SIMON KITURURU- MAWAZONI
-
Fomu za tuzo za Vinara zatolewa!
Posted: March 30, 2008, 9:35 pm by SIMON KITURURU
Habari yako ndugu...
Ifuatayo ni taarifa kwa vyombo vya habari. Tunategemea ushirikiano wako.
Asante!
Fomu za tuzo za Vinara zatolewa!
Fomu za ushiriki katika kinyang'anyiro cha kuwania Tuzo za Vinara wa
filamu Tanzania 2007/8 zimeanza rasmi kutolewa jana katika vituo
mbalimbali nchini ikiwa ni hatua ya kwanza kabla ya kutolewa kwa tuzo
hizo.
Tuzo hizo zitakazotolewa kwa mara ya kwanza nchini, zimeandaliwa na
kampuni ya One Game Promotions na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya dovu Power Malt.
Mratibu tuzo hizo, Khadija Khalili, amesema kuwa, kutokana na sababu
zilizo nje ya uwezo wao, fomu hizo zilichelewa kutoka kwa tarehe ya
awali hivyo kusababisha kuongezwa kwa muda wa kurejeshwa fomu na
kupokea filamu zitakazoshiriki katika tuzo hizo hadi Aprili 18 badala
ya Machi 31 kama ilivyotangazwa awali.
Alisema watengenezaji wa filamu nchini wanakaribishwa kutuma nakala za
filamu zilizotengenezwa kati ya Januari 2007 hadi Machi 31, 2008, kwa
ajili ya kuwania tuzo hizo.
Khalili alisema kuwa, jopo la majaji litakutana baada ya Aprili 18
kuchagua watakaowania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2008.
Alisema fomu za kushiriki kuwania tuzo hizo zinapatikana katika vituo
vilivyotangazwa awali ambavyo ni ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) kwa Omari Mayanga, pia zinapatikana kwa wasambazaji wa filamu
ambao ni Wananchi Wote, GMC, Kapico na Game First Quality.
"Fomu zilizojazwa na nakala ya filamu iliyopo kwenye mfumo wa VCD na
DVD zitumwe kwenye ofisi za BASATA zilizopo Ilala Bungoni jijini Dar
es Salaam au ofisi ya One Game Promotion," alisema.
Vipengele vitavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo kuwa ni Filamu
Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa
Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji
Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Mwongozaji Sinema Bora wa Mwaka,
Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu, Mtunzi Bora wa
Filamu, Filamu Bora ya kutisha, Muigizaji Mwandamizii Bora wa kike
(supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Bora
kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa
Filamu ambao wote watapata tuzo na zawadi. Pia itatolewa tuzo ya
heshima kwa wale waliotoa machango wao kukuza sanaa nchini.
DUH!
Tulia na Mighty Sparrow... baada ya kupata ujumbve hapo juu....
Endelea na COCOA TEA akizidi kukumbusha kuhusu .....BARACK OBAMA
-
ILE KITU NATAKA!
Posted: March 30, 2008, 7:15 pm by SIMON KITURURU
Binadamu tajiri......!
Hapungukiwi ILE KITU NATAKA
Umasikini humfanya mtu awe na busara katika
uchaguzi wa ILE KITU NATAKA
Matajiri wenye uhakika na dengu, malazi na...,
utacheka uchaguzi wao wa ILE KITU NATAKA
Ferarri kwao ni ILE KITU NATAKA,
wakati Corolla ni aina ileile ya ILE KITU NATAKA
Kabla ya kufa binadamu...,
hupungukiwi ILE KITU NATAKA
Kwa sababu......
Ukweli ni kwamba unataka ILE KITU NATAKA.
JUMAPILI NJEMA!
Twende Kameruni kumalizia na msanii MANU DIBANGO
Akikupa CADANCE
Au endelea na MANU DIBANGO katika staili hiii, akiwa na LES LITTLES...
-
ZILE NYIMBO ZIIMBWAZO KATIKA LUGHA TUSIZOELEWA!Duh!
Posted: March 30, 2008, 6:15 pm by SIMON KITURURU
Starehe za miziki, mara nyingi ni jinsi ikusuuzavyo roho.
Hebu mpate huyu dada akiimba wimbo kama asikiavyo....
(Kama unaujua wimbo wa Mariah Carey, unajua naongelea nini!:-))
Katika enzi zangu za kutembelea vilabu, gongo , mbege, konyagi, dodoma waini, na... nilistukia kuwa nyimbo za injili zinapigwa baa, chobisi na... hata kupita pale nyumbani kwa walokole au nyumbani kwa mchungaji.
Maswala ya ndombolo ya solo, sukusu, kibinda nkoi au kibinda nanihii......nk., yalinigundulisha kuwa, naweza kucheza miziki nisiyoelewa inasema nini ,na demu wa nyumba ya jirani aniringiaye, nikampata kama bonasi.
Lakini...
.......kisa cha kumpata hausigeli wa nyumba ya jirani kilikuwa na utata!
Katika kumpata Zubeda wa jirani, ilihitaji kuonyesha ujuzi wa kuondoka Ngwasuma dingiridingiri mpaka chini, nilikatika kisawasa, nilicheza sana, wengine waweza wakasema nilidansi sana, halafu mpaka yule wahusika wamuaminio kuwa ni muhimu ndani ya maeneo, akaja mezani kwangu, halafu akaonyesha kuzimia staili yangu .(Samahani kwa msio na .... au hata msio na uumee ,...au wale wasio na uke , njugu , peremende na....nahisi mnastori zenu za yule hausiboi, baba mkwe,mchaga wa kioski cha jirani, mpare fundi viatu au....yule aliyeng'ang'ania nanihiii na....)
DUH!
Lakini yule Mkongo, Mbongo, na.. aimbaye kwa lugha ya lingala,kikerewe na... au.... na.... atakuwa ni miongoni mwa watu ambao hata kabla sijafa nakumbuka kawimbo fulani ambako sikuelewa anasema nini. Lakini kalikuwa kawimbo kazuri.
Yule bingwa maeneo , si lazima aelewe msanii katika fani anasema nini ndani ya utundu au hata maisha.
KITU KIKUHUSUCHO , UTAELEWA KICHINA, kigagagigikoko kama embe dodo limekuchekea!
DUH!
Swali:- Ushawahi kuelewa mbwa anazungumza lugha gani wakati kakukenulia meno tayari kukuondolea ile siri uifichayo kuwa wewe muoga?
Hebu msikilize kidogo PAPA SAN akilia, kabla sijaendelea kunong'ona.
Nyimbo ni lugha!
Wewe, mimi na yeye, tunajaribu mara nyingine kusikiliza MUHUBIRI , SHEKHE, BABA, HAUSI GELI , MLONDA, na... anasema nini.
AU?
Tupo wengi tutamaindi ukikosea tundu la choo cha shimo na kunya pembeni.
AU?
SAMAHANI!
Nilitaka kusema tuko wengi tutachukia ukikosea sentensi au neno ndani ya lugha.
Nisemavyo si usikiavyo!
Naweza nikakuimbia mpaka juzi yake....
Naweza kukutongoza mpaka nikalia.....
Atanikililia nanihii!
Unajua tabasamu naweza nisipate?
USIKIACHO NDICHO ULICHOSIKIA.
AU?
Swali:- Hapa naandika maandishi, huhisi kama unasikia sauti yangu kuwa nasema nanihii kwa kutumia sauti?
- AU?
Mpate Vanessa Paradis
Swali:- Hivi wewe unaongea lugha gani?
- Unaijua hiyo lugha eeh?
