huyu dada akiimba wimbo kama asikiavyo....

    (Kama unaujua wimbo wa Mariah Carey, unajua naongelea nini!:-))


    Katika enzi zangu za kutembelea vilabu, gongo , mbege, konyagi, dodoma waini, na... nilistukia kuwa nyimbo za injili zinapigwa baa, chobisi na... hata kupita pale nyumbani kwa walokole au nyumbani kwa mchungaji.

    Maswala ya ndombolo ya solo, sukusu, kibinda nkoi au kibinda nanihii......nk., yalinigundulisha kuwa, naweza kucheza miziki nisiyoelewa inasema nini ,na demu wa nyumba ya jirani aniringiaye, nikampata kama bonasi.

    Lakini...
    .......kisa cha kumpata hausigeli wa nyumba ya jirani kilikuwa na utata!
    Katika kumpata Zubeda wa jirani, ilihitaji kuonyesha ujuzi wa kuondoka Ngwasuma dingiridingiri mpaka chini, nilikatika kisawasa, nilicheza sana, wengine waweza wakasema nilidansi sana, halafu mpaka yule wahusika wamuaminio kuwa ni muhimu ndani ya maeneo, akaja mezani kwangu, halafu akaonyesha kuzimia staili yangu .(Samahani kwa msio na .... au hata msio na uumee ,...au wale wasio na uke , njugu , peremende na....nahisi mnastori zenu za yule hausiboi, baba mkwe,mchaga wa kioski cha jirani, mpare fundi viatu au....yule aliyeng'ang'ania nanihiii na....)

    DUH!
    Lakini yule Mkongo, Mbongo, na.. aimbaye kwa lugha ya lingala,kikerewe na... au.... na.... atakuwa ni miongoni mwa watu ambao hata kabla sijafa nakumbuka kawimbo fulani ambako sikuelewa anasema nini. Lakini kalikuwa kawimbo kazuri.

    Yule bingwa maeneo , si lazima aelewe msanii katika fani anasema nini ndani ya utundu au hata maisha.
    KITU KIKUHUSUCHO , UTAELEWA KICHINA, kigagagigikoko kama embe dodo limekuchekea!

    DUH!

    Swali:
    • Ushawahi kuelewa mbwa anazungumza lugha gani wakati kakukenulia meno tayari kukuondolea ile siri uifichayo kuwa wewe muoga?

    Hebu msikilize kidogo PAPA SAN akilia, kabla sijaendelea kunong'ona.


    Nyimbo ni lugha!
    Wewe, mimi na yeye, tunajaribu mara nyingine kusikiliza MUHUBIRI , SHEKHE, BABA, HAUSI GELI , MLONDA, na... anasema nini.

    AU?

    Tupo wengi tutamaindi ukikosea tundu la choo cha shimo na kunya pembeni.

    AU?

    SAMAHANI!

    Nilitaka kusema tuko wengi tutachukia ukikosea sentensi au neno ndani ya lugha.

    Nisemavyo si usikiavyo!
    Naweza nikakuimbia mpaka juzi yake....
    Naweza kukutongoza mpaka nikalia.....

    Atanikililia nanihii!
    Unajua tabasamu naweza nisipate?

    USIKIACHO NDICHO ULICHOSIKIA.

    AU?

    Swali:
    • Hapa naandika maandishi, huhisi kama unasikia sauti yangu kuwa nasema nanihii kwa kutumia sauti?
    • AU?
    Naacha!
    Mpate Vanessa Paradis


    Swali:
    • Hivi wewe unaongea lugha gani?
    • Unaijua hiyo lugha eeh?
    DUH!
  • UKIMUOMBEA MTU KWA MWENYEZI MUNGU . UNAMUOMBEA NINI?

    Posted: March 30, 2008, 5:13 pm by SIMON KITURURU
    Samahani ! Sijaenda Kanisani!
    Samahani! Sijaenda msikitini!
    Samahani!Sijaenda kwenye sinagogi wala pale... na pale....

    DUH!

    Najua lakini maswala ya ijumaa , jumapili , juma kuminatatu, asubuhi ,jioni na...kama mtu wa imani, inaweza kumaanisha kitu fulani.

    AU?

    Duh!

    Nashukuru wewe umeenda msikitini, kanisani , kule wa Hindu , na...... , halafu ukakumbuka kuniombea.

    AU?

    Nami sijaenda na sikuenda maeneo ya kumuomba MWENYEZI MUWEZESHA YOTE, lakini nimekuombea na nakuombea.
    Nahisi katika vitabu fulani , ukisoma haraka haraka , unaweza kuamini mimi ni miongoni mwa wale watoto wapotevu.

    Swali:
    • Katika vitabu fulani ,si ni ukweli mwana mpotevu anastukia akipata kibano ,baaada ya muda fulani uitwao baadaye na kutubu?
    • Lakini wewe ambaye hujapotea, UJAPOATE?
    • Ushatubu dhambi zako?
    • Hivi ni dini gani zile zikuwezeshazo kutubu ukizidisha nanihino?
    • Au hauna dhambi?

    Nashukuru wewe umeenda maeneo ya kukutana au kukuruhusu kupiga magoti , kuinama na........................ katika kunyenyekea na kumtii Mwenyezi Mungu kiheshima, katika hali ya kusawazisha matatizo , dhambi zako na pia kutuombea sisi wenye dhambi.
    Swali:
    • Unauhakika ukipiga magoti , kuinama , kurukaruka, MWENYEZI MUNGU hatastukia kuwa kisiri, unatamani nanihiii......ngono na asiye wako, kilaji , kudokoa mboga jikoni , au kuiba mahindi ya kuchoma shamba la jirani?

    AU?

    Swali:
    • Weye ambaye una uhakika wa ...Unaweza kunipiga jiwe kwa sababu nimepotea?
    • Una uhakika?
    Staili ya kupotea, kwa jina jingine inaitwa UBINADAMU.
    Naamini kabisa, bila ya nguvu za Mwenyezi Mungu, Allah, Yahweh , Murungu na...., unaweza kutamani kakitu kaliko katazwa kinamna.

    Swali:
    • Ushawahi kutamani nanihino ambayo imekatazwa na baba?(Samahani!Nilimaanisha iliyokatazwa na DINI fulani uifuatayo iongeayo ukweli mtupu?)
    Staili ya kupotea, ni ubinadamu.

    Naacha!

    Swali:
    • Kwanini unahisi kwa imani yako wewe au yule , una.. au anaweza kuamini nimepotea kwa sababu nimesema nimepotea?
    • Umepotea?
    • Kwanini imaniyako inakuponza ulazimike kuamini kuwa ni ukweli?

    SAMAHANI ! NAJIULIZA TU!Usinitukane ukiwa chooni au pale sehemu ulipo.

    AU?

    Msikilize MUNISHI....



    Duh!
    Namsikiliza Marvin Gaye lakini vile vile!Msikilize basi.

    AU?

    BAADAYE BASI!

Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs