SIMON KITURURU- MAWAZONI

  • MaUmivu ya Utamu!

    Posted: March 20, 2008, 5:53 pm by SIMON KITURURU
    Hakuna mtu anayeishi bila kugundua hahakakitu kaitwako maumivu.
    Sisi binadamu ni wajanja sana kujaribu kutafuta jinsi ya kuishi bila maumivu.

    Lakini maumivu ni kakitu ambako utake usitake , katakudaka tu maeneo fulani kinamna.

    Kuna watu watakuambia kuwa :

    • Binadamu bila kusikia maumivu maisha yatakuwa magumu zaidi.
    • Wengine watakukumbusha ile dhambi Mungu aliyo wahukumu Adam na Eva kuwa watazaa , kula na ku........
    • Lakini wengine mpaka wanajikata mwili ili kusikia maumivu ya mwili katika kuondoa maumivu ya presha nyingine za maisha.

    DUH!

    Maisha magumu na cha mtema kuni tunakiona .
    Hebu msikilize huyu jamaa kiduchu....



    Lakini....
    Kumbuka kuwa maumivu yanakusaidia kujifunza, yanaokoa kujiumiza zaidi, yana kustua kuwa kuna maeneo umeumia.

    DUH!
    Hebu tujaribu kusahau maumivu kwa kumsikiliza Henry Salvador akiwa na Celin Dion



    Lakini...
    Kama una huzuni kumbuka uko karibu kuifaidi furaha.
    Kama huna maumivu kuna kakitu katakukumbusha ako kakitu kaitwako maumivu kinamna.

    Hebu niache kukuzingua.
    Endelea na MEthod Man akikuletea maumivu..

    BAADAYE BASI!

    ENDELEZA LIBENEKE!
    AU?
  • NANNI kasema kwa sababu KUNA wapenda amani VITA vitaKWISHA?

    Posted: March 20, 2008, 3:13 pm by SIMON KITURURU
    Ukisema unapenda amani, kuna maeneo unaonekana wewe bomba la mtu.
    Kupigana kunafananishwa na unyama fulani.


    Lakini......

    Kama wewe ni kati ya watu wanao amini vitabu fulani kama BIBLIA , vinukuuo watu tokea enzi za siku ya kwanza Mwenyezi Mungu alifanya nini, utastukia kuwa tokea katika familia ya Adam na Eva watu walianza kuleteana mbinde.


    Mpenda amani anaonekana bomba baada ya madhara ya kupigana yanapokuwa wazi.

    Swali:
    • Si unakumbuka utamu wa kupendana unajulikana vizuri kutokana na kujulikana kale kautamu ka chuki?

    Lakini.....

    Madhara ya vita, pamoja na kutaka kujaribu kuyaoanisha na watu kupata busara na jibu la swali la kwanini vita ni mbaya, binadamu kibao wamefanikiwa kuchukia zaidi na kuwa tayari zaidi kupigana baada ya vita kuliko kabla ya vita.

    DUH!

    Kama vita vingelikuwa vinamfundisha mwanadamu aache kupigana, nafikiri dunia ya leo hakungekuwa na hata eneo moja ambalo watu wanachukua hatua ya kupigana ilikusuluhisha jambo.

    Lakini...

    • Ukipigwa , unaweza ukakubali suluhisho na kukubali ya aliyekupiga.
    • Ukipigwa unaweza ukakubali lakini ukawa unasubiria kinafasi uchochoroni ulipe kisasi.
    • Ukipigwa kama binadamu, wanao kuhusudu wanaweza wakawa ndio watakaoumia nakutaka kulipiza kisasi hata kuliko wewe.
    • Ukipigwa , kuna watu watatafsiri kizazi chako chote kimepigwa, hivyo kusababisha hapo mbeleni kizazi chako kutaka kulipiza kisasi kwa kizazi kilichokupiga.

    Swali:
    • Ushawahi kupigwa?

    Mimi mpenda amani, lakini nimejua kuwa mimi ni mpenda amani kutokana na kujua wapendao vita.
    Samahani kwa kukukatisha tamaa mpenda amani mwenzangu, naamini, kama kutakuwa na binadamu hapa ulimwenguni kutakuwa na wapenda vita na wapendao amani.
    Kitakachobadilika ni jinsi wapiganavyo vita vyao , kisaikolojia, kimisuli na hata kimapenzi!


    DUH!
    NAACHA!

    Kwa waaminiyo naniihii!

    PASAKA NJEMA!

    Kwanilio kutananao hivi karibuni kama hawa niwawekao picha hapa chini vilevile......

    Pasaka Njema!

    Anza na kusikiliza wimbo wa amani wa Kenya....


    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket
    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket


    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket
    DUH!
    Pumzika kidogo na THe Streets



    Tuendelee....
    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    DUH!
    Ngojea tujaribu kucheka.....


    Photobucket
    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    Photobucket

    DUH!!
    Ngoja niache basi!

    KWA mara nyingine, PASAKA NJEMA ndugu na jamaa pale mahala fulani mlipo popote duniani!
    Mpate SAM MANGWANA

Blah blah blah

Fish cakes

Alas a fish cake.

Yet more fish cakes

Guess what ... yeah ... fish cakes.

The end of the fish cakes


Kenyan Blogs