-
UKIMUOMBEA MTU KWA MWENYEZI MUNGU . UNAMUOMBEA NINI?
Posted: March 30, 2008, 5:13 pm by SIMON KITURURU
Samahani ! Sijaenda Kanisani!
Samahani! Sijaenda msikitini!
Samahani!Sijaenda kwenye sinagogi wala pale... na pale....
DUH!
Najua lakini maswala ya ijumaa , jumapili , juma kuminatatu, asubuhi ,jioni na...kama mtu wa imani, inaweza kumaanisha kitu fulani.
AU?
Duh!
Nashukuru wewe umeenda msikitini, kanisani , kule wa Hindu , na...... , halafu ukakumbuka kuniombea.
AU?
Nami sijaenda na sikuenda maeneo ya kumuomba MWENYEZI MUWEZESHA YOTE, lakini nimekuombea na nakuombea.
Nahisi katika vitabu fulani , ukisoma haraka haraka , unaweza kuamini mimi ni miongoni mwa wale watoto wapotevu.
Swali:- Katika vitabu fulani ,si ni ukweli mwana mpotevu anastukia akipata kibano ,baaada ya muda fulani uitwao baadaye na kutubu?
- Lakini wewe ambaye hujapotea, UJAPOATE?
- Ushatubu dhambi zako?
- Hivi ni dini gani zile zikuwezeshazo kutubu ukizidisha nanihino?
- Au hauna dhambi?
Nashukuru wewe umeenda maeneo ya kukutana au kukuruhusu kupiga magoti , kuinama na........................ katika kunyenyekea na kumtii Mwenyezi Mungu kiheshima, katika hali ya kusawazisha matatizo , dhambi zako na pia kutuombea sisi wenye dhambi.
Swali:- Unauhakika ukipiga magoti , kuinama , kurukaruka, MWENYEZI MUNGU hatastukia kuwa kisiri, unatamani nanihiii......ngono na asiye wako, kilaji , kudokoa mboga jikoni , au kuiba mahindi ya kuchoma shamba la jirani?
AU?
Swali:- Weye ambaye una uhakika wa ...Unaweza kunipiga jiwe kwa sababu nimepotea?
- Una uhakika?
Naamini kabisa, bila ya nguvu za Mwenyezi Mungu, Allah, Yahweh , Murungu na...., unaweza kutamani kakitu kaliko katazwa kinamna.
Swali:- Ushawahi kutamani nanihino ambayo imekatazwa na baba?(Samahani!Nilimaanisha iliyokatazwa na DINI fulani uifuatayo iongeayo ukweli mtupu?)
Naacha!
Swali:- Kwanini unahisi kwa imani yako wewe au yule , una.. au anaweza kuamini nimepotea kwa sababu nimesema nimepotea?
- Umepotea?
- Kwanini imaniyako inakuponza ulazimike kuamini kuwa ni ukweli?
SAMAHANI ! NAJIULIZA TU!Usinitukane ukiwa chooni au pale sehemu ulipo.
AU?
Msikilize MUNISHI....
Duh!
Namsikiliza Marvin Gaye lakini vile vile!Msikilize basi.
AU?
BAADAYE BASI! -
Nani Hapendi kuwa BWANA MKUBWA kama Robert Mugabe?
Posted: March 28, 2008, 11:44 am by SIMON KITURURU
Sikatai ukweli kuwa wapo binadamu ambao hawapendi kuwa mabwana mkubwa kinamna!
Lakini...
...ukifuatilia vitu fulani, utastukia kuwa asilimia kubwa ya binadamu wote wakiwa katika ulaji , ni vigumu kuwatoa mezani.
Ubwana mkubwa una ulaji wake.
Ubwana mkubwa hauko tu katika vitu au taito za ofisi zilizo waziwazi.
Mtu anaweza akakutawala kisaikolojia , ukatawalika bila hata kujua ukurupuke vipi.
Mabwana mkubwa wako kisaikolojia pia hawataki kuachia kiti hicho.
Swali:- Ushawahi kusikia Mwalimu wako , hata baada ya wewe kumzidi madarasa akakataa kiti cha ukweli kwamba ni mwalimu wako?
- Ushawahi kumstukia aliyekufundisha ukafaulu , awezavyo kutumia kisa hicho kutengeneza ubwana mkubwa sehemu nyingine ? Namaana ,hujawahi kusikia jamaa akisema kitu kama ;`` nilimfundisha Nyerere mimi! ´´, kwa sababu Nyerere baabu kubwa?
UKIFIKIRIA SANA, HAKUNA ALIYEWAHI KUWA KATIKA ULAJI AKAUACHIA KIRAHISI .
Katika Ubwana Mkubwa naamini :- Mwalimu Nyerere alifikia kiwango ambacho hakuhitaji awe ofisini ili awe Bwana Mkubwa,bado alikuwa Bwana Mkubwa. Angenyanyua simu wewe kama Rais ungejibu na kusema; ndio Mzee!
- Bill Clinton bado anauhusudu ubwana mkubwa na ndio moja ya motisha yake ya kufanya kila njia Mrs Clinton awe ofisini.
- Putin wa Russia , kuachia Uraisi na kuchukua Uwaziri Mkuu ni dalili hizo hizo za kutotaka kuondoka jikoni.
- Fidel Castro , kumuachia mdogo wake Urais na kuwa mshauri Mkuu wa serikali, ni dalili za kutotaka kucheza mbali.
- Wanasiasa Tanzania ambao tokea tuzaliwe mpaka leo hii ni waheshimiwa wabunge, ambao wameacha kulala bungeni kutokana na televisheni............ni katika swala hilohilo la ugumu wa kuachia kakitu ulikozoea.
Naweza kuendelea milele........
Lakini watu wanasahau kuwa...........
....Ubwana mkubwa unakuweka katika sehemu ambayo mahitaji yako husikilizwa kirahisi.
Kisaikolojia, ubwana mkubwa unaleta utiifu kwa walengwa iwe kwa nguvu za mabavu au vinginevyo.- Mtoto anaweza akasababisha utii amri zake za kununuliwa pipi kwa kuililia hadharani na wewe ukatii amri.
- Kama unapenda michezo ya ubaba na mama chumbani, unaweza ukajikuta unatii amri ya kununua ile zawadi ambayo ulikuwa unafikiria ni kupoteza fedha , ili usinuniwe chumbani.
Nachojaribu kusema ni:
Robert Mugabe na miaka yake themanini na ushe, hataki kuachia Urais na baadhi ya watu wanashangaa sana, lakini si kitu cha kushangaza.Wengi wangependa kufanya kama yeye kama mazingira yange ruhusu.
Jamaa kanogewa!
Lakini pia....
.... tusisahau kuwa kuna watu kama hawa akina Robert Mugabe ambao wanaonekana wabovu, wakiachia maeneo, yanakuwa kama Iraki. (Siumecheki jinsi hata upinzani ulivyogawanyika Zimbabwe?)
Unakumbuka mambo yakumtoa Saddam Hussein katika uongozi Iraki kwasababu alikuwa mtu mbaya anaye ua watu wengi, yamesababisha watu wazuri walioingia kurekebisha nchi, kutengeneza mazingira ambayo yanaua watu wengi kwa siku kuliko hata mtu mbaya Saddam Hussein . (Lakini nafikiri unajua kisa cha kumtoa Saddam hakikua kwasababu muuaji.)
Sasa nachojaribu tena kusema ni;
Asilimia kubwa ya watu wakiustukia Ubwana Mkubwa katika anga yoyote ya maisha ,ni vigumu kuiachia.- Mtoto akijua akilialia anapewa atakacho, hawezi kuacha kulialia.
- Mwanadada akigundua akikunyima nanihii inakusababisha usikilize matakwa yake ya kumuachia akacheze mdundiko, atakunyima nanihii.
- Dume zima likistukia likinuna lifikapo nyumbani haliulizwi kwanini limechelewa kurudi nyumbani, litanuna halafu na maji ya kuoga litachemshiwa.
Wakati unangalia wikiendi hii Robert Mugabe anavyogombania ubwana Mkubwa, kumbuka kuwa inawezekana hata mimi na wewe kila siku tunagombania kubakia na ubwana mkubwa kinamna , ubwana mkubwa ambao kama unatimiza angalau kupata nanihii, hatutaki kuuachia kirahisi.
Swali:- Ushawahi kuona mzee anakubali kirahisi kuwa kaishiwa nguvu na anahitaji msaada wako kumpeleka chooni na kumchamba?
Hebu twende SENEGAL kidogo kuwasikiliza hawa jamaa DAARA J wakikupa kibao ALLAH
Au endeleza tena na DAARA J live
Baadaye! -
Bikira Wawili Usiku wa Ndoa.
Posted: March 28, 2008, 4:06 am by SIMON KITURURU
Usiku huu wa ndoa.....,
wote tuko butu.
Tufurahi kuanza ndoa.
Maswali ni mengi .
Nashindwa kukohoa.
Matarajio ya umati....
Kuna kitu tutaondoa.
Sijui tuzime taa , kabla hatuja chojoa?
Kama kipofu...,
.....amwongozaye kipofu,
dunia msitu.
Nani atatuokoa?
Tunajua tuna kucha zihitajizo kunoa.
Nani wakumuuliza jinsi ya kunoa?
Na...
....tusipojiuliza nani twa mkomoa?
--------------------------------------
Najaribu kuongelea jinsi dunia inavyobadilika haraka sasa hivi, na ukweli kwamba hakuna ajuaye kwa uhakika jinsi ya kukabili mambo kibao, kisiasa(wengine wanasema siasa ya China bado ni mbaya wakati inakuza uchumi) na , kiuchumi(angalia Marekani kila mtu anavyo ongelea ni njia gani ya kujikwamua), kimaisha, kidini(wengine watakuambia Uislamu bomba na bado wengine watakuambia mambo yote ni Usayantoloji),nk.
Kila mtu anavutia kwake,kwa sababu na uwezo wake wa ubongo wa kibinadamu.
AU?
DUH!
Tulia na Aaron Neville akikuambia TELL IT LIKE IT IS.
Pilipili ni kali, je tuzidi kuinunua?
Baadaye Basi! -
KIJIWENI NA ADUI AKUCHEKEAYE!
Posted: March 27, 2008, 5:27 pm by SIMON KITURURU
Naweza kusema adui mzuri ni yule akuonyeshaye kuwa anakuchukia.
Kujua bomba la kitu!
Binadamu ni mjanja halafu hana uhakika, jambo ambalo hufanya wanadamu wengine wakuchekee ingawa moyoni mwao wanakujambia kinywani.
Lakini.....
...binadamu anaweza akawa anauhakika na nini anataka akufanyie cha kukudhuru lakini akakuchekea kwanza kabla haujakaa golini akulenge.
Swali:- Sasa akikuonyesha chuki halafu akajikuta anahitaji msaada wako hapo baadaye afanyeje?
- Sasa akikuonyesha makucha yake ya uadui, akiwa na kiu utampa maji?
.... matatizo ya adui akuchekeaye kama huna machale fulani, ndiye awezaye kukuumiza zaidi kunako. Akuchekeaye waweza ukajikuta ndiye awezaye kufikia ile sehemu yako ya siri ya maumivu.
Mapenzi yako alinacha na adui akuchekeaye utastukia machungu yake pale anapokuweka konani baada yakustukia umenasa.
Chuki itakayojitokeza baada ya wewe kunasa kutoka kwa adui akuchekeye, inaweza kusababisha ukumbuke sura ya mnuno wa adui uliyejua anakuchukia siku zote kama ilikuwa inakitabasamu fulani vile.
Swali:- Ushamchekea adui leo?
Maadui ndio wafanyao tuwathamini marafiki.
``Maadui ni muhimu sana´´; inaweza ikawa ni sentensi iletayo maana katika anga fulani.
DUH!
Unawakumbuka baadhi ya maadui hawa ambao inasadikika kuwa wanatudhuru Africa, Amerika, Ulaya , Asia na pote duniani?
Nina maanisha ya maadui hawa hapa:- Ujinga
- Magonjwa
- nk
Lakini......
.... Chekewa na Mchekee!
.....Jifanye hujui au Jifanye umesahau!
Kumbuka tu kuwa katika lolote ufanyalo;
KUJUA UNAFANYA NINI NI BOMBA LA KITU, hata kama ujuacho ni busara ya kuwa hujui.
Ngoja YingYang Twins wakunong'oneze(samahani kwa lugha na wadada nusu uchi katika kideo) .
-
NANI KAKUAMBIA KILA MTU ANAKWENDA BAA KWA FURAHA?
Posted: March 27, 2008, 3:16 pm by SIMON KITURURU
Asili ya uelewaji wako kitu, unaweza kujengwa na uzoefu ua ukosefu wa uzoefu wako katika jambo .
Tatizo liwakumbalo binadamu wawili tofauti katika uelewaji wa jambo moja, ni jinsi binadamu hawa wawili wanavyoweza kuwa wamejengeka tofauti kutokana na makuzi tofauti , mazingira tofauti au kutokana na ukweli kuwa hawa binadamu wawili ni tofauti.
Swali:- Ushawahi kuelewa ni kwanini binadamu wengine wengi(hasa wazungu), wanaongea na mbwa au paka wao kama wanaongea na mtu?
- Unakumbuka wenye majonzi na wenye furaha unaweza kuwakuta msikitini au kanisani wakipata na kuwakilisha mahitaji yao ya kidini tofauti kwa pamoja mbele ya Mwenyezi Mungu?
Maeneo, utawasikia watu kibao ambao wamejipa UTAALAMU WA KWANINI.
Taaluma hii ya kujipa ndio huamua mambo kibao kuhusu kwanini watu wengine wanaonekana au wanafanya hiki na kile.- Ni rahisi kufikiri kila uonacho kuhusu mtu fulani ni lazima ukielewe.
- Ni rahisi kufikiri kuwa umekielewa uonacho.
Ngojea ni kupe kastori:
---------Hadithi! Hadithi!-----------
Hapo zamani za kale , wakati bado niko mdogo, mitaa ya Songea, nilikuwa nakatazwa kucheza mpira na unifomu za shule kutokana na udongo mwekundu wa Songea na sababu nyingine kadhaa. Nilikuwa nakatazwa kupitiliza saa kumi na mbili jioni michezoni hasa kutokana na wazazi kutaka kuhakikisha najisomea na kumalizia zile Home Work.
Niliyekuwa namuogopa sana kushikwa naye nikivunja sheria alikuwa ni Baba yangu. Kwa bahati mbaya ilikuwa inatokea mara kwa mara anayenidaka nacheza mpira au nimepitiliza muda ambao natakiwa kuwa nyumbani alikuwa Baba.
Mdingi alichokuwa anafanya kilikuwa kinawashangaza marafiki zangu! Alikuwa anaweza kuja kujiunga katika kushangilia au analeta stori na marafiki zangu na hata pipi anaweza akatununulia.
Kitu ambacho marafiki zangu walikuwa hawajui ni jinsi mimi jasho linavyonitoka, kwa maana pamoja na Mdingi kucheka nasi, ninlikuwa najua ni kibano gani nitapata pale tu nitakapofika nyumbani. Kwa sababu ilikuwa napata kibano cha kuotea mbali.
Lakini....
...Kesho yake nikikutana na marafiki zangu , hawakawii kusifia jinsi gani nilivyokuwa na Baba poa, kutokana na wao kutojua jinsi gani nilipata kibano pale nilipofika nyumbani baada ya kuachana nao.
-------Mwisho wa Hadithi-------
Dhumuni ya hadithi hii ni kutaka kumkumbusha jamaa huyu na yule kuwa , unaweza ukawaunaona kisehemu tu cha sura nzima ya kitu kama utakuwa unajenga hoja kutokana na kumuona mwanadada yule kavaa kimini na yuko uchochoroni. Anaweza akawa kakimbia kibano ndani kwao na hayuko uchochoroni kuuza nanihiii.
Swali:- Unafikiri mtu akiwa na ze bia au ze gongo mbele yake , maana yake anafurahia maisha?
- Ushawahi kujisikia vizuri baada ya kulia?
- Ushawahi kulia kwa furaha?
Kuna watu wanafuraha nyumbani.
Lakini kuna watu wako mbali na furaha za nyumbani.
Kuna watu nyumbani ni sehemu ya kujilaza tayari kwa maumivu ya kesho.
SIKU NJEMA!
Pumzika na..Basement Jaxx wakikuambia DO YOUR THING
- Ushawahi kuelewa ni kwanini binadamu wengine wengi(hasa wazungu), wanaongea na mbwa au paka wao kama wanaongea na mtu?
-
USHAWAHI KUIANGALIA MAITI YA MBU?
Posted: March 25, 2008, 10:17 am by SIMON KITURURU
Mbu hulalamikiwa wote!
Lakini si mbu wote wahitajio damu yako.
Staili za kumuua mbu ziko kibao.
Unaweza ukambinya.
AU?
Mbu aliyeuawa , maiti yake haiangaliwi sana.
Mara kwa mara baada ya kumuuambu, unasahau kuwa umeua, labda mpaka upate malaria ndio unajaribu kukumbuka baadhi ya maiti fulani za matunda.
SWALI:- Unanielewa?
Usitishike!
ENDELEZA LIBENEKE!
Mpate lakini NASIBU MWANUKUZI aka RAS NAS akiwa na Ali Jabang na Aliou Cissokho wakiwa na MANDINGO TRIO
-
Ngojea Niseme!DUH!
Posted: March 24, 2008, 2:39 pm by SIMON KITURURU
Ngojea nikupe dondoo za yaliyonikuta..
DUH!
Kuna watu wananigombania kuhusu post zangu hapa katika blogu yangu kama vile nimewalazimisha wajekunichungulia hapa kinamna!:-(
Wanadai hawaelewi nasema nini.
DUH!
Malizia kidogo Pasaka na Manu DIBANGO akikupa kitu WOA!
-
UTAMU WA WALI na KUKU ULIOKULA JANA!
Posted: March 23, 2008, 5:18 pm by SIMON KITURURU
Leo ni leo!
Ubwabwa uliokula jana hausaidii sana kukidhi mahitaji ya leo ya mlo kama una njaa ya hata kiporo cha mlenda.
Sikukatalii kuwa jana ule wali uliokula ulikuwa mtamu kweli kama huo wali uliula.
Lakini....
... kama leo tumbo halipati kitu unafikiri nikikusimulia utamu wa wali jana unamsaada sana katika kutatua swala la leo?
Swali:- Umestukia hadithi za UTAMU wa pilau jana inavyonoga, kama wakati unasimuliwa leo bado umeshiba na unauhakika wa mlo?
- Ushastukia hadithi zako za utamu wa wali uliokula jana inaweza zikawa ni adhabu masikioni mwangu kama na njaa na sina pakula leo?
DUH!
Nisikutishe!- Napenda stori za jana.
- Nafurahia unapomsifia Nyerere , Kenyatta hata Iddi Amini kwa waliyofanya jana.
- Napenda hata ukumbushiavyo jinsi hali ya hewa ilivyokuwa nzuri jana.
- Napenda hadithi za wanadada na wanakaka walivyokuwa waaminifu katika mahusiano ya walioishi jana.
- Usiseme kwa jinsi navyopenda hasa ugusiapo jinsi miziki ya jana ilivyo kuwa bomba.
- Napenda mpaka zile nakadhalika kadhaa, zilizokuwa bomba jana.
Sasaaaaaaaaaa........!
Swali:- Mimi wa leo , utamu wa wali uliokula jana unanihusu nini?
DUH!
Utamu wa jana unaweza kuwa motisha ya kuongezea kautamu juu ya utamu leo.
Utamu wa wali jana unaweza ukageuka kuwa utamu wa wali leo na kachumbari na glasi ya gongo au mbege juu yake leo.
Lakini hadithi za utamu wa wali uliokula jana waweza ukawa ni ukatili dhidi ya masikio yangu leo mwenye njaa.
NASIKILIZA LAKINI!
ENDELEA KUNIPA HADITHI ZA UTAMU WA UGALI WA MUHOGO ULIOKULA JANA.
Endeleza siku kwa kusikiliza ushahiri wa Rafael Casal
akitukumbusha utamu wa mapenzi ya jana.
Au turudi tu katika ZOUK na kuendelea na Jocelyne Beroad wa Kassav
-
Maswala ya Kujinyea!
Posted: March 23, 2008, 3:52 pm by SIMON KITURURU
Nirahisi kunyoshea mtu mwingine au kitu kingine kidole kwa swala ulilojifanyia mwenyewe.
Lakini pia, mjanja ni lazima ajue kuwa hata kama unamnyoshea mtu au kitu kingine kidole kwa jambo lizaliwalo kutokana na kalkulesheni zako za kudaka kutolipa, ni lazima ukiri icho kitu hata kimoyo moyo kama unataka kujifunza au kutatua.
Lakini.....!
Maswala mengi yatutiayo matatizoni ni maswala ambayo yanaweza kumtokea binadamu yeyote.
Tatizo ni kwamba sisi binadamu tumekuwa watumwa wa mitazamo ya jamii ifanyayo tuwe waoga kufanya chochote ambacho katika jicho la jamii kinatufanya tuonekane hatuna mpango.
Tatizo kubwa zaidi ni kwamba, tukishaanguka katika mtazamo wa jicho la jamii , wengi wetu tunaamua kuzoea mazingira ya pale tulipoangukia.Jambo hili linatufanya tusiweze kujinasua katika makucha ya pale tulipoangukia.Hukawii kujikuta unaamua kuendelea tu kunywa gongo kama ushazoea na unajua jamii inakuita mlevi wa gongo, hata kama mbege ndio kinywaji ulichopenda kunywa hapo enzi za kale.
Kuhusu maswala ya kujinyea......
DUH!
Kwenda haja kubwa kuna starehe zake!(Samahani , nilikuwa namaaninsha kujinyea.)
Kuna watu husahau kuwa moja ya jambo ulifanyalo mapema baada ya kuzaliwa ni kujinyea.
Lakini....
... hili ni jambo ambalo jamii itaendelea kukufunza tokea uanze kuelewa mambo mpaka utakapo zeeka kuwa, ni noma kujinyea.
Kwa bahati mbaya ni kwamba, jamii haiachi mpaka ufe kukukumbusha kuwa kujinyea ni jambo la kukutia aibu na ni jambo la kuwanyea wale wakuhusuo.
Swali:- Hivi unakumbuka ma astronauti waondokapo kwenda anga za juu na waingiapo tena duniani huvaa nepi ili kuwaruhusu wajinyee kistaarabu?
Nadhani unamkumbuka huyu Lisa Novak na alivyodakwa akiwa na nepi yake katika harakati za kumfukuzia mpenzi wa mpenzi wake?
DUH!
Hili swala la kunyewa pia......!
Mara nyingi watu hawataki ujinyee ili kuogopa wao wenyewe kunyewa kiaina na myo wako.
Mambo ufanyayo yanaweza kumdhuru mtu mwingine akuhusuyo bila wewe kunuia kufanya hivyo.
Kwa mfano ; kama wewe unafuatilia uchaguzi wa Uraisi Marekani , utakuwa umeshuhudia jinsi gani akina Obama, Clinton na.... inabidi wajitete sana kutunza uhalali wao katika uchaguzi kwa makosa ya watu wengine wawahusuo.
Unaweza ukajikuta unadanganya kuwa wewe ni nani kutokana tu na kukwepa kuunganishwa na mnyo wa mtu , vitu , hata...... ambavyo jamii inafikiri vimejinyea.
Sasaaa!
Unajua tena mimi na wewe si malaika na tuko katika jamii hii ambayo haiachi kutukumbusha tusijinyee.
SWALI:- Unakumbuka mimi na wewe ndio jamii?
- Wewe ni mnyosheaji vidole eeh?
Basi ngojea na mimi nijaribu kukumbusha kitu ambacho najua kwa njia moja au nyingine ni ngumu kufanikiwa;
USIJINYEE!
Jumapili Njema!
Nakuacha na Sheryl Crow
akikupa kibao LOVE is FREE
-
You are filling up kenyaunlimited with useless posts.
Posted: March 21, 2008, 9:29 am by SIMON KITURURU
DUH!
I tried to get U guys to delete me from that webring.
I am in the mood to do and write... Well, the same useless things.
DUH!
Nilijaribu lakini kutowasumbua!
Ngojea nimuache Culture
Kenyaunlimited watu, kama hamkunielewa its ok. Lakini kusema kuwa nilikuwa na fill up kenyaunlimited with useless posts, NAAMINI HAMUELEWI NASEMA NINI katika post zangu. Naamini naweza nikawa nawalipisha kitu fulani lakini , HAMUWEZI KUSEMA POST ZANGU USELESS!
Naendeleza kujaza hapa nachoandika kama kawaida na naweka picha za wadau wangu niliowadaka kinamna kama kawa .... Na sibadili staili hii NG'OO , Just incase mnaolalamika mnaelewa naongelea nini katika post zangu, kitu ambacho sina uhakika kama mnanielewa.
BASI MBELE KWA MBELE!
AU?
DUH!









DUH!
Pumzika na FELA KUTI






























Kwa wanaonielewa , endelea na Buju Banton















TULIA na GOKH-BI SYSTEM
-
MaUmivu ya Utamu!
Posted: March 20, 2008, 5:53 pm by SIMON KITURURU
Hakuna mtu anayeishi bila kugundua hahakakitu kaitwako maumivu.
Sisi binadamu ni wajanja sana kujaribu kutafuta jinsi ya kuishi bila maumivu.
Lakini maumivu ni kakitu ambako utake usitake , katakudaka tu maeneo fulani kinamna.
Kuna watu watakuambia kuwa :- Binadamu bila kusikia maumivu maisha yatakuwa magumu zaidi.
- Wengine watakukumbusha ile dhambi Mungu aliyo wahukumu Adam na Eva kuwa watazaa , kula na ku........
- Lakini wengine mpaka wanajikata mwili ili kusikia maumivu ya mwili katika kuondoa maumivu ya presha nyingine za maisha.
DUH!
Maisha magumu na cha mtema kuni tunakiona .
Hebu msikilize huyu jamaa kiduchu....
Lakini....
Kumbuka kuwa maumivu yanakusaidia kujifunza, yanaokoa kujiumiza zaidi, yana kustua kuwa kuna maeneo umeumia.
DUH!
Hebu tujaribu kusahau maumivu kwa kumsikiliza Henry Salvador akiwa na Celin Dion
Lakini...
Kama una huzuni kumbuka uko karibu kuifaidi furaha.
Kama huna maumivu kuna kakitu katakukumbusha ako kakitu kaitwako maumivu kinamna.
Hebu niache kukuzingua.
Endelea na MEthod Man akikuletea maumivu..
BAADAYE BASI!
ENDELEZA LIBENEKE!
AU? -
NANNI kasema kwa sababu KUNA wapenda amani VITA vitaKWISHA?
Posted: March 20, 2008, 3:13 pm by SIMON KITURURU
Ukisema unapenda amani, kuna maeneo unaonekana wewe bomba la mtu.
Kupigana kunafananishwa na unyama fulani.
Lakini......
Kama wewe ni kati ya watu wanao amini vitabu fulani kama BIBLIA , vinukuuo watu tokea enzi za siku ya kwanza Mwenyezi Mungu alifanya nini, utastukia kuwa tokea katika familia ya Adam na Eva watu walianza kuleteana mbinde.
Mpenda amani anaonekana bomba baada ya madhara ya kupigana yanapokuwa wazi.
Swali:- Si unakumbuka utamu wa kupendana unajulikana vizuri kutokana na kujulikana kale kautamu ka chuki?
Lakini.....
Madhara ya vita, pamoja na kutaka kujaribu kuyaoanisha na watu kupata busara na jibu la swali la kwanini vita ni mbaya, binadamu kibao wamefanikiwa kuchukia zaidi na kuwa tayari zaidi kupigana baada ya vita kuliko kabla ya vita.
DUH!
Kama vita vingelikuwa vinamfundisha mwanadamu aache kupigana, nafikiri dunia ya leo hakungekuwa na hata eneo moja ambalo watu wanachukua hatua ya kupigana ilikusuluhisha jambo.
Lakini...- Ukipigwa , unaweza ukakubali suluhisho na kukubali ya aliyekupiga.
- Ukipigwa unaweza ukakubali lakini ukawa unasubiria kinafasi uchochoroni ulipe kisasi.
- Ukipigwa kama binadamu, wanao kuhusudu wanaweza wakawa ndio watakaoumia nakutaka kulipiza kisasi hata kuliko wewe.
- Ukipigwa , kuna watu watatafsiri kizazi chako chote kimepigwa, hivyo kusababisha hapo mbeleni kizazi chako kutaka kulipiza kisasi kwa kizazi kilichokupiga.
Swali:- Ushawahi kupigwa?
Mimi mpenda amani, lakini nimejua kuwa mimi ni mpenda amani kutokana na kujua wapendao vita.
Samahani kwa kukukatisha tamaa mpenda amani mwenzangu, naamini, kama kutakuwa na binadamu hapa ulimwenguni kutakuwa na wapenda vita na wapendao amani.
Kitakachobadilika ni jinsi wapiganavyo vita vyao , kisaikolojia, kimisuli na hata kimapenzi!
DUH!
NAACHA!
Kwa waaminiyo naniihii!
PASAKA NJEMA!
Kwanilio kutananao hivi karibuni kama hawa niwawekao picha hapa chini vilevile......
Pasaka Njema!
Anza na kusikiliza wimbo wa amani wa Kenya....

























DUH!
Pumzika kidogo na THe Streets
Tuendelee....





DUH!
Ngojea tujaribu kucheka.....









DUH!!
Ngoja niache basi!
KWA mara nyingine, PASAKA NJEMA ndugu na jamaa pale mahala fulani mlipo popote duniani!
Mpate SAM MANGWANA
-
KUHUSU VITU/TABASAMU/........ na nanihii FEKI!
Posted: March 14, 2008, 12:15 pm by SIMON KITURURU
NI KAUJUMBE tu Kadogo ka kukuanzishia WIKIENDI.
AU?
Sasaaa.......
Ukisikia kuwa asilimia themanini ya madawa ya tiba ndani ya Nigeria ni feki, unaweza ukafikiri kuwa Tanzania labda kuna unafuu kiasilimia fulani za ufeki wa madawa na tiba na.........
Vitu feki viko kila kona, kuanzia kule chooni , kanisani mpaka msikitini.
Siku hizi ukitaka mpaka FERRARI waweza kuipata feki.
Hebu cheki hapa
Soko la mapenzi feki,.....
Samahani, nilikuwa namaanisha soko la vitu feki, lipo sana kwa sababu wapendao na walazimikao kujaribu vitu feki wako bwelele.
Swali:- Ushawahi kunogewa na kitu feki hata kama kitu orijino unauwezo wakuki nanihii?
Vitu feki vinamadhara yake!
Unaweza kufa kiaina kwa matumizi ya vitu feki.
Jiadhari basi wikiendi hii na watu feki!Samahani!Namaanisha jiadhari na vitu feki!
AU?
IJUMAA na WIKIENDI NJEMA!
TUKO PAMOJA!
Endeleza na Yvonne Chaka Chaka
akija na MAMALAND
-
KATIKA kupigania penzi, KAKA aliyempa mimba DADA yake, ameshindwa KESI.DUH!
Posted: March 14, 2008, 6:44 am by SIMON KITURURU
Mapenzi mengine jamani, mie na ujanja wangu wote siyaelewi.
Swali:- Jinsi binadamu walivyo wengi, hivi kuna ulazima wa kaka kuzaa na dada yake au dada kuona katika wanaume wote, kaka yake mzazi ndio dume la mbegu?
Hii story ya huyu Mjerumani aliyemzalisha dada yake watoto wanne nilishaiandika mwaka jana.
Jamaa alifungwa kutokana na kuzaa na dada yake na akawa anapigania iruhusiwe kisheria kuwa ukimzimia nduguyo tumbo moja , mruhusiwe kuoana au kuzaa kisheria.
DUH!
Jikumbushe ile stori basi....
Jamaa kashindwa kesi, hivyo, anarudishwa jela tena.Ila jamaa kapenda kubwa kuliko. Anataka kupeleka kesi yake katika mahakama ya umoja wa ulaya ili wamsaidie aruhusiwe kuendeleza penzi na dada yake.
DUH!
Naacha basi!
Endeleza kufikiria mapenzi kwa kusikiliza ushahiri uitwao THIS TYPE LOVE wa Shihan
BAADAYE BASI! -
FASHENI ZA MAKABURI!
Posted: March 13, 2008, 8:43 am by SIMON KITURURU
Kuongelea kifo ni mwiko kwa watu lukuki.
Kuongelea makaburi kwa wengine ni swala la nuksi.
Kupita makaburini , kwa wengine ni kwa mwendo wa kama umebanwa uharisho.
Sasaaaa....
DUH!
Nahisi umestukia nafikiria sana mambo ya kifo!
Samahani!
Lakini tuendeleee........
Swala la kuchagua uzikwe wapi limenikuna kidogo tena baada ya kukutana na namba zisemazo:- Asilimia 50 ya Waingereza wanataka wachomwe na majivu kutupwa maeneo baada ya kufa.
- Asili mia 40 ya Wamarekani (USA) wanataka wachomwe na majivu kutupwa vilevile.
Lakini....
Kilichonizingua zaidi ni huu mradi wa PIRAMIDI MPYA , ambao na wewe unaweza kushiriki kujiandaa kuzikwa kwenye PIRAMIDI lililoko katika hatua za kuanza kujengwa.
Kama unataka kuzikwa kwenye piramidi hili, BBC inaripoti kuwa bei ya jiwe ni EURO 700 kwa bei ya sasa.
DUH!
Sasaaa......
Swali:- Hivi makaburi umuhimu wake haswa ni nini?
Naamini kuna wengi ambao hutembelea makaburi ili kuendelea kuungana na wapendwa waliotutoka .
Wengi hutembelea makaburi ilikujiliwaza, kutoa heshima na hata kuendeleza uhusiano na wapendwa waliotutoka.
Kwa kweli kuna sababu nyingi sana zilizomfanya binadamu fulani aamue kuwe na kaburi likumbukwalo .
Lakini......
Kuna mtu kaniambia kuwa, kutokana na technolijia, watu wana video, picha na njia nyingi tu juu ya kumbukumbu walizonazo mukichwa ambazo zinaondoa umuhimu wa mtu kuwa na kaburi.
Swali:- Je kumbukumbu mukichwa ya waliotutangulia +video+picha=hatuitaji kuzika tena?
- Unaogopa kufa eeh?
- Unakumbuka enzi fulani za kale , ilikuwa mtu akifa wanamkimbia na kuhamia pengine?
- Unafikiriaje kuhusu huu mradi unaohasisiwa Ujerumani wa Piramidi ambao utachukua mtu milioni baadaya kufa?
SAMAHANI!
HABARI ZA KIFO SI ZA UTANI!
DUH!
MUNGU awapumzishe na kuwapa raha wale wote waliotutangulia mahali pema peponi!
Ngoja nikutoe katika habari hii ya makaburi kwa kukusikilizisha huyu mwana mama kutoka MALI aitwaye Oumou Sangare
SIKU NJEMA! -
Kama YESU na MTUME wakuwa na MAADUI, KAWAWA je?
Posted: March 13, 2008, 8:07 am by SIMON KITURURU
Uhuru wa kusema /kutoa maoni/kujieleza, unamazingaombwe yake.
Ukiruhusu watu wakuambie wanakufikiriaje, watakuambia mpaka yale mambo ambayo yanakutekenya sikio.
Hukawii kusikia:- Mimi nalichukia tu lile jamaa.
- Mdau kwa kupenda misifa , hata mbwa hawamfikii.
- Mtoto mzuri huyo!Ukimbishia , atakwambia kwa sababu wewe hujamuona ziro distansi.
- Jamaa kwa kupenda ubwabwa huyo!
Swali:- Kama mtembeleaji blogu nyingi, umeshastukia hata habari nzuri kuna mtu atakuja na kuitukania?
Kweli binadamu tofauti!
Mwingine matatizo ni kitu kimpacho nguvu kutatua na kwenda mbele wakati kwa mwingine ni kitu kimdhoofishacho na kumfanya asikie kufakufa.
Kweli binadamu tofauti!
Yule umpendaye , kwa mwingine ni adui kutokana na yaleyale yaliyokufanya umpende.
Mpaka dini kadhaa hazikawii kukufunza uwapende kila mtu, lakini zinakukumbusha jinsi gani wasiofuata dini yako walivyo watu nishai.
Zinakufunza umpende aliye kama wewe, na yule mwingine asiye kama wewe, unashauri ujaribu kumfanya awe kama wewe kabla hujampenda kinamna.
DUH!
Sijui kama watu kibao wamefanikiwa kuwapenda wote walioko ndani ya dini moja.
Swali:- Ushawahi kumchukia mtu bila sababu na kukiri unamchukia tu?
- Ushawahi kujikuta kuwa yule uliye kuwa unahisi ni rafiki kumbe ndio adui?
DUH!
Inasemekana kuwa, hii hali ya kujaribu kueneza upendo duniani ni alinacha fulani kutokana na necha ya binadamu.
Inasemekana binadamu watachukiana ili wajue kupenda ni nini.
Swali:- Bila chuki , upendo ni nini?
- Bila maadui, marafiki ni akina nani?
Lakini....
Mimi naamini katika upendo.
Na kaudhaifu kakupendapenda kirahisi.
MAADUI eeh!Si mnajua tunaweza kupendana kama kale kakitu kasababishako tuchukiane kakiwekwa pembeni!
Samahani lakini kwa niliowakosea!
AU?
Naacha basi kukuzingua!
SIKU NJEMA!
Tulia na Brian Mcknight
-
UJANJA WAKUHAKIKISHIA UMATI KUWA HUTAKI UJINGA.
Posted: March 12, 2008, 11:45 am by SIMON KITURURU
Kama mkubwa, ni vigumu kuruhusu umma ushuhudie kuwa mjinga au kunakaujinga unakafurahia kisiri.
Usipokuwa muangalifu, unaweza ukajistukia unakemea kwa sauti au kukiri kwa sauti kuwa hutaki ujinga.
Balaa ya ubinadamu ni jinsi tulivyo binadamu na sio malaika.
Ubinadamu unakuja na viujinga vyake ambavyo umma unaweza pia ukavishangilia kama ni vitu vya maana.
Ukichunguza unaweza kustukia kuna baadhi ya ambao umma unawasifia kuwa hawataki ujinga, ambao ndio vyanzo vya vita, ufisadi, umasikini, na taaluma nyingi muhimu duniani kama utafiti wakufundisha nyani ajuae kusoma.
Swali:- Hivi ujinga ni nini?
- Ushawahi kuchekelea kaujinga wakati unajua ni ujinga?
- Hivi katika TV zetu/Magazeti/vitabu na... vilivyotapakaa na tuangaliavyo au kusoma, asilimia ya ujinga ni ngapi?
DUH!
Lakini ukweli ni kwamba , ujinga nishai!
Tujaribu kuukwepa ikiwa, unauhakika kuwa tunauwezo wa kuukwepa.
Swali:- Hivi kuondokana na ujinga ni lazima uende shule?
Naacha basi!
Siku njema!
Lakini tulia na BILLY PAUL akija na kile kibao cha utamu wa penzi na mke wa mtu,kiitwacho MIMI na Mke wa Bwana JONES
-
KATIKA KUJISIKIA KUFAKUFA.
Posted: March 11, 2008, 7:15 am by SIMON KITURURU
Kuna wajanja wanatumia kila njia kukwepa kufa.
Au inawezekana ikawa ni ujanja kukwepa kufa pale iwezekanapo.
Lakiniiiii.......
......Kufa , kwa mwingine ni kitendo cha kuogopa, wakati kwa mwingine ni kipunguzio cha shida za kuwa hai.
Swali:- Kwa wale wanaojiua na wenzao kwa kisingizio cha dini , ukiwakamata kabla hawajalipua bomu, uwape adhabu gani?
Maisha matamu , maisha machungu kama unaishi.
Mara nyingi ujanja wa kufikiria na kufanikisha uwe hai ndio ukufanyao ukumbuke kuwa kuna kifo.
MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA PEPONI WALE WOTE WALIOTUTANGULIA!
Swali:- Hivi kwanini kwa kiswahili watu tunawaombea waliotutangulia walale huko mahali pema peponi hata kama tunajua baadhi yao wangependa peponi yao iwe baa na sio sehemu ya kulazwa?
Siku njema!
Tuliza siku na Koffi akiwa na Papa
-
KUHUSU MATUMIZI YA KIKOJOLEO!
Posted: March 10, 2008, 3:11 pm by SIMON KITURURU
Matumizi ya kitu fulani , yako mengi ingawa vitu fulani vinapewa jina kutokana na kitu fulani , kitu ambacho kinaweza kuondoa umuhimu wa matumizi fulani ya sehemu fulani.
SWALI:- Unakumbuka matumizi mengine ya takataka yanaweza kupewa jina mbolea, na kwa mmea mbolea ni pilau?
Kitu kiletao umuhimu wa shughuli iitwayo haja ndogo, ni haja kubwa ya uhitaji wako wakwenda haja ndogo katika wasaa nyeti usababisha haja ndogo kuwa ni kitu kikubwa maishani mwako katika dakika zile ambazo umebanwa.
Kama unakiu , unahitaji maji na sio pilau ingawa mbele yako kuna ubwabwa.
DUH!
Ukishiba, pilau/Ugali wa muhogo/nanihiii......,nanihii haina kautamu fulani ambako ingekuwa una njaa udenda ungekutoka.
Staili ya kula ni kula.
Na kuna mtu kadhaa wanaweza kuniambia kuwa matumizi makubwa ya mdomo ni kula.
Swali:- Ushawahi kutumia mdomo kutema mate?
Utamu wa ubwabwa msibani na ule ubwabwa uliojipikia , kisaikolojia unaweza kuwa na tofauti.
Lakini matumizi ya ubwabwa na kiporo cha makande ndani ya mwili hakuna tofauti kubwa sana.
AU?
DUH!
Hebu msikilize kidogo Bill Withers atukumbushe wanaume jinsi yakukubali nanihiii fulani zihusianazo na maamuzi ya wanawake.
DUH!
Tatizo la kula, halisaidii kutumia kikojoleo.
Tatizo la ubongo , halisaidiii kuwa na busara au kuwa na kitu binadamu fulani wamekiita akili.
Swali:- Hivi unaakili?
- Hivi asiyekuwa na akili ni nani?
- Matumizi ya akili yako yameshawahi kukusaidi kukosa furaha?
Naacha basi!
Jumatatu njema!
Tumia lakini kitufulani kinamna.Unajua tena matumizi ya kitu fulani muhimu kinamna kama kitu fulani unacho. Usipotumia si maana yake kitakosa makali kile kitu ikiwa ni ubongo au sindimba.
AU?
Nakuacha na Onyx
BAADAYE BASI! -
UKISHANYIMWA!
Posted: March 9, 2008, 12:18 pm by SIMON KITURURU
- Ukinyimwa, hakuna ujanja zaidi ya kujaribu kutaka kuelewa na kukubali kuwa umenyimwa.
Ukinyimwa maana yake ulitaka.
Kama hutaki, ukinyimwa ni vigumu kukumbuka kuwa ulinyimwa.
Kama unataka , unaweza kukumbuka kona fulani ulipo nyimiwa.
DUH!
Swali:- Unakumbuka kuwa ushawahi kunyimwa?
Cheki kidogo picha kadhaa fulani, za baadhi ya wadau niliowadaka kinamna sehemu sehemu fulani.
DUH!

Ronaldo aka Mzee wa London eehe!
Easy E eeh!Usinitenge lakini

T.I , sasa nini mchezo huu ulionza wa kunitenga?
WAX eeh! Sasa tutafanyaje?Hatukuchagua hii kitu:-)






Raymond aka MKUU wa KIKAO, Kikao kigumu unajua usipotokea!Ilikuwa Ze GUDI lakini. AU?



Lakiniiii........
Utundu wa kujua jinsi ya kujifanya hujanyimwa wakati umenyimwa, kila mtu anao.
Lakiniiii...........
..... wengine kiboko katika ujuzi wakujua hata maswala ya kutaka na kunyimwa.
DUH!
Endelea na Snoop Dogg kidogo wimbo uleule ambao sijivuniiii.(Samahani lakini!:-()
Swali :- Ushastukia watakao na wenye nguvu ya kuto ogopa kunyimwa, ndio wajaribuo , na ndio wapatao zaidi nanihii fulani?
DUH!
Endeleza Jumapili na I-Wayne
-
STAREHE YA KUFUMANIWA!
Posted: March 8, 2008, 12:26 pm by SIMON KITURURU
- Kufumaniwa nishai!
Lakini ukifumaniwa, bonge la pumziko.
Unautua ule mzigo wa kale kasiri fulani.
AU?
Kuwa na siri nishai!
Siri bomba la mzigo.
Si unajua tena kale kamzigo ka kujaribu kufichaaaaaaaaaaaaaa!
DUH!
Kuficha bomba la kazi !
Hasa kama huendani na kale ufichako.
Siri yako ikigundulika bomba la noma!
Unaweza kugungulika unachamba kwa maji, kufukuzwa kazi, kuachika, au hata kunyimwa mishikaki pale kona fulani.
DUH!
Lakini.....
Siri bomba la kitu.
Swali:- Ushastukia ukifanya kijambo kisiri kuna kautamu fulani kanazidi kunoga?
- Ushastukia kastarehe kakajambo kakisiri hupungua ukisharuhusiwa kufanya kale kalikokuwa ni siri wazi wazi?
DUH!- Ushastukia una siri?
DUH!
Msikilize kidogo Baba yake Cuba Gooding Jr, akiwa na band ya The Main Ingredient .Namaanisha, Cuba Gooding Sr akija na Everybody plays The fool.
Naacha!
Pata baadhi ya Picha.....:
















Jumamosi Njema!
Au ngojea niseme basi:
Duh!
Endeleza Weekend na Safari Sound Band wakija na CHAKACHA
-
NAOGOPA KUONJA NANIHII!Ikiwa CHUNGU je?
Posted: March 7, 2008, 2:23 pm by SIMON KITURURU
Kuonja kitu fulani , hukufunza utamu au uchungu wa nanihii!
Ukionja kama ni tamu , kuna utamu wake.
Ukionja ukaungua, kunafundisho lake ingawa uchungu utauona .
Swali:- Hivi ni lazima uonje ili kuwa na uhakika wa utamu wa dagaa wa kigoma?
Duh!
Utamu wa ushabiki wa kitu fulani , hata kama ni mpira wa miguuu, unazidi pale mnaposhinda.Mkishindwa au ladha isipolenga utamu , kasheshe.
Kwa rafiki zangu wamshabikiao Mzee Obama , wiki hii , Hillary Clinton aliposhinda, hata taarifa za habari walikuwa wanakwepa ladha yake.
Kuhusu matokeo ya uchaguzi wa kidemokrasia hapo Kenya, kuna ambao walianza hata kuhisi kuwa labda kweli Afrika tumelaaniwa baada ya kuonja ladha yake fulani ya matokeo fulani.
DUH!
Msikilize kidogo Peter Gabriel akiwa na akina Papa Wemba, na....wakikupa..IN YOUR EYES
Swali:- Ushawahi kufurahia kaladha utamu kunoga, wakati ukisifiwa sifa za uongo mbele za watu, wakati unajua inawezekana watu wanajua kuwa hustahili sifa hizo?
Duh!
Lakini.................- Ukionja kuna ladha itakayokupa jibu.
- Usipoonja kunakakitu utakakokuwa unahisi ndio jibu liwakilishalo ladha ya usichokionja.
Lakini.......
............kuna mambo si lazima uonje.
Si lazima uguse moto ili kujua ladha ya kuungua.
Lakini.....
Katika kufikia jibu kabla ya kuonja.......:- Unaweza kuhusudu mtu mpaka ukaogopa kumuomba urafiki au ile...........kutokana na kuhisi unajua ladha ya jibu lake.
- Unaweza kuhusudu /kupenda /kumisi mtu/watu, mpaka ukashindwa hata kuongea nao, kutokana na kuwa ndani ya moyo wako, maongezi hayafikii hata kiduchu cha jinsi ambavyo ungependa kuonyesha mapenzi yako kwao au kutokana na hisia kuwa maongezi aina ya mawasiliano, haifikii kiwango cha jinsi uuhisivyo ukali wa ladha ya mategemeo yao kwako .
Swali:- Ushawahi kuonja kushindwa kufikia mategemeo watu waliojenga kwako?
- Ushawahi kuonja kushindwa kufikia mategemeo unayohisi watu wamejenga juu yako?
- Ushawahi kuonja hisia kuwa kila mtu anafikiria hujali kwa sababu fulani fulani?
- Ushawahi kuonja kufanikiwa kitu fulani ambacho ndio lengo lako moyoni na sio msukumo wa jamii? (hata kama kitu hicho ni kuonja kifuko cha dhambarau?)
- Ushawahi kuonja?
Sidhani ni lazima uonje ilikujua ladha fulani.
Tatizo hata usipoonja, kuna ladha fulani
Sasaa.........- Tuonje au tusionje?
Utamu na uchungu vyote ni ladha.
Kama hujawahi kuonja pipi, basi naweza kukusimulia kuwa ni tamu, ingawa mimi napendelea toffee na wewe labda unapendelea pipi kijiti.
Sasaaaa...
Unataka mpaka kuonja vita ili, ujue ladha yake?
Ijumaa na Wiki Mwisho Njema!
Tulia na Zap Mama wakikupa SWEET MELODIE
-
DUH!Hii shughuli ya maisha nishai Kweli!
Posted: March 7, 2008, 11:15 am by SIMON KITURURU
Bado nipo!
Ingawa naamini watu kiduchu watahisi nimewakwepa.
Bado nahangaika naye huyu maisha, na imetokea kinamna kipindi hiki kanifanya nisionekane kiduchu hapa na hata kule sehemu sehemu.
DUH!
Lakiniiiiiiiiii......!
Mimi mzima , wewe je?
Nitaandika zaidi baadaye kiduchu..
Pata baadhi ya picha zangu na washikaji kadhaa ambao nimegongana nao maeneo au nchi fulani kadhaa wa kadhaa katika kutafuta ambacho kwa bahati mbaya bado sijapata....
Lakiniiiiii......!
Kabla ya kuchungulia baadhi ya picha zangu mchanganyiko nilizozidaka kipindi hiki ambacho mmenitenga,
........msikilize kidogo....Henry Salvador( ambaye Wabrazil wanaamini kawasaidi kutengeneza muziki wa aina ya Bossa nova ingawa yeye si Mbrazil) akutulize mawazo na kibao kiitwacho - Chambre avec vue.
Huyu jamaa naye ametutoka hivi karibuni :-(




























DUH!
Pumzika na JERU Da DAMAJA akija na kibao Ya Playing Yourself BAADAYE BASI!
Blah blah blah
Fish cakes
Alas a fish cake.
Yet more fish cakes
Guess what ... yeah ... fish cakes.
The end of the fish cakes